Pages

Friday, August 5, 2016

TRA imevuka lengo la ukusanyaji wa kodi wa jumla ya kiasi cha shilingi trilioni 1 sawa na asilimia 95.6 tofauti na lengo lililokuwa limekusudiwa la kukusanya trilioni 1.1 kwa mwezi Julai 2016.

NA JACQUILINE MRISHO - MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevuka lengo la ukusanyaji wa kodi wa jumla ya kiasi cha shilingi trilioni 1 sawa na asilimia 95.6 tofauti na lengo lililokuwa limekusudiwa la kukusanya trilioni 1.1 kwa mwezi Julai 2016.
Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 15.43 ukilinganisha na makusanyo ya awali ya mwaka 2015 ambapo mamlaka hiyo ilikusanya jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 914.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, (pichani), wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jjijini Dar es Salaam.
“Kwa mwezi Julai mwaka huu makusanyo yameongezeka kwa asilimia 15.43 ukilinganisha na kipindi cha mwezi Julai 2015 ambapo tulikusanya shilingi Bilioni 914” alisema Kayombo.
Aidha aliongeza kuwa mamlaka imeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha kuwa inafikia au inavuka lengo la Serikali la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 huku mkakati mmoja wapo ukiwa ni kuhakikisha kuwa walipa kodi wapya wanasajiliwa zaidi.
Bw. Kayombo aliongeza kuwa mkakati mwingine ni kuhuisha taarifa za walipa kodi kwa kuhakikisha kwamba namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) zisizotumika zinafutwa katika mfumo wa TRA.
Pia amefafanua kuwa maandalizi ya kuhuisha taarifa za walipa kodi yapo katika hatua za mwisho ikiwemo upigaji picha,uchukuaji wa alama za vidole pamoja na vielelezo muhimu.
TRA inawakumbusha wananchi kuhakikisha wanakagua tiketi/ risiti zao za manunuzi na kuangalia usahihi wa pesa walizolipa na uhalali wa risiti yenyewe.

CHAMA CHA WAFANYAKAZI COTWU (T) KANDA YA DAR ES SALAAM CHAFANYA MKUTANO WAKE MKUU HOTELI YA VILA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Kaimu Mkurugenzi, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Shanes Nungu (katikati), akihutubia wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mussa Mwakalinga na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine.

Wanawake waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanawake wajumbe wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano huo.
Vigogo wa chama hicho wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine, Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam wakiimba wimbo wa mshikamano katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.
Wajumbe wakionesha mshikamano wao wakati wakiimba wimbo maalumu wa mshikamano.
Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo akizungumza katika mkutano huo.
Makatibu wa matawi wa chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Tanzania (CMA), Shanes Nungu (wa tatu kushoto).
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
WANYANGE 11 watakao panda katika jukwaa la Nashera Hotel mjini Morogoro kesho kuwania taji la Miss Kanda ya Mashariki 2016 wakiwa katika pozi tofauti katika kambi yao mjini Morogoro. Warembo hao ni kutoka mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro.




Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya  Kanda ya Ziwa.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo.
Akifungua rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda ya ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho yatakapomalizika.
Alisema mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa, umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya mikoa hiyo kuwa mwenyeji.
Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ameungana na mwenzake wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, kuwahamasisha wakulima wa mikoa hiyo kufufua kilimo cha pamba ambacho amesema kitachangia kufufua viwanda mbalimbali na kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na hivyo kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa maonesho hayo zikiwemo taasisi za serikali na wajasirimali, wamesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kutembelea maonyesho hayo tofauti na maonesho ya miaka iliyopita.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Damian Chang’a, amesema maonesho ya mwaka huu yanashirikisha jumla ya Halmashauri 18 kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyangana na Mara huku mikoa ya Simiyu na Kagera ikishindwa kushiriki.
Itakumbukwa kwamba, alieyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, nae aliwahi kutoa ahadi kama aliyoitoa Mongela, katika Maonesho ya Nanenane miaka iliyopita.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Benki kuu, kwenye maoneshp ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (kushoto), akifuatilia jambo kwenye maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia).
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa.
Burudani ya asili kutoka kikundi cha ngoma za asili Bujora
Mchezo wa nyoka kutoka Bujora
Wapiga picha wakifuatilia wacheza ngoma kutoka Bujora
Taasisi ya Kuzuia na Kutokomeza Ukatili wa Watoto Majumbani, Foundation Karibu Tanzania pia inatoa elimu kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.


