Thursday, June 16, 2016

JK BALOZI WA HESHIMA MAENDELEO YA KILIMO, AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI

NA BASHIR NKOROMO
……………………………….
KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for
Agricultural and Rural Cooperation, CTA) chenye makao makuu mjini
Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya  Kikwete kuwa
Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika
Mabara ya Afrika, Karibiani na Pasafiki.
Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora,
CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Taifa,
ameteuliwa kwa kutambua mchango wa juhudi zake katika kukiendeleza
kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk.  Kikwete aweze kuiwakilisha
katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umhimu wa
kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha kwa
vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki.
Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na
waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika
kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidia na taasisi hiyo ambayo ni
ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na
Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelijiji.
Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya
CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano
tangu 2013 hadi 2018.

Uchambuzi Wa Habari: Tunafanyaje Na Naibu Spika Tulia Ackson?

TU1 
Ndugu zangu,
Swali hili lilipaswa  wajiulize Wabunge wa upinzani wenye kutoka Bungeni kila baada ya dua ya asubuhi.
Kwa kufuatilia kwangu siasa za nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi kwa sasa, naona mkakati huu wa  wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.
Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa wapinzani huko tunakokwenda kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi Bungeni.
Unapopanga kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo husika. Kwa sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na mengineyo, wapinzani kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza ingeeleweka kwa wapiga kura.
Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya siku ya kazi za Bunge walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga hisia miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni  kukosekana kwa umakini.
Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na hakika nilisikitika moyoni. Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya Watanzania kuwa na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama yale.
Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika nafasi yake na ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang’atuke kwa mujibu wa  kanuni, sheria  na taratibu zetu kimfumo.
Yanapotokea mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni, sheria na taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za kuyabadili hayo ni ndani ya Bunge au Mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge. Na kwa ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku itawalazimu wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo. Tatizo hapa watakuwa wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.
Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio watakaounda Serikali na Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa.
Kama wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu  hawatampenda au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu wabunge hao wa CCM kwa wakati huo.
Maggid Mjengwa,
Mhariri Online
Mjengwablog/KwanzaJamii

MONTAGE LIMITED, SERENA NA NMB ZATOA MSAADA KWENYE KITUO CHA MTC BUNJU

1 
Bi. Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited na Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena wakishiriki kazi ya kupaka rangi kwenye jengo  linalotumiwa na wanafunzi wa kituo  cha mafunzo kwa vijana  cha Multpurpose Training Center kilichopo Bunju wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam kwa ajili  ya kulia chakula jana, Kampuni za Montage Limited, Serena Hotel na Benki ya NMB ziliungana kwa pamoja na kukipa msaada wa vitu mbalimbali  ikiwemo rangi, madaftari, mafuta ya kupaka  chakula vifaa vingine  katika kituo hicho vyenye thamani ya shilingi milioni tano.2 
Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena akipaka rangi kwenye ukuta wa jengo hilo huku wafanyakazi wenzake wakimuangalia.
3
Wafanyakazi wa Hoteli ya Serena wakishiriki kupaka rangi
4
Wafanyakzi wa Kampuni ya Montage wakishiriki kupaka rangi katika jengo hilo.
5
Mratibu wa kituo cha MTC Bw.Issa Buzohela akielezea jambo wakati ugeni huo ulipotembelea kwenye darasa la vijana wanaojifunza ufundi seremala kituoni hapo.
6
Hawa ni wanafunzi wanaojifunza kushona nguo kutuoni hapo wakiendelea na mafunzo.
7
Ugeni huo ukishuhudia jinsi wanafunzi hao wanavyojifunza kushona nguo.
8
Kituo hiki pia kinatoa mafunzo ya kuzima moto na uokoaji haoa wanafunzi wakiwa tayari wamevalia ngua maalum kwa ajili ya kuokoa mtu aliyenasa kwenye jengo refu linalowaka moto.
9
Nguzo hii ya chuma ni mfano wa jengo na mtu aliyenasa yuko juu hivyo wanafanya kazi ya kumuokoa.
10
Tayari wanamshusha kwa kutumia Machela, kamba, na ngazi kama inyoonekana katika picha 
11
Wanaendelea kushusha chini.
12Hapa tayari ameshaokolewa na taratibu zinazofuata sasa ni kumpa huduma ya kwanza na kisha kumpeleka hospitali.

