Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akijibu hoja za Wabunge mapema leo
Bungeni Mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja kuhusu muswaada wa sheria
ya marekebisho ya sheria mbalimbali wamwaka 2016.
———————————————-
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania leo, Mjini Dodoma limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria
ya Elimu kifungu kinachoeleza kuwa mtu anayempatia ujauzito mwanafunzi
wa shule ya msingi au sekondari kuwa adhabu yake ni faini isiyozidi
shilingi laki tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu.
“Muswada unapendekeza kuwa kifungu
hicho kifutwe na badala yake kitungwe kifungu kipya cha 60A ili kuweka
masharti yanayojitosheleza kuhusu zuio la kuoa au kumpatia ujauzito
mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari, kinapendekeza adhabu yake
iwe kifungo cha miaka 30 gerezani,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Mhe. George Masaju.
Vile vile mtu atakayebainika
kusaidia, kushawishi au kuacha mwanafunzi wa shule ya msingi au
sekondari kuolewa au kuoa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni
faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha miaka mitano
gerezani au vyote kwa pamoja.
Mhe. Masaju aliendelea kwa
kufafanua kuwa, sheria hiyo imependekeza kuwa pale ambapo kosa hilo
litafanywa na mtoto basi adhabu yake itakuwa kwa mujibu wa masharti ya
sheria ya mtoto. Hii ni kwa sababu sheria ya mtoto inakataza mtoto
anayetiwa hatiani kufungwa gerezani.
Aidha marekebisho hayo katika
sheria ya Elimu yanalenga kumjengea mwanafunzi wa shule ya msingi au
sekondari mazingira mazuri ya kumaliza ipasavyo elimu yake kwa ngazi
hiyo.Hivyo basi kila Mkuu wa shule au Mwalimu Mkuu atawasilisha kwa
Kamishna wa Elimu taarifa ya robo mwaka kuhusu matukio ya ndoa na mimba
kwa wanafunzi katika shule yake na hatua zilizochukuliwa.
Sheria ya Elimu inamruhusu
mwanafunzi aliyepewa ujauzito kuendelea na masomo mara tu anapojifungua.
Sheria hiyo inasubiri kuwekwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ili ianze kutumika.
Waganga wa tiba asili watakiwa kujisajili
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
—————————-
Waganga wa tiba asili ambao
wamekuwa wakitoa huduma ya tiba pasipo kujisajili wametakiwa kujisajili
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili waweze kutambulika kisheria.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla ameyasema hayo
leo, Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge
Viti Maalum Mhe. Zainabu Mussa Bakar juu ya udanganyifu unaofanywa na
waganga wa tiba asili wa kutoa dawa feki kwa wagonjwa.
“Waganga wa tiba asili wapo
kisheria, ni kweli wapo wanaotoa dawa feki, na wengi wao ni wale ambao
hawajasajiliwa, hivyo tumewaagiza kujisajili ili tuweze kuwatumbua na
dawa zao ziweze kuhakikiwa na kusajiliwa kwa ajili ya matumizi ya
binadamu,” alifanunua Mhe. Kigwangalla.
Mhe. Kigwangalla amesema kuwa,
mganga yoyote atakaye kiuka agizo hilo la kujisajili basi hatua kali
zitachukuliwa dhidi yake. Aidha, amesema Wizara iko makini na
ufuatiliaji wa dawa feki nchini kwani wanapopata fununu ya uwepo wa dawa
feki hutuma kikosi kuchunguza na ikibainika kuwa dawa ni feki basi
hatua kali huchukuliwa kwa muhusika.
Aliendelea kwa kusema kuwa, ili
kudhibiti uingizwaji wa dawa feki nchini Wizara hiyo hufanya uhakiki wa
muda mrefu kuchunguza iwapo dawa inayopendekeza kuingia nchini siyo feki
na inafaa kwa matumizi ya binadamu, ikiwa dawa haina madhara yoyote
basi inasajiliwa kwa ajili ya kuingia sokoni.
Vilevile Mhe. Kigwangalla amesema
kuwa, Wizara imewaagiza waganga wa tiba asili kufunga dawa zao kwa
kutumia vifungashio maalum vya madawa ambavyo vitasaidia dawa hizo
kuendelea kuwa salama kwa mtumiaji kwa kipindi kilichopangwa kutumika.
