Pages

Wednesday, May 25, 2016

Geneva:Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo

um01 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaoendela nchini Geneva-Uswisi
um1 
Waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu kulia,Waziri wa afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Kombo wa nne kutoka kulia na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk Ulisubisya Mpoki kushoto pamoja na wajumbe wengine wa mkutano huo wakifurahia jambo.
um2 
Waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu kushoto akiwa na waziri wa afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Kombo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye mkutano huo unaowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa shirika la afya duniani(WHO),nyuma yao ni katibu mkuu wizara ya afya Tanzania bara dkt.Mpoki Ulisubisya
……………………………………………………………………………………..
Mwandishi maalum-Geneva
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Hayo yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.
Ummy alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000
Aidha, mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.
“Ninaeleza kwa masikitiko kuhusu tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliopo nchini Tanzania ambapo hadi kufikia tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia 21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi Serikali kupitia wizara ya afya itaimarisha na kuzingatia kanuni za afya ya mazingira katika kukabiliana na ugonjwa huu”alisema
Kwa upande wa kutokomeza malaria waziri Ummy alisema Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa hadi kufikia asilimia 0.6 .
Katika kuboresha huduma za afya nchini alisema Serikali ya Tanzania imejipanga na kuhakikisha itaboresha huduma za afya ziweze kumfikia kila mtanzania popote alipo, “ili kuweza kufikia malengo haya ni wakati muhimu sasa kuwekeza zaidi katika sekta hii kwa kuongeza uwekezaji katika raslimali fedha,watu pamoja na kuboresha miundombinu ikiwemo utoaji wa huduma za afya nchini”.
Waziri Ummy alisema katika kufikia mafanikio ,wizara ya afya inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016 wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa mwananchi katika kupata huduma za matibabu wakati wowote anapokuwa na fedha au kutokuwa na fedha kwa kuwa maradhi hayachagui wakati.
Mkutano mkuu wa mwaka wa Afya Duniani hufanyika nchini Geneva –Uswis kila mwaka mwezi mei ambao huwakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Shirika la afya Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na wadau,mashirika na taasisi zinazoshiriki katika kutoa huduma za afya Duniani.Tanzania inawakilishwa na waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy mwalimu na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo.

VIONGOZI WA AFRIKA WATAKA USHIRIKIANO ZAIDI

index  
 Ni katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
WAKUU wa nchi za Afrika wametaka kuwepo na juhudi za pamoja katika kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabiachi yanayolikumba bara hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati wa majadiliano baina ya viongozi kutoka Zambia, Chad, Nigeria, Msumbiji na Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi, jijini Lusaka, Zambia.
Wakishiriki kwenye mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, viongozi hao walisema bara la Afrika linahitaji kupata maendeleo zaidi licha ya tatizo la nishati linalolikumba bara hilo hivi sasa.
Akichangia mjadala huo, Rais wa Zambia, Bw. Edgar Lungu alisema nchi yake imepania kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme vijijini lakini imekuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa mvua kwa zaidi ya miaka miwili hali ambayo alisema imechangia kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi nchini humo.
“Uhaba wa mvua umepunguza kiwango cha maji katika bwawa la Kariba ambalo hutumika kuzalisha umeme nchini mwetu. Na hapa kwetu, karibu asilimia 80 ya umeme wetu, unategemea uzalishaji wa umeme kutokana na vyanzo vya maji,”  alisema.
Rais wa Chad, Bw. Idriss Deby Itno aliitaka benki ya AfDB ichukue nafasi ya mdau mkuu kwenye uwekezaji wa sekta ya nishati na kuzisadia nchi za bara hili kupata mitaji ya uwekezaji na ushauri wa kitaalamu.
“Tunahitaji kutumia fursa ambazo benki yetu inazo katika kukabilianana changamato za ukosefu wa nishati. Tukiweza kutekeleza jambo hilo, tutafanikiwa kuwa na miradi ambayo ni makini na kwa maana hiyo tutaweza kuliangaza bara letu la Afrika kwa kupata mwanga wa uhakika,” alisema.
Kwa upande wake, Makamiu wa Rais wa Nigeria, Prof, Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika halina budi budi kuweka kipaumbele kwenye masuala ya maendeleo yake wakati likitafuta suluhisho la kukabiliana na athari za mazingira.
“Tunapaswa kutafuta njia za kubalance mahitaji makubwa ya umeme ambayo bara letu linakabiliwa nayo dhidi ya athari za kimazingira ambazo zinapigiwa kelele na mataifa makuna na zinahatarisha kutunyima fursa ya kuendelea haraka kama ilivyokuwa kwao,” alisema na kuongeza:
“Kama nchi zilizoendelea zinataka sana kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi, zinatakiwa zitupatie fedha, teknolojia na wataalamu ambao watasaidia kuendesha mitambo ili tupate nishati safi kutokana na mafuta ya petroli na dizeli sababu ni rasilmali ambazo tunazo.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema ili kuondokana na tatizo la nishati, kuna haja ya kuwa na viongozi wenye utashi wa kisiasa ambao watakuwa tayari kuruhusu uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya nishati na kuongeza kuwa Tanzania inapitia upya sheria zake ili kuruhusu miradi mikubwa ya uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi kwa ajili ya wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye sekta hiyo na kutaja fursa ambazo Tanzania inazo kwenye sekta ya nishati ikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo na nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy).
Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema kuna haja ya kuwa na taasisi ya uzalishaji na ugawaji umeme ya pamoja (electricity pool) ambayo itaruhusu wazalishaji wa umeme wawauzie wanunuzi wakubwa.
Waziri Mkuu ambaye yuko Lusaka kuhudhuria mkutano huo wa ADB kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

Darbrew yapata tuzo ya uboreshaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller

