Pages

Wednesday, June 22, 2016

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS NA MCHUMI MKUU WA BENKI YA DUNIA MSTAAFU, AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BENKI KUU YA TANZANIA

 

p1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p2 p3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katima mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Balozi wa China nchini Dkt. Dkt. LU Younqing,
p4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana  na Balozo wa China nchini Dkt Lu Younqing baada ya kuwa na mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizarta ya Viwanda na Biashara Dkt. Adelhem James Meru na Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Asia katika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Mbelwa kairuki.
p5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na  Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar e3s salaam Mhe Paul Makonda  kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p14 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa  maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p13
p7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akibofya kitufe kuashiria uzi8nduzi rasmi wa  maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016

KAMISHNA MSTAAFU SULEIMAN KOVA AAGWA RASMI KIJESHI BAADA YA KUSTAAFU

KOV1 
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV2 
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV3 
Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV4 
Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV5 
Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV6 
Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

SADC kudumisha usalama katika usafiri wa Anga.

index 
Waziri wa Kazi, Usafiri na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa akiongea na wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) hawap[o pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19  wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimia kuimarisha  usafiri wa anga ili luleta huduma bora na kuwapa amani  wananchi wanaotumia usafari wa anga katika Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa  leo na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mheshimiwa  Makame Mbarawa alipokuwa  akifungua  Mkutano wa 19  wa Kamati ya SADC ya usafiri wa Anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
“Mkutano huu unalenga kuadhimia kuimarisha usalama wa anga katika nchi za Jumuiya ya SADC, kwa kuwa unahitajika sana kwa wananchi  ili kuongeza shughuli za kiuchumi na kijamii na kuleta maendeleo ya nchi wanachama” alisema Mbarawa
Ameongeza kuwa “ni lazima tuadhimie mambo yatayoleta maendeleo na huduma bora katika usafiri wa anga kwa jumuiya ya SADC ili kujenga uhusiano na malengo yaliyo bora kwa maendeleo ya nchi zetu.”  
Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bwana Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo unalenga kuhakikisha wanafikia na kutekeleza malengo  Jumuiya ya usafiri wa anga wa kimataifa (ICAO) katika kuboresha huduma  za usafiri huo.
“Ni lazima tuyafanyiekazi   maadhimio ya  mkutano huu  ili kuboresha huduma kwa kiwango cha kimataifa pamoja na kuleta unafuu kwa watumiaji wa usafiri wa anga” alisisitiza  Bw. Johari.
Naye,  Mwenyekiti wa SADC Bw. Geoffrey Moshabesha amesema  kuwa  kamati hiyo inajipanga kuunda taasisi ya kiusalama ili kusimamia mifumo yote kwa nchi nzima ili kuweka mazingira mazuri kwa watumiaji wa usafiri wa anga.
Jumuiya ya SADC imeweka  mikakati ya kutekeleza maadhimio hayo katika kuleta usalama wa anga pamoja na kutunza mazingira ili kuboresha huduma kwa watumiaji wa usafiri wa anga kwa nchi wanachama.

SERIKALI YAIMARISHA UDHIBITI WA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI NA BIASHARA YA MADINI

w1 
Kaimu Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Gilay Shamika akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye wakala hiyo ikiwemo kuongezeka kwa makusanyo ya mirabaha kwenye shughuli za uzalishaji na uuzaji wa madini nchini. Kulia ni Msemaji wa Wakala hiyo Bw. Yisambi Shiwa.
w2 
Msemaji wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Yisambi Shiwa akiwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam namna walivyoimarisha udhibiti wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa kuongeza wakaguzi migodini na vituo vya ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali na kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira. Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa TMAA, Bw. Gilay Shamika na kulia ni Mwanasheria Bw. Gimonge Ngutunyi.
PICHA NA FATMA SALUM (MAELEZO)

Lukuvi atoa siku 10 kwa watendaji wa Wizara kushughulikia suala la Makazi Magomeni.

