Sunday, June 26, 2016

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI ATANGAZA WAKUU WA WILAYA NCHINI

wakuu1
wakuu2 wakuu3 wakuu4

RAIS WA VoWET MAIDA WAZIRI AZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA BIASHARA(BAA) ATOA SEMINA YA UJASILIAMALI, (TIA) DAR ES SALAAAM

Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu  TIA wakati wa uzunduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara (BAA), ambapo aliwahimiza elimu wanayoipata wasiitumie kwenda kuombea kazi tuu lakini pia waitumie kwa ajili ya kufanya ujasiliamali kwa kujiajili wao wenyewe.
Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akikata keki ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa umoja huo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa  BAA Gwamaka Andrew (Kushoto) akimmkabidhi Cheti cha Shukurani Mgeni rasmi Bi. Maida Waziri (Kulia)
Afisa Taaluma wa Chuo cha uhasibu TIA na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo hicho Bw. Mugisha Kamala akitoa neno la utangulizi na shukurani kwa watu wote waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Aliyekuwa Afisa Mipango wa BAA Alex Mujwahuzi akitambulisha baadhi ya Viongozi waliokuwepo katika uzinduzi huo
Afisa Mipango msaidizi mstaafu wa BAA Bi. Grace Samagoda akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo 
Aliyekuwa mwenyekiti wa BAA ambaye amemaliza muda wake Bw. Elisha Benard akitoa historia ya umoja huo
Mwenyekiti mpya wa BAA Bw. William Msemo akitoa neno la shukurani kwa kuchaguliwa pamoja na kuwaomba ushirikiano wanafunzi wenzake katika kipindi chote atakachokuwa madarakani.
Afisa Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard akiwahimiza wanafunzi wa chuo cha TIA kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS) ambapo pamoja na yote ataweza kupata Fao la Elimu.
Mratibu Mkuu wa Shughuli za kampuni ya Tone Multimedia Chande Abdallah akiwatambulisha wanafunzi wa chuo cha TIA blog ya wanachuo ya Matukio na wanavyuo ambapo mwanachuo yeyote atapata nafasi ya kupata matukio na Taarifa mbalimbali za wanavyuo nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara BAA Gwamaka Andrew akitoa neno la Shukurani kwa kufanikisha vema shughuli hiyo.
Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) wakiwa katika uzinduzi wa BAA
 Mgeni Rasmi akipata picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa BBA waliomaliza muda na wale wa sasa
Picha zote na Fredy Njeje 

MAJALIWA AHITIMISHA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR’AN TUKUFU YA KIMATAIFA

hs1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016 kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es slaam . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
hs2 
Baadhi ya Waislamu waliokudhuria katika hitimisho la Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohitimisha mashindano hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hs3 
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dare es salaam Sheikh  Alhadi Mussa Salim akiwa amekaa na Mkurugeni wa Tume ya Ucahguzi Bw. Ramadhan K.Kailima.
hs5
Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ali Hapi akiwa amekaa na Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani nchini Kamanda Mohamed Mpinga na kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Bw. Ramadhan Madabida.
hs6 
Baadhi ya Waislamu waliokudhuria katika hitimisho la Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohitimisha mashindano hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hs7 
Baadhi ya Waislamu waliokudhuria katika hitimisho la Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohitimisha mashindano hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hs8 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery bin Ally baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa Juni 26, 2016. Katikati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhadi Mussa Salum. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
hs9 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hs10 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na watoto wadogo kuliko wote walioshiriki katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016.Watoto hao ni Abuzar Kholidi wa Tajikistan (Kulia) na Ahmad Abdullah Al-Azhar wa wa Bangladesh. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hs11 
Waziri Mkuu, Kassim Maajliwa akiagana na baadhi ya waumini wa Kiislamu walioshiriki katika hitimisho la Mashindano ya Kuhufadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa  wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha mashindano hayo Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wabunge wapewa semina juu ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa

