Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bibi Sihaba Nkinga akihutubia wananachi wa mkoa wa Morogoro
waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
yaliyoandaliwa na Mkoa wa Morogoro katika shule ya Msingi Kigugu, wilaya
ya Mvomero
Kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bibi Sihaba Nkinga, katikati ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe.
Betty Mkwasa na kulia ni Bibi Magreth wakipokea maelezo ya mratibu wa
chanjo Mvomero kabla ya uzinduzi wa matone ya chanjo kwa watoto wa kata
ya Kigugu wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa Maadhimisho ya
Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika shule ya Msingi Kigugu Turiani
mkoani Morogoro tarehe 16.6.2016.
Wapili
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akikabidhi msaada wa vitabu
vilivyotolewa na asasi ya MVIWATA wakati wa kilele cha Maadhimisho ya
Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na mkoa wa Morogoro katika shule
ya Msingi Kigugu, wilayani Mvomero. Kushoto ni Mkuu wa wilya ya Mvomero
Mhe. Betty Mkwasa akifuatiwa na viongozi wa mradi wa MVIWATA na kijiji
cha Kigugu (16.6.2016).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bibi Sihaba, wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Betty
Mkwasa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Bibi Magareth Musai
(kulia), na kushoto ni mwenyekiti wa asasi ya MVIWATA Bw. Mgweno wakiwa
wamesimama mkabala na jiwe la msingi la maktaba ya Kata ya Kigugu
lililozinduliwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa
Afrika yaliyofanyika shule ya Msingi Kigugu Turiani, wilaya ya Mvomero,
mkoani Morogoro tarehe 16.6.2016.
Watoto
wa Shule ya Msingi Kigugu wilaya ya Movomero, mkoani Morogoro wakiingia
uwanjani kwa maandamano wakati wa kilelele cha Maadhimisho ya Siku ya
Mtoto wa Afrika yaliyohudhuriwa na wakazi wa mkoa wa Morogoro katika
kijiji cha Kigugu Turiani, mkoani Morogoro, siku ya Tarehe 16.6.2016.
Mwenyekiti
wa Baraza la Watoto mkoa wa Morogoro mtoto Aprinia M. Joseph,
mwanafunzi wa (kidato cha IV) Shule ya Sekondari Mgulasi, akisoma risala
ya watoto wa mkoa wa Morogoro kwa Mgeni rasmi Katibu Mkuu, wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Sihaba Kinga
(hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mkoani
Morogoro yaliyofanyika katika kijiji cha Kigugu,wilaya ya Mvomero,
tarehe Juni 16, 2016.
KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MAFUNZO JIJINI TANGA
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,
akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa wakati wa Mahafali ya
kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo
cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira(kushoto), akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu 156 wakati wa
Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili ,
yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni,
jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira(kushoto), akimvisha nyota mmoja wa wahitimu 156 wakati wa
Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili ,
yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni,
jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Gwaride
la heshima likipita mbele ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasiara, wakati wa
Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili ,
yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni,
jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,
akizungumza wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi
Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo,
Wilayani Handeni, jijini Tanga.Ambapo aliwaasa wahitimu kwenda
kulihudumia Taifa kwa uadilifu.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
TANZANIA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MAAFISA UGANI 6,266
Na Jonas Kamaleki -MAELEZO -Dodoma
Tanzania ina upungufu wa maafisa ugani 6,266 ambao serikali inahitaji kuajiri kadri ya upatikanaji wa fedha.
Kauli hiyo imetolewa leo
Bungeni Dodoma na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles
Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mkoa wa
Kagera lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa
wa Kagera, Mhe. Oliva Semuguruka aliyetaka kufahamu mpango wa serikali
katika kuwasaidia wakulima waweze kunufaika na kilimo cha Ndizi, Kahawa,
Mahindi na Maharage.
“Mathalani mwaka 2006 wizara
yangu ilibaini kuwa walikuwepo maafisa ugani 3,377, ukilinganishwa na
mahitaji ya maafisa hao 15,022″ alisema Dkt. Tizeba.
Aliongeza kuwa Serikali
inajitahidi kusomesha vijana wengi kwenye vyuo vya kilimo na kuajiri
maafisa ugani 5,377 na kufanya jumla ya wataalam kuwa 8,756 kwa sasa
ambao wanatoa elimu na kanuni bora za kilimo.
