Pages

Thursday, April 28, 2016

. MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS VLADMIR PUTIN WA URUSI NA KUFUNGUA MKUTANO WA MAMBO YA FEDHA KWA WANAWAKE LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
SU2
SU4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
SU5 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
SU6 
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na Kimataifa Mhe. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Kwa ajili ya kuonana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi. Katikati Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
SU7 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu  mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa leo April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR)
SU8 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu  mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa leo April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR)
SU9

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

DOM1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
DOM2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
DOM3 
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Dodoma kutokea mjini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 

Timu za mpira wa pete na miguu za Bunge zapongezwa kwa kufanya vizuri mashindano ya MuunganoAK1 
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Tabora mjini Mhe. Mwanne Nchemba (CCM) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
AK3 
Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (CHADEMA) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
AK4 
Wabunge wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
AK5 
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (katikati) mara baada ya kumalizika mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma.
AK6 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi Seleman Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake waliomtembelea leo Bungeni, mjini Dodoma.
AK8 
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Bungeni, mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewapongeza wabunge kwa kushiriki vizuri mashindano ya Muungano yaliyofanyika Zanzibar na kurudi salama mjini Dodoma kuendelea na majukumu yao.
Pongezi hizo za Spika zimetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kwa niaba ya Spika alipokuwa akitoa matangazo kabla ha kuahirisha shughuli za Bunge hadi jioni ambapo Bunge linaendelea kujadili hoja ya Hotuba za Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo.
Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo ni timu za mpira wa miguu na pete ambapo timu ya mpira wa pete imefanya vizuri kwa kuishinda timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa magoli 18 kwa magoli 15 wakati timu ya mpira wa miguu zilitoka sare ya kufungana goli 1:1
Kushiriki kwa Wabunge katika mashindano hayo yamelenga kuimarisha udugu uliopo kati ya pande mbili za Muungano na kuwapa fursa Wabunge kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha afya zao.
Aidha, michezo kwa Wabunge inatoa nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni kielelezo cha msingi kinachozaa Viongozi bora wanaotokana na sekta ya michezo.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanafursa kubwa ya kufanya mazoezi mbalimbali katika kujenga na kuimarisha timu za Bunge hilo ili kujenga pia ujirani mwema.
Ushiriki wa Wabunge kwenye mashindano siyo mara ya kwanza, Wabunge hao hushiriki michezo mbalimbali, wanashiriki mpira wa miguu wakiwa watani wa Jadi wa timu za Simba na Yanga, Februari 4, 2012 walishiriki mazoezi ya viungo yaliyoendeshwa na klabu inayojulikana kama “Kitambi noma” kutoka mjini Unguja kwa kuzingatia Bunge lina eneo mahususi la kufanyia mazoezi mazoezi ya viungo (Gym).

WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUWAWA MKOANI MBEYA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Butusyo Mwambelo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya  (Hawapo pichani)katika kuzngumzia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu wakati wakijaribu kufanya uhalifu katika duka la kuuzia  vinywaji mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ambayo ilikuwa ikitumika na majambazi hao katika tukio la kutaka kufanya uhalifu kwenye duka la vinywaji mali ya Hamisi mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya April 27 mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao .
Baadhi ya askari polisi wakifuatilia kwa makini mkutano wa kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa mbeya Butusyo Mwambelo wakati akizungumza na waandsihi wa habari kufuatia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu waliotaka kufanya uhalifu katika duka la vinywaji vya jumla linalomilikiwa na ndugu Hamisi Mkazi wa Matundasi Chunya Mkoani Mbeya .
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.

Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu-Mbeya)
JESHI  la Polisi mkoani Mbeya  limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.

MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF

NSSF 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF), Profesa Godius Kahyarara, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

bun1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (kulia) wakati alipomuuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Kushoto ni Mbenge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
bun5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kwahani na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi  (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge  mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Katikati ni Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun6 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Bariadi na Mwenyekiti wa Bunge Mtemi Andrew Chenge kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun7 
Mbunge wa Welezo, Saada  Salum Mkuya akichangia Bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

