Pages

Friday, June 17, 2016

Kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika chafanyika Mvomero Mkoani Morogoro

New Picture (11) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akihutubia wananachi wa mkoa wa Morogoro  waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Mkoa wa Morogoro katika shule ya Msingi Kigugu, wilaya ya Mvomero
New Picture (12) 
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga, katikati ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa na kulia ni Bibi Magreth wakipokea maelezo ya mratibu wa chanjo Mvomero kabla ya uzinduzi wa matone ya chanjo kwa watoto wa kata ya Kigugu wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika shule ya Msingi Kigugu Turiani mkoani Morogoro tarehe 16.6.2016.
New Picture (13) 
Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akikabidhi msaada wa vitabu vilivyotolewa na asasi ya MVIWATA wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na mkoa wa Morogoro katika shule ya Msingi Kigugu, wilayani Mvomero. Kushoto ni Mkuu wa wilya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa akifuatiwa na viongozi wa mradi wa MVIWATA na kijiji cha Kigugu (16.6.2016).
New Picture (14) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba, wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Bibi Magareth Musai (kulia), na kushoto ni mwenyekiti wa asasi ya MVIWATA Bw. Mgweno wakiwa wamesimama mkabala na jiwe la msingi la maktaba ya Kata ya Kigugu lililozinduliwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika shule ya Msingi Kigugu Turiani, wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro tarehe 16.6.2016.
Watoto wa Shule ya Msingi Kigugu wilaya ya Movomero, mkoani Morogoro wakiingia uwanjani kwa maandamano wakati wa kilelele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyohudhuriwa na wakazi wa mkoa wa Morogoro katika kijiji cha Kigugu Turiani, mkoani Morogoro, siku ya Tarehe 16.6.2016.
New Picture (16)Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Morogoro mtoto Aprinia M. Joseph, mwanafunzi wa (kidato cha IV) Shule ya Sekondari Mgulasi, akisoma risala ya watoto wa mkoa wa Morogoro kwa Mgeni rasmi Katibu Mkuu, wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Sihaba Kinga (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mkoani Morogoro yaliyofanyika katika kijiji cha Kigugu,wilaya ya  Mvomero, tarehe Juni 16, 2016.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MAFUNZO JIJINI TANGA

BG1 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.
BG2 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu 156 wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
BG3 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akimvisha nyota mmoja wa wahitimu 156 wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
BG4 
Gwaride la heshima likipita mbele ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasiara,  wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
BG5 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa Mahafali ya kufunga  Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.Ambapo aliwaasa wahitimu kwenda kulihudumia Taifa kwa uadilifu.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

TANZANIA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MAAFISA UGANI 6,266

BUSHOSA 
Na Jonas Kamaleki -MAELEZO -Dodoma
Tanzania ina upungufu wa maafisa ugani 6,266 ambao serikali inahitaji kuajiri kadri ya upatikanaji wa fedha.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mkoa wa Kagera lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliva Semuguruka aliyetaka kufahamu mpango wa serikali katika kuwasaidia wakulima waweze kunufaika na kilimo cha Ndizi, Kahawa, Mahindi na Maharage.
“Mathalani mwaka 2006 wizara yangu ilibaini kuwa walikuwepo maafisa ugani 3,377, ukilinganishwa na mahitaji ya maafisa hao 15,022″ alisema Dkt. Tizeba.
Aliongeza kuwa Serikali inajitahidi kusomesha vijana wengi kwenye vyuo vya kilimo na kuajiri maafisa ugani 5,377 na kufanya jumla ya wataalam kuwa 8,756 kwa sasa ambao wanatoa elimu na kanuni bora za kilimo.
Tizeba alisema Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, inaendelea kueneza matumizi ya vituo vya rasilimali za Kilimo vya Kata ambapo jumla ya vituo 322 vimejengwa katika Halmashauri 106 kwenye mikoa 20.
“Kati ya vituo hivyo vituo 224 vimekamilika na vinafanya ya kutoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji, mashamba ya majaribio, kutoa huduma kwa wafugsjio na matumizi ya zana za kilimo” alisema Dkt. Tizeba.
Aidha Waziri Tizeba aliongeza kuwa Wizara yake inaandaa na kurusha vipindi vya redio kuhusu kanuni za kilimo bora kupitia vituo mbalimbali vyas redio, ambapo kwa mwaka 2015/16 jumla ya vipindi 122 vilirushwa na vipindi 52 vilirushwa kupitia TBC Taifa na vipindi 70 vilirushwa kupitia redio jamii.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti MaaluM (CCM), Mhe. Oliver Semguruka aliyetaka kujua ni lini bei ya kahawa itapanda ili wakulima wasiuze nje ya nchi, Dkt Tizeba alisema bei ya kahawa itakuwa nzuri ikiondolewa kodi 26 zilizopo hivi sasa.