Tizeba alisema Serikali kwa
kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, inaendelea kueneza matumizi ya
vituo vya rasilimali za Kilimo vya Kata ambapo jumla ya vituo 322
vimejengwa katika Halmashauri 106 kwenye mikoa 20.
“Kati ya vituo hivyo vituo 224
vimekamilika na vinafanya ya kutoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji,
mashamba ya majaribio, kutoa huduma kwa wafugsjio na matumizi ya zana za
kilimo” alisema Dkt. Tizeba.
Aidha Waziri Tizeba aliongeza
kuwa Wizara yake inaandaa na kurusha vipindi vya redio kuhusu kanuni za
kilimo bora kupitia vituo mbalimbali vyas redio, ambapo kwa mwaka
2015/16 jumla ya vipindi 122 vilirushwa na vipindi 52 vilirushwa kupitia
TBC Taifa na vipindi 70 vilirushwa kupitia redio jamii.
Akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Viti MaaluM (CCM), Mhe. Oliver Semguruka aliyetaka kujua ni
lini bei ya kahawa itapanda ili wakulima wasiuze nje ya nchi, Dkt Tizeba
alisema bei ya kahawa itakuwa nzuri ikiondolewa kodi 26 zilizopo hivi
sasa.
Waziri Nape akutana na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akisalimiana
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati
akiwasili katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO ili kuzungumza na
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati)
akiongea na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani)
ambao aliwataka kutengeneza mikakati madhubuti itakayoimarisha
Mawasiliano ya Serikali kwa Umma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi
kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Jamal Zubeir.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika
picha ya pamoja na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika
picha ya pamoja na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo
Jijini Dar es Salaam.
Wakuu
wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wa kikao cha pamoja
ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa umma.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Bi. Prisca Ulomi akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kwa niaba na Maafisa
Mawasiliano wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO WA BUNGE LA BAJETI LEO TAREHE 17 JUNI, 2016 MJINI DODOMA
Mbunge
wa Nchemba (CCM), Mhe. Juma Nkamia akifurahia jambo na Mbunge wa Kaliua
(CUF), Mhe. Magnalena Sakaya wakati wakiingia katika viwanja vya Bunge
leo mjini Dodoma kuanza kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo.
Waziri
wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo
na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju ndani ya ukumbi wa
Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na
Ulemavu, Mhe. Antony Mavunde akijibu maswali ya Wabunge leo Bungeni
mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Mhe. Almas Maige akiuliza swali Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Wabunge
wa CCM Viti (Maalum) kutoka kushoto, Christine Ishengoma, Martha
Umbulla na Magreth Sitta wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge
wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo leo.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Halima Bulembo, akiuliza swali Bungeni leo
wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo. Kulia ni Mbunge
wa Busega, Mhe. Raphael Chegeni.
Naibu
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia Ackson akibadilishana mawazo na Wabunge
mara baada ya kuahirisha kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo mjini
Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge, Mhe.Dkt. Tulia Ackson akifurahia jambo na Mbunge wa
Kibiti, Mhe. Ally Ungando mara baada ya kuahirisha kipindi cha asubuhi
cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
Hospitali ya Amana yaboresha huduma zake
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Hospitali ya Rufaa ya Amana
Jijini Dar es Salaam imeboresha huduma za afya kwa kuweka mashine
maalumu ya kutibu meno ijulikanayo kama (Ceramic dental machine) lengo
ikiwa ni kuboresha huduma hizo katika hospitali za umma.
Akiongea katika mahojiano kwa
njia ya simu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bw.Meshack Shimwela ameeleza
kuwa kwa sasa wataweza pia kutoa huduma ya afya kwa viongozi wa serikali
pamoja na wabunge kupitia wodi maalum iliyotengwa kwa ajili yao ili
kupata huduma hiyo wanapokuwa jijini hapa.
“Tunaishukuru sana Serikali yetu
kwa kutuletea mashine hii maalumu kwa ajili ya magonjwa yote ya meno na
tunaishkuru pia kwa kutushauri kutenga wodi maalumu kwa ajili ya
kuwatibia viongozi mbalimbali wakati wakiwa hapa Dar es Salaam,ushauri
huo tumeupokea na tumeufanyia kazi”, alisema Simwela.