wab1 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi Nasama Massinda akiwasilisha mada leo Mjini Dodoma kwa Wabunge  wa Kamati ya Bunge ya Biashara, Viwanda na Mazingira na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji( hawapo pichani)kuhusu uanzishwaji wa Masoko ya Bidhaa hapa nchini ili kuwainua wakulima.
wab2Mkurugenzi wa Usimamizi na Uendelezaji wa Masoko Kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Bw. Godfrey Malekano akijibu hoja za Wabunge (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kuwasaidia wakulima kupitia Masoko ya Bidhaa ili waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha.
wab3 
Mbunge wa Newala Mjini Mhe. George Mkuchika akichangia mada juu ya namna bora ya kuwainua wakulima hapa nchini hasa wanaozalisha Korosho na mazao mengine ya biashara wakati wa semina kuhusu Masoko ya Mitaji na Dhamana iliyofanyika Mjini Dodoma leo.
wab4 
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia mada kuhusu Masoko ya Bidhaa iliyowasilishwa wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Biashara Viwanda na Mazingira na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kuhusu mikakati ya mamlaka hiyo kuwainua wakulima hapa nchini.
wab5Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Mfaume Juma akijibu hoja za Wabunge kuhusu mikakati ya Bodi hiyo kuimarisha zao la korosho ili liweze kuwainua wananchi kiuchumi wakati wa semina kuhusu Masoko ya Mitaji na Dhamana iliyofanyika Mjini Dodoma leo.
(Picha Zote Na: Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma)
…………………………………………………………………………………………………………….
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Kilimo kinachangia asilimia 26 ya pato la Taifa na kuchangia zaidi ya asilimia 75 ya kipato kwa wananchi waishio vijijijini, pamoja na mchango mkubwa wa kilimo kwenye uchumi wa nchi, wakulima wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali ya masoko yenye bei zenye ushindani.
Kwa kuliona hilo Serikali ilipitisha sera ya masoko ya bidhaa mwaka 2014 kwa kuanza na mazao manne ya majaribio ambayo ni, Korosho, Ufuta, Alizeti na Mchele.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi. Nasama Massinda wakati wa semina  kwa Wabunge juu ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa nchini iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.
Akieleza kazi kuu za soko la bidhaa Massinda amesema kuwa soko la bidhaa linaleta uwazi wa bei za mazao na mwenendo wa soko, kila mtu ataweza kujua bei ya mazao sokoni ambapo bei zitatolewa kwa vyombo vya habari pamoja na kuondoa ulazima wa wakulima kusafirisha mazao yao toka eneo moja kwenda lingine kutafuta wanunuzi.
“Vile vile soko la bidhaa litasaidia kutoa bei zenye ushindani kwa kuzingatia upatikanaji wa bidhaa na mahitaji ya bidhaa, litaboresha bei ya mazao vijijini kwa kuwa na soko la bidhaa litakalo toa taarifa kwa wakulima wote kuhusu soko, bei na mwenendo wa soko,” alifafanua Massinda.
Kwa upande wake Mbunge wa Nanyamba, Mhe. Abdallah Chikota alilitaka soko hilo kupanua wigo wa uelimishaji kwa kushuka mpaka kwa wakulima na watendaji wa Serikali katika ngazi ya chini kuliko kuishia kwa mawakala ambao wanaweza wasitoe elimu hiyo kama ilivyotarajiwa.
Soko hilo la Bidhaa linalotarajia kuanza Septemba mwaka huu linategemea kumnufaisha mkulima mdogo, wakulima wakubwa, wenye viwanda, wakusanya mazao (ushirika), wauzaji mazao nje, wakopeshaji na vyombo vya fedha pamoja na Serikali kupata mapato kupitia tozo kutokana na uwepo wa takwimu na uwazi.

