Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu,akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaoendela nchini
Geneva-Uswisi
Waziri
wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu kulia,Waziri wa afya Zanzibar
Mhe.Mahmoud Kombo wa nne kutoka kulia na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk
Ulisubisya Mpoki kushoto pamoja na wajumbe wengine wa mkutano huo
wakifurahia jambo.
Waziri
wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu kushoto akiwa na waziri wa afya
Zanzibar Mhe.Mahmoud Kombo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye
mkutano huo unaowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa
shirika la afya duniani(WHO),nyuma yao ni katibu mkuu wizara ya afya
Tanzania bara dkt.Mpoki Ulisubisya
……………………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………..
Mwandishi maalum-Geneva
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Hayo yamesemwa na waziri wa
afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati
akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini
Geneva,Uswisi.
Ummy alisema licha ya kukabiliwa
na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua katika sekta ya afya
kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000
kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000
Aidha, mkutano huo ambao ni wa
ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania imetambuliwa na
kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa
kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.
“Ninaeleza kwa masikitiko kuhusu
tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliopo nchini Tanzania
ambapo hadi kufikia tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia
21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi Serikali kupitia
wizara ya afya itaimarisha na kuzingatia kanuni za afya ya mazingira
katika kukabiliana na ugonjwa huu”alisema
Kwa upande wa kutokomeza malaria
waziri Ummy alisema Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa
huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa Tanzania bara na kwa upande wa
Zanzibar imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa hadi kufikia asilimia
0.6 .
Katika kuboresha huduma za afya
nchini alisema Serikali ya Tanzania imejipanga na kuhakikisha itaboresha
huduma za afya ziweze kumfikia kila mtanzania popote alipo, “ili kuweza
kufikia malengo haya ni wakati muhimu sasa kuwekeza zaidi katika sekta
hii kwa kuongeza uwekezaji katika raslimali fedha,watu pamoja na
kuboresha miundombinu ikiwemo utoaji wa huduma za afya nchini”.
Waziri Ummy alisema katika
kufikia mafanikio ,wizara ya afya inatarajia kuwasilisha muswada wa
sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016 wa kila mtanzania kuwa na
bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa mwananchi
katika kupata huduma za matibabu wakati wowote anapokuwa na fedha au
kutokuwa na fedha kwa kuwa maradhi hayachagui wakati.
Mkutano mkuu wa mwaka wa Afya
Duniani hufanyika nchini Geneva –Uswis kila mwaka mwezi mei ambao
huwakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Shirika la afya
Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na wadau,mashirika na taasisi zinazoshiriki
katika kutoa huduma za afya Duniani.Tanzania inawakilishwa na waziri wa
afya Tanzania bara Mhe.Ummy mwalimu na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.
Mahmoud Kombo.
VIONGOZI WA AFRIKA WATAKA USHIRIKIANO ZAIDI
Ni katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
WAKUU wa nchi za Afrika wametaka
kuwepo na juhudi za pamoja katika kukabiliana na majanga yatokanayo na
mabadiliko ya tabiachi yanayolikumba bara hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mchana
(Jumanne, Mei 24, 2016) wakati wa majadiliano baina ya viongozi kutoka
Zambia, Chad, Nigeria, Msumbiji na Tanzania mara baada ya ufunguzi wa
Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi,
jijini Lusaka, Zambia.
Wakishiriki kwenye mjadala wa
Wakuu wa Nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi,
viongozi hao walisema bara la Afrika linahitaji kupata maendeleo zaidi
licha ya tatizo la nishati linalolikumba bara hilo hivi sasa.
Akichangia mjadala huo, Rais wa
Zambia, Bw. Edgar Lungu alisema nchi yake imepania kuboresha hali ya
upatikanaji wa umeme vijijini lakini imekuwa ikikabiliwa na tatizo la
uhaba wa mvua kwa zaidi ya miaka miwili hali ambayo alisema imechangia
kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi nchini humo.
“Uhaba wa mvua umepunguza kiwango
cha maji katika bwawa la Kariba ambalo hutumika kuzalisha umeme nchini
mwetu. Na hapa kwetu, karibu asilimia 80 ya umeme wetu, unategemea
uzalishaji wa umeme kutokana na vyanzo vya maji,” alisema.
Rais wa Chad, Bw. Idriss Deby
Itno aliitaka benki ya AfDB ichukue nafasi ya mdau mkuu kwenye uwekezaji
wa sekta ya nishati na kuzisadia nchi za bara hili kupata mitaji ya
uwekezaji na ushauri wa kitaalamu.
“Tunahitaji kutumia fursa ambazo
benki yetu inazo katika kukabilianana changamato za ukosefu wa nishati.
Tukiweza kutekeleza jambo hilo, tutafanikiwa kuwa na miradi ambayo ni
makini na kwa maana hiyo tutaweza kuliangaza bara letu la Afrika kwa
kupata mwanga wa uhakika,” alisema.
Kwa upande wake, Makamiu wa Rais
wa Nigeria, Prof, Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika halina budi budi
kuweka kipaumbele kwenye masuala ya maendeleo yake wakati likitafuta
suluhisho la kukabiliana na athari za mazingira.
“Tunapaswa kutafuta njia za kubalance
mahitaji makubwa ya umeme ambayo bara letu linakabiliwa nayo dhidi ya
athari za kimazingira ambazo zinapigiwa kelele na mataifa makuna na
zinahatarisha kutunyima fursa ya kuendelea haraka kama ilivyokuwa kwao,”
alisema na kuongeza:
“Kama nchi zilizoendelea zinataka
sana kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi, zinatakiwa
zitupatie fedha, teknolojia na wataalamu ambao watasaidia kuendesha
mitambo ili tupate nishati safi kutokana na mafuta ya petroli na dizeli
sababu ni rasilmali ambazo tunazo.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
alisema ili kuondokana na tatizo la nishati, kuna haja ya kuwa na
viongozi wenye utashi wa kisiasa ambao watakuwa tayari kuruhusu
uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya nishati na kuongeza kuwa Tanzania
inapitia upya sheria zake ili kuruhusu miradi mikubwa ya uwekezaji
kwenye sekta hiyo.
Aliwaambia washiriki wa mkutano
huo kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi kwa ajili ya
wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye sekta hiyo na kutaja fursa
ambazo Tanzania inazo kwenye sekta ya nishati ikiwemo gesi asilia, makaa
ya mawe, madini ya urani, maji, upepo na nishati ya joto kutoka ardhini
(geothermal energy).
Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw.
Carlos Agostinho do Rosário alisema kuna haja ya kuwa na taasisi ya
uzalishaji na ugawaji umeme ya pamoja (electricity pool) ambayo
itaruhusu wazalishaji wa umeme wawauzie wanunuzi wakubwa.
Waziri Mkuu ambaye yuko Lusaka
kuhudhuria mkutano huo wa ADB kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John
Pombe Magufuli, amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).
Darbrew yapata tuzo ya uboreshaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller
Mkurugenzi
wa kampuni ya Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason
akiongea na wafanyakazi wakati ya hafla ya kusherehekea kushinda tuzo
ya uendelezaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller iliyofanyika
kiwandani hapo jana.
Maofisa waandamizi wa kampuni wakati wa sherehe hiyo.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Kampuni
ya Darbrew inayotengeneza pombe ya Chibuku imetunukiwa tuzo kutoka
SABMiller ya uendelezaji vinywaji vya asili nchini katika kongamano la
masoko la viwanda lililofanyika mjini Cape Town nchini Afrika ya
Kusini.
Darbrew
iliyopo chini ya TBL Group iliibuka kidedea baada ya kushindanishwa na
viwanda vinavyotengeneza vinywaji vya kienyeji vilivyopo chini ya
SABMiller vilivyopo katika nchi za Botswana,Malawi na Uganda.
Akitangaza
mafanikio hayo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam
jana,Mkurugenzi Mkuu wa Darbrew, David Cason alisema kuwa tuzo hiyo ni
mafanikio makubwa kwa kampuni na aliwapongeza wafanyakazi wote kwa
kujituma na kuhakikisha yanapatikana mafanikio siku hadi siku.