Aliongeza kuwa maboresho hayo
yatasaidia wananchi kupata huduma bora za afya na kupunguza gharama za
matibabu na kuondoa usumbufu wa kwenda kutafuta huduma hiyo katika
hospitali binafsi.
Bw. Shimwela anabainisha kuwa
mashine hiyo ilikuwa ikipatikana katika Hospitali chache za binafsi na
matibabu yake huchukua muda mwingi na gharama kubwa jambo ambalo
lilikuwa likiwaumiza wananchi wenye kipato cha chini, hivyo upatikanaji
wa huduma hiyo imekuwa msaada mkubwa sana.
Vilevile aliongeza kwa kutolea
ufafanuzi suala la huduma ya wodi maalumu itakayokuwa ikitoa huduma za
afya kwa viongozi na wabunge tayari imeshaanza kufanya kazi tangu mwezi
Machi mwaka huu ikiwa na vyumba viwili vya wagonjwa mahututi (ICU)
pamoja na vyumba 24 ambavyo vina sehemu ya kukaa, kulala pamoja na choo.
Aidha, amefafanua kuwa matibabu
katika wodi hiyo yanaweza kulipiwa kwa bima ya afya au kwa fedha taslimu
pia ameongeza kuwa wodi hizo hazijatengwa kwa ajili ya viongozi pekee
bali zinaweza kutumika pia kwa wananchi wa kawaida watakaoweza kulipia
gharama za matibabu zilizopangwa katika wodi hiyo.
Naye Afisa Habari wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala, David Langa amesema kuwa kufunguliwa kwa wodi hiyo
kumesaidia sana waganga kuwepo katika vituo vyao vya kazi muda wote
kwasababu huduma za afya kwenye wodi hiyo ni masaa 24 pia mganga
anapomtibu mgonjwa anapatiwa asilimia 30 ya gharama za matibabu yale
papo hapo,fedha hizo ni nje ya mshahara wa mwisho wa mwezi.
Ametoa rai kwa Serikali kuongeza
mashine hizo maalumu kwa ajili ya magonjwa ya meno na kuziweka katika
Hospitali mbalimbali ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa wengi katika
Hospitali moja.
MERCY KITOMARI, MJASIRIAMALI KIJANA ANAYETAKA KUMUONA ‘ROLE MODEL’ WAKE RAIS MAGUFULI
Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige (hayupo pichani).
MJASIRIAMALI kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao.
Amesema Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara , inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika magumu mbalimbali .
Alisema katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama ‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
“Nimekuwa nikikutana na wanawake wenzangu ambao wamekata tamaa na wamekuwa wakiniuliza ninawezaje kuendelea, nikawambia wasi-give up (wasikate tama) na kwamba serikali hii ni ya viwanda na kuchapa kazi “ alisema na kufafanua kwamba wanachohitaji wanawake hao ni mazingira mazuri ya kufanya ujasiriamali.
Mercy ambaye anatengeneza ‘ice cream’ zinazotumia matunda yote ya kitanzania kama vile fenesi, nanasi, bungo, ndizi, embe ana ndoto ya kumiliki kiwanda kikubwa kinachoweza kutengeneza na kufikisha ashkrimu kwa Tanzania na Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2020.
Akiwa ameanza kazi hiyo mwaka 2010 kutoka ‘jiko’ la nyumbani Mercy amefanikiwa kutambua wigo wake wa biashara ambayo amesema ina changamoto nyingi hasa mifumo ya vibali na ulipaji kodi na ushuru.
Muonekano wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.
Alisema uwapo wa kodi nyingi zenye viwango sawa kati ya anayeanza na aliyekuwepo; anayeingiza kidogo na kikubwa kunaleta athari kubwa kwa wajasiriamali wanaotaka kuchomoza.
“To be honest (nikiwa mkweli) zinavunja moyo… nyingi zinakwamisha kwani sisi waelewe tu kwamba tunatengeneza ajira na tunatengeneza soko kama mimi nanunua matunda natengeneza soko la mkulima.,.. natengeneza ashkrimu (Ice Cream) natengeneza ajira.. ipo haja ya kuangalia mambo mengi na hasa hili la kodi na ushuru” alisema.
Alisema ana mambo mengi ya kumwambia Rais Magufuli kama mjasiriamali mwanamke kijana.