index 
Jonas Kamaleki, MAELEZO
——————————
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi ametoa siku 10 kwa watendaji wa Wizara yake kumshauri ili aweze kutatua mgogoro wa makazi wa watu wa Kinondoni Quarters.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati Lukuvi na timu ya wataalaam wa Wizara walipokuwa wakisikiliza malalamiko ya wakazi hao katika Wiki ya Utumishi wa Umma.
“Kazi ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kurekebisha yaliyopinda na kutoa suluhu haraka ili kuwafuta wananchi machozi,”alisema Lukuvi na kuongeza kuwa Serikali haitaki kuona haki za wananchi zinacheleweshwa.
Aliongeza kuwa ni nia ya Serikali kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapatiwa makazi bora kama ilivyo katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015.
Waziri Lukuvi alisema kuhusu makazi bora, Wizara inafanya mapitio ya Sera ya Makazi ya Mwaka 2010 ili iweze kwenda na wakati na pia kutengeneza Sera ya Nyumba.
Awali, akitoa malalamiko, Mwenyekiti wa Kamati wakazi waliovunjiwa nyumba zao, Bw. George Abel alisema kuwa suala hili limechukua muda mrefu tangu mwaka 2009 hivyo wanamuomba waziri amshauri Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli abatilishe umiliki wa ardhi hiyo na kuukabidhi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili nyumba zijengwe na wao wako tayari kununua.
“Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeshindwa kujenga kwani tuliahidiwa kuwa mwaka 2011 nyumba zitakuwa zimekamilika na sisi ndio tutakuwa wapangaji na wanunuzi wa kwanza, lakini hadi leo ni miaka mitano nyumba hazijajengwa nasi tunaishi kwa shida,”alisema Abel.
Aidha, Bw. Abel alisema kuwa  wakazi 644 wa Kinondoni Quarters walivunjiwa nyumba zao na Manispaa ya Kinondoni kwa madai kuwa ni nyumba chakavu na zitajengwa nyumba za kisasa ambazo watapangishwa na hatimaye kuuziwa jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa.

WAZIRI WA AFYA , ATEMBELEA VIJIJI VILIVYOKUMBWA NA MLIPUKO WA UGONJWA USIOJULIKANA WILAYANI KONDOA.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa
usiojulikana  katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa. 
Katika ziara hilyo ameambatana na wataalam mbalimbali ambao wameweka kambi kwenye vijiji hivyo ili
kufuatilia wagonjwa majumbani.vile vile ametembelea wagonjwa
waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
Mbunge wa Kondoa Mhe. Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara hiyo.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kondoa.Mhe.Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana  katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.

kikao cha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

a1 
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi (kushoto) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasimimali watu Bibi Victroria Fovo.
a2 
Baadhi ya wakuu wa Idara wakinukuu hoja na maoni ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakati wa kikao kati ya Katibu wa Sekretarieti hiyo na Watumishi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
a3 
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa Katibu wa Sekretarieti hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) baada ya kuwasilisha maoni na ushauri kuhusiana na utendaji kazi wa taasisi hiyo.

Serikali yapokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania.

K1 
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akikabdhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
K2 
Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem wakati akipokea msaada wa madawati toka kwa balozi huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
K4 
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) akikabidhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapemahii leo jijini Dar es Salaam.
K5 
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (kulia) wakiwa wamekalia madawati ambayo yametolewa msaada kwa serikali ya Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima  mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
K6 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (Katikati aliyekaa) kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima  wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na Wakurugenzi toka wizara hiyo mara baada ya kupokea msaada wa madawati toka ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
———————————————————————–
Na Eliphace Marwa- Maelezo
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati katika shule za msingi hapa nchini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
“Waziri Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema Balozi Maige.
Balozi Maigaaliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi.
Naye Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.
Aidha Balozi Maiga alitumia muda huo kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu  ujio wa Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini siku ya Julai Mosi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya  kikazi.
“Rais wa Rwanda atawasili hapa nchini Julai Mosi na ataweka saini makubaliano mbalimbali waliyofikia kati ya Tanzania na Rwanda baada ya hapo Rais Kagame ataambatana na mwenyeji wake Rais Magufuli mpaka katika viwanja vya maonesho vya Sabasaba ambapo Rais Kagame atayazindua rasmi maonesho hayo ya arobaini”, alisema Balozi Maiga.
Aidha Balozi Maiga aliongeza kuwa Rais Kagame jioni atakaribishwa Ikulu na mwenyeji wake Rais Magufuli kwa ajili ya dhifa ya kitaifa.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA

