……………………………….
KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for
Agricultural and Rural Cooperation, CTA) chenye makao makuu mjini
Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa
Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika
Mabara ya Afrika, Karibiani na Pasafiki.

Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora,
CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Taifa,
ameteuliwa kwa kutambua mchango wa juhudi zake katika kukiendeleza
kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Taifa,
ameteuliwa kwa kutambua mchango wa juhudi zake katika kukiendeleza
kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha
katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umhimu wa
kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha kwa
vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki.
Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na
waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.

Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika
kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidia na taasisi hiyo ambayo ni
ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na
Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelijiji.
kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidia na taasisi hiyo ambayo ni
ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na
Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelijiji.
Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya
CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano
tangu 2013 hadi 2018.
CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano
tangu 2013 hadi 2018.
Uchambuzi Wa Habari: Tunafanyaje Na Naibu Spika Tulia Ackson?
Swali hili lilipaswa wajiulize Wabunge wa upinzani wenye kutoka Bungeni kila baada ya dua ya asubuhi.
Kwa kufuatilia kwangu siasa za nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi kwa sasa, naona mkakati huu wa wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.
Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa wapinzani huko tunakokwenda kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi Bungeni.
Unapopanga kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo husika. Kwa sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na mengineyo, wapinzani kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza ingeeleweka kwa wapiga kura.
Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya siku ya kazi za Bunge walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga hisia miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni kukosekana kwa umakini.
Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na hakika nilisikitika moyoni. Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya Watanzania kuwa na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama yale.
Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika nafasi yake na ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang’atuke kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu zetu kimfumo.
Yanapotokea mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni, sheria na taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za kuyabadili hayo ni ndani ya Bunge au Mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge. Na kwa ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku itawalazimu wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo. Tatizo hapa watakuwa wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.
Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio watakaounda Serikali na Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa.
Kama wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu hawatampenda au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu wabunge hao wa CCM kwa wakati huo.
Maggid Mjengwa,
Mhariri Online
Mjengwablog/KwanzaJamii

MONTAGE LIMITED, SERENA NA NMB ZATOA MSAADA KWENYE KITUO CHA MTC BUNJU
Bi. Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited na Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena wakishiriki kazi ya kupaka rangi kwenye jengo linalotumiwa na wanafunzi wa kituo cha mafunzo kwa vijana cha Multpurpose Training Center kilichopo Bunju wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam kwa ajili ya kulia chakula jana, Kampuni za Montage Limited, Serena Hotel na Benki ya NMB ziliungana kwa pamoja na kukipa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo rangi, madaftari, mafuta ya kupaka chakula vifaa vingine katika kituo hicho vyenye thamani ya shilingi milioni tano.
Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena akipaka rangi kwenye ukuta wa jengo hilo huku wafanyakazi wenzake wakimuangalia.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Serena wakishiriki kupaka rangi
Wafanyakzi wa Kampuni ya Montage wakishiriki kupaka rangi katika jengo hilo.
Mratibu wa kituo cha MTC Bw.Issa
Buzohela akielezea jambo wakati ugeni huo ulipotembelea kwenye darasa la
vijana wanaojifunza ufundi seremala kituoni hapo.
Hawa ni wanafunzi wanaojifunza kushona nguo kutuoni hapo wakiendelea na mafunzo.
Ugeni huo ukishuhudia jinsi wanafunzi hao wanavyojifunza kushona nguo.
Kituo hiki pia kinatoa mafunzo ya
kuzima moto na uokoaji haoa wanafunzi wakiwa tayari wamevalia ngua
maalum kwa ajili ya kuokoa mtu aliyenasa kwenye jengo refu linalowaka
moto.
Nguzo hii ya chuma ni mfano wa jengo na mtu aliyenasa yuko juu hivyo wanafanya kazi ya kumuokoa.
Tayari wanamshusha kwa kutumia Machela, kamba, na ngazi kama inyoonekana katika picha
Wanaendelea kushusha chini.
KISHAPU YANUFAIKA NA MRADI WA KUIJENGEA JAMII UWEZO WA KUJIANDAA NA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Hawa Ng’humbi akizungumza na baadhi ya wataalam wa masuala ya maafa walipomtembelea
ofisini kwake ili kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Juni 16, 2016.

Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika
Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison Chinyuka (wa kwanza kulia) akifuatilia mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kujadili utekelezaji wa mradi huo, Wilaya ya Kishapu tarehe 16 Juni, 2016.