“Atupe nafasi tukutane naye wanawake wajasiriamali vijana kisha tutamweleza mengi yakiwemo ya kodi na mifumo yake, mimi ningemweleza haja ya vyombo vyote vya huduma kutumia mtandao, kutoa huduma ,ningemweleza haja ya halmashauri na taasisi kutoa mafunzo mbalimbali ili kuinua wajasiriamali hawa na kuwasapoti si tu kuchukua kodi na ushuru” anasema Mercy.
Anasema wajasiriamali wengi wadogo hawaendelei kwa kukosa sapoti ya mafunzo na namna ya kufanya biashara zao zikue.
“Wasiwe wanachukua kodi na ushuru tu, halmashauri hizi lazima zianze kufikiria kukuza wajasiriamali kwa kuwapa elimu inayostahili katika biashara zao” anasisisitiza Mercy ambaye amesema angelipenda kumuona Role Model wake (Rais Magufuli) kumweleza mengi yanayohusu wanawake vijana na viwanda vidogo kuelekea viwanda vikubwa na hamu ya wajasiriamali wanawake vijana kuchangia pato la taifa na kulipa heshima.
Anasema anapokutana na wajasiriamali wa Uganda, Rwanda anaona jinsi serikali zao zinavyowasaidia kunyanyuka na anaona serikali ya awamu ya tano inaweza kuwasikia na wao wakanyanyuka.
UVCCM MKOA WA ARUSHA WALAANI VIKALI SHUTUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA
Na Mahmoud Ahmad Arusha
UMOJA wa vijana mkoa wa Arusha umelaani vikali kitendo cha
jenerali Twaha ulimwengu kumkashifu Rais Mstaafu na mwenyekiti wa CCM
taifa, Dkt Jakaya Kikwete kwa madai kuwa ashitakiwe mahakamani kwa
kutumia fedha za umma vibaya kwa kuanzisha mchakato wa katiba ambao
ulikwama kufikia tamati yake
Akitoa tamko hilio mbele ya wana habari mkoa wa Arusha
mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha Lengai Ole sabaya alisema
kuwa matamshi ya upotosha ji yaliyotolewa na jenerali twaha ulimwengu
ni ya kupotosha umma
Aliongeza kuwa kutokana na matamshi hayo UVCCM wanamtaka
jenerali aache kupotosha ukweli kama ulivyo kwani mchakato bado
haujakwama ila umezingwa na miingiliano ya vipindi vya uitishaji wa kura
ya maoni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Aidha idhini ya matumizi ya fedha za mchakato wa Katiba
ziliweza kuiidhinishwa na bunge kwa nia ya dhamira njema ya taifa ya
kuandika katika yake mpya na wala sio ubadilifu au matumizi mabaya kama
anavyotaka jenerali huyo.
Sabaya alisema kuwa alichokionesha jenerali mbele ya
kadamnasi na vyombo vya habari ni kejeli pamoja na dharau isiyo staili
kwani alionekana kujawa na nyongo kutokana na kumbukumbu zile za kuwekwa
kando na utawala wa mkapa kasha kuzikwa kwenye kaburi la sahau utawala
wa kikwete.
Aidha kutokana na matasmhi hayo umoja huo umewaomba na
kuwasihi watanzania kuwa makini na kutuipilia mbali sanjari na kuweka
tahadhari kwa watu wenye matamshi ya hamaki pamoja na hasira ambao wana
nia mbaya ya kubomoa taifa.
Kutokana na hilo pia umoja huo umesema kuwa
endapo kama ataendelea basi wao hawataweza kumtambua tena kama
mwanachama mwenzao na pia watashinikiza hata uanachama wake utiliwe
shaka kabisa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA
TAREHE
16.06.2016 MAJIRA YA SAA MAJIRA YA SAA 14:00HRS KATIKA ENEO LA
LUCHELELE WILAYA YA NYAMAGANA MKOA WA MWANZA, ASKARI POLISI WALIFIKA
KATIKA ENEO HILO TAJWA NA KUFANYA MISAKO PAMOJA DORIA NAKUWEZA
KUFANIKIWA KUKAMATA WATU NANE WAKIWA NA POMBE AINA YA GONGO PAMOJA
NAMITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA
SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA, 1. JESCA
SIMONI MIAKA [14], MWANAFUNZI, AMBAYE ALIKAMATWA AKIWA NA LITA 42 ZA
POMBE AINA YA GONGO, 2.NYANGE BIHEMO MIAKA [46] ALIYEKAMATWA AKIWA NA
MITAMBO MIWILI YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, 3. MARIAM OMARY MIAKA
[28] ALIYEKAMATWA NA POMBE YA GONGO LITA 3, 4. MAOLA LUCHUPA MIAKA 32
ALIYEKAMATWA AKIWA NA LITA 20 ZA POMBE AINA YA GONGO. WENGINE NI, 5.
