Monday, June 20, 2016

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA MAKAMPUNI YA POLYTRA INTERNATIONAL NA IMPALA


index 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bw. Jaskaran Chugh  ambaye ni  Mwakilishi Mkazi wa Kampuni  ya Polytra International yenye Makao yake nchini Ubelgiji  (katikati) na  Bw. Mark Lemki  wa Kampuni ya Impala ya Switzerland, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

 

Milioni 200 kupanua mfumo wa maji safi Kasulu

index 
Na: Lilian Lundo – Maelezo – Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetenga jumla ya shilingi milioni 200 katika bajeti ya Mwaka 2016/2017 ili kupanua mfumo wa maji safi katika Mji wa Kasulu.
Hayo yamesemwa leo, Bungeni Mjini Dodoma na Naibu  Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kasulu Mhe. Daniel Nswanzugwako juu ya ukabarati wa vyanzo vya maji vilivyopo Mjini Kasulu ili maji yafike katika mitaa ya kata za Mrusi, Mwilavya na Kidyama.
“Serikali inatambua changamoto ya mtandao wa maji inayoukabili Mji wa Kasulu, katika mwaka wa fedha 2016/17 imetenga Milioni 200 kwa ajili ya kupanua mfumo wa maji safi katika mji huo,” alisema Mhe. Kamwelwe
Aidha, Mhe. Kamwelwe aliendelea kwa kusema kuwa, fedha hizo zitatumika katika kuboresha hali ya huduma ya maji ikiwemo kuongeza mtandao wa maji Mjini Kasulu ambapo pia kata za Mrusi, Mwilavya na Kidyama zitapata huduma ya maji safi na salama.
Pia Mhe. Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali imekamilisha usanifu na uandaaji wa makabrasha ya zaburi kwa ajili ya mradi wa majisafi wa kujenga chujio katika Mji wa Kasulu ili kuondokana na tatizo la maji kuwa machafu.
Wizara hiyo pia imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya upanuzi wa miundombinu ya usambazaji maji Masasi – Nachingwea kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi – Nachingwea.
Mradi huo unaohudumia wakazi wapatao 188,250 wa Miji ya Masasi na Nachingwea pamoja na baadhi ya Halmashauri za Wilaya ya Masasi, Nachingwea na Ruangwa. Aidha wizara hiyo itaendelea kutenga fedha zaidi katika bajeti zijazo ili kupanua huduma ya upatikanaji wa maji nchi nzima.

SERIKALI YAONYA MATUMIZI MABAYA YA VYANDARUA.

mpo1 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikata utepe kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.
mpo2 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.
mpo3 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akionyesha kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 kwa wadau  wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam.
mpo4 
Wadau mbalimbali wa takwimu wakifauatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati  wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam
……………………………………………………………………………………………………………………
Na Ally Daud-Maelezo
SERIKALI imetoa wito kwa wananchi kuacha matumizi mabaya ya vyandarua ili kusaidia jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyopewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi kama kuvulia samaki, kuwekea wigo mifugo na kuzungushia wigo bustani.
‘‘Watu wengi wamekuwa wakitumia vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi badala ya kujikinga na Mbu waenezao malaria. Hii ni kutokana na utafiti huu kuonyesha kuwa asilimia 14 ya watoto wa chini ya miaka 5 ambao walipimwa Malaria kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid Diagnostic Tests (RDT) walikuwa na Malaria,” amesema Dkt. Ulisubisya.
Aidha amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria bado ni kikubwa ikilinganishwa na kiwango kilichopatikana wakati wa Utafiti wa UKIMWI na Malaria wa Mwaka 2011-12 hivyo ni vyema jamii ikaendelea kupambana na ugonjwa huu kwani bado ni tishio kwa watoto na Wananchi kwa ujumla.
Dkt. Ulisubisya amesema kuzinduliwa kwa Matokeo haya kutasaidia Serikali kuboresha  huduma za afya kwa kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyopo katika utoaji wa huduma za malaria nchini.
Akizungmzia huduma za afya kwa akinamama wajawazito, Dkt. Ulisubisya amesema utafiti umeonyesha kuwa kiwango cha akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya, kutoka asilimia 51 mwaka 2010 kufikia asilimia 60 mwaka 2015 na kuongezeka kwa kiwango cha akina mama wanaosaidiwa na wataalam waliosomea wakati wa kujifungua kutoka asilimia 50 kufikia asilimia 60 mwaka 20015/16.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Kitakwimu, Mr. Irenius Ruyobya amesema kuwa utafiti huu ni wa muhimu sana katika kuboresha huduma za afya hasa katika kupambana na  Malaria.
Amesema ili Serikali iweze kuboresha huduma za afya na kupambana na Malaria, takwimu hizi ambazo zimezinduliwa leo zitasaidia Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya katika kupanga, kutekeleza na kupima utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya nchini.
Mr. Ruyobya amesema utafiti huu ni wa sita kufanyika nchini ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1991 na kufuatiwa na utafiti wa mwaka 1996, 1999, 2004/5 na 2010.   

Mangula azindua Kitabu cha “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es salaam

MANG1 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akizindua Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw.  Daniel Zenda. Kampeni hiyo inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
MANG2Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula  na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw.  Daniel Zenda.
MANG3 
Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi Yetu “Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu hiko kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (hayupo pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na  utambulisho wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
MANG4 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw.  Daniel Zenda. Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI LEO

bue1  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Bernadeta Mushashu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

bue2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano  na Mazingira   Luhaga  Jaelson  Mpina  kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 20, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

bue3 

bue4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, bungeni mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

ua1 
Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
ua2 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero.
ua3 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero  na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
……………………………………………………………………………………………………………
Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
“Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino,” alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
“Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino,” alisema Nyanduga..
Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

No comments :

Post a Comment