APPOINTMENT TO THE CHAIRMAN, VICE CHAIRMAN AND BOARD MEMBERS OF THE TANZANIA COMMUNICATION REGULATORY AUTHORITY (TCRA)

logo 
The Chairman of the Nomination Committee, established under section 8(1) (a) of the TCRA Act. No. 12 of 2003, invites Tanzanians with relevant qualifications as spelt out herein to apply for appointment to fill the positions of the Chairman, Vice Chairman and  Board members of Tanzania Communication Regulator Authority.  Attention is hereby drawn that all applicants are required to observe the provisions of Sections 7(5) and 11 of the TCRA Act,  2003 as well as the TCRA Code of Conduct relating to conflict of interest.
Qualifications required:
As per the First Schedule of the TCRA Act 2003, the following are the minimum qualifications for appointment to the TCRA Board:
  1. Should be a graduate of a recognized university;
  2. Have at least 10 years experience in one or more of the fields of Management, Law, Economics, Finance, Engineering, Broadcasting, ICT or related fields;
  3. Have knowledge of the communication industry;
  4. Should satisfy the Nomination Committee that he/she is unlikely to have a conflict of interest under Section11 of the Act;
  5. Be willing to serve as member to the board.
All applications including detailed Curriculum Vitae and names and addresses of three references (including current or last employer) should be sent to the address below so  as reach the Chairman of the TCRA Nomination Committee by 23rd May, 2016
The Chairman,
TCRA Nomination Committee,
Ministry of Works, Transport and Communication,
14 Jamhuri Street,
P.O.BOX 2645,
11470 DAR ES SALAAM

Tigo, mgahawa wa Samaki Samaki waingia ubia

Meneja wa Huduma za Masoko Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiongea na wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na Mgahawa wa Samaki samaki. Kulia ni Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa Samaki samaki, Saum Wengert.
 
Meneja wa Huduma za Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiwa na Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa wa Samaki samaki, Saum Wengert wakionyesha mkataba wa ushirikiano wa kibiashara waliosaini kati ya kampuni ya Tigo na Mgahawa huo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar Es salaam.   
…………………………………………………………………………………………….
Kampuni ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania, leo imeingia   ubia na mgahawa ya Samaki Samaki  ambao ilianzishwa tangu  mwaka 2007  ukiwa na matawi matatu  yaliyopo Mlimani City, City Centre na Masaki Jijini Dar es salaam,  ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja  kwa kuleta  bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja. Akitangaza ubia huyo jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout aliviambia
vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo  ni moja ya alama ambazo zinajenga imani  kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha  kupitia migahawa ya Samaki Samaki Tigo imeweka  mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya
Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja  wake kufurahia  intaneti ya kasi na ya haraka wakati wakila  na kunywa  kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula  vinavyotokana na mazao ya baharini hapa nchini.
“Tunaamini ushirikiano wetu  utandelea kuonesha ni jinsi gani tumejikita  kwenye kuboresha  mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya
kidijitali na kuongoza kwenye kutoa  teknolojia ya kisasa  na ubunifu kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez.
  Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema  Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania  na wameungana na Tigo  ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa ubunifu  nchini kuwapatia wateja wake   kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za Tigo  zilivyo  hususani uzoefu kwenye mtandao wa bure na wa kasi wa  intaneti. Kwa ushirikiano huu  tutawapatia wateja wetu  miradi mingi mipya, maboresho  pamoja na ofa. Kufanya kazi na Tigo sio kwamba kunahusu  sisi kupata fedha tu, bali inahusu  ni nini cha ziada tunachoweza kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika  ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza  kufanya kazi pamoja  na kampuni iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.Tunaweza kuwa ni  mgahawa unaoongoza kwa vyakula  vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini  tunapenda kufanya  jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu. Huduma za Tigo zinazotarajiwa kuwepo  kwenye migahawa ya Samaki Samaki ni pamoja  huduma ya bure ya intaneti  bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na Tigo Music.

