Pages

Monday, June 20, 2016

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI 2016 KWA KUSIKILIZA KERO ZA WAFANYAKAZI.

mabu1 
 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Dkt. Yamungu Kayandabila akisisitiza jambo kwa watumishi wa wizara hiyo, alipokutana nao katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016. Dkt Yamungu alipokea kero mbalimbali kutoka kwa watumishi hao pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
mabu2   
Baadhi ya watumishi na watendaji wa Wizara ya Ardhi, wakimsikiliza Katibu Mkuu Dtk. Yamungu akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwake na watumishi hao kama sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
mabu3  
Mtumishi Beatus Kashangaki akitoa kero zake kwa Katibu Mkuu Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

Watanzania wapata fursa ya kushiriki mafunzo kuhusu Tsunami

una1 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kitengo kinachoshughulikia Tsunami, Ardito Kodijat akifungua mafunzo hayo kwa kuwaeleza washiriki aina ya mafunzo ambayo watapatiwa una2 
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi kwa niaba ya UNESCO Tanzania na kueleza sababu ya kufanyika mafunzo hayo. una3 
Mkuu wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa nchini (TMA, Dk. Ladislauds Chang`a akizungumza jinsi TMA imejipanga kuendeleza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Tsunami na kuwataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kufatilia hali ya hewa nchini hasa katika kipindi hiki ambacho ni kuna mabadiliko ya tabia ya nchi. una04 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yanayohusu kuwapa elimu washiriki ya kuhusu Tsunami.
una4 
Baadhi ya washiriki ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kufanyika kwa siku tano. una5 
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
……………………………………………………………………………………………………………
Kutokana na kuwa na athari kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha watu mbalimbali nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga.
Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata elimu kuhusiana na Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo yanasababishwa na hivyo ni matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine.
“Watu wengi wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na hapa,” alisema Bi. Rodrigues.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo lilitokea eneo lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na kusababisha vifo vya waogeleaji watano.
“Mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika mengine na yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha kufanya siku athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila mtu kujua athari za Tsunami hata likitokea mbali,” alisema Dk. Chamuriho.

Mkutano wa Magavana unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).

images 
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali imesema itaendelea kufanya biashara na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia fursa zilizopo nchini ikiwemo uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndulu alipokuwa akifungua mkutano wa Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 14 za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).
“Tanzania imeanza miaka 2 hadi 3 kujiwekea akiba ya sarafu ya Yuan ya nchini China kutokana biashara mbalimbali ambapo hadi sasa nchi ina akiba ya asilimia 5 za fedha ya China Yuan” alisema Profesa Ndulu.
Hatua hiyo ya Tanzania inafuatia Sarafu ya China ijulikanayo kama Yuan kuingizwa kuwa miongoni mwa sarafu sita zinazotumika Duniani.
Mkutano huo unafuatia majumu ya Benki Kuu hizo za nchi wanachama kuwa na jukumu la kuwa walinzi wa akiba ya fedha za kigeni na wawezeshaji wa masuala ya biashara za kimataifa.
Maweneo ambayo Tanzania inayatumia kama njia moja wapo ya kujiongezea sarafu ya China ni pamoja na uwekezaji katika hati fungani inafaida zaidi ikilinganishwa na nchi za Ulaya na nchi nyingine duniani.
Profesa Ndulu alizitaja sarafu nyingine ambazo zinatumika duniani zinazotambuliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ni pamoja na Dola ya Marekani, Euro inayotumiwa na nchi za Ulaya, Swiss Frank ya Uswiss, Paund ya Uingereza, Yen ya Japani pamoja na Yuan ambayo itaanza kutumika kimataifa kuanzia mwezi Septemba 2016.
Mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na China ni ya kihistoria yanayohusisha Serikali za nchi hizo mbili ambao ulijengwa kwa msingi imara wa Waasisi wa mataifa hayo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Muasisi wa Taifa la China Mwenyekiti Mao Tse Tung.
Mkutano wa huo wa MEFMI unatoa fursa ya kipekee kubadilishana mawazo kwa viongozi hao juu ya ushirikishwaji wa Yuan Kichina ndani ya kikapu cha hifadhi ya sarafu ya IMF / Benki ya Dunia katika nchi wanachama wa MEFMI.
Kufanyika kwa mkutano huo ni moja matukio ya kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yanayotarajiwa kutahudhuriwa na Wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya  Afrika  Mashariki  (EAC)  na  wa  Jumuiya  ya  Maendeleo  ya  Nchi  za  Kusini  mwa  Afrika (SADC).