1Mkurugenzi wa kampuni ya  Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason  akiongea na wafanyakazi wakati ya hafla ya kusherehekea kushinda  tuzo ya uendelezaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller  iliyofanyika kiwandani hapo jana.
2Wafanyakazi wakifuatilia matukio
3 
Maofisa waandamizi wa kampuni wakati wa sherehe hiyo.
4 5Mkurugenzi na wafanyakazi wakifurahia tuzo.
6Wafanyakazi katika picha ya pamoja.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya Darbrew inayotengeneza pombe ya Chibuku imetunukiwa  tuzo kutoka SABMiller  ya uendelezaji vinywaji vya asili nchini katika kongamano la masoko la viwanda  lililofanyika mjini Cape Town nchini Afrika ya Kusini.
Darbrew iliyopo chini ya TBL Group iliibuka kidedea baada ya kushindanishwa na viwanda vinavyotengeneza vinywaji vya kienyeji vilivyopo chini ya SABMiller vilivyopo katika nchi za Botswana,Malawi na Uganda.
Akitangaza mafanikio hayo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi Mkuu wa Darbrew, David Cason alisema kuwa tuzo hiyo ni mafanikio makubwa kwa kampuni na aliwapongeza wafanyakazi wote kwa kujituma na kuhakikisha yanapatikana mafanikio siku hadi siku.
“Tuzo hii sio ya mtu mmoja imepatikana kutokana na mchango wa kila mfanyakazi wa DarBrew na inabidi kuongeza bidii zaidi katika kazi ili mafanikio zaidi yapatikane na kampuni izidi kusonga mbele na kuwa miongoni mwa makampuni makubwa ya vinywaji katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”.Alisema Cason.
Alisema hatua ya kampuni kushindanishwa na viwanda vikubwa na kuibuka na tuzo ni jambo la kujivunia kila mfanyakazi  na aliwashukuru mawakala na wateja wote wa Chibuku kwa kuunga mkono biashara ya kampuni.
Kwa upande wake Meneja wa Mauzo wa DarBrew,Freddy Kazindongo alisema aliwapongeza wafanyakazi na kuwashukuru wateja kwa mafanikio yaliyopatikana na kuongeza kuwa kampuni imejizatiti kuongeza zaidi ubora wa huduma za uzalishaji na usambazaji na kuhakikisha kinywaji cha Chibuku kinawafikia wananchi popote walipo na wanakipata kulingana na kila mtu na uwezo wake .
Katika kuthibitisha hilo alisema wiki hii kampuni imezindua chibuku super ya mililita 750 ambayo itawawezesha wateja kupata  kinywaji  hicho kwa gharama nafuu.
Kazindogo alisema mkakati wa kampuni ni kuhakikisha  urasimishaji wa pombe za kienyeji unafanikiwa ambapo wananchi wataweza kupata kinywaji cha asili katika mazingira bora ya usafi wakati huohuo wakikinunua wanachanga pato la serikali kwa njia ya kodi kitu ambacho hakipo kwa pombe nyingine za asili.
Pia alisema kuwa kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja  ambazo zinawawezesha mawakala wakubwa na wadogo na akina mama wanaouza pombe za asili kujipatia mapato ya uendesha maisha vilevile kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na akina mama waliokuwa wanapika pombe za asili kwa kutumia kuni na mkaa watakuwa wanauza pombe ambayo tayari imetengenezwa badala ya kutumia muda mwingi kutengeneza pombe.

Wataka EU na AU kutoshiriki katika mazungumzo ya amani ya Burundi

buj1
Jiji la Bujumbura linavyoonekana katika picha.
………………………………………………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Vyama tisa vya upinzani vilivyoshiriki  uchaguzi wa Burundi  wa mwaka 2015 na ambavyo vinashiriki mazungumzo ya kutafuta amani ya Burundi vimetaka wawakilishi wa  umoja wa Ulaya  na Umoja wa Afrika kutoshiriki katika mazungumzo ya amani ya Burundi.
Viongozi wa vyama hivyo kwa pamoja wanasema kuwa  wawakilishi wa taasisi hizo wameonyesha kuegemea upande katika mgogoro wa Burundi kufuatia msimo wao wa kutaka chama cha CNARED ambayo wanadai imeshiriki katika vurugu na mauaji nchini Burundi kushiriki katika mazungumzo hayo.
Katika taarifa yao ilitiwa sahihi  na viongozi wote tisa  wa vyama hivyo ,wamesema kutokana na lugha  na misimamo ya wawakilishi hao wa taasisi za juu  ni wazi wataharibu mchakato huo unaoendelea wa n kutafuta amani ya Burundi.
Taaarifa iliyotolewa na viongozi wa vyama hivyo baada ya kumalizika mazungumzo  ya awali ,viongozi hao wamemtaka msuluhishi wa mgogoro huo Rais  mstaafu wa Tanzania  kutokukubalina  na wawakilishi hao na kushirikisha pande zote zenye masilahi na mgogoro wa Burundi. 
“Tunamtaka msuluhishi alione hili  na kuonya taasisi hizo kuacha propaganda za kuwagawa Warundi katika mgogoro huo “taaarifa hiyo ilisema .
Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa Burundi itizamwe kama serikali halali iliyochaguliwa na wananchi na haipaswi kuingiliwa uhuru wake na watu ama taasisi za nje.
Aidha taarifa hiyo ilivitaja vyama hivyo kuwa ni UPRONA ,FNL,FNL IRYAGIRAGAHUTU,RADEBU,zingine ni RADEBU,FLORINA,MSPINKINZO Y’IJAMBO ,PMP,PRP na PIEBU.
Na katika hatua nyingine akifunga mazungumzo hayo ya awali msuluhishi wa mgogoro huo Rais Benjamen Mkapa ameeleza kuridhishwa na jinsi wajumbe wa mazungumzo hayo walivyoshiriki mazungumzo hayo ya awali kwa dhati na kuonyesha nia kutaka amani katika taifa lao.
“Nimeguswa na namna mlivyoonyesha katika fikra na mawazo yenu ,mmeonyesha uzalendo mkubwa kwa kuonyesha madhara ya mgogoro katika nchi yenu kiuchumi na maisha ya watu  yanayoharibiwa na mgogoro huo”Alisema Mkapa .
Mkapa ambaye anafanya usuluhishi huo chini ya rais Yoweri Mseveni aliyeteuliwa na marais wa Afrika mashariki kutatua mgogoro alishukuru uwepo uwepo wa taasisi za kimataifa na za kikanda katika mazungumzo hayo.
Aidha rais Mkapa aliwaambia wajumbe  wa mkutano  huo kwa muda wa wiki tatu zijazo atahakikisha kuwa anafanya mazungumzo na makundi mengine ambayo yalialikwa lakini hayakuweza kufika Arusha kutoa maoni yao kuhusu utatuzi wa mgogoro wa nchi yao

MAONYESHO YA BIDHAA ZA PLASTIKI, KUFANYIKA MEI 27-29 MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni kuhusu maonyesho hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Hamza Mohamed Hamza akizungumza katika mkutano huo.
Taswira meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Africa-PPB Tanzania, Mohamed Sami akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Khaled Abu El M karem akizungumza kwenye mkutano huo.
………………………………………………………………………………..
Na Doto Mwaibale
 
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza  ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi  yanayotarajiwa kufanyika katika  Mei 27 hadi 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat,  alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zitashiriki katika maonesho hayo.
Alisema Maonesho ya Afrika –PPB-EXPRO yatakuwa ni jukwaa la kipekee la bidhaa mpya  na yatatoa mwanya wa kuyaelewa  masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.
 “Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la  kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara  kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika  kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha  kuwa Tanzania ni ya kwanza  katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.
“Aramex Africa ni mshirika rasmi wa usafirishaji wa Africa-PBB-EXPO na itakwua inatoa mchango mkubwa katika kutoa huduma za ugavi na usafirishaji  kutoka Misri hadi Tanzania,” alisema.
Alisema kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO  inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji  walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.
Alieleza kwamba kanzidata hizo zinajumuisha hali ilivyo ndani ya soko la Tanzania na thamani yake pamoja na takwimu sahihi ya kuuza na kuagiza, hii inatoa  fursa ya uhakika kwa mikutano ya mkakati ya B2B pamoja na ufanisi unaohusiana pindi zinapofika.
Barakat alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili kuweza  ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara. 
“Kwa kushiriki katika maonesho ya Africa-PPB-EXPO, pamoja na mambo mengine washiriki watajifunza jinsi maudhui ya kina ya sekta yanaweza kuathiri biashara zao,  umoja uliopo miongoni mwa viongozi wa sekta, kupata washirika wapya na kulinganisha kiwango chao katika mitazamo ya ubunifu.
“Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya  usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika  kuandaa na kutoa huduma kwa maonesho ya  biashara ya kimataifa  pamoja na 
kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
 Alisema kwamba maonesho mengine  ya Africa-PPB-EXPO yanatarajiwa kufanyika nchini Senegal na baadaye nchini Angola.

