Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na Kimataifa Mhe. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Kwa ajili ya kuonana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi. Katikati Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa leo April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa leo April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR)
RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
Timu za mpira wa pete na miguu za Bunge zapongezwa kwa kufanya vizuri mashindano ya Muungano
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Tabora mjini Mhe. Mwanne Nchemba (CCM) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (CHADEMA) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
Wabunge wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (katikati) mara baada ya kumalizika mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi Seleman Jafo akiwa katika
picha ya pamoja na wageni wake waliomtembelea leo Bungeni, mjini Dodoma.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Bungeni, mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewapongeza wabunge kwa kushiriki
vizuri mashindano ya Muungano yaliyofanyika Zanzibar na kurudi salama
mjini Dodoma kuendelea na majukumu yao.
Pongezi hizo za Spika zimetolewa
leo Bungeni Dodoma na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kwa niaba ya Spika
alipokuwa akitoa matangazo kabla ha kuahirisha shughuli za Bunge hadi
jioni ambapo Bunge linaendelea kujadili hoja ya Hotuba za Ofisi ya
Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George
Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo.
Timu za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo ni timu za mpira wa
miguu na pete ambapo timu ya mpira wa pete imefanya vizuri kwa kuishinda
timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa magoli 18 kwa magoli 15
wakati timu ya mpira wa miguu zilitoka sare ya kufungana goli 1:1
Kushiriki kwa Wabunge katika
mashindano hayo yamelenga kuimarisha udugu uliopo kati ya pande mbili za
Muungano na kuwapa fursa Wabunge kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga
na kuimarisha afya zao.
Aidha, michezo kwa Wabunge inatoa
nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni kielelezo cha msingi kinachozaa
Viongozi bora wanaotokana na sekta ya michezo.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wanafursa kubwa ya kufanya mazoezi mbalimbali katika kujenga na
kuimarisha timu za Bunge hilo ili kujenga pia ujirani mwema.
Ushiriki wa Wabunge kwenye
mashindano siyo mara ya kwanza, Wabunge hao hushiriki michezo
mbalimbali, wanashiriki mpira wa miguu wakiwa watani wa Jadi wa timu za
Simba na Yanga, Februari 4, 2012 walishiriki mazoezi ya viungo
yaliyoendeshwa na klabu inayojulikana kama “Kitambi noma” kutoka mjini
Unguja kwa kuzingatia Bunge lina eneo mahususi la kufanyia mazoezi
mazoezi ya viungo (Gym).
WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUWAWA MKOANI MBEYA
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akizungumza na
waandishi wa habari jijini Mbeya (Hawapo pichani)katika kuzngumzia
tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu wakati wakijaribu kufanya uhalifu
katika duka la kuuzia vinywaji mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya
Mkoani Mbeya.
|
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silaha aina
ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ambayo
ilikuwa ikitumika na majambazi hao katika tukio la kutaka kufanya
uhalifu kwenye duka la vinywaji mali ya Hamisi mji mdogo wa Matundasi
Wilayani Chunya Mkoani Mbeya April 27 mwaka huu.
|
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina
ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao .
|
Baadhi
ya askari polisi wakifuatilia kwa makini mkutano wa kaimu kamanda wa
Polisi Mkoa wa mbeya Butusyo Mwambelo wakati akizungumza na waandsihi wa
habari kufuatia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu waliotaka kufanya
uhalifu katika duka la vinywaji vya jumla linalomilikiwa na ndugu
Hamisi Mkazi wa Matundasi Chunya Mkoani Mbeya .
|
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.
|
Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu- Mbeya)
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (kulia) wakati alipomuuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Kushoto ni Mbenge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Katikati ni Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
APPOINTMENT TO THE CHAIRMAN, VICE CHAIRMAN AND BOARD MEMBERS OF THE TANZANIA COMMUNICATION REGULATORY AUTHORITY (TCRA)
The Chairman of the Nomination Committee, established under section 8(1) (a) of the TCRA Act. No. 12 of 2003, invites Tanzanians with relevant qualifications as spelt out herein to apply for appointment to fill the positions of the Chairman, Vice Chairman and Board members of Tanzania Communication Regulator Authority. Attention is hereby drawn that all applicants are required to observe the provisions of Sections 7(5) and 11 of the TCRA Act, 2003 as well as the TCRA Code of Conduct relating to conflict of interest.
