Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bw. Jaskaran Chugh ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Polytra International yenye Makao yake nchini Ubelgiji (katikati) na Bw. Mark Lemki wa Kampuni ya Impala ya Switzerland, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Milioni 200 kupanua mfumo wa maji safi Kasulu
Serikali kupitia Wizara ya Maji
na Umwagiliaji imetenga jumla ya shilingi milioni 200 katika bajeti ya
Mwaka 2016/2017 ili kupanua mfumo wa maji safi katika Mji wa Kasulu.
Hayo yamesemwa leo, Bungeni Mjini
Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe
alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kasulu Mhe. Daniel Nswanzugwako juu
ya ukabarati wa vyanzo vya maji vilivyopo Mjini Kasulu ili maji yafike
katika mitaa ya kata za Mrusi, Mwilavya na Kidyama.
“Serikali inatambua changamoto ya
mtandao wa maji inayoukabili Mji wa Kasulu, katika mwaka wa fedha
2016/17 imetenga Milioni 200 kwa ajili ya kupanua mfumo wa maji safi
katika mji huo,” alisema Mhe. Kamwelwe
Aidha, Mhe. Kamwelwe aliendelea
kwa kusema kuwa, fedha hizo zitatumika katika kuboresha hali ya huduma
ya maji ikiwemo kuongeza mtandao wa maji Mjini Kasulu ambapo pia kata za
Mrusi, Mwilavya na Kidyama zitapata huduma ya maji safi na salama.
Pia Mhe. Naibu Waziri huyo
amesema kuwa Serikali imekamilisha usanifu na uandaaji wa makabrasha ya
zaburi kwa ajili ya mradi wa majisafi wa kujenga chujio katika Mji wa
Kasulu ili kuondokana na tatizo la maji kuwa machafu.
Wizara hiyo pia imetenga kiasi
cha shilingi bilioni 1 katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya
kutekeleza miradi ya upanuzi wa miundombinu ya usambazaji maji Masasi –
Nachingwea kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi –
Nachingwea.
Mradi huo unaohudumia wakazi
wapatao 188,250 wa Miji ya Masasi na Nachingwea pamoja na baadhi ya
Halmashauri za Wilaya ya Masasi, Nachingwea na Ruangwa. Aidha wizara
hiyo itaendelea kutenga fedha zaidi katika bajeti zijazo ili kupanua
huduma ya upatikanaji wa maji nchi nzima.
SERIKALI YAONYA MATUMIZI MABAYA YA VYANDARUA.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikata utepe kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akionyesha kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 kwa wadau wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa takwimu wakifauatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam
……………………………………………………………………………………………………………………
Na Ally Daud-Maelezo
SERIKALI imetoa wito kwa wananchi
kuacha matumizi mabaya ya vyandarua ili kusaidia jitihada za Serikali
katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.
Akizungumza leo Jijini Dar es
salaam katika Uzinduzi wa Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto
na Malaria wa Mwaka 2015/16, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa
kumekuwepo na tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyopewa na
Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi kama kuvulia samaki, kuwekea wigo
mifugo na kuzungushia wigo bustani.
‘‘Watu wengi wamekuwa wakitumia
vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi badala ya
kujikinga na Mbu waenezao malaria. Hii ni kutokana na utafiti huu
kuonyesha kuwa asilimia 14 ya watoto wa chini ya miaka 5 ambao walipimwa
Malaria kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid
Diagnostic Tests (RDT) walikuwa na Malaria,” amesema Dkt. Ulisubisya.
Aidha amesema kuwa kiwango cha
maambukizi ya Malaria bado ni kikubwa ikilinganishwa na kiwango
kilichopatikana wakati wa Utafiti wa UKIMWI na Malaria wa Mwaka 2011-12
hivyo ni vyema jamii ikaendelea kupambana na ugonjwa huu kwani bado ni
tishio kwa watoto na Wananchi kwa ujumla.
Dkt. Ulisubisya amesema
kuzinduliwa kwa Matokeo haya kutasaidia Serikali kuboresha huduma za
afya kwa kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyopo katika utoaji wa
huduma za malaria nchini.
Akizungmzia huduma za afya kwa
akinamama wajawazito, Dkt. Ulisubisya amesema utafiti umeonyesha kuwa
kiwango cha akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma
ya afya, kutoka asilimia 51 mwaka 2010 kufikia asilimia 60 mwaka 2015 na
kuongezeka kwa kiwango cha akina mama wanaosaidiwa na wataalam
waliosomea wakati wa kujifungua kutoka asilimia 50 kufikia asilimia 60
mwaka 20015/16.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Shughuli za Kitakwimu, Mr. Irenius Ruyobya amesema kuwa utafiti huu
ni wa muhimu sana katika kuboresha huduma za afya hasa katika kupambana
na Malaria.
Amesema ili Serikali iweze
kuboresha huduma za afya na kupambana na Malaria, takwimu hizi ambazo
zimezinduliwa leo zitasaidia Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya
katika kupanga, kutekeleza na kupima utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya afya nchini.
Mr. Ruyobya amesema utafiti huu
ni wa sita kufanyika nchini ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka
1991 na kufuatiwa na utafiti wa mwaka 1996, 1999, 2004/5 na 2010.
Mangula azindua Kitabu cha “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es salaam
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akizindua Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi
wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini
Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula
na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini
(KVM) Bw. Daniel Zenda.
Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi Yetu “Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu hiko kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (hayupo pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na utambulisho wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO
WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI LEO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Bernadeta Mushashu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Luhaga Jaelson Mpina kwenye
viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 20, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa
Jumanne Maghembe, bungeni mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Mtaalam
Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero
akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni
Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez
akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto
ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa
Ero.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame
Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa
Ngozi, Ikponwosa Ero na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
……………………………………………………………………………………………………………
Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Pamoja na juhudi ambazo
serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino
wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya
hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango
kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu
ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa
Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa
ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi
ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
“Tangu nimeingia sijawahi
kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua
sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi
mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu
walio na uablino,” alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano
hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili
kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
“Tumejadili mambo mengi lakini
tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na
ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia
waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino,”
alisema Nyanduga..
Kwa upande wa Shirika la Umoja
wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez
alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha
kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.
No comments:
Post a Comment