Waziri Nape akutana na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma

nap1 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati akiwasili katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO ili kuzungumza na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo Jijini Dar es Salaam.
nap2 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati) akiongea na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani) ambao aliwataka kutengeneza mikakati madhubuti itakayoimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Jamal Zubeir.
nap3 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo Jijini Dar es Salaam.
nap5 
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wa kikao cha pamoja ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa umma.
nap6 nap7 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bi. Prisca Ulomi akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kwa niaba na Maafisa Mawasiliano wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO WA BUNGE LA BAJETI LEO TAREHE 17 JUNI, 2016 MJINI DODOMA

bug1 
Mbunge wa Nchemba (CCM), Mhe. Juma Nkamia akifurahia jambo na Mbunge wa Kaliua (CUF), Mhe. Magnalena Sakaya wakati wakiingia katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma  kuanza kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo.
bug2 
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
bug3 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu, Mhe. Antony Mavunde akijibu maswali ya Wabunge leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
bug4 
Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Mhe. Almas Maige akiuliza swali Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
bug5 
Wabunge wa CCM Viti (Maalum) kutoka kushoto, Christine Ishengoma, Martha Umbulla na Magreth Sitta wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo leo.
bug6 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Halima Bulembo, akiuliza swali Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo. Kulia ni Mbunge wa Busega, Mhe. Raphael Chegeni.
bug7 
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia Ackson akibadilishana mawazo na Wabunge mara baada ya kuahirisha   kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
bug8 
Naibu Spika wa Bunge, Mhe.Dkt. Tulia Ackson akifurahia jambo na Mbunge wa Kibiti, Mhe. Ally Ungando mara baada ya kuahirisha kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

Hospitali ya Amana yaboresha huduma zake

index 
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Hospitali ya Rufaa ya Amana Jijini Dar es Salaam imeboresha huduma za afya kwa kuweka mashine maalumu ya kutibu meno ijulikanayo kama (Ceramic dental machine) lengo ikiwa ni kuboresha huduma hizo katika hospitali za umma.
Akiongea katika mahojiano kwa njia ya simu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bw.Meshack Shimwela ameeleza kuwa kwa sasa wataweza pia kutoa huduma ya afya kwa viongozi wa serikali pamoja na wabunge kupitia wodi maalum iliyotengwa kwa ajili yao ili kupata huduma hiyo wanapokuwa jijini hapa.
“Tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kutuletea mashine hii maalumu kwa ajili ya magonjwa yote ya meno na tunaishkuru pia kwa kutushauri kutenga wodi maalumu kwa ajili ya kuwatibia viongozi mbalimbali wakati wakiwa hapa Dar es Salaam,ushauri huo tumeupokea na tumeufanyia kazi”, alisema Simwela.
Aliongeza kuwa maboresho hayo yatasaidia wananchi kupata huduma bora za afya na kupunguza gharama za matibabu na kuondoa usumbufu wa kwenda kutafuta huduma hiyo katika hospitali binafsi.
Bw. Shimwela anabainisha kuwa mashine hiyo ilikuwa ikipatikana katika Hospitali chache za binafsi na matibabu yake huchukua muda mwingi na  gharama kubwa jambo ambalo lilikuwa likiwaumiza wananchi wenye kipato cha chini, hivyo upatikanaji wa huduma hiyo imekuwa msaada mkubwa sana.
Vilevile aliongeza kwa kutolea ufafanuzi suala la huduma ya wodi maalumu itakayokuwa ikitoa huduma za afya kwa viongozi na wabunge  tayari imeshaanza kufanya kazi tangu mwezi Machi mwaka huu ikiwa na   vyumba viwili vya wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na vyumba 24 ambavyo vina sehemu ya kukaa, kulala pamoja na choo.
Aidha, amefafanua kuwa matibabu katika wodi hiyo yanaweza kulipiwa kwa bima ya afya au kwa fedha taslimu pia ameongeza kuwa wodi hizo hazijatengwa kwa ajili ya viongozi pekee bali zinaweza kutumika pia kwa wananchi wa kawaida watakaoweza kulipia gharama za matibabu zilizopangwa katika wodi hiyo.
Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, David Langa amesema kuwa kufunguliwa kwa wodi hiyo kumesaidia sana waganga kuwepo katika vituo vyao vya kazi muda wote kwasababu huduma za afya kwenye wodi hiyo ni masaa 24 pia mganga anapomtibu mgonjwa anapatiwa asilimia 30 ya gharama za matibabu yale papo hapo,fedha hizo ni nje ya mshahara wa mwisho wa mwezi.
Ametoa rai kwa Serikali kuongeza mashine hizo maalumu kwa ajili ya magonjwa ya meno na kuziweka katika Hospitali mbalimbali ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa wengi katika Hospitali moja.