KANISA LA EAGT LAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO wanaotoka katika familia duni
Mkurugenzi
wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia
mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na
vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT
Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Na BMG
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba katika Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza, limekabidhi misaada ya vitu
mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika
familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.
mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika
familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.
Akikabidhi
msaada huo hii leo, Askofu wa kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola,
amesema watoto 18 waliokabidhiwa msaada huo ni sehemu ya watoto 264
wanaolelewa na kanisa hilo kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto
iliyoanzishwa
kanisani hapo tangu mwaka 2010.
kanisani hapo tangu mwaka 2010.
Askofu Dkt.Kulola amesema hiyo si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa msaada wa vitu hivyo na kueleza kuwa limekuwa
likifanya hivyo mara kwa mara ikiwemo kuwalea watoto hao kwenye maadili na afya njema na kuwaandaa kuwa watumishi wema katika jamii kwa baadae.
likifanya hivyo mara kwa mara ikiwemo kuwalea watoto hao kwenye maadili na afya njema na kuwaandaa kuwa watumishi wema katika jamii kwa baadae.
Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel, amesema msaada huo umetolewa baada ya
uongozi wa Kanisa kuzitembelea familia hizo na kujionea hali duni za maisha wanayoishi ambapo baadhi yao hulazimika kulala chini baada ya nyumba zao kuathiriwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana.
uongozi wa Kanisa kuzitembelea familia hizo na kujionea hali duni za maisha wanayoishi ambapo baadhi yao hulazimika kulala chini baada ya nyumba zao kuathiriwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana.
Wazazi, walezi na watoto walionufanika na msaada huo, wameushukuru uongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kupitia Kituo
cha Huduma ya Mtoto, ambapo wametanabaisha kwamba msaada huo utawasaidia kuondokana adha ya kulala chini iliyokuwa ikiwakabiri.
cha Huduma ya Mtoto, ambapo wametanabaisha kwamba msaada huo utawasaidia kuondokana adha ya kulala chini iliyokuwa ikiwakabiri.
Msaada huo wa vitanda, magodoro, mashuka, mahindi na mchele umegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa ambazo zilitolewa
na wahisani kutoka nje ya nchi ambapo wazazi na walezi wametakiwa kutambua
kwamba jukumu la kuwalea watoto katika maadili mema ni la jamii nzima badala ya
kuwaachia viongozi wa dini na taasisi za kijamii pekee.
na wahisani kutoka nje ya nchi ambapo wazazi na walezi wametakiwa kutambua
kwamba jukumu la kuwalea watoto katika maadili mema ni la jamii nzima badala ya
kuwaachia viongozi wa dini na taasisi za kijamii pekee.
MKUTANO WA MASHAURIANO YA KITALAM JUU YA KUANZISHA VITUO BORA VYA UVUVI WAFANYIKA ZANZIBAR
Mkurugenzi
kutoka Umoja wa Africa- Ofisi ya rasilimali wanyama Simplice Noula
akitoa tarifa ya ofisi yake katika Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya
Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
JAMII imeshauriwa kubadilisha mfumo wa kupenda kukaa nje ya nyumba zao kuepuka kupata maambukizo ya ugonjwa wa malaria
Na Masanja Mabula –Pemba
———————————-
JAMII imeshauriwa kubadilisha
mfumo wa kupenda kukaa nje ya nyumba zao kwa ajili ya mazungumzo hasa
nyakati za usiku ili kuepuka kupata maambukizo ya ugonjwa wa malaria .
Mkuu wa kitengo cha
kudhibiti ugonjwa wa malaria Pemba Bakar Omar Khatib alitoa ushauri huo
wakati akizungumza na maafisa wa Wizara ya afya kutoka Wilaya ya
Micheweni na Wete kwenye mkutano wa uhamasishaji zoezi la utoaji wa
vyandarua vilivyotiwa dawa uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha
uwalimu Benjamini Mkapa.
Amesema kwamba utafiti
uliofanywa na wataalamu wa kitengo hicho umebaini kwamba mbu
anayesababisha malaria hupenda kukaa nje ya nyumba na kwamba njia ya
kukabiliana na ugonjwa huo ni kwa jamii kuachana na tabia ya kukaa nje
kufanya mazungumzo .
