Pages

Friday, June 24, 2016

SERIKALI YASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA BILIONI 440 NA BENKI YA DUNIA


BEN1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kushoto), wakisaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
BEN2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird wakibadilishana Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II, Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
BEN3 
Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine wakifuatilia  maelezo  ya Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
BEN4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Makubaliano yaliyofanywa kati ya Tanzania na Benki ya Dunia ya ili kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II.  Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
BEN5 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akibadilishana mawazo na  Mratibu Maendeleo ya Sekta Binafsi na SAGCOT kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza kusaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II.  Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam 
……………………………………………………………………………………………………………………..
Benny Mwaipaja
Kaimu Msemaji Wizara ya Fedha na Mipango
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini hati ya makubaliano na Benki ya Dunia itayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya fedha katika mradi wa Tasaf kiasi cha Shilingi Bilioni 440.
Hati hiyo ilisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, Dar es Salaam, leo, Juni 23, 2016.
Akiongea wakati wa kusaini hati hiyo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika mradi wa Tasaf II kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kukuza kipato chao kupitia ajira za muda zitakazowawezesha kupeleka watoto shule na kuwapatia huduma za afya.
Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imefanya kazi kubwa iliyowezesha miradi kumi kupitishwa ambayo ina thamani ya Shilingi Trilioni 1.9.
“Miongoni mwa miradi iliyopata ufadhili ni pamoja na mradi wa kuboresha mazingira ya biashara uliopata shilingi Bilioni 168, mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA), uliopata Shilingi Bilioni 440” Aliongeza Dkt. Likwelile
Aidha, alisema kuwa Serikali inaendelea na majadiliano na Benki hiyo kwa ajili ya kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, ambapo kiasi cha dola Milioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Dkt. Likwelile ameishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake mkubwa na kusema kuwa Serikali itahakikisha kuwa inazisimamia taasisi zinazotekeleza miradi hiyo ili ziweze kutumia fedha hizo vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird, amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa  na kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi.
Aliongeza kuwa sekta binafsi ndizo zinatoa ajira kwa wingi na kusaidia kuchangia katika kuongeza mapato ya Serikali.
Ameahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuiwezesha kufikia malengo yake ya kiuchumi na kijamii kwa faida ya wananchi wake.

 

TANZANIA BADO INAHITAJI WATAALAM WALIOBOBEA KATIKA BIASHARA YA KIMATAIFA

 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
Mmoja wa washiriki wa Mkutano huo akichangia wakati wa Mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano kuhusu program mpya mbili za masomo katika ngazi ya
Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na CBE.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema akiwa katika picha ya pamoja  na wadau mbalimbali waliohudhuria katika chuo hicho kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika
Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
 ……………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa Dar es salasam.
 
Tanzania bado inahitaji wataalam waliobobea katika Biashara ya Kimataifa na wale wanaosimamia mfumo wa uzalishaji, usambazaji na utunzaji  wa bidhaa mbalimbali hususan mazao ya chakula ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya uagizaji, utunzaji, usambazaji na hasara ya kuharibika  kwa mazao inayowakumba wafanyabiashara walio wengi kabla ya kufikisha bidhaa zao kwa walaji.
 Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters)katika Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
 Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo zinazowakumba wakulima na wafanyabiashara walio wengi hasa wale wa matunda ambao hupoteza karibu asilimia 40 ya mazao yao, lazima hatua madhubuti zichukuliwe kwa kuwajengea
uwezo wa kitaalamu vijana wa Kitanzania ambao wataweza kukabiliana na changamoto ya wakulima kupata hasara kwa kuhakikisha mazao yanayotoka kwenye maeneo ya uzalishaji yanafika yakiwa salama.
Leo tuna mkutano wa wadau kwa sababu CBE tuko katika hatua za mwisho za mchakato wa kuanzisha Programu mpya za Shahada za uzamili katika katika masuala ya Ugavi (Procurement and Supply Chain Management) pia Shahada ya
Uzamili katika Biashara ya Kimataifa (International Business Management) ili tuweze kutoa mafunzo yatakayowasaidia watanzania
’’
Amebainisha kuwa mazao kama matunda mara nyingi yamekuwa yakiharibika katika hatua ya kuvunwa, kusafirishwa na
kuhifadhiwa jambo linalowasababishia hasara wakulima pamoja na wasafirishaji kwa kuwa hawana ujuzi na utalaam wa usimamizi wa bidhaa na mazao yao.
Aidha, ameongeza kuwa asilimia 40 ya gharama hizo hutumika katika masuala ya usafirishaji na  ufuatiliaji wa bidhaa husika kuifikisha kwa mlaji na kusisitiza kwamba gharama hizo husababishwa na mfumo mzima unaopaswa kupitiwa kabla ya kuifikisha bidhaa husika sokoni jambo ambalo lingerekebishwa kwa kuwa na wataalam wa kutosha kusimamia sekta hiyo.