MERCY KITOMARI, MJASIRIAMALI KIJANA ANAYETAKA KUMUONA ‘ROLE MODEL’ WAKE RAIS MAGUFULI


Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige (hayupo pichani).
…………………………………………………………………………..
MJASIRIAMALI kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao.
Amesema Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara , inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika magumu mbalimbali .
Alisema katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama ‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
“Nimekuwa nikikutana na wanawake wenzangu ambao wamekata tamaa na wamekuwa wakiniuliza ninawezaje kuendelea, nikawambia wasi-give up (wasikate tama) na kwamba serikali hii ni ya viwanda na kuchapa kazi “ alisema na kufafanua kwamba wanachohitaji wanawake hao ni mazingira mazuri ya kufanya ujasiriamali.
Mercy ambaye anatengeneza ‘ice cream’ zinazotumia matunda yote ya kitanzania kama vile fenesi, nanasi, bungo, ndizi, embe ana ndoto ya kumiliki kiwanda kikubwa kinachoweza kutengeneza na kufikisha ashkrimu kwa Tanzania na Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2020.
Akiwa ameanza kazi hiyo mwaka 2010 kutoka ‘jiko’ la nyumbani Mercy amefanikiwa kutambua wigo wake wa biashara ambayo amesema ina changamoto nyingi hasa mifumo ya vibali na ulipaji kodi na ushuru.

Muonekano wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.
Alisema uwapo wa kodi nyingi zenye viwango sawa kati ya anayeanza na aliyekuwepo; anayeingiza kidogo na kikubwa kunaleta athari kubwa kwa wajasiriamali wanaotaka kuchomoza.
“To be honest (nikiwa mkweli) zinavunja moyo… nyingi zinakwamisha kwani sisi waelewe tu kwamba tunatengeneza ajira na tunatengeneza soko kama mimi nanunua matunda natengeneza soko la mkulima.,.. natengeneza ashkrimu (Ice Cream) natengeneza ajira.. ipo haja ya kuangalia mambo mengi na hasa hili la kodi na ushuru” alisema.
Alisema ana mambo mengi ya kumwambia Rais Magufuli kama mjasiriamali mwanamke kijana.
“Atupe nafasi tukutane naye wanawake wajasiriamali vijana kisha tutamweleza mengi yakiwemo ya kodi na mifumo yake, mimi ningemweleza haja ya vyombo vyote vya huduma kutumia mtandao, kutoa huduma ,ningemweleza haja ya halmashauri na taasisi kutoa mafunzo mbalimbali ili kuinua wajasiriamali hawa na kuwasapoti si tu kuchukua kodi na ushuru” anasema Mercy.
Anasema wajasiriamali wengi wadogo hawaendelei kwa kukosa sapoti ya mafunzo na namna ya kufanya biashara zao zikue.
“Wasiwe wanachukua kodi na ushuru tu, halmashauri hizi lazima zianze kufikiria kukuza wajasiriamali kwa kuwapa elimu inayostahili katika biashara zao” anasisisitiza Mercy ambaye amesema angelipenda kumuona Role Model wake (Rais Magufuli) kumweleza mengi yanayohusu wanawake vijana na viwanda vidogo kuelekea viwanda vikubwa na hamu ya wajasiriamali wanawake vijana kuchangia pato la taifa na kulipa heshima.
Anasema anapokutana na wajasiriamali wa Uganda, Rwanda anaona jinsi serikali zao zinavyowasaidia kunyanyuka na anaona serikali ya awamu ya tano inaweza kuwasikia na wao wakanyanyuka.

