RAIS WA VoWET MAIDA WAZIRI AZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA BIASHARA(BAA) ATOA SEMINA YA UJASILIAMALI, (TIA) DAR ES SALAAAM
Rais
wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida
Waziri akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu TIA wakati wa
uzunduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara (BAA), ambapo
aliwahimiza elimu wanayoipata wasiitumie kwenda kuombea kazi tuu lakini
pia waitumie kwa ajili ya kufanya ujasiliamali kwa kujiajili wao
wenyewe.
Rais
wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida
Waziri akikata keki ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa umoja huo.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa BAA Gwamaka Andrew (Kushoto)
akimmkabidhi Cheti cha Shukurani Mgeni rasmi Bi. Maida Waziri (Kulia)
Afisa
Taaluma wa Chuo cha uhasibu TIA na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo hicho Bw.
Mugisha Kamala akitoa neno la utangulizi na shukurani kwa watu wote
waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Aliyekuwa Afisa Mipango wa BAA Alex Mujwahuzi akitambulisha baadhi ya Viongozi waliokuwepo katika uzinduzi huo
Afisa Mipango msaidizi mstaafu wa BAA Bi. Grace Samagoda akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo
Aliyekuwa mwenyekiti wa BAA ambaye amemaliza muda wake Bw. Elisha Benard akitoa historia ya umoja huo
Mwenyekiti
mpya wa BAA Bw. William Msemo akitoa neno la shukurani kwa kuchaguliwa
pamoja na kuwaomba ushirikiano wanafunzi wenzake katika kipindi chote
atakachokuwa madarakani.
Afisa
Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard akiwahimiza
wanafunzi wa chuo cha TIA kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari
(PSS) ambapo pamoja na yote ataweza kupata Fao la Elimu.
Mratibu
Mkuu wa Shughuli za kampuni ya Tone Multimedia Chande Abdallah
akiwatambulisha wanafunzi wa chuo cha TIA blog ya wanachuo ya Matukio na
wanavyuo ambapo mwanachuo yeyote atapata nafasi ya kupata matukio na
Taarifa mbalimbali za wanavyuo nchini Tanzania.
Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa
Biashara BAA Gwamaka Andrew akitoa neno la Shukurani kwa kufanikisha
vema shughuli hiyo.
Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) wakiwa katika uzinduzi wa BAA
Mgeni Rasmi akipata picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa BBA waliomaliza muda na wale wa sasa
Picha zote na Fredy Njeje
MAJALIWA AHITIMISHA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR’AN TUKUFU YA KIMATAIFA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,
Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016 kuhitimisha Mashindano ya
Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es slaam . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baadhi
ya Waislamu waliokudhuria katika hitimisho la Mashindano ya Kuhifadhi
Qur’an Tukufu ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipohitimisha mashindano hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dare es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim akiwa amekaa na Mkurugeni wa Tume ya Ucahguzi Bw. Ramadhan K.Kailima.
Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mh. Ali Hapi akiwa amekaa na Kamanda wa kikosi cha usalama
Barabarani nchini Kamanda Mohamed Mpinga na kulia kwake ni Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Dar es salaam Bw. Ramadhan Madabida.
Baadhi
ya Waislamu waliokudhuria katika hitimisho la Mashindano ya Kuhifadhi
Qur’an Tukufu ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipohitimisha mashindano hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya Waislamu waliokudhuria katika hitimisho la Mashindano ya Kuhifadhi
Qur’an Tukufu ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipohitimisha mashindano hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti wa Tanzania, Sheikh
Abubakary Zubery bin Ally baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es salaam kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an
Tukufu ya Kimataifa Juni 26, 2016. Katikati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es
salaam, Alhadi Mussa Salum. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha Mashindano ya
Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es salaam Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na watoto wadogo kuliko wote
walioshiriki katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Kimataifa
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26,
2016.Watoto hao ni Abuzar Kholidi wa Tajikistan (Kulia) na Ahmad
Abdullah Al-Azhar wa wa Bangladesh. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Maajliwa akiagana na baadhi ya waumini wa Kiislamu
walioshiriki katika hitimisho la Mashindano ya Kuhufadhi Qur’an Tukufu
ya Kimataifa kwenye ukumbi wa wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
baada ya kuhitimisha mashindano hayo Juni 26, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Wabunge wapewa semina juu ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi
Nasama Massinda akiwasilisha mada leo Mjini Dodoma kwa Wabunge wa
Kamati ya Bunge ya Biashara, Viwanda na Mazingira na Kamati ya Bunge ya
Uwekezaji( hawapo pichani)kuhusu uanzishwaji wa Masoko ya Bidhaa hapa
nchini ili kuwainua wakulima.