BOSTON CITY CAMPUS TANZANIA, BRANCH NOW OPEN

Boston City Campus and Business College carries a legacy of over 20 years in South
Africa. It currently has 44 branches with over 25000 students studying every
year. In Tanzania, Boston has opened its first branch outside South Africa, 45th
Branchin total this year.
Boston offers Professional Courses and Short Learning Programs with plans to introduce tertiary education in the future. These are further learning programs which will enhance one’s skills and assist to get better jobs. They have extended their wide range of
courses which they offer in South Africa in various fields to Tanzania. 
Students can choose from multiple course under various categories such as
Accounting, ICT, Business Management, Business Communications, Marketing and
many more. There are professional courses offered at their college such as ACCA
and CompTIA certified A+, N+ and many more.
The teaching methodology Boston is bringing to Tanzania is quite different from the conventional way of classroom teaching. At Boston, a student would study on a computer assigned to him or her, for a scheduled time slot. All the teachings are imparted in the form of video tutorials which the student views on his computer screen and listens to through earphones. This enables the student to learn on a one to one
basis.
This type of teaching method gives multiple benefits to the student: The student will be able to study at his own pace without having to worry about keeping pace with other students. The student will have a prescheduled flexible timetable to study at the college, unlike going to a classroom where he has to adjust his schedule to
the class’s timings.
While a student can be studying one subject on a computer, the student sitting next to him can be studying an entirely different subject at the same time. There is a flexibility for the student to enroll whenever he wants, all round the year. Also, as the student is studying, he can view the videos multiple times, till he understands the concepts, by forwarding or rewinding the video.
The exams too are taken at their own ease, once they are done studying a module. Most of these exams are
computer based and will be assessed at their headquarters in South Africa. While the learning is computer based, Boston also provides course books to the students, price of which is already included in the fee.
In the case that the student is having difficulty in understanding the tutorial, there are Training Advisors to help the students clear their doubts and move forward. The training advisor will be able to tutor the student on a one to one basis. 
If the student still does not understand, they have the option to contact experts in South Africa who are qualified for each subject that is being taught here.
This will be done from the college itself. Further, for benefit ofthe students, refresher sessions are conducted in their workshop room on weekly basis where a student can participate if he is having any difficulty understanding any concepts and get clarifications.
Access to the computers and video tutorials is only from the college. It is mandatory for the student to be present at the college for the tutorials, as Boston wants the students to study under a controlled environment. This way the progress of each student can be monitored. However, the student is provided with study material and books which are kept by them, to be used to revise and prepare for the next class.
More information on Boston City Campus & Business College is available at www.boston.co.tz  0765 008827 or 0685 626366

Wamuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuteketeza ghala la meno ya tembo liliopo nchini

temMwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Bw. Shubert Mwarabu (katikati) akielezea kuhus Kampeni yao ya kuokoa Tembo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Kampeni hiyo Bw. Lameck Mkuburo pamoja na Bw. Arafat Mtui (wa kwanza kulia).
(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
……………………………………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO-  Dar es Salaam.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Okoa Tembo Tanzania imemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuteketeza ghala la meno ya tembo liliopo nchini kufuatia Tanzania kusaini mpango wa kuwalinda Tembo mwaka 2014 unaozuia uuzaji wa meno ya Tembo kwa muda wa miaka 10.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar s Salaam na Mwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Tanzania Bw.Shubert  Mwarabu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Barua ya Wazi waliyomwandikia Mheshimiwa Rais.
Amesema Tanzania inafungwa na mkataba wa kimataifa wa biashara juu ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka (Convetion on International Trade in Endangered Species-CITES) ambao unabainisha kuwa Tanzania kwa sasa haiwezi kuuza ghala lake la meno ya Tembo.
Amesema uhifadhi wa meno hayo unaigharimu serikali fedha nyingi  na kufafanua kuwa kwa sasa Tanzania ina hifadhi kubwa ya meno ya Tembo yaliyokamamwa kutokana na ujangili.
“Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kasi yake ya utendaji tangu kuchaguliwa kwake,tunamuomba atekeleze lengo la tatu la kampeni yetu ya Okoa Tembo wa Tanzania kwa kuliteketeza hadharani ghala la meno ya tembo,tunaona hakuna haja ya kuendelea kuwa na ghala hili” amesema Bw.Mwarabu.
Amesisitiza kuwa ombi lao kwa Rais kutaka ghala la meno ya Tembo liteketezwe kutasidia kutuma ujumbe mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa kiasi cha serikali kuona wepesi kuteketeza hazina hiyo.
“ Tunataka ieleweke kwamba kuharibu ghala la meno ya Tembo kunatuma ujumbe mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa na kuwa ujangili ni kosa la jinai lisilokubalika” Amesisitiza.
Amesema ipo haya ya Tanzania kuunga mkono mpango wao wa kuteketeza ghala la meno ya Tembo kama inavyotarajiwa katika nchi ya Kenya ambayo inatarajia kuteketeza ghala lake la meno ya Tembo hadharani Aprili 30 mwaka  huu.
Amezitaja nchi ambazo zina mpango wa kuchukua hatua kama ya Kenya kuwa ni Ethiopia,Chad,Gabon, Mozambique na Congo.
Naye mmoja wa wajumbe wa Kampeni ya Okoa Tembo wa Tanzania Bw.Arafat Mtui akizungumza katika mkutano huo amesisitiza kuwa kuendelea kuwepo kwa ghala hilo nchini Tanzania kunawapa moyo wafanyabiashara haramu wa meno hayo kuona kuwa ipo siku biashara hiyo itaendelea tena.
Amesema Kampeni yao ya Okoa Tembo wa Tanzania  inaendelea kusisitiza kuwa  kuwa hatma ya Tembo wa Tanzania iko mikononi mwa watanzania,  hivyo ni vema Serikali ikashirikiana na wadau mbalimbali  kuchukua hatua madhubuti kuokoa viumbe hao walio hatarini kutoweka kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Uchukuzi SC, Tamisemi kama fainali kesho

