Kampuni ya Tigo Tanzania imeshiriki katika kumbukumbu ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2016 kwa kuchangia zaidi ya shilingi 26.4m/-($12,000) kwa asasi isiyo ya kiserikali ya C-Sema ambayo inaendesha kituo cha kupokelea simu cha Huduma ya Simu kwa Mtoto (Child Helpline Call Centre) mjini Zanzibar ambacho kinatoa ushauri na kuwaunganisha watoto kupata huduma sahihi za kijamii kikishirikiana na serikali.
Tigo na asasi ya C-Sema watafanya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu katika Kituo cha Michezo cha JMK Park jijini Dar es Salaam Alhamisi Juni 16. Siku ya Mtoto wa Afrika ni tukio linalofanyika duniani kote kila Juni 16 ya kila mwaka.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja wa Huduma za Jamii wa Tigo, Woinde Shisael alisema msaada huo ni sehemu ya mkakati wa kampuni wa kuwekeza katika ajenda ya kumlinda mtoto iwe kwa njia ya mtandao na hata nje ya mtandao.
Akitoa shukrani kutokana na msaada, huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa C-Sema, Kiiya JK aliishukuru kampuni hiyo ya simu kwa kutoa mchango sahihi katika kuwekeza rasilimali zake ili kuhakikisha kwamba watoto na wazazi wanakuwa na uhakika wa kupata jukwaa ambalo wanaweza kutoa taarifa kuhusu aina yoyote ya ukatili dhidi yao.
“Ninaishukuru Tigo kwa msaada huu wakati leo tunasherehekea watoto wa Afrika kwa kuzisikiliza sauti zao wakati wakitueleza kile wanachokifikiria kuhusu masuala mbalimbali yanayowasibu na nini kitu gani kifanyike kutokomeza matendo mabaya ambayo yanaweza kukwamisha maendeleo yao.”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la mwaka huu la Siku ya Mtoto wa Afrika.
Kituo cha taifa cha kupokelea simu za huduma ya simu kwa mtoto (Child Helpline call centre) kilianzishwa rasmi Juni 15, 2013 kikiwa na kituo cha Dar es Salaam na Zanzibar.
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YAELEZA HALI YA ULINZI NA USALAMA KWA MTOTO WA TANZANIA
Mkurugenzi
wa Haki za Binadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.
Francis Nzuki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
Mapendekezo ya Tume hiyo kwa Serikali na Jamii katika kuhakikisha Ulinzi
na Usalama kwa Mtoto unaimarika. Katikati ni Kamishna wa Tume hiyo Bi.
Salma Ali Hassan.
Kamishna
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Salma Ali Hassan
akiongea na waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu hali ya mtoto wa
Tanzania na mazingira hatarishi wanayokutana nayo ikiwemo ubakaji,
ulawiti na unyanyasaji wa kijinsia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Haki za
Binadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Francis
Nzuki
MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO
Wabunge
wa Upinzani wakitoka Bungeni baada ya dua kusomwa na Naibu Spika Dkt.
Tulia Ackson Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wageni
waliofika Bungeni mjini Dodoma kujionea shughuli mbalimbali za bunge
wakifuatilia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Juni 16, 2016. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Nkansi Kaskazini, Ally
Kessy bungeni mjini Dodoma Juni16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa zamani wa Singida mjini ,
Mohammed Dewji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 16, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Singida
mjini , Mohammed Dewji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 16,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mwibara, Kange Lugola
kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 16, 2016. (Picha na ofisi ya
Waziri Mkuu)
Watanzania watakiwa kutumia fursa za soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO,
WAFANYABIASHARA wa Tanzania
wametakiwa kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko la nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuuza bidhaa zao ndani ya
Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari.
“Wafanyabiashara wanatakiwa
kuchangamkia fursa ya biashara katika soko la pamoja kwa kuwa ni haki
yao na ni utekelezaji wa malengo ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki kifungu cha tano ambapo ilianzishwa itifaki ya umoja
wa forodha ” ,alisema Bi. Mindi
Wafanyabiashara hao pamoja na
wasafirishaji wanaotaka kufanya biashara katika soko la Jumuiya hiyo
watatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati wakiingia nchi
wananchama wa Jumuiya hasa kwa wafanyabiashara wadogo wenye bidhaa
zisizozidi dola za kimarekani 2000, ambapo hawalazimiki kuwa na wakala
wa forodha.
