Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia
nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kushoto), wakisaini Hati ya
Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440
kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa
Wizara Jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi.
Bella Bird wakibadilishana Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania
kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II,
Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
Waandishi
wa habari pamoja na wadau wengine wakifuatilia maelezo ya Hati ya
Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440
kwa ajili ya mradi wa Tasaf kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na
Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird. Tukio hilo
limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
kuhusu Makubaliano yaliyofanywa kati ya Tanzania na Benki ya Dunia ya
ili kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II.
Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile akibadilishana mawazo na Mratibu Maendeleo ya Sekta
Binafsi na SAGCOT kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza
kusaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya
Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika
katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
……………………………………………………………………………………………………………………..
Benny Mwaipaja
Kaimu Msemaji Wizara ya Fedha na Mipango
Serikali kupitia Wizara ya Fedha
na Mipango imesaini hati ya makubaliano na Benki ya Dunia itayoiwezesha
Tanzania kupata nyongeza ya fedha katika mradi wa Tasaf kiasi cha
Shilingi Bilioni 440.
Hati hiyo ilisainiwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird, Makao Makuu ya Wizara ya
Fedha, Dar es Salaam, leo, Juni 23, 2016.
Akiongea wakati wa kusaini hati
hiyo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika mradi wa
Tasaf II kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kukuza kipato chao
kupitia ajira za muda zitakazowawezesha kupeleka watoto shule na
kuwapatia huduma za afya.
Aliongeza kuwa katika mwaka wa
fedha 2015/2016 Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imefanya
kazi kubwa iliyowezesha miradi kumi kupitishwa ambayo ina thamani ya
Shilingi Trilioni 1.9.
“Miongoni mwa miradi iliyopata
ufadhili ni pamoja na mradi wa kuboresha mazingira ya biashara uliopata
shilingi Bilioni 168, mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA), uliopata
Shilingi Bilioni 440” Aliongeza Dkt. Likwelile
Aidha, alisema kuwa Serikali
inaendelea na majadiliano na Benki hiyo kwa ajili ya kuboresha Bandari
ya Dar es Salaam, ambapo kiasi cha dola Milioni 600 zimetengwa kwa ajili
ya kazi hiyo.
Dkt. Likwelile ameishukuru Benki
ya Dunia kwa mchango wake mkubwa na kusema kuwa Serikali itahakikisha
kuwa inazisimamia taasisi zinazotekeleza miradi hiyo ili ziweze kutumia
fedha hizo vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi
wa Benki ya Dunia, Bella Bird, amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya
tano katika kupambana na rushwa na kuweka mazingira rafiki kwa sekta
binafsi.
Aliongeza kuwa sekta binafsi ndizo zinatoa ajira kwa wingi na kusaidia kuchangia katika kuongeza mapato ya Serikali.
Ameahidi kuwa Benki yake
itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuiwezesha kufikia malengo yake
ya kiuchumi na kijamii kwa faida ya wananchi wake.
TANZANIA BADO INAHITAJI WATAALAM WALIOBOBEA KATIKA BIASHARA YA KIMATAIFA
Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati
akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za
masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
Mmoja wa washiriki wa Mkutano huo akichangia wakati wa Mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano kuhusu program mpya mbili za masomo katika ngazi ya
Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na CBE.
Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na CBE.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema akiwa katika picha ya pamoja na
wadau mbalimbali waliohudhuria katika chuo hicho kujadili program mpya
mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika
Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
……………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – Dar es salasam.
Tanzania
bado inahitaji wataalam waliobobea katika Biashara ya Kimataifa na wale
wanaosimamia mfumo wa uzalishaji, usambazaji na utunzaji wa
bidhaa mbalimbali hususan mazao ya chakula ili kukabiliana na
changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya uagizaji, utunzaji,
usambazaji na hasara ya kuharibika kwa mazao inayowakumba wafanyabiashara walio wengi kabla ya kufikisha bidhaa zao kwa walaji.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau
mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya
Shahada ya Uzamili (Masters)katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
Amesema
ili kukabiliana na changamoto hizo zinazowakumba wakulima na
wafanyabiashara walio wengi hasa wale wa matunda ambao hupoteza karibu
asilimia 40 ya mazao yao, lazima hatua madhubuti zichukuliwe kwa
kuwajengea
uwezo wa kitaalamu vijana wa Kitanzania ambao wataweza kukabiliana na changamoto ya wakulima kupata hasara kwa kuhakikisha mazao yanayotoka kwenye maeneo ya uzalishaji yanafika yakiwa salama.
uwezo wa kitaalamu vijana wa Kitanzania ambao wataweza kukabiliana na changamoto ya wakulima kupata hasara kwa kuhakikisha mazao yanayotoka kwenye maeneo ya uzalishaji yanafika yakiwa salama.
