Monday, June 27, 2016

Bunge limepitisha muswada wa marekebisho ya Sheria ya Elimu

B3Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akijibu hoja za Wabunge mapema leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja kuhusu muswaada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wamwaka 2016.
———————————————-
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria ya Elimu kifungu kinachoeleza kuwa mtu anayempatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuwa adhabu yake ni faini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo kisichozidi  miaka mitatu.
“Muswada unapendekeza kuwa kifungu hicho kifutwe na badala yake kitungwe kifungu kipya cha 60A ili kuweka masharti yanayojitosheleza kuhusu zuio la kuoa au kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari, kinapendekeza adhabu yake iwe kifungo cha miaka 30 gerezani,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.
Vile vile mtu atakayebainika kusaidia, kushawishi au kuacha mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuolewa au kuoa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha miaka mitano gerezani au vyote kwa pamoja.
Mhe. Masaju aliendelea kwa kufafanua kuwa, sheria hiyo imependekeza kuwa pale ambapo kosa hilo litafanywa na mtoto basi adhabu yake itakuwa kwa mujibu wa masharti ya sheria ya mtoto. Hii ni kwa sababu sheria ya mtoto inakataza mtoto anayetiwa hatiani kufungwa gerezani.
Aidha marekebisho hayo katika sheria ya Elimu yanalenga kumjengea mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari mazingira mazuri ya kumaliza ipasavyo elimu yake kwa ngazi hiyo.Hivyo basi kila Mkuu wa shule au Mwalimu Mkuu atawasilisha kwa Kamishna wa Elimu taarifa ya robo mwaka kuhusu matukio ya ndoa na mimba kwa wanafunzi katika shule yake na hatua zilizochukuliwa.
Sheria ya Elimu inamruhusu mwanafunzi aliyepewa ujauzito kuendelea na masomo mara tu anapojifungua. Sheria hiyo inasubiri kuwekwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ili ianze kutumika.

Waganga wa tiba asili watakiwa kujisajili

st0F40Nn_400x400 
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
—————————-
Waganga wa tiba asili ambao wamekuwa wakitoa huduma ya tiba pasipo kujisajili wametakiwa kujisajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili waweze kutambulika kisheria.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla ameyasema hayo leo, Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge Viti Maalum Mhe. Zainabu Mussa Bakar juu ya udanganyifu unaofanywa na waganga wa tiba asili wa kutoa dawa feki kwa wagonjwa.
“Waganga wa tiba asili wapo kisheria, ni kweli wapo wanaotoa dawa feki, na wengi wao ni wale ambao hawajasajiliwa, hivyo tumewaagiza kujisajili ili tuweze kuwatumbua na dawa zao ziweze kuhakikiwa na kusajiliwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu,” alifanunua Mhe. Kigwangalla.
Mhe. Kigwangalla amesema kuwa, mganga yoyote atakaye kiuka agizo hilo la kujisajili basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Aidha, amesema Wizara iko makini na ufuatiliaji wa dawa feki nchini kwani wanapopata fununu ya uwepo wa dawa feki hutuma kikosi kuchunguza na ikibainika kuwa dawa ni feki basi hatua kali huchukuliwa kwa muhusika.
Aliendelea kwa kusema kuwa, ili kudhibiti uingizwaji wa dawa feki nchini Wizara hiyo hufanya uhakiki wa muda mrefu kuchunguza iwapo dawa inayopendekeza kuingia nchini siyo feki na inafaa kwa matumizi ya binadamu, ikiwa dawa haina madhara yoyote basi inasajiliwa kwa ajili ya kuingia sokoni.
Vilevile Mhe. Kigwangalla amesema kuwa, Wizara imewaagiza waganga wa tiba asili kufunga dawa zao kwa kutumia vifungashio maalum vya madawa ambavyo vitasaidia dawa hizo kuendelea kuwa salama kwa mtumiaji kwa kipindi kilichopangwa kutumika.

