Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi
Mwakilishi
wa Katibu Tawalawa mkoa wa Manyara Bw.Longino Kazimoto (katikati),
akifungua kikao cha pamoja kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na
wanachama wake wa mkoa wa Manyara. Mkutano huo ambao uliandaliwa na PSPF
katika utaratibu wake wa kukutana na wanachama wake katika maeneo
mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuboresha
huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa wateja ulifanyiki mjini
Babati.
Afisa
Mfadhiwi wa PSPF mkoa wa Manyara Bw. Said Ismail, akitoa hotuba wakati
wa kikao cha pamoja kati ya PSPF na wanachama wake wa mkoani Manyara
kilichofanyika mjini Babati. PSPF inautaratibu wa kukutana na wanachama
wake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna
bora ya kuboresha huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa
wateja.Wengine pichani ni Mwakilishi wa Katibu Tawalawa mkoa wa Manyara
Bw.Longino Kazimoto (katikati) na na Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF
Bi. Laila Maghimbi
Meneja
wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi akizungumza wakati wa
kikao cha pamoja na wanachama hao wakati wa semina hiyo.
SEKTA ISIYO RASMI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII.
Mkurugenzi
wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi
ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme
ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe. Kulia ni
Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde
akiwaeleza waandishi wa habari juhudi za Serikali katika kuboresha na
kupanua wigo wa huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa wananchi walio
kwenye sekta isiyo rasmi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria kutoka SSRA,
Bw. Onorius Njole.
Mkurugenzi
wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuhusu Program maalum ya kutoa elimu ya hifadhi
ya jamii kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Waratibu wa Mifuko
ya Bima ya Afya ya Jamii nchini kote. Zoezi hilo linaenda sambamba na
usajili wa mifuko hiyo. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa
SSRA, Bi. Sarah Kibonde na kushoto ni Afisa Uhusiano Ally Masaninga.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa SSRA uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam ambao ulilenga kuufahamisha umma maboresho
mbalimbali katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini.
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kupitia Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imejizatiti
kupanua wigo na kuboresha huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa kundi la
watu walio kwenye sekta isiyo rasmi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole wakati akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya
hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector
Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe.
Bw. Njole alisema kuwa katika
kuhakikisha watanzania wote wananufaika na huduma za hifadhi ya jamii,
SSRA inafanya tafiti mbalimbali na kuhamasisha Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii kubuni mafao mbalimbali yanayolenga kuwafikia wananchi wote walio
kwenye sekta isiyo rasmi.
Ili kufanikisha hilo, mwaka 2015
SSRA ilifanya utafiti katika sekta ya usafirishaji na kubaini kuwa
asilimia 83 ya waendesha vyombo vya usafiri mijini wakiwemo waendesha
bodaboda wako tayari kuchangia kwa hiari katika Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii.
“Kutokana na matokeo hayo mamlaka
ilipendekeza kuanzishwa kwa Mpango Maalum ujulikanao kama Informal
Sector Scheme ambapo watu waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi watapata
nafasi ya kunufaika na huduma ya hifadhi ya jamii.” Alisema Njole.
Njole aliongeza kuwa tayari
baadhi ya mifuko imekwishaandaa mafao maalum yanayowalenga waendesha
bodaboda, bajaji, daladala na mama lishe ambao watapata fursa ya
kuchangia kiasi kidogo kila siku kulingana na kipato chao ili kupata
huduma za hifadhi ya jamii kama vile akiba ya uzeeni, matibabu na
mikopo.
Aidha, Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde alieleza kuwa
mamlaka hiyo inaendelea na zoezi la kutambua na kusajili Mifuko yote ya
Bima ya Afya ya Jamii (CHFs) kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha
mfumo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi.
Pia Bi. Sarah alisema kuwa SSRA
imeandaa program maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa
Wakurugenzi wa Halmashauri na Waratibu wa Mifuko ya Bima ya Afya ya
Jamii nchini kote na zoezi hilo linaenda sambamba na usajili wa mifuko
hiyo kwa mujibu wa Sheria ya SSRA, Sura ya 135.
“Program hii imeanzia Kanda ya
Kati ambako ilihusisha Wilaya 27 na jumla ya CHF 5 zilisajiliwa na
nyingine 22 zinakamilisha taratibu za usajili. Zoezi hili linatarajiwa
kuendelea Juni 22 kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambako jumla ya CHF
25 zinatarajiwa kusajiliwa.”
Sambamba na program hiyo Serikali
kupitia Wizara ya Afya na Wizara yenye dhamana ya masuala ya hifadhi ya
jamii na SSRA inafanya mapitio ya mfumo wa usimamizi wa Mifuko ya Bima
ya Afya ya Jamii (CHF) ili kupata mfumo utakaoweza kutoa huduma ya afya
kwa watanzania wote.
MERCY KITOMARI: MJASIRIAMALI KIJANA ANAYEFIKIRIA MAKUBWA
Mjasiriamali kijana Mercy Kitomari akiwa ofisini kwake wakati wa mahojiano.
Modewjiblog ilipata
bahati ya kuzungumza ana kwa ana na Mercy Kitomari mmoja wa
wajasiriamali wanawake vijana ambaye anafikiria kuwa na kiwanda kikubwa
cha ashkrimu (ice cream) ifikapo mwaka 2020 akizisafirisha na kuziuza
Tanzania nzima na Afrika Mashariki. Wapi alipotokea, yuko wapi kwa sasa,
ni machungu gani aliyokumbana nayo na anaishauri nini serikali na
wajasiriamali wenzake. Haya yote utayajua katika mahojiano haya .Soma…
MODEWJI BLOG: Role model wako nani?
MERCY:
Magufuli. You know why?(unajua kwanini?) ametuweka wazi kabisa kwamba
maisha ni changamoto na tusikubali kushindwa ni lazima kupambana na
kufanyakazi kwa bidii na maarifa kuondoa vigingi vyote
vinavyotukwamisha. Amenifanya nifanye kazi kwa bidii. Nataka kuwa
mwanamke anayefanya mabadiliko. Hakuna kitu kinachokuja kirahisi. Nataka
kuwa mwanamke yule ambaye anaonesha tofauti nataka kuifanya nchi yangu
iniringie.
Sijisikii
vibaya kwa kuwa niko mpweke, kitu cha kwanza ni kazi, nataka kuifanya
mwenyewe ili wanawake wenzangu watambue kwamba tunaweza kufanya wenyewe,
bila msaada wa mwanaume. Ndio unahitaji mume lakini si katika hili
suala la ujasiriamali, mwanamke peke yako unaweza kuleta mabadiliko.