‘Leo
tuna mkutano wa wadau kwa sababu CBE tuko katika hatua za mwisho za
mchakato wa kuanzisha Programu mpya za Shahada za uzamili katika katika
masuala ya Ugavi (Procurement and Supply Chain Management) pia Shahada
ya
Uzamili katika Biashara ya Kimataifa (International Business Management) ili tuweze kutoa mafunzo yatakayowasaidia watanzania’’
Uzamili katika Biashara ya Kimataifa (International Business Management) ili tuweze kutoa mafunzo yatakayowasaidia watanzania’’
Amebainisha kuwa mazao kama matunda mara nyingi yamekuwa yakiharibika katika hatua ya kuvunwa, kusafirishwa na
kuhifadhiwa jambo linalowasababishia hasara wakulima pamoja na wasafirishaji kwa kuwa hawana ujuzi na utalaam wa usimamizi wa bidhaa na mazao yao.
Aidha, ameongeza kuwa asilimia 40 ya gharama hizo hutumika katika masuala ya usafirishaji na ufuatiliaji
wa bidhaa husika kuifikisha kwa mlaji na kusisitiza kwamba gharama hizo
husababishwa na mfumo mzima unaopaswa kupitiwa kabla ya kuifikisha
bidhaa husika sokoni jambo ambalo lingerekebishwa kwa kuwa na wataalam
wa kutosha kusimamia sekta hiyo.kuhifadhiwa jambo linalowasababishia hasara wakulima pamoja na wasafirishaji kwa kuwa hawana ujuzi na utalaam wa usimamizi wa bidhaa na mazao yao.
Bunge lapitisha muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka 2016
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha muswada wa sheria ya
Fedha ya mwaka 2016 ili kuwezesha utekelezaji wa bajeti ya Serikali
kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Muswada huo umepitishwa na Bunge pamoja na marekebisho yake ambayo yametolewa na kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti na wabunge.
Marekebisho
yaliyofanyika katika muswada huo ni pamoja na kutoongeza ushuru wa
kuingiza sukari ya viwandani kutoka asilimia 10 kwenda 15 ambapo kamati
ya kudumu ya bunge ya bajeti ilishauri Serikali isiendelee na pendekezo
hilo kutokana na hatua hiyo kuwa na athari kwa viwanda vinavyotumia
sukari viwandani kama malighafi ya kuzalisha bidhaa nyingine kama juisi
na soda.
“Serikali
imekubali pendekezo lililotolewa na kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti
ya kutoongeza ushuru wa kuingiza sukari ya viwandani kutoka asilimia 10
kwenda asimilia 15, hivyo kuendelea kutoza asilimia 10 iliyokuwepo kwa
mwaka huu wa fedha,” alifafanua Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Mpango.
Marekebisho
mengine yaliyofanyika ni pamoja na kuondoa adhabu ya kifungo cha miezi
Sita kwa wale ambao hawatodai risiti baada ya kununua bidhaa au huduma
na kubaki na adhabu ya kulipa faini kulingana na thamani ya bidhaa.
Aidha
Mhe. Mpango amesema kuwa muswada huo umezingatia kwa kiwango kikubwa
mapendekezo ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, wamiliki wa viwanda,
wafanyabiashara na taasisi za Serikali.
MRADI WA PS3 WAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA WASIMAMIZI RASILIMALI WATU
Mkurugenzi wa Mradi wa PS3 Dk. Emmanuel Malangalila
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyo
wakutanisha pamoja wataalam mbalimbali wanaohusika na usimamizi wa
rasilimali watu kutoka katika mikoa na tasisi za serikali ili kupata
kitini cha kutolea mafunzo kwa watumishi wapya wanaoajiriwa serikalini.