ELIZABETH JOHN MIAKA 35 ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MITATU YA KUTENGENEZEA
POMBE YA GONGO, 6. ANASTAZIA ALOYCE MIAKA 25 ALIYEKAMATWA NA POMBE YA
GONGO LITA 2, 7. TEDY PIUS MIAKA 40 ALIYEKAMATWA NA LITA 30 ZA POMBE YA
GONGO NA, 8. PASKAZIA THOMAS ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MIWILI YA
KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, WATUHUMIWA WOTE NI WAKAZI WA LUCHELELE.
AIDHA INADAIWA KUWA WATUHUMIWA
HUFANYA BIASHARA HARAMU YA POMBE YA GONGO NA WAKAZI WA MAENEO HAYO,
HUKU WAKIIHALALISHA BIASHARA HIYO KUWA KAMA CHANZO CHAO KIKUU CHA KIPATO
CHA KILA SIKU KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA
NCHI. NDIPO JESHI LA POLISI LILIPOKEA TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA
KUHUSIANA NA UHALIFU HUO UNATENDWA NA BAADHI YA WAKAZI WA LUCHELELE NA
KUFANIKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU.
WATUHUMIWA WOTE WAPO CHINI YA
ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUFANYA WA
KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA POMBE AINA YA GONGO UKIENDELEA, PINDI
UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYO
WAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA WAFANYE KAZI NYINGINE
HALALI AMBAZO ZITAWAINGIZIA KIPATO, LAKINI BIASHARA HARAMU ZA POMBE YA
GONGO NA MADAWA YA KULEVYA NAWAOMBA MUACHE KUJIHUSISHA NAZO KABISA,
KWANI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEJIPANGA VIZURI KUKABILIANA NA
WAHALIFU WA AINA KAMA HIYO NA KUHAKIKISHA WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA
KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
PEMBA WAMUOMBA KAMISHNA WA POLISI KIKOSIKAZI KWA AJILI YA UPELELEZI NA UKAMATAJI WA WANAOFANYA HUJUMA KWENYE MAZAO
Na Masanja Mabula –Pemba
SERIKALI katika Wilaya ya
Wete , imemuomba Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar kuleta kikosi kazi
cha Polisi Kisiwani Pemba kwa ajili ya kusaidia upelelezi na
ukamatwaji wa watu wanaofanya hujuma za kuharibu vipando na mali za
wananchi .
Mkuu wa Wilaya ya Wete ,
Rashid Hadid Rashid aliyasema hayo baada kutembelea shamba la aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi lililoko Finya Mianzini ,
kukatwa minazi 46 , mikarafuu 5 na mashina ya mihogo 51.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa ombi
hilo kufuatia vitendo hivyo kuongezeka kila uchao na kusababisha
hasara kwa wenye mali na Taifa kwa ujumla, jambo ambalo linaweza
kudhoofisha uchumi wa nchi na wananchi wake .
“Kutokana na kuongezeka kwa
matukio ya hujuma , iko haja kwa Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar
kuleta kikosi kazi kwa ajili ya kufanya upelelezi ili wahusika waweze
kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ”alisema Mkuu wa Wilaya
.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati na ulinzi na usalama amelaani vikali
vitendo hivyo vya hujuma vinavyofanywa na watu wasiojulikana na
kuvitaja kwamba ni njama za makusudi zinazofanywa na baadhi ya watu kwa
misingi ya itikadi za kisiasa .
Akitoa taarifa kwa kamati ya
Ulinzi ya Ulinzi na Usalama , Mlinzi wa Shamba hilo Ali Naulima Ulamu
alisema , hujuma hizo alizibaini baada ya kufika katika eneo hilo kwa
ajili ya shughuli za kilimo majira ya saa kumi na mbili (12) asubuhi .
