Pages

Tuesday, June 21, 2016

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAKUTANA NA WANACHAMA WAKE WA MKOA WA MANYARA KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YAHUSUYO HUDUMA ZA MFUKO


Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi
Mwakilishi wa Katibu Tawalawa mkoa wa Manyara Bw.Longino Kazimoto (katikati), akifungua kikao cha pamoja kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na wanachama wake wa mkoa wa Manyara. Mkutano huo ambao uliandaliwa na PSPF katika utaratibu wake wa kukutana na wanachama wake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuboresha huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa wateja ulifanyiki mjini Babati.
p3 
Afisa Mfadhiwi wa PSPF mkoa wa Manyara Bw. Said Ismail, akitoa hotuba wakati wa kikao cha pamoja kati ya PSPF na wanachama wake wa mkoani Manyara kilichofanyika mjini Babati. PSPF inautaratibu wa kukutana na wanachama wake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuboresha huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa wateja.Wengine pichani ni Mwakilishi wa Katibu Tawalawa mkoa wa Manyara Bw.Longino Kazimoto (katikati) na na Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi
p4
Baadhi ya washiriki wa kikao cha pamoja  wakifuatilia kwa karibu.p5 
Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na  wanachama hao wakati wa semina hiyo.

SEKTA ISIYO RASMI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII.

KIBO1Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde.
KIBO2 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji  kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde akiwaeleza waandishi wa habari juhudi za Serikali katika kuboresha na kupanua wigo wa huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Sheria kutoka SSRA, Bw. Onorius Njole.
KIBO3Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Program maalum ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Waratibu wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii nchini kote. Zoezi hilo linaenda sambamba na usajili wa mifuko hiyo. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde na kushoto ni Afisa Uhusiano Ally Masaninga.
KIBO4 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa SSRA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam ambao ulilenga kuufahamisha umma maboresho mbalimbali katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini.
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imejizatiti kupanua wigo na kuboresha huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa kundi la watu walio kwenye sekta isiyo rasmi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole wakati  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe.
Bw. Njole alisema kuwa katika kuhakikisha watanzania wote wananufaika na huduma za hifadhi ya jamii, SSRA inafanya tafiti mbalimbali na kuhamasisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kubuni mafao mbalimbali yanayolenga kuwafikia wananchi wote walio kwenye sekta isiyo rasmi.
Ili kufanikisha hilo, mwaka 2015 SSRA ilifanya utafiti katika sekta ya usafirishaji na kubaini kuwa asilimia 83 ya waendesha vyombo vya usafiri mijini wakiwemo waendesha bodaboda wako tayari kuchangia kwa hiari katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
“Kutokana na matokeo hayo mamlaka ilipendekeza kuanzishwa kwa Mpango Maalum ujulikanao kama Informal Sector Scheme ambapo watu waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi watapata nafasi ya kunufaika na huduma ya hifadhi ya jamii.” Alisema Njole.
Njole aliongeza kuwa tayari baadhi ya mifuko imekwishaandaa mafao maalum yanayowalenga waendesha bodaboda, bajaji, daladala na mama lishe ambao watapata fursa ya kuchangia kiasi kidogo kila siku kulingana na kipato chao ili kupata huduma za hifadhi ya jamii kama vile akiba ya uzeeni, matibabu na mikopo.
Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde alieleza kuwa mamlaka hiyo inaendelea na zoezi la kutambua na kusajili Mifuko yote ya Bima ya Afya ya Jamii (CHFs) kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi.
Pia Bi. Sarah alisema kuwa SSRA imeandaa program maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Waratibu wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii nchini kote na zoezi hilo linaenda sambamba na usajili wa mifuko hiyo kwa mujibu wa Sheria ya SSRA, Sura ya 135.
“Program hii imeanzia Kanda ya Kati ambako ilihusisha Wilaya 27 na jumla ya CHF 5 zilisajiliwa na nyingine 22 zinakamilisha taratibu za usajili. Zoezi hili linatarajiwa kuendelea Juni 22 kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambako jumla ya CHF 25 zinatarajiwa kusajiliwa.”
Sambamba na program hiyo Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wizara yenye dhamana ya masuala ya hifadhi ya jamii na SSRA inafanya mapitio ya mfumo wa usimamizi wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF) ili kupata mfumo utakaoweza kutoa huduma ya afya kwa watanzania wote.

MERCY KITOMARI: MJASIRIAMALI KIJANA ANAYEFIKIRIA MAKUBWA

Mjasiriamali kijana Mercy Kitomari akiwa ofisini kwake wakati wa mahojiano.
 
Modewjiblog ilipata bahati ya kuzungumza ana kwa ana na Mercy Kitomari mmoja wa wajasiriamali wanawake vijana ambaye anafikiria kuwa na kiwanda kikubwa cha ashkrimu (ice cream) ifikapo mwaka 2020 akizisafirisha na kuziuza Tanzania nzima na Afrika Mashariki. Wapi alipotokea, yuko wapi kwa sasa, ni machungu gani aliyokumbana nayo na anaishauri nini serikali na wajasiriamali wenzake. Haya yote utayajua katika mahojiano haya .Soma…
 