KANISA LA EAGT LAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO wanaotoka katika familia duni

Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Na BMG
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba katika Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza, limekabidhi misaada ya vitu
mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika
familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.
Akikabidhi msaada huo hii leo, Askofu wa kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola, amesema watoto 18  waliokabidhiwa msaada huo ni sehemu ya watoto 264 wanaolelewa na kanisa hilo kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto iliyoanzishwa
kanisani hapo tangu mwaka 2010.
Askofu Dkt.Kulola amesema hiyo si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa msaada wa vitu hivyo na kueleza kuwa limekuwa
likifanya hivyo mara kwa mara ikiwemo kuwalea watoto hao kwenye maadili na afya njema na kuwaandaa kuwa watumishi wema katika jamii kwa baadae.
Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel, amesema msaada huo umetolewa baada ya
uongozi wa Kanisa kuzitembelea familia hizo na kujionea hali duni za maisha wanayoishi ambapo baadhi yao hulazimika kulala chini baada ya nyumba zao kuathiriwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana.
Wazazi, walezi na watoto walionufanika na msaada huo, wameushukuru uongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kupitia Kituo
cha Huduma ya Mtoto, ambapo wametanabaisha kwamba msaada huo utawasaidia kuondokana adha ya kulala chini iliyokuwa ikiwakabiri.
Msaada huo wa vitanda, magodoro, mashuka, mahindi na mchele umegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa ambazo zilitolewa
na wahisani kutoka nje ya nchi ambapo wazazi na walezi wametakiwa kutambua
kwamba jukumu la kuwalea watoto katika maadili mema ni la jamii nzima badala ya
kuwaachia viongozi wa dini na taasisi za kijamii pekee.

MKUTANO WA MASHAURIANO YA KITALAM JUU YA KUANZISHA VITUO BORA VYA UVUVI WAFANYIKA ZANZIBAR

W1Meza kuu ikisikiliza utaratibu wa Mkuta kutoka kwa Masta Solomon hayupo (pichani).
W2Mkurugenzi kutoka Umoja wa Africa- Ofisi ya rasilimali wanyama Simplice Noula akitoa tarifa ya ofisi yake katika Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
W3Waziri wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid Muhammed akifungua Mkutano wa siku mbili wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa, uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
W4  

JAMII imeshauriwa kubadilisha mfumo wa kupenda kukaa nje ya nyumba zao kuepuka kupata maambukizo ya ugonjwa wa malaria

PEMBA-ZANZIBAR 
Na  Masanja Mabula –Pemba
———————————-
JAMII imeshauriwa kubadilisha mfumo wa kupenda kukaa nje ya nyumba zao kwa ajili ya mazungumzo hasa nyakati za usiku ili kuepuka kupata maambukizo ya ugonjwa wa malaria .
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti ugonjwa wa malaria Pemba Bakar Omar Khatib alitoa ushauri huo wakati akizungumza na maafisa wa Wizara ya afya kutoka Wilaya ya Micheweni na Wete kwenye  mkutano wa uhamasishaji zoezi la utoaji wa vyandarua  vilivyotiwa dawa uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha uwalimu Benjamini Mkapa.
Amesema kwamba utafiti uliofanywa na wataalamu wa kitengo hicho umebaini kwamba  mbu anayesababisha malaria hupenda kukaa nje ya nyumba na kwamba  njia ya kukabiliana na ugonjwa huo ni kwa jamii kuachana na tabia ya kukaa nje kufanya mazungumzo .
“Mbu anayesababisha malaria nao ni wajanja wanapenda kukaa nje , hivyo ili kukabioliana na ugonjwa huu , ni vyema jamii kubadilisha mfumo wa kukaa ya nje ya nyumba zao kwa ajili ya mazungumzo ”alifahamisha.
Aidha amesema kwamba kutokana na hali hiyo , walio katika hatari   ya kupata maambulizi ya ugonjwa huo  zaidi ni watu wazima kuliko watoto kwani ndiyo wanaopenda kukaa nje , hususani kwa  kuangalia TV na mazungumzo .
Nao washiriki wa kikioa hicho wamekishauri kitengo hicho kuzungumza na makampuni ya simu za mikononi ili yatumike kusambaza ujumbe ka wamiliki wa simu unaotambulisha matumizi sahihi ya vyandarua .
Juma Shaame Salim kutoka mamlaka ya usimamizi wa mazingira Wilaya ya Wete , alisema utaratibu huo utasaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa wakati muafaka kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanamiliki ya simu za mikononi
“Kutokana umuhimu wa suala hili ,  ni vyema kitengo hichi kuzungumza na makampuni wa simu za mikononi ili yasaidie kueneza ujumbe kwani wananchi wengi wanamiliki simu za mikononi ”alishauri .
Naye Ali Rajabu kutoka Wilaya ya Micheweni akichangia kaatika mkutano huo aliomba kitengo kuandaa sheria ndogo ndogo ambazo zitatumika akuwabana wananchi ambao wanavitumia vyandarua kinyume na ilivyokusudiwa
Alifahamisha kwamba baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo vyandarua vimezungushiwa bustani huku baadhi wakivitumia kwa ajili ya uvuvi wa dagaa , jambo ambalo  linakwamisha ufanisi wamapambano dhidin ya malaria .
Akifunga kikao hicho kwa niaba ya Afisa Mdhamini wizara ya afya pemba , dk Harouk Khalifan hamad alisema mapambano dhidi ya malaria yanahitaji nguvu ya pamoja kutoka wadau na wananchi wote .
katika zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa msimu huu jumla ya wananchi laki mbili hasini na tisa elfu na mia nane thelethini na sita (259,836) ambapo walioandikishwa ni wananchi laki nne sitini na saba elfu nan mia saba na sitini na tatu (467,763) kwa kisiwa cha Pemba .