Ulima alifahamisha kwamba bado
hajawabaini watu waliohusika na kitendo hicho ambapo , alichukua hatua
ya kumupa taarifa Sheha pamoja na mmiliki wa Shamba kuhusiana na hujuma
hizo .
“Nilibaini kuwepo na uharibifu
huu majira ya saa 12 asubuhi baada ya kufika kwa ajili ya shughuli za
kilimo , lakini nilichokifanya ni kutoa taarifa Serikalini pamoja na
kumpa taarifa mmiliki wa shamba ”alieleza.
Kwa upande wake mmiliki wa
shamba hilo Dadi Faki Dadi aliwataka wananchi kuwa na hofu ya Mungu kwa
kuhakikisha wanajiepusha matendo ambayo yanakinzana na Haki na Binadamu
na utawala wa misingi ya Sheria .
Alieleza kwamba ni jambo la
kushangaza kwa muumini wa dini kutekeleza vitendo vya kuhujumu mali za
mwenzake hasa katika kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhan .
Aidha amewashauri viongozi wa
dini kutumia fursa waliyonayo kwa kutenga muda wa kuyaungumzia matendo
hayo wakiwa katika sehemu zao Ibada , ili waumini waweze kutambua athari
zake .
Hili ni tukio la nane kutokea
katika Wilaya ya Wete la kuhujumiwa kwa mali , mazao na vipando vya
wananchi ikiwemo uchomaji moto nyumba , mashamba ya mikarafuu , majengo
ya Serikali , kufyekwa kwa mashamba ya mipunga na kung’olewa kwa vipando
baada ya kumalizika uchaguzi Mkuu wa marejeo uliofanyika machi 20
mwaka huu .
Tangu kuanza kutokea kwa
matukio hayo katika Wilaya hiyo , hakuna mtu au kikundi cha watu
waliokamatwa wakihusishwa na hujuma hizo .
DKT SHEIN AKUTANA NA WAZIRI AUGUSTINO MAHIGA
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
(kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa
mazungumzo,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akifuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki Mhe,Augustino Mahiga baada ya mazungumzo yao leo alipofika
Ikulu Mjini,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki
Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya
mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.
MTANZANIA BW. MAKALA JASPER ATUNIKIWA TUZO NA NATIONAL GEOGRAPHIC SOCIETY
Bw.
Makala Jasper, Mkurugenzi Mwandamizi wa NGO ya Mpingo Conservation
& Development Initiative (MCDI) ametunukiwa tuzo ya National
Geographic Society/Buffett Award forLeadership in African Conservation.
Tuzo
Mhe.
Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marekani
akiwa na Bw. Makala Jasper alipotembelea ofisi za Ubalozi
Pichani:
Rais wa National Geographic Society Bw. Gary E. Knell mara baada ya
kumkabidhi Bw. Makala Jasper tuzo. Kulia ni Mhe. Balozi Wilson M.
Masilingi na Bi.
Bw. Makala Jasper akitoa shukurani kwa kupewa tuzo
National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation
Bw.
Gary Knell akiwa na Bi. Mounia Mechbal, Mwakilishi wa Rolex, Bw. Lee
Berger mshindi wa tuzo ya Explorer of the Year, na Terry Garcia, Mkuu wa
Masuala ya Sayansi na Utafutaji, National Geographic
Bi. Pasang Akita akipokea tuzo ya Adventurer of the Year
Pichani katikati: Washindi wa Tuzo ya Hubbard Medal Bw. Nainoa Thompson na Bi. Meave Leakey
Miss Universe Tanzania 2015 afuturu na watoto, Makonda atoa neno
Katika kusherekea siku maalum
ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni, 16 ya kila mwaka, Kamati ya
Miss Universe Tanzania kupitia mpango wake mpya uitwao Binti Jasiri
ilikutanisha kwa pamoja watoto 90 kutoka vituo mbalimbali vya mkoa wa
Dar es Salaam ambapo halfa hiyo ilihudhuliwa na Miss Universe Tanzania
2015, Lorraine Marriot na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza na watoto hao,
Makonda aliwambia kuwa serikali ya awamu ya tano inawathamini watoto na
hata kuwawekea elimu bure hivyo waongeze juhudi katika masomo yao ili
nao waweze kuja kuwa na maisha mazuri na hata kuwasaidia wengine kama
jinsi wao wanavyosaidiwa na watu wengine ambao wamefanikiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda akizungumza na watoto kutoka vituo mbalimbali vya kulea
watoto kutoka mkoa wa Dar es Salaam katika halfa maalum ya kusherekea
siku ya mtoto wa Afrika, Kushoto ni Miss Universe Tanzania 2015,
Lorraine Marriot. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)
“Watu wenye maisha mazuri
wasiwachanganye hata nyie mnaweza kuwa na maisha mazuri hata zaidi yao,
mnatakiwa muongeze bidii katika masomo yenu ili na nyie mfanikiwe na
kuwasaidia wenzenu kama jinsi mnavyosaidiwa na wengine kwa sasa,”
alisema Makonda.