“Tuzo
hii sio ya mtu mmoja imepatikana kutokana na mchango wa kila mfanyakazi
wa DarBrew na inabidi kuongeza bidii zaidi katika kazi ili mafanikio
zaidi yapatikane na kampuni izidi kusonga mbele na kuwa miongoni mwa
makampuni makubwa ya vinywaji katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki”.Alisema Cason.
Alisema
hatua ya kampuni kushindanishwa na viwanda vikubwa na kuibuka na tuzo
ni jambo la kujivunia kila mfanyakazi na aliwashukuru mawakala na
wateja wote wa Chibuku kwa kuunga mkono biashara ya kampuni.
Kwa
upande wake Meneja wa Mauzo wa DarBrew,Freddy Kazindongo alisema
aliwapongeza wafanyakazi na kuwashukuru wateja kwa mafanikio
yaliyopatikana na kuongeza kuwa kampuni imejizatiti kuongeza zaidi ubora
wa huduma za uzalishaji na usambazaji na kuhakikisha kinywaji cha
Chibuku kinawafikia wananchi popote walipo na wanakipata kulingana na
kila mtu na uwezo wake .
Katika
kuthibitisha hilo alisema wiki hii kampuni imezindua chibuku super ya
mililita 750 ambayo itawawezesha wateja kupata kinywaji hicho kwa
gharama nafuu.
Kazindogo
alisema mkakati wa kampuni ni kuhakikisha urasimishaji wa pombe za
kienyeji unafanikiwa ambapo wananchi wataweza kupata kinywaji cha asili
katika mazingira bora ya usafi wakati huohuo wakikinunua wanachanga pato
la serikali kwa njia ya kodi kitu ambacho hakipo kwa pombe nyingine za
asili.
Pia
alisema kuwa kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira za moja kwa moja na
zisizo za moja kwa moja ambazo zinawawezesha mawakala wakubwa na wadogo
na akina mama wanaouza pombe za asili kujipatia mapato ya uendesha
maisha vilevile kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na akina mama
waliokuwa wanapika pombe za asili kwa kutumia kuni na mkaa watakuwa
wanauza pombe ambayo tayari imetengenezwa badala ya kutumia muda mwingi
kutengeneza pombe.
Wataka EU na AU kutoshiriki katika mazungumzo ya amani ya Burundi
Jiji la Bujumbura linavyoonekana katika picha.
………………………………………………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Vyama tisa vya upinzani
vilivyoshiriki uchaguzi wa Burundi wa mwaka 2015 na ambavyo
vinashiriki mazungumzo ya kutafuta amani ya Burundi vimetaka wawakilishi
wa umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kutoshiriki katika mazungumzo ya
amani ya Burundi.
Viongozi wa vyama hivyo kwa
pamoja wanasema kuwa wawakilishi wa taasisi hizo wameonyesha kuegemea
upande katika mgogoro wa Burundi kufuatia msimo wao wa kutaka chama cha
CNARED ambayo wanadai imeshiriki katika vurugu na mauaji nchini Burundi
kushiriki katika mazungumzo hayo.
Katika taarifa yao ilitiwa
sahihi na viongozi wote tisa wa vyama hivyo ,wamesema kutokana na
lugha na misimamo ya wawakilishi hao wa taasisi za juu ni wazi
wataharibu mchakato huo unaoendelea wa n kutafuta amani ya Burundi.
Taaarifa iliyotolewa na viongozi
wa vyama hivyo baada ya kumalizika mazungumzo ya awali ,viongozi hao
wamemtaka msuluhishi wa mgogoro huo Rais mstaafu wa Tanzania
kutokukubalina na wawakilishi hao na kushirikisha pande zote zenye
masilahi na mgogoro wa Burundi.
“Tunamtaka msuluhishi alione
hili na kuonya taasisi hizo kuacha propaganda za kuwagawa Warundi
katika mgogoro huo “taaarifa hiyo ilisema .
Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa
Burundi itizamwe kama serikali halali iliyochaguliwa na wananchi na
haipaswi kuingiliwa uhuru wake na watu ama taasisi za nje.
Aidha taarifa hiyo ilivitaja
vyama hivyo kuwa ni UPRONA ,FNL,FNL IRYAGIRAGAHUTU,RADEBU,zingine ni
RADEBU,FLORINA,MSPINKINZO Y’IJAMBO ,PMP,PRP na PIEBU.
Na katika hatua nyingine akifunga
mazungumzo hayo ya awali msuluhishi wa mgogoro huo Rais Benjamen Mkapa
ameeleza kuridhishwa na jinsi wajumbe wa mazungumzo hayo walivyoshiriki
mazungumzo hayo ya awali kwa dhati na kuonyesha nia kutaka amani katika
taifa lao.
“Nimeguswa na namna mlivyoonyesha
katika fikra na mawazo yenu ,mmeonyesha uzalendo mkubwa kwa kuonyesha
madhara ya mgogoro katika nchi yenu kiuchumi na maisha ya watu
yanayoharibiwa na mgogoro huo”Alisema Mkapa .
Mkapa ambaye anafanya usuluhishi
huo chini ya rais Yoweri Mseveni aliyeteuliwa na marais wa Afrika
mashariki kutatua mgogoro alishukuru uwepo uwepo wa taasisi za kimataifa
na za kikanda katika mazungumzo hayo.
Aidha rais Mkapa aliwaambia
wajumbe wa mkutano huo kwa muda wa wiki tatu zijazo atahakikisha kuwa
anafanya mazungumzo na makundi mengine ambayo yalialikwa lakini
hayakuweza kufika Arusha kutoa maoni yao kuhusu utatuzi wa mgogoro wa
nchi yaoMAONYESHO YA BIDHAA ZA PLASTIKI, KUFANYIKA MEI 27-29 MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM
Meneja
Mkuu wa Expo One, Ahmed Barakat, akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni kuhusu maonyesho hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Hamza Mohamed Hamza akizungumza katika mkutano huo.
Taswira meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Africa-PPB Tanzania, Mohamed Sami akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Khaled Abu El M karem akizungumza kwenye mkutano huo.
………………………………………………………………………………..
Na Doto Mwaibale
TANZANIA
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza ya bidhaa za plastiki,
mpira, kemikali za petrol na ujenzi yanayotarajiwa kufanyika katika
Mei 27 hadi 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Mlimani City jijiniDare s Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Expo One, Ahmed Barakat,
alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zitashiriki katika
maonesho hayo.
Alisema
Maonesho ya Afrika –PPB-EXPRO yatakuwa ni jukwaa la kipekee la bidhaa
mpya na yatatoa mwanya wa kuyaelewa masoko yake ambayo hayafahamiki
vizuri.
“Maonesho
haya yamebuniwa kwa lengo la kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa
kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Misri na Tanzania na hali
kadhalika kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha kuwa
Tanzania ni ya kwanza katika orodha ya nchi za Afrika ambapo
Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.
“Aramex
Africa ni mshirika rasmi wa usafirishaji wa Africa-PBB-EXPO na itakwua
inatoa mchango mkubwa katika kutoa huduma za ugavi na usafirishaji
kutoka Misri hadi Tanzania,” alisema.
Alisema
kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji
walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.
Alieleza
kwamba kanzidata hizo zinajumuisha hali ilivyo ndani ya soko la
Tanzania na thamani yake pamoja na takwimu sahihi ya kuuza na kuagiza,
hii inatoa fursa ya uhakika kwa mikutano ya mkakati ya B2B pamoja na
ufanisi unaohusiana pindi zinapofika.
Barakat
alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili
kuweza ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na
mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara.
“Kwa
kushiriki katika maonesho ya Africa-PPB-EXPO, pamoja na mambo mengine
washiriki watajifunza jinsi maudhui ya kina ya sekta yanaweza kuathiri
biashara zao, umoja uliopo miongoni mwa viongozi wa sekta, kupata
washirika wapya na kulinganisha kiwango chao katika mitazamo ya ubunifu.