Mmoja wa wanachama wa kikundi cha Mazingira Bi. Juliana Peter akichangia hoja wakati wa kikao cha
tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Juni 16, 2016.
tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Juni 16, 2016.
Baadhi ya wanakikundi cha Muungano wakifurahia mafanikio ya kuongezeka kwa mbuzi ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari
za Maafa wakati wa tathimini ya utekelezaji wake iliyofanywa na Idara ya Maafa
Ofisi ya Waziri mkuu tarehe 16 Juni, 2016 Wilaya ya Kishapu Shinyanga.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
SERIKALI MKOANI MBEYA YASITISHA MATUMIZI YA DARAJA LA MBAKA WILAYANI RUNGWE MPAKA LITAKAPO KAMILIKA
Baadhi
ya akinana wakazi wa kijiji cha Mbaka Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
wakikatiza katika ya mto kutokana na Daraja walilokuwa wakitumia kuzuiwa
na serikali ili kupisha ujenzi wake.
|
WAZIRI POSSI AIWAKILISHA VYEMA AFRIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUTOKOMEZA UMASIKINI NA KULETA USAWA KWA WATU WENYE ULEMAVU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe.Dkt.Abdallah Possi akichukua dondoo za Mkutano wa 9 wa nchi ambazo
zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Marekani tarehe 15 Juni, 2016.
zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Marekani tarehe 15 Juni, 2016.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 9 wa nchi ambazo zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu wakifuatilia mada wakati wa
mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa New York Marekani Juni
15, 2016.
mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa New York Marekani Juni
15, 2016.
…………………………………………………………………………………………..
Na.MWANDISHI WETU
Siku ya tarehe 15 Juni, 2016, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (MB),
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu alishiriki katika Mjadala wa
kutokomeza umasikini na kuleta usawa kwa watu wenye ulemavu. Majadiliano hayo
yalikuwa ni moja ya mikutano muhimu iliyolifanyika katika Mkutano wa 9 wa nchi
ambazo zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliofanyika New York,
Marekani.

Mwenyekiti wa majadiliano hayo alikuwa ni Bi. Ellen Maduhu,
Afisa katika ofisi ya uwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Kamati ya Mkutano wa Nchi ambazo zimeridhia
Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (Vice President of the Conference of
State Parties to the Convention on the Rights of Persons of Disabilities)

WAZIRI MKUU, MHE. KASSIM MAJALIWA AWAFUTURISHA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipata futari
iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufanyika
katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwaongoza wabunge kupata futari iliyoandaliwa na Wazri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia Ackson akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa mara
baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu akitoa neon la shukrani kwa Wazri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa mara baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Majaliwa mara baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Mhe. Andrew Chenge akitoa neon la shukrani kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisikiliza neon la shukrni kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia
Ackson mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Ackson mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwashukuru wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mara baada ya kujumuika naye katika futari aliyowaandalia leo na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Muungano wa Tanzania mara baada ya kujumuika naye katika futari aliyowaandalia leo na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
TANZANIA NA SWEDEN ZATILIANA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA MAENDELEO
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya Tanzania na Sweden, kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo Juni 16, 2016
Katibu Mkuu Wizara ra Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa maendeleo wa miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Tasaf Ladislaus Mwamanga (kushoto) wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
Ujumbe wa Sweden ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (Katikati), wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka mine kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka mine kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
Pichana na Benny Mwaipaja
Kaimu Msemaji wa Serikali Wizara ya Fedha na Mipango
…………………………………………………………………………………………………………………
Benny Mwaipaja, WFM-DODOMA
SERIKALI za Tanzania na Sweden
zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka 4 kuanzia mwaka 2016
hadi mwaka 2019 utakaojikita kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya
watu katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, utafiti, nishati jadidifu
na kupambana na umasikini.
Tukio hilo limefanyika leo Juni
16, 2016, mjini Dodoma kati ya Katibu Mkuu na mlipaji Mkuu wa Serikali,
Dkt. Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Naibu Waziri wa
Ushirikiano wa Kimaendeleo wa Sweden, Mhe. Ulrika Modeer.
Dkt. Likwelile ameeleza kuwa
katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2019, Serikali ya
Sweden itatoa ruzuku ya fedha za Kiswidi, SEK 5.5 Biln, sawa na shilingi
Trilioni 1.42 za Kitanzania.