TAHADHARI KWA YOUNG AFRICANS SC

TAMBWEE 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea taarifa juu ya mpango na kauli za baadhi ya viongozi wa Young Africans SC kushawishi mashabiki wao kufanya vurugu dhidi ya warushaji matangazo ya televisheni ya moja kwa moja wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika ngazi ya Makundi kati ya Young Africans ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaofanyika Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Dar es Salaam.
TFF ikiwa msimamizi mkuu wa mpira wa miguu Tanzania, inawajibika na mara moja inachukua nafasi hii kuwatahadharisha baadhi ya viongozi wa Young Africans, wanachama na mashabiki wao kutofanya hivyo kwani itakuwa ni kinyume na  kanuni za mashindano na mikataba ya udhamini katika hatua hii.
Ikumbukwe kwamba CAF inamiliki asilimia mia moja ya haki za habari na masoko katika ngazi hii ya makundi na jaribio lolote la kukwamisha matangazo ya biashara au utengenezaji na urushaji wa matangazo ya televisheni au ukwamishaji wa shughuli zingine kama hizo kwa CAF au wakala aliyeteuliwa na CAF kutaigharimu klabu mwenyeji si kwa kutozwa faini tu lakini pia uwezekano wa kuondolewa mashindanoni.
Pia TFF inatoa tahadhari hiyo ikiwamo ile ya utamaduni wa kukaa uwanjani ili kuepusha aina yoyote ya vurugu kwenye michezo yake hususani hii ya hatua ya makundi. TFF inafahamu kuwa tayari viongozi wa Young Africans walikwisha kusoma nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusu kanuni na masuala ya udhamini kwa timu zinazofuzu hatua ya Nane Bora.Wapenzi wa Yanga wanaombwa kufika kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu  timu yao ikiwa ni njia ya kuitia hamasa.Hata hivyo shamrashamra hizo zifanyike kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za Mpira wa Miguu na sheria za nchi.
Vitendo vya kuashiria vurugu na kufanya vurugu vikithibitishwa katika taarifa ya Mwamuzi, Janny Sikazwe wa Zambia; Kamishna wa mchezo, Celestin Ntangungira wa Rwanda na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza, hatua zake zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo KUONDOLEWA KWENYE MASHINDANO. Vilevile vitendo vya kutishia amani,kudhuru mwili au kuharibu mali vitachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kijinai.
Katika mchezo huo wa kimataifa Na. 107, Mwamuzi Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba.
Wakati huohuo, kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kinatarajia kukaa siku ya Jumamosi tarehe 2 Julai 2016. Taarifa zaidi itatolewa karibuni.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yapanga mikakati ya kufilisi magari yatakayokamatwa na dawa za kulevya

index 
Na Miza Kona       Maelezo – Zanzibar
 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga mikakati maalum ya kuzifilisi gari zitakazokamatwa au kuhusika uingizaji wa dawa za kulevya  kwa lengo la kudhibiti  uingizaji,  usambazaji na utumiaji wadawa hizo nchini .
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed  huko Mnara wa kumbukumbu Kisonge katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani amesema serikali haitamuonea muhali yoyote atakae husika na uingizaji wa biashara ya dawa za kulevya kwa lengo la kutomeza janga hilo linathiri jamii na kupoteza nguvu ya Taifa.
Amesema wafanyabiasha wa bidhaa hiyo hawalitakii mema Taifa kwani wao ni wahujumu  wanaorejesha maendeleo ya nchini wanawaumiza vijana na watoto na kupoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo wanahitaji kufichuliwa kwa nguvu bila ya kuwaonea muhali.
Ameeleza kuwa tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya linamtoa mtu katika hadhi yake ya ubinadamu kwa kutengwa na jamii na kumsababishia madhara makubwa ikiwemo maradhi ya Ini, Figo, Ukimwi na Ugonjwa wa akili pamoja na kupoteza viungo muhimu vya mwili.
 Aidha Waziri Aboud amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa siasa wanawatumia vibaya madaraka yao kwa maslahi yao binafsi kuwatumia vijana kinyume na sheria jambo ambalo linachangia vijana hao kijiingiza katika vikundi viovu na hatimae kujiingiza katika utumiaji wa dawa hizo kwa kuwapotezea malengo na kuiathiri jamii.
Waziri huyo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni 200 Duniani  wameathitika na utumiaji wa dawa za Kulevya ambapo Zanzibar watu 10000 wameathirika na utumiaji wa dawa hizo kati ya 3200 wanatumia niia ya kujidunga sindano .
Hata hivyo Waziri huyo amewata wazee na walezi kuwalea vyema watoto wao kwa kuwafunza maaadili mema ili kuweza kujiepusha na kujiingiza katika vikundi viovu sambamba na kuwapokea walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwajali , kuwakubali, kuwasidiana pamoja na kuwapa ushauri  kwa lengo la kuwaondolea matatizo yao ili wasirejee tena katika janga hilo.
 Nae Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Moh’d Mahmoud ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja  ili kuweza kuwadhiti janga hilo kupitia njia zote zinatumika kupitishia dawa hizo kwa kukata minyororo iliomo katika sehemu husika kwa lengo la kutokomeza uingizaji wa bidhaa haramu nchini.  
Akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi Mngwali Ussi amesema jumla ya kesi 79  zimeripotiwa  kati ya kesi saba zinahusiana na dawa za kulevya ambazo zinaendelea mahakani na kesi 72 za makosa tofauti ambazo ziko chini ya upelele wa polisi.
Wakitoa ushahidi vijana waliopata nafuu wameionya jamii wasiwaachie watoto wao kukaa katika vikundi na kujiepusha na marafiki waovu  kwani ndio kishawishi kikubwa  kinachopelekea watoto hao kujiingiza katika dimbwi la dawa hizo
Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Utumiaji wa Dawa za Kulevya Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 Juni ambapo Ujumbe wa Mwaka huu Tuwajali, Tuwasikilize  Watoto na Vijana.