KITWANGA AKABIDHI RASMI OFISI KWA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

C1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo.
C2 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.  
C3 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu) akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano ofisini humo.  
C4 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
C5 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
C6 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

mkutano wa kikao kazi cha wafanyakazi, maendeleo ya jamii CHAFANYIKA DAR ES SALAAM

New Picture 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Bibi Sihaba Nkinga akifungua Mkutano wa watumishi wa Wizara (hawapo pichani) walioshiriki kikao kazi cha watumishi wote katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Wiki ya Utumishi wa Umma katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Raslimaliwatu Erasmus T. Rugarabamu na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE wa Tawi Edwin B. Mtembei. (Tarehe 24/6/2016).
Pcha na Mpiga Picha Wetu

Mashine za tiketi za kieletroniki kuanza kutumika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.

M1 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisisitiza jambo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji  wa mashine za tiketi zakieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
M2 
Mhandisi kutoka kampuni ya B.C.E.G ya China Bw. Xiong (kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(kulia) kuhusu mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
M3 
Mtaalamu wa Mashine za tiketi za kieletroniki kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel (kushoto) akimuelekeza jinsi ya kutumia moja ya mashine hizo Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine hizo  uwanjani hapo Leo Juni 27,2016.
M4 
Mtaalamu kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel akirekebisha moja ya mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
M5
M6 
Baadhi ya wananchi wakijaribu kutumia mashine ya tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TZTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Maliasili na Utalii itashiriki katikaMaonesho ya40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(SABASABA)kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 8 Julai, 2016 katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere, Dar es Salaam.
Wizara itakuwa na washiriki kumi na sita (16) ambao ni Idara pamoja na Taasisi zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki.
Kwa upande wa Taasisi ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na Vyuo vya Wanyamapori (Mweka, Pasiansi na Likuyu Semaganga).
Taasisi nyingine ni Vyuo vya Misitu na Nyuki (Olmotonyi, FITI Moshi na Chuo cha Nyuki Tabora), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wakala wa Mbegu za Miti, Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Washiriki wote hao watakuwa kwenye banda moja la MALIASILI, Wizara inawakaribisha wananchi wote kwenye banda hilowaweze kujionea na kuelimika namambombalimbali yanayohusu Utalii,  Ufugaji wa Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.
Aidha, Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumikwa gharama nafuu. Safari ya kwenda na kurudi kwa watoto itakua Tsh. 10,000 na watu wazima Tsh. 20,000. Safari ya kulala itakuwa Tsh. 50,000.
Pia katika maonesho hayo itakuwepo fursa ya kuwaona wanyamapori hai mbalimbali kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na SIMBA.
Kaulimbiu ya Maonesho hayo mwaka huu inasema“Tunaunganisha Uzalishaji wa Masoko”
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii
27 Juni, 2016.

BALOZI WA JAMHURI YA KOREA NCHINI AKUATANA NA RAIS DK.SHEIN

d1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo
d2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumsalimia Rais,
d3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar baada  mazungumzo yao.
[Picha na Ikulu.]

WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC BOTSWAN

MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Juni 27, 2016) kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit)   utakaofanyika kesho (Jumanne, Juni 28, 2016).
Mhe. Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Gaborone (GICC).
Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu   utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).
Pia mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe. Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Wengine ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti anayeondoka wa SADC.
Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na Maofisa wengine waandamizi.