J1 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Utumishi na Utawala Bora,  George Simbachawene (wapili kulia)  na Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama   watatu kulia) bungeni mjini Dodoma Juni 22, 2016.  Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Babati Vijijini  Jitu Vrajlal Son, , Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza,Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, Mbunge wa Korogwe Stephen Ngonya na Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto.
J2 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wananchi kutoka jimbo la Ukongwa waliotembeklea  bunge  kwa mwaliko wa Mbunge  (wapili kulia)  Juni 22, 2016.
J3 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Utumishi, na Utawala Bora , George Simbachawene  (kulia) na Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei  Massay (kushoto) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 22, 2016. Wapili kushoto ni Mosses Kirway  na wapili  kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaTaifa ya  CCM, Thomas Lulu, wote  wakiwa ni wageni waliotembelea Bunge wakitoka Mbulu.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Magari yanayoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi kuwa na namba na rangi maalum

Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango akiwasilisha taarifa ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano Bungeni mjini Dodoma jana. (Picha na Robert Okanda).
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
———————————–
Katika kuthibiti matumizi  ya magari yanayoingia Nchini kwa msamaha wa kodi  Serikali imesema kuanzia Julai Mosi magari hayo sasa yatakuwa na namba na rangi maalum.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu tamko la kuondoa misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini kwa kuwa zinatoa huduma za kijamii kama shule na hospitali.
“Kwa kutambuua mchango mkubwa wa Taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu na afya, napendekeza kufuta utaratibu niliotangaza katika hotuba ya bajeti na badala yake Serikali itaimarisha zaidi hatua mbalimbali za uthibiti misamaha ya kodi ikiwemo magari yaliyoingia kwa msamaha wa kodi kuwa na namba na rangi maalum,” alifafanua Mhe.Dkt. Mpango.
Aliendelea kutaja hatua nyingine kuwa ni taasisi za kidini kuwasilisha vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwazo mwa mwaka wa kalenda na kuthibitisha kama vifaa vilivyopewa msamaha mwaka uliopita vilitumika kama sheria inavyotaka.
Pia, kuwasilisha majina ya watu walioidhinishwa na Shirika au Taasisi kuandika barua ya kuomba msamaha wa kodi, wakiainisha cheo, saini, picha, anwani na namba zao za simu ili kuiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa msamaha kama zimepata kibali cha taasisi hizo.
Vile vile taasisi hizo zinatakiwa kupata barua kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa na Mkuu wa Wilaya mahali Taasisi au Mradi unaotekelezwa ulipo.
Mhe. Mpango amesema kuwa hatua hizo zimekuja kutokana na bidhaa zinazoombewa msamaha wa kodi kutumika tofauti na kusudi la msamaha huo.
Aidha ametoa tahadhari kwa mashirika ya kidini kuanzia sasa, kuhakikisha kuwa yanafuata taratibu zote na Kuzingatia masharti ya msamaha unaotolewa ili kuepuka kufutiwa leseni zao pale zitakapokwenda kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa.