“Kampuni
ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya usimamizi wa
mikutano na maonesho ambayo imejikita katika kuandaa na kutoa huduma
kwa maonesho ya biashara ya kimataifa pamoja na
kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
Alisema kwamba maonesho mengine ya Africa-PPB-EXPO yanatarajiwa kufanyika nchini Senegal na baadaye nchini Angola.
Yanga walivyopokea Kombe lao la pili kwa kuifunga Azam FC BAO 3-1 UWANJA WA Taifa
Rais wa Shirikisho la soka nchini, Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe la
Ubingwa wa Shirikisho (ASFC), Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub,
mara baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuichapa Timu ya Azam FC, Bao 3-1,
katika mchezo uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar
es salaam.
Wachezaji
wa Timu ya Yanga pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa
Kombe la Shirikisho, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Picha kwa hisani ya Michuziblog.
RAIS DKT.MAGUFULI MGENI RASMI Mkutano wa CRB
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa mashauriano wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi Nchini (CRB) kesho tarehe 26 Mei, 2016 katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mkutano
huo wa mwaka wa mashauriano na wadau wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi
unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya Makandarasi na wadau wa Sekta ya
Ujenzi wapatao 1000 na utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26 Mei,
2016 hadi tarehe 27 Mei 20l6.
Kaulimbiu
ya mwaka huu ni ‘Juhudi za Makusudi za Kukuza Uwezo wa Makandarasi
Wazalendo kwa Maendeleo Endelevu ya Kiuchumi; Changamoto na Mustakabali
Wake’.
Lengo
la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau wa Bodi ya Usajili Makandarasi na
Sekta ya Ujenzi ili kujadili changamoto zinazowakabili na kuweka
mikakati ya kuwajengea uwezo Makandarasi Wazalendo.
Imetolewa; Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
25 Mei, 2016
RAIS DkT Shein Alekea Nchini Comoro Kuhudhuria sherehe za Kumuapisha Rais Mteule wa Comoro.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,
akiagana na Wazee na Viongozi wa Serikali, wakati akiondoka Zanzibar
kuelekea Nchini Comoro kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteuli wa
Muungano wa Visiwa vha Comoro akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,
na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangana na Viongozi wa Serikali,
waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kumuaga
akielekea Nchini Conoro kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteule wac
Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe.Azali Assouman Boinakher.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed
Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuhudhuria
sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe.
Azali Assouman Boinakher. akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
(Picha na Ikulu)
Tanzania yapiga hatua kubwa katika matumizi ya huduma za mitandao
Kaimu Mkurugenzi Mamlakaya Mawasiliano Tanzania(TCRA)Mhandishi James Kilaba.
……………………………………………………………………………………………….
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Tanzania
imepiga hatua kubwa sana katika sekta ya mawasiliano hadi kufikia kuwa
kwenye kundi la nchi zilizoendelea kimawasiliano Duniani.
Takwimu
zinaonyesha kuwa watanzania takribani milioni 39 wana laini za simu za
kiganjani pamoja na watumiaji wa intaneti takribani milioni 20 ambapo
miaka ya nyuma idadi ya laini za simu za kiganjani zilikuwa 2,963,737.
Haya
ni maendeleo makubwa yanayoifanya Tanzania kuwa nchi bora kwa upande wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi
James Kilaba alisikika akisema kwamba,”Ukuaji wa kasi wa sekta ya
mawasiliano nchini umechangia sio tu katika kuboresha maisha ya wananchi
kijamii na kiuchumi bali unachangia sana katika kuinua pato la Taifa”.
Ukuaji huu umetokana na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za mawasiliano.
Kama wasemavyo wahenga kuwa ya Kaisari tumpe Kaisari basi sifa zote ziwaendee Mamlaka ya
WATANZANIA KUWAPUUZA WAONABEZA JUHUDI ZA RAIS JOHN MAGUFULI- DKT. KONDO
Na Anitha Jonas – MAELEZO
……………………………………….
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Dkt.Haruni
Kondo amewasihi Watanzania kuwapuuza waonabeza juhudi za Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Dkt.
Kondo ametoa wosia huo alipokuwa akizungumza na waandishi jijini Dar es
Salaam leo kuhusu jitihada mbalimbali anazozifanya Rais katika kupambana
na ufisadi, rushwa pamoja na kudhibiti nidhamu ya kazi kwa watumishi wa
umma.
“Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akifanya jitihada za kujenga
taifa na kuleta maendeleo kwa Watanzania bila kujali tofauti zetu za
kiitikadi, rangi au jinsia, hivyo ni vyema tumuunge mkono kwa kumuombea
ili aendelee kuwa na ujasiri huo, hekima na busara katika kufanya kazi
yake,”alisema Dkt.Kondo.
Mjumbe
huyo NEC ya CCM alisema ni vyema Watanzania wakajitathimini kwa
kuangalia tulipotoka na tulipo na wapi tunaelekea ikiwa lengo la Rais ni
kunyanyua uchumi wa taifa na nchi kuwa ya viwanda kwa kutumia
rasilimali za nchi.
Mbali
na hayo Dkt. Kondo alisema Watanzania hawana budi kumuunga mkono Dkt
Magufuli katika kupambana na kundi la watu wachache wanaopinga juhudi
zake huku nia ikiwa ni kuikomboa nchi kuepuka kuwa miongoni mwa nchi
tegemezi duniani.
Dkt.
Kondo alisisitiza kwa kusema kuwa Tanzania imejaa rasilimali nyingi
ikiwemo Madini, Mbuga za wanyama pamoja na ardhi yenye rutuba hivyo
rasilimali hizo zikisimamiwa vizuri na kila mtu akiwajibika kwa nafasi
yake hakika nchi itabadilika.
“Hata
hivyo suala la kukuza uchumi wa Taifa bado uko mikononi mwa Watanzania
wenyewe hivyo wananchi wote wasikate tamaa kwa maana “Penye nia Pana
Njia” alisema Dkt.Kondo.
Alisema
madudu yaliyoibuliwa na kufichuliwa na Rais Dkt. Magufuli katika baadhi
ya taasisi za umma ni kielelezo tosha kinachobainisha hatua ya
ubadhirifu, wizi na utapeli ulioikumba Tanzania.
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.
Selemani Jafo akiingia ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao
vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
Mbunge
wa Viti Maalum CCM , Mhe. Halima Bulembo akiwasili viwanja vya Bunge
mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
Mbunge
wa Bukoba Mjini CHADEMA , Mhe. Wilfred Lwakatare akiwasili viwanja vya
Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya bunge hilo leo 25 Mei,
2016.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiingia ndani
ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga
Mpina (kushoto) akiwa ameongozana na Wabunge wenzie wakielekea ndani
ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto)
akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiwasili
katika Viwanja vya Bunge leo Bungeni mjini Dodoma 25 mEI, 2016.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (kushoto)
akiwa ameongozana na Wabunge wenzie wakielekea ndani ya Bunge mjini
Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, DODOMA.
MATUKIO YA BUNGE NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO
Mbunge
wa jimbo la Nkasi Kaskazini (CCM) Mhe. Allya Kessy akizungumza jambo na
Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee nje ya ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma leo.
Mwekekezaji
na Msambazaji wa nguzo za umeme nchini kutoka Kampuni ya New Forest
iliyoko mkoani Iringa akiwaonesha jambo Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe.
Ally Kessy (kushoto) na Mbunge wa jimbo laKilolo Mhe. Venance Mwamoto
kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani waifuatilia hoja
mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani
waifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani
waifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi akifuatilia kwa
makini mjadala wa Waheshimiwa Wabunge wakati wa kipindi cha maswali na
Majibu.
Mbunge
wa Bunda Mjini Mhe. Esther Bulaya akichangia Hotuba ya Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ndani ya Ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wananchi kutoka jamii ya Wafugaji waliohudhuria kikao cha Bunge leo
mjini Dodoma kushuhudia Michango ya Wabunge wakati wa Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya (kulia) na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Elisha Eliya leo mjini Dodoma.