Yanga walivyopokea Kombe lao la pili kwa kuifunga Azam FC BAO 3-1 UWANJA WA Taifa

MMG_6402 copy 
Rais wa Shirikisho la soka nchini, Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Shirikisho (ASFC), Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub, mara baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuichapa Timu ya Azam FC, Bao 3-1, katika mchezo uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es salaam. 
MMG_6429 copy Wachezaji wa Timu ya Yanga pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Picha kwa hisani ya  Michuziblog.

RAIS DKT.MAGUFULI MGENI RASMI Mkutano wa CRB

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
TZTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Nchini (CRB) kesho tarehe 26 Mei, 2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa mwaka wa mashauriano na wadau wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi unatarajiwa kuhudhuriwa na  zaidi ya Makandarasi na wadau wa Sekta ya Ujenzi wapatao 1000 na utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26 Mei, 2016 hadi tarehe 27 Mei 20l6.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Juhudi za Makusudi za Kukuza Uwezo wa Makandarasi Wazalendo kwa Maendeleo Endelevu ya Kiuchumi; Changamoto na Mustakabali Wake’.
Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau wa Bodi ya Usajili Makandarasi na Sekta ya Ujenzi ili kujadili changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kuwajengea uwezo Makandarasi Wazalendo.
Imetolewa; Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
25 Mei, 2016

RAIS DkT Shein Alekea Nchini Comoro Kuhudhuria sherehe za Kumuapisha Rais Mteule wa Comoro.

1 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Wazee na Viongozi wa Serikali, wakati akiondoka Zanzibar kuelekea Nchini Comoro kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteuli wa Muungano wa Visiwa vha Comoro akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
2 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangana na Viongozi wa Serikali, waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kumuaga akielekea Nchini Conoro kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteule wac Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe.Azali Assouman Boinakher.
3 4 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assouman Boinakher. akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
(Picha na Ikulu)

RAIS DKT.MAGUFULI AMTEUA WAZIRI MKUU MSITAAFU MIZENGO PINDA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA OUT

IMG-20160525-WA0018

Tanzania yapiga hatua kubwa katika matumizi ya huduma za mitandao

TC3 
Kaimu Mkurugenzi Mamlakaya Mawasiliano Tanzania(TCRA)Mhandishi James Kilaba. 
……………………………………………………………………………………………….
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika sekta ya mawasiliano  hadi kufikia kuwa kwenye kundi la  nchi zilizoendelea kimawasiliano Duniani.
Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania takribani milioni 39 wana laini za simu za kiganjani pamoja na watumiaji wa intaneti takribani milioni 20 ambapo miaka ya nyuma idadi ya laini za simu za kiganjani zilikuwa 2,963,737.
Haya ni maendeleo makubwa yanayoifanya Tanzania kuwa nchi bora kwa upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba alisikika akisema kwamba,”Ukuaji wa kasi wa sekta ya mawasiliano nchini umechangia sio tu katika kuboresha maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi bali unachangia sana katika kuinua pato la Taifa”.
Ukuaji huu umetokana na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za mawasiliano.
Kama wasemavyo wahenga kuwa ya Kaisari tumpe Kaisari basi sifa zote ziwaendee Mamlaka ya

WATANZANIA KUWAPUUZA WAONABEZA JUHUDI ZA RAIS JOHN MAGUFULI- DKT. KONDO

1 
Na Anitha Jonas – MAELEZO
……………………………………….
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Dkt.Haruni Kondo amewasihi Watanzania kuwapuuza waonabeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Dkt. Kondo ametoa wosia huo alipokuwa akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo kuhusu jitihada mbalimbali anazozifanya Rais katika kupambana na ufisadi, rushwa pamoja na kudhibiti nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.
“Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akifanya jitihada za kujenga taifa na kuleta maendeleo kwa Watanzania bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, rangi au jinsia, hivyo ni vyema tumuunge mkono kwa kumuombea ili aendelee kuwa na ujasiri huo, hekima na busara katika kufanya kazi yake,”alisema Dkt.Kondo.
Mjumbe huyo NEC ya CCM alisema ni vyema Watanzania wakajitathimini kwa kuangalia tulipotoka na tulipo na wapi tunaelekea ikiwa lengo la Rais ni kunyanyua uchumi wa taifa na nchi kuwa ya viwanda kwa kutumia rasilimali za nchi.
Mbali na hayo Dkt. Kondo alisema Watanzania hawana budi kumuunga mkono Dkt Magufuli katika kupambana na kundi la watu wachache wanaopinga juhudi zake huku nia ikiwa ni kuikomboa nchi kuepuka kuwa miongoni mwa nchi tegemezi duniani.
Dkt. Kondo alisisitiza kwa kusema kuwa Tanzania imejaa rasilimali nyingi ikiwemo Madini, Mbuga za wanyama pamoja na ardhi yenye rutuba hivyo rasilimali hizo zikisimamiwa vizuri na kila mtu akiwajibika kwa nafasi yake hakika nchi itabadilika.
“Hata hivyo suala la kukuza uchumi wa Taifa bado uko mikononi mwa Watanzania wenyewe hivyo wananchi wote wasikate tamaa kwa maana “Penye nia Pana Njia” alisema Dkt.Kondo.
Alisema madudu yaliyoibuliwa na kufichuliwa na Rais Dkt. Magufuli katika baadhi ya taasisi za umma ni kielelezo tosha kinachobainisha hatua ya ubadhirifu, wizi na utapeli ulioikumba Tanzania.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA.

b7 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo  akiingia ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
b5 
Mbunge wa Viti Maalum CCM , Mhe. Halima Bulembo akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
b4 
Mbunge wa Bukoba Mjini CHADEMA , Mhe. Wilfred Lwakatare akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
b3 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiingia ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
b6 
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina (kushoto)  akiwa ameongozana na Wabunge wenzie  wakielekea ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
b1 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiwasili katika Viwanja vya Bunge leo Bungeni mjini Dodoma 25 mEI, 2016.
b2 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (kushoto) akiwa ameongozana na Wabunge wenzie  wakielekea ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 25 Mei, 2016.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, DODOMA.

