Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akisalimiana na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya
Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam
leo Juni 22, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa
katima mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki
ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es
salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Balozi wa China nchini Dkt. Dkt. LU
Younqing,
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akiagana na Balozo wa China nchini Dkt Lu Younqing baada ya kuwa na
mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia
Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo
Juni 22, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizarta ya Viwanda na
Biashara Dkt. Adelhem James Meru na Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Asia
katika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Mbelwa kairuki.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius
Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya
Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na Mkuu
Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Gavana wa Benki Kuu
ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar e3s salaam Mhe
Paul Makonda kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania
kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania
kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akibofya kitufe kuashiria uzi8nduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 50 ya
benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo
Juni 22, 2016
KAMISHNA MSTAAFU SULEIMAN KOVA AAGWA RASMI KIJESHI BAADA YA KUSTAAFU
Kamishna
Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa,
wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga
rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi
Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Kamishna
Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu
lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa sherehe za kumuaga rasmi
Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta
Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Maofisa
wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi
la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi
wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi
zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Gari
maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova
likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika
katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa
Polisi, Abdulrahman Kaniki (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Gwaride
Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake
kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya
kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Gwaride
Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake
kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya
kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
SADC kudumisha usalama katika usafiri wa Anga.
Waziri wa Kazi, Usafiri na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa akiongea na wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) hawap[o pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19 wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi
zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimia kuimarisha usafiri wa anga
ili luleta huduma bora na kuwapa amani wananchi wanaotumia usafari wa
anga katika Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Makame Mbarawa alipokuwa
akifungua Mkutano wa 19 wa Kamati ya SADC ya usafiri wa Anga
uliofanyika jijini Dar es salaam.
“Mkutano huu unalenga kuadhimia
kuimarisha usalama wa anga katika nchi za Jumuiya ya SADC, kwa kuwa
unahitajika sana kwa wananchi ili kuongeza shughuli za kiuchumi na
kijamii na kuleta maendeleo ya nchi wanachama” alisema Mbarawa
Ameongeza kuwa “ni lazima
tuadhimie mambo yatayoleta maendeleo na huduma bora katika usafiri wa
anga kwa jumuiya ya SADC ili kujenga uhusiano na malengo yaliyo bora kwa
maendeleo ya nchi zetu.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bwana Hamza Johari amesema kuwa
mkutano huo unalenga kuhakikisha wanafikia na kutekeleza malengo
Jumuiya ya usafiri wa anga wa kimataifa (ICAO) katika kuboresha huduma
za usafiri huo.
“Ni lazima tuyafanyiekazi
maadhimio ya mkutano huu ili kuboresha huduma kwa kiwango cha
kimataifa pamoja na kuleta unafuu kwa watumiaji wa usafiri wa anga”
alisisitiza Bw. Johari.
Naye, Mwenyekiti wa SADC Bw.
Geoffrey Moshabesha amesema kuwa kamati hiyo inajipanga kuunda taasisi
ya kiusalama ili kusimamia mifumo yote kwa nchi nzima ili kuweka
mazingira mazuri kwa watumiaji wa usafiri wa anga.
Jumuiya ya SADC imeweka mikakati
ya kutekeleza maadhimio hayo katika kuleta usalama wa anga pamoja na
kutunza mazingira ili kuboresha huduma kwa watumiaji wa usafiri wa anga
kwa nchi wanachama.
SERIKALI YAIMARISHA UDHIBITI WA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI NA BIASHARA YA MADINI
Kaimu
Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw.
Gilay Shamika akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye wakala hiyo ikiwemo kuongezeka
kwa makusanyo ya mirabaha kwenye shughuli za uzalishaji na uuzaji wa
madini nchini. Kulia ni Msemaji wa Wakala hiyo Bw. Yisambi Shiwa.
Msemaji
wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Yisambi Shiwa
akiwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam namna
walivyoimarisha udhibiti wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini
kwa kuongeza wakaguzi migodini na vituo vya ukaguzi kwenye maeneo
mbalimbali na kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia
uhifadhi wa mazingira. Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa TMAA, Bw. Gilay
Shamika na kulia ni Mwanasheria Bw. Gimonge Ngutunyi.