Picha/Aron Msigwa – MAELEZO
DK. PINDI CHANA AKUTANA NA VIONGOZI WA UHURU PUBLICATIONS LTD NA PEOPLES MEDIA LEO
Kaimu
Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk.
Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, akisalimiana na
Meneja Rasilimali watu wa zamani wa Uhuru Publications Ltd, Lucas
Kisasa, baada ya kumkuta nje wakati akienda ofisi za kampuni hiyo leo
kujitambulisha kwa viongozi wa Kampuni hiyo ambayo ni wachapishaji wa
magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na viongozi wa Peoples Media Ltd
ya Uhuru FM, leo. Kulia ni mpigapicha wa Magazeti ya Uhuru, Emmanuel
Ndege na Wapili ni dereva wa UPL Chamlungu
Kaimu
Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk.
Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, akisalimiana na
Kaimu Mkurugenzi wa Peoples Media, Angel Akilimali, alipowasili
kujitambulisha kwa viongozi wa Kampuni hiyo ambayo ni wachapishaji wa
magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na viongozi wa Peoples Media Ltd
ya Uhuru FM, leo.
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,
akisalimiana na Kaimu Meneja Rasilimali watu na Utawala, Paul Mg’ong’o,
alipowasili kujitambulisha kwa viongozi wa Kampuni hiyo ambayo ni
wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na viongozi wa
Peoples Media Ltd ya Uhuru FM,
Kaimu
Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk.
Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (wapili kushoto)
akifuatana na viongozi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Paul
Mg’ong’o (kulia) na na Angel Akilimali wa Peoples Media Ltd ya Uhuru
FM, Kushoto ni Ofisa kutoka Makao Makuu ya CCM, Amos Siyantemi
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (wapili
kushoto) akifuatana na viongozi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd,
Paul Mg’ong’o (kulia) na na Angel Akilimali wa Peoples Media Ltd ya
Uhuru FM, Kushoto ni Ofisa kutoka Makao Makuu ya CCM, Amos Siyantemi
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
akisalimiana na Kaimu Mhasibu Mkuu wa UPL Mama Masota
Baadhi ya viongozi wa UPL na Peoples Media wakimsubiri Dk. Pindi Chana
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akisoma
nakala ya gazeti la Uhuru la leo, kabla ya mazungumzo na viongozi hao
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
akimsalimia Mhariri wa Habari wa Uhuru FM Pius Ntiga. Kushoto ni Kaimu
Mhariri Mtendaji wa UPL Ramadhani Mkoma
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akisaini
kitabu cha wageni kabla ya kuanza mazungumzo yake na viongozi hao. Kulia
ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UPL Ramadhani Mkoma na Kushoto ni Kaimu
Mkueugenzi wa Peoples Media Angel Akilimali
Ofisa
wa Chama kutoka Makao Makuu ya CCM, Amos Siyantemi akitoa maneno ya
utangulizi kabla ya Dk. Pindi Chana kuzungumza na viongozi hao
Kaimu Mkurugenzi wa Peoples Media Angel Akilimali akijitambulisha
Kaimu Meneja Rasilimali watu na Utumishi Paul Mg’ong’o akijitambulisha
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
akizungumza na viongozi hao.
Kaimu
Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk.
Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizungumza na
viongozi hao.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
MATUKIO YA BUNGE NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO
Mbunge
wa jimbo la Nkasi Kaskazini (CCM) Mhe. Allya Kessy akizungumza jambo na
Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee nje ya ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma leo.
Mwekekezaji
na Msambazaji wa nguzo za umeme nchini kutoka Kampuni ya New Forest
iliyoko mkoani Iringa akiwaonesha jambo Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe.
Ally Kessy (kushoto) na Mbunge wa jimbo laKilolo Mhe. Venance Mwamoto
kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani waifuatilia hoja
mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani
waifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi akifuatilia kwa makini mjadala wa Waheshimiwa Wabunge wakati wa kipindi cha maswali na Majibu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani
waifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
Mbunge
wa Bunda Mjini Mhe. Esther Bulaya akichangia Hotuba ya Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ndani ya Ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wananchi kutoka jamii ya Wafugaji waliohudhuria kikao cha Bunge leo
mjini Dodoma kushuhudia Michango ya Wabunge wakati wa Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya (kulia) na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Elisha Eliya leo mjini Dodoma.Picha/Aron Msigwa – MAELEZO
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya (kulia) na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Elisha Eliya leo mjini Dodoma.Picha/Aron Msigwa – MAELEZO
Serikali yaadhimisha siku ya Afrika kwa kumuenzi nguli mpigania uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kulia) akiongoza msafara wa
ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuzuru
Kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid
Kaluta katika kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro na
kushoto ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru
Halfan Mshiro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema
wakiokota baadhi ya uchafu katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa
Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta walipozuru kaburi hilo katika
kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni
mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi na
kulia ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
Mtoto
wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi (watatu
kulia) akiongoza dua ya kumuombea baba yake hayati sheikh Kaluta Amri
Abeid wakati ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo
Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kushotombele) akizungumza wakati
ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru
katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri
Abeid Kaluta kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru
Halfan Mshiro (kulia) akizungumzia siku ya Afrika alipozuru katika
kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid
Kaluta kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. kushoto
mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema.
Katibu
Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa Dkt. Suleimani Sewangi (mwenye
miwani) akisoma tawasifu ya hayati Sheikh Kaluta Amri Abeid Kaluta
wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo
Jijini Dar es Salaam.
Bw.
Kassim Amotile (mwenye miwani) akigani Shairi lililoandikwa na marehemu
Mathias Mnyampala mwaka 1964 wakati wa kifo cha hayati Sheikh Kaluta
Amri Abeid Kaluta na kulipa jina la Kifo cha Sheikh Abeid, Pengo kuu kwa
Taifa wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika
leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia
Mjema na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo Bibi Nuru
Halfan Mrisho
Serikali yawezesha vikundi 1,200 vya wakulima kupata masoko.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………….
Serikali
imefanikiwa kuwezesha vikundi 1200 vya wakulima wadogo wadogo nchini
ili kupata masoko ya uhakika ya mazao yao wanayozalisha.
Akizungumza
kuhusu mradi wa kuboresha miundombinu ya masoko,uongezaji wa thamani na
huduma za kifedha vijijini (MIVARF) Mratibu wa Taifa wa Mradi huo Bw.
Walter Swai amesema malengo ya mradi huo ni kuongeza kipato cha wakulima
na uhakika wa chakula kwa kutengeneza miundombinu ya upatikanaji wa
masoko kwa wakulima kwa kuboresha barabara za kutoka mashambani kuelekea
sokoni na kuwapa taarifa sahihi kuhusu masoko na mahitaji yake.
Bw
Walter Swai ameongeza kuwa lengo la mradi ni kufikia vikundi 1,600 kwa
nchi nzima katika kutoa elimu ya kuwezesha wakulima kupata masoko ya
mazao yao ikiwa ni jitihada za Serikali kuwawezesha wakulima hao
kujikwamua kiuchumi.
“Nia
yetu ni kufikia vikundi 1,600 katika mikoa yote Tanzania Bara na
Visiwani na hadi sasa tumefika asilimia 75 ya lengo tulilojiwekea la
kuwawezesha wakulima wadogo kupata masoko ya mazao yao” alisema Bw.Swai.
Naye
Mtaalamu wa Masoko ya mazao ya kilimo wa MIVARF Bw. Muhoni Leonard
amesema kuwa mradi huo utasaidia kuwapa wakulima taarifa sahihi juu ya
masoko na mahitaji yake na kupunguza gharama ambazo zilikuwa zinatumika
kwa ajili ya kupata taarifa hizo kutoka kwa madalali.
“Azma
ya mradi huu ni kubadili muundo na utendaji wa wakulima wadogo kuongeza
ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji wa masoko ya mazao husika”
alisistiza Bw Leonard.