MATUKIO YA BUNGE NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO

 Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini (CCM) Mhe. Allya Kessy akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
 Mwekekezaji na Msambazaji wa nguzo za umeme nchini kutoka Kampuni ya New Forest iliyoko mkoani Iringa akiwaonesha jambo Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe. Ally Kessy (kushoto) na Mbunge wa jimbo laKilolo Mhe. Venance Mwamoto kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani waifuatilia hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani
waifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi akifuatilia kwa makini mjadala wa Waheshimiwa Wabunge wakati wa kipindi cha maswali na Majibu.
 Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Esther Bulaya akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
 Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Wananchi kutoka jamii ya Wafugaji waliohudhuria kikao cha Bunge leo mjini Dodoma kushuhudia Michango ya Wabunge wakati wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma leo.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya (kulia) na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Elisha Eliya leo mjini Dodoma.
Picha/Aron Msigwa – MAELEZO

DK. PINDI CHANA AKUTANA NA VIONGOZI WA UHURU PUBLICATIONS LTD NA PEOPLES MEDIA LEO

 Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, akisalimiana na Meneja Rasilimali watu wa zamani wa Uhuru Publications Ltd, Lucas Kisasa, baada ya kumkuta nje wakati akienda ofisi za kampuni hiyo leo kujitambulisha kwa viongozi wa Kampuni hiyo ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na viongozi wa Peoples Media Ltd ya Uhuru FM, leo. Kulia ni mpigapicha wa Magazeti ya Uhuru, Emmanuel Ndege na Wapili ni dereva wa UPL Chamlungu
 Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Peoples Media, Angel Akilimali, alipowasili kujitambulisha kwa viongozi wa  Kampuni hiyo ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na viongozi wa Peoples Media Ltd ya Uhuru FM, leo.
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, akisalimiana na Kaimu Meneja Rasilimali watu na Utawala, Paul Mg’ong’o, alipowasili kujitambulisha kwa viongozi wa Kampuni hiyo ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na viongozi wa Peoples Media Ltd ya Uhuru FM,
 Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (wapili kushoto) akifuatana na viongozi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Paul Mg’ong’o (kulia) na  na Angel Akilimali wa Peoples Media Ltd ya Uhuru FM, Kushoto ni Ofisa kutoka Makao Makuu ya CCM, Amos Siyantemi
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (wapili kushoto) akifuatana na viongozi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Paul Mg’ong’o (kulia) na  na Angel Akilimali wa Peoples Media Ltd ya Uhuru FM, Kushoto ni Ofisa kutoka Makao Makuu ya CCM, Amos Siyantemi
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  akisalimiana na Kaimu Mhasibu Mkuu wa UPL Mama Masota
 Baadhi ya viongozi wa UPL na Peoples Media wakimsubiri Dk. Pindi Chana
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akisoma nakala ya gazeti la Uhuru la leo, kabla ya mazungumzo na viongozi hao
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akimsalimia Mhariri wa Habari wa Uhuru FM Pius Ntiga. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Ramadhani Mkoma
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza mazungumzo yake na viongozi hao. Kulia ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UPL Ramadhani Mkoma na Kushoto ni Kaimu Mkueugenzi wa Peoples Media Angel Akilimali
 Ofisa wa Chama kutoka Makao Makuu ya CCM, Amos Siyantemi akitoa maneno ya utangulizi kabla ya Dk. Pindi Chana kuzungumza na viongozi hao
 Kaimu Mkurugenzi wa Peoples Media Angel Akilimali akijitambulisha 
 Kaimu Meneja Rasilimali watu na Utumishi Paul Mg’ong’o akijitambulisha
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizungumza na viongozi hao.
Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizungumza na viongozi hao.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MATUKIO YA BUNGE NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO

 Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini (CCM) Mhe. Allya Kessy akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
 Mwekekezaji na Msambazaji wa nguzo za umeme nchini kutoka Kampuni ya New Forest iliyoko mkoani Iringa akiwaonesha jambo Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe. Ally Kessy (kushoto) na Mbunge wa jimbo laKilolo Mhe. Venance Mwamoto kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani waifuatilia hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani
waifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi akifuatilia kwa makini mjadala wa Waheshimiwa Wabunge wakati wa kipindi cha maswali na Majibu.
 Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Esther Bulaya akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
 Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Wananchi kutoka jamii ya Wafugaji waliohudhuria kikao cha Bunge leo mjini Dodoma kushuhudia Michango ya Wabunge wakati wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya (kulia) na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Elisha Eliya leo mjini Dodoma.
Picha/Aron Msigwa – MAELEZO
 

Serikali yaadhimisha siku ya Afrika kwa kumuenzi nguli mpigania uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta

kal1 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kulia) akiongoza msafara wa ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuzuru Kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta katika kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni  Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro na kushoto ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
kal2 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Halfan Mshiro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema wakiokota baadhi ya uchafu katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta walipozuru kaburi hilo katika kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi na kulia ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
kal3 
Mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi (watatu kulia) akiongoza dua ya kumuombea baba yake hayati sheikh Kaluta Amri Abeid wakati ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
kal4 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kushotombele) akizungumza wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro.
kal5 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Halfan Mshiro (kulia) akizungumzia siku ya Afrika alipozuru katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta  kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. kushoto mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema.
kal6 
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa Dkt. Suleimani Sewangi (mwenye miwani) akisoma tawasifu ya hayati Sheikh Kaluta Amri Abeid  Kaluta wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
kal7 
Bw. Kassim Amotile (mwenye miwani) akigani Shairi lililoandikwa na marehemu Mathias Mnyampala mwaka 1964 wakati wa kifo cha hayati Sheikh Kaluta Amri Abeid Kaluta na kulipa jina la Kifo cha Sheikh Abeid, Pengo kuu kwa Taifa wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo Bibi Nuru Halfan Mrisho

Serikali yawezesha vikundi 1,200 vya wakulima kupata masoko.

index 
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………….
Serikali imefanikiwa kuwezesha vikundi 1200 vya wakulima wadogo wadogo nchini ili kupata masoko ya uhakika ya mazao yao wanayozalisha.
Akizungumza kuhusu mradi wa kuboresha miundombinu ya masoko,uongezaji wa thamani na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) Mratibu wa Taifa wa Mradi huo Bw. Walter Swai amesema malengo ya mradi huo ni kuongeza kipato cha wakulima na uhakika wa chakula kwa kutengeneza miundombinu ya upatikanaji wa masoko kwa wakulima kwa kuboresha barabara za kutoka mashambani kuelekea sokoni na kuwapa taarifa sahihi kuhusu masoko na mahitaji yake.
Bw Walter Swai ameongeza kuwa lengo la mradi ni kufikia vikundi 1,600 kwa nchi nzima katika kutoa elimu ya kuwezesha wakulima kupata masoko ya mazao yao ikiwa ni jitihada za Serikali kuwawezesha wakulima hao kujikwamua kiuchumi.
“Nia yetu ni kufikia vikundi 1,600 katika mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na hadi sasa tumefika asilimia 75 ya lengo tulilojiwekea la kuwawezesha wakulima wadogo kupata masoko ya mazao yao” alisema Bw.Swai.
Naye Mtaalamu wa Masoko ya mazao ya kilimo wa MIVARF Bw. Muhoni Leonard amesema kuwa mradi huo utasaidia kuwapa wakulima taarifa sahihi juu ya masoko na mahitaji yake na kupunguza gharama ambazo zilikuwa zinatumika kwa ajili ya kupata taarifa hizo kutoka kwa madalali.
“Azma ya mradi huu ni kubadili muundo na utendaji wa wakulima wadogo kuongeza ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji wa masoko ya mazao husika” alisistiza Bw Leonard.
Aidha, mmoja wa wakulima na msindikaji wa mchele kutoka Wilaya ya Chato mkoani Geita Bw.Joseph Nchimani amesema kuwa elimu aliyoipata kutoka MIVARF imemuwezesha kuendesha kilimo cha mpunga kwa njia ya kisasa ambayo imemuwezesha kuongeza thamani ya mchele kwa kuufunga kwenye mifuko iliyo katika hali ya
ubora unaokubalika kwenye soko.
“Kabla ya kuanza kufunga mchele kwenye mifuko nilikuwa nauza jumla ya tani mbili mpaka kumi kwa mwaka ila baada ya MIVARF kuja na kunipa elimu hii nimeweza kuuza mpaka kufikia tani 50 kwa mwaka” alisistiza Bw.Nchimani.
Program hiyo ya MIVARF inajushughulisha pia na kutoa huduma za kifedha vijijini ambayo ni ya miaka saba inayotekelezwa kwa mikoa 30 ya Tanzania Bara na Visiwani na inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