Umeme vijijini utawatoa watanzania katika umasikini

leo3 
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – DODOMA
Injini ya kuinua uchumi wa Tanzania kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati imetajwa kuwa ni uwepo wa umeme wa uhakika unaoendana na mahitaji.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo alipokuwa akijibu hoja mbalimabli za Wabunge zinazohusu upataikanaji wa nishati ya umeme.
“Bajeti ya mwaka 2016/17 itahakikisha umeme unapatikana vijijini ambapo Wizara ya Nishati na Madini katika bajeti hii imeongezewa asilimia 50 zaidi ya bajeti inayoisha ya mwaka 2015/2016, ili kuhakikisha umeme unapatikana Vijijini,” alisema Mhe. Muhongo.
Mhe. Muhongo aliendelea  kusema kuwa, bajeti hiyo inahakikishha vyanzo vyote vya umeme kama vile gesi asilia, upepo, mawimbi, makaa ya mawe, jotoardhi na jua vinazalisha umeme Nchi nzima.
Aidha, Waziri huyo amesema kuwa bajeti hiyo itapelekea kuboreshwa kwa upatikanaji wa umeme kwa kupitia sheria na taratibu zinazoipa mamlaka TANESCO peke yake kutoa huduma ya umeme kwa kuleta ushindani katika kutoa na kusambaza umeme Nchini.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akijibu hoja kuhusu swala la kuwepo kwa watumishi hewa na hatua zinazochukuliwa kukomesha tatizo hilo, amesema kuwa Serikali iko tayari kufukuza Maafisa Utumishi wote ambao wamesababisha kuwepo kwa watumishi hewa ili kubaki na Maafisa Utumishi ambao ni wazalendo, waadilifu na wachapakazi.

Bilioni 2.5 kuanza kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro

index 
Na: Lilian Lundo – Maelezo – Dodoma
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetenga jumla ya shilingi Bilioni 2.5 katika bajeti ya mwaka 2016/017 ili kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro.
Hayo yamesemwa leo,Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Selemani Jaffo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Azizi Abood juu ya msongamano mkubwa wodi za akina mama hospitali ya Rufaa Morogoro.
“Msongamano wa wagonjwa katika wodi ya wazazi Hospitali ya Mkoa unatokana na kukosekana kwa hospitali ya Wilaya ya Morogoro.Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali immepanga kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Morogoro katika bajeti ya mwaka 2016/17,” alisema Mhe. Jaffo
Mhe. Jaffo aliendelea  kusema kuwa, fedha hizo zilizotengwa zitaanza kwa ujenzi wa jengo la utawala na jengo la wagonjwa wa nje.(OPD).
Aidha, aliendelea kujibu maswali ya yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kwa kusema kuwa, Serikali katika bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary) Wilaya ya Chunya.
Chumba hicho cha kuhifadhi maiti kinatarajiwa kugharimu shilingi milioni 230 ambapo ujenzi wa jengo utagharimu shilingi milioni 60 na Majokofu yatagharimu shilingi milioni 160.
Kwa sasa Wilaya hiyo ina chumba maalum ambacho kimetengwa kwa ajili ya kuhifadhi mati mbili tu ambacho hakitoshelezi huduma hiyo hali ambayo huwalazimu wahitaji kufuata huduma ya kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa wa Mbeya

No comments:

Post a Comment