Nataka kuwa mwanamke ambaye Afrika itaniringia na taifa langu litanichekelea kwamba mimi ni binti yao.
MODEWJI
BLOG: Turejee katika masuala ya kodi. Kodi ni muhimu sana kwa mapato ya
serikali. Je Kodi zinazowatoza zinawasaidia au zinawavunja moyo?
MERCY:
To be honest (kusema ukweli) zinatuvunja moyo. Nyingi ya hizi kodi
hazitusaidii sisi watu wa hali ya chini kunyanyuka, zinatukwamisha.Kodi
zimewekwa bila kujali madaraja. Anayeanza na aliyemo, mwenye kipato
kidogo na kikubwa. Na yote hayo yanafanyika bila kuzingatia kwamba
kuwapo kwa wajasiriamali wengi ndio kuchangamka kwa soko la wakulima na
pia ajira viwandani.
Mimi
ninayetengeneza ashkrimu natengeneza ajira; ninatengeneza soko kwa yule
anayeleta matunda sokoni kwani naenda kununua matunda kwa ajili ya
ashkrimu. Kodi nyingi zinakandamiza, haziangalii ukubwa na udogo wa
biashara. Mtu anabiashara inayoingiza mamilioni kwa siku anawekwa kundi
moja na anayeingiza laki moja.
Muonekano
wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato la Mercy Kitomari
lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni
Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.
MODEWJI BLOG: Ukikutakana na role model wako utamuomba nini?
MERCY:
Nikikutana na Magufuli? Kwanza naomba nikutane naye! Nikikutana naye
nitamwambia ofisi zote za huduma kwa wananchi ziwe katika mtandao
(online) watu tuweze kufanya kila kitu katika mtandao. Na Serikali za
mitaa lazima zirejeshe faida kwa wananchi kwa kodi zao.
Wanatakiwa
watufundishe vitu vingi. Watufundishe kuwa wajasiriamali namna ya
kufunga na kuuza bidhaa zetu wasifanye tu shughuli za kukusanya ushuru
na kodi, watuambie namna ya kuendelea mbele ili waendelee kukusanya
ushuru na kodi au hawatakusanya kitu tukikwama.
Ni lazima wawekeze kwa wajasiriamali ili kuwepo na hali bora zaidi.
Ukitazama
soka katika televisheni unaona matangazo mengi ya krisp hapa kwetu wapo
wadada wanaotembeza za ndizi au viazi hawa wakifundishwa namna nzuri ya
kuweka chakula chao ni dhahiri tutakuwa na wajasiriamali wengi.
Wanatakiwa watuelekeze mambo mengi bidhaa za kwenye ‘super market’
zinakuaje na kadhalika wasibaki kudai na kuvuna hela tu watusaidie
tuweze kuwapatia fedha zaidi. Lakini nambieni lini nitakutana na role
model wangu huyu…….ha ha ha ha….kicheko….!
MODEWJI
BLOG: Wasaidizi wake wakisoma makala haya watajua nini unahitaji na
pasi shaka watakukutanisha naye.Ni watu wema hawa, hawawezi kukosa
kukupangia muda wa kumuona Role Model wako umweleze mambo ya kukusaidia
wewe na wengine wa aina yako.
MERCY:
Nakudai hilo kwani natamani sana atukutanishe wanawake vijana
wajasiriamali ili azungumze nasi. Najua ameshazungumza na
wafanyabiashara wakubwa, lakini akituona na sisi atatambua uwezo wetu na
namna ambavyo angetusaidia tungeibuka wengi na kuweka ndoto ya Tanzania
ya viwanda katika ukweli.
You
know (unajua) nilikutana na wanawake wenzetu wajasiriamali kutoka
Uganda na Rwanda naona wameendelea kwelikweli na siri ni serikali zao
kuhakikisha kwamba wanaendelea.
Wapo
wanawake waliokata tamaa hapa, nimekutana nao nikasema tusichoke hata
kidogo serikali ya sasa inataka viwanda ni lazima kuisaidia kujua
tunawezaje kufikia ndoto hiyo, kuna vizingiti hapa wakiviondoa tutaweza.
Hatupaswi kukata tama hasa kutokana na serikali ya sasa kutaka kuwapo na viwanda.
Mkutano wa ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika mjini Beijing Nchini China
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akieleza jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuhama kutoka mfumo wa urushaji
wa matangazo ya Televisheni kutoka Analogia kwenda Digitali katika
mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za
Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa
katika ukumbi wa mikutano leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu
wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China
unaofanyika Beijing nchini China.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel
(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang
wakibadilishana mawazo leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa
ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China
unaofanyika Beijing nchini China.
Mkutano wa Ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya nchi za Afrika na China ukiendelea mjini Beijing nchini China.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba na Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa wakibadilishana mawazo leo kabla ya
kuanza kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya
nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Picha na Mpigapicha wetu
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA OFISINI HAZINA.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Gideon
Manambo akizungumza na watumishi wa Wizara (hawapo pichani) katika
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Wizara hiyo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Doto
James.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifurahia jambo wakati
Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Doto
James akifafanua hoja mbalimbali za watumishi.
Watumishi
wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa wamesimama kwa dakika chache
kuwakumbuka watumishi waliotangulia mbele za haki kwa mwaka huu, katika
mkutano huo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Picha ya pamoja.
——————————————————————-
Wizara
ya Fedha na Mipango imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya
mkutano na Watumishi wake, lengo likiwa ni kujadili mafanikio na
changamoto wanazo kabiliana nazo mahali pa kazi.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James aliwataka Watumishi kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Magufuli
katika kupambana na masuala ya rushwa, uzembe kazini na Watumishi hewa
ambao wamekuwa wakiigharimu Serikali fedha nyingi katika kutekeleza
majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema
Wizara inajipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa
watumishi hasa kwa wale wenye ulemavu kwa kuwajengea miundombinu rafiki
sehemu za kazi ili kuongeza ufanisi kazini.
“Wizara
pia inafanya vizuri katika masuala ya usawa wa kijinsia kwa kuwa na
idadi inayoridhisha ya wanawake hasa katika ngazi za maamuzi, ikiwa ni
pamoja na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wawili wanawake” . Alisisitiza
James
Naye
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Gideon Manambo alisema kuwa, watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa
ufanisi na kwa bidii ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo
ambayo yanahitaji watendaji wenye weledi wa kutosha ili kukabiliana na
changamoto zinazojitokeza.