PICHA NA FATMA SALUM (MAELEZO)
Lukuvi atoa siku 10 kwa watendaji wa Wizara kushughulikia suala la Makazi Magomeni.
Jonas Kamaleki, MAELEZO
——————————
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi ametoa siku 10 kwa watendaji wa
Wizara yake kumshauri ili aweze kutatua mgogoro wa makazi wa watu wa
Kinondoni Quarters.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar
es Salaam wakati Lukuvi na timu ya wataalaam wa Wizara walipokuwa
wakisikiliza malalamiko ya wakazi hao katika Wiki ya Utumishi wa Umma.
“Kazi ya Serikali ya Awamu ya Tano
ni kurekebisha yaliyopinda na kutoa suluhu haraka ili kuwafuta wananchi
machozi,”alisema Lukuvi na kuongeza kuwa Serikali haitaki kuona haki za
wananchi zinacheleweshwa.
Aliongeza kuwa ni nia ya Serikali
kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapatiwa makazi bora kama ilivyo katika
ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015.
Waziri Lukuvi alisema kuhusu
makazi bora, Wizara inafanya mapitio ya Sera ya Makazi ya Mwaka 2010 ili
iweze kwenda na wakati na pia kutengeneza Sera ya Nyumba.
Awali, akitoa malalamiko,
Mwenyekiti wa Kamati wakazi waliovunjiwa nyumba zao, Bw. George Abel
alisema kuwa suala hili limechukua muda mrefu tangu mwaka 2009 hivyo
wanamuomba waziri amshauri Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt John Pombe Magufuli abatilishe umiliki wa ardhi hiyo na kuukabidhi
kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili nyumba zijengwe
na wao wako tayari kununua.
“Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni imeshindwa kujenga kwani tuliahidiwa kuwa mwaka 2011 nyumba
zitakuwa zimekamilika na sisi ndio tutakuwa wapangaji na wanunuzi wa
kwanza, lakini hadi leo ni miaka mitano nyumba hazijajengwa nasi
tunaishi kwa shida,”alisema Abel.
Aidha, Bw. Abel alisema kuwa
wakazi 644 wa Kinondoni Quarters walivunjiwa nyumba zao na Manispaa ya
Kinondoni kwa madai kuwa ni nyumba chakavu na zitajengwa nyumba za
kisasa ambazo watapangishwa na hatimaye kuuziwa jambo ambalo
halijatekelezwa hadi sasa.
WAZIRI WA AFYA , ATEMBELEA VIJIJI VILIVYOKUMBWA NA MLIPUKO WA UGONJWA USIOJULIKANA WILAYANI KONDOA.
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu
amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa
usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.
usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.
Katika ziara hilyo ameambatana na wataalam mbalimbali ambao wameweka kambi kwenye vijiji hivyo ili
kufuatilia wagonjwa majumbani.vile vile ametembelea wagonjwa
waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
kufuatilia wagonjwa majumbani.vile vile ametembelea wagonjwa
waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kondoa.Mhe.Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.
kikao cha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi
(kushoto) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti hiyo ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Mkurugenzi wa
Utawala na Rasimimali watu Bibi Victroria Fovo.
Baadhi
ya wakuu wa Idara wakinukuu hoja na maoni ya watumishi wa Sekretarieti
ya Ajira wakati wa kikao kati ya Katibu wa Sekretarieti hiyo na
Watumishi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Baadhi
ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa
Katibu wa Sekretarieti hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) baada ya
kuwasilisha maoni na ushauri kuhusiana na utendaji kazi wa taasisi hiyo.
Serikali yapokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akikabdhi msaada wa madawati
kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (hayupo pichani) mapema hii
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe.
Jaseem Al Najem wakati akipokea msaada wa madawati toka kwa balozi huyo
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) akikabidhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah
Kilima mapemahii leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga (kulia) wakiwa wamekalia madawati ambayo yametolewa msaada kwa
serikali ya Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati
Balozi Abdallah Kilima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga (Katikati aliyekaa) kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania
Mhe. Jaseem Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati
Balozi Abdallah Kilima wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na
Wakurugenzi toka wizara hiyo mara baada ya kupokea msaada wa madawati
toka ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
———————————————————————–
Na Eliphace Marwa- Maelezo
Serikali
ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait
nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati
katika shule za msingi hapa nchini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati
hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
“Waziri
Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali
ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi
kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema
Balozi Maige.