MODEWJI BLOG: Role model wako nani?
MERCY: Magufuli. You know why?(unajua kwanini?) ametuweka wazi kabisa kwamba maisha ni changamoto na tusikubali kushindwa ni lazima kupambana na kufanyakazi kwa bidii na maarifa kuondoa vigingi vyote vinavyotukwamisha. Amenifanya nifanye kazi kwa bidii. Nataka kuwa mwanamke anayefanya mabadiliko. Hakuna kitu kinachokuja kirahisi. Nataka kuwa mwanamke yule ambaye anaonesha tofauti nataka kuifanya nchi yangu iniringie.
Sijisikii vibaya kwa kuwa niko mpweke, kitu cha kwanza ni kazi, nataka kuifanya mwenyewe ili wanawake wenzangu watambue kwamba tunaweza kufanya wenyewe, bila msaada wa mwanaume. Ndio unahitaji mume lakini si katika hili suala la ujasiriamali, mwanamke peke yako unaweza kuleta mabadiliko.
Nataka kuwa mwanamke ambaye Afrika itaniringia na taifa langu litanichekelea kwamba mimi ni binti yao.
MODEWJI BLOG: Turejee katika masuala ya kodi. Kodi ni muhimu sana kwa mapato ya serikali. Je Kodi zinazowatoza zinawasaidia au zinawavunja moyo?
MERCY: To be honest (kusema ukweli) zinatuvunja moyo. Nyingi ya hizi kodi hazitusaidii sisi watu wa hali ya chini kunyanyuka, zinatukwamisha.Kodi zimewekwa bila kujali madaraja. Anayeanza na aliyemo, mwenye kipato kidogo na kikubwa. Na yote hayo yanafanyika bila kuzingatia kwamba kuwapo kwa wajasiriamali wengi ndio kuchangamka kwa soko la wakulima na pia ajira viwandani.
Mimi ninayetengeneza ashkrimu natengeneza ajira; ninatengeneza soko kwa yule anayeleta matunda sokoni kwani naenda kununua matunda kwa ajili ya ashkrimu. Kodi nyingi zinakandamiza, haziangalii ukubwa na udogo wa biashara. Mtu anabiashara inayoingiza mamilioni kwa siku anawekwa kundi moja na anayeingiza laki moja.
Muonekano wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato la Mercy Kitomari lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.
 
MODEWJI BLOG: Ukikutakana na role model wako utamuomba nini?
 
MERCY: Nikikutana na Magufuli? Kwanza naomba nikutane naye! Nikikutana naye nitamwambia ofisi zote za huduma kwa wananchi ziwe katika mtandao (online) watu tuweze kufanya kila kitu katika mtandao. Na Serikali za mitaa lazima zirejeshe faida kwa wananchi kwa kodi zao.
Wanatakiwa watufundishe vitu vingi. Watufundishe kuwa wajasiriamali namna ya kufunga na kuuza bidhaa zetu wasifanye tu shughuli za kukusanya ushuru na kodi, watuambie namna ya kuendelea mbele ili waendelee kukusanya ushuru na kodi au hawatakusanya kitu tukikwama.
Ni lazima wawekeze kwa wajasiriamali ili kuwepo na hali bora zaidi.
Ukitazama soka katika televisheni unaona matangazo mengi ya krisp hapa kwetu wapo wadada wanaotembeza za ndizi au viazi hawa wakifundishwa namna nzuri ya kuweka chakula chao ni dhahiri tutakuwa na wajasiriamali wengi. Wanatakiwa watuelekeze mambo mengi bidhaa za kwenye ‘super market’ zinakuaje na kadhalika wasibaki kudai na kuvuna hela tu watusaidie tuweze kuwapatia fedha zaidi. Lakini nambieni lini nitakutana na role model wangu huyu…….ha ha ha ha….kicheko….!
MODEWJI BLOG: Wasaidizi wake wakisoma makala haya watajua nini unahitaji na pasi shaka watakukutanisha naye.Ni watu wema hawa, hawawezi kukosa kukupangia muda wa kumuona Role Model wako umweleze mambo ya kukusaidia wewe na wengine wa aina yako.
MERCY: Nakudai hilo kwani natamani sana atukutanishe wanawake vijana wajasiriamali ili azungumze nasi. Najua ameshazungumza na wafanyabiashara wakubwa, lakini akituona na sisi atatambua uwezo wetu na namna ambavyo angetusaidia tungeibuka wengi na kuweka ndoto ya Tanzania ya viwanda katika ukweli.
You know (unajua) nilikutana na wanawake wenzetu wajasiriamali kutoka Uganda na Rwanda naona wameendelea kwelikweli na siri ni serikali zao kuhakikisha kwamba wanaendelea.
Wapo wanawake waliokata tamaa hapa, nimekutana nao nikasema tusichoke hata kidogo serikali ya sasa inataka viwanda ni lazima kuisaidia kujua tunawezaje kufikia ndoto hiyo, kuna vizingiti hapa wakiviondoa tutaweza.
Hatupaswi kukata tama hasa kutokana na serikali ya sasa kutaka kuwapo na viwanda.

Mkutano wa ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika mjini Beijing Nchini China

N5 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akieleza jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuhama kutoka mfumo wa urushaji wa matangazo ya Televisheni kutoka Analogia kwenda Digitali katika mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za  Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
N1 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa katika ukumbi wa mikutano leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za  Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
N2 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang wakibadilishana mawazo leo  kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
N3 
Mkutano wa Ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya nchi za Afrika na China ukiendelea mjini Beijing nchini China.
N4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa wakibadilishana mawazo  leo kabla ya kuanza  kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Picha na Mpigapicha wetu

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA OFISINI HAZINA.

1Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Gideon Manambo akizungumza na watumishi wa Wizara (hawapo pichani) katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Doto James.
2 
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa mkutano  huo  ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Doto James akifafanua hoja mbalimbali za  watumishi.
3 
Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa wamesimama kwa dakika chache kuwakumbuka watumishi waliotangulia mbele za haki kwa mwaka huu, katika mkutano huo.
4 
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
6 
Picha ya pamoja.
——————————————————————-
Wizara ya Fedha na Mipango imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano na Watumishi wake, lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto wanazo kabiliana nazo mahali pa kazi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James aliwataka Watumishi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Magufuli katika  kupambana na masuala ya rushwa, uzembe kazini na Watumishi hewa ambao wamekuwa wakiigharimu Serikali fedha nyingi katika kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema Wizara inajipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi hasa kwa wale wenye ulemavu kwa  kuwajengea miundombinu rafiki sehemu za kazi ili  kuongeza ufanisi kazini.
“Wizara pia inafanya vizuri katika masuala ya usawa wa kijinsia kwa kuwa na idadi inayoridhisha ya wanawake hasa katika ngazi za maamuzi, ikiwa ni pamoja na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wawili wanawake” . Alisisitiza James
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Bw. Gideon Manambo alisema kuwa, watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa  bidii ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ambayo yanahitaji watendaji wenye weledi wa kutosha ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Kwa upande wa watumishi wa Wizara, wameuomba uongozi kuhakikisha kunakuwepo na vitendea kazi vya kutosha ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na matokeo chanya ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.
Maadhimisho hayo yamefanyika kufuatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo uliagiza Wizara pamoja na Taasisi kuadhimisha Wiki hiyo kwa kutatua matatizo ya watumishi wa Umma pamoja na wananchi kwa ujumla katika maeneo yao ya kazi.
Imetolewa na: Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.