AHADI YA RAIS JPM KUHUSU MAJI MJI WA ILULA KUTEKELEZWA -WAZIRI LWENGE

Bw Venance Mwamoto
…………………………………………………………………………………………..
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI  wa maji na  umwagiliaji mhadisi Geryson Lwenge amewaondoa  hofu   wananchi  wa  mji  wa Ilula  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa kuhusu  ahadi  ya Rais Dr John Magufuli ya  kumaliza kero ya  maji  katika  mji  huo  wa Ilula kuwa  itaanza kutekelezwa mwaka  huu.
Alisema  kuwa serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dr Magufuli  ni  serikali ya ukweli na  uwazi na ni  serikali ya  hapa  kazi Tu  hivyo kila ilichoahidi  kukifanya  itafanya kwa  wakati na  kuwataka  wananchi  kuendelea kujenga  imani  zaidi.
 
Waziri mhandisi  Lwenge aliyasema  hayo jana katika Mgahawa wa Bunge mjini  Dodoma , wakati  akizungumza katika  kikao chake na mbunge wa  jimbo la Kilolo Venance Mwamoto na mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati na wawakilishi   11 wa wananchi  wa mji  wa Ilula waliofika bungeni  mjini Dodoma kufuatilia ahadi ya maji  iliyotolewa na Rais Dr  Magufuli  wakati wa kampeni kwa wananchi  wa mji  wa Ilula .  
 Mwamoto  akishiriki na  wananchi wa mji wa Ilula  kukingas maji ambayo hutoka kwa mgao 
………………………………………………………………………………………………
Alisema  kuwa wizara  yake  imekwisha  ingiza  katika bajeti  yake ya mwaka 2016/2017 itakayosomwa mapema wiki  hii na  kuwa mbali ya  maeneo  mengine ambayo  yatapatiwa ufumbuzi  wa  kero ya maji mji  wa Ilula ni  miongoni mwa maeneo  hayo .
Waziri  huyo  alisema  kuwa lengo la  serikali ni  kuendelea  kusogeza  huduma ya  maji kwa  wananchi  wake na  kutekeleza ahadi  zake kupitia  ilani ya uchaguzi ya  chama tawala hivyo.
Hata  hivyo  waziri Lwenge  alimpongeza mbunge  wa Kilolo Bw Mwamoto na mbunge Kabati  kwa kuendelea  kupambana  bungeni kwa ajili ya kuwatumikia  wananchi  wao na  hata   kufuatilia baadhi ya ahadi  na  kuwa hatua hiyo ni nzuri na  inaonyesha  ni  kiasi gani wabunge  wao  walivyokaribu na changamoto  za  wananchi  wao.
Mbali ya waziri Lwenge  kuzungumza na  wananchi hao pia  mbunge  Mwamoto  aliwakutanisha  wananchi hao na  waziri  wa Kilimo ,mifugo na Uvuvi  Mwigulu Nchemba ambae katika  kikao  chake na  wananchi hao  alieleza mkakati wa   wizara yake  kushirikiana na  wizara ya viwanda na biashara pamoja na  wizara ya vijana na ajira ili  kuanzisha viwanda  vidogo vya  nyanya katika  mji  wa Ilula na  kuwa kazi ya  wizara  yake ni  kutoa mafunzo ya  kilimo cha  kisasa cha nyanya na  kuwawezesha  wakulima hao  wa mafano mpango ambao   utafanyika katika kanda mbali mbali ila kwa nyanda za juu  kusini  wanakusudia  kuufanya  wilaya ya Kilolo .
Kijana  wa Ilula  akichambua nyanya
Kwa  upande  wake waziri  wa vijana na ajira Antony Mavunde alisema  kuwa wizara  yake  ipo  tayari  kuwasaidia  vijana katika  wilaya ya  Kilolo kwani  tayari  wameonyesha  nia ya  kujikwamua  kiuchumi  kupitia  kilimo  cha nyanya na  kuwa kazi ambayo  mbunge na  viongozi wa wilaya ya  Kilolo wanapaswa  kuifanya ni kuwaunganisha  vijana  hao katika  vikundi na kuanzisha  Saccos zao  ili  pesa  itakapotolewa na  serikali  kupitia katika  saccos  hiyo .
Alisema  kuwa upo  uwezekano wa vijana hao  kuanzisha  kilimo  cha  nyanya  na  kuwa na  viwanda  vidogo  vya  kuchakata  nyanya na  kuziuza badala ya  sasa  kuuza kwa hasara.
Mbunge  wa Kilolo Bw.  Mwamoto aliwapongeza  mawaziri  hao  kwa kuonyesha  utayari  wao katika  kuwasaidia  wananchi  wa Kilolo na  kuwa kilio  kikubwa kwa  wananchi wa mji wa Ilula ni maji ,masoko ya uhakika  ya mazao na hivyo  kusaidiwa maji na vijana  kupata viwanda  vidogo  vidogo  wataweza  kukuza  kilimo cha  kisasa  zaidi.
 Katika ziara  yao  hiyo  bungeni wananchi  hao  ambao ni  wawakilishi  wa  wananchi wa Ilula  waliongozana na katibu  wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya ya  Kilolo Bw Clemence Mponzi na  aliyekuwa diwani wa Ilula Anna Msolla, Peter Mdanginyali , diwani wa kata ya Mlafu Bw  Isdori Kihenge , Vicent Gaifalo,Anna
Msolla, kada  wa hadema Bw Khalid  Muhel , Jocob Ngusulu
,Uzebeo Mhando  na katibu tarafa ya
Mazombe Bw. King’ung’e