KISHAPU YANUFAIKA NA MRADI WA KUIJENGEA JAMII UWEZO WA KUJIANDAA NA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA.

 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Hawa Ng’humbi akizungumza na baadhi ya wataalam wa masuala ya maafa walipomtembelea
ofisini kwake ili kufanya tathimini ya utekelezaji wa  mradi wa  Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Juni 16, 2016.
 Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika
Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison Chinyuka (wa kwanza kulia) akifuatilia mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kujadili utekelezaji wa mradi huo, Wilaya ya Kishapu tarehe 16 Juni, 2016.
 Mmoja wa wanachama wa kikundi cha Mazingira Bi. Juliana Peter akichangia hoja wakati wa kikao cha
tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Juni 16, 2016.
Baadhi ya wanakikundi cha Muungano wakifurahia mafanikio ya kuongezeka kwa mbuzi ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari
za Maafa wakati wa tathimini ya utekelezaji wake iliyofanywa na Idara ya Maafa
Ofisi ya Waziri mkuu tarehe 16 Juni, 2016 Wilaya ya Kishapu Shinyanga.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

SERIKALI MKOANI MBEYA YASITISHA MATUMIZI YA DARAJA LA MBAKA WILAYANI RUNGWE MPAKA LITAKAPO KAMILIKA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mwenye miwani akitizama maendeleo ya ujenzi wa daraja Mbaka katika kijiji cha Kibhundughulu  wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ambalo ujenzi wake ulikwama kutokana na ukosefu wa fedha hali ambayo iliwalazimu wananchi wa kijiji hicho kupita juu ya daraja hilo kwa kutumia kamba kitendo ambacho kilikuwa kikihatarisha maisha yao.
(PICHA E.MADAFA JAMIIMOJABLOG) .
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mwenye miwani akijaribu kupita kwa lengo  kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mbaka katika kijiji cha Kibhundughulu  katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ambalo  ujenzi wake ulianza toka mwaka 2015 na  ulishindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 58 ambapo katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa wa mbeya aliambatana na baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo.
Mafundi wa kampuni ya Richer Ivestment ya Mkoani Mbeya ambao ndio wanajenga daraja hilo wakiendelea na ujenzi daraja hilo ambapo hadi kukamilika kwakwe linataji kukagharimu kiasi cha shilingi milioni 58 .
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibhundughulu  Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya ambao ndio watumiaji wa daraja hilo la Mbaka ambalo lilikwama kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha hali iliyopelekea wananchi wa kuanza kutumia daraja hilo kwa kupita juu kwa kutumia kamba hali ambayo iliatalisha maisha yao.
Katika mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuwapa ushirikiano mafundi wanaojenga daraja hilo ili liweze kukamilika kwa wakati .
Aidha Makalla amekemea baadhi watu wasio waaminifu ambao walikuwa wakipita juu ya daraja hilo kabla ya kukamilika kwakwe kitendo ambacho kilikuwahatari kwa maisha ya wananchi hao.
Aidha amemtaka mkarandasi anaye jenga daraja hilo kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo katika kipindi cha wiki mbili ili kutoa fursa kwa wananchi hao kuanza kulitumia . 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akisiadiana na mafundi wa kampuni ya Richer Investment ambao wanajenga daraja la Mbaka kwa kiasi cha fedha shilingi Milioni 58 mara baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kibhundughulu ambao ndio watumiaji wa daraja hilo.
Baadhi ya akinana wakazi wa kijiji cha Mbaka Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakikatiza katika ya mto kutokana na Daraja walilokuwa wakitumia kuzuiwa na serikali ili kupisha ujenzi wake.