Kwa
upande wa watumishi wa Wizara, wameuomba uongozi kuhakikisha kunakuwepo
na vitendea kazi vya kutosha ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa
na matokeo chanya ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili
wananchi.
Maadhimisho
hayo yamefanyika kufuatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali ya Awamu
ya Tano ambapo uliagiza Wizara pamoja na Taasisi kuadhimisha Wiki hiyo
kwa kutatua matatizo ya watumishi wa Umma pamoja na wananchi kwa ujumla
katika maeneo yao ya kazi.
Imetolewa na: Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.
SERIKALI YAREJESHA MISAMAHA YA KODI KWA TAASISI ZA DINI, YATOA MASHARTI MAZITO
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
——————————–
Serikali imelegeza msimamo wake
kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake
itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha
hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na
vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na
wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na
Bunge.
Amesema kuwa uamuzi huo wa
serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka
serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na
umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa
na taasisi hizo.
“Kwa kutambua mchango mkubwa wa
taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya,
maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti,
badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo”Alisema
Dkt. Mpango
Alizitaja baadhi ya hatua
zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa
ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa
kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja
na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia
vilitumika kwa mujibu wa sheria
Aidha, utaratibu mpya utazitaka
Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha
kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini,
picha, anuani na namba za simu za wahusika.
“Taarifa hizo ni muhimu katika
kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama
zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi
iliyokusudiwa” Aliongeza Dkt. Mpango
Dkt. Mpango alisema katika
utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za
dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha
waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje
Alizitaja hatua nyingine kuwa ni
wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini,
Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa
Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali
Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na
mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha
Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari
yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja
na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti
matumizi yake.
Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.
African countries and China have agreed to strengthen Africa – China Media Cooperation to improve media quality
By Zamaradi Kawawa, Maelezo, Beijing, China.
………………………………………..
African countries and China have agreed to strengthen Africa – China Media Cooperation to improve media quality through experience sharing of implementation of media policies, capacity building programs for journalists, digitalization and development of new media.
Sharing Tanzanian experience in digital migration at the Third Forum on China – Africa Media Cooperation in Beijing today, Deputy Minister for Information, Culture, Arts and Sports Mrs Annastazia Wambura said Tanzania is now commemorating one year of migration from analogue to digital terrestrial television (DTT). She said although the process was challenging it was accomplished due to sound policies, regulatory framework and Government Commitment.
She told the forum that as of now, close to two million Tanzanians are enjoying quality television programmes from locally and foreign produced content enriching the people’s choice and diversity.
Mrs Wambura pointed out a digital migration road map, political will, consultation with stakeholders, a communication strategy , public private partnership (PPP) in the area of cost sharing and consumer consideration in the purchase of affordable services and equipment contributed to the smooth analogue to digital migration in broadcasting ahead of ITU deadline of 17th June, 2015.
She said the achievement was contributed largely by the Public Private Partnership between Star Communication Network Technology (Star Times ) from China which in May 2009 formed a joint venture company – Star Media (Tanzania) Limited with the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC), the Country’s public broadcaster.
However, the Zimbabwe Minister for Media, Information and Broadcasting Mr. Christopher Chindoti Mushohwe said efforts that strengthen African Media to fight against negative media coverage of African countries and China by Western countries should be applauded.
” The establishment of strong indigenous media in African countries will reduce dependence of western global media which is negative to African countries and China. Zimbabwe is ready to cooperate with China in fighting western media negative coverage”, he said.
………………………………………..
African countries and China have agreed to strengthen Africa – China Media Cooperation to improve media quality through experience sharing of implementation of media policies, capacity building programs for journalists, digitalization and development of new media.
Sharing Tanzanian experience in digital migration at the Third Forum on China – Africa Media Cooperation in Beijing today, Deputy Minister for Information, Culture, Arts and Sports Mrs Annastazia Wambura said Tanzania is now commemorating one year of migration from analogue to digital terrestrial television (DTT). She said although the process was challenging it was accomplished due to sound policies, regulatory framework and Government Commitment.
She told the forum that as of now, close to two million Tanzanians are enjoying quality television programmes from locally and foreign produced content enriching the people’s choice and diversity.
Mrs Wambura pointed out a digital migration road map, political will, consultation with stakeholders, a communication strategy , public private partnership (PPP) in the area of cost sharing and consumer consideration in the purchase of affordable services and equipment contributed to the smooth analogue to digital migration in broadcasting ahead of ITU deadline of 17th June, 2015.
She said the achievement was contributed largely by the Public Private Partnership between Star Communication Network Technology (Star Times ) from China which in May 2009 formed a joint venture company – Star Media (Tanzania) Limited with the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC), the Country’s public broadcaster.
However, the Zimbabwe Minister for Media, Information and Broadcasting Mr. Christopher Chindoti Mushohwe said efforts that strengthen African Media to fight against negative media coverage of African countries and China by Western countries should be applauded.
” The establishment of strong indigenous media in African countries will reduce dependence of western global media which is negative to African countries and China. Zimbabwe is ready to cooperate with China in fighting western media negative coverage”, he said.
MKUSANYIKA WA HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
WAAMUZI WA MECHI SERENGETI BOYS, SHELISHELI
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia,
ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana
wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli
utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi
ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya
miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa
kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na
Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma
Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini
tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika
Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo
wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2,
2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo,
Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya
vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu
katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti Boys ilicheza
mfululizo michezo saba ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2),
India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo
ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20
bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya AIFF, timu
hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika
jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika
mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani
CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Awali timu ya Serengeti Boys
ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa
zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za
Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa
kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa
iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi
cha kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
Serengeti Boys ilimaliza
Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao
3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo hata mmoja na
awali walipokutana walitoka sare ya 2-2
MWAMUZI WA ANGOLA KUWAAMUA YOUNG AFRICANS, TP MAZEMBE
Mchezo wa kuwania Kombe la
Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya Dar es Salaam,
Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia
Sikazwe atasaidiwa na Jarson
Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line
1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2)
huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna wa
mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo
utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.
SUALA LA STAND UNITED YA SHINYANGA
Kutokana na mkanganyiko wa
uendeshaji wa mchakato wa uchaguzi katika Klabu ya Stand United ya
Shinyanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF), limeagiza
michakato yote miwili inayoendeshwa sambamba ndani ya klabu ya Stand
United, isimamishwe mara moja kisha kusubiri maelekezo mengine.