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI,

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TZ 
TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI, PAMOJA NA MLIPUKO WA UGONJWA WILAYANI CHEMBA NA KONDOA, MKOANI DODOMA,  LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 27 JUNI, 2016
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inaendelea na utaratibu wa kutoa tahadhari kwa wananchi na maelekezo ya hatua za kuchukua katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu. Huu ni mwendelezo wa utoaji wa taarifa ya kila wiki, kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu kama tulivyoahidi. Hadi kufikia tarehe 26 Juni 2016, jumla ya wagonjwa 22,185 wametolewa taarifa, na kati yao, watu wapatao 344 wamepoteza maisha, tangu ugonjwa huu uliporipotiwa mnamo mwezi Agosti 2015.
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika wiki hii inayoishia   tarehe 26 Juni 2016, idadi ya wagonjwa wa Kipindupindu walioripotiwa ni 365 na hakuna aliyepoteza maisha.  Idadi kubwa ya wagonjwa hawa walitolewa taarifa kutoka wilaya ya Ukerewe (316) ambapo imejumlisha wagonjwa kutoka tarehe 7 Aprili hadi tarehe 21 Juni 2016. Hivyo, wagonjwa wa Kipindupindu wapya walioumwa kati ya 20 hadi 26 Juni 2016 pekee ni takriban 49. Takwimu hii inaashiria kuwa wagonjwa wameongezeka kidogo ikilinganishwa na wiki iliyotangulia, ambapo kulikuwa na wagonjwa 46 na vifo viwili. Mikoa iliyoripoti ugonjwa wa Kipindupindu wiki hii ni Morogoro (Morogoro mjini 15, Kilosa 9 na Mvomero 3), Mara (Tarime vijijini 18), Mwanza (Ukerewe 319) na Arusha (Arusha Vijijini (1).

Sekta binafsi ishirikishwe katika utekelezaji wa Mpango

2 
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika katika ukumbi wa Hazina, Dodoma.
SONY DSC
………………………………………………………………………………………………
Na Joyce Mkinga
SEKTA Binafsi katika ngazi zote ni lazima ishirikishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21 uliozinduliwa hivi karibuni.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri aliyasema hayo alipokuwa akifunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Bibi Florence Mwanri amesema sekta binafsi ni wadau muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo hivyo, wanatakiwa kushirikishwa katika mipango yote ya Serikali.
“Katika mipango yetu katika ngazi zote lazima sekta binafsi ishirikishwe kwa sababu wao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo” alisema Bibi Mwanri
Amesema maafisa mipango wanapoibu miradi mbalimbali katika ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa ni lazima sekta binafsi ishirikishwe ili kuwapa fursa nzuri ya kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo ambao unalenga katika Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na Maendeleo ya watu
Mkutano huo uliwashirikisha wachumi na maafisa mipango 170 kutoka katika wizara, idara za serikali, sekretarieti na mikoa na wilaya, taasisi za utafiti, na sekta binafsi ulikuwa na kaulimbiu ya Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21.
Lengo kuu la Mkutano huo ilikuwa ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na utelekezaji wake.
Mpango huo unatarajia kugharimu Trilioni 107 ambapo Sekta binafsi itachangia  Trilioni 48.
Akiwasilisha maazimio ya mkutano huo Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kutoka Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete amesema Serikali na sekta binafsi wakutane pamoja na kupanga mikakati ya kutekeleza mpango huo wa maendeleo.
Vile vile, Dkt Madete alisema kuwa kuna haja ya Serikali kuingiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia katika mipango ya Serikali ikiwa ni pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Mkutano huo uliandaliawa Tume ya Mipango kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.

ZULMIRA ATAKA KAZI KWA PAMOJA KUHAMI MAENEO YA URITHI WA DUNIA

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues amewakumbusha wadau wa urithi wa dunia na maeneo ya hifadhi kufanyakazi kwa pamoja kwa lengo la kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo bila kuondoa ushiriki wa wananchi wanayozunguka.
 
Kauli hiyo ameitoa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lake kwa wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia mjini Marangu Moshi, kufuatia makubaliano na serikali ya Tanzania.
 
Alisema akizungumza na washiriki kwamba UNESCO inachofanya ni kuanzisha safari ambayo inaweza kuwa ngumu na ndefu lakini washiriki wake ni lazima kutambua namna ya kuendelea kufanya menejimenti ya maeneo ya hifadhi na urithi wa dunia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
 
Akifungua mafunzo hayo ambayo wataalamu ni washiriki wenyewe wakitumia njia ya kuelewa ya methodolojia ya uchambuzi wa vikwazo (Bottleneck Analysis Methodology) alisema safari ya kufanikisha menejimenti ya maeneo hayo duniani na hasa hapa nchini ni yenye changamoto nyingi na kwamba wadau wote wanatakiwa kuwa pamoja kuvishinda vikwazo hivyo na kuifanikisha safari.
 