Wanatakiwa kufuata utaratibu kwa
kufika katika kituo chochote cha forodha kilichopo mpakani wakiwa na
bidhaa zao ili wapewe cheti cha uasilia wa bidhaa.
Naye, Mkurugenzi wa Biashara,
Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, katika Wizara hiyo, Bw. Geofrey
Mwambe, amesema ni vyema wafanyabiashara wakatoa taarifa endapo
watakumbana na vikwazo visivyo vya kiforodha kupitia mfumo wa ujumbe
mfupi kwa kuandika neno ‘NTB’ kwenda namba 15539.
Bw. Mwambe amesema pia ,madereva
wanaosafirisha mizigo kwenda nchi wanachama watakapokutana na vikwazo
visivyo vya kiforodha barabarani watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi
kupitia namba 0713631780.
Kwa mujibu wa Mkataba wa
uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu namba 5 ambapo
Jukuiya ilianzisha Itifaki ya Umoja wa Forodha (East African Community
Customs Union) wafanyabiashara wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo wana
fursa za kufanya biashara kwa kuuza bidhaa zao ndani ya nchiwanachama
wa Jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi
bila kutozwa ushuru wa forodha ilimradi bidhaa zao zimezingatia vigezo
na kufuata utaratibu ulioainishwa katika itifaki hiyo.
Japokuwa Sudani ya Kusini
imeridhia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki bado fursa za kufanya
biashara nchini humo hazijakamilika.
WAZIRI MKUU: KILA MKOA UUNDE KAMATI YA AMANI
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari aliyoiandaa kwenye
makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa
mkoa wa Dodoma, Alhaj Adam Kimbisa na Wapili kushoto ni Kaimu Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ahmed Said.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na mazingira, January Makamba.(Picha na ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, John
Malecela katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni
16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ulanga, Goodluck
Mlinga katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni
15, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika futari aliyoianda
kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge Dkt.
Tulia Ackson katika fuatari aliyondaa kwenye makazi kake mjini Dodoma
Juni 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema kila mkoa unatakiwa kuunda Kamati ya Amani kama njia ya
kudumisha amani na utulivu kwenye mikoa yote nchini.
Waziri Mkuu ametoa wito huo jana
usiku (Jumatano, Juni 15, 2016) wakati akizungumza na viongozi wa dini
wa mkoa wa Dodoma na baadhi ya wazee maarufu wa mkoa huo aliowaalika
kwenye futari katika makazi yake mjini Dodoma.
Amesema anatambua kuwa mkoa wa
Dodoma uko shwari kwa sababu ya mshikamano uliopo baina viongozi wa dini
za Kiislamu na Kikristo. “Nimegundua kuwa siri kubwa ya mkoa wa Dodoma
kuwa na utulivu ni kuwepo kwa kamati ya amani yenye viongozi mahiri,
kwani sote tunatambua kuwa kazi ya viongozi wa dini ni kuwaimarisha watu
kiroho,” alisema.
Waziri Mkuu alisema ziko nchi
zinatamani kuwa kama Tanzania kwa sababu wao hawana uhakika wa kulala na
kuamka salama asubuhi. “Pamoja na yote sisi tuna uhakika wa asilimia 99
kulala usiku na kuamka salama asubuhi, kwa sababu ya amani iliyopo,”
alisema.
Hadi sasa mikoa ambayo
imekwishaunda kamati za amani ni Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Dodoma,
Arusha, Lindi, Mtwara, Tanga na Mbeya.
Akigusia suala la mauaji ya hivi
karibuni, Waziri Mkuu alisema anawaomba Watanzania kila mmoja kwa imani
yake akemee kwa nguvu matendo hayo kwa sababu yeye haamini kama
yamefanywa na Watanzania ambao wamelelewa kwenye misingi ya dini.
“Siamini kama kuna mtoto
aliyelelewa kwenye misingi ya Uislamu anaweza kuingia msikitini na
kuwaua wenzake wakati wakimwomba Mungu. Na wala siamini kama kuna mtoto
aliyelelewa na kukuzwa Kikristo anaweza kuingia kwenye nyumba ya ibada
akakuta watu wanasali na kuamua kuwaua. Ninawaomba tukemee kwa nguvu
zote tabia hii,” alisisitiza.
Aliwataka watanzania wote wawe na
walinzi wa wenzao kwa sababu kila mmoja ana jukumu la kumlinda
mwenzake. “Tusiachie majeshi kazi hii kwa sababu kila mmoja na jukumu la
kwanza kujilinda yeye mwenyewe na kisha kumlinda jirani yake,” alisema.