MAKAMPUNI 52 YAJITOKEZA KUWEKEZA SEKTA YA UMEME

lu7 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad,  Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Carlos Agostino do Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi sasa Serikali imekwishapokea maombi 52 kutoka makampuni mbalimbali ambayo yanataka kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini Tanzania.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia.
“Haya maombi yamekwishapokelewa na wenye makampuni wamekwishahojiwa kuangalia uwezo walionao katika suala zima la uwekezaji wanaotaka kuufanya, na tukiwapata wenye uwezo na wenye nia ya dhati watapatiwa miradi ya kuiendesha,” alisema.
Aliwataka Watanzania hao waishio Zambia watumie fursa ya uwepo wao huko kutafuta marafiki ambao wanaweza kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali nchini kwani Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu wakati wananchi wanahitaji kupatiwa huduma muhimu.
“Serikali peke yake haiwezi kufanya kazi ya uwekezaji kwa hiyo tunahitaji kushirikiana na sekta binafsi, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo na ndiyo maana kule kwenye mkutano nimewaeleza washiriki kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi.
Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutawezesha wananchi wengi zaidi kujiingiza katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuinua uchumi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Alisema malengo ya Serikali ya awamu ya tano ni kuona kuwa nchi inakuwa na mitambo mingi ya kuzalisha umeme na umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo inaunganishwa na gridi ya Taifa ili kuondokana na tatizo la mgao wa umeme nchini.
Alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati vikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo, nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy) na nishati inayotokana na vinyesi vya mifugo (biomass) ambayo alisema vinatumika kwa watu wachache (siyo kitaifa).
Alisema kupatikana kwa gesi asilia nchini kumeleta neema ambapo mabomba ya gesi yamekwishajengwa kutoka Mtwara hadi Kinyerezi na kutoka Kilwa-Songosongo hadi Dar es Salaam. “Sasa hivi kuna utafiti unaendelea juu ya uwezekano wa kusambaza gesi ya kupikia majumbani. Tumeanza pale Mikocheni (DSM) na sasa hivi wanafanya utafiti mwingine kule Mtwara ili wananchi waweze kutumia gesi hii kupikia badala ya mkaa,” alisema.
Akielezea kuhusu uwekezaji kwenye makaa ya mawe, Waziri Mkuu alisema Serikali imelenga kutumia makaa ya mawe ili kuendeshea mitambo ya kwenye viwanda vikubwa badala ya kutumia umeme au mafuta ya dizeli kama inavyofanyika sasa. “Baadhi ya wenye viwanda wanabadilisha mifumo ya kuendeshea mashine zao ili iweze kuendana na teknolojia ya makaa ya mawe pindi tu uchimbaji ukishika kasi,” alisema.
Akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kusambaza nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), vijiji zaidi ya 3,000 katika ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vimefikiwa na nishati ya umeme.
“Tulianza na REA awamu ya kwanza, awamu ya pili na sasa tunaenda awamu ya tatu. Hata mkipiga simu kwa ndugu zenu vijijini, mtakuta katika kila kata kuna vijiji kati ya vinne hadi vitano ambavyo vimefikiwa na nishati ya umeme kupitia mradi wa REA,” alisema.
Waziri Mkuu amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

PROF. MBARAWA AFUNGUA KIKAO CHA MPANGO KAZI – TEMESA

index 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka Watendaji wakuu, Mameneja na Wazalishaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kutumia maarifa na taaluma zao ili kuboresha utendaji kazi wa wakala huo na kuongeza mapato.
Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha TEMESA Taifa mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa amewataka watendaji wa temesa kubadili mfumo wa utendaji na kufanya kazi kwa kuzingatia matokeo na faida.
“Tengenezeni magari 60 kwa siku muone namna mtakavyopata wateja wengi na kuongeza mapato”, amesema Prof. Mbarawa.
Kikao kazi hicho chenye malengo ya kuboreshaj utendaji wa wakala huo kitajadili kwa kina changamoto mbalimbali zinazoikabili TEMESA na kutengeneza mpango wa  kuboresha huduma zao.
“Tumieni elimu mliyonayo kwa ajili ya maslahi ya watanzania na kuibadilisha TEMESA hii kuwa ya tofauti  na ya pekee”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amehimiza Wakala huo kuhakikisha wanadhibiti mapato na matumizi ya mfumo wa kielektroniki kwenye vivuko vyote ili kukuza na kujiendesha kwa vivuko vyenyewe.
Amesema mpaka sasa TEMESA ina jumla ya vivuko 27  lakini mapato yake bado yapo chini ya inavyotegemewa
na kushindwa kumudu hata matengenezo ya wakati ya vivuko hivyo.
Wakala huo pia umesisitizwa juu ya  usimamizi wa kina wa usalama wa vivuko na kanuni za usafiri wa majini ili kuepuka ajali zinazotokana na uzembe wa kutofuata kanuni na taratibu zilizowekwa.
“Andaeni kozi fupi kwa ajili ya watumishi wanaosimamia vivuko na kuja na mikakati madhubuti ya jinsi ya kuziepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. MBARAWA amewataka TEMESA kutengeneza magari yote ya serikali na kutafuta soko katika magari ya watu binafsi ili kuongeza mapato na ufanisi kwa wakala huo.
“Bado mmelala, hamjaamka,  nataka temesa itengeneze magari yote ya serikali hadi kufikia asilimia 65 ya matengenezo, tumieni fursa hii ya wizara yenye taasisi nyingi ili kufanya biashara na kujilipa wenyewe na kwani inajitosheleza kukua”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Ameongeza kuwa temesa wamepewa rasiliamali zote hivyo ni lazima wafanye kazi na kujisimamia wenyewe kwa kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza mahitaji ya watanzania.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan amemhakikishia Waziri kuandaa mikakati madhubuti ya kuikuza wakala huo kwa kutoa huduma bora zinazolingana na thamani ya fedha yenyewe kwa wateja wake.
Katika Hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa daraja la Ruvu chini katika barabara ya Msata-Bagamoyo lenye urefu wa mita 140 na kumtaka Mkandarasi Estim Construction kuhakikisha daraja hilo linakamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.
Aidha amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Pwani Eng. Tumainieli Sarakikya kuhakikisha kipande cha barabara kilichobakia katika barabara ya Msata-Bagamoyo kinaunganishwa ifikapo Februari mwakani.
“Hakikisheni wananchi hawavamii maeneo ya hifadhi ya barabara kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na tutachukua hatua kali kwa watakaovunja sheria ya barabara”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Zaidi ya Shilingi Bilioni 127 zimetumika katika ujenzi wa barabara ya Msata-Bagamoyo yenye urefu wa km 63.

BILIONI 8 KUTUMIKA KUBORESHA VYUO VYA AFYA NCHINI

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala.
………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa – Dodoma.
Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 8
kuboresha miundombinu ya vyuo vya Afya kote nchini katika mwaka wa fedha
2016/2017 ili kuwawezesha wanafunzi wa fani ya Afya kusoma katika  mazingira mazuri.
 
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali la Mbunge wa Muhambwe Mhe.Atashasta Justus Ntitiye, alieyata
kujua mkakati wa Serikali wa kuboresha vyuo vya Afya nchini hususan chuo cha
Uuguzi wilayani Kibondo kilicho katika jimboni lake.  
 