Tübingen International Africa Festival in Germany opens it doors from the 21 to 24 July 2016
The
International Afrika Festival Tübingen in Southern Germany The Republic
of Burundi is country of honor 2016 From the 21 to 24 July 2016,
Tübingen International Africa Festival in Germany opens it doors wide
open to arts, culture, dialog tourism, media.. operators under the theme
„ not black, not white but colored for a peaceful world“ Exhibitors,
festival lovers and cultural tourist in search of plattforms for a short
vacation are cordially invited to attend and enjoy.
Founded since 2007 by Sunjo &
Susan TATAH; the International Africa Festival Tübingen in Germany, is a
FOUR DAY annual festival with focused on showing casing Africa´s role
and contribution to humanity and diversity as well as world peace and
stability bringing people of African descent and others from all over
the globe, irrespective of their countries of origin, religious
background, gender and status together.
The Festival tells the story of people
of Africa descent worldwide, thereby providing a platform to all
African interested persons to share and be part of the heritage.As a
young, dynamic rapidly growing forward thinking NGO, The International
African Festival Tübingen is a platform for mobilization and
presentation of cultural activist, Business and developmental activist, ,
individual donors and philantrophic activist in all sectors.
The festival is a compact format
composed of a varierty of authentic projects- presenting Africa´s
know-how – Huge market of Arts, Handworks, Authors, Producers,
Designers, Film makers, culinary Arts… as well as full package
entertainment such as talents shows with bands playing live music,
traditional Ballets, dance performances, Forums, workshops and parties
with top Djs / Mcs.
Each edition bringing together more
than 100,000 fun and peace loving visitors. AfrikAktiv invites you to
come and visit the International African festival in Germany powered by
the African Diaspora and dedicated to the development of its continent
and people. Come and have full service funtime. As a family oriented
Festival, children and youths are the heartbeat for our festival, we
cherish every one of them.
Our festival offers a special
integrated children and youth mini format festival with activities for
our young people – special artist with workshops –Acrobatics, clowning,
graffitis, dance, creative handworks, special concert just for the young
generation under the theme “Empowering the next generation with
cultural diversity and humanity values“ For a more visibility on
opportunities and potentials available on the African continent and its
Diaspora, our festival offers a platform for partnership to all
pan-african media and journalist.
Our festival reaches out to more than
million people worldwide particularly on the African continent, here you
meet your tailored made target groups. Join and follow us on social
media – Facebook, Instagrams, Twitter, youtube..The International
African Festival Tübingen, Germany offers opens you the door to enjoy
Africa´s authentic Arts and listen to African tell their story the way
it is.For more information: Web: www.afrikafestival.net‘
MV. MAGOGONI KUKAMILIKA AGOSTI MWAKA HUU
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia),
akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme Nchini (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa
ukarabati wa ujenzi wa vivuko vitatu jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia)
akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa ukarabati wa
ujenzi wa vivuko vitatu jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Le- Kujan
Manase akitoa maelezo ya moja ya kifaa kinachotumika kwenye kivuko cha
MV Magogoni kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kulia Profesa
Makame Mbarawa wakati alipokagua mradi huo.
Muonekano
wa Kivuko cha MV. Magogoni kikiwa kwenye hatua za mwisho za matengezo
yanayofanywa na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya
Mwanza na TEMESA Jijini Dar es salaam.
Mtaalam
wa kampuni M/S Songoro Marine Transport Cortyard ya Mwanza (Wanne
kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa alipokagua ukarabati na ujenzi wa Vivuko vya Old
Magogoni, Pangani na New Magogoni.
Mafundi
wa M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya Mwanza na TEMESA
wakiendelea na kazi ya ujenzi wa kivuko kipya jijini Dar es salaam.
ULEDI: MICHANGO YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII TUTAPELEKA KWA WAKATI
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu,
Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa akizungumza na watumishi wa ofisi
hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni
21,2016). Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM
anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Bw. Uledi
Mussa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo
kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21,
2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM
anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Bw. Uledi
Mussa alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao
kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21, 2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………….
KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Uledi Mussa
amesema atahakikisha michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya watumishi
wa Ofisi hiyo inafikishwa kwa wakati.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo
leo (Jumanne, 21 Juni, 2016) wakati akijibu maswali ya watumishi wa
Ofisi hiyo mjini Dodoma katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma
inayoanzia Juni 16 hadi 23 ya kila mwaka.
Kila mwaka Tanzania imekuwa
ikiungana na mataifa mengine ya Bara la Afrika kuadhimisha Wiki ya
Utumishi wa Umma Barani Afrika ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni
Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi:kuelekea katika Afrika tunayoitaka.
“Nitafuatilia michango ya
watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha inafika kama
inavyotakiwa na kwa wakati ili hata wanapomaliza muda wao wa utumishi
wasihangaike,” amesema.
Katika hatua nyingine Uledi
amewataka Wakuu wa Idara kuandaa mpango wa mafunzo kwa watumishi na
washirikishe kila mtu katika idara husika kabla ya kuuwasilisha kwake.
Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati
akijibu maswali ya baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, ambapo Anjani
Ngulukia (Msaidizi wa Ofisi) alitaka kupatiwa ufanunuzi kuhusu suala la
michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imekuwa haipelekwi kwa
wakati.
Pia mtumishi mwingine Ernest
Msabalala ambaye ni Mtunza Kumbukumbu Mkuu aliomba ofisi iandae
utaratibu wa kuwa na mafunzo kwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.
WIZARA YA HABARI YAKUTANA NA WADAU WA KUJADILI NA KUBORESHA SERA YA SANAA ZA MAONESHO
Kaimu
Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akizungumza na wadau wa Shirikisho la
Sanaa za Maonesho kuhusu mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za
Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha
Bibi. Shani Kitogo na kulia ni Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw.
Richard Kundi.Na Anitha Jonas – WHUSM
Rais
wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. William Chitanda akieleza
changamoto za shirikisho kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya
kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Bw. Efraim Zakaria kutoka kikundi cha Watoto Arts
Organization (WAAO).
Katibu
wa Kikundi cha Binti Leo Bi. Agness Lukanga (katikati) akieleza
utendaji wa kikundi chao kwa watendaji wa masuala ya Sanaa na
Utamaduni wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya
sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Chama
cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga.