Kwa upande wake, Kaimu Sheikh wa
Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmed Said alisema wanawaombea dua Mheshimiwa
Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu katika kazi za kuleta maendeleo kwa
Watanzania. “Pia tutaendelea kuiombea nchi yetu ili Mwenyezi Mungu
azidishe amani yake na watu wake waishi kwa amani, upendo na utulivu,”
aliongeza.
Naye Waziri Mkuu mstaafu, Dk.
John S. Malecela ambaye alikuwa miongoni mwa wazee maarufu walioalikwa
kwenye futari hiyo aliwataka waalikwa wenzake waendelee kuwaombea
viongozi wa kitaifa na kusisitiza kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuombea
amani ya Tanzania ambayo imedumu kwa miaka mingi iendelee kuwepo.
Katika hatua nyingine, Askofu wa
Kanisa la Mennonite Tanzania Dayosisi ya Kati, Askofu Amos Muhagachi,
ambaye alipewa fursa ya kutoa salamu fupi kwenye hafla hiyo, alisema
kwenye mkoa huo hakuna magomvi ya kidini kwa sababu viongozi wa dini
zote wanashirikiana kwa karibu sana.
“Hapa Dodoma Maaskofu
tunashirikiana vizuri na Masheikh. Hivi sasa, masheikh vijana na
wachungaji vijana wameanza kuiga haya tunayofanya, na zaidi ya yote
tunashirikiana pia kuwaombea Rais wetu, Makamu wa Rais pamoja na wewe
Mheshimiwa Waziri Mkuu,” alisema
TANZANIA MWENYEJI MAADHIMISHO YA 6 WIKI YA MAJI BARANI AFRIKA
Mkurugenzi
Msaidizi Maji Shirikishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw.
Sylivester Matemu akiongea na waandishi (hayupo pichani) kuhusu
Maadhimisho ya 6 ya Wiki ya Maji Barani Afrika na Mkutano wa 10 wa
Baraza la Mawaziri wa Maji wa Nchi za Afrika utakaofanyika kuanzia
tarehe 18-22 Julai 2016. Kulia ni Afisa Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw.
Dennis Kiilu.
…………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi- Maelezo
Tanzania Mwenyeji maadhimisho ya 6
ya wiki ya Maji Barani Afrika na Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa
Maji wa Nchi za Afrika yatakayofanyika Julai,2016 Jijini Dar es
salaam.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkurugenzi Msaidizi Maji Shirikishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Bw. Sylivester Matemu wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo
jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa
Maonyesho ya Wiki ya maji yatakayofanyika kabla ya mkutano wa Baraza la
Mawaziri atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Akifafanua Matemu amesema kuwa
mkutano huo utahusisha washiriki zaidi ya 1000 kutoka mataifa 54 kutoka
Bara la Afrika na wengine kutoka nje ya Afrika.
Maadhimisho hayo yataambatana na
maonyesho ya shughuli za wadau wa sekta ya maji na umwagiliaji, kwenye
Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.
Kauli mbiu ya kongomanao hilo ni “
Kufikia lengo la maendeleo Endelevu Juu ya usalama wa Maji na usafi wa
mazingira” alibainisha Matemu.
Mkutano huo utawasaidia wataalamu
wa maji kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika kujadiliana kuhusu
mikakati mbalimbali itakayosaidia kupambana na changamoto zinazoikabili
sekta ya maji katika bara la Afrika.
Akizungumzia faida za Mkutano huo
Matemu amesema kuwa utasaidia kufungua fursa mbalimbali zilizopo
katika sekta ya maji na Sekta nyingine ikiwemo kukuza na Kutangaza
vivutio vilivyopo hapa nchini hali itakayosaidia kukuza Utalii.
MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAKULIMA (AFP) AZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI JUU YA HUJUMA ALIYOFANYIWA
Mhariri
Mkuu Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhan Ali akimkaribisha
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) ambae pia ni Waziri wa SMZ asie
na Wizara Maalum Saidi Sudi azungumze na Waandishi wa Habari katika
ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wakulima (AFP) Saidi Sudi akizungumza na waandishi wa
Habari hawapo (pichani) kuhusiana na kadhia ya kukatwa mikarafuu, minazi
na mihogo katika shamba lake lenye urefu wa eka moja na nusu huko
Pemba.