Qualifications required:
As per the First Schedule of the TCRA Act 2003, the following are the minimum qualifications for appointment to the TCRA Board:
- Should be a graduate of a recognized university;
- Have at least 10 years experience in one or more of the fields of Management, Law, Economics, Finance, Engineering, Broadcasting, ICT or related fields;
- Have knowledge of the communication industry;
- Should satisfy the Nomination Committee that he/she is unlikely to have a conflict of interest under Section11 of the Act;
- Be willing to serve as member to the board.
All applications including
detailed Curriculum Vitae and names and addresses of three references
(including current or last employer) should be sent to the address below
so as reach the Chairman of the TCRA Nomination Committee by 23rd May, 2016
The Chairman,
TCRA Nomination Committee,
Ministry of Works, Transport and Communication,
14 Jamhuri Street,
P.O.BOX 2645,
11470 DAR ES SALAAM
Tigo, mgahawa wa Samaki Samaki waingia ubia
Meneja
wa Huduma za Masoko Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiongea na
wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati
ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na Mgahawa wa Samaki samaki. Kulia
ni Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa Samaki samaki, Saum Wengert.
Meneja wa Huduma za Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiwa na Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa wa Samaki samaki, Saum Wengert wakionyesha mkataba wa ushirikiano wa kibiashara waliosaini kati ya kampuni ya Tigo na Mgahawa huo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar Es salaam.
…………………………………………………………………………………………….
Kampuni ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali ya Tigo
Tanzania, leo imeingia ubia na mgahawa ya Samaki Samaki ambao
ilianzishwa tangu mwaka 2007 ukiwa na matawi matatu yaliyopo Mlimani
City, City Centre na Masaki Jijini Dar es salaam, ambapo pande hizo
mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja kwa kuleta bidhaa/huduma zao
kwa wateja wa kila mmoja. Akitangaza ubia huyo jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout aliviambia
vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo ni moja ya alama ambazo zinajenga imani kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha kupitia migahawa ya Samaki Samaki Tigo imeweka mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya
Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja wake kufurahia intaneti ya kasi na ya haraka wakati wakila na kunywa kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula vinavyotokana na mazao ya baharini hapa nchini.“Tunaamini ushirikiano wetu utandelea kuonesha ni jinsi gani tumejikita kwenye kuboresha mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya
kidijitali na kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez. Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania na wameungana na Tigo ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa ubunifu nchini kuwapatia wateja wake kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za Tigo zilivyo hususani uzoefu kwenye mtandao wa bure na wa kasi wa intaneti. Kwa ushirikiano huu tutawapatia wateja wetu miradi mingi mipya, maboresho pamoja na ofa. Kufanya kazi na Tigo sio kwamba kunahusu sisi kupata fedha tu, bali inahusu ni nini cha ziada tunachoweza kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza kufanya kazi pamoja na kampuni iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.Tunaweza kuwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini tunapenda kufanya jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu. Huduma za Tigo zinazotarajiwa kuwepo kwenye migahawa ya Samaki Samaki ni pamoja huduma ya bure ya intaneti bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na Tigo Music.
vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo ni moja ya alama ambazo zinajenga imani kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha kupitia migahawa ya Samaki Samaki Tigo imeweka mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya
Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja wake kufurahia intaneti ya kasi na ya haraka wakati wakila na kunywa kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula vinavyotokana na mazao ya baharini hapa nchini.“Tunaamini ushirikiano wetu utandelea kuonesha ni jinsi gani tumejikita kwenye kuboresha mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya
kidijitali na kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez. Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania na wameungana na Tigo ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa ubunifu nchini kuwapatia wateja wake kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za Tigo zilivyo hususani uzoefu kwenye mtandao wa bure na wa kasi wa intaneti. Kwa ushirikiano huu tutawapatia wateja wetu miradi mingi mipya, maboresho pamoja na ofa. Kufanya kazi na Tigo sio kwamba kunahusu sisi kupata fedha tu, bali inahusu ni nini cha ziada tunachoweza kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza kufanya kazi pamoja na kampuni iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.Tunaweza kuwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini tunapenda kufanya jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu. Huduma za Tigo zinazotarajiwa kuwepo kwenye migahawa ya Samaki Samaki ni pamoja huduma ya bure ya intaneti bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na Tigo Music.
BOSTON CITY CAMPUS TANZANIA, BRANCH NOW OPEN
Boston City Campus and Business College carries a legacy of over 20 years in South
Africa. It currently has 44 branches with over 25000 students studying every
year. In Tanzania, Boston has opened its first branch outside South Africa, 45th
Branchin total this year.
Africa. It currently has 44 branches with over 25000 students studying every
year. In Tanzania, Boston has opened its first branch outside South Africa, 45th
Branchin total this year.
Boston
offers Professional Courses and Short Learning Programs with plans to
introduce tertiary education in the future. These are further learning
programs which will enhance one’s skills and assist to get better jobs.
They have extended their wide range of
courses which they offer in South Africa in various fields to Tanzania.
courses which they offer in South Africa in various fields to Tanzania.
Students can choose from multiple course under various categories such as
Accounting, ICT, Business Management, Business Communications, Marketing and
many more. There are professional courses offered at their college such as ACCA
and CompTIA certified A+, N+ and many more.
Accounting, ICT, Business Management, Business Communications, Marketing and
many more. There are professional courses offered at their college such as ACCA
and CompTIA certified A+, N+ and many more.
The
teaching methodology Boston is bringing to Tanzania is quite different
from the conventional way of classroom teaching. At Boston, a student
would study on a computer assigned to him or her, for a scheduled time
slot. All the teachings are imparted in the form of video tutorials
which the student views on his computer screen and listens to through
earphones. This enables the student to learn on a one to one
basis.
basis.
This
type of teaching method gives multiple benefits to the student: The
student will be able to study at his own pace without having to worry
about keeping pace with other students. The student will have a
prescheduled flexible timetable to study at the college, unlike going to
a classroom where he has to adjust his schedule to
the class’s timings.
the class’s timings.
While
a student can be studying one subject on a computer, the student
sitting next to him can be studying an entirely different subject at the
same time. There is a flexibility for the student to enroll whenever he
wants, all round the year. Also, as the student is studying, he can
view the videos multiple times, till he understands the concepts, by
forwarding or rewinding the video.
The exams too are taken at their own ease, once they are done studying a module. Most of these exams are
computer based and will be assessed at their headquarters in South Africa. While the learning is computer based, Boston also provides course books to the students, price of which is already included in the fee.
computer based and will be assessed at their headquarters in South Africa. While the learning is computer based, Boston also provides course books to the students, price of which is already included in the fee.
In
the case that the student is having difficulty in understanding the
tutorial, there are Training Advisors to help the students clear their
doubts and move forward. The training advisor will be able to tutor the
student on a one to one basis.
If
the student still does not understand, they have the option to contact
experts in South Africa who are qualified for each subject that is being
taught here.
This will be done from the college itself. Further, for benefit ofthe
students, refresher sessions are conducted in their workshop room on
weekly basis where a student can participate if he is having any
difficulty understanding any concepts and get clarifications.
Access
to the computers and video tutorials is only from the college. It is
mandatory for the student to be present at the college for the
tutorials, as Boston wants the students to study under a controlled
environment. This way the progress of each student can be monitored.