Dkt.Kigwangala amesema Serikali katika mwaka wa fedha
2016/2017 imejipanga kuboresha mazingira ya vyuo vya Afya katika maeneo
mbalimbali nchini kikiwemo Chuo cha Uuguzi Kibondo ambacho kimetengewa shilingi
milioni 680.
 
Aidha, ameeleza kuwa vyuo vya Afya vimekuwa
vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni ya wazabuni wa vyakula
waliokuwa wakiidai  Serikali  kiasi cha shilingi Bilioni 6.8 kuanzia mwaka
2009 hadi 2015.
 
Amebainisha  kuwa tayari Serikali imekwishahakiki madeni
yote ya wazabuni   ili yaweze
kulipwa  katika mwaka wa fedha 2016/2017
na kuongeza kuwa suala la usambazaji wa vyakula limeachwa chini Sekta binafsi
ili zifanye kazi hiyo.
 
Katika hatua nyingine Dkt.Kigwangala amesema Serikali
inaendelea kuangalia uwezekano wa kuyatumia majengo yaliyoachwa kwenye kambi za
wakimbizi zilizofungwa mkoani Kigoma hususan wilayani Kibondo ili yaweze
kutumika kama vyuo vya kutolea elimu ya Afya.
 
” Niko tayari nikishirikiana na waheshimiwa
wabunge kwenda mkoani Kigoma kuzungumza na viongozi wa mkoa huo ili tuweke
utaratibu wa namna ya kuyatumia majengo hayo” Amesisitiza Dkt.Kigwangala.

Waimbaji nyimbo za ziinjili tutangaze injili tuache kuimba kwa biashara tu

Ambwene Mwasongwe John Lisu Mbeya SM GK (6)
Mwimbaji wa nyimbo za injili Ambwene Mwasongwe akiimba katika moja ya kazi zake za kumtumikia Bwana Yesu Kristo.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Waimbaji wa Nyimbo za Injili nchini wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa kujitolea ikiwa kama sehemu ya ibada ya kumtumikia Mungu kwa kulitangaza neno lake na si kugeuza kazi hiyo kuwa mtaji wa biashara.
Hayo yamesemwa na Mwalimu wa kwaya ya Wateule Elikana Simatiya kutoka kanisa la Anglikani, St. James lililoko Tabata Segera jiijini Dar es Salaam, maarufu kama  kunyata nyata  jina lililotokana na nyimbo ya kunyata nyata aliyoifundisha akiwa kwaya ya Mennonite.
“Waimbaji wengi wa nyimbo za injili wameacha kutumikia Mungu na badala yake   wamekuwa wakiuunda vikundi binafsi vya uimbaji ambavyo hutumika kama vyanzo vya fedha na hualikwa kwenye mikutano ya injili na sherehe mbalimbali kwa malipo maalum,” alisema Simatiya.
Aidha ameeleza kuwa, uimbaji wa nyimbo za injili ni wito kama ulivyo wito wa uchungaji lakini hivi sasa muimbaji wa injili akialikwa katika mikutano ya injili au sherehe huomba malipo hadi ya shilingi milioni moja.
Simatiya aliongeza kuwa, ziko gharama ambazo muimbaji anaweza kuomba kupewa kama usafiri kwa ajili ya kumfikisha eneo husika au malazi na chakula ikiwa atahitajika kulala nje ya makazi yake, lakini waimbaji wa leo wamebadilisha wito wa kutangaza injili kwa njia ya uimbaji kuwa biashara.
Hivyo mwalimu huyo amewataka waimbaji kubadilika kwa kuacha kuharibu kazi ya Mungu na kufanya kazi hiyo kwa kujitolea kwani wapo wanaopokea uponyaji na wanaotiwa moyo kupitia nyimbo za injili.
Kwaya ya Wateule inatarajia kuzindua albamu mpya ijulikanayo kama Wateule tutakwenda siku ya Jumapili Mei 29, 2016 Tabata Segerea katika kanisa la St. James, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda,huku wakisindikizwa na  waimbaji wa injili ambao ni Ambwene Mwasongwe, Christina Shusho, Edson Mwasabwite pamoja na kwaya za Anglikan kutoka Vingunguti na Ukonga.

TANESCO yawataka wateja wake kuunganishiwa umeme na mafundi waliosajiliwa.

TAN1 
Meneja wa Afya na Usalama kazini wa TANESCO, Mhandisi Majige  Mabulla.
………………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Shirika la Umeme Tanzania Nchini (TANESCO) limewataka wateja wake kuhakikisha wanaunganishiwa umeme na mafundi au wakandarasi waliosajiliwa na shirika hilo ili kupunguza ajali za moto.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini wa TANESCO, Mhandisi Majige  Mabulla alipokua akiongea na waandishi wa habari juu ya vyanzo vya ajali za moto vinavyosababishwa na umeme.
Mhandisi Mabulla alisema kuwa matukio ya moto yanayosababishwa na umeme hutokea kutokana na kuzalishwa kwa joto kali ndani ya nyaya kunakosababishwa na umeme kuwa mkubwa kuliko uwezo, kulegea kwa maungio ya nyaya pamoja na radi au nyaya za umeme kuangukia juu ya paa la nyumba.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mabulla aliongeza kuwa ajali za moto zinazosababishwa na umeme huanza kama unavyoanza moto wa kiberiti au viwashio vinginevyo vya moto na husambaa haraka kwa kutegemea na aina ya vitu vilivyopo kwenye eneo husika kwa kuwa baadhi ya vitu hushika moto haraka na kuenea kwa kasi.
“Ajali za moto zinazosababishwa na umeme ni ngumu kutokea kama umeme utasukwa na mtaalam aliyebobea kwenye fani hiyo, TANESCO tunatoa wito kwa wateja wetu kuhakikisha wanafungiwa umeme na fundi au mkandarasi aliyesajiliwa na kampuni yetu,”alisema Mabulla.
Pia Mhandisi Mabulla alisema ili kuepukana na ajali za moto zinazotokana na hitilafu za umeme wateja wanapaswa ;kuepuka kupitisha nyaya za umeme juu ya paa za nyumba, kutokuunganisha umeme kutoka nyumba moja kwenda nyingine bila kupata maelekeza kutoka TANESCO.
Aidha Mhandisi Mabula alisema wateja pia wanapaswa kuhakikisha mfumo wa umeme unapitiwa upya kila baada ya miaka mitano pamoja na kuwa makini katika utumiaji wa vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi, hita za umeme.