Baadhi
ya wandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima
(AFP) Saidi Sudi hayo pichani katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini
Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MWANZA
MNAMO
TAREHE 15.06.2016 MAJIRA YA SAA 14:20HRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA
BUHAMA TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, NDIMILA
LUPOGOSHA MIAKA 30 MVUVI NA MKAZI WA KIJIJI CHA BUHAMA ALIUAWA KWA
KUPIGWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA SHINGONI NA MKEWE AITWAYE
MARTHA MAGUGU MIAKA 40 PINDI WALIPOKUWA WAKINYWA POMBE KATIKA GROCERY YA
MAMA ALI ILIYOPO KATIKA KIJIJI HICHO.
INADAIWA KUWA TAREHE 14.06.2016
MAJIARA YA SAA 23:00HRS USIKU WAKATI WAKINYWA POMBE KATIKA GROCERY TAJWA
HAPO JUU, MKE WA MAREHEMU BI MARTHA ALIMUONA MUMEWE AKIONGEA NA
MWANAMKE MWINGINE KITENDO AMBACHO HAKIKUMFURAHISHA NA KUAMUA KUMPIGA NA
KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA SHINGONI HALI ILIYOPELEKEA KUTOKWA NA
DAMU NYINGI KICHWANI NA KUFARIKI DUNIA SIKU YA JANA YA TAREHE 15.06.2016
MAJIRA YA SAA 14:20HRS MCHANA WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALI, NA BAADA YA
KIFO NDUGU WA MAREHEMU NDIPO WALIPOTOA TAARIFA POLISI.
CHANZO CHA MAUAJI INADAIWA KUWA
WIVU WA KIMAPENZI NA MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO AMEKAMATWA YUPO CHINI YA
ULINZI WA JESHI LA POLISI, HUKU MAHOJIANO DHIDI YA TUHUMA ZA MAUAJI
ANAYODAIWA KUTENDA YAKIENDELEA. PINDI UCHUNGUZI PAMOJA NA UPELELEZI
KUHUSIANA NA TUKIO HILO UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI ,
MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA
KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WANANCHI AKIWATAKA KUWA MAKINI WAKATI WOTE NA MAAMUZI WANAYOYACHUKUA
PINDI WANAPOKUWA KATIKA UGOMVI ILI KUWEZA KUZUIA MAJERAHA NA VIFO
VINAVYOWEZA KUEPUKIKA, KWANI KUJERUHI AU KUUA NI KOSA LA JINAI HIVYO
JESHI LA POLISI LITAMSHUHULIKIA MHUSIKA NA KUHAKIKISHA ANAFIKISHWA
KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KUJIBU TUHUMA ZITAKAZO MKABALI.
Mkurugenzi Kinondoni amewataka walipa kodi na ushuru kupewa stakabadhi za kielektroniki
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondoni amewataka walipa kodi na ushuru katika Manispaa hiyo kudai
stakabadhi za kielektroniki baada ya kufanya malipo ili kuziba mianya ya
upotevu wa mapato.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli alipokuwa
akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya njia wanazozitumia katika
ukusanyaji wa ushuru wa Manispaa hiyo.
“Napenda kuwasisitiza wananchi
kuwa unapofanya malipo yoyote ya Manispaa lazima uhakikishe unapewa
stakabadhi ya kielekroniki na iwapo hutopewa, unaruhusiwa kutoa taarifa
kwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda 0767643460 na utapatiwa maelekezo ya nini cha kufanya”,alisema Kagurumjuli.
Kagurumjuli ameongeza kuwa Ofisa
yeyote atakayekaidi kutoa stakabadhi hizo atachukuliwa hatua kali za
kisheria kwani kukwepa kulipa mapato ni kurudisha nyuma uchumi wa nchi.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameyataja
maeneo ambayo mwananchi anaweza kulipia kodi au ushuru na kupata
stakabadhi za kielekroniki ni Ofisi za Manispaa, Ofisi za Kata, Benki ya
CRDB pamoja na watumishi wa Manispaa waliopo katika shughuli maalumu za
ufuatiliaji wa kodi na ushuru.
Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni ilianza kutumia mfumo wa kulipa kodi na ushuru kwa njia ya
kielekroniki mnamo mwaka 2013 , na mwaka 2015 ilipata tuzo ya ukusanyaji
bora wa mapato kwa njia hiyo kwa Tanzania na Afrika nzima.