Mafunzo hayo yanafanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nchini ambao unatekelezwa katika mikoa 13 na kuzinufaisha halmashauri 97.
Baadhi
ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na serikali za Mitaa
(TAMISEMI). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa,
Miriam Mmbaga akifuatiwa na Beatice Kimoleta
Washiriki
wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu
katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga
kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha
mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea
kufanya kazi katika mazingira yeyote.
Mkuu
wa Kitengo cha Mifumo ya Rasilimali wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo
ya Sekta za Umma (PS3) Josephine Kimaro akitoa mafunzo kwa viongozi wa
sekta ya Afya waliojitokeza kushiriki semina hiyo mjini Bagamoyo mkoani
Pwani.
Washiriki
wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu
katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga
kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha
mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea
kufanya kazi katika mazingira yeyote.
MTOTO LUQMAN ALLY AMEPOTEA NA ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE
Luqman
Ally (14) anatafutwa na wazazi wake, amepotea tarehe 13 Juni mwaka huu,
anasoma shule ya Msingi Mbagala Islamic Darasa la Sita iliyopo Mbagala
jijini Dar es Salaam.
Mara ya kwanza alitoroka wiki mbili zilizopita na akapatikana katika kituo cha kulelea
watoto wanaoishi katika mazingira Magumu cha Chad kilichopo Mazese.
watoto wanaoishi katika mazingira Magumu cha Chad kilichopo Mazese.
Taarifa imetolewa katika kituo cha Polisi cha Majimajitu Mbagala jijini Dar es Salaam
kwa RB .NO MAT/RB/618/16.
kwa RB .NO MAT/RB/618/16.
Yeyote ambaye atamwona mtoto huyo apige
NAMBAYA YA
SIMU. 0655891200. MAMA YAKE MZAZI WA LUQMAN.
SIMU. 0655891200. MAMA YAKE MZAZI WA LUQMAN.
SERIKALI yawataka wazalishaji wa vyakula, vinywaji na viwanda vya mikate kuzingatia ubora
SERIKALI imewataka wazalishaji wa vyakula, vinywaji na
viwanda vya mikate,kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango kwa kutambua
kuwa hiki ni kipindi cha utandawazi ambacho kina ushindani mkubwa
vinginevyo watashindwa kuzalisha na kupata masoko ya uhakika.
Rai hiyo imetolewa jana na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,
Richard Kwitega, alipokuwa akifungua mafunzo ya uelimishaji
,wazalishaji wa vyakula,kuhusu umuhimu wa kuzalisha bidhaa bora zenye
viwango sanjari na kuzingatia usalama wa vyakula na afya ya
mlaji,mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA, kanda
ya kaskazini..
Kwitega,alisema kuwa serikali inatambua zipo changamoto
mbalimbali katika kipindi hiki cha utandawazi na biashara huria hivyo
hakuna mzalishaji ambae ataweza kudumu katika biasharabila kuhakikisha
kuwa bidhaa inayozalishwa inakidhi vigezo vya ubora wa viwango na
usalama kwa afya ya mlaji.
Kwitega, alisema wazalishaji hao watazishinda changamoto
hizo ikiwa iwapo watazalisha bidhaa zenye ubora na viwango katika
mazingira ya ushindani vinginevyo tuaishia kununua bidhaa toka nje kwa
kuwa bidhaa zetu zimeshindwa kukidhi ushindani wa ubora .
Alisema ,suala la usalama wa vyakula ni la msingi kwa
sababu linaathari kubwa kiafya ,kiuchumi,na kijamii,kwa sababu hiyo wao
wakiwa ni wadau muhimu wana wajibu mkubwa wa kufanikisha lengo la
kuimarisha usafi sehemu zao za uzalishaji.
‘’Ninasema tatizo kubwa na sugu ni baadhi yanu wazalishaji
ambao wamekuwa hawazingatii usafi kwenye maeneo yao ya uzalishaji hivyo
lazima wazalishe kwa kulinda afya za walaji’’alisema Kwitega.
Alisema kuwa mamlaka ya chakula na dawa TFDA,ina jukumu la
kudhibiti uhifadhi,usafirishaji ,usindikaji, uangalizaji na usambazaji
wa vyakula pamoja na kusajili majengo yote yanayotumika kwenye
uzalishaji wa vyakula na utoaji wa vibali vya kusindika uingizaji wa
bidhaa nje.