Wizara ya Ardhi kubaini taasisi zinazodaiwa fidia na wananchi

IMGS0787 
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
————————————
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika  kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 itabaini taasisi zote na watu binafsi wanaodaiwa fidia na wananchi ili waweze kulipa fidia hizo.
Akiongea leo Bungeni, mjini Dodoma Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Angelina Mabula amesema kuwa ni kweli tatizo hilo lipo na tayari Serikali imechukua hatua kwa kuzielekeza Halmashauri zote na taasisi nyingine kulipa fidia stahiki kwa wananchi pale wanapotaka kutwaa maeneo yao.
Mhe. Mabula amesema kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikichukua mashamba ya wananchi na kushindwa kuwalipa fidia hivyo kulimbikiza madeni hayo kwa muda mrefu hali inayokwamisha shughuli  za maendeleo.
“Halmashauri za Wilaya, Taasisi na Maafisa Ardhi hawaruhusiwi kuchukua mashamba ya wananchi kabla hawajakamilisha utaratibu wa malipo ya fidia kwa wananchi hao, ili kuondokana na malimbikizo ya madeni ya fidia ambayo malipo yake huchukua muda mrefu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi,” alisema Mhe. Mabula.
Aidha Mhe. Mabula amewataka wananchi wanaodai fidia kuwa wavumilivu wakati Wizara yake inaendelea kufanya upembuzi wa taasisi hizo ili ziweze kulipa fidia zote zinazodaiwa na wananchi.
Vilevile Wizara hiyo imetoa ramani za mitaa kwa wenyeviti wa mitaa wa Jiji la Dar es Salaam ili wenyeviti hao waweze kutambua matumizi ya maeneo yao, kwa mfano maeneo ya wazi, na nini kijengwe katika maeneo yao kama vile nyumba fupi au ndefu, hoteli au chuo ili kuondokana na migogoro ya kubolewa nyumba kwa kujenga eneo lisiloruhusiwa.
“Tumeanza kwa mkoa wa Dar es Salaam lakini zoezi litaendelea kila Mkoa na kila Wilaya Nchi nzima, ili Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji waweze kutambua matumizi ya maeneo yao, hivyo kuchukua hatua kwa haraka pindi ambapo maeneo hayo yanatumika tofauti na matumizi yaliyoko” alifafanua Mhe. Mabula.
Aidha Mhe. Mabula amezitaka Halmashauri kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi kuwapa uwezo wenyeviti hao ili waweze kufanya kazi hiyo kiufanisi.

Mkoa wa Kaskazini Pemba imejipanga kuidhibiti hali YA matendo ya hujuma yanavyoendelea.