TANESCO yawataka wateja wake kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme

TAN1 
Meneja wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi Kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Majige Mabula akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo aliwataka wateja wa shirika hilo kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Yasini Silayo.
TAN2 
Baadhi ya Waandishi wahabari wakifuatilia mkutano huo. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
…………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Shirika la Umeme Tanzania limewataka wateja wake kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini Mhandisi Majige  Mabulla wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Majige amesema kuwa moto hauwezi  kutokea endapo mtumiaji wa umeme atahakikisha kuwa mfumo wa umeme katika nyumba yake umesukwa na fundi ama mkandarasi aliyesajiliwa.
“Kuwa makini katika matumizi bora ya vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi,hita za umeme,kuchaji simu,kompyuta kutasaidia kupunguza au kuondoa tatizo la majanga ya moto” alisisitiza Mabulla.
Akizungumzia hatua nyingine zinazoweza kusaidia kuzuia majanga ya moto Mhandisi  Majige ni kuepuka kuweka vitu vinavyoweza kushika moto kirahisi karibu na nyaya ama maungio ya nyaya za umeme ndani ya nyumba .
Majige alitoa wito kwa watumiaji wa umeme kutoa taarifa pale wanapotaka kuongeza matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa ndani ya makazi ya watu ili tathmini ya uwezo wa nyaya kukidhi mahitaji yaliyoongezeka ifanyike.
Katika kuzuia matukio ya moto TANESCO imekuwa ikihakisha kuwa inamfikishia mteja umeme ulio salama na usiokuwa na madhara kwa mtumiaji kutoka kwenye nguzo mpaka kwenye mita.
Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwepo na matukio ya ajali za moto katika makazi ya watu ambayo yamekuwa yakisababisha madhara  ikiwemo kusababisha vifo,majeruhi  na uharibifu wa mali.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA OMAN NCHINI TANZANIA LEO

OM1 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi, wakati Balozi Saud alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Mei 25,2016 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
OM2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi, wakati Balozi Saud alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Mei 25,2016 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. (Picha na OMR)

JARIDA LA WIZARA TOLEO LA 7

index 
Jipatie Jarida hili bure kujua masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Ardhi/ Nakala ni chache.Fika Wizarani; Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Kampuni ya Sta Tavel yaendelea kuwa suluhisho la usafiri kwa watanzania wanosoma nje ya nch

Students at desks in classroom, teacher by board, portrait of young woman smiling
Na: Frank Shija, MAELEZO
Wanafunzi na vijana wakitanzania kuendelea kunufaida na usafiri wa njia ya anga kwa gharama nafuu kupitia Kampuni ya Sta Travel yenye maskami yake mtaa wa mtendeni manispa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Hayo
yamebainishwa na Meneja uendeshajji wa Kampuni hiyo Abass Takim alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake jana.
Takim amesema kuwa watanzania wanaosoma elimu ya juu nje ya nchi wanayofurusa ya kunufaiki na huduma zaokwa kuwaunganisha na usafiri wa gharama ndogo zenye punguzo maalum za kusafiri wakati wa kwenda na kurudi kutoka masomoni katika nchi wanazosomea.
Takkim amesema kuwa taasisi yao imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaopata fursa ya kusoma nje ya nchi kwani wanatoa huduma ya usafiri ikiwa na punguzo maalum la gharama za usafiri ili waweze kumudu gharama hizo, ambapo huduma hiyo ya usafirishaji wa wanafunzi kwa gharama nafuu inaenda sambamba na huduma za malazi kwa gharama nafuu wakati wa kwenda na kurudi,Bima ya safari na  Kitambulisho cha Kimataifa cha Mwanafunzi
Aliongeza kuwa mpaka sasa Taasisi yake imetoa huduma ya hiyo kwa watanzania wengi hasa wanafunzi wanaoenda kusoma katika vyuo vya Kuala Lumpar Malyasia, London Uingereza, na Guangzhou China.
Aidha Abbas alisema kuwa pamoja na kutoa huduma hiyo kwa watanzania kumekuwa na changamoto katika upatikanajji wa Viza kwa wateja wao na kupelekea kujitokeza kwa usumbufu, hata hivyo Sta Travel imekuwa ikijitahidi kuwasaidia wateja wake ili wakamilishe taratibu zao kwa wakati.
Sta Travel niasasi inayojihusisha na utoaji wa huduma ya kusafirisha wanafunzi kwa gharama nafuu ikiwa na punguzo kwa lengo la kuwasaidia watanzania kufikia ndoto zao bila kuwapo na kikwazo.
Katika kuhakikisha inafikia wateja wake kwa urahisi zaidi Sta Travel imefungua zaidi ya matawi 400 katika nchi 100 dunia kote ambapo kwa Tanzania ofisi zake zinapatikana katika mtaa wa Mtendeni, Kisutu (Posta),Takims Holidays / STA Travel Partner mkabala na Supermarket ya Shrijee jijini Dar es Salaam unaweza pia kuwasiliana nao kupitia simu namba +255 758 828384/85 au tembelea tovuti yao http://www.escape-tanzania.com/

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA KAMATI YA UTENDAJI TASWA

TASWALOGO 
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam Mei 24, 2016 kujadili masuala mbalimbali.
 
A; Tuzo za Wanamichezo Bora
 
Kikao kilikubaliana Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na TASWA, safari hii zifanyike Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
 
TASWA imeuanda kamati maalum kwa ajili ya kusimamia upatikanaji wa wanamichezo hao bora, kamati ambayo inajumuisha waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari na wataalamu kutoka vyama mbalimbali vya michezo. Sekretarieti ya TASWA inaendelea kufanya mawasiliano na wateule wa kamati hiyo kabla ya kuwatangaza.
 
Kwa kawaida kila mwaka TASWA inatoa tuzo kwa wanamichezo bora wa kila mchezo na pia kunakuwa na mwanamichezo bora wa jumla kwa mwaka husika.
 
Baadhi ya waliopata kutwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora Tanzania wa jumla kwa miaka kumi iliyopia na miaka yao katika mabano ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wanariadha.
 
Mwaka 2009 tuzo ilienda kwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan, ambaye pia alitwaa tuzo hiyo mwaka 2010, wakati mwaka 2011, ambapo tuzo yake ilitolewa mwaka 2012 mshindi alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe. Mwaka 2013/2014 ilienda kwa mwanasoka Sheridah Boniface.
 
Mwaka 2015 tuzo ilifanyika katika aina nyingine,  ambapo walizawadiwa wanamichezo 10 tu waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya urais wa Jakaya Kikwete na pia TASWA ilitoa Tuzo ya Heshima kwa Kikwete.
 
B; Media Day
Kama inavyojulikana chama chetu kimekuwa kikiandaa bonanza maalum likihusisha waandishi na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, lakini kwa miaka miwili bonanza hilo limekwama kufanyika kutokana na sababu mbalimbali. Kikao kimekubaliana nguvu zaidi ielekezwe ili jambo hilo lifanyike na kuwapa raha wadau. Taarifa zaidi kuhusu Media Day itatolewa Jumamosi wiki hii.
 
C: Changamoto kwa waandishi
 
Kikao kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi wa habari za michezo na chama kwa ujumla, ambazo zimewekewa mikakati ya muda mfupi na mrefu na utekelezaji wake utaanza kuonekana siku chache zijazo.

MACHINGA, MFUPA ULIOISHINDIKA HALMASHAURI YA JIJI MWANZA

Ipo kauli isemayo “Mfupa Uliomshinda Fisi” ikiashiria jambo gumu mithiri ya mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyama bingwa wa kutafuna mifupa ya kila aina.
Ndivyo unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri ya jiji la Mwanza.
 
Mara kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu licha ya nguvu kubwa kutumika.
 
Kabla ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la mwanza machinga wamezagaa ovyo.
 
Baadhi  ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa
maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia
kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa
wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.

No comments:

Post a Comment