Nae Miss Universe Tanzania
2015, Lorraine Marriot ambaye pamoja na kupata chakula cha pamoja na
watoto hao pia alipata nafasi ya kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu
maisha, kuwashauri na kuwatia moyo ili waongeze bidii katika masomo yao
na hata baadae waweze kufanikiwa kimaisha.
Halfa hiyo ilisimamiwa na
Magdalena Gisse na kuhudhuliwa na watoto kutoka Kituo cha Malaika Kids
Orphanage, Kurasini Orphanage, Sarafina Orphanage na Makini Orphanage
vyote kutoka mkoa wa Dar es Salaam
Na Rabi Hume, MO Blog.
Watoto wakimpigia makofi Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza nao
katika halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika
Hoteli ya Golden Tulip.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda akimsalimu mmoja wa watoto waliohudhulia halfa maamul ya
kumkumbuka mtoto wa Afrika, Aliyembeba mtoto huyo ni Miss Universe
Tanzania 2015, Lorraine Marriot na katikati ni Mkurugenzi Kitaifa wa
Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai.
Watoto mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo wakifurahi kwa pamoja.
Baadhi ya watoto waliohudhuria halfa hiyo walio na imani ya Kiislamu wakisali.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji,
Barbara Gonzalez akifuturu kwa pamoja na watoto kutoka vituo mbalimbali
waliohudhuria halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika.
Miss Universe Tanzania 2015,
Lorraine Marriot akifuturu kwa pamoja na watoto waliohudhuria katika
siku maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli
ya Golden Tulip.
Miss Universe Tanzania 2015,
Lorraine Marriot akimlisha mmoja wa watoto waliohudhuria halfa maalum ya
kumkumbuka mtoto wa Afrika.
Watoto mbalimbali waliohudhuria
halfa hiyo wakifuturu na kujiburudisha na vinywaji kutoka Kampuni ya
Mohammed Enterprises ambayo ilijitolea vinywaji katika halfa maalum ya
kumkumbuka mtoto wa Afrika.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji,
Barbara Gonzalez akifurahi na watoto waliohudhuria halfa hiyo kwa
kuwaonyesha jinsi mtandao wa kijamii wa Snapchat jinsi unavyotumika.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akizungumza na watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Mmoja wa watu waliokulia katika
kituo cha kulelea watoto cha DogoDogo, Dk. Yusuph akiwatia moyo watoto
hao na jinsi ambavyo wanaweza kufanya ili na wao waweze kufanikiwa kama
ilivyo kwake.
Msimamizi wa halfa hiyo, Magdalena Gisse akiwashukuru watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwasaidia watoto kufungua maputo baada ya halfa hiyo kumalizika.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji,
Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto
waliohudhuria halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika iliyofanyika
katika Hoteli ya Golden Tulip.
Washiriki wa halfa maalum ya mtoto wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja.
KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
KITUO
cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for
Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya
(EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais
Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador)
wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pacific.
Katika barua iliyokabidhiwa na
mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk.
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameteuliwa kwa kutambua
mchango na juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na
barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA
imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya
kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili
ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na uhakika kwa vijana na wanawake
katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA
katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika
nchi mbalimbali.
Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo
na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa
kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya
na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu
mjini Brussels, Ubelgiji.