Bunge lapitisha muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka 2016

bunge-1-3————————————————————-
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha muswada wa sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ili kuwezesha utekelezaji wa  bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Muswada huo umepitishwa na Bunge pamoja na marekebisho yake ambayo yametolewa na kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti na wabunge.
Marekebisho yaliyofanyika katika muswada huo ni pamoja na kutoongeza ushuru wa kuingiza sukari ya viwandani kutoka asilimia 10 kwenda 15 ambapo kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti ilishauri Serikali isiendelee na pendekezo hilo kutokana na hatua hiyo kuwa na athari  kwa viwanda vinavyotumia sukari viwandani kama malighafi ya kuzalisha bidhaa nyingine kama juisi na soda.
“Serikali imekubali pendekezo lililotolewa na kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti ya kutoongeza ushuru wa kuingiza sukari ya viwandani kutoka asilimia 10 kwenda asimilia 15, hivyo kuendelea kutoza asilimia 10 iliyokuwepo kwa mwaka huu wa fedha,” alifafanua Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Marekebisho mengine yaliyofanyika ni pamoja na kuondoa adhabu ya kifungo cha miezi Sita kwa wale ambao hawatodai risiti baada ya kununua bidhaa au huduma na kubaki na adhabu ya kulipa faini kulingana na thamani ya bidhaa.
Aidha Mhe. Mpango amesema kuwa muswada huo umezingatia kwa kiwango kikubwa mapendekezo ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, wamiliki wa viwanda, wafanyabiashara na taasisi za Serikali.

MRADI WA PS3 WAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA WASIMAMIZI RASILIMALI WATU

Mkurugenzi wa Mradi wa PS3 Dk. Emmanuel Malangalila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyo wakutanisha pamoja wataalam mbalimbali wanaohusika na usimamizi wa rasilimali watu kutoka katika mikoa na tasisi za serikali ili kupata kitini cha kutolea mafunzo kwa watumishi wapya wanaoajiriwa serikalini. Mafunzo hayo yanafanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani. 
 
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nchini ambao unatekelezwa katika mikoa 13 na kuzinufaisha halmashauri 97. 
Baadhi ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa, Miriam Mmbaga akifuatiwa na Beatice  Kimoleta
Washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira yeyote. 
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Rasilimali wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)  Josephine Kimaro akitoa mafunzo kwa viongozi wa sekta ya Afya waliojitokeza kushiriki semina hiyo mjini Bagamoyo mkoani Pwani. 
Washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira yeyote. 
Continue reading →

MTOTO LUQMAN ALLY AMEPOTEA NA ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

Luqman Ally (14) anatafutwa na wazazi wake, amepotea tarehe 13 Juni mwaka huu, anasoma shule ya Msingi Mbagala Islamic Darasa la Sita iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mara ya kwanza alitoroka wiki mbili zilizopita na akapatikana katika kituo cha kulelea
watoto wanaoishi katika mazingira Magumu cha Chad kilichopo Mazese.
Taarifa imetolewa katika kituo cha Polisi cha Majimajitu Mbagala jijini Dar es Salaam
kwa  RB .NO MAT/RB/618/16.
Yeyote ambaye atamwona mtoto huyo apige
NAMBAYA YA
SIMU. 0655891200. MAMA YAKE MZAZI WA LUQMAN.