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA AMANI NA UMOJA WAKATI WA TAFRIJA YA FUTARI ILIYOANDALIWA NA BAKWATA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waisalm wa Tanzania  (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa  na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri  Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya wageni waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Jopo la Masheikh Sheikh Suleiman Amran Kilemile akitafsiri moja ya aya ya Quran inayojenga na kuimarisha umoja na mshikamano kwa waislam.
 Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Viongozi wa Wanawake Waislamu Tanzania wakisikiliza kwa makini nasaha za viongozi mara baada ya kufuturu katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania.

Wakulima wa zabibu Dodoma wanufaika na mpango wa kilimo shirikishi wa TBL Group

shay001 
Wakulima wanapenda kupata ushauri wa kitaalamu ili wapate mafanikio pichani wakulima wa shahiri wilayani Karatu wakimsikiliza mtaalamu wa kilimo na mshauri wa TBL Group Dk. Bennie Basson alipowatembelea
shay01 
Wakulima wanaoshirikiana na TBL wilayani Karatu wakisikiza ushauri wa wataalamu wa kilimo walipotembelewa hivi karibuni
shay1Wataalamu wa Kilimo kutoka SABmiller Francois Potgieter na Gerhard Greeff wakikagua mashamba ya wakulima wilayani Karatu walipowatembelea na kuwapatia ushauri
…………………………………………………………………………………………………….
Zaidi ya wakulima  700 wa zao la zabibu mkoani Dodoma wananufaika na  mpango wa kilimo shirikishi unaoendeshwa na kampuni ya TDL iliyopo chini ya kampuni ya TBL Group ambao umeanza kuonesha mafanikio kwa kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji  katika mashamba yao ya zabibu.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin amebainisha hayo wakati akitoa ripoti ya mwelekeo wa biashara ya kampuni W kwa kipindi cha mwaka ujao ambapo alisema kuwa mpango shirikishi na wakulima wa zabibu umeanza kutekelezwa katika vijiji vya Bihawana, Mpunguzi, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala
Alisema kuwa Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC) ambapo mafanikio ya mpango huu yameanza kuleta mafanikio kwa wakulima kupatiwa elimu ya kilimo cha kisasa cha zao la zabibu na kuanza kufanya utekelezaji kwa kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo.
Katika kuwapatia wakulima motisha wakulima ili wajiunge na  waweze kuboresha maisha yao kupitia kilimo cha zao la zabibu chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa  zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia  mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza
Jarrin alisema kuwa mpango huu shirikishi tayari umeonyesha mafanikio makubwa  kwa wakulima wa zao la Shahiri katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambao wengi maisha yao yamebadilika kuwa bora na kuwepo ongezeko kubwa la ajira kutokana na kilimo cha zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengeneza kinywaji cha bia.