WAZIRI POSSI AIWAKILISHA VYEMA AFRIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUTOKOMEZA UMASIKINI NA KULETA USAWA KWA WATU WENYE ULEMAVU

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe.Dkt.Abdallah Possi akichukua dondoo za Mkutano wa 9 wa nchi ambazo
zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Marekani tarehe 15 Juni, 2016.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 9 wa nchi ambazo zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu wakifuatilia mada wakati wa
mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa New York Marekani Juni
15, 2016.
…………………………………………………………………………………………..
Na.MWANDISHI WETU
Siku ya tarehe 15 Juni, 2016, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (MB),
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu alishiriki  katika  Mjadala wa
kutokomeza umasikini na kuleta usawa kwa watu wenye ulemavu. Majadiliano hayo
yalikuwa ni moja ya mikutano muhimu iliyolifanyika katika Mkutano wa 9 wa nchi
ambazo zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliofanyika New York,
Marekani.
Mwenyekiti wa majadiliano hayo alikuwa ni Bi. Ellen Maduhu,
Afisa katika ofisi ya uwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Kamati ya Mkutano wa Nchi ambazo zimeridhia
Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (Vice President of the Conference of
State Parties to the Convention on the Rights of Persons of Disabilities)

WAZIRI MKUU, MHE. KASSIM MAJALIWA AWAFUTURISHA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwaongoza wabunge kupata futari iliyoandaliwa na Wazri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia Ackson akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa mara
baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu akitoa neon la shukrani kwa Wazri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa mara baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Mhe. Andrew Chenge akitoa neon la shukrani kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisikiliza neon la shukrni kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia
Ackson mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwashukuru wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mara baada ya kujumuika naye katika futari aliyowaandalia leo na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

TANZANIA NA SWEDEN ZATILIANA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA MAENDELEO

swe2 
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya Tanzania na Sweden, kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo Juni 16, 2016
swe3 
Katibu Mkuu Wizara ra Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya  kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa maendeleo wa miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
swe4 
Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Tasaf Ladislaus Mwamanga (kushoto) wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
swe5 
Ujumbe wa Sweden ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (Katikati), wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka mine kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
swe6 
Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
swe7 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya  kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka mine kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
Pichana na Benny Mwaipaja
Kaimu Msemaji wa Serikali Wizara ya Fedha na Mipango
…………………………………………………………………………………………………………………
Benny Mwaipaja, WFM-DODOMA
SERIKALI za Tanzania na Sweden zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka 4 kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2019 utakaojikita kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya watu katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, utafiti, nishati jadidifu na kupambana na umasikini.
Tukio hilo limefanyika leo Juni 16, 2016, mjini Dodoma kati ya Katibu Mkuu na mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimaendeleo wa Sweden, Mhe. Ulrika Modeer.
Dkt. Likwelile ameeleza kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2019, Serikali ya Sweden itatoa ruzuku ya fedha za Kiswidi, SEK 5.5 Biln, sawa na shilingi Trilioni 1.42 za Kitanzania.
Amesema kuwa kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano huo kutafuatiwa na utiwaji saini wa mikataba ya kifedha  ambapo fedha hizo zitaelekezwa katika miradi kadhaa ikiwemo kusaidia Elimu, Maendeleo ya Jamii-TASAF, Utafiti, Nishati, Demokrasia, Haki za Binadamu, na Sekta Binafsi.
“Ushirikiano huu umelenga kusaidia kujenga mazingira ya maendeleo endelevu na kuwapatia Watanzania maskini fursa za kujikwamua katika umaskini kwa kujipatia ajira na kuweza kuanzisha biashara za kujipatia kipato ambapo vikundi vinavyolengwa zaidi ni wanawake, watoto na vijana” Alisema Dkt. Likwelile
Dkt. Servacius Likwelile ametoa wito kwa Serikali ya Sweden na nchi nyingine duniani kuwekeza katika biashara na vitega uchumi ili ziweze kunufaika na rasimali kubwa ambazo nchi imejaaliwa ikiwemo maliasili, ardhi yenye rutuba na jiografia ya kimkakati inayochochea uwekezaji na biashara
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ushirikianno na Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer, amepongeza uongozi mahili wa Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupambana na vitendo vya kifisadi ikiwemo rushwa.
“Sweden inaunga mkono kwa nguvu zote hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli kupambana na mauvu nchini na tunaamini nchi itapiga hatua kubwa kimaendeleo” Alisistiza Modeer.
Mhe. Ulrika Modeer ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa fedha kupitia mfuko mkuu wa Bajeti ili kuwezesha kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa hifadhi ya mazingira, kilimo endelevu, kuwawezesha wananawake kiuchumi na kumsaidia mtoto wa kike na kiume kielimu.
“Tunataka kuona kuwa maendeleo ya nchi yanakwenda sambamba na maendeleo ya wananchi wake ambapo tunaamini kuwa utafiti utasaidia kupata njia bora za kupambana na umasikini”Alisisitiza Mhe. Modeer
Amesema kuwa pamoja na nchi yake kutaka kuyasaidia makundi  mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu, wanataka kuona suala la demokrasia na utawala bora vinapewa kipaumbele katika mipango mbalimbali ya maendeleo
“Vilevile uwekezaji wetu mkubwa wa fedha katika maendeleo ya Taifa hautakuwa na maana sana kama suala la hifadhi ya mazingira halitapewa kipaumbele kwa kuanzisha miradi ya nishati jadidifu “Renewable energy” ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi: aliongeza Mhe. Ulrika Modeer
Uhusiano wa Tanzania na Sweden umedumu tangu mwaka 1960 ambapo katika kipindi chote cha miaka 50, serikali hizi mbili zimeshirikiana katika kubuni na kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo
Programu na miradi itakayotekelezwa katika ushirikiano uliosainiwa leo unaendena pia na Mpango wa Taifa wa Pili wa Miaka Mitano unaoanzia mwaka 2016/17 hadi 2020/21 na unalenga kuondoa utegemezi wa misaada kwa Tanzania.