However, the student is provided with study material and books which are
kept by them, to be used to revise and prepare for the next class.
More information on Boston City Campus & Business College is available at www.boston.co.tz / 0765 008827 or 0685 626366
Wamuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuteketeza ghala la meno ya tembo liliopo nchini
Mwenyekiti
wa Kampeni ya Okoa Tembo Bw. Shubert Mwarabu (katikati) akielezea kuhus
Kampeni yao ya kuokoa Tembo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari
uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Kampeni hiyo Bw. Lameck Mkuburo pamoja na
Bw. Arafat Mtui (wa kwanza kulia).
(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
……………………………………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO- Dar es Salaam.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya
Okoa Tembo Tanzania imemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli kuteketeza ghala la meno ya tembo liliopo nchini
kufuatia Tanzania kusaini mpango wa kuwalinda Tembo mwaka 2014 unaozuia
uuzaji wa meno ya Tembo kwa muda wa miaka 10.
Ombi hilo limetolewa leo jijini
Dar s Salaam na Mwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Tanzania Bw.Shubert
Mwarabu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Barua ya
Wazi waliyomwandikia Mheshimiwa Rais.
Amesema Tanzania inafungwa na
mkataba wa kimataifa wa biashara juu ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka
(Convetion on International Trade in Endangered Species-CITES) ambao
unabainisha kuwa Tanzania kwa sasa haiwezi kuuza ghala lake la meno ya
Tembo.
Amesema uhifadhi wa meno hayo
unaigharimu serikali fedha nyingi na kufafanua kuwa kwa sasa Tanzania
ina hifadhi kubwa ya meno ya Tembo yaliyokamamwa kutokana na ujangili.
“Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa
kasi yake ya utendaji tangu kuchaguliwa kwake,tunamuomba atekeleze
lengo la tatu la kampeni yetu ya Okoa Tembo wa Tanzania kwa kuliteketeza
hadharani ghala la meno ya tembo,tunaona hakuna haja ya kuendelea kuwa
na ghala hili” amesema Bw.Mwarabu.
Amesisitiza kuwa ombi lao kwa
Rais kutaka ghala la meno ya Tembo liteketezwe kutasidia kutuma ujumbe
mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani
ya pesa kiasi cha serikali kuona wepesi kuteketeza hazina hiyo.
“ Tunataka ieleweke kwamba
kuharibu ghala la meno ya Tembo kunatuma ujumbe mzito kwa majangili na
wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa na kuwa
ujangili ni kosa la jinai lisilokubalika” Amesisitiza.
Amesema ipo haya ya Tanzania
kuunga mkono mpango wao wa kuteketeza ghala la meno ya Tembo kama
inavyotarajiwa katika nchi ya Kenya ambayo inatarajia kuteketeza ghala
lake la meno ya Tembo hadharani Aprili 30 mwaka huu.
Amezitaja nchi ambazo zina mpango wa kuchukua hatua kama ya Kenya kuwa ni Ethiopia,Chad,Gabon, Mozambique na Congo.
Naye mmoja wa wajumbe wa Kampeni
ya Okoa Tembo wa Tanzania Bw.Arafat Mtui akizungumza katika mkutano huo
amesisitiza kuwa kuendelea kuwepo kwa ghala hilo nchini Tanzania
kunawapa moyo wafanyabiashara haramu wa meno hayo kuona kuwa ipo siku
biashara hiyo itaendelea tena.
Amesema Kampeni yao ya Okoa Tembo
wa Tanzania inaendelea kusisitiza kuwa kuwa hatma ya Tembo wa
Tanzania iko mikononi mwa watanzania, hivyo ni vema Serikali
ikashirikiana na wadau mbalimbali kuchukua hatua madhubuti kuokoa
viumbe hao walio hatarini kutoweka kwa ajili ya kizazi cha sasa na
vizazi vijavyo.