SERIKALI yawataka wazalishaji wa vyakula, vinywaji na viwanda vya mikate kuzingatia ubora

indexNa Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imewataka wazalishaji wa vyakula, vinywaji na viwanda vya mikate,kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango kwa  kutambua kuwa hiki ni kipindi cha utandawazi ambacho kina ushindani mkubwa vinginevyo watashindwa kuzalisha na kupata masoko ya uhakika.
Rai hiyo imetolewa jana na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, alipokuwa akifungua mafunzo ya uelimishaji ,wazalishaji wa vyakula,kuhusu umuhimu wa kuzalisha bidhaa bora zenye viwango sanjari na kuzingatia usalama wa vyakula na afya ya mlaji,mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA, kanda ya kaskazini..
Kwitega,alisema kuwa serikali inatambua zipo changamoto mbalimbali katika kipindi hiki cha utandawazi  na biashara huria hivyo hakuna mzalishaji ambae ataweza kudumu katika biasharabila kuhakikisha kuwa bidhaa inayozalishwa inakidhi vigezo vya ubora wa viwango na usalama kwa afya ya mlaji.
Kwitega, alisema wazalishaji hao watazishinda changamoto hizo ikiwa iwapo watazalisha bidhaa zenye ubora na viwango katika mazingira  ya ushindani vinginevyo tuaishia kununua bidhaa toka nje kwa kuwa bidhaa zetu zimeshindwa kukidhi ushindani wa ubora .
Alisema ,suala la usalama wa vyakula  ni la msingi  kwa sababu linaathari kubwa kiafya ,kiuchumi,na kijamii,kwa  sababu hiyo wao wakiwa ni wadau muhimu   wana wajibu mkubwa wa kufanikisha lengo  la kuimarisha usafi sehemu zao za uzalishaji.
‘’Ninasema tatizo kubwa na sugu ni baadhi yanu  wazalishaji ambao wamekuwa hawazingatii usafi kwenye maeneo yao ya uzalishaji hivyo lazima wazalishe kwa kulinda afya za walaji’’alisema Kwitega.
Alisema kuwa mamlaka ya chakula na dawa TFDA,ina jukumu la kudhibiti uhifadhi,usafirishaji ,usindikaji, uangalizaji na usambazaji wa vyakula pamoja na kusajili majengo yote yanayotumika kwenye uzalishaji wa vyakula na utoaji wa vibali vya kusindika uingizaji wa bidhaa nje.
Alisema kama taasisi ya udhibiti vyakula  ina wajibu wa kuwasaidia wazalishaji ili waweze kukua,na kuzalisha vyakula kwa mjibu wa sheria  na kanuni  bora za uzalishaji  ili waweze kumudu  ushindani wa soko la ndani na je .
Kuhusu viwanda, Kwitega, amesema sera ya serikali  ni kuongeza na kukuza viwanda kwa kuwa viwanda vina nafasi kubwa ya kuchangia kwenye pato la taifa na vinaweza  kuleta mchango wa athari  za kiafya ikiwa bidhaa zake hazitakidhi viwango vya ubora na usalama.
Awali meneja wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA, kanda ya kaskazini, Damasi Matiko,mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa awamu ni mwendelezo ili kuwajengea uwezo wazalishaji hao waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuhimili ushindani kwenye masoko.
Alisema kuwa tangia mafunzo hayo yaanze kutolewa  makundi mbalimbali ya wazalishaji hao wameongeza viwango vya ubora wa bidhaa zao tofauti na miaka iliyopita ambapo viwanda vyetu vilivkuwa  havifanyi vizuri  na matokeo yake kulazimika kutumia bidhaa toka nje.
Matiko, alisema TFDA, itaendelea kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya wazalishaji ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa bora hivyo kuepuka kuzalisha bidhaa hafifu ambazo zitawakosesha masoko .
 Alisema kuwa TFDA, inashirikiana na shirika la viwanda vidogo ,SIDO na shirika la viwango nchini TBS, katika kutoa elimu kwa wazalishaji mbalimbali ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora waweze kupata masoko ya ndani na nje na kujiongezea vipato.

DK. MENGI ACHANGIA MADAWATI 1,000, ATOA SOMO KWA WATU MATAJIRI

Katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika wilaya hizo.
 
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi pesa hizo kwa wakuu wa wilaya wa kampuni hizo, Dk. Mengi alisema ni muhimu kwa watanzania kuungana kwa pamoja na kusaidia kupatikana kwa madawati kwani kwa kufanya hivyo ni kulisaidia taifa.
 