Mjumbe
wa Kikundi cha Sherehe Arts Association (SAA) Bi. Columba Samjela
akiwaeleza watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
(hawapo pichani) mikakati waliyonayo ya kuimarisha Sanaa leo jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa (SAA) Bi. Grace Meena.
Mjumbe
wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. Denis Mango akifafanua shughuli
za shirikisho katika kikao kilichofanyika Juni 21,2016 Jijini Dar es
Salaam na Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katikati ni Bw. Omari Kichapwi, Mjumbe wa Umoja wa Washairi Tanzania
(UWASHATA).
Mjumbe
wa Kikundi cha Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) akieleza jambo
kwa Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo
pichani) kuhusu umuhimu wa Sanaa ya Mashairi. Kulia ni Mjumbe wa
UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala.
Baadhi
ya wadau wa Sanaa za Maonesho walioshiriki kikao na watendaji wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bibi. Shani Kitogo (hayupo pichani) alipokuwa akifafanua jambo
kuhusu fani ya ushariri leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga akitoa
maoni ya kuboresha sekta ya Sanaa za Maonesho kwa watendaji wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) leo jijini Dar
es Salaam. Wapili kushoto ni Mjumbe wa UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala.
MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira Mhe. Jenista
Mhagama akitoa maelezo Bungeni leo kuhusu hatua zitakazochukuliwa na
Serikali dhidi ya waajiri wote wanaoshindwa kuwasilisha michango ya
waajiriwa wao katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuwa watachukuliwa hatua
kali za kisheria ambapo tayari Serikali iko kwenye hatua za mwisho
kukamilisha mchakato wa kuunda kikosi kazi kitakachoshughulikia swala
hilo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mh. George Masaju leo Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrisom Mwakyembe akijibu moja ya hoja
zilizotolewa Bungeni leo na Mbunge wa Nchemba Mhe. Juma Nkamia
aliyetaka kujua uhalali wa mtuhumiwa aliyetenda kosa la jinai la
kumtukana Rais kuachiwa huru na kwenda kutafuta fedha za kulipa faini
ilihali kosa alilotenda limemdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira, Mhe. Jenista
Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde leo
Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia
Ackson akijibu miongozo iliyoombwa na wabunge mapema leo Bungeni mjini
Dodoma kabla ya Kuahirisha shughuli za Bunge leo Mjini Dodoma.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Kisasa ya mjini Dodoma wakiwa katika ukumbi wa
Bunge kwa lengo la kujifunza majukumu ya Bunge leo Mjini Dodoma wakati
wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe.Dkt. Susan Kolimba akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa ili
kuimarisha Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwa ni moja ya
hatua za kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na mataifa
mbalimbali.
Naibu
Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe.
Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu maswali yaliyoulizwa na Wabunge leo
Bungeni juu ya mikakati ya Serikali kuwawezesha wanawake kupitia Benki
ya wanawake kwa kufungua madirisha maalum Katika Mikoa mbalimbali hapa
Nchini yatakayosaidia kuwasogezea wanawake huduma za Benki hiyo ili
waweze kujikwamua kiuchumi.
Wanafunzi
wa chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Wakiwasili katika ukumbi wa Msekwa Bungeni
Mjini Dodoma leo kwa lengo la kujifunza jinsi Bunge linavyotekeleza
majukumu yake.
Muhimbili watoa ufafanuzi kuhusu wagonjwa wa Seli Mundu
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Profesa.
Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa na Gazeti la
Mwananchi kuhusu huduma hospitalini hapo leo jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Bibi.
Agness Mtawa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitalini hapo Aminiel
Aligaesha.
Picha na: Frank Shija, MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………………
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru ametoa
ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwanchi la tarehe
21 Juni 2016 zilizo kuwa zinasema kuwa wagonjwa wa Seli Mundu
wanalipishwa ili kupata huduma ya matibabu yao tofauti ilivyokuwa awali.
Akitoa ufafanuzi huo Profesa
Mseru amesema kuwa kwa habari hizo siyo za kweli kwani wagonjwa wa Seli
Mundu wanatumia utaratibu wa kawaida ambapo mgonjwa utibiwa katika
maeneo wanayotoka na anapaswa kuchangia gharama za matibabu isipokuwa
kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Aliongeza kuwa hapo awali
kulikuwa na mradi wa utafiti wa Seli Mundu ulioenda sambamba na utoaji
wa matibabu kwa wagonjwa waliojumuishwa katika mradi huo uliodumu kwa
muda wa miaka 10 hadi ulipofikia ukomo machi 30 mwaka huu.
Baada ya mradi huo kumalizika
wagonjwa wote walirejea katika maeneo yao ambapo huko wanaendelea na
matibabu kupitia utaratibu wa kawaida huduma za matibabu.
KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI NA NAIBU WAKE WAKUTANA NA WANANCHI ANA KWA ANA NA KUTATUA KERO ZA ARDHI
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu
Kayandabila Akiwakaribisha wananchi walio na kero za migogoro ya Ardhi
ofisini kwake ili kuzitatua kero zao ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma 2016.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses
Kusiluka (katikati mwenye suti na tai) akipokea kero za wananchi
zinazohusu migogoro ya Ardhi ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma 2016.
……………………………………………………………………………………………………….
Katika kuadhimisha Wiki ya
Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kwa kupitia watendaji wake wakuu leo tarehe 21/06/2016 amefanya
utaratibu maalumu wa kukutana na wananchi wenye kero na migogoro ya
ardhi. Katika kutekeleza hilo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka
wamekutana na wananchi ana kwa ana ili kuwasikiliza na kuzipatia
ufumbuzi kero na migogoro yao inayohusu ardhi na nyumba.
Hatua hii imefuatia baada ya hapo
jana tarehe 20/06/2016 viongozi hao kukutana na watumishi wa Wizara
hiyo na kutatua kero zao zinazohusu maslahi ya watumishi ambapo kwa
mwaka huu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameamuliwa yafanyike
kwa utaratibu huu.
DK. MWAKYEMBE AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI LEO MJINI DODOMA
Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Waandishi wa
Habari leo Mjini Dodoma kuhusu maadili ya Vyombo vya Habari katika
kuhabarisha Umma juu ya miradi ya maendeleo na jinsi vinavyoweza
kuwasidia wananchi kuleta maendeleo na kuepuka kutoa taarifa za
upotoshaji.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Katiba na
Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Vyombo vya Habari leo Mjini Dodoma.