UVCCM MKOA WA ARUSHA WALAANI VIKALI SHUTUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA

index
Na Mahmoud Ahmad Arusha
UMOJA wa vijana mkoa wa Arusha umelaani vikali kitendo cha jenerali Twaha ulimwengu kumkashifu Rais Mstaafu na mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt Jakaya Kikwete kwa madai kuwa ashitakiwe mahakamani kwa kutumia fedha za umma vibaya kwa kuanzisha mchakato wa katiba ambao ulikwama kufikia tamati yake
 
Akitoa tamko hilio mbele ya wana habari mkoa wa Arusha mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha  Lengai Ole sabaya  alisema kuwa matamshi ya upotosha ji yaliyotolewa na jenerali twaha ulimwengu ni ya kupotosha umma
 
Aliongeza kuwa kutokana na matamshi hayo UVCCM wanamtaka jenerali aache kupotosha ukweli kama ulivyo kwani mchakato bado haujakwama ila umezingwa na miingiliano ya vipindi vya uitishaji wa kura ya maoni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
Aidha idhini ya matumizi ya fedha za mchakato wa Katiba ziliweza kuiidhinishwa na bunge kwa nia ya dhamira njema ya taifa ya kuandika katika yake mpya na wala sio ubadilifu au matumizi mabaya kama anavyotaka jenerali huyo.
 
Sabaya alisema kuwa alichokionesha jenerali mbele ya kadamnasi na vyombo vya habari ni kejeli pamoja na dharau isiyo staili kwani alionekana kujawa na nyongo kutokana na kumbukumbu zile za kuwekwa kando na utawala wa mkapa kasha kuzikwa kwenye kaburi la sahau utawala wa kikwete.
 
Aidha kutokana na matasmhi hayo umoja huo umewaomba na kuwasihi watanzania kuwa makini na kutuipilia mbali sanjari na kuweka tahadhari kwa watu wenye matamshi ya hamaki pamoja na hasira ambao wana nia mbaya ya kubomoa taifa.
 
Kutokana na hilo pia umoja huo umesema kuwa endapo kama ataendelea basi wao hawataweza kumtambua tena kama mwanachama mwenzao na pia watashinikiza hata uanachama wake utiliwe shaka kabisa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

ut6TAREHE 16.06.2016 MAJIRA YA SAA MAJIRA YA SAA 14:00HRS KATIKA ENEO LA LUCHELELE WILAYA YA NYAMAGANA MKOA WA MWANZA, ASKARI POLISI WALIFIKA KATIKA ENEO HILO TAJWA NA KUFANYA MISAKO PAMOJA DORIA NAKUWEZA KUFANIKIWA KUKAMATA WATU NANE WAKIWA NA POMBE AINA YA GONGO PAMOJA NAMITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA, 1. JESCA SIMONI MIAKA [14], MWANAFUNZI, AMBAYE ALIKAMATWA AKIWA NA LITA 42 ZA POMBE AINA YA GONGO, 2.NYANGE BIHEMO MIAKA [46] ALIYEKAMATWA AKIWA NA MITAMBO MIWILI YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, 3. MARIAM OMARY MIAKA [28] ALIYEKAMATWA NA POMBE YA GONGO LITA 3, 4. MAOLA LUCHUPA MIAKA 32 ALIYEKAMATWA AKIWA NA LITA 20 ZA POMBE AINA YA GONGO. WENGINE NI, 5. ELIZABETH JOHN MIAKA 35 ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MITATU YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, 6. ANASTAZIA ALOYCE MIAKA 25 ALIYEKAMATWA NA POMBE YA GONGO LITA 2, 7. TEDY PIUS MIAKA 40 ALIYEKAMATWA NA LITA 30 ZA POMBE YA GONGO NA, 8. PASKAZIA THOMAS ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MIWILI YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, WATUHUMIWA WOTE NI WAKAZI WA LUCHELELE.
AIDHA INADAIWA KUWA WATUHUMIWA HUFANYA BIASHARA  HARAMU YA POMBE YA GONGO NA WAKAZI WA MAENEO HAYO, HUKU WAKIIHALALISHA BIASHARA HIYO KUWA KAMA CHANZO CHAO KIKUU CHA KIPATO CHA KILA SIKU KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI. NDIPO JESHI LA POLISI LILIPOKEA TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KUHUSIANA NA UHALIFU HUO UNATENDWA NA BAADHI YA WAKAZI WA LUCHELELE NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU.
WATUHUMIWA WOTE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA POMBE AINA YA GONGO UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA WAFANYE KAZI NYINGINE HALALI AMBAZO ZITAWAINGIZIA KIPATO, LAKINI BIASHARA HARAMU ZA POMBE YA GONGO NA MADAWA YA KULEVYA NAWAOMBA MUACHE KUJIHUSISHA NAZO KABISA, KWANI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEJIPANGA VIZURI KUKABILIANA NA WAHALIFU WA AINA KAMA HIYO NA KUHAKIKISHA WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA

PEMBA WAMUOMBA KAMISHNA WA POLISI KIKOSIKAZI KWA AJILI YA UPELELEZI NA UKAMATAJI WA WANAOFANYA HUJUMA KWENYE MAZAO

Polisi+Zenji+PHOTO 
Na Masanja Mabula –Pemba
SERIKALI  katika   Wilaya  ya Wete , imemuomba Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar kuleta kikosi kazi cha Polisi Kisiwani Pemba kwa ajili ya kusaidia  upelelezi na ukamatwaji wa watu wanaofanya hujuma za kuharibu vipando na mali za wananchi .
Mkuu wa Wilaya ya Wete  , Rashid Hadid Rashid aliyasema hayo baada kutembelea shamba la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba  Dadi Faki Dadi lililoko Finya Mianzini , kukatwa minazi 46 , mikarafuu 5 na mashina ya mihogo 51.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa ombi hilo  kufuatia vitendo hivyo kuongezeka kila uchao na kusababisha hasara kwa wenye mali na Taifa kwa ujumla, jambo ambalo linaweza kudhoofisha uchumi wa nchi na wananchi wake .
“Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya hujuma , iko haja kwa Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar kuleta kikosi kazi kwa ajili ya kufanya upelelezi ili wahusika waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ”alisema Mkuu wa Wilaya .
Aidha  Mkuu huyo wa Wilaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati na ulinzi na usalama  amelaani vikali vitendo hivyo vya hujuma vinavyofanywa na watu wasiojulikana na kuvitaja kwamba ni njama za makusudi zinazofanywa na baadhi ya watu kwa misingi ya itikadi za kisiasa .
Akitoa taarifa  kwa kamati ya Ulinzi ya Ulinzi na Usalama , Mlinzi wa Shamba hilo Ali Naulima Ulamu alisema , hujuma hizo alizibaini baada ya kufika katika eneo hilo kwa ajili ya shughuli za kilimo majira ya saa kumi na mbili (12) asubuhi .
Ulima alifahamisha kwamba bado hajawabaini watu waliohusika na kitendo hicho ambapo , alichukua hatua ya kumupa taarifa Sheha pamoja na mmiliki wa Shamba kuhusiana na hujuma hizo  .
“Nilibaini kuwepo na uharibifu huu majira ya saa 12 asubuhi baada ya kufika kwa ajili ya shughuli za kilimo , lakini nilichokifanya ni kutoa taarifa Serikalini pamoja na kumpa taarifa mmiliki wa shamba ”alieleza.
Kwa upande wake mmiliki wa shamba hilo Dadi Faki Dadi aliwataka wananchi kuwa na  hofu ya Mungu kwa kuhakikisha wanajiepusha matendo ambayo yanakinzana na Haki na Binadamu na utawala wa misingi ya Sheria .
Alieleza kwamba ni jambo la kushangaza kwa muumini wa dini kutekeleza vitendo vya kuhujumu mali za mwenzake hasa katika kipindi hichi cha mfungo wa mwezi  mtukufu wa Ramadhan  .
Aidha amewashauri viongozi wa dini kutumia fursa waliyonayo kwa kutenga muda wa kuyaungumzia matendo hayo wakiwa katika sehemu zao Ibada , ili waumini waweze kutambua athari zake .
Hili ni tukio la nane kutokea katika Wilaya ya Wete la kuhujumiwa kwa mali , mazao na vipando vya wananchi ikiwemo uchomaji moto nyumba , mashamba ya mikarafuu , majengo ya Serikali , kufyekwa kwa mashamba ya mipunga na kung’olewa kwa vipando   baada ya kumalizika uchaguzi Mkuu wa marejeo uliofanyika machi 20 mwaka huu .
Tangu kuanza kutokea kwa matukio hayo katika Wilaya hiyo , hakuna mtu au kikundi cha watu waliokamatwa wakihusishwa na hujuma hizo .