Mkurugenzi
wa Usimamizi na Uendelezaji wa Masoko Kutoka Mamlaka ya Masoko ya
Mitaji na Dhamana Bw. Godfrey Malekano akijibu hoja za Wabunge (hawapo
pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kuwasaidia wakulima kupitia
Masoko ya Bidhaa ili waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha.
Mbunge
wa Newala Mjini Mhe. George Mkuchika akichangia mada juu ya namna bora
ya kuwainua wakulima hapa nchini hasa wanaozalisha Korosho na mazao
mengine ya biashara wakati wa semina kuhusu Masoko ya Mitaji na Dhamana
iliyofanyika Mjini Dodoma leo.
Baadhi
ya Wabunge wakifuatilia mada kuhusu Masoko ya Bidhaa iliyowasilishwa
wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Biashara
Viwanda na Mazingira na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kuhusu mikakati ya
mamlaka hiyo kuwainua wakulima hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Mfaume Juma akijibu hoja za Wabunge
kuhusu mikakati ya Bodi hiyo kuimarisha zao la korosho ili liweze
kuwainua wananchi kiuchumi wakati wa semina kuhusu Masoko ya Mitaji na
Dhamana iliyofanyika Mjini Dodoma leo.
(Picha Zote Na: Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma)
…………………………………………………………………………………………………………….
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Kilimo kinachangia asilimia 26 ya
pato la Taifa na kuchangia zaidi ya asilimia 75 ya kipato kwa wananchi
waishio vijijijini, pamoja na mchango mkubwa wa kilimo kwenye uchumi wa
nchi, wakulima wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali ya masoko yenye bei
zenye ushindani.
Kwa kuliona hilo Serikali
ilipitisha sera ya masoko ya bidhaa mwaka 2014 kwa kuanza na mazao manne
ya majaribio ambayo ni, Korosho, Ufuta, Alizeti na Mchele.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
Bibi. Nasama Massinda wakati wa semina kwa Wabunge juu ya uanzishwaji
wa masoko ya bidhaa nchini iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.
Akieleza kazi kuu za soko la
bidhaa Massinda amesema kuwa soko la bidhaa linaleta uwazi wa bei za
mazao na mwenendo wa soko, kila mtu ataweza kujua bei ya mazao sokoni
ambapo bei zitatolewa kwa vyombo vya habari pamoja na kuondoa ulazima wa
wakulima kusafirisha mazao yao toka eneo moja kwenda lingine kutafuta
wanunuzi.
“Vile vile soko la bidhaa
litasaidia kutoa bei zenye ushindani kwa kuzingatia upatikanaji wa
bidhaa na mahitaji ya bidhaa, litaboresha bei ya mazao vijijini kwa kuwa
na soko la bidhaa litakalo toa taarifa kwa wakulima wote kuhusu soko,
bei na mwenendo wa soko,” alifafanua Massinda.
Kwa upande wake Mbunge wa
Nanyamba, Mhe. Abdallah Chikota alilitaka soko hilo kupanua wigo wa
uelimishaji kwa kushuka mpaka kwa wakulima na watendaji wa Serikali
katika ngazi ya chini kuliko kuishia kwa mawakala ambao wanaweza wasitoe
elimu hiyo kama ilivyotarajiwa.
Soko hilo la Bidhaa linalotarajia
kuanza Septemba mwaka huu linategemea kumnufaisha mkulima mdogo,
wakulima wakubwa, wenye viwanda, wakusanya mazao (ushirika), wauzaji
mazao nje, wakopeshaji na vyombo vya fedha pamoja na Serikali kupata
mapato kupitia tozo kutokana na uwepo wa takwimu na uwazi.
TAHADHARI KWA YOUNG AFRICANS SC
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea taarifa juu ya mpango na
kauli za baadhi ya viongozi wa Young Africans SC kushawishi mashabiki
wao kufanya vurugu dhidi ya warushaji matangazo ya televisheni ya moja
kwa moja wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika ngazi ya
Makundi kati ya Young Africans ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaofanyika Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni
kwenye Uwanja wa Dar es Salaam.