SERIKALI YAREJESHA MISAMAHA YA KODI KWA TAASISI ZA DINI, YATOA MASHARTI MAZITO

bajeti
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
——————————–
Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.
Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.
“Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo”Alisema Dkt. Mpango
Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria
Aidha, utaratibu mpya utazitaka Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.
“Taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi iliyokusudiwa” Aliongeza Dkt. Mpango
Dkt. Mpango alisema katika utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje
Alizitaja hatua nyingine kuwa ni wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini, Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha
Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake.
Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.

African countries and China have agreed to strengthen Africa – China Media Cooperation to improve media quality

Picha no. 5 
By Zamaradi Kawawa, Maelezo, Beijing, China.            
………………………………………..
African countries and China have agreed to strengthen Africa – China Media Cooperation to improve media quality through experience sharing of implementation of media policies, capacity building programs for journalists, digitalization and development of new media.
Sharing  Tanzanian experience in digital migration at the Third Forum on China – Africa Media Cooperation in Beijing today, Deputy Minister for Information, Culture, Arts and Sports Mrs Annastazia Wambura said Tanzania is now commemorating one year of migration from analogue to digital terrestrial television (DTT). She said although the process was challenging it was accomplished due to sound policies, regulatory framework and Government Commitment.
She told the forum that as of now, close to two million Tanzanians are enjoying quality television programmes from locally and foreign produced content enriching the people’s choice and diversity.
Mrs Wambura pointed out a digital migration road map, political will, consultation with stakeholders, a communication strategy , public private partnership (PPP) in the area of cost sharing and  consumer consideration in the purchase of affordable services and equipment contributed to the smooth analogue to digital migration in broadcasting ahead of ITU deadline of 17th June, 2015.
She said the achievement was contributed largely by the Public Private Partnership between Star  Communication Network Technology (Star Times ) from China which in May 2009 formed a joint venture company – Star Media (Tanzania)  Limited  with the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC), the Country’s public broadcaster.
However,  the Zimbabwe Minister for Media, Information and Broadcasting Mr. Christopher Chindoti Mushohwe said efforts that strengthen African Media to fight against negative  media coverage of African countries and China by Western countries should be applauded.
” The establishment of strong indigenous media in African countries will reduce dependence  of western global media which is negative to African countries and China. Zimbabwe is ready to cooperate with China in fighting western media negative coverage”, he said.

MKUSANYIKA WA HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

tff_LOGO1 
WAAMUZI WA MECHI SERENGETI BOYS, SHELISHELI
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba  ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Awali timu ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
Serengeti Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2
MWAMUZI WA ANGOLA KUWAAMUA YOUNG AFRICANS, TP MAZEMBE
Mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia
Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.
SUALA LA STAND UNITED YA SHINYANGA
Kutokana na mkanganyiko wa uendeshaji wa mchakato wa uchaguzi katika Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF), limeagiza michakato yote miwili inayoendeshwa sambamba ndani ya klabu ya Stand United, isimamishwe mara moja kisha kusubiri maelekezo mengine.

Tübingen International Africa Festival in Germany opens it doors from the 21 to 24 July 2016

MAKUN1 MAKUN2The International Afrika Festival Tübingen in Southern Germany The Republic of Burundi is country of honor 2016 From the 21 to 24 July 2016, Tübingen International Africa Festival in Germany opens it doors wide open to arts, culture, dialog tourism, media.. operators under the theme „ not black, not white but colored for a peaceful world“ Exhibitors, festival lovers and cultural tourist in search of plattforms for a short vacation are cordially invited to attend and enjoy.
Founded since 2007 by Sunjo & Susan TATAH; the International Africa Festival Tübingen in Germany, is a FOUR DAY annual festival with focused on showing casing Africa´s role and contribution to humanity and diversity as well as world peace and stability bringing people of African descent and others from all over the globe, irrespective of their countries of origin, religious background, gender and status together.
The Festival tells the story of people of Africa descent worldwide, thereby providing a platform to all African interested persons to share and be part of the heritage.As a young, dynamic rapidly growing forward thinking NGO, The International African Festival Tübingen is a platform for mobilization and presentation of cultural activist, Business and developmental activist, , individual donors and philantrophic activist in all sectors.
The festival is a compact format composed of a varierty of authentic projects- presenting Africa´s know-how – Huge market of Arts, Handworks, Authors, Producers, Designers, Film makers, culinary Arts… as well as full package entertainment such as talents shows with bands playing live music, traditional Ballets, dance performances, Forums, workshops and parties with top Djs / Mcs.
Each edition bringing together more than 100,000 fun and peace loving visitors. AfrikAktiv invites you to come and visit the International African festival in Germany powered by the African Diaspora and dedicated to the development of its continent and people. Come and have full service funtime. As a family oriented Festival, children and youths are the heartbeat for our festival, we cherish every one of them.
Our festival offers a special integrated children and youth mini format festival with activities for our young people – special artist with workshops –Acrobatics, clowning, graffitis, dance, creative handworks, special concert just for the young generation under the theme “Empowering the next generation with cultural diversity and humanity values“ For a more visibility on opportunities and potentials available on the African continent and its Diaspora, our festival offers a platform for partnership to all pan-african media and journalist.
Our festival reaches out to more than million people worldwide particularly on the African continent, here you meet your tailored made target groups. Join and follow us on social media – Facebook, Instagrams, Twitter, youtube..The International African Festival Tübingen, Germany offers opens you the door to enjoy Africa´s authentic Arts and listen to African tell their story the way it is.For more information: Web: www.afrikafestival.net