“Mbu anayesababisha malaria nao
ni wajanja wanapenda kukaa nje , hivyo ili kukabioliana na ugonjwa huu ,
ni vyema jamii kubadilisha mfumo wa kukaa ya nje ya nyumba zao kwa
ajili ya mazungumzo ”alifahamisha.
Aidha amesema kwamba kutokana na
hali hiyo , walio katika hatari ya kupata maambulizi ya ugonjwa huo
zaidi ni watu wazima kuliko watoto kwani ndiyo wanaopenda kukaa nje ,
hususani kwa kuangalia TV na mazungumzo .
Nao washiriki wa kikioa hicho
wamekishauri kitengo hicho kuzungumza na makampuni ya simu za mikononi
ili yatumike kusambaza ujumbe ka wamiliki wa simu unaotambulisha
matumizi sahihi ya vyandarua .
Juma Shaame Salim kutoka mamlaka
ya usimamizi wa mazingira Wilaya ya Wete , alisema utaratibu huo
utasaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa wakati muafaka kutokana na
idadi kubwa ya wananchi wanamiliki ya simu za mikononi
“Kutokana umuhimu wa suala hili
, ni vyema kitengo hichi kuzungumza na makampuni wa simu za mikononi
ili yasaidie kueneza ujumbe kwani wananchi wengi wanamiliki simu za
mikononi ”alishauri .
Naye Ali Rajabu kutoka Wilaya ya
Micheweni akichangia kaatika mkutano huo aliomba kitengo kuandaa sheria
ndogo ndogo ambazo zitatumika akuwabana wananchi ambao wanavitumia
vyandarua kinyume na ilivyokusudiwa
Alifahamisha kwamba
baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo vyandarua vimezungushiwa bustani huku
baadhi wakivitumia kwa ajili ya uvuvi wa dagaa , jambo ambalo
linakwamisha ufanisi wamapambano dhidin ya malaria .
Akifunga kikao hicho
kwa niaba ya Afisa Mdhamini wizara ya afya pemba , dk Harouk Khalifan
hamad alisema mapambano dhidi ya malaria yanahitaji nguvu ya pamoja
kutoka wadau na wananchi wote .
katika zoezi la
ugawaji wa vyandarua kwa msimu huu jumla ya wananchi laki mbili hasini
na tisa elfu na mia nane thelethini na sita (259,836) ambapo
walioandikishwa ni wananchi laki nne sitini na saba elfu nan mia saba na
sitini na tatu (467,763) kwa kisiwa cha Pemba .
KITWANGA AKABIDHI RASMI OFISI KWA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea
taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo,
Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa
Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji
Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa
ya makabidhiano.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu)
akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa
anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo,
kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam
leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano
ofisini humo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili
kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo,
Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu.
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara
baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati)
kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa
Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya
Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio
lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mkutano wa kikao kazi cha wafanyakazi, maendeleo ya jamii CHAFANYIKA DAR ES SALAAM
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,
Bibi Sihaba Nkinga akifungua Mkutano wa watumishi wa Wizara (hawapo
pichani) walioshiriki kikao kazi cha watumishi wote katika ukumbi wa
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha
Wiki ya Utumishi wa Umma katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii. Kulia ni
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Raslimaliwatu Erasmus T.
Rugarabamu na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE wa Tawi Edwin B. Mtembei.
(Tarehe 24/6/2016).
Pcha na Mpiga Picha Wetu
Mashine za tiketi za kieletroniki kuanza kutumika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisisitiza jambo wakati
alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi
zakieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mhandisi
kutoka kampuni ya B.C.E.G ya China Bw. Xiong (kushoto) akifafanua jambo
kwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(kulia) kuhusu
mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kutumika kuingia katika
Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mtaalamu
wa Mashine za tiketi za kieletroniki kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew
Emmanuel (kushoto) akimuelekeza jinsi ya kutumia moja ya mashine hizo
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipotembelea kuangalia
maendeleo ya uwekaji wa mashine hizo uwanjani hapo Leo Juni 27,2016.