TFF ikiwa msimamizi mkuu wa mpira
wa miguu Tanzania, inawajibika na mara moja inachukua nafasi hii
kuwatahadharisha baadhi ya viongozi wa Young Africans, wanachama na
mashabiki wao kutofanya hivyo kwani itakuwa ni kinyume na kanuni za
mashindano na mikataba ya udhamini katika hatua hii.
Ikumbukwe kwamba CAF inamiliki
asilimia mia moja ya haki za habari na masoko katika ngazi hii ya
makundi na jaribio lolote la kukwamisha matangazo ya biashara au
utengenezaji na urushaji wa matangazo ya televisheni au ukwamishaji wa
shughuli zingine kama hizo kwa CAF au wakala aliyeteuliwa na CAF
kutaigharimu klabu mwenyeji si kwa kutozwa faini tu lakini pia uwezekano
wa kuondolewa mashindanoni.
Pia TFF inatoa tahadhari hiyo
ikiwamo ile ya utamaduni wa kukaa uwanjani ili kuepusha aina yoyote ya
vurugu kwenye michezo yake hususani hii ya hatua ya makundi. TFF
inafahamu kuwa tayari viongozi wa Young Africans walikwisha kusoma
nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusu kanuni na masuala ya udhamini kwa
timu zinazofuzu hatua ya Nane Bora.Wapenzi wa Yanga wanaombwa kufika kwa
wingi na kuishangilia kwa nguvu timu yao ikiwa ni njia ya kuitia
hamasa.Hata hivyo shamrashamra hizo zifanyike kwa kufuata sheria,kanuni
na taratibu za Mpira wa Miguu na sheria za nchi.
Vitendo vya kuashiria vurugu na
kufanya vurugu vikithibitishwa katika taarifa ya Mwamuzi, Janny Sikazwe
wa Zambia; Kamishna wa mchezo, Celestin Ntangungira wa Rwanda na Mratibu
Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza, hatua zake
zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo KUONDOLEWA KWENYE MASHINDANO. Vilevile
vitendo vya kutishia amani,kudhuru mwili au kuharibu mali vitachukuliwa
hatua kwa mujibu wa taratibu za kijinai.
Katika mchezo huo wa kimataifa
Na. 107, Mwamuzi Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka
Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa
Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa
Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba.
Wakati huohuo, kikao cha Kamati
ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kinatarajia kukaa siku
ya Jumamosi tarehe 2 Julai 2016. Taarifa zaidi itatolewa karibuni.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yapanga mikakati ya kufilisi magari yatakayokamatwa na dawa za kulevya
Na Miza Kona Maelezo – Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga mikakati maalum ya kuzifilisi gari zitakazokamatwa au kuhusika uingizaji wa dawa za kulevya kwa lengo la kudhibiti uingizaji, usambazaji na utumiaji wadawa hizo nchini .
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed huko Mnara wa kumbukumbu Kisonge katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani amesema serikali haitamuonea muhali yoyote atakae husika na uingizaji wa biashara ya dawa za kulevya kwa lengo la kutomeza janga hilo linathiri jamii na kupoteza nguvu ya Taifa.
Amesema wafanyabiasha wa bidhaa hiyo hawalitakii mema Taifa kwani wao ni wahujumu wanaorejesha maendeleo ya nchini wanawaumiza vijana na watoto na kupoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo wanahitaji kufichuliwa kwa nguvu bila ya kuwaonea muhali.
Ameeleza kuwa tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya linamtoa mtu katika hadhi yake ya ubinadamu kwa kutengwa na jamii na kumsababishia madhara makubwa ikiwemo maradhi ya Ini, Figo, Ukimwi na Ugonjwa wa akili pamoja na kupoteza viungo muhimu vya mwili.
Aidha Waziri Aboud amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa siasa wanawatumia vibaya madaraka yao kwa maslahi yao binafsi kuwatumia vijana kinyume na sheria jambo ambalo linachangia vijana hao kijiingiza katika vikundi viovu na hatimae kujiingiza katika utumiaji wa dawa hizo kwa kuwapotezea malengo na kuiathiri jamii.
Waziri huyo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni 200 Duniani wameathitika na utumiaji wa dawa za Kulevya ambapo Zanzibar watu 10000 wameathirika na utumiaji wa dawa hizo kati ya 3200 wanatumia niia ya kujidunga sindano .