MV. MAGOGONI KUKAMILIKA AGOSTI MWAKA HUU

MAGO1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa ukarabati wa ujenzi wa vivuko vitatu jijini Dar es Salaam.
MAGO2 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Prof. Makame Mbarawa  (kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa ukarabati wa ujenzi wa vivuko vitatu  jijini Dar es Salaam.
MAGO3 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase akitoa maelezo ya moja ya kifaa kinachotumika kwenye kivuko cha MV Magogoni kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kulia Profesa Makame Mbarawa  wakati alipokagua mradi huo.
MAGO4Muonekano wa Kivuko cha MV. Magogoni kikiwa kwenye hatua za mwisho za matengezo yanayofanywa na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya Mwanza na TEMESA Jijini Dar es salaam.
MAGO5 
Mtaalam wa kampuni M/S Songoro Marine Transport Cortyard ya Mwanza (Wanne kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa alipokagua ukarabati na ujenzi wa Vivuko vya Old Magogoni, Pangani na New Magogoni.
MAGO6 
Mafundi wa M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya Mwanza na TEMESA wakiendelea na kazi ya ujenzi wa kivuko kipya  jijini Dar es salaam.

WABUNGE, WAANDISHI WA HABARI NA WASANII KUOSHA MAGARI KATIKA TAMASHA LA MEDIA CAR WASH MJINI DODOMA JUMAMOSI HII


DK. JIM JAMES YONAZI ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN)

YONAZJIM

ULEDI: MICHANGO YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII TUTAPELEKA KWA WAKATI

KATIB1 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21,2016).  Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
KATIB2 
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM  anayeshughulikia masuala ya Waziri   Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa  (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye  kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21, 2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
KATIB3 
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM anayeshughulikia masuala ya Waziri   Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa  alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21, 2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………….
KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Uledi Mussa amesema atahakikisha michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya watumishi wa Ofisi hiyo inafikishwa kwa wakati.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, 21 Juni, 2016)  wakati akijibu maswali ya watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma katika  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma inayoanzia Juni 16 hadi 23 ya kila mwaka.
Kila mwaka Tanzania imekuwa ikiungana na mataifa mengine ya Bara la Afrika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika  ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi:kuelekea katika Afrika tunayoitaka.
“Nitafuatilia michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha inafika kama inavyotakiwa na kwa wakati ili hata wanapomaliza muda wao wa utumishi wasihangaike,” amesema.
Katika hatua nyingine Uledi amewataka Wakuu wa Idara kuandaa  mpango wa mafunzo kwa watumishi na washirikishe kila mtu katika idara husika kabla ya kuuwasilisha kwake.
Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, ambapo Anjani Ngulukia (Msaidizi wa Ofisi) alitaka kupatiwa ufanunuzi kuhusu suala la michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imekuwa haipelekwi kwa wakati.
Pia mtumishi mwingine Ernest Msabalala ambaye ni Mtunza Kumbukumbu Mkuu aliomba ofisi iandae utaratibu wa kuwa na mafunzo kwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.

WIZARA YA HABARI YAKUTANA NA WADAU WA KUJADILI NA KUBORESHA SERA YA SANAA ZA MAONESHO

HAB1 
Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akizungumza na wadau wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho kuhusu mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo na kulia ni Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Richard Kundi.Na Anitha Jonas – WHUSM
HAB2 
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. William Chitanda akieleza changamoto za shirikisho kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam.  Katikati  ni Bw. Efraim Zakaria kutoka kikundi cha Watoto Arts Organization (WAAO).
HAB3 
Katibu wa Kikundi cha Binti Leo Bi. Agness Lukanga  (katikati) akieleza utendaji wa kikundi chao  kwa  watendaji wa masuala ya Sanaa na Utamaduni  wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga.
HAB4 
Mjumbe wa Kikundi cha Sherehe Arts Association (SAA) Bi. Columba Samjela  akiwaeleza watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  (hawapo pichani) mikakati waliyonayo ya kuimarisha Sanaa leo  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa (SAA) Bi. Grace Meena.
HAB5 
Mjumbe wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. Denis Mango  akifafanua shughuli za shirikisho katika kikao kilichofanyika Juni 21,2016 Jijini Dar es Salaam na Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Katikati ni Bw. Omari Kichapwi,  Mjumbe wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA).
HAB6 
Mjumbe wa Kikundi  cha Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) akieleza jambo kwa Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa Sanaa ya Mashairi. Kulia ni Mjumbe wa UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala.
HAB7 
Baadhi ya wadau wa Sanaa za Maonesho walioshiriki kikao na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Shani Kitogo (hayupo pichani) alipokuwa akifafanua jambo kuhusu fani ya ushariri leo jijini Dar es Salaam.
HAB8 
Mjumbe wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga akitoa maoni ya kuboresha  sekta ya Sanaa za Maonesho  kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani)  leo jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mjumbe wa UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala.

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

MHA1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo Bungeni leo kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali dhidi ya  waajiri wote wanaoshindwa kuwasilisha michango ya waajiriwa wao katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ambapo tayari Serikali iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kuunda kikosi kazi kitakachoshughulikia swala hilo.
MHA3
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. George Masaju leo Bungeni Mjini Dodoma.
MHA4 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrisom Mwakyembe akijibu moja ya hoja zilizotolewa Bungeni  leo na Mbunge wa Nchemba Mhe. Juma Nkamia aliyetaka kujua uhalali wa mtuhumiwa aliyetenda kosa la jinai la kumtukana Rais kuachiwa huru na kwenda kutafuta fedha za kulipa faini ilihali kosa alilotenda limemdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli.
MHA5
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira, Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde leo Bungeni Mjini Dodoma.
MHA6 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo iliyoombwa na wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma kabla ya Kuahirisha shughuli za  Bunge leo Mjini Dodoma.
MHA7 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisasa  ya mjini Dodoma wakiwa katika ukumbi wa Bunge kwa lengo la kujifunza majukumu ya Bunge leo Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
kol1 
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Susan Kolimba akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa ili kuimarisha Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwa ni moja ya hatua za kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali.
kol2 
Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu maswali yaliyoulizwa na Wabunge  leo Bungeni juu ya mikakati ya Serikali kuwawezesha wanawake kupitia Benki ya wanawake kwa kufungua madirisha maalum  Katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini yatakayosaidia kuwasogezea wanawake huduma za Benki hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
kol3 
Wanafunzi wa chuo Kikuu Dodoma  (UDOM) Wakiwasili katika ukumbi wa Msekwa Bungeni  Mjini Dodoma leo kwa lengo la kujifunza jinsi Bunge linavyotekeleza majukumu yake.