Alisema kama taasisi ya udhibiti vyakula ina wajibu wa
kuwasaidia wazalishaji ili waweze kukua,na kuzalisha vyakula kwa mjibu
wa sheria na kanuni bora za uzalishaji ili waweze kumudu ushindani
wa soko la ndani na je .
Kuhusu viwanda, Kwitega, amesema sera ya serikali ni
kuongeza na kukuza viwanda kwa kuwa viwanda vina nafasi kubwa ya
kuchangia kwenye pato la taifa na vinaweza kuleta mchango wa athari za
kiafya ikiwa bidhaa zake hazitakidhi viwango vya ubora na usalama.
Awali meneja wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA, kanda ya
kaskazini, Damasi Matiko,mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa awamu ni
mwendelezo ili kuwajengea uwezo wazalishaji hao waweze kuzalisha bidhaa
zenye ubora na kuhimili ushindani kwenye masoko.
Alisema kuwa tangia mafunzo hayo yaanze kutolewa makundi
mbalimbali ya wazalishaji hao wameongeza viwango vya ubora wa bidhaa zao
tofauti na miaka iliyopita ambapo viwanda vyetu vilivkuwa havifanyi
vizuri na matokeo yake kulazimika kutumia bidhaa toka nje.
Matiko, alisema TFDA, itaendelea kutoa mafunzo kwa makundi
mbalimbali ya wazalishaji ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa bora
hivyo kuepuka kuzalisha bidhaa hafifu ambazo zitawakosesha masoko .
Alisema kuwa TFDA, inashirikiana na shirika la viwanda
vidogo ,SIDO na shirika la viwango nchini TBS, katika kutoa elimu kwa
wazalishaji mbalimbali ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora waweze
kupata masoko ya ndani na nje na kujiongezea vipato.
DK. MENGI ACHANGIA MADAWATI 1,000, ATOA SOMO KWA WATU MATAJIRI
Katika kuunga mkono
jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini
linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa
Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa
wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35
kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza
tatizo hilo katika wilaya hizo.
Akizungumza katika halfa ya
kukabidhi pesa hizo kwa wakuu wa wilaya wa kampuni hizo, Dk. Mengi
alisema ni muhimu kwa watanzania kuungana kwa pamoja na kusaidia
kupatikana kwa madawati kwani kwa kufanya hivyo ni kulisaidia taifa.
Hata hivyo Dk. Mengi alisema
kuwa anaamini kama watu matajiri nchini wakiungana kwa pamoja na
kujadili jinsi ya kumaliza tatizo la madawati nchini basi jambo hilo
litaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka tofauti na sasa ambapo linakwenda
kwa mwendo wa kusuasua.
“Ukisaidia mtu mmoja katika
elimu ni sawa umesaidia jamii na taifa kwa ujumla kama watu matajiri
wakisema wakae kwa pamoja na kuangalia jinsi ya kumaliza tatizo hili
linaweza kutatuliwa na shida ya madawati kumalizika.
Mkurugenzi Mtendaji wa
makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza katika halfa ya
kukabidhi milioni 70 kwa wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo
zitawezesha wilaya hizo kununua madawati 1,000 na kila wilaya kupata
madawti 500.
“Matajiri wanatakiwa kutambua
kuwa wanatakiwa kurudisha shukrani zao kwa Mungu, taifa na wananchi na
hasa kwa walio na hali ya chini kwani hao ndiyo wanaowasaidia kufanya
biashara zao kwa amani,” alisema Dk. Mengi.
Aidha amewataka wakuu wa wilaya
hizo kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kama watakuwa hawajakamilisha na
wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuongeza juhudi huku akiwashauri
kuandaa mikutano katika wilaya zao na kushirikisha wananchi wao ili
waweze kuchangia na hatimaye tatizo hilo kumalizika.
Kwa upande wa mkuu w wilaya ya
Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga na mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab
wamemshukuru Dk. Mengi kwa msaada ambao amewapatia na kuwataka
watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama jinsi amevyofanya Dk.
Mengi kwa kuchangia upatikanaji wa elimu bora.