PROF MBARAWA ATETA NA BODI MPYA BANDARI

MBA1 
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mh. Profesa Makame Mbarawa hayupo pichani.
MBA2 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kuanza kazi mara moja kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo hapa nchini.
Akizungumza na bodi hiyo kupitia Teknolojia ya Video (Video Conference) toka mjini Dodoma Prof. Mbarawa ameitaka bodi hiyo kufahamu kuwa miundombinu ya banadri nchini iko katika hali duni, isiyo uwiana na malengo ya Serikali ya kuwa na bandari itakayoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
“Kazi yenu kubwa ya kwanza ni kurudisha uadilifu na ufanyakazi wa uzalendo na unaozingatia weledi kwa watumishi wote wa bandari nchini”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amesema TPA inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo watu kuajiriana kindugu, utendaji usiozingatia matokeo, mifumo mibovu ya ukusanyaji mapato, baadhi ya watendaji kuwa na maslahi binafsi katika kampuni zinazofanya kazi bandarini na utendaji dhaifu wa matumizi ya mifumo ya elektoniki hali inayosababisha utendaji usio na ufanisi.
Aidha Prof. Mbarawa amezungumzia umuhimu wa bodi hiyo kuangalia upya muundo wa bodi ya zabuni ya bandari na namna kampuni zinazopewa zabuni zinavyopatikana ili kuondoa manung’uniko na mikwamo katika utekelezaji wa miradi.
“Hakikisheni mnaweka watu waadilifu, wasio na maslahi binafsi katika bodi za zabuni ili kuiwezesha bandari kushindana na bandari za nchi nyingine na hivyo kuvutia wasafirishaji wengi hali itakayoongeza mapato ya bandari na kukuza uchumi wa nchi”,
 amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TPA Prof. Ignas Rubaratuka amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga kubadili changamoto zote za bandari nchini kuwa fursa na kazi hiyo itafanywa kwa weledi na kwa muda mfupi.
Amesema watahakikisha kuwa malalamiko yanayotokana na bandari yanashughulikiwa kwa weledi na kwa kufuata sheria ili haki itendeke na kuiwezesha bandari kuwa na hadhi inayostahili.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho ameitaka bodi hiyo kujifunza majukumu yake kwa haraka na kutenda kazi kwa mujibu wa sheria.