Aidha,
mmoja wa wakulima na msindikaji wa mchele kutoka Wilaya ya Chato mkoani
Geita Bw.Joseph Nchimani amesema kuwa elimu aliyoipata kutoka MIVARF
imemuwezesha kuendesha kilimo cha mpunga kwa njia ya kisasa ambayo
imemuwezesha kuongeza thamani ya mchele kwa kuufunga kwenye mifuko iliyo
katika hali ya
ubora unaokubalika kwenye soko.
“Kabla
ya kuanza kufunga mchele kwenye mifuko nilikuwa nauza jumla ya tani
mbili mpaka kumi kwa mwaka ila baada ya MIVARF kuja na kunipa elimu hii
nimeweza kuuza mpaka kufikia tani 50 kwa mwaka” alisistiza Bw.Nchimani.
Program
hiyo ya MIVARF inajushughulisha pia na kutoa huduma za kifedha vijijini
ambayo ni ya miaka saba inayotekelezwa kwa mikoa 30 ya Tanzania Bara na
Visiwani na inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
AHADI YA RAIS JPM KUHUSU MAJI MJI WA ILULA KUTEKELEZWA -WAZIRI LWENGE
Bw Venance Mwamoto
…………………………………………………………………………………………..
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI wa maji na umwagiliaji mhadisi Geryson Lwenge amewaondoa hofu wananchi wa mji wa Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuhusu ahadi ya Rais Dr John Magufuli ya kumaliza kero ya maji katika mji huo wa Ilula kuwa itaanza kutekelezwa mwaka huu.
…………………………………………………………………………………………..
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI wa maji na umwagiliaji mhadisi Geryson Lwenge amewaondoa hofu wananchi wa mji wa Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuhusu ahadi ya Rais Dr John Magufuli ya kumaliza kero ya maji katika mji huo wa Ilula kuwa itaanza kutekelezwa mwaka huu.
Alisema
kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr Magufuli ni
serikali ya ukweli na uwazi na ni serikali ya hapa kazi Tu hivyo
kila ilichoahidi kukifanya itafanya kwa wakati na kuwataka
wananchi kuendelea kujenga imani zaidi.
Waziri mhandisi Lwenge aliyasema hayo jana katika Mgahawa wa Bunge mjini Dodoma , wakati akizungumza katika kikao chake na mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na wawakilishi 11 wa wananchi wa mji wa Ilula waliofika bungeni mjini Dodoma kufuatilia ahadi ya maji iliyotolewa na Rais Dr Magufuli wakati wa kampeni kwa wananchi wa mji wa Ilula .
Waziri mhandisi Lwenge aliyasema hayo jana katika Mgahawa wa Bunge mjini Dodoma , wakati akizungumza katika kikao chake na mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na wawakilishi 11 wa wananchi wa mji wa Ilula waliofika bungeni mjini Dodoma kufuatilia ahadi ya maji iliyotolewa na Rais Dr Magufuli wakati wa kampeni kwa wananchi wa mji wa Ilula .
Mwamoto akishiriki na wananchi wa mji wa Ilula kukingas maji ambayo hutoka kwa mgao
………………………………………………………………………………………………
Alisema kuwa wizara yake imekwisha ingiza katika bajeti yake ya mwaka 2016/2017 itakayosomwa mapema wiki hii na kuwa mbali ya maeneo mengine ambayo yatapatiwa ufumbuzi wa kero ya maji mji wa Ilula ni miongoni mwa maeneo hayo .
………………………………………………………………………………………………
Alisema kuwa wizara yake imekwisha ingiza katika bajeti yake ya mwaka 2016/2017 itakayosomwa mapema wiki hii na kuwa mbali ya maeneo mengine ambayo yatapatiwa ufumbuzi wa kero ya maji mji wa Ilula ni miongoni mwa maeneo hayo .
Waziri
huyo alisema kuwa lengo la serikali ni kuendelea kusogeza huduma
ya maji kwa wananchi wake na kutekeleza ahadi zake kupitia ilani
ya uchaguzi ya chama tawala hivyo.
Hata
hivyo waziri Lwenge alimpongeza mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto na mbunge
Kabati kwa kuendelea kupambana bungeni kwa ajili ya kuwatumikia
wananchi wao na hata kufuatilia baadhi ya ahadi na kuwa hatua hiyo
ni nzuri na inaonyesha ni kiasi gani wabunge wao walivyokaribu na
changamoto za wananchi wao.
Mbali ya
waziri Lwenge kuzungumza na wananchi hao pia mbunge Mwamoto
aliwakutanisha wananchi hao na waziri wa Kilimo ,mifugo na Uvuvi
Mwigulu Nchemba ambae katika kikao chake na wananchi hao alieleza
mkakati wa wizara yake kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara
pamoja na wizara ya vijana na ajira ili kuanzisha viwanda vidogo
vya nyanya katika mji wa Ilula na kuwa kazi ya wizara yake ni
kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha nyanya na kuwawezesha
wakulima hao wa mafano mpango ambao utafanyika katika kanda mbali
mbali ila kwa nyanda za juu kusini wanakusudia kuufanya wilaya ya
Kilolo .
Kijana wa Ilula akichambua nyanya |
Kwa
upande wake waziri wa vijana na ajira Antony Mavunde alisema kuwa
wizara yake ipo tayari kuwasaidia vijana katika wilaya ya Kilolo
kwani tayari wameonyesha nia ya kujikwamua kiuchumi kupitia
kilimo cha nyanya na kuwa kazi ambayo mbunge na viongozi wa wilaya
ya Kilolo wanapaswa kuifanya ni kuwaunganisha vijana hao katika
vikundi na kuanzisha Saccos zao ili pesa itakapotolewa na serikali
kupitia katika saccos hiyo .
Alisema kuwa upo uwezekano wa
vijana hao kuanzisha kilimo cha nyanya na kuwa na viwanda
vidogo vya kuchakata nyanya na kuziuza badala ya sasa kuuza kwa
hasara.Mbunge wa Kilolo Bw. Mwamoto aliwapongeza mawaziri hao kwa kuonyesha utayari wao katika kuwasaidia wananchi wa Kilolo na kuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa mji wa Ilula ni maji ,masoko ya uhakika ya mazao na hivyo kusaidiwa maji na vijana kupata viwanda vidogo vidogo wataweza kukuza kilimo cha kisasa zaidi.
Katika
ziara yao hiyo bungeni wananchi hao ambao ni wawakilishi wa
wananchi wa Ilula waliongozana na katibu wa chama cha mapinduzi (ccm)
wilaya ya Kilolo Bw Clemence Mponzi na aliyekuwa diwani wa Ilula Anna
Msolla, Peter Mdanginyali , diwani wa kata ya Mlafu Bw Isdori Kihenge ,
Vicent Gaifalo,Anna
Msolla, kada wa hadema Bw Khalid Muhel , Jocob Ngusulu
,Uzebeo Mhando na katibu tarafa ya
Mazombe Bw. King’ung’e
Msolla, kada wa hadema Bw Khalid Muhel , Jocob Ngusulu
,Uzebeo Mhando na katibu tarafa ya
Mazombe Bw. King’ung’e
MAKAMPUNI 52 YAJITOKEZA KUWEKEZA SEKTA YA UMEME
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka
Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais
wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad, Idriss Debyo, Rais wa
Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do
Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema hadi sasa Serikali imekwishapokea maombi 52 kutoka makampuni
mbalimbali ambayo yanataka kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini
Tanzania.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo
jana jioni (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akizungumza na Watanzania
waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania
jijini Lusaka, Zambia.
“Haya maombi yamekwishapokelewa
na wenye makampuni wamekwishahojiwa kuangalia uwezo walionao katika
suala zima la uwekezaji wanaotaka kuufanya, na tukiwapata wenye uwezo na
wenye nia ya dhati watapatiwa miradi ya kuiendesha,” alisema.
Aliwataka Watanzania hao waishio
Zambia watumie fursa ya uwepo wao huko kutafuta marafiki ambao wanaweza
kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali nchini kwani Serikali peke yake
haiwezi kufanya kila kitu wakati wananchi wanahitaji kupatiwa huduma
muhimu.