Awali kabla ya msaada ambao
umetolewa na Dk. Mengi, wilaya ya Bagamoyo ilikuwa ikikabiliwa na
upungufu wa madawati 2,463 na Handeni ikikabiliwa na tatizo la upungufu
wa madawati 4,000.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab akizungumza katika halfa hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,
Alhaj Majid Mwanga akizungumza katika halfa ya kupokea pesa kwa ajili ya
madawati 500 yatakayokwenda katika wilaya yake kusaidia kupunguza
tatizo la madawati.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisaini mfano wa hundi kabla ya kuanza kuwakabidhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya
milioni 35, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab. Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Kenneeth Haule, Mwenyekiti wa Mji wa
Handeni, Twaha Mgaya na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Handeni, Ramadhani
Diliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa
makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya
milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 500, Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Chalinze,
Edes Lukoa, Mkurugenzi wa Bagamoyo, Natujwa Melau, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Issa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Chalinze, Said Zikatimu.
Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya TBS na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya
Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake.
Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Utaratibu
wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu
kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu
akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu
Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kinyume chake
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Juni, 2016
JANNY SIKAZWE WA ZAMBIA KUAMUA MCHEZO WA YOUNG AFRICANS NA TP MAZEMBE
Mchezo
wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya
Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia.
Sikazwe atasaidiwa na Jarson
Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line
1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2)
huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna wa
mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo
utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.
Wakati huo huo Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limekataa ombi la Young Africans ya Dar es
Salaam juu ya kubadili siku na muda wa mchezo dhidi ya T.P. Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika taarifa ya CAF iliyofika
TFF imesema mchezo huo utafanyika Jumanne Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni
kama ulivyopangwa awali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Young
Africans kwa upande wao waliomba mchezo huo ufanyike Juni 29, 2016 saa
1.30 usiku.
Kadhalika, kikao cha maandalizi
katika mchezo huo kiliochofanyika leo Juni 23, 2016 kimeagiza uongozi wa
Young Africans kuwaelimisha mashabiki wao kukaa katika eneo la mazoea
tofauti na mipango yao ya kutaka kukaa eneo lote la Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
SHELISHELI KUTUA USIKU HUU
Timu
ya soka ya Vijana ya Shelisheli, inatarajiwa kuingia Dar es Salaam,
Tanzania kesho saa 7.45 usiku (usiku wa kuamkia Ijumaa Juni 24, 2016),
kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini
ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa
10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo inaingia wachezaji na
pamoja na viongozi 25 ka ujumla wake na itafikia hoteli ya Southern Sun
iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia,
ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana
wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli
utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi
ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya
miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa
kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na
Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma
Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini
tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika
Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo
wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2,
2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo,
Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya
vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu
katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WANASAYANSI
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano
wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa
na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye
ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano
wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa
na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye
ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wasomi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa
wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha
Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)
uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
Sehemu
ya walohudhuria wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa
wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha
Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa
wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari mara
baada ya kufungua mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na
nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili
(MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF
jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na
viongozi pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba mara
baada ya kufungua mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani
na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili
(MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF
jijini Dar es salaam .
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Alex Msama: Amwangukia Mwakyembe, asema “Nakuomba radhi”
Bw
. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomuomba
Radhi Mh. Dk. Harisson Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba kutokana na
Gazeti la Dira analomiliki kumuandika vibaya.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
MFANYABIASHARA Alex Msama
amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe
kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania
analolimiliki.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.
Habari nyingine ambayo imeonekana
kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2
ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.
Alisema yeye kama mmiliki wa
gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza
anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe.
Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.
“Nimesikitishwa na habari hii kwa
kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari, ilihukumu na
kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe,
ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,”
alisema Msama.
Aidha Msama alisema hatua
nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa
Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha
habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.
Alisema Mkama alipaswa
kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo
anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.
“Mimi ni mfanyabiashara sijui
mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa
chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza
Msama.
Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni 27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.
Hivi karibuni Waziri Mwakyembe
aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa
habari mbili za gazeti hilo iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya
Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na
kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.