(Picha Zote na Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma)
NCC yapanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)
chini ya mkakati wa kukuza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi
Tanzania (CoST -Tanzania) limepanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji
katika sekta hiyo ili kuondokana rushwa na kuhakikisha wananchi
wanaelewa thamani halisi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya umma.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt
Leonard Chamuriho wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowashirikisha wadau
wa ujenzi kutoka nchi mbalimbali Duniani kujadili changamoto
zinazoikabili sekta hiyo.
Dkt. Leonard Chamuriho amesema
kuwa kikao hicho kina lengo la kuweka uwazi katika miradi yote
inayotekelezwa kwa fedha za wananchi ili kuondokana na rushwa
zinazojitokeza katika kufanikisha miradi hiyo.
“Rushwa inazungumziwa sana katika
suala la ujenzi ila naomba tuzidishe uwazi katika sekta hii na
kuwafanya wananchi waelewe kinachoendelea katika miradi yao hii
itatutasaidia sana kupambana na rushwa, na taswira ya kuwa na rushwa
katika miradi ya ujenzi haitakuwepo”,alisema Dkt. Chamuriho.
Dkt. Chamuriho ameongeza kuwa
msimamo wa Serikali ni kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa katika
miradi ya ujenzi na kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji Kutasaidia
kuondokana kabisa na suala la rushwa.
Aidha, Dkt. Chamuriho
amewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo Idara ya Maendeleo ya Kimataifa
(DFID), Benki ya Dunia (WB) pamoja na Serikali ya Uholanzi wanaoendelea
kusaidia miradi ya ujenzi iliyo chini ya Baraza la Taifa la Ujenzi
(NCC) na kutoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kusaidia
katika miradi mingine ya maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
CoST -Tanzania, Kazungu Magili amesema kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo
ni kuifanya CoST-Tanzania kujitegemea kwa kutosimamiwa na taasisi
yoyote na kupitia mazungumzo yaliyofanywa kati ya CoST na Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ana imani kuwa yataweza kufikia muafaka
na kuifanya kuwa sekta inayojitegemea kabla ya mwezi Julai mwaka 2016.
MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 MKOANI KILIMANJARO
Waziri
wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki
(Mb) akizungumza na watumishi wa umma wa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni
muendelezo wa ziara zake katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma
2016.
Waziri
wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki
(Mb) akizungumza na Menejimenti ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni sehemu
ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 Mkoani Kilimanjaro. Mhe.
Kairuki amesisitiza Maafisa Rasilimaliwatu wafanye kazi kwa weledi na
watakaoshindwa hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Baadhi
ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa
Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki
(hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016
Mkoani Kilimanjaro.
Vyombo vya Habari nchini Vimetakiwa kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yake
Na: Frank Mvungi – MAELEZO- Dodoma
Vyombo vya Habari nchini
Vimetakiwa kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yake ili kusaidia
Taifa kufikia maendelo ya kweli na endelevu.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa
mkutano na vyombo vya habari.
Akifafanua Mhe. Mwakyembe
amesema ili Taifa liwe na Maendeleo ni lazima kuwa na Vyombo vya Habari
vinavyozingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari pamoja na Sheria
na Kanuni zinazosimamia tasnia hiyo.
“Navipongeza Vyombo vingi vya
Habari hapa nchini ambavyo vinafanya kazi nzuri ya kuelemisha Umma na
kuchochea maendeleo ya nchi yetu ila kuna wachache ambao kwa makusudi
wameamua kupotosha Umma” alisisistiza Dkt. Mwakyembe
Hivi Karibuni gazeti moja lilitoa
taarifa zinapotosha Umma kwa kumhusisha Waziri huyo na maswala ya
Ufisadi ambapo alitumia fursa hiyo kuviasa vyombo vya habari kuepuka
kuandika au kusambaza habari ambazo ni za upotoshaji na hazina maslahi
kwa Taifa na hazijafanyiwa uchunguzi wa kina.
Akitolea mfano chombo hicho cha
habari Mwakyembe amesema kuwa, kimekuwa kikiripoti taarifa zinazogusa
masuaa ya Ulinzi na Usalama pasipo kuangalia maslahi ya Taifa kwanza
hali inayoonyesha kukosekana kwa uzalendo.
Mwakyembe aliongeza kuwa tasnia
ya habari imekuwa na ni vema sasa waandishi wote kuzingatia maadili ya
taaluma hiyo ili kuepuka kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa
kukiuka sheria na kanuni za uandishi wa habari.
Tasnia ya Habari ni muhimili
muhimu katika kuchochea Maendelo ya Taifa lolote lile kwa kuelimisha
kuhamasisha na kuamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo.
Serikali kuendelea kutoa dawa bure kwa wagonjwa wa ukimwi na kifua kikuu
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa sera yake ya
kutoa dawa bure kwa wagonjwa wa kifua kikuu, ukimwi, mama wajawazito,
wazee na watoto chini ya miaka mitano inaendelea.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma
na waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akitolea ufafanuzi
wa swali la Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani kikwete juu ya taarifa
zilizotolewa na vyombo vya habari kuwa utoaji wa dawa bure kwa makundi
hayo ya watu umesitishwa na wanatakiwa kulipia.
“Hakuna mabadiliko yoyote katika
sera ya kutoa dawa bure kwa wagonjwa wa ukimwi, kifua kikuu, mama
wajawazito, wazee na watoto chini ya miaka mitano, aidha nitaitaka
hospitali ya Taifa ya Muhimbili inipatie maelezo juu ya taarifa hizo,”
alisisitiza, Mhe. Ummy.
Wakati huo huo, naibu waziri wa
wizara hiyo, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa wizara hiyo kwa
kushirikiana na wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji wanaandaa
mkakati wa kuongeza uzalishaji wa dawa nchini ili angalau kukidhi
asilimia 60 ya mahitaji katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aidha wizara hiyo pia iko katika
mikakati ya kuunda chombo cha kusimamia gharama na bei zinazotozwa na
vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa pamoja na bei za dawa na vifaa
tiba ili kuthibiti uongezaji holela wa bei za dawa na vifaa tiba.
Huduma ya chakula kwa wagonjwa wanaolazwa Muhimbili kuanza mwezi Julai
Mkurugenzzi
wa Uuguzi Hospital ya Taifa Muhimbili Bibi. Agness Mtawa wakati
akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkuu wa Kitenggo cha Mawasilinano Bw. Aminiel Aligaesha.