Amesema kuwa kutiwa saini kwa
mkataba wa ushirikiano huo kutafuatiwa na utiwaji saini wa mikataba ya
kifedha ambapo fedha hizo zitaelekezwa katika miradi kadhaa ikiwemo
kusaidia Elimu, Maendeleo ya Jamii-TASAF, Utafiti, Nishati, Demokrasia,
Haki za Binadamu, na Sekta Binafsi.
“Ushirikiano huu umelenga
kusaidia kujenga mazingira ya maendeleo endelevu na kuwapatia Watanzania
maskini fursa za kujikwamua katika umaskini kwa kujipatia ajira na
kuweza kuanzisha biashara za kujipatia kipato ambapo vikundi
vinavyolengwa zaidi ni wanawake, watoto na vijana” Alisema Dkt.
Likwelile
Dkt. Servacius Likwelile ametoa
wito kwa Serikali ya Sweden na nchi nyingine duniani kuwekeza katika
biashara na vitega uchumi ili ziweze kunufaika na rasimali kubwa ambazo
nchi imejaaliwa ikiwemo maliasili, ardhi yenye rutuba na jiografia ya
kimkakati inayochochea uwekezaji na biashara
Kwa upande wake Naibu Waziri wa
Ushirikianno na Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer,
amepongeza uongozi mahili wa Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kupambana na vitendo vya kifisadi ikiwemo rushwa.
“Sweden inaunga mkono kwa nguvu
zote hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli kupambana na mauvu nchini na
tunaamini nchi itapiga hatua kubwa kimaendeleo” Alisistiza Modeer.
Mhe. Ulrika Modeer ameahidi kuwa
serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa fedha
kupitia mfuko mkuu wa Bajeti ili kuwezesha kufanikisha miradi mbalimbali
ya maendeleo inayogusa hifadhi ya mazingira, kilimo endelevu,
kuwawezesha wananawake kiuchumi na kumsaidia mtoto wa kike na kiume
kielimu.
“Tunataka kuona kuwa maendeleo ya
nchi yanakwenda sambamba na maendeleo ya wananchi wake ambapo tunaamini
kuwa utafiti utasaidia kupata njia bora za kupambana na
umasikini”Alisisitiza Mhe. Modeer
Amesema kuwa pamoja na nchi yake
kutaka kuyasaidia makundi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu,
wanataka kuona suala la demokrasia na utawala bora vinapewa kipaumbele
katika mipango mbalimbali ya maendeleo
“Vilevile uwekezaji wetu mkubwa
wa fedha katika maendeleo ya Taifa hautakuwa na maana sana kama suala la
hifadhi ya mazingira halitapewa kipaumbele kwa kuanzisha miradi ya
nishati jadidifu “Renewable energy” ili kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi: aliongeza Mhe. Ulrika Modeer
Uhusiano wa Tanzania na Sweden
umedumu tangu mwaka 1960 ambapo katika kipindi chote cha miaka 50,
serikali hizi mbili zimeshirikiana katika kubuni na kutekeleza miradi
kadhaa ya maendeleo
Programu na miradi
itakayotekelezwa katika ushirikiano uliosainiwa leo unaendena pia na
Mpango wa Taifa wa Pili wa Miaka Mitano unaoanzia mwaka 2016/17 hadi
2020/21 na unalenga kuondoa utegemezi wa misaada kwa Tanzania.
PROF MBARAWA ATETA NA BODI MPYA BANDARI
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mh. Profesa Makame Mbarawa hayupo pichani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kuanza kazi mara moja kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo hapa nchini.
Akizungumza na bodi hiyo kupitia
Teknolojia ya Video (Video Conference) toka mjini Dodoma Prof. Mbarawa
ameitaka bodi hiyo kufahamu kuwa miundombinu ya banadri nchini iko
katika hali duni, isiyo uwiana na malengo ya Serikali ya kuwa na bandari
itakayoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
“Kazi yenu kubwa ya kwanza ni
kurudisha uadilifu na ufanyakazi wa uzalendo na unaozingatia weledi kwa
watumishi wote wa bandari nchini”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amesema TPA inakabiliwa na
changamoto nyingi zikiwemo watu kuajiriana kindugu, utendaji
usiozingatia matokeo, mifumo mibovu ya ukusanyaji mapato, baadhi ya
watendaji kuwa na maslahi binafsi katika kampuni zinazofanya kazi
bandarini na utendaji dhaifu wa matumizi ya mifumo ya elektoniki hali
inayosababisha utendaji usio na ufanisi.