Muhimbili watoa ufafanuzi kuhusu wagonjwa wa Seli Mundu

MSERU1 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Profesa. Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa na Gazeti la Mwananchi kuhusu huduma hospitalini hapo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Bibi. Agness Mtawa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitalini hapo Aminiel Aligaesha.
Picha na: Frank Shija, MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………………
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru ametoa ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwanchi la tarehe 21 Juni 2016 zilizo kuwa zinasema kuwa wagonjwa wa Seli Mundu wanalipishwa ili kupata huduma ya matibabu yao tofauti ilivyokuwa awali.
Akitoa ufafanuzi huo Profesa Mseru amesema kuwa kwa habari hizo siyo za kweli kwani wagonjwa wa Seli Mundu wanatumia utaratibu wa kawaida ambapo mgonjwa utibiwa katika maeneo wanayotoka na anapaswa kuchangia gharama za matibabu isipokuwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Aliongeza kuwa hapo awali kulikuwa na mradi wa utafiti wa Seli Mundu ulioenda sambamba na utoaji wa matibabu kwa wagonjwa waliojumuishwa katika mradi huo uliodumu kwa muda wa miaka 10 hadi ulipofikia ukomo machi 30 mwaka huu.
Baada ya mradi huo kumalizika wagonjwa wote walirejea katika maeneo yao ambapo huko wanaendelea na matibabu kupitia utaratibu wa kawaida huduma za matibabu.

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI NA NAIBU WAKE WAKUTANA NA WANANCHI ANA KWA ANA NA KUTATUA KERO ZA ARDHI

KATI1 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila  Akiwakaribisha wananchi walio na kero za migogoro ya Ardhi ofisini kwake ili kuzitatua kero zao ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
KATI2 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka (katikati mwenye suti na tai) akipokea kero za wananchi zinazohusu migogoro ya Ardhi ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
……………………………………………………………………………………………………….
Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kupitia watendaji wake wakuu leo tarehe 21/06/2016 amefanya utaratibu maalumu wa kukutana na wananchi wenye kero na migogoro ya ardhi. Katika kutekeleza hilo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila  na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka wamekutana na wananchi ana kwa ana ili kuwasikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero na migogoro yao inayohusu ardhi na nyumba.
Hatua hii imefuatia baada ya hapo jana tarehe 20/06/2016 viongozi hao kukutana na watumishi wa Wizara hiyo na kutatua kero zao zinazohusu maslahi ya watumishi ambapo kwa mwaka huu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameamuliwa yafanyike kwa utaratibu huu.

DK. MWAKYEMBE AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI LEO MJINI DODOMA

KYE1 
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mjini Dodoma kuhusu maadili ya Vyombo vya Habari katika kuhabarisha Umma juu ya miradi ya maendeleo na jinsi vinavyoweza kuwasidia wananchi kuleta maendeleo na kuepuka kutoa taarifa za upotoshaji.
KYE2 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Vyombo vya Habari leo Mjini Dodoma.
(Picha Zote na Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma)

NCC yapanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi

index 
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) chini ya mkakati wa kukuza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi Tanzania (CoST -Tanzania) limepanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta hiyo ili kuondokana rushwa na kuhakikisha wananchi wanaelewa thamani halisi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya umma.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowashirikisha wadau wa ujenzi kutoka nchi mbalimbali Duniani kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Dkt. Leonard Chamuriho amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kuweka uwazi katika miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za wananchi ili kuondokana na rushwa zinazojitokeza katika kufanikisha miradi hiyo.
“Rushwa inazungumziwa sana katika suala  la ujenzi ila naomba tuzidishe uwazi katika sekta hii na kuwafanya wananchi waelewe kinachoendelea katika miradi yao hii itatutasaidia sana kupambana na rushwa, na taswira ya kuwa na rushwa katika miradi ya ujenzi haitakuwepo”,alisema Dkt. Chamuriho.
Dkt. Chamuriho ameongeza kuwa msimamo wa Serikali ni kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa katika miradi ya ujenzi na kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji Kutasaidia kuondokana kabisa na suala la rushwa.
Aidha, Dkt. Chamuriho amewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), Benki ya Dunia (WB) pamoja na Serikali ya Uholanzi wanaoendelea kusaidia miradi ya ujenzi iliyo chini ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) na kutoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kusaidia katika miradi mingine ya maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CoST -Tanzania, Kazungu Magili amesema kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo ni kuifanya CoST-Tanzania kujitegemea kwa kutosimamiwa na taasisi yoyote na kupitia mazungumzo yaliyofanywa kati ya CoST na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ana imani kuwa yataweza kufikia muafaka na kuifanya kuwa sekta inayojitegemea kabla ya mwezi Julai mwaka 2016.

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 MKOANI KILIMANJARO

SONY DSC 
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa umma wa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
ANG2 
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na Menejimenti ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 Mkoani Kilimanjaro. Mhe. Kairuki amesisitiza Maafisa Rasilimaliwatu wafanye kazi kwa weledi na watakaoshindwa hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
ANG3 
Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 Mkoani Kilimanjaro.