Mtaalamu
kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel akirekebisha moja ya
mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia
katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
Baadhi
ya wananchi wakijaribu kutumia mashine ya tiketi za kieletroniki
zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi
karibuni.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Wizara
ya Maliasili na Utalii itashiriki katikaMaonesho ya40 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam(SABASABA)kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 8
Julai, 2016 katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere, Dar es Salaam.
Wizara
itakuwa na washiriki kumi na sita (16) ambao ni Idara pamoja na Taasisi
zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni Utalii, Wanyamapori, Mambo ya
Kale na Misitu na Nyuki.
Kwa
upande wa Taasisi ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha
Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro,Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na
Vyuo vya Wanyamapori (Mweka, Pasiansi na Likuyu Semaganga).
Taasisi
nyingine ni Vyuo vya Misitu na Nyuki (Olmotonyi, FITI Moshi na Chuo cha
Nyuki Tabora), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wakala wa Mbegu za
Miti, Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na
Utalii.
Washiriki
wote hao watakuwa kwenye banda moja la MALIASILI, Wizara inawakaribisha
wananchi wote kwenye banda hilowaweze kujionea na kuelimika
namambombalimbali yanayohusu Utalii, Ufugaji wa Nyuki, Uhifadhi wa
Misitu, Malikale na Wanyamapori.
Aidha,
Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa ya
Mikumikwa gharama nafuu. Safari ya kwenda na kurudi kwa watoto itakua
Tsh. 10,000 na watu wazima Tsh. 20,000. Safari ya kulala itakuwa Tsh.
50,000.
Pia
katika maonesho hayo itakuwepo fursa ya kuwaona wanyamapori hai
mbalimbali kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na
SIMBA.
Kaulimbiu ya Maonesho hayo mwaka huu inasema“Tunaunganisha Uzalishaji wa Masoko”
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii
27 Juni, 2016.
BALOZI WA JAMHURI YA KOREA NCHINI AKUATANA NA RAIS DK.SHEIN
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin
akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song
Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin
akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song
Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumsalimia Rais,
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin
akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song
Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar baada mazungumzo yao.
[Picha na Ikulu.]
WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC BOTSWAN
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Juni 27, 2016)
kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi
na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit) utakaofanyika kesho (Jumanne, Juni 28, 2016).
Mhe.
Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye
mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Gaborone (GICC).
Mkutano
huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse
Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na
usalama nchini Lesotho. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa
Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).
Pia
mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti
aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe.
Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na
Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Wengine
ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti
wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti
anayeondoka wa SADC.
Waziri
Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na
Maofisa wengine waandamizi.
TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI,
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAMKO
KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI, PAMOJA NA MLIPUKO WA
UGONJWA WILAYANI CHEMBA NA KONDOA, MKOANI DODOMA, LILILOTOLEWA NA MHE.
UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO, TAREHE 27 JUNI, 2016
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inaendelea na utaratibu wa kutoa tahadhari
kwa wananchi na maelekezo ya hatua za kuchukua katika kukabiliana na
mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu. Huu ni mwendelezo wa utoaji wa
taarifa ya kila wiki, kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu kama tulivyoahidi.
Hadi kufikia tarehe 26 Juni 2016, jumla ya wagonjwa 22,185 wametolewa
taarifa, na kati yao, watu wapatao 344 wamepoteza maisha, tangu ugonjwa
huu uliporipotiwa mnamo mwezi Agosti 2015.
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika
wiki hii inayoishia tarehe 26 Juni 2016, idadi ya wagonjwa wa
Kipindupindu walioripotiwa ni 365 na hakuna aliyepoteza maisha. Idadi
kubwa ya wagonjwa hawa walitolewa taarifa kutoka wilaya ya Ukerewe (316)
ambapo imejumlisha wagonjwa kutoka tarehe 7 Aprili hadi tarehe 21 Juni
2016. Hivyo, wagonjwa wa Kipindupindu wapya walioumwa kati ya 20 hadi 26
Juni 2016 pekee ni takriban 49. Takwimu hii inaashiria kuwa wagonjwa
wameongezeka kidogo ikilinganishwa na wiki iliyotangulia, ambapo
kulikuwa na wagonjwa 46 na vifo viwili. Mikoa iliyoripoti ugonjwa wa
Kipindupindu wiki hii ni Morogoro (Morogoro mjini 15, Kilosa 9 na
Mvomero 3), Mara (Tarime vijijini 18), Mwanza (Ukerewe 319) na Arusha
(Arusha Vijijini (1).
