Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Dkt. Yamungu Kayandabila akisisitiza jambo kwa
watumishi wa wizara hiyo, alipokutana nao katika Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma 2016. Dkt Yamungu alipokea kero mbalimbali kutoka kwa
watumishi hao pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza ufanisi katika
utoaji wa huduma kwa wananchi.
Baadhi
ya watumishi na watendaji wa Wizara ya Ardhi, wakimsikiliza Katibu Mkuu
Dtk. Yamungu akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwake na
watumishi hao kama sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
2016.
Mtumishi
Beatus Kashangaki akitoa kero zake kwa Katibu Mkuu Dkt. Yamungu
Kayandabila wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
Watanzania wapata fursa ya kushiriki mafunzo kuhusu Tsunami
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kitengo kinachoshughulikia Tsunami, Ardito
Kodijat akifungua mafunzo hayo kwa kuwaeleza washiriki aina ya mafunzo
ambayo watapatiwa
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akitoa neno
la ufunguzi kwa niaba ya UNESCO Tanzania na kueleza sababu ya kufanyika
mafunzo hayo.
Mkuu
wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa nchini
(TMA, Dk. Ladislauds Chang`a akizungumza jinsi TMA imejipanga kuendeleza
kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Tsunami na kuwataka Watanzania kuwa na
utaratibu wa kufatilia hali ya hewa nchini hasa katika kipindi hiki
ambacho ni kuna mabadiliko ya tabia ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard
Chamuriho akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yanayohusu kuwapa elimu
washiriki ya kuhusu Tsunami.
Baadhi ya washiriki ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kufanyika kwa siku tano.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
……………………………………………………………………………………………………………
Kutokana na kuwa na athari
kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa, Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha watu mbalimbali
nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga.
Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema
kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata elimu kuhusiana na
Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo yanasababishwa na hivyo ni
matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa kusambaza elimu hiyo kwa
Watanzania wengine.
“Watu wengi wamepoteza maisha
tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha
kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani
Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na hapa,” alisema
Bi. Rodrigues.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema
kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa
yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo lilitokea eneo
lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na
kusababisha vifo vya waogeleaji watano.
“Mafunzo haya yanatakiwa
kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika mengine na
yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha kufanya siku
athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila mtu kujua
athari za Tsunami hata likitokea mbali,” alisema Dk. Chamuriho.
Mkutano wa Magavana unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali imesema itaendelea
kufanya biashara na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia fursa
zilizopo nchini ikiwemo uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndulu
alipokuwa akifungua mkutano wa Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 14
za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi
wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).
“Tanzania imeanza miaka 2 hadi 3
kujiwekea akiba ya sarafu ya Yuan ya nchini China kutokana biashara
mbalimbali ambapo hadi sasa nchi ina akiba ya asilimia 5 za fedha ya
China Yuan” alisema Profesa Ndulu.
Hatua hiyo ya Tanzania inafuatia
Sarafu ya China ijulikanayo kama Yuan kuingizwa kuwa miongoni mwa sarafu
sita zinazotumika Duniani.
Mkutano huo unafuatia majumu ya
Benki Kuu hizo za nchi wanachama kuwa na jukumu la kuwa walinzi wa akiba
ya fedha za kigeni na wawezeshaji wa masuala ya biashara za kimataifa.
Maweneo ambayo Tanzania
inayatumia kama njia moja wapo ya kujiongezea sarafu ya China ni pamoja
na uwekezaji katika hati fungani inafaida zaidi ikilinganishwa na nchi
za Ulaya na nchi nyingine duniani.
Profesa Ndulu alizitaja sarafu
nyingine ambazo zinatumika duniani zinazotambuliwa na Shirika la Fedha
la Kimataifa (IMF) ni pamoja na Dola ya Marekani, Euro inayotumiwa na
nchi za Ulaya, Swiss Frank ya Uswiss, Paund ya Uingereza, Yen ya Japani
pamoja na Yuan ambayo itaanza kutumika kimataifa kuanzia mwezi Septemba
2016.