DKT SHEIN AKUTANA NA WAZIRI AUGUSTINO MAHIGA

mah1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.
mah2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.
mah3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya  mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]17/06/2016. 

MTANZANIA BW. MAKALA JASPER ATUNIKIWA TUZO NA NATIONAL GEOGRAPHIC SOCIETY

Bw. Makala Jasper, Mkurugenzi Mwandamizi wa NGO ya Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI) ametunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award forLeadership in African Conservation. 
Tuzo 
Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marekani akiwa na Bw. Makala Jasper alipotembelea ofisi za Ubalozi
Pichani: Rais wa National Geographic Society Bw. Gary E. Knell mara baada ya kumkabidhi Bw. Makala Jasper tuzo. Kulia ni Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi na Bi. 
Bw. Makala Jasper akitoa shukurani kwa kupewa tuzo
National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation 
Bw. Gary Knell akiwa na Bi. Mounia Mechbal, Mwakilishi wa Rolex, Bw. Lee Berger mshindi wa tuzo ya Explorer of the Year, na Terry Garcia, Mkuu wa Masuala ya Sayansi na Utafutaji, National Geographic
Bi. Pasang Akita akipokea tuzo ya Adventurer of the Year
Pichani katikati: Washindi wa Tuzo ya Hubbard Medal  Bw. Nainoa Thompson na Bi. Meave Leakey

Miss Universe Tanzania 2015 afuturu na watoto, Makonda atoa neno

Katika kusherekea siku maalum ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni, 16 ya kila mwaka, Kamati ya Miss Universe Tanzania kupitia mpango wake mpya uitwao Binti Jasiri ilikutanisha kwa pamoja watoto 90 kutoka vituo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam ambapo halfa hiyo ilihudhuliwa na Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 
Akizungumza na watoto hao, Makonda aliwambia kuwa serikali ya awamu ya tano inawathamini watoto na hata kuwawekea elimu bure hivyo waongeze juhudi katika masomo yao ili nao waweze kuja kuwa na maisha mazuri na hata kuwasaidia wengine kama jinsi wao wanavyosaidiwa na watu wengine ambao wamefanikiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watoto kutoka vituo mbalimbali vya kulea watoto kutoka mkoa wa Dar es Salaam katika halfa maalum ya kusherekea siku ya mtoto wa Afrika, Kushoto ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)
 
“Watu wenye maisha mazuri wasiwachanganye hata nyie mnaweza kuwa na maisha mazuri hata zaidi yao, mnatakiwa muongeze bidii katika masomo yenu ili na nyie mfanikiwe na kuwasaidia wenzenu kama jinsi mnavyosaidiwa na wengine kwa sasa,” alisema Makonda.
 
Nae Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot ambaye pamoja na kupata chakula cha pamoja na watoto hao pia alipata nafasi ya kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu maisha, kuwashauri na kuwatia moyo ili waongeze bidii katika masomo yao na hata baadae waweze kufanikiwa kimaisha.
 
Halfa hiyo ilisimamiwa na Magdalena Gisse na kuhudhuliwa na watoto kutoka Kituo cha Malaika Kids Orphanage, Kurasini Orphanage, Sarafina Orphanage na Makini Orphanage vyote kutoka mkoa wa Dar es Salaam
Na Rabi Hume, MO Blog.
 
Watoto wakimpigia makofi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza nao katika halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsalimu mmoja wa watoto waliohudhulia halfa maamul ya kumkumbuka mtoto wa Afrika, Aliyembeba mtoto huyo ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na katikati ni Mkurugenzi Kitaifa wa Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai.
Watoto mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo wakifurahi kwa pamoja.
Baadhi ya watoto waliohudhuria halfa hiyo walio na imani ya Kiislamu wakisali.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akifuturu kwa pamoja na watoto kutoka vituo mbalimbali waliohudhuria halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akifuturu kwa pamoja na watoto waliohudhuria katika siku maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akimlisha mmoja wa watoto waliohudhuria halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika.
Watoto mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo wakifuturu na kujiburudisha na vinywaji kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises ambayo ilijitolea vinywaji katika halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika.
 