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na shirika lake kwa wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.
 
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
 —————————————
Akizungumza katika warsha hiyo ambayo imechukua wadau mbalimbali wa masuala ya urithi na menejimenti zake kutoka serikalini, taasisi zisizo za kiserikali na wananchi wengine, alisema kwamba maeneo hayo yamezungukwa na wananchi na pamoja na kuwawekea sheria za kutoharibu na kuyachakaza ipo haja ya kushirikiana nao namna ya kupanga kuyaendeleza maeneo hayo huku yakiwa yamebaki katika hali inayotakiwa.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kupanga maendeleo katika maeneo ambayo ni ya urithi wa dunia, binadamu na maeneo ambayo uhai unaweza kuwepo.
Aidha akifafanua zaidi mtawala huyo wa UNESCO nchini Tanzania amesema mafunzo hayo yamelenga kuwapa wahusika nadharia zinazofaa katika safari ndefu ambayo UNESCO nayo itashiriki na isingelipenda kumwacha hata mtu mmoja nyuma.
Mafunzo hayo yanatolewa kufuatia mpango wa UNESCO wa kutaka kuwa na uhakika na kuhami maeneo hayo ya urithi; huku mamlaka zikitoa ushirikiano ili kuwezesha malengo ya maendeleo endelevu, ambayo ndiyo ajenda ya dunia kuelekea 2030, yanafikiwa bila kuathiri maeneo tajwa.
Ofisa anayeshughulikia watu na maeneo yenye uhakika wa uhai: Biashara zinazozingatia mazingira na uchumi unaombatana nao kutoka Sekta ya Sayansi Ofisi ya Unesco, Dar es salaam, Myoung Su Ko akiwasilisha mada kwa washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Resort mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.
 
Alisema kwa kuwa kitaifa, serikali imeshatoa matamko ya kisera na kuweka mikakati ya utekelezaji wa taratibu za kuhami maeneo ya kiutamaduni na ya asili ipo haja ya wadau wengine kuona namna ya kufanyakazi kama timu katika safari ambayo kila mmoja anastahili kuwaijibika kwa namna yake hata kama kunatokea changamoto.
Alisema wadau wanatakiwa kuangalia namna ya safari zao zinavyostahili kufanywa na kuwa, kwa lengo la kutumia raslimali zilizopo kutekeleza mipango ya maendeleo na ya kuhami maeneo hayo bila kutegemea msaada wa wafadhili au wahisani.
Awali katika ujengaji wa wazo la mafunzo ilielezwa kuwa pamoja na kuwapo na juhudi kubwa za kuhami maeneo ya urithi wa dunia na kuyasajili maeneo ambayo uhai unaweza kuwapo na wanadamu, kumekuwepo na changamoto kubwa za maendeleo ambazo zinatishia kuvuruga mfumo tete wa ikolojia uliopo.
Katika kufanikisha hifadhi ya maeneo hayo kumeonekana changamoto za upungufu wa rasilimali watu wenye uwezo na vifaa vya kushughulikia uharibifu, ukosefu wa uwezo wa kuhifadhi maeneo hayo kwa kuoanisha na uwapo wa watu.
Mtaalamu wa programu na utamaduni kutoka Ofisi za Unesco Afrika Mashariki Bi. Karalyn Monteil akiwasilisha mada kuhusu makubaliano ya ulinzi katika maeneo ya urithi na utamaduni wa dunia katika warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Marangu, Moshi.
 

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU ITAKUTANA NA WADAU PAMOJA NA WANANCHI 28 JUNI, 2016

New Picture (1) New PictureO
fisiyaTaifayaTakwimu
 Taarifa kwa UmmaKatika kuazimisha “WIKI YA UTUMISHI WA UMMA” yenye kauli mbiu “Uongozi wa Umma kwa ukuaji Jumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka”, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawajulisha wananchi na wadau wote kuwa imetenga siku ya Jumanne tarehe 28 Juni, mwaka huu, kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi ili kutoa elimu na kusikiliza hoja na maoni kuhusu utoaji wa takwimu rasmi nchini.
Muda ni kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu.
KARIBUNI WOTE
ImetolewanaMkurugenzi Mkuu,
OfisiyaTaifayaTakwimu.
24June, 2016


No comments :

Post a Comment