Vyombo vya Habari nchini Vimetakiwa kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yake

index 
Na: Frank Mvungi – MAELEZO- Dodoma
Vyombo vya Habari  nchini Vimetakiwa kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yake ili kusaidia Taifa kufikia maendelo ya kweli na endelevu.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Akifafanua Mhe.  Mwakyembe amesema ili Taifa liwe na Maendeleo ni lazima kuwa na Vyombo vya Habari vinavyozingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari pamoja na Sheria na Kanuni zinazosimamia tasnia hiyo.
“Navipongeza Vyombo vingi vya Habari hapa nchini ambavyo vinafanya kazi nzuri ya kuelemisha Umma na kuchochea maendeleo ya nchi yetu ila kuna wachache ambao kwa makusudi wameamua kupotosha Umma” alisisistiza Dkt. Mwakyembe
Hivi Karibuni gazeti moja lilitoa taarifa zinapotosha Umma kwa kumhusisha Waziri huyo na maswala ya Ufisadi ambapo alitumia fursa hiyo kuviasa vyombo vya habari kuepuka kuandika au kusambaza habari ambazo ni za upotoshaji na hazina maslahi kwa Taifa na hazijafanyiwa uchunguzi wa kina.
Akitolea mfano chombo hicho cha habari Mwakyembe amesema kuwa, kimekuwa kikiripoti taarifa zinazogusa masuaa ya Ulinzi na Usalama pasipo kuangalia maslahi ya Taifa kwanza hali inayoonyesha kukosekana kwa uzalendo.
Mwakyembe aliongeza kuwa tasnia ya habari imekuwa na ni vema sasa waandishi wote kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ili kuepuka kufikishwa katika vyombo vya sheria  kwa kukiuka sheria na kanuni za uandishi wa habari.
Tasnia ya Habari ni muhimili muhimu katika kuchochea Maendelo ya Taifa lolote lile kwa kuelimisha kuhamasisha na kuamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo.

Serikali kuendelea kutoa dawa bure kwa wagonjwa wa ukimwi na kifua kikuu

index 
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa sera yake ya kutoa dawa bure kwa wagonjwa wa kifua kikuu, ukimwi, mama wajawazito, wazee na watoto chini ya miaka mitano inaendelea.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma na waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akitolea ufafanuzi wa swali la Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani kikwete juu ya taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuwa utoaji wa dawa bure kwa makundi hayo ya watu umesitishwa na wanatakiwa kulipia.
“Hakuna mabadiliko yoyote katika sera ya kutoa dawa bure kwa wagonjwa wa ukimwi, kifua kikuu, mama wajawazito, wazee na watoto chini ya miaka mitano, aidha nitaitaka hospitali ya Taifa ya Muhimbili inipatie maelezo juu ya taarifa hizo,” alisisitiza, Mhe. Ummy.
Wakati huo huo, naibu waziri wa wizara hiyo, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa wizara hiyo kwa kushirikiana na wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji wanaandaa mkakati wa kuongeza uzalishaji wa dawa nchini ili angalau kukidhi asilimia 60 ya mahitaji katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aidha wizara hiyo pia iko katika mikakati ya kuunda chombo cha kusimamia gharama na bei zinazotozwa na vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa pamoja na bei za dawa na vifaa tiba ili kuthibiti uongezaji holela wa bei za dawa na vifaa tiba.

Huduma ya chakula kwa wagonjwa wanaolazwa Muhimbili kuanza mwezi Julai

mul3Mkurugenzzi wa Uuguzi Hospital ya Taifa Muhimbili Bibi. Agness Mtawa wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitenggo cha Mawasilinano Bw. Aminiel Aligaesha.
……………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, MAELEZO
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kuanzia tarehe 1 mwezi Julai 2016 ambapo mgonjwa atachangia gharama ya shilingi elfu hamsini.
Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
Aligaesha amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo ili kutoa fursa kwa Hospitali hiyo kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.
Aliongeza kuwa kutokana na kutolewa kwa huduma ya chakula hospitalini hapo kutasababisha mabadiliko ya  ratiba ya kuona wagonjwa kwa kuondoa muda wa saa 6 – 8 mchana ambao ulikuwa unatumiwa na ndugu kwa kuleta chakula kwa wagonjwa wao, badala yake muda wa kuona wagonjwa utabaki saa 12.00 -1.00 Asubuhi na saa 10.00 -12 jioni.
Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa anaweza kutumia kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri.
Kwa uande wake Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali hiyo Agness Mtawa amesema kuwa huduma hizo za chakula zitaondoa adha kwa ndugu wa wagonjwa kwa ambao walikuwa wanatumia muda huo kufika Hospitalini hapo.
Agness iliongeza katika huduma hiyo ya chakula wahudumu na wauguzi ndiyo wenye jukumu la kusaidia wagonjwa wenye mahitaji maalumu kama ktutoweza kujilisha wenyewe.
Huduma hiyo ya chakula itatolewa kupitia mzabuni aliyepatikana na kuongeza kuwa mgonjwa atachangia gharama ya shilingi 50,000 ambapo shilingi 10,000 itatumika kwa huduma ya Kitanda, huduma ya ushauri wa Daktari 10,000 na shilingi 30,000 kwa ajili ya chakula kwa siku muda wa siku tano.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA MAFUNZO YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiriamali  yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.(PICHA NA OMR)
 Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19.
 Sehemu ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
 Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za  ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline Maleko akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.

KIKUNDI CHA UPENDO WOMEN’S GROUP CHA UBELGIJI CHATOA SHUKRANI KWA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI

Baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe za umoja wa kikundi cha kina mama wenye makazi nchini Ubelgiji kijulikanacho kwa jina la Upendo Women’s Group.Kina mama wa Upendo wanatoa shukrani kwa kina mmoja aliyeshiriki katika hafla yao ya uchangishaji wa fedha za kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,sherehe hizi zilifanyika nchini Ubelgiji.
Dr.Pendo Maro ambaye ndiye alikuwa mshehereshaji wa hafla ya uchangishaji wa fedha kwa kikundi cha kina mama cha Upendo Women’s Group nchini Ublgiji akifungua uchangishaji wa sherehe hizo
Rais wa kikundi cha Upendo Women’s Group ambaye pia ndiye mwenyekiti cha kikundi hicho Mh:Theresia Greca,ametoa shukrani za dhati kabisa kwa Rais mstaafu wa Tanzania Mh: Benjamin William Mkapa kwa kuwachangia kikundi chao,Shukrani za pekee kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa mchango wao mkubwa wa kufanikisha zoezi zima la ufanikishaji wa fedha za kuisaidia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.{picha na maelezo toka Maganga One Blog}
Pichani wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria sherehe za uchangishaji wa fedha kwa ajili ya hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Shukrani zinatolewa na wana Upendo Women’s Group kwa ufanikishaji wa zoezi zima
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Upendo Women’s Group,kina mama wenye makazi yao nchini Ubegiji wametoa shukrani zao za dhati kabisaa kwa kila mmoja alishiriki vyema katika kufanikisha shughuli yao ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Wana Upendo wanapeleka shukrani zao kwa Rais Mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa kujitolea mchango wake,Bila kusahau shukrani zao kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima wa Tanzania nchini Ubelgiji.Wanatoa shukrani kwa vikundi mbalimbali vya maonyesho na kila mmoja aliyefanikisha zoezi zima.
{picha na maelezo toka Maganga One Blog}