Uchukuzi SC, Tamisemi kama fainali kesho
Nahodha
wa timu ya Uchukuzi SC, Godwin Ponda akimtambulisha mgeni rasmi wa
mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tamisemi, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa
kamati ya Mei Mosi, Joyce Benjamin kwa kipa wake Herbat Steven, nyuma ni
mkuu wa benchi, Kenneth Mwaisabula. Uchukuzi walifungwa magoli 2-0.
Mwamuzi Robert Mkatakiu (aliyeshika kadi ya njano) akimuangalia mchezaji Kombo Ally wa Tamisemi aliyelala chini baada ya kuumia. Mchezaji huyo alionyeshwa kadi hiyo pamoja na nahodha wa Uchukuzi Godwin Ponda (kulia). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
Wachezaji wa timu za Uchukuzi SC na Tamisemi wakisubiri mpira wa kona upigwe na Omary Said wa Uchukuzi (haonekani pichani). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
Kipa wa Tamisemi,, Leonard Mkinga (katikati ya goli) akiwapanga wachezaji wake kabla Uchukuzi hawajapiga mpira wa kona. Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
Tatu Kitula (mwenye mpira) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga bao katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Mei Mosi dhidi ya TPDC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 33-14.
Matalena Mhagama (GA) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga, pembeni ni Dora Njau (GD) wa TPDC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 33-14.
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Uchukuzi SC na Tamisemi
kesho zitacheza mchezo wao wa mwisho wa netiboli, ambao ni kama fainali
kutokana na timu zote kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa mashindano ya
Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, kila mmoja
akiwa na pointi tisa.
Netiboli inachezwa kwa mtindo wa
ligi, ambapo timu hizo zinakamilisha ratiba na mmoja akimfunga mwenzake
atakuwa bingwa au zikitoka sare ya idadi yeyote ya magoli, basi Tamisemi
atatawazwa bingwa kwa kuwa anaidadi kubwa ya magoli ya kufunga, 94 na
wenzao wana 87.
Timu ya CDA Dodoma wanafuatia
wakiwa watatu baada ya kushinda mchezo mmoja, huku Tanesco na chipukizi
wa TPDC wakimaliza mashindano bila kushinda mchwezo wowote. Lakini TPDC
inayofundishwa na kocha mzoefu Rose Mkisi inayoundwa na wachezaji wenye
umri mdogo kati ya 20-30, ndio timu changa baada na inaonyesha baada ya
mwaka mmoja itakuwa tishio kwani itakuwa na uzoefu tofauti na sasa ndio
wameanza mwaka huu kushiriki mashindano haya ya Mei Mosi.
Katika mchezo wa soka timu ya Geita Gold Mine itakwaana na Tamisemi kesho katika mchezo wa fainali.
GGM wametinga hatua hiyo baada ya
kuwafunga Tanesco kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumaliza mchezo wa
nusu fainali bila kufungana.
Penati zote nne za GGM zilifungwa
na Gwetu Guvette, Oswald Binamungu, Ally Twist na Mohamed, wakati za
Tanesco walizopata ni Said Kondo na Stan Uhagile, na walizokosa ni Hemed
Mtumwa na Betwel Kagimbo.Nao Tamisemi waliwachapa Uchukuzi SC kwa
magoli 2-0.
Katika mchezo wa netiboli
uliochezwa jana jioni Uchukuzi SC waliwafunga chipukizi wa TPDC kwa
magoli 33-14. Uchukuzi walikuwa mbele kwa magoli 15-8.
Nayo Tamisemi waliwapeleka jamaa zao CDA na kuwachapa magoli 18-13. Washindi walikuwa mbele kwa magoli 9-8.
Katika kamba kwa wanaume Ukaguzi
waliwavuta CWT kwa mivuto 2-0, nayo TPDC wakiwavuta UDOM mivuto 2-0, na
Uchukuzi SC walipata ushindi wa chee baada ya Tanesco kuingia mitini;
wakati kwa wanawake Tamisemi waliwavuta bila huruma Tanesco mivuto 2-0.