WENGI WAJIUNGA NA NSSF JIJINI MWANZA
Ofisa
Uandikishaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kwandu
Ikombe (kushoto), akiwaandikisha wanachama wapya wa NSSF katika eneo la
Tanganyika Bus mjini Mwanza. (Na Mpigapicha Wetu)
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango akigawa vipeperushi vyenye taarifa kuhusu NSSF wakati wa zoezi maalum la utoaji elimu kwa umma kuhusu mafao na huduma mbalimbali za NSSF .
Ofisa
Masoko Mwandamiza wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amina
Mmbaga akitoa elimu kuhusu NSSF kwa wanawake wajasiriamali wa kuuza
viatu katika eneo la Tanganyika jijini Mwanza.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna
Nguzo akitoa elimu kuhusu NSSF wakati wa zoezi maalum la utoaji elimu kwa umma kuhusu mafao na huduma mbalimbali za NSSF.
Nguzo akitoa elimu kuhusu NSSF wakati wa zoezi maalum la utoaji elimu kwa umma kuhusu mafao na huduma mbalimbali za NSSF.
KAMATI YA MAWASILIANO MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Mkoa wa Mwanza, Jonathan Abdallah Kasibu, akizungumza katika Semina
kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwanza.
……………………………………………………………………………………………..
Katika semina hiyo, watumiaji wa hudumza za mawasiliano ikiwemo simu pamoja na vyombo vya habari ambao waliwakilisha makundi mbalimbali kama vile wanahabari, wajasiriamali na walemavu, walipewa elimu juu ya uwepo wa Kamati hiyo pamoja na uwepo wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC).
Pia walielimishwa juu ya mwongozo wa kuwasilisha malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za mawasiliano pamoja na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015.
Semina hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC) ambapo iliambatana na viongozi wa Kamati ya Mawasiliano mkoani Mwanza kujitambulisha kwa baraza hilo.
Watumiaji wa huduma za mawasiliano walielezwa kwamba ni wajibu wao kuwasilisha malalamiko yao ikiwa
wanapokea huduma zilizo chini ya kiwango ama ikiwa wana malalamiko ya aina yoyote kuhusu huduma za mawasiliano.
Walihimizwa kuwasilisha malalamiko yao kwa kuanza na mtoa huduma, yasiposhughulikiwa wanawayawasilisha
katika Kamati ya Huduma za Mawasiliano mkoa, yasipotatuliwa yatawasilishwa katika Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka TCRA na hata ngazi nyingine zaidi hadi pale utatuzi utakapofanyika.
Semina hiyo ilionekana kuwafungua ufahamu watumiaji wa huduma za mawasiliano jijini Mwanza kwani
baadhi yao walieleza kuwa awali walikuwa hawatambui haki na wajibu wao katika kutumia huduma za mawasiliano.
Baadhi ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza, wakiwa katika semina yakwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwanza.
……………………………………………………………………………………………..
Katika semina hiyo, watumiaji wa hudumza za mawasiliano ikiwemo simu pamoja na vyombo vya habari ambao waliwakilisha makundi mbalimbali kama vile wanahabari, wajasiriamali na walemavu, walipewa elimu juu ya uwepo wa Kamati hiyo pamoja na uwepo wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC).
Pia walielimishwa juu ya mwongozo wa kuwasilisha malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za mawasiliano pamoja na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015.
Semina hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC) ambapo iliambatana na viongozi wa Kamati ya Mawasiliano mkoani Mwanza kujitambulisha kwa baraza hilo.
Watumiaji wa huduma za mawasiliano walielezwa kwamba ni wajibu wao kuwasilisha malalamiko yao ikiwa
wanapokea huduma zilizo chini ya kiwango ama ikiwa wana malalamiko ya aina yoyote kuhusu huduma za mawasiliano.
Walihimizwa kuwasilisha malalamiko yao kwa kuanza na mtoa huduma, yasiposhughulikiwa wanawayawasilisha
katika Kamati ya Huduma za Mawasiliano mkoa, yasipotatuliwa yatawasilishwa katika Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka TCRA na hata ngazi nyingine zaidi hadi pale utatuzi utakapofanyika.
Semina hiyo ilionekana kuwafungua ufahamu watumiaji wa huduma za mawasiliano jijini Mwanza kwani
baadhi yao walieleza kuwa awali walikuwa hawatambui haki na wajibu wao katika kutumia huduma za mawasiliano.
kuwaelimisha juu ya Matumizi ya Huduma za Mawasiliano
No comments:
Post a Comment