“Serikali peke yake haiwezi
kufanya kazi ya uwekezaji kwa hiyo tunahitaji kushirikiana na sekta
binafsi, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo na ndiyo maana
kule kwenye mkutano nimewaeleza washiriki kwamba milango ya uwekezaji
Tanzania iko wazi.
Alisema kupatikana kwa umeme wa
uhakika kutawezesha wananchi wengi zaidi kujiingiza katika shughuli za
kiuchumi na hivyo kuinua uchumi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa
ujumla.
Alisema malengo ya Serikali ya
awamu ya tano ni kuona kuwa nchi inakuwa na mitambo mingi ya kuzalisha
umeme na umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo inaunganishwa na gridi
ya Taifa ili kuondokana na tatizo la mgao wa umeme nchini.
Alisema Tanzania ina vyanzo vingi
vya nishati vikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji,
upepo, nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy) na nishati
inayotokana na vinyesi vya mifugo (biomass) ambayo alisema vinatumika
kwa watu wachache (siyo kitaifa).
Alisema kupatikana kwa gesi
asilia nchini kumeleta neema ambapo mabomba ya gesi yamekwishajengwa
kutoka Mtwara hadi Kinyerezi na kutoka Kilwa-Songosongo hadi Dar es
Salaam. “Sasa hivi kuna utafiti unaendelea juu ya uwezekano wa kusambaza
gesi ya kupikia majumbani. Tumeanza pale Mikocheni (DSM) na sasa hivi
wanafanya utafiti mwingine kule Mtwara ili wananchi waweze kutumia gesi
hii kupikia badala ya mkaa,” alisema.
Akielezea kuhusu uwekezaji kwenye
makaa ya mawe, Waziri Mkuu alisema Serikali imelenga kutumia makaa ya
mawe ili kuendeshea mitambo ya kwenye viwanda vikubwa badala ya kutumia
umeme au mafuta ya dizeli kama inavyofanyika sasa. “Baadhi ya wenye
viwanda wanabadilisha mifumo ya kuendeshea mashine zao ili iweze
kuendana na teknolojia ya makaa ya mawe pindi tu uchimbaji ukishika
kasi,” alisema.
Akifafanua kuhusu juhudi za
Serikali katika kusambaza nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema tangu
kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), vijiji zaidi ya 3,000
katika ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vimefikiwa na nishati ya umeme.
“Tulianza na REA awamu ya kwanza,
awamu ya pili na sasa tunaenda awamu ya tatu. Hata mkipiga simu kwa
ndugu zenu vijijini, mtakuta katika kila kata kuna vijiji kati ya vinne
hadi vitano ambavyo vimefikiwa na nishati ya umeme kupitia mradi wa
REA,” alisema.
Waziri Mkuu amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).
PROF. MBARAWA AFUNGUA KIKAO CHA MPANGO KAZI – TEMESA
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka
Watendaji wakuu, Mameneja na Wazalishaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme
nchini (TEMESA), kutumia maarifa na taaluma zao ili kuboresha utendaji
kazi wa wakala huo na kuongeza mapato.
Akizungumza wakati
akifungua kikao kazi cha TEMESA Taifa mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa
amewataka watendaji wa temesa kubadili mfumo wa utendaji na kufanya kazi
kwa kuzingatia matokeo na faida.
“Tengenezeni magari 60 kwa siku muone namna mtakavyopata wateja wengi na kuongeza mapato”, amesema Prof. Mbarawa.
Kikao kazi hicho chenye
malengo ya kuboreshaj utendaji wa wakala huo kitajadili kwa kina
changamoto mbalimbali zinazoikabili TEMESA na kutengeneza mpango wa
kuboresha huduma zao.
“Tumieni elimu
mliyonayo kwa ajili ya maslahi ya watanzania na kuibadilisha TEMESA hii
kuwa ya tofauti na ya pekee”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa
amehimiza Wakala huo kuhakikisha wanadhibiti mapato na matumizi ya mfumo
wa kielektroniki kwenye vivuko vyote ili kukuza na kujiendesha kwa
vivuko vyenyewe.
Amesema mpaka sasa TEMESA ina jumla ya vivuko 27 lakini mapato yake bado yapo chini ya inavyotegemewa
na kushindwa kumudu hata matengenezo ya wakati ya vivuko hivyo.
na kushindwa kumudu hata matengenezo ya wakati ya vivuko hivyo.
Wakala huo pia
umesisitizwa juu ya usimamizi wa kina wa usalama wa vivuko na kanuni za
usafiri wa majini ili kuepuka ajali zinazotokana na uzembe wa kutofuata
kanuni na taratibu zilizowekwa.
“Andaeni kozi fupi kwa
ajili ya watumishi wanaosimamia vivuko na kuja na mikakati madhubuti ya
jinsi ya kuziepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika”, amesisitiza Prof.
Mbarawa.
Prof. MBARAWA amewataka
TEMESA kutengeneza magari yote ya serikali na kutafuta soko katika
magari ya watu binafsi ili kuongeza mapato na ufanisi kwa wakala huo.
“Bado mmelala,
hamjaamka, nataka temesa itengeneze magari yote ya serikali hadi
kufikia asilimia 65 ya matengenezo, tumieni fursa hii ya wizara yenye
taasisi nyingi ili kufanya biashara na kujilipa wenyewe na kwani
inajitosheleza kukua”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Ameongeza kuwa temesa
wamepewa rasiliamali zote hivyo ni lazima wafanye kazi na kujisimamia
wenyewe kwa kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza mahitaji ya watanzania.
Kwa upande wake Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase Ole
Kujan amemhakikishia Waziri kuandaa mikakati madhubuti ya kuikuza wakala
huo kwa kutoa huduma bora zinazolingana na thamani ya fedha yenyewe kwa
wateja wake.
Katika Hatua nyingine
Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa daraja la Ruvu chini katika
barabara ya Msata-Bagamoyo lenye urefu wa mita 140 na kumtaka Mkandarasi
Estim Construction kuhakikisha daraja hilo linakamilika ifikapo Oktoba
mwaka huu.
Aidha amemuagiza Meneja
wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Pwani Eng. Tumainieli
Sarakikya kuhakikisha kipande cha barabara kilichobakia katika barabara
ya Msata-Bagamoyo kinaunganishwa ifikapo Februari mwakani.
“Hakikisheni wananchi
hawavamii maeneo ya hifadhi ya barabara kwani kufanya hivyo ni kosa
kisheria na tutachukua hatua kali kwa watakaovunja sheria ya barabara”,
amesisitiza Waziri Mbarawa.
Zaidi ya Shilingi Bilioni 127 zimetumika katika ujenzi wa barabara ya Msata-Bagamoyo yenye urefu wa km 63.
BILIONI 8 KUTUMIKA KUBORESHA VYUO VYA AFYA NCHINI
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala.
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala.
………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa – Dodoma.
Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 8
kuboresha miundombinu ya vyuo vya Afya kote nchini katika mwaka wa fedha
2016/2017 ili kuwawezesha wanafunzi wa fani ya Afya kusoma katika mazingira mazuri.
kuboresha miundombinu ya vyuo vya Afya kote nchini katika mwaka wa fedha
2016/2017 ili kuwawezesha wanafunzi wa fani ya Afya kusoma katika mazingira mazuri.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali la Mbunge wa Muhambwe Mhe.Atashasta Justus Ntitiye, alieyata
kujua mkakati wa Serikali wa kuboresha vyuo vya Afya nchini hususan chuo cha
Uuguzi wilayani Kibondo kilicho katika jimboni lake.
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali la Mbunge wa Muhambwe Mhe.Atashasta Justus Ntitiye, alieyata
kujua mkakati wa Serikali wa kuboresha vyuo vya Afya nchini hususan chuo cha
Uuguzi wilayani Kibondo kilicho katika jimboni lake.
Dkt.Kigwangala amesema Serikali katika mwaka wa fedha
2016/2017 imejipanga kuboresha mazingira ya vyuo vya Afya katika maeneo
mbalimbali nchini kikiwemo Chuo cha Uuguzi Kibondo ambacho kimetengewa shilingi
milioni 680.