Balozi
Maigaaliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa
kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na
gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi.
Naye
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa
Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania
kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.
Aidha
Balozi Maiga alitumia muda huo kutoa taarifa kwa waandishi wa habari
kuhusu ujio wa Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini siku ya Julai
Mosi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi.
“Rais
wa Rwanda atawasili hapa nchini Julai Mosi na ataweka saini makubaliano
mbalimbali waliyofikia kati ya Tanzania na Rwanda baada ya hapo Rais
Kagame ataambatana na mwenyeji wake Rais Magufuli mpaka katika viwanja
vya maonesho vya Sabasaba ambapo Rais Kagame atayazindua rasmi maonesho
hayo ya arobaini”, alisema Balozi Maiga.
Aidha
Balozi Maiga aliongeza kuwa Rais Kagame jioni atakaribishwa Ikulu na
mwenyeji wake Rais Magufuli kwa ajili ya dhifa ya kitaifa.
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Utumishi na Utawala Bora, George
Simbachawene (wapili kulia) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu,Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama
watatu kulia) bungeni mjini Dodoma Juni 22, 2016. Wengine kutoka
kushoto ni Mbunge wa Babati Vijijini Jitu Vrajlal Son, , Mbunge wa
Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza,Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde,
Mbunge wa Korogwe Stephen Ngonya na Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wananchi kutoka
jimbo la Ukongwa waliotembeklea bunge kwa mwaliko wa Mbunge (wapili
kulia) Juni 22, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais ,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Utumishi, na Utawala Bora , George
Simbachawene (kulia) na Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay
(kushoto) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 22, 2016. Wapili
kushoto ni Mosses Kirway na wapili kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu
yaTaifa ya CCM, Thomas Lulu, wote wakiwa ni wageni waliotembelea Bunge
wakitoka Mbulu.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Magari yanayoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi kuwa na namba na rangi maalum
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
———————————–
Katika kuthibiti matumizi ya
magari yanayoingia Nchini kwa msamaha wa kodi Serikali imesema kuanzia
Julai Mosi magari hayo sasa yatakuwa na namba na rangi maalum.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari mjini Dodoma kuhusu tamko la kuondoa misamaha ya kodi kwenye
taasisi za dini kwa kuwa zinatoa huduma za kijamii kama shule na
hospitali.
“Kwa kutambuua mchango mkubwa wa
Taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu na afya,
napendekeza kufuta utaratibu niliotangaza katika hotuba ya bajeti na
badala yake Serikali itaimarisha zaidi hatua mbalimbali za uthibiti
misamaha ya kodi ikiwemo magari yaliyoingia kwa msamaha wa kodi kuwa na
namba na rangi maalum,” alifafanua Mhe.Dkt. Mpango.
Aliendelea kutaja hatua nyingine
kuwa ni taasisi za kidini kuwasilisha vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa
kutoka nje ya nchi kila mwazo mwa mwaka wa kalenda na kuthibitisha kama
vifaa vilivyopewa msamaha mwaka uliopita vilitumika kama sheria
inavyotaka.
Pia, kuwasilisha majina ya watu
walioidhinishwa na Shirika au Taasisi kuandika barua ya kuomba msamaha
wa kodi, wakiainisha cheo, saini, picha, anwani na namba zao za simu ili
kuiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania kufuatilia bidhaa zilizoombewa na
kupewa msamaha kama zimepata kibali cha taasisi hizo.
Vile vile taasisi hizo zinatakiwa
kupata barua kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa na Mkuu wa
Wilaya mahali Taasisi au Mradi unaotekelezwa ulipo.
Mhe. Mpango amesema kuwa hatua
hizo zimekuja kutokana na bidhaa zinazoombewa msamaha wa kodi kutumika
tofauti na kusudi la msamaha huo.
Aidha ametoa tahadhari kwa
mashirika ya kidini kuanzia sasa, kuhakikisha kuwa yanafuata taratibu
zote na Kuzingatia masharti ya msamaha unaotolewa ili kuepuka kufutiwa
leseni zao pale zitakapokwenda kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa.
