Pages

Sunday, June 26, 2016

Mkubwa na Wanawe watoa msaada Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke

Kituo cha kuvumbua na kuendeleza vipaji vya muziki cha Mkubwa na Wanawe, kimetoa msaada ya vifaa vya tiba na vifaa mbalimbali vikiwe vile vya usafi, dawa za meno, sabuni, maji na juisi kwa wodi ya Watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es Salaam.

Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, kiongoni wa kituo hicho, Said Fella, amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ya Temeke ambayo pia ni majirani zao ambapo pia amebainisha kuwa kundi hilo limekuwa likifika Hospitalini hapo kuchangia misaada mbalimbali.

Said Fella ameongeza kuwa, alishauriwa na vijana wake waliopo katika kituo chake kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na wote kwa pamoja kukubaliana kutoa msaada huo.

“Nasi pia ni kama wagonjwa watarajiwa, hivyo tumeona ni vema kuja kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kama tulivyoshauriwa na wenyeji wetu, tukiwa pamoja na mabalozi wetu. Msaada tuliotoa una thamani ya Sh milioni tatu,” alisema Fella.

Akipokea msaada huo, mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage, alikishukuru kituo hicho kwa kuwakumbuka akiwataka wasanii na viongozi wake pamoja na wengineo wenye nafasi kuendelea kuwakumbuka.

“Vifaa tulivyoletewa ni Paso-Oximeter cha kupimia kiwango cha oksijeni mwilini, HB Culvate cha kupima kiwango cha damu, mashine ya BP ambayo kazi yake ni kufahamu kama presha ya damu (BP) imeshuka au la na Mashine ya Nebulizer yenye kazi ya kuwapimia dawa wagonjwa wa pumu,” alisema Nyumbiage.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake takribani 50 alioambatana nao hospitalini hapo, msanii anayeunda kundi la Yamoto, Dog Aslay, alisema kuwa wamefarijika kuwasaidia wagonjwa akiahidi kufanya hivyo wakati mwingine watakapopata nafasi.

Tukio hilo la aina yake kwa kundi hilo ambalo ufanya mara kwa mara katika kutembelea jamii na kusaidia misaada, limeweza kupongezwa na baadhi ya ndugu wa wagonjwa na wagonjwa wenyewe kwa kueleza kuwa ni tendo la kuigwa na kila mmoja wetu hasa wasanii ambao ni kioo cha jamii.Baadhi ya vijana wanaounda kundi la Mkubwa na Wanawe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati wa tukio hilo lililofanyika leo Juni 26.2016.Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akielezea namna vijana wake walivyoguswa na kuamua kujitolea kwa ajili ya watu wenye kuhitaji wakiwemo wa Hospitali hiyo ya Temeke.Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akimkabidhi baadhi ya vifaa Daktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage Baadhi ya wasanii wa kundi la Yamoto Band ambao pia wanatoka Mkubwa na Wanawe wakitoa vionjo kadhaa wakati wa tukio hilo.

Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella akishukuru kwa hatua hiyo ya kurudisha fedhila kwa JamiiMsanii Kiongozi wa Kundi la Yamoto Band,"Aslay Isihaka"-Dogo Aslay akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake wa Yamoto pamoja na kundi hilo la Mkubwa na Wanawe

Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella akionyesha moja ya vifaa hivyo vya tiba
Daktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage akionyesha moja ya kifaa huku akielezea namna kinavyofanya kaziMakabidhiano yakiendelea..
Vijana na Mabalozi wa kundi la Mkubwa na Wanawe wakibeba baadhi ya vifaa walivyotoa msaada hospitalini hapo.
Wakielekea wodini...
Amani James a.k.a Chiba wa kundi la Yamoto Band akitoa msaada katika tukio hiloMsanii Kiongozi wa Kundi la Yamoto Band,"Aslay Isihaka"-Dogo Aslay akimfariji mmoja wa Watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Temeke
Said Fella (kulia) na Mh. Temba (kushoto) wakielezea jambo wakati wa tukio hilo leo Juni 26
Enock Deogratius 'Enock Bella' akimfariji mtoto
Amani James a.k.a Chiba wa kundi la Yamoto Band aliweza kuwafariji watoto na ndugu wanaouguza watoto wao pale walipomuomba awachezee kidogo kwani imekuwa faraja kwa kumuona kwa mara ya kwanza
Mkubwa na Wanawe..
Mkubwa na Wanawe Baadhi ya vijana wanaounda kundi hilo la Mkubwa na Wanawe wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa tukio hilo la kutoa msaada hospitali ya Temeke. leo Juni 26.2016. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

No comments:

Post a Comment