Hata hivyo Waziri huyo amewata wazee na walezi kuwalea vyema watoto wao kwa kuwafunza maaadili mema ili kuweza kujiepusha na kujiingiza katika vikundi viovu sambamba na kuwapokea walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwajali , kuwakubali, kuwasidiana pamoja na kuwapa ushauri kwa lengo la kuwaondolea matatizo yao ili wasirejee tena katika janga hilo.
Nae Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Moh’d Mahmoud ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuwadhiti janga hilo kupitia njia zote zinatumika kupitishia dawa hizo kwa kukata minyororo iliomo katika sehemu husika kwa lengo la kutokomeza uingizaji wa bidhaa haramu nchini.
Akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi Mngwali Ussi amesema jumla ya kesi 79 zimeripotiwa kati ya kesi saba zinahusiana na dawa za kulevya ambazo zinaendelea mahakani na kesi 72 za makosa tofauti ambazo ziko chini ya upelele wa polisi.
Wakitoa ushahidi vijana waliopata nafuu wameionya jamii wasiwaachie watoto wao kukaa katika vikundi na kujiepusha na marafiki waovu kwani ndio kishawishi kikubwa kinachopelekea watoto hao kujiingiza katika dimbwi la dawa hizo
Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Utumiaji wa Dawa za Kulevya Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 Juni ambapo Ujumbe wa Mwaka huu Tuwajali, Tuwasikilize Watoto na Vijana.
MAKAMU WA RAIS AHIMIZA AMANI NA UMOJA WAKATI WA TAFRIJA YA FUTARI ILIYOANDALIWA NA BAKWATA
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya wageni waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jopo la Masheikh Sheikh Suleiman Amran Kilemile akitafsiri moja ya aya ya Quran inayojenga na kuimarisha umoja na mshikamano kwa waislam.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi wa Wanawake Waislamu Tanzania wakisikiliza kwa makini nasaha za viongozi mara baada ya kufuturu katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania.
Wakulima wa zabibu Dodoma wanufaika na mpango wa kilimo shirikishi wa TBL Group
Wakulima
wanapenda kupata ushauri wa kitaalamu ili wapate mafanikio pichani
wakulima wa shahiri wilayani Karatu wakimsikiliza mtaalamu wa kilimo na
mshauri wa TBL Group Dk. Bennie Basson alipowatembelea
Wakulima wanaoshirikiana na TBL wilayani Karatu wakisikiza ushauri wa wataalamu wa kilimo walipotembelewa hivi karibuni
Wataalamu
wa Kilimo kutoka SABmiller Francois Potgieter na Gerhard Greeff
wakikagua mashamba ya wakulima wilayani Karatu walipowatembelea na
kuwapatia ushauri
…………………………………………………………………………………………………….
Zaidi ya wakulima 700 wa zao la
zabibu mkoani Dodoma wananufaika na mpango wa kilimo shirikishi
unaoendeshwa na kampuni ya TDL iliyopo chini ya kampuni ya TBL Group
ambao umeanza kuonesha mafanikio kwa kuwawezesha wakulima kuongeza
uzalishaji katika mashamba yao ya zabibu.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin amebainisha hayo wakati akitoa ripoti ya mwelekeo
wa biashara ya kampuni W kwa kipindi cha mwaka ujao ambapo alisema kuwa
mpango shirikishi na wakulima wa zabibu umeanza kutekelezwa katika
vijiji vya Bihawana, Mpunguzi, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula,
Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala
Alisema kuwa Chini ya mpango huo
wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na
taasisi ya Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC)
ambapo mafanikio ya mpango huu yameanza kuleta mafanikio kwa wakulima
kupatiwa elimu ya kilimo cha kisasa cha zao la zabibu na kuanza kufanya
utekelezaji kwa kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo.
Katika kuwapatia wakulima motisha
wakulima ili wajiunge na waweze kuboresha maisha yao kupitia kilimo
cha zao la zabibu chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zabibu
wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia mfuko unaojulikana kama Zabibu na
Shule Kwanza
Jarrin alisema kuwa mpango huu
shirikishi tayari umeonyesha mafanikio makubwa kwa wakulima wa zao la
Shahiri katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambao wengi maisha yao
yamebadilika kuwa bora na kuwepo ongezeko kubwa la ajira kutokana na
kilimo cha zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengeneza kinywaji cha bia.