MICHUANO YA COPA AMERICA YAFIKIA ROBO FAINALI

Na Mwandishi Wetu
 MICHUANO ya Copa America inayoonekana moja kwa moja kupitia visimbuzi vya StarTimes Tanzania imefikia hatua ya robo fainali ambayo itaanza kutimua vumbi kesho Juni 16 mpaka 19.
Timu zilizotinga hatua hiyo ni Argentina, Chile, Mexico, Marekani, Venezuela, Peru, Colombia na Ecuador huku mashabiki wa soka wakishuhudia miamba ya soka ya timu za Brazil na Uruguay wenye nyota lukuki kama vile Luis Suarez, Edinson Cavani, Willian, Countinho na wengineo wakishindwa kuzisaidia timu zao.
Katika michuano hii ya kusisimua kikosi cha timu ya taifa cha Argentina kikiongozwa na mchezaji bora wa dunia mara tano, Lionel Messi, ambacho kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kimeingia kwa kishindo hatua ya robo fainali baada kushinda michezo yote mitatu na kuongoza kundi D kwa alama tisa.
Kupitia chaneli za Sports Focus na World Football wateja na watanzania wanatazama michezo yote moja kwa moja huku wakiwa na nafasi ya kusinda zawadi mbalimbali kama vile vifurushi vya bure pamoja na pesa taslimu na safari kwenda Ujerumani kutazama mechi za Bundesliga za msimu ujao unaotarajiwa kuanza mwezi wa nane.
Akitoa ufafanuzi juu ya michuano hiyo Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa, “Mbali na kufurahia matangazo ya moja kwa moja ya mechi zinazochezwa nchini Marekani pia tuna kampeni inayoendelea ya ‘Tabiri na Ushinde’ inayoenedelea kupitia mitandao yetu ya facebook na instagram. Kupitia kampeni hiyo mteja anaebashiri kwa usahihi matokeo ya mechi ya siku husika hupata fursa ya kujishindia kifurushi cha Mambo pamoja na cha michezo cha Sports Plus cha jumla ya shilingi 36,000/-.”
“Mbali na hapo pia kuna zawadi zingine zinazotokana na kampeni ya hashtag ya #CopaAmericaonStarTimes kupitia mitandao yetu pia. Mshindi wa kampeni hii hupatikana kwa kushea mara nyingi zaidi post atakayoiona kuwekwa na kurasa za StarTimes na kufikia watu wengi zaidi. Mshindi wa kwanza wa kampeni atapatiwa tiketi VIP ya kwenda ya kwenda Ujerumani kutazama mechi za Bundesliga msimu ujao pamoja na dola za Kimarekani 1500/-, huku wa pili na wa tatu watapatiwa simu za mkononi za kisasa aina ya Solar 5. Tumefanya hivi ili kuwazawadia wateja wetu waaminifu na wanaofuatilia huduma zetu ili kunogesha zaidi shamra shamra za kombe la Copa America.” Alimalizia Bi. Hanif 
Hatua ya robo fainali itakayoanza kupigwa kesho itazijumuisha timu zote zilizoshika nafasi ya pili katika makundi yao.
Wapenzi wa soka ulimwenguni wanazidi kusononeshwa na mwenedo mbovu wa kikosi cha taifa cha Brazil ambacho kimeshindwa kutinga hatua hiyo kwa kufanikiwa kushinda mechi moja tu kati ya tatu. Matokea hayo mabovu yamepelekea kocha wa taifa timu hiyo Dunga kutimuliwa kazi.
Timu na ratiba kwa timu zitakazopambana ni  pamoja na Marekani na Ecuador (Juni 16), Peru na Colombia (Juni 17), na mechi za mwisho ni Argentina na Venezuela; Mexico na Chile (Juni 18). Timu zitakazopita hatua hii zitakutana katika hatua ya nusu fainali siku ya Juni 21.