PEMBA-ZANZIBAR 
Na Masanja Mabula –Pemba
——————————–
 SERIKALI ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imeelezea kusiitishwa na matendo ya hujuma yanavyoendelea kutokea katika Mkoa huo ambapo kwa sasa imejipanga kuidhibiti hali hiyo kwa nguvu zote ili isiendelea kuleta athari zaidi kwa wananchi .
Hayo yamebinishwa na Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis Othman katika kikao cha Pamoja kati ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama , Maafisa wadhamini wa Wizara pamoja na wakuu wa Wilaya pamoja na watendaji kutoka Halmashauri na Baraza la Mji Wete katika Ukumbi wa Jamhuri Wete .
Amesema uvumilivu na ustahamilivu uliofaywa na Serikali dhidi ya matendo hayo licha ya kutoa taaluma ya kuachana na matendo hayo kupitia viongozi wa dini , wanasiasa na watu maarufu lakini imeonekana kwamba vitendo hivyo vinazidi kushamiri siku hadi siku kwa kuhujumu mali na kutishia usalama wa wananchi  jambo ambalo kwa sasa halikubaliki tena.
Aidha ameelezea kusikitikishwa na maafia wadhamini kushindwa kuyakemea matukio hayo licha ya kwamba yanagusa wizara wanazoziongoza huku akibainisha kwamba baadhi ya watendaji katika wizara hizo wanatumika kufanya ushawishi wa matendo hayo katika vijiji wanavyoishi .
“Imefika wakati serikali kuchukua hatua stahiki juu ya wahusika wa matendo hayo , kwani inashangaza kwamba tangu yaanze kutokea hakuna Afisa mdhamini aliyeweza kukemea na imaaminika baadhi ya wafanyakazi wenu wanatumika kufanya ushawishi ili yaendelee kutokea ”alisema .
Hata hivyo Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo ,Maliasili , Mifugo na  Uvuvi ameanza kufanya tathmini na mali na mazao yaliyoharibiwa pamoja na kuwapa misaada ya mbegu na mbolea kwa wakulima waliopata kuharibiwa mazao yao ili kujiimarisha za shughuli zao za kilimo .
Alisema wakulima waliopatiwa msaada ni wale wa mpunga , mihogo , viazi na migomba wakati walioharibiwa mikarafuu na minazi wanasubiri mpaka kuanza kwa msimu wa mvua za masika ili wawape miche .
“Tayari sisi Wizara tumewafanyia tathmini wakulima walioharibiwa mazao yao , ambapo wengine tumewapa mbegu na mbolea lakini wananchi walioharibiwa mikarafuu na minazi ambao wao tutawapa miche wakati wa mvua za masika kuanza ”alieleza.
Hata hivyo Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Issa Suleiman Juma aliwataka watendaji wa Wizara ya Kilimo kuharakisha kutoa tathmini na thamani ya mali zilizo haribiwa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Alisema , mbali na kuharakisha kutoa tathmini pia aliwataka kuwa tayari kwenda kutoa ushahidi unapohitajika jambo ambalo litasaidia  wahusika kutiwa hatiani na kukomesha matendo hayo .

CCM YAWASILISHA KWA MSAJILI WA VYAMA HATI NA VIELELEZO VYA MATUMIZI YAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo akimkabidhi vielelezo vya CCM vya matumizi ya Uchaguzi mkuu uliopita, kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala  Galasia Simbachawene, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo)
Na Bashir Nkoromo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana,  na kuwa chama cha pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.
Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala  Galasia Simbachawene.
Akikabidhi hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25, 2016.
“Sisi hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo haina budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee kuwa chama cha kuigwa “, alisema Mamilo.
Mamililo aliwasilisha hati na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.
Alisema, uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.
Kulingana na Sheria ya Uchaguzi, chama kinatakiwa kisitumie ghara inayozidi sh. bilioni 17, na kikilazimika kuzidi kiwango hicho kisididi zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachotakiwa, huku kwa upande wa wagombea kiasi kinachotakiwa ni sh. bilioni  saba na kwa wabunge sh. milioni 33 hadi 88 kulingana na mazingira ya jimbo.

OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUKUTANA NA WADAU WAKE KUJIBU KERO MBALIMBALI KUHUSU UTENDAJI KAZI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
TZ 
TAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa taarifa kuwa itakutana na  wadau wake wote siku ya  ALHAMISI  TAREHE 23 JUNI  21016, ili kupokea  na kujibu malalamiko, kero, hoja na maoni mbalimbali kuhusu Utendaji kazi wa Ofisi ikiwa ni maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016.
Mkutano huo utafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.
Wadau wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanaombwa kuhudhuria katika Mkutano huo muhimu.
Imetolewa na: Gerson Mdemu
                             NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

PROFESA MBARAWA AFUNGUA mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga.

b1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifungua mkutano wa 19 wa  Usafiri  wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam jana (leo).
b2Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bwana Hamza  Johari akifafanua jambo katika mkutano wa 19 wa  Usafiri  wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam jana (leo).
b3 
Mkuu wa oganaizesheni ya Usafiri wa Anga kwa nchi za SADC Bwana Geofrey Moshabesh akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya usalama wa anga kwa wajumbe wa mkutano wa  19 wa  Usafiri  wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam jana (leo).
b4 
Wajumbe wa  Mkutano wa 19 wa  Usafiri  wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)  wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).

No comments:

Post a Comment