“Kwa upande wa zao la Shahiri
wakulima zaidi ya 3000 wanaendelea kunufaika.Katika kipindi cha mwaka
2015 mpango huu umewezesha ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kufikia
tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka lengo la matumizi na mahitaji ya
kampuni”.Alisema.
aliongeza kuwa kampuni inao
mkakati wa kuendelea kufanya kazi na wakulima na kubadilisha maisha yao
kupitia mpango wa kampuni mama ya SABMiller ujulikanao kama Go Farming
ambao tayari umeanza kutekelezwa katika nchi mbalimbali ambazo
imewekeza.
Alisema lengo kubwa la mpango huu
ni kuinua maisha ya wakulima wadogowadogo,kuongeza kasi ya kukua uchumi
na kujenga mfumo mzuri na endelevu wa kupata malighafi kwa ajili ya
viwanda kampuni ya TBL Group kwa hapa nchini na SABMiller vilivyopo
kwenye nchi mbalimbali barani Afrika
“Mpango wa Go Farming haulengi
kunufaisha wakulima wa Shahiri pekee bali pia wa mazao mengine kama
mtama na mihogo na katika siku za usoni wakulima wa zao la mahindi
watawezeshwa pia na inategemewa hadi kufikia mwaka 2020 zaidi ya
wakulima nusu milioni watakuwa wamewezeshwa sehemu mbalimbali duniani
ambako kampuni imewekeza na mamilioni ya wananchi watajipatia riziki
kutokana na kufanya kazi za utekelezaji wake”.
Aliongeza kuwa matarajio ya
mafanikio ya mpango huu katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020
yanaonyesha kukua kwa asilimia 44 katika nchi 10 ambako umeanza
kutekelezwa na inakadiriwa kuwepo ongezeko la uzalishaji wa mazao kutoka
tani 300,000 kufikia zaidi ya tani 600,000.
Hayawi
hayawi yamekuwa Adam Steven Mabiki na Dominica Thadei Kissela wakiwa
katika pozi la piwa mara baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa la
Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam, Juni,18 ,2016 na
kufauatiwa na shereha ya kukata na shoka iliyoifanyika kwenye ukumbi wa
Alli Hassan Mwinyi uliopo Chuku Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
Hayawi
hayawi yamekuwa Adam Steven Mabiki na Dominica Thadei Kissela wakiwa
katika pozi la piwa mara baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa la
Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam, Juni,18 ,2016 na
kufauatiwa na shereha ya kukata na shoka iliyoifanyika kwenye ukumbi wa
Alli Hassan Mwinyi uliopo Chuku Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
Bwanaharusi na bibi harusi Adam
Steven Mabiki na Dominica Thadei Kissela, wakiwa na wasimamizi wao
Dk.Evodius Zege na Sophia Nchini kwenye picha ya pamoja mara baada ya
kufunga ndoa yao katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar
es Salaam, Juni,18 ,2016 na kufauatiwa na shereha ya kukata na shoka
iliyoifanyika kwenye ukumbi wa Alli Hassan Mwinyi uliopo Chuku Kikuu
Huria jijini Dar es Salaam.
Mr,& mrs Adam Steven Mabiki wakiwa kwenye picha ya pamoja katika ufukwe wa bahari ya hindi Cocobeach jijini Dar es Salaam.
Wapambe
wa bwanaharusi Adam Steven ambao ni wanakwaya wa Moyo mtakatifu wa Yesu
wakiwa wamembeba bibi harusi Dominica wakati walipokuwa wapiga picha
Cocobeach.
Wapembe wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi Adam na Dominica.
Wapambe wa bwanaharusi Adam Steven ambao ni wanakwaya wa Moyo mtakatifu wa Yesu wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi.
Sebene linapokolea ukumbini.
Benkiya CBA Tanzania Yafuturisha wateja wake
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania,DK.Gift Shoko akiongea na wateja wa benki
hiyo (hawapo pichani) waliohudhuria futari maalumu iliyoandaliwa kwa
wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Imam
Mkuu wa Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa akitoa mawaidha
wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya CBA katika Hoteli ya Serana
jijini Dar es Salaam, jana kwa ajili ya wateja wakati wa kipindi hiki
cha mfungo mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CBA,Dk.Gift Shoko (wa nne kushoto ) na Imam Mkuu wa
Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa (wa tano) wakiwa kwenye picha
ya pamoja na Maofisa waandamizi wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari
iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.