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KESHO KWENYE SHEREHE ZA SIKU YA WAHITIMU WA CHUO CHA MZUMBE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria  sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Manisapaa ya Morogoro mjini Ndugu Fikiri Juma  mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria  sherehe ya siku wahitimuwa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa chuo cha Mzumbe  mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria  sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 YAANZA RASMI

MIS1 
Baadhi ya wateja waliofika kuhudumiwa siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016. Anayeelekeza (katikati) ni Afisa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bi. Rehema Msemo.
MIS2 
Wateja wakihudumiwa katika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni Siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
MIS3 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt.Laurean Ndumbaro (kushoto) akisikiliza matatizo/maoni kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Ofisi yake katika siku ya kwanza ya wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
MIS4 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt.Laurean Ndumbaro (kushoto) akisikiliza matatizo/maoni kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Ofisi yake katika siku ya kwanza ya wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YAKABIDHI MADAWATI 800 KWA WILAYA YA KILWA


Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akifafanua jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati kwaajili ya watoto wa shule za msingi wilayani Kilwa

Baadhi ya madawati yaliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy
Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilay ya Kilwa Juma A. Njwayo madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani mwake. Wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Kilwa, viongozi kutoka PanAfrican Energy na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Masoko katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kilwa Masoko.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma Abdallah Njwayo akiwaasa wanafunzi wa shule ya Msingi Masoko ambao ni moja ya wanufaikaji wa madawati 800 kutoka PanAfrican Energy kuyatunza madawati waliyopewa na kusoma kwa bidii.

Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akitoa neno wakati akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma A. Njwayo madawati 800 yatakayosaidia watoto 2400 na kupunguza tatizo la uhaba wa madawati.

Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akitoa neno wakati akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma A. Njwayo madawati 800 yatakayosaidia watoto 2400 na kupunguza tatizo la uhaba wa madawati.
………………………………………………………………………………………………
PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YATOA MADAWATI 800 KWA WILAYA YA KILWA 