Aidha Prof. Mbarawa amezungumzia
umuhimu wa bodi hiyo kuangalia upya muundo wa bodi ya zabuni ya bandari
na namna kampuni zinazopewa zabuni zinavyopatikana ili kuondoa
manung’uniko na mikwamo katika utekelezaji wa miradi.
“Hakikisheni mnaweka watu
waadilifu, wasio na maslahi binafsi katika bodi za zabuni ili kuiwezesha
bandari kushindana na bandari za nchi nyingine na hivyo kuvutia
wasafirishaji wengi hali itakayoongeza mapato ya bandari na kukuza
uchumi wa nchi”,
amesisitiza Prof. Mbarawa.
amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya
wa Bodi ya TPA Prof. Ignas Rubaratuka amemhakikishia Waziri Prof.
Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga kubadili changamoto zote za bandari
nchini kuwa fursa na kazi hiyo itafanywa kwa weledi na kwa muda mfupi.
Amesema watahakikisha kuwa
malalamiko yanayotokana na bandari yanashughulikiwa kwa weledi na kwa
kufuata sheria ili haki itendeke na kuiwezesha bandari kuwa na hadhi
inayostahili.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard
Chamuriho ameitaka bodi hiyo kujifunza majukumu yake kwa haraka na
kutenda kazi kwa mujibu wa sheria.
MICHUANO YA COPA AMERICA YAFIKIA ROBO FAINALI
Na Mwandishi Wetu
MICHUANO
ya Copa America inayoonekana moja kwa moja kupitia visimbuzi vya
StarTimes Tanzania imefikia hatua ya robo fainali ambayo itaanza kutimua
vumbi kesho Juni 16 mpaka 19.
Timu
zilizotinga hatua hiyo ni Argentina, Chile, Mexico, Marekani,
Venezuela, Peru, Colombia na Ecuador huku mashabiki wa soka wakishuhudia
miamba ya soka ya timu za Brazil na Uruguay wenye nyota lukuki kama
vile Luis Suarez, Edinson Cavani, Willian, Countinho na wengineo
wakishindwa kuzisaidia timu zao.
Katika
michuano hii ya kusisimua kikosi cha timu ya taifa cha Argentina
kikiongozwa na mchezaji bora wa dunia mara tano, Lionel Messi, ambacho
kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kimeingia kwa kishindo hatua
ya robo fainali baada kushinda michezo yote mitatu na kuongoza kundi D
kwa alama tisa.
Kupitia
chaneli za Sports Focus na World Football wateja na watanzania
wanatazama michezo yote moja kwa moja huku wakiwa na nafasi ya kusinda
zawadi mbalimbali kama vile vifurushi vya bure pamoja na pesa taslimu na
safari kwenda Ujerumani kutazama mechi za Bundesliga za msimu ujao
unaotarajiwa kuanza mwezi wa nane.
Akitoa
ufafanuzi juu ya michuano hiyo Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania,
Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa, “Mbali na kufurahia matangazo ya moja kwa
moja ya mechi zinazochezwa nchini Marekani pia tuna kampeni
inayoendelea ya ‘Tabiri na Ushinde’ inayoenedelea kupitia mitandao yetu
ya facebook na instagram. Kupitia kampeni hiyo mteja anaebashiri kwa
usahihi matokeo ya mechi ya siku husika hupata fursa ya kujishindia
kifurushi cha Mambo pamoja na cha michezo cha Sports Plus cha jumla ya
shilingi 36,000/-.”
“Mbali
na hapo pia kuna zawadi zingine zinazotokana na kampeni ya hashtag ya
#CopaAmericaonStarTimes kupitia mitandao yetu pia. Mshindi wa kampeni
hii hupatikana kwa kushea mara nyingi zaidi post atakayoiona kuwekwa na
kurasa za StarTimes na kufikia watu wengi zaidi. Mshindi wa kwanza wa
kampeni atapatiwa tiketi VIP ya kwenda ya kwenda Ujerumani kutazama
mechi za Bundesliga msimu ujao pamoja na dola za Kimarekani 1500/-, huku
wa pili na wa tatu watapatiwa simu za mkononi za kisasa aina ya Solar
5. Tumefanya hivi ili kuwazawadia wateja wetu waaminifu na wanaofuatilia
huduma zetu ili kunogesha zaidi shamra shamra za kombe la Copa
America.” Alimalizia Bi. Hanif
Hatua ya robo fainali itakayoanza kupigwa kesho itazijumuisha timu zote zilizoshika nafasi ya pili katika makundi yao.