Mjumbe
wa Kamati ya Mashindano namUsajili ya Klabu ya Coastal Union,Steven
Mguto akiuliza swali wakati wa kikao cha kamatihiyo kujadili masuala ya
usajili na mashindano kilichoketi juzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya
klabu hiyo
Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union,Salim Bawaziri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kumalizika kikao hicho Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wengine ambao ni Abdi Masamaki,Salim Bawaziri,Hemed Mbaruku,Hussein Chuse,Abdallah Zuberi “Unenge” na Juma Mgunda ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia mashindano na usajili.
kumalizika kikao hicho Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wengine ambao ni Abdi Masamaki,Salim Bawaziri,Hemed Mbaruku,Hussein Chuse,Abdallah Zuberi “Unenge” na Juma Mgunda ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia mashindano na usajili.
Picha kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano cha timu ya Coastal Union.
MASAUNI AKABIDHI MSAADA WA PAMPU NA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KIKWAJUNI
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto),
akimkabidhi Mkurugenzi wa Operesheni za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji
Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji
itakayotumika kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa
kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia
mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi
wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi
wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mhandisi
wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni,
Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical,
akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae
pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo,
Nassor Salum Jazeera.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na
wataalamu wa Mradi wa Uwekaji Taa za Barabarani katika Jimbo la
Kikwajuni.
Mafundi
kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa nyaya za
umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la Kikwajuni
ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad
Masauni.
(Picha na Mpiga Picha Wetu)
WATUMISHI EGA WAASWA KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI SERIKALI.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao
(eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye
ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms
mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari
akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki ili aweze kuzindua Baraza la
Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la
Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah
KairukiMwenyekiti
wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai
akitoa taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati
wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo
Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Angellah Kairuki.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA)
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la
Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la
Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa
Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya
uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
——————————————————-
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Watumishi
wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na
mikakati ya kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na
kutoa huduma ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya
Serikali.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua
baraza la wafanyakazi la Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
“Nataka
mbuni na kutengeneza mifumo tumizi mipya pamoja na kuiboresha mifumo
tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta za kimkakati hususan sekta
za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara” alisema Kairuki.
Waziri
Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika
ukusanyaji na kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja
na sekta za fedha, rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.
Hatua
hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha
uwezo wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake
na amewataka watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana
na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.
Aidha,
watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi
ni moja ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika
usimamizi wa kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki
na wajibu waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora
za kazi na maslahi na kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.
Akizungumzia
utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali
kuona Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila
siku bali watumishi wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika
kuzipatia suluhisho changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt.
Jabiri Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi
wa Umma alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa
katika kukodisha jengo ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Dkt
Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama
mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia
mtandaoni, hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.
Katika
kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina
wafanyakazi wapatao 94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126
mara Serikali itakapotoa kibali cha kuajiri watumishi wapya.
Wakala
hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza
hilo ambapo Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29
zilizopigwa za wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye
historia hiyo kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Baraza
la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya
kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye
sheria ya majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na
mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004.
Mh.January Makamba Ashiriki MaHafaLi ya 24 ya Chuo cha Biblia
Mhe.January Makamba Akiwasili chuoni hapo.
Mhe.January
Makamba (MB),WaziriwaNchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira ) ameitumia SikuyaTarehe 25 /6/2016 kushiriki katika mahafali
24 yachuo cha bibliaVuga (VUGA BIBLE )kilichopo katika halmashauri ya
Bumbuli mkoani Tanga Vilevile Mhe.January Makamba alipata fursa ya
kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayofanywa na chuo hicho,
Pia aliupongeza uongozi wa chuo kwakutoa elimu mbalimbali kwa wananchi waishio karibu na chuo na bumbuli kwa ujumla.
Akitazama sehemu ya maaandalizi ya bwawa la kufuga samaki Akitazama sehemu ya maaandalizi ya bwawa la kufuga samaki.
Akijifunza
namna ya utengenezaji wa Mizinga ya nyuki kwakutumia udongo wa
mfanyanzi,mizinga hiyo inauwezo wa kudumu miaka 80-100.
Akitazama baadhi ya kazi za mikono za kikundi cha wakina mama wa Upendo,kikundi hicho kimepata mafunzo chuoni hapo.
Pichazotena Imani Selemani Nsamila
No comments:
Post a Comment