2016/2017 imejipanga kuboresha mazingira ya vyuo vya Afya katika maeneo
mbalimbali nchini kikiwemo Chuo cha Uuguzi Kibondo ambacho kimetengewa shilingi
milioni 680.
Aidha, ameeleza kuwa vyuo vya Afya vimekuwa
vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni ya wazabuni wa vyakula
waliokuwa wakiidai Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 6.8 kuanzia mwaka
2009 hadi 2015.
vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni ya wazabuni wa vyakula
waliokuwa wakiidai Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 6.8 kuanzia mwaka
2009 hadi 2015.
Amebainisha kuwa tayari Serikali imekwishahakiki madeni
yote ya wazabuni ili yaweze
kulipwa katika mwaka wa fedha 2016/2017
na kuongeza kuwa suala la usambazaji wa vyakula limeachwa chini Sekta binafsi
ili zifanye kazi hiyo.
yote ya wazabuni ili yaweze
kulipwa katika mwaka wa fedha 2016/2017
na kuongeza kuwa suala la usambazaji wa vyakula limeachwa chini Sekta binafsi
ili zifanye kazi hiyo.
Katika hatua nyingine Dkt.Kigwangala amesema Serikali
inaendelea kuangalia uwezekano wa kuyatumia majengo yaliyoachwa kwenye kambi za
wakimbizi zilizofungwa mkoani Kigoma hususan wilayani Kibondo ili yaweze
kutumika kama vyuo vya kutolea elimu ya Afya.
inaendelea kuangalia uwezekano wa kuyatumia majengo yaliyoachwa kwenye kambi za
wakimbizi zilizofungwa mkoani Kigoma hususan wilayani Kibondo ili yaweze
kutumika kama vyuo vya kutolea elimu ya Afya.
” Niko tayari nikishirikiana na waheshimiwa
wabunge kwenda mkoani Kigoma kuzungumza na viongozi wa mkoa huo ili tuweke
utaratibu wa namna ya kuyatumia majengo hayo” Amesisitiza Dkt.Kigwangala.
wabunge kwenda mkoani Kigoma kuzungumza na viongozi wa mkoa huo ili tuweke
utaratibu wa namna ya kuyatumia majengo hayo” Amesisitiza Dkt.Kigwangala.
Waimbaji nyimbo za ziinjili tutangaze injili tuache kuimba kwa biashara tu
Mwimbaji wa nyimbo za injili Ambwene Mwasongwe akiimba katika moja ya kazi zake za kumtumikia Bwana Yesu Kristo.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Waimbaji wa Nyimbo za Injili
nchini wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa kujitolea ikiwa kama sehemu ya
ibada ya kumtumikia Mungu kwa kulitangaza neno lake na si kugeuza kazi
hiyo kuwa mtaji wa biashara.
Hayo yamesemwa na Mwalimu wa
kwaya ya Wateule Elikana Simatiya kutoka kanisa la Anglikani, St. James
lililoko Tabata Segera jiijini Dar es Salaam, maarufu kama kunyata
nyata jina lililotokana na nyimbo ya kunyata nyata aliyoifundisha akiwa
kwaya ya Mennonite.
“Waimbaji wengi wa nyimbo za
injili wameacha kutumikia Mungu na badala yake wamekuwa wakiuunda
vikundi binafsi vya uimbaji ambavyo hutumika kama vyanzo vya fedha na
hualikwa kwenye mikutano ya injili na sherehe mbalimbali kwa malipo
maalum,” alisema Simatiya.
Aidha ameeleza kuwa, uimbaji wa
nyimbo za injili ni wito kama ulivyo wito wa uchungaji lakini hivi sasa
muimbaji wa injili akialikwa katika mikutano ya injili au sherehe huomba
malipo hadi ya shilingi milioni moja.
Simatiya aliongeza kuwa, ziko
gharama ambazo muimbaji anaweza kuomba kupewa kama usafiri kwa ajili ya
kumfikisha eneo husika au malazi na chakula ikiwa atahitajika kulala nje
ya makazi yake, lakini waimbaji wa leo wamebadilisha wito wa kutangaza
injili kwa njia ya uimbaji kuwa biashara.
Hivyo mwalimu huyo amewataka
waimbaji kubadilika kwa kuacha kuharibu kazi ya Mungu na kufanya kazi
hiyo kwa kujitolea kwani wapo wanaopokea uponyaji na wanaotiwa moyo
kupitia nyimbo za injili.
Kwaya ya Wateule inatarajia
kuzindua albamu mpya ijulikanayo kama Wateule tutakwenda siku ya
Jumapili Mei 29, 2016 Tabata Segerea katika kanisa la St. James, ambapo
mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul
Makonda,huku wakisindikizwa na waimbaji wa injili ambao ni Ambwene
Mwasongwe, Christina Shusho, Edson Mwasabwite pamoja na kwaya za
Anglikan kutoka Vingunguti na Ukonga.
TANESCO yawataka wateja wake kuunganishiwa umeme na mafundi waliosajiliwa.
Meneja wa Afya na Usalama kazini wa TANESCO, Mhandisi Majige Mabulla.
………………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Shirika la Umeme Tanzania Nchini
(TANESCO) limewataka wateja wake kuhakikisha wanaunganishiwa umeme na
mafundi au wakandarasi waliosajiliwa na shirika hilo ili kupunguza ajali
za moto.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini wa TANESCO, Mhandisi Majige
Mabulla alipokua akiongea na waandishi wa habari juu ya vyanzo vya ajali
za moto vinavyosababishwa na umeme.
Mhandisi Mabulla alisema kuwa
matukio ya moto yanayosababishwa na umeme hutokea kutokana na kuzalishwa
kwa joto kali ndani ya nyaya kunakosababishwa na umeme kuwa mkubwa
kuliko uwezo, kulegea kwa maungio ya nyaya pamoja na radi au nyaya za
umeme kuangukia juu ya paa la nyumba.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mabulla
aliongeza kuwa ajali za moto zinazosababishwa na umeme huanza kama
unavyoanza moto wa kiberiti au viwashio vinginevyo vya moto na husambaa
haraka kwa kutegemea na aina ya vitu vilivyopo kwenye eneo husika kwa
kuwa baadhi ya vitu hushika moto haraka na kuenea kwa kasi.
“Ajali za moto zinazosababishwa
na umeme ni ngumu kutokea kama umeme utasukwa na mtaalam aliyebobea
kwenye fani hiyo, TANESCO tunatoa wito kwa wateja wetu kuhakikisha
wanafungiwa umeme na fundi au mkandarasi aliyesajiliwa na kampuni
yetu,”alisema Mabulla.
Pia Mhandisi Mabulla alisema ili
kuepukana na ajali za moto zinazotokana na hitilafu za umeme wateja
wanapaswa ;kuepuka kupitisha nyaya za umeme juu ya paa za nyumba,
kutokuunganisha umeme kutoka nyumba moja kwenda nyingine bila kupata
maelekeza kutoka TANESCO.
Aidha Mhandisi Mabula alisema
wateja pia wanapaswa kuhakikisha mfumo wa umeme unapitiwa upya kila
baada ya miaka mitano pamoja na kuwa makini katika utumiaji wa vifaa
vinavyotumia umeme kama vile pasi, hita za umeme.
TANESCO yawataka wateja wake kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme
Meneja
wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi Kutoka Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Mhandisi Majige Mabula akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) ambapo aliwataka wateja wa shirika hilo kuzingatia sheria na
kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na
hitilafu za umeme.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Yasini
Silayo.
Baadhi ya Waandishi wahabari wakifuatilia mkutano huo. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
…………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Shirika la Umeme Tanzania
limewataka wateja wake kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme
ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini Mhandisi Majige
Mabulla wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Majige amesema kuwa moto hauwezi
kutokea endapo mtumiaji wa umeme atahakikisha kuwa mfumo wa umeme
katika nyumba yake umesukwa na fundi ama mkandarasi aliyesajiliwa.