Hata hivyo Dk. Mengi alisema kuwa anaamini kama watu matajiri nchini wakiungana kwa pamoja na kujadili jinsi ya kumaliza tatizo la madawati nchini basi jambo hilo litaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka tofauti na sasa ambapo linakwenda kwa mwendo wa kusuasua.
 
“Ukisaidia mtu mmoja katika elimu ni sawa umesaidia jamii na taifa kwa ujumla kama watu matajiri wakisema wakae kwa pamoja na kuangalia jinsi ya kumaliza tatizo hili linaweza kutatuliwa na shida ya madawati kumalizika.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza katika halfa ya kukabidhi milioni 70 kwa wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo zitawezesha wilaya hizo kununua madawati 1,000 na kila wilaya kupata madawti 500.
 
“Matajiri wanatakiwa kutambua kuwa wanatakiwa kurudisha shukrani zao kwa Mungu, taifa na wananchi na hasa kwa walio na hali ya chini kwani hao ndiyo wanaowasaidia kufanya biashara zao kwa amani,” alisema Dk. Mengi.
 
Aidha amewataka wakuu wa wilaya hizo kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kama watakuwa hawajakamilisha na wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuongeza juhudi huku akiwashauri kuandaa mikutano katika wilaya zao na kushirikisha wananchi wao ili waweze kuchangia na hatimaye tatizo hilo kumalizika.
 
Kwa upande wa mkuu w wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga na mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab wamemshukuru Dk. Mengi kwa msaada ambao amewapatia na kuwataka watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama jinsi amevyofanya Dk. Mengi kwa kuchangia upatikanaji wa elimu bora.
 
Awali kabla ya msaada ambao umetolewa na Dk. Mengi, wilaya ya Bagamoyo ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa madawati 2,463 na Handeni ikikabiliwa na tatizo la upungufu wa madawati 4,000.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab akizungumza katika halfa hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga akizungumza katika halfa ya kupokea pesa kwa ajili ya madawati 500 yatakayokwenda katika wilaya yake kusaidia kupunguza tatizo la madawati.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisaini mfano wa hundi kabla ya kuanza kuwakabidhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Kenneeth Haule, Mwenyekiti wa Mji wa Handeni, Twaha Mgaya na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Handeni, Ramadhani Diliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 500, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Chalinze, Edes Lukoa, Mkurugenzi wa Bagamoyo, Natujwa Melau, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Issa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu.

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya TBS na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
TZ 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake.
Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Jiolojia  katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Utaratibu wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinyume chake
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Juni, 2016

JANNY SIKAZWE WA ZAMBIA KUAMUA MCHEZO WA YOUNG AFRICANS NA TP MAZEMBE

images 
Mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia.
Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.
Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limekataa ombi la Young Africans ya Dar es Salaam juu ya kubadili siku na muda wa mchezo dhidi ya T.P. Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika taarifa ya CAF iliyofika TFF imesema mchezo huo utafanyika Jumanne Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kama ulivyopangwa awali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Young Africans kwa upande wao waliomba mchezo huo ufanyike Juni 29, 2016 saa 1.30 usiku.
Kadhalika, kikao cha maandalizi katika mchezo huo kiliochofanyika leo Juni 23, 2016 kimeagiza uongozi wa Young Africans kuwaelimisha mashabiki wao kukaa katika eneo la mazoea tofauti na mipango yao ya kutaka kukaa eneo lote la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SHELISHELI KUTUA USIKU HUU

IMA 
Timu ya soka ya Vijana ya Shelisheli, inatarajiwa kuingia Dar es Salaam, Tanzania kesho saa 7.45 usiku (usiku wa kuamkia Ijumaa Juni 24, 2016), kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo inaingia wachezaji na pamoja na viongozi 25 ka ujumla wake na itafikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WANASAYANSI

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
S1 
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.

  Baadhi ya Wasomi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)
uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
 Sehemu ya walohudhuria wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
S2 
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba mara baada ya kufungua  mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam .
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Alex Msama: Amwangukia Mwakyembe, asema “Nakuomba radhi”

1a 
Bw . Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomuomba Radhi Mh. Dk. Harisson Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba kutokana na Gazeti la Dira analomiliki kumuandika vibaya.
………………………………………………………………………………………………………..