Sekta binafsi ishirikishwe katika utekelezaji wa Mpango
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akizungumza
wakati wa kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika
katika ukumbi wa Hazina, Dodoma.
………………………………………………………………………………………………
Na Joyce Mkinga
SEKTA Binafsi katika ngazi zote ni
lazima ishirikishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo
2016/17 – 2020/21 uliozinduliwa hivi karibuni.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya
Mipango Bibi Florence Mwanri aliyasema hayo alipokuwa akifunga mkutano
wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki.
Bibi Florence Mwanri amesema sekta
binafsi ni wadau muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa
Maendeleo hivyo, wanatakiwa kushirikishwa katika mipango yote ya
Serikali.
“Katika mipango yetu katika ngazi
zote lazima sekta binafsi ishirikishwe kwa sababu wao ndio watekelezaji
wakubwa wa mpango huo” alisema Bibi Mwanri
Amesema maafisa mipango wanapoibu
miradi mbalimbali katika ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa ni lazima sekta
binafsi ishirikishwe ili kuwapa fursa nzuri ya kushiriki kikamilifu
katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo ambao unalenga katika
Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na
Maendeleo ya watu
Mkutano huo uliwashirikisha
wachumi na maafisa mipango 170 kutoka katika wizara, idara za serikali,
sekretarieti na mikoa na wilaya, taasisi za utafiti, na sekta binafsi
ulikuwa na kaulimbiu ya Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21.
Lengo kuu la Mkutano huo ilikuwa
ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka
Mitano na utelekezaji wake.
Mpango huo unatarajia kugharimu Trilioni 107 ambapo Sekta binafsi itachangia Trilioni 48.
Akiwasilisha maazimio ya mkutano
huo Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kutoka Klasta ya
Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete amesema Serikali na sekta binafsi
wakutane pamoja na kupanga mikakati ya kutekeleza mpango huo wa
maendeleo.
Vile vile, Dkt Madete alisema kuwa
kuna haja ya Serikali kuingiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia
katika mipango ya Serikali ikiwa ni pamoja na Mpango wa Taifa wa
Maendeleo wa Miaka Mitano.
Mkutano huo uliandaliawa Tume ya Mipango kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
ZULMIRA ATAKA KAZI KWA PAMOJA KUHAMI MAENEO YA URITHI WA DUNIA
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
amewakumbusha wadau wa urithi wa dunia na maeneo ya hifadhi kufanyakazi
kwa pamoja kwa lengo la kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo bila
kuondoa ushiriki wa wananchi wanayozunguka.
Kauli
hiyo ameitoa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lake kwa wadau wa
mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia mjini Marangu Moshi, kufuatia
makubaliano na serikali ya Tanzania.
Alisema
akizungumza na washiriki kwamba UNESCO inachofanya ni kuanzisha safari
ambayo inaweza kuwa ngumu na ndefu lakini washiriki wake ni lazima
kutambua namna ya kuendelea kufanya menejimenti ya maeneo ya hifadhi na
urithi wa dunia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Akifungua
mafunzo hayo ambayo wataalamu ni washiriki wenyewe wakitumia njia ya
kuelewa ya methodolojia ya uchambuzi wa vikwazo (Bottleneck Analysis
Methodology) alisema safari ya kufanikisha menejimenti ya maeneo hayo
duniani na hasa hapa nchini ni yenye changamoto nyingi na kwamba wadau
wote wanatakiwa kuwa pamoja kuvishinda vikwazo hivyo na kuifanikisha
safari.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akizungumza katika warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na shirika lake kwa
wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia iliyomalizika mwishoni
mwa wiki mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
—————————————
Akizungumza
katika warsha hiyo ambayo imechukua wadau mbalimbali wa masuala ya
urithi na menejimenti zake kutoka serikalini, taasisi zisizo za
kiserikali na wananchi wengine, alisema kwamba maeneo hayo yamezungukwa
na wananchi na pamoja na kuwawekea sheria za kutoharibu na kuyachakaza
ipo haja ya kushirikiana nao namna ya kupanga kuyaendeleza maeneo hayo
huku yakiwa yamebaki katika hali inayotakiwa.