“Kwa upande wa zao la Shahiri wakulima zaidi ya 3000 wanaendelea kunufaika.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni”.Alisema.
aliongeza kuwa  kampuni inao mkakati wa kuendelea kufanya kazi na wakulima  na kubadilisha maisha yao kupitia mpango wa kampuni mama ya SABMiller ujulikanao  kama Go Farming ambao tayari umeanza kutekelezwa katika nchi mbalimbali ambazo imewekeza.
Alisema lengo kubwa la mpango huu ni kuinua maisha ya wakulima wadogowadogo,kuongeza kasi ya kukua uchumi na kujenga mfumo mzuri na endelevu wa  kupata malighafi kwa ajili ya viwanda kampuni ya TBL Group kwa hapa nchini na SABMiller vilivyopo kwenye nchi mbalimbali barani Afrika
“Mpango wa Go Farming haulengi kunufaisha wakulima wa Shahiri pekee bali pia wa mazao mengine kama mtama na mihogo na katika siku za usoni wakulima wa zao la mahindi watawezeshwa pia na inategemewa hadi kufikia mwaka 2020 zaidi ya wakulima nusu milioni watakuwa wamewezeshwa sehemu mbalimbali duniani ambako kampuni imewekeza na mamilioni ya wananchi watajipatia riziki kutokana na kufanya kazi za utekelezaji wake”.
Aliongeza kuwa matarajio ya mafanikio ya mpango huu katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 yanaonyesha kukua kwa asilimia 44 katika nchi 10 ambako umeanza kutekelezwa na inakadiriwa kuwepo ongezeko la uzalishaji wa mazao kutoka tani 300,000 kufikia zaidi ya tani 600,000.
MWALIMU WA KWAYA YA MOYO MT.WA YESU ADAM MABIKI AUKIMBIA UKAPELA.
har1 
Hayawi hayawi yamekuwa Adam Steven Mabiki na Dominica Thadei Kissela wakiwa katika pozi la piwa  mara baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam, Juni,18 ,2016 na kufauatiwa na shereha ya kukata na shoka iliyoifanyika kwenye ukumbi wa Alli Hassan Mwinyi uliopo Chuku Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
har2 
Hayawi hayawi yamekuwa Adam Steven Mabiki na Dominica Thadei Kissela wakiwa katika pozi la piwa  mara baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam, Juni,18 ,2016 na kufauatiwa na shereha ya kukata na shoka iliyoifanyika kwenye ukumbi wa Alli Hassan Mwinyi uliopo Chuku Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
har3
Bwanaharusi na bibi harusi Adam Steven Mabiki na Dominica Thadei Kissela, wakiwa na wasimamizi wao Dk.Evodius Zege na Sophia Nchini kwenye picha ya pamoja  mara baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam, Juni,18 ,2016 na kufauatiwa na shereha ya kukata na shoka iliyoifanyika kwenye ukumbi wa Alli Hassan Mwinyi uliopo Chuku Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
har4 
Mr,& mrs Adam Steven Mabiki wakiwa kwenye picha ya pamoja katika ufukwe wa bahari ya hindi Cocobeach jijini Dar es Salaam.
har5 
Wapambe wa bwanaharusi Adam Steven ambao ni wanakwaya wa Moyo mtakatifu wa Yesu wakiwa wamembeba bibi harusi Dominica wakati walipokuwa wapiga picha Cocobeach.
har6 
Wapembe wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi Adam na Dominica.
har7 
Wapambe wa bwanaharusi Adam Steven ambao ni wanakwaya wa Moyo mtakatifu wa Yesu wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi.
har8 
Sebene linapokolea ukumbini.