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akifurahi na watoto waliohudhuria halfa hiyo kwa kuwaonyesha jinsi mtandao wa kijamii wa Snapchat jinsi unavyotumika.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akizungumza na watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Mmoja wa watu waliokulia katika kituo cha kulelea watoto cha DogoDogo, Dk. Yusuph akiwatia moyo watoto hao na jinsi ambavyo wanaweza kufanya ili na wao waweze kufanikiwa kama ilivyo kwake.
Msimamizi wa halfa hiyo, Magdalena Gisse akiwashukuru watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwasaidia watoto kufungua maputo baada ya halfa hiyo kumalizika.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waliohudhuria halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.
Washiriki wa halfa maalum ya mtoto wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja.

KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya (EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya  Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pacific.
Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameteuliwa kwa kutambua mchango na juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk.  Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na uhakika kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelgiji.
Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA VIKAO KAZI NA WATUMISHI WA MKOA WA SINGIDA

mwak1 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, MenejimentiyaUtumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watendaji hao kilichofanyika jana Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016.
mwak2 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Watumishi mbalimbali wa Mkoa wa Singida (hawapo pichani) alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki yaUtumishi wa Umma kwa mwaka 2016, mkoani Singida jana, wanaofuata kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Mathew Mtigumwe, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Saidi Amanzi.
mwak3 
Baadhi ya Watumishi wa umma mkoani Singida wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016, mkoani Singida jana.
mwak4Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na Watumishi wa Mkoa wa Singida kilichofanyika jana ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni kila mwaka.
mwak5 
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dkt. John Mwombeki akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na Watumishi wa Mkoa wa Singida kilichofanyika jana ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni kila mwaka,
mwak6 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akipokea Ripoti ya Utendaji wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Singida kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha Utumishiwa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo jana, wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Bw. Rajabu Mirambo na Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Singida, Bw. Ramadhani Marijani
mwak7 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na tawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida mara baada ya kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika jana ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni kila mwaka, kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo na kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
…………………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Umma nchini waliopewa dhamana serikalini kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima kwa wanaowahudumia.
Waziri Kairuki aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016 mkoani Singida.
“Najua miongoni mwa watumishi wa umma wapo watumishi waliopewa dhamana lakini utoaji wao wahuduma unatiliwa shaka. Hawapendi kusikiliza matatizo ya wateja wa ndani yaani watumishi wenzao,” Mhe. Kairuki alisema.
Amewataka watumishi wenye tabia hizo kuacha mara moja na kuishi maisha ya kazi kama Mkataba wa Huduma kwa Mteja unavyowaongoza katika kutoa huduma kwa kiwango kwa wateja wote wa ndani na nje ya taasisi.
Aidha, Mhe. Kairuki amewataka Watendaji kutenga muda wa kukaa na watumishi wao ili kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
“Uzoefu unaonyesha kuwa watumishi wanaposhirikishwa katika masuala yanayowagusa kama tulivyo hapa basi huduma kwa wananchi na wadau wengine zitaboreka na kazi kufanyika kwa ari na hivyo kuongeza tija na ufanisi kazini,” Waziri Kairuki aliongeza.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kairuki alifanya ziara katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho ambapo aliwataka watumishi hao kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika ili kuleta matokeo bora kwa taifa.
“Tuwewabunifu, tuangalievipaumbele, tufundishe kozi ambazo hazifundishwi sehemu nyingine ili kuweza kupata soko zuri zaidi,” Waziri Kairuki alisisitiza.
Aliwasisitiza watumishi hao kuwa na ushirikiano na vyuo mbalimbali hasa katika nyanja za utafiti, mafunzo na masuala mengine ya maendeleo ili kuboresha chuo hicho.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16-23 Juni, kila mwaka, kwa mwaka 2016 yanafanyika kwa namna tofautia mbapo Viongozi na Watendaji wanakutana na wateja wao wa ndani na nje ya taasisi zao kwa lengo na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika kutekeleza hilo, Mhe. Kairuki amezindua maadhimisho hayo kwakufanya vikao kazi na watumishi wa mkoa wa Singida kutoka katika kada mbalimbali za utumishi wa umma.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika kwa mwaka 2016 ni “Uongozi wa Umma kwa ukuajiJumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka.”
Kaulimbiu hiyo inaambatana na kaulimbiu ndogo ambazo ni: Mchango wa Utumishi wa Umma katika Ukuaji wa Uchumi Barani Afrika na Mchango wa Utumishi wa Umma katika Kuiwezesha Ajenda ya Afrika ya 2063 ambayo inaweka mkazo katika Maendeleo ya Afrika na Haki za Wanawake.

No comments:

Post a Comment