Monday, May 2, 2016

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. WAZIRI UMMY MWALIMU

UMMY 
Ni miezi  minane sasa imepita tangu mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu uanze nchini, ambapo wizara yangu imekuwa ikitoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa huu kila wiki, na kufanya majumuisho kila mwezi, ili kutoa tahadhari kwa wananchi na maelekezo ya hatua za kuchukua ili kukabiliana na mlipuko huu. Kwa mara nyingine tena, ninatoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa wa Kipindupindu, ikiwa ni ya mwisho wa mwezi wa nne mwaka huu wa 2016

NSSF YADHAMINI SIKU YA MADANSA DUNIANI

 
 
Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya madansa duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF.  (Na Mpiga Picha Wetu)
 Ofisa Mwandamizi  Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto) akimkabidhi fulana,  Jumanne Mnola alipotembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
 
 Ofisa Mwandamizi  Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto), akimkabidhi fulana mmoja wa wateja wao, Said Ally, alipotembelea banda lao wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF.
 Ofisa Mwandamizi  Masoko na Uhusiano (Nssf), Amina Mbaga akigawa vipeperushi kwa baadhi ya
wananchi waliotembelea banda lao.
 
 Ofisa Uhusiano wa NSSF, Faides Mdee, akigawa vipeperushi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe jijini Dares Salaam, mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na NSSF.
 
 Wafanyakazi wa NSSF wakimkabidhi fulana mteja wao, Antela Salumu (katikati).
 
 Ofisa wa NSSF, Innocent Shao, (kulia) akiwaandikisha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF walipotembelea banda la NSSF katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyoadhimishwa kwenye
viwanja vya TCC Club Chang’ombe na kudhaminiwa na NSSF.
 
Ofisa uandikishaji NSSF, Amina Kisawaga (kulia) akitoa maelezo kwa mteja alietembelea banda lao Fumbwe Juma, katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
 
Picha ya pamoja.

KATA YA KISESA YAKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA KIMAZINGIRA

uga3 
uga1 
Sehemu wa Wakazi wa Kijiji cha Mwabukoli, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mpina (Hayupo Pichani) alipokuwa akiwafafanulia namna ya kukabiliana na changamoto za utunzaji wa mazingira katika ziara yake Mkoani Simiyu ya Utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kupanda miti na kuhifadhi vyanzo vya maji.
uga2 
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwabukoli wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wakifuatilia Hotuba ya Naibu Waziri Mpina (hayupo Pichani) alipotembelea kijijini hapo, wenyeji hao wa kabila la kisukuma, wapo na vifaa vyao vya jadi wakifanya dawa kwa utaratibu wa kudumisha mila zao wakati wa ngoma ya mavuno.

Wanadiaspora watakiwa kuwekeza nyumbani

Nembo ya ZADIA
                                              Na Mwandishi wetu Washington 
Wazanzibari waishio nchi za nje wametakiwa kuwekeza nyumbani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya taifa.
 
Wito huo ulitolewa jana na maofisa kutoka Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zaznzibar (ZSSF) wakati wakizungumza na Wazanzibari waishio nchini Marekani.
 
Akizungumza kwenye mkutano huo uliondaliwa na Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA), Meneja wa Mipango na Uwekezaji kutoka ZSSF Bwana Khalifa Muumin Hilal alisema kuwa Taasisi yake ina miradi kadhaa ya uwekezaji inayoendeshwa kwa ushirikiano na Benki ya Watu wa Zanzibar, na kwamba inawahamasisha Wazanzibari waishio Ughaibuni kuwekeza katika miradi hiyo.
 
Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa nyumba za kisasa katika eneo la Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar ambao ujenzi wake tayari umeanza na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.
 
Bwana Hilal alifafanua kuwa eneo hilo litakuwa na majengo ya nyumba za kuishi yenye urefu wa ghorofa saba, ambapo kila ghorofa itakuwa na nyumba mbili.
 
“Kutakuwa na nyumba za vyumba viwili, vitatu na vinne” alifafanua Meneja Hilal, na kuongeza kuwa nyumba hizo zitapatikana kwa bei nafuu.