BENKI YA BARCLAYS YAFUNGUA TAWI JIPYA LA CITY MALL JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na Mtendaji Mkuu
Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na
bashara wa benki hiyo, Roy Ross wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa
kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini
Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na Mtendaji Mkuu
Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na
bashara wa benki hiyo, Roy Ross pamoja na viongozi wengine wakifurahia
mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa kufunguliwa tawi la
benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na Mtendaji Mkuu
Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na
bashara wa benki hiyo, Roy Ross wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wafanyakazi mara baada ya uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya
Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na Mtendaji Mkuu
Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na
bashara wa benki hiyo, Roy Ross wakifurahia jambo kwenye kaunta ya
kuchukua na kuweka fedha mara baada ya uzinduzi wa kufunguliwa tawi la
benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo
Baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali vya benki ya Barclays Tanzania wakiwa katika uzinduzi huo leo.
Mtendaji
Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na
bashara wa benki hiyo, Roy Ross akizungumza na wafanyakazi wa benki ya
Barclays hapa nchini pamoja na wateja wakati wa uzinduzi wa tawi jipya
la benki hiyo katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed nakizungumza
wakati wa uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo
la City Mall jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa Benki hiyo Afrika na Tanzania wakiwa katika meza kuu.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi huo.
According to the Finance and Planning
Minister, Dr Phillip Mpango, the move will enable Tanzanians own shares
in listed communication companies. A heated debate ensued after Nzega
Urban MP Hussein Bashe (CCM) moved a motion to oppose the proposal for
mandatory listing at the DSE of shares for communication companies.
Despite clarification from the Finance
and Planning Minister, Dr Mpango and Attorney General George Masaju, the
legislator stuck to his guns. He demanded the government to scrap
section 26 of the Electronic and Postal Communication that establishes
mandatory listing of shares for mobile phone companies, asserting that
the firms could take the matter to the international tribunal court.
The decision had to be reached by voice
vote, with the majority voting in favour of the government’s amendment.
Responding to Bashe’s motion, Dr Mpango explained that the mandatory
listing of shares was not a new aspect as it was established in Section
26 of the Electronic and Postal Communication Act, 2010.
He noted that the mobile phone companies
were required within three years from the commencement of the Act, to
offer shares to the public and subsequently list with the stock
exchange, something that the firms didn’t comply.
“The amendment now makes it mandatory
for these companies to list with the stoke exchange. This is very
important as it would help the government trace the exact revenue
generated by these companies,” Dr Mpango said.
The new Finance Bill which also offers
legal cover to budgetary proposals for the next financial year, provides
for the amendment of 16 laws that seek to impose and alter certain
taxes, duties, levies and fees.
The Bill also proposes amendments to
other written laws relating to the collection and management of public
revenue. In his speech, Dr Mpango asserted that the Bill among other key
objectives, is intended to get rid of costly tax exemptions and retain
tax exemptions that are beneficial to the country and should stimulate
the growth of local industries.
He said the Bill is also envisaged to
boost government revenues and promote economic growth especially in the
industrial sector, agriculture, transportation and job creation. To
achieve that, the Finance minister said he had proposed amendments to
the Excise Management Act, Cap. 147.
“The Bill intends to amend specific
rates for some excisable items in order to protect our currency. The
rate for imported furniture is also increased from 15 to 20 per cent in
order to protect our local industry and increases job creation.”
The Bill proposes amendments in the
Income Tax Act, Cap. 339. Section 86 of the Act has been amended to make
compulsory the use of EFD machines and establish penalties for non-use
of the EFDs and for not demanding receipts.
Furthermore, the Finance Bill seeks to
introduce a special income taxation regime from prospecting and mining
and petroleum operations to increase government revenue.
Debating the bill earlier, most MPs
emphasized on the importance of increasing tax collection to enable the
government to implement its development plans. Mkuranga lawmaker
Abdallah Ulega (CCM) urged the government to enlighten the public on the
use of Electronic Fiscal Devices (EFDs) and possible penalties for
non-compliance.
“I believe that a patriotic Tanzanian is
one who pays tax, but it’s important to provide education so that the
public can comprehend the importance of paying taxes,” Mr Ulega said. He
advised the taxman to introduce a bonus for good taxpayers.
Mr Ally Keissy (Nkasi North-CCM) called
for tax extension, arguing that everyone, including small income
earners, livestock keepers and all others in the society be subjected to
paying taxes
No comments :
Post a Comment