Mafunzo
hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kupanga maendeleo katika maeneo
ambayo ni ya urithi wa dunia, binadamu na maeneo ambayo uhai unaweza
kuwepo.
Aidha
akifafanua zaidi mtawala huyo wa UNESCO nchini Tanzania amesema mafunzo
hayo yamelenga kuwapa wahusika nadharia zinazofaa katika safari ndefu
ambayo UNESCO nayo itashiriki na isingelipenda kumwacha hata mtu mmoja
nyuma.
Mafunzo
hayo yanatolewa kufuatia mpango wa UNESCO wa kutaka kuwa na uhakika na
kuhami maeneo hayo ya urithi; huku mamlaka zikitoa ushirikiano ili
kuwezesha malengo ya maendeleo endelevu, ambayo ndiyo ajenda ya dunia
kuelekea 2030, yanafikiwa bila kuathiri maeneo tajwa.
Ofisa
anayeshughulikia watu na maeneo yenye uhakika wa uhai: Biashara
zinazozingatia mazingira na uchumi unaombatana nao kutoka Sekta ya
Sayansi Ofisi ya Unesco, Dar es salaam, Myoung Su Ko akiwasilisha mada
kwa washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro
Resort mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.
Alisema
kwa kuwa kitaifa, serikali imeshatoa matamko ya kisera na kuweka
mikakati ya utekelezaji wa taratibu za kuhami maeneo ya kiutamaduni na
ya asili ipo haja ya wadau wengine kuona namna ya kufanyakazi kama timu
katika safari ambayo kila mmoja anastahili kuwaijibika kwa namna yake
hata kama kunatokea changamoto.
Alisema
wadau wanatakiwa kuangalia namna ya safari zao zinavyostahili kufanywa
na kuwa, kwa lengo la kutumia raslimali zilizopo kutekeleza mipango ya
maendeleo na ya kuhami maeneo hayo bila kutegemea msaada wa wafadhili au
wahisani.
Awali
katika ujengaji wa wazo la mafunzo ilielezwa kuwa pamoja na kuwapo na
juhudi kubwa za kuhami maeneo ya urithi wa dunia na kuyasajili maeneo
ambayo uhai unaweza kuwapo na wanadamu, kumekuwepo na changamoto kubwa
za maendeleo ambazo zinatishia kuvuruga mfumo tete wa ikolojia uliopo.
Katika
kufanikisha hifadhi ya maeneo hayo kumeonekana changamoto za upungufu
wa rasilimali watu wenye uwezo na vifaa vya kushughulikia uharibifu,
ukosefu wa uwezo wa kuhifadhi maeneo hayo kwa kuoanisha na uwapo wa
watu.
Mtaalamu
wa programu na utamaduni kutoka Ofisi za Unesco Afrika Mashariki Bi.
Karalyn Monteil akiwasilisha mada kuhusu makubaliano ya ulinzi katika
maeneo ya urithi na utamaduni wa dunia katika warsha hiyo iliyomalizika
mwishoni mwa juma mjini Marangu, Moshi.
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU ITAKUTANA NA WADAU PAMOJA NA WANANCHI 28 JUNI, 2016
fisiyaTaifayaTakwimu
Taarifa
kwa UmmaKatika kuazimisha “WIKI YA UTUMISHI WA UMMA” yenye kauli mbiu
“Uongozi wa Umma kwa ukuaji Jumuishi: kuelekea katika Afrika
tunayoitaka”, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawajulisha wananchi na wadau
wote kuwa imetenga siku ya Jumanne tarehe 28 Juni, mwaka huu, kuwa siku
maalumu ya kukutana na wananchi ili kutoa elimu na kusikiliza hoja na
maoni kuhusu utoaji wa takwimu rasmi nchini.
Muda ni kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu.
KARIBUNI WOTE
ImetolewanaMkurugenzi Mkuu,
OfisiyaTaifayaTakwimu.
24June, 2016
No comments:
Post a Comment