“Kuwa makini katika matumizi bora
ya vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi,hita za umeme,kuchaji
simu,kompyuta kutasaidia kupunguza au kuondoa tatizo la majanga ya moto”
alisisitiza Mabulla.
Akizungumzia hatua nyingine
zinazoweza kusaidia kuzuia majanga ya moto Mhandisi Majige ni kuepuka
kuweka vitu vinavyoweza kushika moto kirahisi karibu na nyaya ama
maungio ya nyaya za umeme ndani ya nyumba .
Majige alitoa wito kwa watumiaji
wa umeme kutoa taarifa pale wanapotaka kuongeza matumizi ya umeme kwa
kiwango kikubwa ndani ya makazi ya watu ili tathmini ya uwezo wa nyaya
kukidhi mahitaji yaliyoongezeka ifanyike.
Katika kuzuia matukio ya moto
TANESCO imekuwa ikihakisha kuwa inamfikishia mteja umeme ulio salama na
usiokuwa na madhara kwa mtumiaji kutoka kwenye nguzo mpaka kwenye mita.
Kwa kipindi kirefu sasa
kumekuwepo na matukio ya ajali za moto katika makazi ya watu ambayo
yamekuwa yakisababisha madhara ikiwemo kusababisha vifo,majeruhi na
uharibifu wa mali.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA OMAN NCHINI TANZANIA LEO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Saud Ali Mohamed
Al-ruqaishi, wakati Balozi Saud alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais
Ikulu Dar es salaam leo Mei 25,2016 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza
muda wake wa kazi hapa Nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na kuzungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Saud
Ali Mohamed Al-ruqaishi, wakati Balozi Saud alipofika Ofisini kwa Makamu
wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Mei 25,2016 kwa ajili ya kuaga baada ya
kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. (Picha na OMR)
Kampuni ya Sta Tavel yaendelea kuwa suluhisho la usafiri kwa watanzania wanosoma nje ya nch
Na: Frank Shija, MAELEZO
Wanafunzi na vijana wakitanzania
kuendelea kunufaida na usafiri wa njia ya anga kwa gharama nafuu kupitia
Kampuni ya Sta Travel yenye maskami yake mtaa wa mtendeni manispa ya
Ilala jijini Dar es Salaam.
Hayo
yamebainishwa na Meneja
uendeshajji wa Kampuni hiyo Abass Takim alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari hii ofisini kwake jana.
Takim amesema kuwa watanzania
wanaosoma elimu ya juu nje ya nchi wanayofurusa ya kunufaiki na huduma
zaokwa kuwaunganisha na usafiri wa gharama ndogo zenye punguzo maalum za
kusafiri wakati wa kwenda na kurudi kutoka masomoni katika nchi
wanazosomea.
Takkim amesema kuwa taasisi yao
imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaopata fursa ya kusoma nje ya
nchi kwani wanatoa huduma ya usafiri ikiwa na punguzo maalum la gharama
za usafiri ili waweze kumudu gharama hizo, ambapo huduma hiyo ya
usafirishaji wa wanafunzi kwa gharama nafuu inaenda sambamba na huduma
za malazi kwa gharama nafuu wakati wa kwenda na kurudi,Bima ya safari
na Kitambulisho cha Kimataifa cha Mwanafunzi
Aliongeza kuwa mpaka sasa Taasisi
yake imetoa huduma ya hiyo kwa watanzania wengi hasa wanafunzi
wanaoenda kusoma katika vyuo vya Kuala Lumpar Malyasia, London
Uingereza, na Guangzhou China.
Aidha Abbas alisema kuwa pamoja
na kutoa huduma hiyo kwa watanzania kumekuwa na changamoto katika
upatikanajji wa Viza kwa wateja wao na kupelekea kujitokeza kwa
usumbufu, hata hivyo Sta Travel imekuwa ikijitahidi kuwasaidia wateja
wake ili wakamilishe taratibu zao kwa wakati.
Sta Travel niasasi inayojihusisha
na utoaji wa huduma ya kusafirisha wanafunzi kwa gharama nafuu ikiwa na
punguzo kwa lengo la kuwasaidia watanzania kufikia ndoto zao bila
kuwapo na kikwazo.
Katika kuhakikisha inafikia
wateja wake kwa urahisi zaidi Sta Travel imefungua zaidi ya matawi 400
katika nchi 100 dunia kote ambapo kwa Tanzania ofisi zake zinapatikana
katika mtaa wa Mtendeni, Kisutu (Posta),Takims Holidays / STA Travel
Partner mkabala na Supermarket ya Shrijee jijini Dar es Salaam unaweza
pia kuwasiliana nao kupitia simu namba +255 758 828384/85 au tembelea
tovuti yao http://www.escape-tanzania.com/
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA KAMATI YA UTENDAJI TASWA
KAMATI
ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) ilikutana Dar es Salaam Mei 24, 2016 kujadili masuala
mbalimbali.
A; Tuzo za Wanamichezo Bora
Kikao kilikubaliana Tuzo za
Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na TASWA, safari hii zifanyike
Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
TASWA imeuanda kamati maalum
kwa ajili ya kusimamia upatikanaji wa wanamichezo hao bora, kamati
ambayo inajumuisha waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari na wataalamu kutoka vyama mbalimbali vya michezo. Sekretarieti ya
TASWA inaendelea kufanya mawasiliano na wateule wa kamati hiyo kabla ya
kuwatangaza.
Kwa kawaida kila mwaka TASWA
inatoa tuzo kwa wanamichezo bora wa kila mchezo na pia kunakuwa na
mwanamichezo bora wa jumla kwa mwaka husika.
Baadhi ya waliopata kutwaa tuzo
ya Mwanamichezo Bora Tanzania wa jumla kwa miaka kumi iliyopia na miaka
yao katika mabano ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007) na
Mary Naali (2008) wote wanariadha.
Mwaka 2009 tuzo ilienda kwa
mcheza netiboli Mwanaidi Hassan, ambaye pia alitwaa tuzo hiyo mwaka
2010, wakati mwaka 2011, ambapo tuzo yake ilitolewa mwaka 2012 mshindi
alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe. Mwaka 2013/2014 ilienda kwa mwanasoka
Sheridah Boniface.
Mwaka 2015 tuzo ilifanyika
katika aina nyingine, ambapo walizawadiwa wanamichezo 10 tu waliofanya
vizuri zaidi katika miaka 10 ya urais wa Jakaya Kikwete na pia TASWA
ilitoa Tuzo ya Heshima kwa Kikwete.
B; Media Day
Kama inavyojulikana chama chetu
kimekuwa kikiandaa bonanza maalum likihusisha waandishi na wafanyakazi
wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, lakini kwa miaka miwili
bonanza hilo limekwama kufanyika kutokana na sababu mbalimbali. Kikao
kimekubaliana nguvu zaidi ielekezwe ili jambo hilo lifanyike na kuwapa
raha wadau. Taarifa zaidi kuhusu Media Day itatolewa Jumamosi wiki hii.
C: Changamoto kwa waandishi
Kikao kilijadili changamoto
mbalimbali zinazowakabili waandishi wa habari za michezo na chama kwa
ujumla, ambazo zimewekewa mikakati ya muda mfupi na mrefu na utekelezaji
wake utaanza kuonekana siku chache zijazo.
MACHINGA, MFUPA ULIOISHINDIKA HALMASHAURI YA JIJI MWANZA
Ipo
kauli isemayo “Mfupa Uliomshinda Fisi” ikiashiria jambo gumu mithiri ya
mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyama bingwa wa kutafuna
mifupa ya kila aina.
Ndivyo
unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa
wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini
Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri
ya jiji la Mwanza.
Mara
kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka
wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya
biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake
umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu
licha ya nguvu kubwa kutumika.
Kabla
ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji
la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi
lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya
ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la
mwanza machinga wamezagaa ovyo.
Baadhi ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa
maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia
kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa
wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.
maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia
kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa
wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.
No comments :
Post a Comment