Wapenzi
wa soka ulimwenguni wanazidi kusononeshwa na mwenedo mbovu wa kikosi
cha taifa cha Brazil ambacho kimeshindwa kutinga hatua hiyo kwa
kufanikiwa kushinda mechi moja tu kati ya tatu. Matokea hayo mabovu
yamepelekea kocha wa taifa timu hiyo Dunga kutimuliwa kazi.
Timu
na ratiba kwa timu zitakazopambana ni pamoja na Marekani na Ecuador
(Juni 16), Peru na Colombia (Juni 17), na mechi za mwisho ni Argentina
na Venezuela; Mexico na Chile (Juni 18). Timu zitakazopita hatua hii
zitakutana katika hatua ya nusu fainali siku ya Juni 21.
MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KESHO KWENYE SHEREHE ZA SIKU YA WAHITIMU WA CHUO CHA MZUMBE
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe mara baada ya
kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa
chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Manisapaa ya Morogoro mjini Ndugu
Fikiri Juma mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria
sherehe ya siku wahitimuwa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa chuo cha Mzumbe mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 YAANZA RASMI
Baadhi ya wateja waliofika kuhudumiwa siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016. Anayeelekeza (katikati) ni Afisa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bi. Rehema Msemo.
Wateja wakihudumiwa katika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni Siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YAKABIDHI MADAWATI 800 KWA WILAYA YA KILWA
Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akifafanua jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati kwaajili ya watoto wa shule za msingi wilayani Kilwa
Baadhi ya madawati yaliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy
Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilay ya Kilwa Juma A. Njwayo madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani mwake. Wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Kilwa, viongozi kutoka PanAfrican Energy na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Masoko katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kilwa Masoko.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma Abdallah Njwayo akiwaasa wanafunzi wa shule ya Msingi Masoko ambao ni moja ya wanufaikaji wa madawati 800 kutoka PanAfrican Energy kuyatunza madawati waliyopewa na kusoma kwa bidii.
Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akitoa neno wakati akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma A. Njwayo madawati 800 yatakayosaidia watoto 2400 na kupunguza tatizo la uhaba wa madawati.

………………………………………………………………………………………………
PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YATOA MADAWATI 800 KWA WILAYA YA KILWA
PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YATOA MADAWATI 800 KWA WILAYA YA KILWA
Kapuni ya uchimbaji gesi asilia PanAfrican Energy jana imekabidhi madawati 800 kwa ajili ya shule za msingi wilayani Kilwa yenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 104. Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Masoko iliyopo wilayani humo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni hiyo, huku ikishuhudiwa na wana habari, viongozi mbali mbali wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Juma Njwayo, walimu, wanafunzi na wananchi wa Kilwa Masoko. Msaada huo wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Msingi ni kuunga mkono Kampeni ya uchangiaji madawati iliyoanzishwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.Akiongea wakati akipokea madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma Njwayo, ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla hiyo aliwashukuru sana Kampuni ya PanAfrican Energy kwa msaada wao mkubwa wanaotoa kwa wilaya ya Kilwa.
“Kwa
niaba ya wana Kilwa naomba kutoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa
PanAfrican Energy kwa siku zote kutuangalia kwa jicho la tatu kwa mmekua
mkijitoa kawa hali na mali kuwezesha huduma mbali mbali katika Wilaya
yangu Ya Kilwa. Leo napokea madawati 800 ambayo yatasaidia kupunguza
uhaba wa madawati mashuleni kwani yatasaidia watoto 2400 kutokukaa
chini, hili si jambo dogo kabisa hivyo mnahitaji pongezi.
Natoa
wito kwa wadau wengine kuiga mfano huu walionesha PanAfrican Energy
kwani bado tuna uhaba wa madawati katika shule zetu za msingi hapa
Kilwa. Hapa katika Shule ya Msingi Masoko watapata madawati 145 ambayo
yapo mbele yetu hapa na mengine 655 yaliyobakia yatagawiwa kwa shule
zingine zenye uhaba huo. Tunategemea ifikapo katikati ya mwezi Julai
tutakua tumemaliza tatizo la madawati katika shule za msingi wilayani
humu. Pia alitoa wito kwa wanafunzi kutunza madawati hayo ili yaweze
kunufaisha wanafunzi wengi zaidi.”“Mbali
na kupata madawati pia tunawapongeza kwa kuwa na uzalendo na wilaya
yetu kwani hata mzabuni aliyepata kazi ya kutengeneza madawati haya ni
mwananchi wa Kilwa ambapo vijana kadhaa wamepata ajira kupitia kazi hiyo
na kuongeza kipato chao.