Benkiya CBA Tanzania Yafuturisha wateja wake

b1
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania,DK.Gift Shoko akiongea na wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) waliohudhuria futari maalumu iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
b2
Imam Mkuu wa Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa akitoa  mawaidha wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya CBA  katika Hoteli ya Serana jijini Dar es Salaam, jana kwa ajili ya wateja wakati wa kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani.
b3 b4 b6
Baadhi ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam .
b7
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA,Dk.Gift Shoko  (wa nne kushoto )  na Imam Mkuu wa Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa (wa tano) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa waandamizi wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

KAMATI YA MASHINDANO NA USAJILI YA COASTAL UNION YAWEKA BAYANA MIKAKATI YAO


Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili  katika Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketijuzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo,kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo,Abdallah Zuberi,kulia ni Hussein Chuse na anayefuatia ni
Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri,
 Mjumbe wa Kamati ya Mashindano namUsajili ya Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akiuliza swali wakati wa kikao cha kamatihiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketi juzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo
Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union,Salim Bawaziri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kumalizika kikao hicho 
Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wengine ambao ni Abdi Masamaki,Salim Bawaziri,Hemed Mbaruku,Hussein Chuse,Abdallah Zuberi “Unenge” na Juma Mgunda ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia mashindano na usajili.
Picha kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano cha timu ya Coastal Union.

MASAUNI AKABIDHI MSAADA WA PAMPU NA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KIKWAJUNI

m1 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi  wa Operesheni  za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji itakayotumika  kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo.m2 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.m3 
Mhandisi wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical, akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Jazeera.m4 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wataalamu  wa Mradi wa Uwekaji  Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni.m5 
Mafundi kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa nyaya za umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la Kikwajuni ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni.
(Picha na Mpiga Picha Wetu)

WATUMISHI EGA WAASWA KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI SERIKALI.

k1 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k2 
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari  akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki ili aweze kuzindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairukik3Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai akitoa taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki.
k4 k6 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k7 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
——————————————————-
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na mikakati ya kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na kutoa huduma ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya Serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua baraza la wafanyakazi la Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
“Nataka mbuni na kutengeneza mifumo tumizi mipya pamoja na kuiboresha mifumo tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta za kimkakati hususan sekta za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara” alisema Kairuki.
Waziri Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika ukusanyaji na kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja na sekta za fedha, rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.
Hatua hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha uwezo wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake na amewataka watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.
Aidha, watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi ni moja ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika usimamizi wa kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na wajibu waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi na maslahi na kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.
Akizungumzia utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali kuona Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila siku bali watumishi wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika kuzipatia suluhisho changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa katika kukodisha jengo ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Dkt Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia mtandaoni, hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.
Katika kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina wafanyakazi wapatao 94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126 mara Serikali itakapotoa kibali cha kuajiri watumishi wapya.
Wakala hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza hilo ambapo Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29 zilizopigwa za wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye historia hiyo kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Baraza la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004.

Mh.January Makamba Ashiriki MaHafaLi ya 24 ya Chuo cha Biblia

1 2
Mhe.January Makamba Akiwasili chuoni hapo.
Mhe.January Makamba (MB),WaziriwaNchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) ameitumia SikuyaTarehe 25 /6/2016 kushiriki katika mahafali 24 yachuo cha bibliaVuga  (VUGA BIBLE )kilichopo katika halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga Vilevile Mhe.January Makamba alipata fursa ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayofanywa na chuo hicho,
Pia  aliupongeza uongozi wa chuo kwakutoa elimu mbalimbali kwa wananchi waishio karibu na chuo na bumbuli kwa ujumla.3 
Akitazama sehemu ya maaandalizi ya bwawa la kufuga samaki Akitazama sehemu ya maaandalizi ya bwawa la kufuga samaki.
4 
Akijifunza namna ya utengenezaji wa Mizinga ya nyuki kwakutumia udongo wa mfanyanzi,mizinga hiyo inauwezo wa kudumu miaka 80-100.
6 
Akijifunza historia ya chuo hicho kwanjia ya picha.7 10 
Akitazama baadhi ya kazi za mikono za kikundi cha wakina mama wa Upendo,kikundi hicho kimepata mafunzo chuoni hapo.
Pichazotena Imani Selemani Nsamila

No comments :

Post a Comment