Katika kuchangisha fedha ili kusaidia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania, Upendo Women’s Group waliaanda maonyesho mbalimbali ikiwemo na maonyesho ya mavazi.{picha zote na Maganga One Blog}
Afisa Ubalozi Mr.Shayo {kushoto} pia nae alishiriki katika sherehe hizi fupi za uchangishaji wa pesa wa kuisaidia hospital ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Wana Upendo Group wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki na mchango wao mkubwa waliojitolea wa maafisa ubalozi wa Tanzania katika kufanikisha zoezi zima.
Mmoja wa wageni ambaye siku hiyo alinunua bidhaa nyingi kutoka Tanzania ikiwa ni moja ya kuchangia wakina wa Upendo Women’s Group ambao walifanya sherehe ya mfuko wa uchangishiaji hospital ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,kina mama wa Upendo wanatoa shukrani zao za dhati kwa kila mmoja aliyewezesha ufanikishaji wa Harambee hiyo.
{picha na maelezo toka Maganga One Blog}

Mmoja wa wageni waalikwa ambaye alichangia Harambee siku hiyo kwa kununua Kahawa halisi kutoka Tanzania.Wana Upendo wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki wa wageni hao
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mrs Agnes Kayola akielezea ushiriki wa serikali katika kuisaidia jamii na wananchi wake katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya.Kaimu huyo alikisifia kikundi cha kinamama wa Upendo Women’s Group cha nchini Ubelgiji kwa jitihada wanazofanya kuisaidia hosptali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam. Wana Upendo Women’s Group wanatoa shukrani zao za dhati kwa msaada waliopata kutoka kwa kaimu Balozi Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa ushiriki wao,shukrani zingine kwa Rais mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa mchango wake wa kukisaidia kikundi.
{picha na maelezo toka Maganga One Blog}

TIGO PESA YATOA FURSA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Mkuu wa Huduma za Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Makumbusho Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Tigo Pesa kutoa fursa za biashara kwa wajasiriamali. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedum na kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
 ………………………………………………
Na Dotto Mwaibale 
 WAJASIRIAMALI wa kidijitali pamoja na wabunifu wa matumizi ya simu Tanzania hivi sasa wanaweza kuleta ufumbuzi zaidi kwa mteja katika soko na kuongeza  shughuli zao za kibiashara  kupitia  jukwaa  la huduma za kifedha kwa simu la Tigo Pesa.
 
Tigo Pesa ambayo inaongoza Tanzania kwa kutoa  huduma za kifedha kwa njia ya simu imefuatilia  uhusiano wake wa karibu na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuanzisha programu ambazo zinatoa mwongozo wa hatua kwa hatua  kwa wajasiliamali wa kijitali kwa kuiunganisha Tigo Pesa katika matumizi yao. Hatua hiyo inajionesha katika wavuti wa www.tigo.co.tz.
 
 Akizungumza katika mkutano na waandioshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za 
Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Tigo imewekeza  zaidi ya dola milioni 15 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita  katika kuboresha jukwaa la ngazi ya kimataifa  na huduma  ili kuendelea  kutoa  huduma sahihi za uhakika, zinazofikiwa na salama  kwa wateja.”
 
Swanepoel  alifafanua:“Jukwaa hilo la kuwanunganisha wateja wa Tigo Pesa na mitandao mingine  kwa kiwango kikubwa itapunguza  changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo  katika kuunganisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika kupokea malipo  kutoka kwa wateja wake katika hali isiyo na hitilafu na hivyo kuongeza  wigo jumuishi kifedha kote nchini.”
 
Swanepoel  aliongeza kwamba, “Tigo pesa imejikita kuangalia  hali na uwezo wa kuwezesha maendeleo ya  huduma za ubunifu na kujumuisha bila tatizo mitandao mingine  ili kuwapa wateja  faida zaidi za huduma ya fedha kwa njia ya simu.”
 
Itakumbukwa kwamba kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, Tigo Pesa  ilikamilisha  ushirikiano wake na  watoaji wengine wa huduma za fedha kwa njia ya simu  na benki nchini  kwa kuzifanya huduma hizo kupatikana kwa watu wengi zaidi.  Tigo Pesa pia ilizindua kifaa cha wateja kwa Android kwa watumiaji IOS, kwa kuwapatia njia rahisi watumiaji pindi wanapotumia  huduma zake.
 
Mfumo wa kuendesha na kutumia program hii ijulikanayo kama ‘Application Program Interface (API)  ni muundo wa maelekezo  na viwango vya kufikia mtandao  kwa kutumia zana  za kompyuta au zana za kimtandao. Ili kuzifikia programu za Tigo Pesa  inamaanisha wanafunzi wa vyuo, wajasiriamali wa biashara elektroniki , wabunifu wa vifaa  na wataalamu wengine wa teknolojia ya habari  wanaweza kuibuka na  vifaa  au kuwezesha  vifaa vilivyopo  kwa kuunganisha  ufumbuzi wao na Tigo Pesa.
 