Mgeni Rasmi katika mahafali ya Shule ya awali ya Brookhouse International  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mh. Mhandisi Stella Manyanya akitoa Hotuba kwa wanafunzi pamoja na wageni waalikwa
Mwalimu wa Taaluma wa Brookhouse International School Omega Kessy akitoa neno la utangulizi wakati wa mahafali hayo.
Mwalimu Mkuu wa Sunrise Nursery  and Primary School Bw. Onesphor Vitalis akitoa utambulisho kwa wageni waalikwa waliofika katika Mahafali hayo ya shule ya awali.
Mkurugenzi Mkuu wa Sunrise Nursery and Primary School Bi. Marry Shirima akitoa maelezo ya kina juu ya shule hiyo, kumshukuru mgeni rasmi kufika katika mahafali hayo ya watoto wa shule ya awali pamoja kuwapongeza kwa kuhitimu
Mgeni Rasmi katika mahafali ya Shule ya awali ya Brookhouse International School Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mh. Mhandisi Stella Manyanya akimpa mmoja wa watoto cheti cha kuhitimu Elimu ya awali 
Watoto wahitimu wa Shule ya awali wakiendelea kupokea Vyeti vyao 
Mh. Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee akiwa katika mahafali hayo 
Baadhi ya watoto wahitimu wa shule ya awali  wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi
Mgeni Rasmi katika mahafali ya Shule ya awali ya Brookhouse International School Naibu Waziri wa Elimu Mh. Mhandisi Stella Manyanya  akiadhimisha siku yake ya Kuzaliwa hapa akimlisha keki  Mkurugenzi mkuu wa Shule hiyo Mary Shirima
 Wahitimu wa Shule ya awali wakionesha uwezo wao wa kusoma kwa makini
 Wahitimu wa Shule ya awali wakionesha uwezo wao wakitoa Burudani kwa kucheza moja ya ngoma za asili za hapa Tanzania  
Mshehereshaji katika mahafali hayo Mwalimu Isaria akiendelea kutoa utaratibu wakati wa Sherehe hizo
  Watoto wa  Shule ya awali ya Brookhouse International School ambao wanandoto ya kuja kuwa Marubani wakiwa wanaelezea juu ya ndoto zao
Walimu nao hawakuwa nyuma waliendelea na Burudani 
Baadhi ya wahitimu wa shule ya awali wakiwa katika sherehe yao
Baadhi ya wanafunzi wanaobaki wakiwa katika mahafali hayo
Wazazi wa watoto wanaosoma shule hiyo pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika mahafali ya shule ya awali ya Brookhouse.

Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa
1
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza kwa unyenyekevu mbele ya Wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakati alipokutana nao ili kujitambulisha na kufahamiana nao baada ya kuanza kazi kama mkuu wa wilaya hiyo, Aliwaomba wazee hao kushirikiana naye bega kwa bega na kumpa ushauri wa kila mara ili aweze kutekeleza majukumbu yake ya kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo na kufanikisha mipango ya Rais Mh. Dk John Pombe Magufuli ili kutekeleza kwa ufanisi ilani ya uchaguzi ya CCM, Katika picha kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Asaa Simba , Mkutano huo ulifanyika kwenye ofisi za CCM wilaya ya Ilala.
2
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Asaa Simba akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema ili kuongea na wazee wa CCM wilaya ya Ilala.
3
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akimsikiliza Katibu wa CCwilaya ya Ilala Bw. Kafuge Joel alipokuwa akizungumza mambo kadhaa kabla ya umkaribisha mwenyekiti wake ili kumkaribisha mkuu wa wilaya.
4
Baadhi ya wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa katika mkutano huo uliowakutanisha na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
5
Baadhi ya wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa katika mkutano huo uliowakutanisha na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.