Prof. Kamuzora ambaye pia ni
Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za
ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018
WAZIRI KAIRUKI AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA VIKAO KAZI NA WATUMISHI WA MKOA WA SINGIDA
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, MenejimentiyaUtumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Angellah Kairuki akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Mkoa wa Singida
wakati wa kikao kazi na watendaji hao kilichofanyika jana Ofisini kwa
Mkuu wa Mkoa wa Singida ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa
Umma kwa mwaka 2016.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Watumishi mbalimbali wa Mkoa
wa Singida (hawapo pichani) alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki
yaUtumishi wa Umma kwa mwaka 2016, mkoani Singida jana, wanaofuata kulia
kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Mathew Mtigumwe, Katibu Tawala
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Singida,
Mhe. Saidi Amanzi.
Baadhi ya Watumishi wa umma
mkoani Singida wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (hayupo
pichani) alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa
mwaka 2016, mkoani Singida jana.
Mkurugenzi
wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji akifafanua jambo
wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na Watumishi wa
Mkoa wa Singida kilichofanyika jana ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya
Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni kila mwaka.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dkt. John Mwombeki
akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Waziri waNchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki
na Watumishi wa Mkoa wa Singida kilichofanyika jana ikiwa ni katika
kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni
kila mwaka,
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah Kairuki akipokea Ripoti ya Utendaji wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tawi la Singida kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha
Utumishiwa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo jana, wanaoshuhudia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala wa Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania, Bw. Rajabu Mirambo na Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma
Tawi la Singida, Bw. Ramadhani Marijani
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na tawala Bora,
Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya
pamoja na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida mara
baada ya kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika jana ikiwa ni katika
kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni
kila mwaka, kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha Utumishi wa
Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo na kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa
Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
…………………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Umma nchini waliopewa dhamana
serikalini kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuepuka
malalamiko yasiyo ya lazima kwa wanaowahudumia.
Waziri Kairuki aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016 mkoani Singida.
“Najua miongoni mwa watumishi wa
umma wapo watumishi waliopewa dhamana lakini utoaji wao wahuduma
unatiliwa shaka. Hawapendi kusikiliza matatizo ya wateja wa ndani yaani
watumishi wenzao,” Mhe. Kairuki alisema.
Amewataka watumishi wenye tabia
hizo kuacha mara moja na kuishi maisha ya kazi kama Mkataba wa Huduma
kwa Mteja unavyowaongoza katika kutoa huduma kwa kiwango kwa wateja wote
wa ndani na nje ya taasisi.
Aidha, Mhe. Kairuki amewataka
Watendaji kutenga muda wa kukaa na watumishi wao ili kusikiliza kero na
changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
“Uzoefu unaonyesha kuwa watumishi
wanaposhirikishwa katika masuala yanayowagusa kama tulivyo hapa basi
huduma kwa wananchi na wadau wengine zitaboreka na kazi kufanyika kwa
ari na hivyo kuongeza tija na ufanisi kazini,” Waziri Kairuki aliongeza.
Katika hatua nyingine, Mhe.
Kairuki alifanya ziara katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida
na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho ambapo aliwataka watumishi hao
kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika ili kuleta
matokeo bora kwa taifa.
“Tuwewabunifu,
tuangalievipaumbele, tufundishe kozi ambazo hazifundishwi sehemu
nyingine ili kuweza kupata soko zuri zaidi,” Waziri Kairuki alisisitiza.
Aliwasisitiza watumishi hao kuwa
na ushirikiano na vyuo mbalimbali hasa katika nyanja za utafiti, mafunzo
na masuala mengine ya maendeleo ili kuboresha chuo hicho.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16-23 Juni, kila mwaka, kwa
mwaka 2016 yanafanyika kwa namna tofautia mbapo Viongozi na Watendaji
wanakutana na wateja wao wa ndani na nje ya taasisi zao kwa lengo na
kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika kutekeleza hilo, Mhe.
Kairuki amezindua maadhimisho hayo kwakufanya vikao kazi na watumishi wa
mkoa wa Singida kutoka katika kada mbalimbali za utumishi wa umma.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika kwa mwaka 2016 ni “Uongozi wa Umma kwa ukuajiJumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka.”
Kaulimbiu hiyo inaambatana na kaulimbiu ndogo ambazo ni: Mchango wa Utumishi wa Umma katika Ukuaji wa Uchumi Barani Afrika na Mchango
wa Utumishi wa Umma katika Kuiwezesha Ajenda ya Afrika ya 2063 ambayo
inaweka mkazo katika Maendeleo ya Afrika na Haki za Wanawake.
No comments :
Post a Comment