Muhimbili yaboresha Huduma ya Chakula kwa Wagonjwa

mul1 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),  Bw. Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari LEO kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa (special diet) wanaolazwa MNH kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.
mul2 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo hicho LEO katika hospitali hiyo.
mul3Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akifafanua jambo LEO katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha akiwa kwenye mkutano huo.
mul4 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aligaesha akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari LEO jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………….
Yawaondolea usumbufu ndugu wa wagonjwa kupeleka  chakula mara tatu kwa siku
·         Ndugu watapata muda wa kuendelea na shughuli za uzalishaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa mara tatu kwa siku katika hospitali hiyo.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa.
 
Bw. Aligaesha amesema Hospitali inataka kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.
“Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri” amesema Bw. Aligaesha
                   
    Ameongeza kuwa adha ya pili wanayopata ndugu ni usumbufu ambapo inabidi kuacha shughuli nyingine za uzalishaji ili kuja kuleta chakula mara tatu kwa siku, hivyo kuingiliana na shughuli zao za kiuchumi na kimandeleo na kushindwa kuzalisha. Hivyo jukumu hili linachukuliwa na Hospitali kuwaondolea adha hii.
·                      
“Pia kuna baadhi ya ndugu wamekuwa wakishindwa kuwaletea chakula wagonjwa wao hivyo hospitali ililazimika kuwapatia chakula ambacho kilikuwa kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka mikoani wasio na ndugu hapa Dar Es Salaam” amesisitiza Bw. Aligaesha.
 
  Amesema kumekuwepo na ongezeko la msongamano wa watu ndani ya Hospitali toka asubuhi saa 12 mpaka saa 12 jioni, suala linaloingiliana na utoaji huduma hasa saa za mchana kwani muda wa saa 6.00 hadi saa 8.00 mchana ulikuwa unaingiliana na majukumu ya kiutendaji ambapo majopo mbalimbali ya watalaamu yamekuwa yakiendelea na raundi za wagonjwa waliolazwa. Hii wakati mwingine imesababisha mgonjwa kutokupata huduma stahiki kutokana na muingiliano huu.
·                      
“Vile vile msongamano huu ni changamoto kwa ajili ya masuala ya kiusalama ambapo kati ya watu wanaoingia Hospitali kwa kigezo cha kuja kuona wagonjwa kuna wanaoingia kwa lengo la kufanya uhalifu ikiwemo wizi wa mali za Hospitali, magari  pamoja na vifaa vya magari” alisisitiza.
 
Amesema kwa kufanya hivyo, Hospitali itapunguza baadhi ya gharama za uagizaji wa vyakula kwa wazabuni, kulinda upotevu na baadhi ya vyakula kuharibika wakati mwingine kwani utunzaji wa vyakula una mahitaji makubwa.
      Bw. Aligaesha amesema Hospitali inakusudia kutoa chakula chenye ubora na viwango vinavyotakiwa kwa wagonjwa ikiwemo kutoa chakula maalumu (special diet) kwa wagonjwa wenye uhitaji huo.
 Kuhusu utaratibu huo Bw. Aligaesha amesema Mzabuni ndiye atakayepika chakula kwa wagonjwa wote waliolazwa na atatayarisha, atakipeleka na kukikabidhi katika wodi husika ambapo jukumu la kumpa mgonjwa kifungua kinywa, chakula cha mchana na jioni linabaki wa Hospitali.
    Amesema wagonjwa watapatiwa milo mitatu kwa siku yaani asubuhi, mchana na jioni kazi itakayofanywa na muuguzi wa zamu ambaye atahakikisha wagonjwa wote wamepata chakula kufuatana na mahitaji (diet list) iliyowasilishwa jikoni kutokana na mahitaji yao ya kiafya. 
Kutokana na uamuzi huu, utaratibu wa ndugu kuleta chakula kwa wagonjwa waliolazwa wakati wa mchana umefutwa na hivyo mchana hatutakuwa na nafasi ya ndugu kuja kutembelea wagonjwa. Muda wa kutembelea wagonjwa utakuwa asubuhi saa 12 hadi saa moja kamili na saa 10:00 jioni hadi saa 12:00jioni ndipo ndugu wataruhusiwa kuingia ndani kuwaona ndugu zao waliolazwa. Katika muda huo ndugu ataruhusiwa kuja na chakula chochote anachofikiri atamuongezea mgonjwa wake kama matunda n.k
 
  Bw. Aligaesha amesema mgonjwa aliyelazwa atachangia kiasi cha shilingi 50,000 atakapolazwa ambapo kati ya hizo, shilingi elfu 10,000 itakuwa ni gharama ya kumuona daktari (Consultation), shilingi elfu 10,000 ikiwa ni gharama ya kulazwa na bei ya chakula itakuwa shilingi elfu 30,000 sawa na shilingi elfu 6,000 kwa siku. Wastani wa mgonjwa kukaa wodini ni siku tano. Gharama hizo zinahusika kwa muda wote atakaokuwa amelazwa.
 
Kwa sasa Hospitali inatoa chakula kwa wagonjwa 650 ambao wamepata rufaa kutoka hospitali za nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama wastani wa shilingi 1.8 bilioni kwa mwaka, sawa na shilingi 150 milioni kwa mwezi kwa vyakula pamoja na  gharama nyingine kama vile za nishati. Takribani wagonjwa kati ya 600 na 700 ambao rufaa zao ni kutoka Hospitali za Dar es Salaam walikuwa hawapati chakula kutoka Hospitalini, na ilibidi ndugu zao wawaletee chakula. Hata hivyo, Hospitali ilikuwa inawapatia chakula tu kama ndugu zao wakishindwa kufanya hivyo.
“Uongozi wa Hospitali unaamini kwamba mabadiliko haya hayatamuongezea mgonjwa gharama, bali yatampunguzia gharama pamoja na ile adha kama ilivyoainishwa hapo juu. Aidha, uongozi unaamini kwamba uamuzi huu unaendana na azma nzima ya kuboresha utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuboresha mazingira ya Hospitali. Tunaomba ushirikiano wenu katika kutekeleza jukumu hili ili kusudi wagonjwa waweze kuhudumiwa vizuri zaidi” amesisitiza Bw. Aligaesha.

No comments:

Post a Comment