NSSF ILIVYOSHIRIKI MEI MOSI KITAIFA MKOANI DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (kulia) na Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF nje ya Ofisi ya Mkoa wa Dodoma wakati wa sherehe za Sikukuu za Mei Mosi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma wakati wa sherehe za Sikukuu za Mei Mosi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais John Magufuli (wa pili kushoto) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia), Rais wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba (wa pili kulia) na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu , Jenista Mhagama wakati wa kilele cha sherehe za Sikukuu za Mei
Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Wafanyazi wa NSSF wakiwa na bango lao.
Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni  rasmi Rais John Magufuli (hayupo pichani), katika kilele cha Sherehe  za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Dodoma. 
 Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika Mei Mosi.
 Maandamano ya wafanyakazi wa NSSF yakipita mbele ya mgeni rasmi Rais John Magufuli (hayupo pichani) katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi.
 Wafanyakazi wakiwa katika maandamano.
 Wafanyakazi wa NSSF wakiingia kwa maandamano.
 wafanyakazi wakiwa katika sherehe za sikukuu ya Mei Mossi
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia), Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma,  Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori wakitoka bada ya kumalizika kwa sherehe za Sikukuu ya Mei Mosi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ATEMBELEA BARABARA YA KILEMA NA KUJIONEA ILIVYO HARIBIKA VIBAYA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitizama barabara ya kuelekea Hospitali ya wilaya ,Kilema Hospital namna ambavyo imeharibika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule iliyo jirani na barabara hiyo wakitizama sehemu ya korongo lililopo katika barabara hiyo ambayo ni tegemeo kwa Chuo cha Ualimu Mandaka,Seminari ya Mtakatifu James ,shle za sekondari pamoja na msingi.
Baaadhi ya madreva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakipita katika barabara hiyo ambapo kwa sasa nauli ya kupandisha abiria kwenda Hospitali ya wilaya ya Moshi,Kilima imepanda kutoka kiasi cha sh 3000 hadi 6000 .
Moja ya Magari yanayotumia barabara hiyo likijaribu kupita katika barabar hiyo ambayo imeharibika vibaya kutokana na maji yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya barabara hiyo likionekana korongo ambalo limeanza kumegwa na maji na kuhatarisha kukatika kwa mawasiliano katika baina ya vijiji 12 ambavyo wakazi wake wanatumia barabara hiyo.
 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ATUNUKU VYETI KWA WASHIRIKI WA KAMPENI YA SIKU 10 YA USAFI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO (KINAPA)

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akitoa vyeti kwa wawakilishi
wa Kampuni mbalimbali zilizosaidia katika kampeni ya siku 10 ya kufanya
usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Zoezi la
utoaji Vyeti limefanyika katika lango la Marangu wakati wa hafla fupi ya
kuwapokea washiriki wa zoezi hilo la usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na washiriki wa
kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro (KINAPA) muda mfupi mara baada ya kurejea. 
Baadhi ya Washiriki wa Kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya
Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Said Mecky Sadicky alipokuwa mgeni rasmi katika Hafla ya
kutunuku vyeti kwa washiriki pamoja na wamiliki wa kampuni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika Hafla hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntibenda AHUTUBIA WAFANYAKAZI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MEI MOSI

S9 
Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa katika sherehe za mei day kabla ya kuwahutubia wafanyakazi Leo jijini Arusha katika uwanja wa sheikh Amri Abeid .
S6 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntibenda akihutubia wakazi na wafanyakazi wa mkoa wa Arusha wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi duniani Leo kwenye uwanja wa sheikh amri abeid jijini Arusha.
S10Wafanyakazi wa kampuni na mashirika mbalimbali mkoani Arusha wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha daud ntibenda hayupo picha kwenye kilele cha sherehe za wafanyakazi Leo jijini Arusha
S7 
Zawadi za washindi wa maonyesho ya mei mosi kama zinavyoonekana pichani picha na Mahmoud Ahmad arusha
S8 
Moja ya gari la maonyesho kwenye mei mosi la idara ya misitu kama lionekanavyo pichani picha na Mahmoud Ahmad Arusha
S1 
Msafara wa magari ya maonyesho ukielekea uwanja wa sheikh amri Abeid jijini Arusha.  

HOSPITALI ZATAKIWA KUWALINDA WAPOKEA KUMBUKUMBU NA MAAMBUKIZI

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufunga mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi.
Na Mwandishi Wetu.

YALIYOJIRI SIKU YA MEI MOSI UWANJA WA JAMUHURI MJINI DODOMA

FRais John Pombe Magufuli , Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  (wapili kushoto) wakishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano wa wafanyakazi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na kuhutubiwa na Rais, Mei 1, 2016.  Wapili kulia ni Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi  Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba.
DWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Dodoma baada ya Rais John Magufuli kuhutubia katika sherehe za Mei Mosi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei1, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WATOA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2015, RAIS MAGUFULI AMKABIDHI CHETI NA KITITA CHA SH. MILIONI TANO

1Rais Dkt. John Magufuli,  akimkabidhi cheti cha mfanyakazi bora wa mwaka 2015 Enock Kalege, na zawadi ya Sh. milioni 5 iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa mfanyakazi huyo bora wa mwaka, wakati wa Kilele cha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Kitaifa mkoani Dodoma leo,Mei 1,2016.
2Kutoka kushoto, ni Kaimu Murugenzi wa Bernard Konga,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni PPF, William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Eliud Sanga, wakiwa katika sherehe za Mei Mosi Mkoani Dodoma leo,
Picha na Mpiga Picha Wetu

No comments :

Post a Comment