……………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, MAELEZO
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kuanza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo
kuanzia tarehe 1 mwezi Julai 2016 ambapo mgonjwa atachangia gharama ya
shilingi elfu hamsini.
Hayo yamebainishwa na Afisa
Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha
wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
Aligaesha amesema kuwa wameamua
kuchukua hatua hiyo ili kutoa fursa kwa Hospitali hiyo kujikita katika
majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.
Aliongeza kuwa kutokana na
kutolewa kwa huduma ya chakula hospitalini hapo kutasababisha mabadiliko
ya ratiba ya kuona wagonjwa kwa kuondoa muda wa saa 6 – 8 mchana ambao
ulikuwa unatumiwa na ndugu kwa kuleta chakula kwa wagonjwa wao, badala
yake muda wa kuona wagonjwa utabaki saa 12.00 -1.00 Asubuhi na saa 10.00
-12 jioni.
Aidha Hospitali inataka
kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama
kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo
kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa anaweza
kutumia kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na
mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa
ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi
ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha
nyingi kwenye usafiri.
Kwa uande wake Mkurugenzi wa
Uuguzi wa Hospitali hiyo Agness Mtawa amesema kuwa huduma hizo za
chakula zitaondoa adha kwa ndugu wa wagonjwa kwa ambao walikuwa
wanatumia muda huo kufika Hospitalini hapo.
Agness iliongeza katika huduma
hiyo ya chakula wahudumu na wauguzi ndiyo wenye jukumu la kusaidia
wagonjwa wenye mahitaji maalumu kama ktutoweza kujilisha wenyewe.
Huduma hiyo ya chakula itatolewa
kupitia mzabuni aliyepatikana na kuongeza kuwa mgonjwa atachangia
gharama ya shilingi 50,000 ambapo shilingi 10,000 itatumika kwa huduma
ya Kitanda, huduma ya ushauri wa Daktari 10,000 na shilingi 30,000 kwa
ajili ya chakula kwa siku muda wa siku tano.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA MAFUNZO YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake
Wajasiriamali yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF)
kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.(PICHA NA OMR)
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia
kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni
Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mtendaji
Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa
ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19.
Sehemu
ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake
Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther
Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi
wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar
es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa
mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa
Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna
Mkapa.
Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline
Maleko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa
Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo
kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani
jijini Dar es Salaam.
KIKUNDI CHA UPENDO WOMEN’S GROUP CHA UBELGIJI CHATOA SHUKRANI KWA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI
Dr.Pendo Maro ambaye ndiye alikuwa mshehereshaji wa hafla ya uchangishaji wa fedha kwa kikundi cha kina mama cha Upendo Women’s Group nchini Ublgiji akifungua uchangishaji wa sherehe hizo |
Katika kuchangisha fedha ili kusaidia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania, Upendo Women’s Group waliaanda maonyesho mbalimbali ikiwemo na maonyesho ya mavazi.{picha zote na Maganga One Blog} |
Mmoja wa wageni waalikwa ambaye alichangia Harambee siku hiyo kwa kununua Kahawa halisi kutoka Tanzania.Wana Upendo wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki wa wageni hao |
TIGO PESA YATOA FURSA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI
Mkuu wa Huduma za Kifedha
za Tigo, Ruan Swanepoel (katikati), akizungumza na waandishi wa habari
Makao Makuu ya Tigo Makumbusho Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Tigo
Pesa kutoa fursa za biashara kwa wajasiriamali. Kulia ni Mkuu wa Masoko
wa Tigo, Temitope Ayedum na kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William
Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
WAJASIRIAMALI
wa kidijitali pamoja na wabunifu wa matumizi ya simu Tanzania hivi sasa
wanaweza kuleta ufumbuzi zaidi kwa mteja katika soko na kuongeza shughuli zao za kibiashara kupitia jukwaa la huduma za kifedha kwa simu la Tigo Pesa.
Tigo Pesa ambayo inaongoza Tanzania kwa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya simu imefuatilia uhusiano
wake wa karibu na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuanzisha
programu ambazo zinatoa mwongozo wa hatua kwa hatua kwa wajasiliamali wa kijitali kwa kuiunganisha Tigo Pesa katika matumizi yao. Hatua hiyo inajionesha katika wavuti wa www.tigo.co.tz.
Akizungumza katika mkutano na waandioshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za
Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Tigo imewekeza zaidi ya dola milioni 15 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika kuboresha jukwaa la ngazi ya kimataifa na huduma ili kuendelea kutoa huduma sahihi za uhakika, zinazofikiwa na salama kwa wateja.”
Swanepoel alifafanua:“Jukwaa hilo la kuwanunganisha wateja wa Tigo Pesa na mitandao mingine kwa kiwango kikubwa itapunguza changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo katika kuunganisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika kupokea malipo kutoka kwa wateja wake katika hali isiyo na hitilafu na hivyo kuongeza wigo jumuishi kifedha kote nchini.”
Swanepoel aliongeza kwamba, “Tigo pesa imejikita kuangalia hali na uwezo wa kuwezesha maendeleo ya huduma za ubunifu na kujumuisha bila tatizo mitandao mingine ili kuwapa wateja faida zaidi za huduma ya fedha kwa njia ya simu.”
Itakumbukwa kwamba kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, Tigo Pesa ilikamilisha ushirikiano wake na watoaji wengine wa huduma za fedha kwa njia ya simu na benki nchini kwa kuzifanya huduma hizo kupatikana kwa watu wengi zaidi. Tigo Pesa pia ilizindua kifaa cha wateja kwa Android kwa watumiaji IOS, kwa kuwapatia njia rahisi watumiaji pindi wanapotumia huduma zake.
Mfumo wa kuendesha na kutumia program hii ijulikanayo kama ‘Application Program Interface (API) ni muundo wa maelekezo na viwango vya kufikia mtandao kwa kutumia zana za kompyuta au zana za kimtandao. Ili kuzifikia programu za Tigo Pesa inamaanisha wanafunzi wa vyuo, wajasiriamali wa biashara elektroniki , wabunifu wa vifaa na wataalamu wengine wa teknolojia ya habari wanaweza kuibuka na vifaa au kuwezesha vifaa vilivyopo kwa kuunganisha ufumbuzi wao na Tigo Pesa.