Mbali na netiboli na soka
itakayochezwa kesho, pia kutakuwa mechi za kamba wanaume TPDC kucheza na
CWT, huku UDOM kuumana na Tanesco; wakati wanaume Uchukuzi SC
watakutana na TPDC.
KAMPUNI YA SGA SECURITY YAGAWA VIFAA VYA USALAMA BARABARANI KWA WAENDESHA BODABODA MBEZI
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti
maalum la usalama barabarani Bw. Thobias Msua mmoja wa waendesha
Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni
hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4 na wametoa
msaada huo kwa waendesha bodaboda zaidi ya 4000, makabidhiano hayo
yamefanyika Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti
maalum la usalama barabarani kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu
jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye
thamani ya shilingi milioni 4
Waendesha Bodaboda wakiwa wamejipanga mara baada ya kukabodhiwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vikoti maalum vya usalama
barabarani kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es
salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya
shilingi milioni 4. Kulia ni Ofisa mwandamizi wa kampuni hiyo Bi. Sophia
Kaihula.
……………………………………………………………………………………………………………
Nape Apania Kuiboresha Tasnia ya Habari
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu. ……………………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Sekta ya
habari ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi na serikali
yao. Ndiyo maana wanazuoni hupenda kusema kuwa habari ni muhimili wa nne
wa dola. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kuchekecha huku na huko,
Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli akamteua mtu mahiri kuongoza sekta hii, Mhe. Nape Moses
Nnauye.
Kwa uteuzi
huu ninadiriki kusema hatimaye Wizara imepata mtu sahihi na mchapakazi
anayeweza kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais Magufuli na ni dhahiri
kabisa kuwa kumpa Mhe. Nape ni kuthibitisha usemi wa wahenga usemao
upele umepata mkunaji.
DC HAPI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU, MBWENI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo
amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero
mbalimbali.
Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mkuu wa Wilaya akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam na mainjinia wa manispaa alitembelea eneo hilo na kuona adha inayowapata wananchi.
Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mkuu wa Wilaya akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam na mainjinia wa manispaa alitembelea eneo hilo na kuona adha inayowapata wananchi.
MBUNGE WA MONDULI JULIUS KALANGA AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MORINGE
Mbunge wa Monduli Julius Kalanga akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Moringe iliyoko wilayani huko jana wakati wa mahafali ya kidato cha sita.picha zote na Mahmoud Ahmad arusha
Mbunge wa Monduli Julius Kalanga akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Moringe iliyoko wilayani huko jana wakati wa mahafali ya kidato cha sita.picha zote na Mahmoud Ahmad arusha
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika mahafali hayo yaliyofanyika jana wilayani Monduli.
Mkakati wa utozaji wa faini kwa Wamiliki wa ardhi.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rehema Kilonzi (Kushoto) akielezea mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu hatua ya kazi ya mkakati wa utozaji wa faini kwa Wamiliki wa ardhi waliokiuka masharti ya uendelezaji na ulipaji kodi ya pango la ardhi leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Uliopo jijini Dar es Salaam.
Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO.
MKUU WA WILAYA YA MOSHI ,NOVATUS MAKUNGA AAJIONEA ATHARI YA MAFURIKO
Mkuu
wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu
alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya
kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya
kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu
wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi
ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau
anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi
kabla ya ndege kuruka.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa
ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo
lililo athirika kwa mafuriko.
Maeneo
mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji
vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.
Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.
Maashamba yamejaa maji ,
Maeneo
mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika
maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.
Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.
Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MAAFISA WATEULE DARAJA LA KWANZA , MKOANI MOROGORO
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum
iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja
la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi
la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akimvisha cheo cha RSM mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili.