Na Mwandishi Wetu
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.
Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.
Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe.
Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.
“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari,  ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.
Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.
“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.
Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni  27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.
Hivi karibuni  Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo  iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.

BENKI YA BARCLAYS YAFUNGUA TAWI JIPYA LA CITY MALL JIJINI DAR ES SALAAM

1Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross  wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.
2Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross pamoja na viongozi wengine wakifurahia mara baada ya  kukata utepe kuashiria uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.
3Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi mara baada ya uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.
5Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross  wakifurahia jambo kwenye kaunta ya kuchukua na kuweka fedha mara baada ya uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo
6 
Baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali vya benki ya Barclays Tanzania wakiwa katika uzinduzi huo leo.
7 
Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini pamoja na wateja wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam. 8Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  nakizungumza wakati wa uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.
10
Viongozi wa Benki hiyo Afrika na Tanzania wakiwa katika meza kuu.
11 
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi huo.

TUME YA UCHAGUZI YAKABIDHI TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015

IMG-20160623-WA0021 IMG-20160623-WA0022

THE National Assembly yesterday passed the Finance Bill, 2016, requiring electronic communication companies registered in the country to float their stakes on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE), within six months from July 1, this year.

According to the Finance and Planning Minister, Dr Phillip Mpango, the move will enable Tanzanians own shares in listed communication companies. A heated debate ensued after Nzega Urban MP Hussein Bashe (CCM) moved a motion to oppose the proposal for mandatory listing at the DSE of shares for communication companies.
Despite clarification from the Finance and Planning Minister, Dr Mpango and Attorney General George Masaju, the legislator stuck to his guns. He demanded the government to scrap section 26 of the Electronic and Postal Communication that establishes mandatory listing of shares for mobile phone companies, asserting that the firms could take the matter to the international tribunal court.
The decision had to be reached by voice vote, with the majority voting in favour of the government’s amendment. Responding to Bashe’s motion, Dr Mpango explained that the mandatory listing of shares was not a new aspect as it was established in Section 26 of the Electronic and Postal Communication Act, 2010.
He noted that the mobile phone companies were required within three years from the commencement of the Act, to offer shares to the public and subsequently list with the stock exchange, something that the firms didn’t comply.
“The amendment now makes it mandatory for these companies to list with the stoke exchange. This is very important as it would help the government trace the exact revenue generated by these companies,” Dr Mpango said.
The new Finance Bill which also offers legal cover to budgetary proposals for the next financial year, provides for the amendment of 16 laws that seek to impose and alter certain taxes, duties, levies and fees.
The Bill also proposes amendments to other written laws relating to the collection and management of public revenue. In his speech, Dr Mpango asserted that the Bill among other key objectives, is intended to get rid of costly tax exemptions and retain tax exemptions that are beneficial to the country and should stimulate the growth of local industries.
He said the Bill is also envisaged to boost government revenues and promote economic growth especially in the industrial sector, agriculture, transportation and job creation. To achieve that, the Finance minister said he had proposed amendments to the Excise Management Act, Cap. 147.
“The Bill intends to amend specific rates for some excisable items in order to protect our currency. The rate for imported furniture is also increased from 15 to 20 per cent in order to protect our local industry and increases job creation.”
The Bill proposes amendments in the Income Tax Act, Cap. 339. Section 86 of the Act has been amended to make compulsory the use of EFD machines and establish penalties for non-use of the EFDs and for not demanding receipts.
Furthermore, the Finance Bill seeks to introduce a special income taxation regime from prospecting and mining and petroleum operations to increase government revenue.
Debating the bill earlier, most MPs emphasized on the importance of increasing tax collection to enable the government to implement its development plans. Mkuranga lawmaker Abdallah Ulega (CCM) urged the government to enlighten the public on the use of Electronic Fiscal Devices (EFDs) and possible penalties for non-compliance.
“I believe that a patriotic Tanzanian is one who pays tax, but it’s important to provide education so that the public can comprehend the importance of paying taxes,” Mr Ulega said. He advised the taxman to introduce a bonus for good taxpayers.
Mr Ally Keissy (Nkasi North-CCM) called for tax extension, arguing that everyone, including small income earners, livestock keepers and all others in the society be subjected to paying taxes

No comments:

Post a Comment