NA KHALFAN SAID NA MWASHIRIKAYA HABARI
BILIONEA Donald Trump, ambaye anataka kuwa Rais wa Marekani, ameendelea “kupigwa madongo” kutoka kila kona, kufuatia kauli zake za “kukurupuka” ambazo ni tata na kali.
Akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong na waandishi wa habari Ikulu ya White Hosue siku mbili zilizopita, Obama amemualezea Donald Trump kuwa ana uelewa mdogo kwenye masuala ya msingi ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia, na kwamba anasikitika kuwa Tajiri huyo hakujiandaa kuwa Rais.
“Maoni haya siyo yangu pekee bali pia ni maoni ya Viongozi wengine mashuhuri kama Spika wa Baraza la Wawakilishi anayetoka chama chake cha Republicans, Paul Ryan na Kiongozi wa walio wengi wa Baraza la Senet, Mitch McConnell”, Obama alishangazwa na viongozi hao waandamizi wa Republicans, na kusema, “Swali nafikiri ni wao kujiuliza, kama kama wamekwishatoa maonyo mara kadhaa tena kwa hisia kali kwamba semayo Trump si sahihi, sasas ni vipi tena bado mnamkumbatia, hii ina maana gani kwenye chamachenu kuwa huyu ndiye mpeperusha bendera wenu kwenye uchaguzi wa Rais wa Marekani.” Alishangazwa Obama.
“Madongo” hayo hayakuishia hapo, Mjumbe wa Baraza la Congress anayetokachama cha Republicans,  Adam Kinzinger, amesema, haoni maana yoyote ya kumuunga mkono mgombea wa chama chake Donald Trump, ilhali mgombea huyo anaonyesha tabia za kushangaza ukitazama mlolongo wa matukio wiki hii. “Mimi ni Mmarekani kabla ya kuwa mwana Republica.” Alisema Kinzinger katika kipindi cha CNN cha Situation Room kinachoendeshwa na mangazaji wa televisheni  hiyo Wolf Blitzer

Naye Rais wa Ufaransa Fracoise Holande amesema kauli za Trump zinatia kichefuchefu, na kuonya madhara makubwa yataikumba Dunia kama Tajiri huyo atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani.

Naye Mwakilishi wa Baraza la Congres kutoka New York ambaye ni mwanachama wa Republican,Richard Hanna, yeye amebainisha wazi kuwa kutokana na mlolongo wa matamshi na visa visivyoeleweka vya mgombea wao Dolald Trump, yeye atampigia kura mgombea wa chamacha Democrat, Bibi. Hillary Clinton, ameandikakwenye barua yake iliyokwenda sambamba na mahojiano na mtandao wa Syracuse.com “Chama change cha Republican kinazidi kupoteza mwelekeo wa uwezo wake wa kuteua wagombea Urais wanaoweza kuletea chama ushindi, na Trump hafai kukiongoza chama wa Urais wa Marekani.” Alibainisha Hanna.
Hasira za Wamarekani, kuhusu Donald Trump, zimeongezeka kufuatia kauli zake kuhusu Rais wa Russia, Vladimir Putin, na wazazi wa Mwanajeshi Musilamu wa Marekani aliyeuawa akiwa vitani Kapteni Humayun Khan.
Wakati hayoyakiendelea mgombea wa Urais wa nchi hiyo kutoka chama cha Democrat, Bibi Hillary Clinton, yeye amechagua kukaa kimya bila hata kutia neno kwani upepo sasa unavuma upande wake


 Adam Kinzinger
 Richard Hanna
 Bibi. Hillary Clinton

Fracoise Holande

Seneta, Mitch McConnell

Paul Ryan

No comments:

Post a Comment