Baadhi ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano na baadhi ya Wawakilishi wa Vyombo vya Habari, Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza waliosimama mstari wa nyuma.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO SAID MECKY SADICK AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WILAYA YA HAI.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na
watumishi,wakuu wa idara za Halmashauri na Wenyeviti wa vijiji na
vitongoji katika wilaya ya Hai wakati wa kikao cha utamburisho
kilichoafnyika katika ukumbi wa KKKT Bomang’ombe.
Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali katika wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya watumishi na viongozi mbalimbali wa Dini wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Hai,Said Mderu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Wenyeviti wa vitobgoji na vijiji,
PROF.MUHONGO ASAINI KIBALI CHA KUHAMISHA LESENI YA MADINI
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo,(katikati) akiwa na ujumbe utoka ubalozi wa china ukuongozwa na kansela Gou
Haodong(kulia kwa Waziri) pamoja na watendaji wa Wizara wakiwa katika kikao cha pamoja kabla ya kusainiwa kwa kibali cha
uhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo-
ngeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu EM Tanzania Limited.
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo akisaini kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa
Dhahabu ZEM Tanzania Limited, tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini .
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo( wa pili kulia), Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(wa pili kushoto) na Maneja wa
ampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo kwa pamoja wakionesha kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa
kati wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda
Kampunia uchimbaji wa Dhahabu ZEM
Tanzania Limited,uchimbaji wa madini hayo utafanyika katika kijiji cha
Nyasirori Wilayani Butiama Mkoani Mara kuanzia mwezi Desemba mwaka 2016.
Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(kushoto) akiweka saini kitabu cha wageni ofisi kwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo(kulia) mara baada ya kumaliza kutano wao.
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kulia), Wakibadilishana mawazo na Kansela wa ubalozi wa China, Gou
Haodong(wa pili kushoto) katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini baada ya kumaliza kusaini kibali cha kuhamisha leseni
chimbaji wa madini katika kijiji cha Nyasirori wilayani Butiama utakaoanza mwezi Desemba mwaka huo, Maneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo(kulia)
WANDISHI ZANZIBAR WAPEWA semina JUU YA GONJWA LA KIPINDUPINDU
Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Muh’d Dahoma akifungua mafunzo ya
siku moja kwa wandishi wa Habari kuhusu maradhi ya kipindupindu katika
Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Zanzibar Nd. Kheri Makame Kheri akitoa ufafanuzi kuhusiana na maradhi hayo na kuwataka waandishi kujikita zaidi kuelimsha jamii.
Mwandishi wa habari kutoka Zenj F M Radio Mustafa akichangia mada zilizowasilishwa katika mafunzo ya siku moaja ya waandishi wa habari iliyofanyika Wizara ya Afya Zanzibar Mnazimmoja.
Waajiri Wote Wanaodaiwa Malimbikizo Ya Michango Ya NSSF watakiwa Kulipa Michango Kabla Ya Tarehe 30.06.2016
Bw. James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza na waandhishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Benjamin Mkapa wakati akielezea kuhusu waajiri wanaodaiwa madeni sugu ya michango ya wafanyakazi wao na kutamka kwamba wasipolipa michango hiyo mpaka ifikapo Juni 30 mwaka huu shirika hilo linawapeleka mahakamani, kulia ni mmoja wa maofisa waandamizi wa shirika hilo Bw. Salim Khalifan pamoja na maofisa wengine wa shirika hilo waliohudhuria katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo wakati Bw James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza nao katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………………………………
Shirika la Taifa la Hifadhi ya
jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa
malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla
ya tarehe 30.06.2016.
Waajiri ni moja kati ya wadau
wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12
(1) cha sheria ya NSSF, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili.
- Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa.
- Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika.
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha
sheria ya NSSF no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe
michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa
mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe
umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo
ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.
Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa
sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la
kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi
wao kwa wakati.
Kitendo cha kutowasilisha
michango ya wafanyakazi wao kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai
kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya NSSF na ambayo adhabu
yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu
unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.
BANDARI YA DAR KUUNGANISHA SINGAPORE NA EAC
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia ) na ujumbe wake kabla ya mazungumzo yao , Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………….
BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU YAPITISHWA NA BUNGE MJINI DODOMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihitimisha hoja ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akijibu baadhi ya hoja za kuhitimisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akijibu baadhi ya hoja za kuhitimisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipongezwa na wabungeu)baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na wabungeu)baada ya
bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili
27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akipongezwa na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Angella mabula (kulia) na Mbunge wa Buchosa, Dkt. Charles Tizeba baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Makatibu Wakuu wa Ofisi yake baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Kutoka kushoto ni Erick Shitindi, Dkt. Hamis Mwinyimvua na Uledi Mussa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Wengine pichani ni Makatibu Wakuu wa ofisi ya Waziri Mkuu, Erick Shitinidi ( kushoto) na Dkt. Hamis Mwinyimvua (watatu kushoto)) na Dkt (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Wengine ni Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto) na na wapili kushoto ni Uledi Mussa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyakazi na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Watendaji wakuu wa mifuko ya Jamii baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Watendaji wakuu wa mifuko ya Jamii baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Wafanyakazi na Watendaji wa Ofisi
ya Waziri Mkuu, baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni
mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri, Naibu
Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watndaji wa Ofisi na Taasisi zilizochini ya
Wizara yake baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni
mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MJANE WA MWALIMU BABA WA TAIFA MAMA MARIA ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI LEO
Mama
Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na
mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari
wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana
mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka mingi
iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John
Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo
yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na
nvijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa..
PICHA NA IKULU
Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.
Mama Maria Nyerere aliyeongozana
na Mwanae Mheshimiwa Makongoro Nyerere amesema kukamilika kwa daraja
hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha
mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo
hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti
haikuwezekana.
Aidha, Mama Maria Nyerere
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha
kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa
na mmewe katika ujenzi wa nchi.
“Mimi ninamshukuru sana Rais
kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu akamjaalia akasema
kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana, na
familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania
wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa
ni nani?” Amesisitiza Mama Maria Nyerere.
Daraja la Nyerere lenye urefu wa
meta 680, upana wa meta 32, njia sita za magari na barabara unganishi
zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano Dkt.
John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi
muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016
CCM ZANZIBAR YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SH. MIL.5 KWA WAHANGA WA MAFURIKO NA KIPINDUPINDU ZANZIBAR
Katibu
wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi,
Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa
pili wa rais, Joseph Abdallah Meza huko kwa ajili ya kuwasaidia wahanga
wa mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere “C” Unguja.Katibu
wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi,
Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa
pili wa rais, Joseph Abdallah Meza huko kwa ajili ya kuwasaidia wahanga
wa mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere “C” Unguja.
Katibu wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi, Waride Bakar Jabu akikagua wahanga wa mafuriko katika kambi ya mwanakwere zanzibar.
USAID WAZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MTWARA
MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akizungumza wakati wa Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Abdul
Kitula ambaye ni mtaalam wa fedha wa mradi wa PS3 akizungumza kwa niaba
ya Mkurugenzi wa Mradi huo wakati wa uzinduzi hii leo mjini Mtwara.
Mwakilishi
wa USAID, Laura Kikuli alikuwepo na kutoa salamu zake katika uzinduzi
huo a,mbao ulishirikisha watendaji wa Halamashauri zote za Mkoa wa
Mtwara.
Baadhi ya viongozi wa meza kuu wakifuatilia hotuba za ufunguzi
Washiriki mbalimbali ambao ni watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Msaidizi Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akisema neno.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu pamoja na wakuu wa Wilaya za Mkoa huo
wakifuatilia mawasilisho kutoka kwa maafisa Mradi wa PS3.
Afisa Rasilimali watu wa mradi wa PS3, Godfrey Nyombi akitoa mada.
**************
Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma,
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID),
umefanyika mjini Mtwara siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016.
No comments :
Post a Comment