Muhimbili yaboresha Huduma ya Chakula kwa Wagonjwa
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), Bw. Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari LEO
kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa
(special diet) wanaolazwa MNH kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini
wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo hicho LEO katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi
wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa
akifafanua jambo LEO katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu
hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa. Kushoto
ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha akiwa
kwenye mkutano huo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aligaesha akifafanua jambo
kwenye mkutano na waandishi wa habari LEO jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………….
Yawaondolea usumbufu ndugu wa wagonjwa kupeleka chakula mara tatu kwa siku
· Ndugu watapata muda wa kuendelea na shughuli za uzalishaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa
kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu
na gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao
waliolazwa mara tatu kwa siku katika hospitali hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari leo Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya
Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha amesema
hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa
wote wanaolazwa.
Bw. Aligaesha amesema Hospitali inataka kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.
“Aidha Hospitali inataka
kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama
kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo
kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya
shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea
bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara
nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano
hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye
usafiri” amesema Bw. Aligaesha
Ameongeza kuwa adha ya pili
wanayopata ndugu ni usumbufu ambapo inabidi kuacha shughuli nyingine za
uzalishaji ili kuja kuleta chakula mara tatu kwa siku, hivyo
kuingiliana na shughuli zao za kiuchumi na kimandeleo na kushindwa
kuzalisha. Hivyo jukumu hili linachukuliwa na Hospitali kuwaondolea adha
hii.
·
“Pia kuna baadhi ya ndugu
wamekuwa wakishindwa kuwaletea chakula wagonjwa wao hivyo hospitali
ililazimika kuwapatia chakula ambacho kilikuwa kwa ajili ya wagonjwa
wanaotoka mikoani wasio na ndugu hapa Dar Es Salaam” amesisitiza Bw.
Aligaesha.
Amesema kumekuwepo na
ongezeko la msongamano wa watu ndani ya Hospitali toka asubuhi saa 12
mpaka saa 12 jioni, suala linaloingiliana na utoaji huduma hasa saa za
mchana kwani muda wa saa 6.00 hadi saa 8.00 mchana ulikuwa unaingiliana
na majukumu ya kiutendaji ambapo majopo mbalimbali ya watalaamu yamekuwa
yakiendelea na raundi za wagonjwa waliolazwa. Hii wakati mwingine
imesababisha mgonjwa kutokupata huduma stahiki kutokana na muingiliano
huu.
·
“Vile vile msongamano huu ni
changamoto kwa ajili ya masuala ya kiusalama ambapo kati ya watu
wanaoingia Hospitali kwa kigezo cha kuja kuona wagonjwa kuna wanaoingia
kwa lengo la kufanya uhalifu ikiwemo wizi wa mali za Hospitali, magari
pamoja na vifaa vya magari” alisisitiza.
Amesema kwa kufanya hivyo,
Hospitali itapunguza baadhi ya gharama za uagizaji wa vyakula kwa
wazabuni, kulinda upotevu na baadhi ya vyakula kuharibika wakati
mwingine kwani utunzaji wa vyakula una mahitaji makubwa.
Bw. Aligaesha amesema
Hospitali inakusudia kutoa chakula chenye ubora na viwango vinavyotakiwa
kwa wagonjwa ikiwemo kutoa chakula maalumu (special diet) kwa wagonjwa wenye uhitaji huo.
Kuhusu utaratibu huo Bw.
Aligaesha amesema Mzabuni ndiye atakayepika chakula kwa wagonjwa wote
waliolazwa na atatayarisha, atakipeleka na kukikabidhi katika wodi
husika ambapo jukumu la kumpa mgonjwa kifungua kinywa, chakula cha
mchana na jioni linabaki wa Hospitali.
Amesema wagonjwa watapatiwa
milo mitatu kwa siku yaani asubuhi, mchana na jioni kazi itakayofanywa
na muuguzi wa zamu ambaye atahakikisha wagonjwa wote wamepata chakula
kufuatana na mahitaji (diet list) iliyowasilishwa jikoni kutokana na mahitaji yao ya kiafya.
Kutokana na uamuzi huu,
utaratibu wa ndugu kuleta chakula kwa wagonjwa waliolazwa wakati wa
mchana umefutwa na hivyo mchana hatutakuwa na nafasi ya ndugu kuja
kutembelea wagonjwa. Muda wa kutembelea wagonjwa utakuwa asubuhi saa 12
hadi saa moja kamili na saa 10:00 jioni hadi saa 12:00jioni ndipo ndugu
wataruhusiwa kuingia ndani kuwaona ndugu zao waliolazwa. Katika muda huo
ndugu ataruhusiwa kuja na chakula chochote anachofikiri atamuongezea
mgonjwa wake kama matunda n.k
Bw. Aligaesha amesema mgonjwa
aliyelazwa atachangia kiasi cha shilingi 50,000 atakapolazwa ambapo
kati ya hizo, shilingi elfu 10,000 itakuwa ni gharama ya kumuona daktari
(Consultation), shilingi elfu 10,000 ikiwa ni gharama ya kulazwa
na bei ya chakula itakuwa shilingi elfu 30,000 sawa na shilingi elfu
6,000 kwa siku. Wastani wa mgonjwa kukaa wodini ni siku tano. Gharama
hizo zinahusika kwa muda wote atakaokuwa amelazwa.
Kwa sasa Hospitali inatoa
chakula kwa wagonjwa 650 ambao wamepata rufaa kutoka hospitali za nje ya
mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama wastani wa shilingi 1.8 bilioni kwa
mwaka, sawa na shilingi 150 milioni kwa mwezi kwa vyakula pamoja na
gharama nyingine kama vile za nishati. Takribani wagonjwa kati ya 600
na 700 ambao rufaa zao ni kutoka Hospitali za Dar es Salaam walikuwa
hawapati chakula kutoka Hospitalini, na ilibidi ndugu zao wawaletee
chakula. Hata hivyo, Hospitali ilikuwa inawapatia chakula tu kama ndugu
zao wakishindwa kufanya hivyo.
“Uongozi wa Hospitali unaamini
kwamba mabadiliko haya hayatamuongezea mgonjwa gharama, bali
yatampunguzia gharama pamoja na ile adha kama ilivyoainishwa hapo juu.
Aidha, uongozi unaamini kwamba uamuzi huu unaendana na azma nzima ya
kuboresha utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuboresha
mazingira ya Hospitali. Tunaomba ushirikiano wenu katika kutekeleza
jukumu hili ili kusudi wagonjwa waweze kuhudumiwa vizuri zaidi”
amesisitiza Bw. Aligaesha.
No comments :
Post a Comment