Kapuni ya uchimbaji gesi asilia PanAfrican Energy jana imekabidhi madawati 800 kwa ajili ya shule za msingi wilayani Kilwa yenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 104. Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Masoko iliyopo wilayani humo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni hiyo, huku ikishuhudiwa na wana habari, viongozi mbali mbali wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Juma Njwayo, walimu, wanafunzi na wananchi wa Kilwa Masoko. Msaada huo wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Msingi ni kuunga mkono Kampeni ya uchangiaji madawati iliyoanzishwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Akiongea wakati akipokea madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma Njwayo, ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla hiyo aliwashukuru sana Kampuni ya PanAfrican Energy kwa msaada wao mkubwa wanaotoa kwa wilaya ya Kilwa. 
“Kwa niaba ya wana Kilwa naomba kutoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa PanAfrican Energy kwa siku zote kutuangalia kwa jicho la tatu kwa mmekua mkijitoa kawa hali na mali kuwezesha huduma mbali mbali katika Wilaya yangu Ya Kilwa. Leo napokea madawati 800 ambayo yatasaidia kupunguza uhaba wa madawati mashuleni kwani yatasaidia watoto 2400 kutokukaa chini, hili si jambo dogo kabisa hivyo mnahitaji pongezi. 
Natoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huu walionesha PanAfrican Energy kwani bado tuna uhaba wa madawati katika shule zetu za msingi hapa Kilwa. Hapa katika Shule ya Msingi Masoko watapata madawati 145 ambayo yapo mbele yetu hapa na mengine 655 yaliyobakia yatagawiwa kwa shule zingine zenye uhaba huo. Tunategemea ifikapo katikati ya mwezi Julai tutakua tumemaliza tatizo la madawati katika shule za msingi wilayani humu. Pia alitoa wito kwa wanafunzi kutunza madawati hayo ili yaweze kunufaisha wanafunzi wengi zaidi.”“Mbali na kupata madawati pia tunawapongeza kwa kuwa na uzalendo na wilaya yetu kwani hata mzabuni aliyepata kazi ya kutengeneza madawati haya ni mwananchi wa Kilwa ambapo vijana kadhaa wamepata ajira kupitia kazi hiyo na kuongeza kipato chao. 
Ukiachilia mbali swala la elimu Kampuni hii imekua mstari wa mbele katika swala la afya pia ambapo katika kuupunguza vifo vya kina mama na watoto wanatujengea jengo la Mama Ngojea katika hospitali yetu ya Wilaya ambako kabla yam waka huu kuisha tutakua tumeshakabidhiwa jengo hilo pia wanakarabati kituo cha afya cha Kilwa Masoko.” Aliongeza Mh. Njwayo.Naye Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za jamii wa Kampuni ya Uchimbaji wa Gesi ya PanAfrican Energy Andrew Kashangaki alisema, “Ni furaha yetu kuona watoto wa kitanzania wanasoma kwa Amani bila kuwa na matatizo yeyote na ndomana tumesukumwa kuunga mkono sekta ya elimu nchini kwa kuanza na wilaya ya Kilwa. 
Leo tunakabidhi madawati 800 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa yatakayosaidia kupunguza tatizo la watoto wetu kukaa chini na wadawati haya yatagawanywa kwa shule za msingi mbalimbali kutokana na uhitaji wao. Sisi kama wadau wa Elimu tumefanya kile tulichoweza kufanya hivyo tunaamini kwa madawati haya tunawawezesha watoto wa kitanzania watakaosomea katika shule hizo kutoa ujinga na tunatengeneza Taifa la wasomi.Aliongeza kwa kusema kuwa, “Tayari tuna programu ya kusomesha watoto kutoka kisiwa cha Songosongo ambako kila mwaka tunasomesha watoto 28, tumejenga mabweni kwaajili ya watoto wa kike kisiwani songosongo, pia ujenzi wa maabara za kisasa kwa ajili ya masomo ya sayansi kwa shule za Sekondari hiyo yote ni kuhakikisha tunaweka mazingira mazuri ya kusomea kwa watoto wetu.” Wilaya ya Kilwa ilikua ina uhaba mkubwa wa madawati tangu mwaka jana lakini inaaminika kuwa ifikapo katikati ya mwezi Julai watakua wameshatatua tatizo hilo. Wamepata madawati kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy iliyotoa madawati mengi zaidi yaw engine, huu ni mfano wa kuigwa kwa wadau wengine kwani mtoto wa mwenzako ni wako na kila mtoto ana haki ya kusoma katika mazingira rafiki.

Serikali yatenga Tsh. Bilioni 5 kujenga jengo la Mionzi Hospitali ya Rufaa Mbeya.

umi1 
Jonas Kamaleki-Maelezo-Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka 2016/17 zitazotumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la X-Ray katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
Hayo yalisemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi aliyetaka kujua lini jengo la Maabara ya Mionzi linalojengwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya litakamilika.
Ummy alisema katika mwaka wa Fedha 2015/16  Tsh. Bilioni 8 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi huo, ingawa ujenzi huo haukufanyika lakini nia ya Serikali ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo uko pale pale.
Akiainisha matumizi ya pesa zilizotengwa kwa mwaka wa Fedha 2016/17, Ummy alisema Tsh. Bilioni 3 zitatumika kuendeleza ujenzi pamoja na kulipa deni lililobaki kwa mkandarasi aliyekuwa anajenga na bilioni 2 zitatumika kununua vifaa tiba vikiwemo CT- Scanner na MRI.
Akijibu swali la nyongeza toka kwa Mhe. Catherine Majige (Viti Maalum CCM), Mkoa wa Arusha, Ummy alisema bilioni 9 zimetengwa kwa ajili mya kununua vifaa tiba ikiwemo kuweka CT-Scanner na MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa Wizara imepata kibali cha kuajiri wafanyakazi 10,000 wa afya nchini kati ya maombi ya kuajiri wafanyakazi 30,000.
Aliongeza kuwa Serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 kwa ajili ya kuboresha Hospitali za rufaa nchini ikiwemo ya Singida, Sekou Toure ya Mwanza, Mbeya na Arusha.
Ummy alisisitiza kuwa ni nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuboresha sekta ya afya  nchini na kuwafanya wananchi kuwa na afya bora

No comments :

Post a Comment