Mahusiano ya kibiashara kati ya
Tanzania na China ni ya kihistoria yanayohusisha Serikali za nchi hizo
mbili ambao ulijengwa kwa msingi imara wa Waasisi wa mataifa hayo Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Muasisi wa
Taifa la China Mwenyekiti Mao Tse Tung.
Mkutano wa huo wa MEFMI unatoa
fursa ya kipekee kubadilishana mawazo kwa viongozi hao juu ya
ushirikishwaji wa Yuan Kichina ndani ya kikapu cha hifadhi ya sarafu ya
IMF / Benki ya Dunia katika nchi wanachama wa MEFMI.
Kufanyika kwa mkutano huo ni moja
matukio ya kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) yanayotarajiwa kutahudhuriwa na Wachumi waliobobea wa ndani na nje
ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC).
Umeme vijijini utawatoa watanzania katika umasikini
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – DODOMA
Injini ya kuinua uchumi wa
Tanzania kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati imetajwa kuwa ni
uwepo wa umeme wa uhakika unaoendana na mahitaji.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma
na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo alipokuwa
akijibu hoja mbalimabli za Wabunge zinazohusu upataikanaji wa nishati ya
umeme.
“Bajeti ya mwaka 2016/17
itahakikisha umeme unapatikana vijijini ambapo Wizara ya Nishati na
Madini katika bajeti hii imeongezewa asilimia 50 zaidi ya bajeti
inayoisha ya mwaka 2015/2016, ili kuhakikisha umeme unapatikana
Vijijini,” alisema Mhe. Muhongo.
Mhe. Muhongo aliendelea kusema
kuwa, bajeti hiyo inahakikishha vyanzo vyote vya umeme kama vile gesi
asilia, upepo, mawimbi, makaa ya mawe, jotoardhi na jua vinazalisha
umeme Nchi nzima.
Aidha, Waziri huyo amesema kuwa
bajeti hiyo itapelekea kuboreshwa kwa upatikanaji wa umeme kwa kupitia
sheria na taratibu zinazoipa mamlaka TANESCO peke yake kutoa huduma ya
umeme kwa kuleta ushindani katika kutoa na kusambaza umeme Nchini.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah Kairuki akijibu hoja kuhusu swala la kuwepo kwa watumishi hewa
na hatua zinazochukuliwa kukomesha tatizo hilo, amesema kuwa Serikali
iko tayari kufukuza Maafisa Utumishi wote ambao wamesababisha kuwepo kwa
watumishi hewa ili kubaki na Maafisa Utumishi ambao ni wazalendo,
waadilifu na wachapakazi.
Bilioni 2.5 kuanza kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro
Na: Lilian Lundo – Maelezo – Dodoma
Serikali kupitia Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetenga jumla ya
shilingi Bilioni 2.5 katika bajeti ya mwaka 2016/017 ili kujenga
hospitali ya Wilaya ya Morogoro.
Hayo yamesemwa leo,Mjini Dodoma
na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Selemani Jaffo alipokuwa akijibu
swali la Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Azizi Abood juu ya msongamano
mkubwa wodi za akina mama hospitali ya Rufaa Morogoro.
“Msongamano wa wagonjwa katika
wodi ya wazazi Hospitali ya Mkoa unatokana na kukosekana kwa hospitali
ya Wilaya ya Morogoro.Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali immepanga
kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Morogoro katika bajeti ya mwaka
2016/17,” alisema Mhe. Jaffo
Mhe. Jaffo aliendelea kusema
kuwa, fedha hizo zilizotengwa zitaanza kwa ujenzi wa jengo la utawala na
jengo la wagonjwa wa nje.(OPD).
Aidha, aliendelea kujibu maswali
ya yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kwa kusema kuwa, Serikali katika
bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi
wa chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary) Wilaya ya Chunya.
Chumba hicho cha kuhifadhi maiti
kinatarajiwa kugharimu shilingi milioni 230 ambapo ujenzi wa jengo
utagharimu shilingi milioni 60 na Majokofu yatagharimu shilingi milioni
160.
Kwa sasa Wilaya hiyo ina chumba
maalum ambacho kimetengwa kwa ajili ya kuhifadhi mati mbili tu ambacho
hakitoshelezi huduma hiyo hali ambayo huwalazimu wahitaji kufuata huduma
ya kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
No comments :
Post a Comment