Ukiachilia
mbali swala la elimu Kampuni hii imekua mstari wa mbele katika swala la
afya pia ambapo katika kuupunguza vifo vya kina mama na watoto
wanatujengea jengo la Mama Ngojea katika hospitali yetu ya Wilaya ambako
kabla yam waka huu kuisha tutakua tumeshakabidhiwa jengo hilo pia
wanakarabati kituo cha afya cha Kilwa Masoko.” Aliongeza Mh. Njwayo.Naye
Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za jamii wa Kampuni ya Uchimbaji wa
Gesi ya PanAfrican Energy Andrew Kashangaki alisema, “Ni furaha yetu
kuona watoto wa kitanzania wanasoma kwa Amani bila kuwa na matatizo
yeyote na ndomana tumesukumwa kuunga mkono sekta ya elimu nchini kwa
kuanza na wilaya ya Kilwa.
Leo
tunakabidhi madawati 800 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa yatakayosaidia
kupunguza tatizo la watoto wetu kukaa chini na wadawati haya
yatagawanywa kwa shule za msingi mbalimbali kutokana na uhitaji wao.
Sisi kama wadau wa Elimu tumefanya kile tulichoweza kufanya hivyo
tunaamini kwa madawati haya tunawawezesha watoto wa kitanzania
watakaosomea katika shule hizo kutoa ujinga na tunatengeneza Taifa la
wasomi.Aliongeza kwa kusema kuwa,
“Tayari tuna programu ya kusomesha watoto kutoka kisiwa cha Songosongo
ambako kila mwaka tunasomesha watoto 28, tumejenga mabweni kwaajili ya
watoto wa kike kisiwani songosongo, pia ujenzi wa maabara za kisasa kwa
ajili ya masomo ya sayansi kwa shule za Sekondari hiyo yote ni
kuhakikisha tunaweka mazingira mazuri ya kusomea kwa watoto wetu.”
Wilaya ya Kilwa ilikua ina uhaba mkubwa wa madawati tangu
mwaka jana lakini inaaminika kuwa ifikapo katikati ya mwezi Julai
watakua wameshatatua tatizo hilo. Wamepata madawati kutoka kwa wadau
mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy
iliyotoa madawati mengi zaidi yaw engine, huu ni mfano wa kuigwa kwa
wadau wengine kwani mtoto wa mwenzako ni wako na kila mtoto ana haki ya
kusoma katika mazingira rafiki.
Serikali yatenga Tsh. Bilioni 5 kujenga jengo la Mionzi Hospitali ya Rufaa Mbeya.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka 2016/17 zitazotumika kwa
ajili ya ujenzi wa jengo la X-Ray katika hospitali ya Rufaa mkoani
Mbeya.
Hayo
yalisemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa
Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi aliyetaka kujua lini jengo la Maabara
ya Mionzi linalojengwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya litakamilika.
Ummy alisema
katika mwaka wa Fedha 2015/16 Tsh. Bilioni 8 zilitengwa kwa ajili ya
ujenzi huo, ingawa ujenzi huo haukufanyika lakini nia ya Serikali ya
kukamilisha ujenzi wa jengo hilo uko pale pale.
Akiainisha
matumizi ya pesa zilizotengwa kwa mwaka wa Fedha 2016/17, Ummy alisema
Tsh. Bilioni 3 zitatumika kuendeleza ujenzi pamoja na kulipa deni
lililobaki kwa mkandarasi aliyekuwa anajenga na bilioni 2 zitatumika
kununua vifaa tiba vikiwemo CT- Scanner na MRI.
Akijibu
swali la nyongeza toka kwa Mhe. Catherine Majige (Viti Maalum CCM), Mkoa
wa Arusha, Ummy alisema bilioni 9 zimetengwa kwa ajili mya kununua
vifaa tiba ikiwemo kuweka CT-Scanner na MRI katika Hospitali ya Rufaa ya
Mount Meru.
Aidha Waziri
Ummy alisema kuwa Wizara imepata kibali cha kuajiri wafanyakazi 10,000
wa afya nchini kati ya maombi ya kuajiri wafanyakazi 30,000.
Aliongeza
kuwa Serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 kwa ajili ya
kuboresha Hospitali za rufaa nchini ikiwemo ya Singida, Sekou Toure ya
Mwanza, Mbeya na Arusha.
No comments:
Post a Comment