Wizara ya Ardhi kubaini taasisi zinazodaiwa fidia na wananchi
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
————————————
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kipindi cha mwaka wa
fedha 2016/2017 itabaini taasisi zote na watu binafsi wanaodaiwa fidia
na wananchi ili waweze kulipa fidia hizo.
Akiongea
leo Bungeni, mjini Dodoma Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Angelina
Mabula amesema kuwa ni kweli tatizo hilo lipo na tayari Serikali
imechukua hatua kwa kuzielekeza Halmashauri zote na taasisi nyingine
kulipa fidia stahiki kwa wananchi pale wanapotaka kutwaa maeneo yao.
Mhe.
Mabula amesema kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikichukua mashamba ya
wananchi na kushindwa kuwalipa fidia hivyo kulimbikiza madeni hayo kwa
muda mrefu hali inayokwamisha shughuli za maendeleo.
“Halmashauri
za Wilaya, Taasisi na Maafisa Ardhi hawaruhusiwi kuchukua mashamba ya
wananchi kabla hawajakamilisha utaratibu wa malipo ya fidia kwa wananchi
hao, ili kuondokana na malimbikizo ya madeni ya fidia ambayo malipo
yake huchukua muda mrefu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi,”
alisema Mhe. Mabula.
Aidha
Mhe. Mabula amewataka wananchi wanaodai fidia kuwa wavumilivu wakati
Wizara yake inaendelea kufanya upembuzi wa taasisi hizo ili ziweze
kulipa fidia zote zinazodaiwa na wananchi.
Vilevile
Wizara hiyo imetoa ramani za mitaa kwa wenyeviti wa mitaa wa Jiji la
Dar es Salaam ili wenyeviti hao waweze kutambua matumizi ya maeneo yao,
kwa mfano maeneo ya wazi, na nini kijengwe katika maeneo yao kama vile
nyumba fupi au ndefu, hoteli au chuo ili kuondokana na migogoro ya
kubolewa nyumba kwa kujenga eneo lisiloruhusiwa.
“Tumeanza
kwa mkoa wa Dar es Salaam lakini zoezi litaendelea kila Mkoa na kila
Wilaya Nchi nzima, ili Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji waweze kutambua
matumizi ya maeneo yao, hivyo kuchukua hatua kwa haraka pindi ambapo
maeneo hayo yanatumika tofauti na matumizi yaliyoko” alifafanua Mhe.
Mabula.
Aidha
Mhe. Mabula amezitaka Halmashauri kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi,
Nyumba, na Maendeleo ya Makazi kuwapa uwezo wenyeviti hao ili waweze
kufanya kazi hiyo kiufanisi.
Mkoa wa Kaskazini Pemba imejipanga kuidhibiti hali YA matendo ya hujuma yanavyoendelea.
Na Masanja Mabula –Pemba
——————————–
SERIKALI
ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imeelezea kusiitishwa na matendo ya hujuma
yanavyoendelea kutokea katika Mkoa huo ambapo kwa sasa imejipanga
kuidhibiti hali hiyo kwa nguvu zote ili isiendelea kuleta athari zaidi
kwa wananchi .
Hayo
yamebinishwa na Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis Othman katika kikao cha
Pamoja kati ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama , Maafisa wadhamini wa
Wizara pamoja na wakuu wa Wilaya pamoja na watendaji kutoka Halmashauri
na Baraza la Mji Wete katika Ukumbi wa Jamhuri Wete .
Amesema
uvumilivu na ustahamilivu uliofaywa na Serikali dhidi ya matendo hayo
licha ya kutoa taaluma ya kuachana na matendo hayo kupitia viongozi wa
dini , wanasiasa na watu maarufu lakini imeonekana kwamba vitendo hivyo
vinazidi kushamiri siku hadi siku kwa kuhujumu mali na kutishia usalama
wa wananchi jambo ambalo kwa sasa halikubaliki tena.
Aidha
ameelezea kusikitikishwa na maafia wadhamini kushindwa kuyakemea
matukio hayo licha ya kwamba yanagusa wizara wanazoziongoza huku
akibainisha kwamba baadhi ya watendaji katika wizara hizo wanatumika
kufanya ushawishi wa matendo hayo katika vijiji wanavyoishi .
“Imefika
wakati serikali kuchukua hatua stahiki juu ya wahusika wa matendo hayo ,
kwani inashangaza kwamba tangu yaanze kutokea hakuna Afisa mdhamini
aliyeweza kukemea na imaaminika baadhi ya wafanyakazi wenu wanatumika
kufanya ushawishi ili yaendelee kutokea ”alisema .
Hata
hivyo Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo ,Maliasili , Mifugo na Uvuvi
ameanza kufanya tathmini na mali na mazao yaliyoharibiwa pamoja na
kuwapa misaada ya mbegu na mbolea kwa wakulima waliopata kuharibiwa
mazao yao ili kujiimarisha za shughuli zao za kilimo .
Alisema
wakulima waliopatiwa msaada ni wale wa mpunga , mihogo , viazi na
migomba wakati walioharibiwa mikarafuu na minazi wanasubiri mpaka kuanza
kwa msimu wa mvua za masika ili wawape miche .
“Tayari
sisi Wizara tumewafanyia tathmini wakulima walioharibiwa mazao yao ,
ambapo wengine tumewapa mbegu na mbolea lakini wananchi walioharibiwa
mikarafuu na minazi ambao wao tutawapa miche wakati wa mvua za masika
kuanza ”alieleza.
Hata
hivyo Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Issa Suleiman
Juma aliwataka watendaji wa Wizara ya Kilimo kuharakisha kutoa tathmini
na thamani ya mali zilizo haribiwa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo
vya sheria.
Alisema
, mbali na kuharakisha kutoa tathmini pia aliwataka kuwa tayari kwenda
kutoa ushahidi unapohitajika jambo ambalo litasaidia wahusika kutiwa
hatiani na kukomesha matendo hayo .
CCM YAWASILISHA KWA MSAJILI WA VYAMA HATI NA VIELELEZO VYA MATUMIZI YAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA
Na Bashir Nkoromo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, na kuwa chama cha pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.
Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala Galasia Simbachawene.
Akikabidhi hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25, 2016.
“Sisi hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo haina budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee kuwa chama cha kuigwa “, alisema Mamilo.
Mamililo aliwasilisha hati na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.
Alisema, uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.
Kulingana na Sheria ya Uchaguzi, chama kinatakiwa kisitumie ghara inayozidi sh. bilioni 17, na kikilazimika kuzidi kiwango hicho kisididi zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachotakiwa, huku kwa upande wa wagombea kiasi kinachotakiwa ni sh. bilioni saba na kwa wabunge sh. milioni 33 hadi 88 kulingana na mazingira ya jimbo.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, na kuwa chama cha pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.
Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala Galasia Simbachawene.
Akikabidhi hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25, 2016.
“Sisi hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo haina budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee kuwa chama cha kuigwa “, alisema Mamilo.
Mamililo aliwasilisha hati na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.
Alisema, uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.
Kulingana na Sheria ya Uchaguzi, chama kinatakiwa kisitumie ghara inayozidi sh. bilioni 17, na kikilazimika kuzidi kiwango hicho kisididi zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachotakiwa, huku kwa upande wa wagombea kiasi kinachotakiwa ni sh. bilioni saba na kwa wabunge sh. milioni 33 hadi 88 kulingana na mazingira ya jimbo.
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUKUTANA NA WADAU WAKE KUJIBU KERO MBALIMBALI KUHUSU UTENDAJI KAZI.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
TAARIFA KWA UMMA
Ofisi
ya mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa taarifa kuwa itakutana na wadau
wake wote siku ya ALHAMISI TAREHE 23 JUNI 21016, ili kupokea na
kujibu malalamiko, kero, hoja na maoni mbalimbali kuhusu Utendaji kazi
wa Ofisi ikiwa ni maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma kwa mwaka 2016.
Mkutano
huo utafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana katika
Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.
Wadau wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanaombwa kuhudhuria katika Mkutano huo muhimu.
Imetolewa na: Gerson Mdemu
NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
PROFESA MBARAWA AFUNGUA mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifungua
mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam jana (leo).
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bwana Hamza Johari
akifafanua jambo katika mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam jana
(leo).
Mkuu
wa oganaizesheni ya Usafiri wa Anga kwa nchi za SADC Bwana Geofrey
Moshabesh akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya usalama wa anga
kwa wajumbe wa mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam jana (leo).
Wajumbe
wa Mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
No comments :
Post a Comment