mol1Nahodha wa timu ya Uchukuzi SC, Godwin Ponda akimtambulisha mgeni rasmi wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tamisemi, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mei Mosi, Joyce Benjamin kwa kipa wake Herbat Steven, nyuma ni mkuu wa benchi, Kenneth Mwaisabula. Uchukuzi walifungwa magoli 2-0.
mol2 
Mwamuzi Robert Mkatakiu (aliyeshika kadi ya njano) akimuangalia mchezaji Kombo Ally wa Tamisemi aliyelala chini baada ya kuumia. Mchezaji huyo alionyeshwa kadi hiyo pamoja na nahodha wa Uchukuzi Godwin Ponda (kulia). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
mol3 

Wachezaji wa timu za Uchukuzi SC na Tamisemi wakisubiri mpira wa kona upigwe na Omary Said wa Uchukuzi (haonekani pichani). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
mol4 
Kipa wa Tamisemi,, Leonard Mkinga (katikati ya goli) akiwapanga wachezaji wake kabla Uchukuzi hawajapiga mpira wa kona. Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
mol5 
Tatu Kitula (mwenye mpira) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga bao katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Mei Mosi dhidi ya TPDC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 33-14.
mol6 
Matalena Mhagama (GA) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga, pembeni ni Dora Njau (GD) wa TPDC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 33-14.
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Uchukuzi SC na Tamisemi kesho zitacheza mchezo wao wa mwisho wa netiboli, ambao ni kama fainali kutokana na timu zote kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, kila mmoja akiwa na pointi tisa.
Netiboli inachezwa kwa mtindo wa ligi, ambapo timu hizo zinakamilisha ratiba na mmoja akimfunga mwenzake atakuwa bingwa au zikitoka sare ya idadi yeyote ya magoli, basi Tamisemi atatawazwa bingwa kwa kuwa anaidadi kubwa ya magoli ya kufunga, 94 na wenzao wana 87.
Timu ya CDA Dodoma wanafuatia wakiwa watatu baada ya kushinda mchezo mmoja, huku Tanesco na chipukizi wa TPDC wakimaliza mashindano bila kushinda mchwezo wowote. Lakini TPDC inayofundishwa na kocha mzoefu Rose Mkisi inayoundwa na wachezaji wenye umri mdogo kati ya 20-30, ndio timu changa baada na inaonyesha baada ya mwaka mmoja itakuwa tishio kwani itakuwa na uzoefu tofauti na sasa ndio wameanza mwaka huu kushiriki mashindano haya ya Mei Mosi.
Katika mchezo wa soka timu ya Geita Gold Mine itakwaana na Tamisemi kesho katika mchezo wa fainali.
GGM wametinga hatua hiyo baada ya kuwafunga Tanesco kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumaliza mchezo wa nusu fainali bila kufungana.
Penati zote nne za GGM zilifungwa na Gwetu Guvette, Oswald Binamungu, Ally Twist na Mohamed, wakati za Tanesco walizopata ni Said Kondo na Stan Uhagile, na walizokosa ni Hemed Mtumwa na Betwel Kagimbo.Nao Tamisemi waliwachapa Uchukuzi SC kwa magoli 2-0.
Katika mchezo wa netiboli uliochezwa jana jioni Uchukuzi SC waliwafunga chipukizi wa TPDC kwa magoli 33-14. Uchukuzi walikuwa mbele kwa magoli 15-8.
Nayo Tamisemi waliwapeleka jamaa zao CDA na kuwachapa magoli 18-13. Washindi walikuwa mbele kwa magoli 9-8.
Katika kamba kwa wanaume Ukaguzi waliwavuta CWT kwa mivuto 2-0, nayo TPDC wakiwavuta UDOM mivuto 2-0, na Uchukuzi SC walipata ushindi wa chee baada ya Tanesco kuingia mitini; wakati kwa wanawake Tamisemi waliwavuta bila huruma Tanesco mivuto 2-0.
Mbali na netiboli na soka itakayochezwa kesho, pia kutakuwa mechi za kamba wanaume TPDC kucheza na CWT, huku UDOM kuumana na Tanesco; wakati wanaume Uchukuzi SC watakutana na TPDC.

 

KAMPUNI YA SGA SECURITY YAGAWA VIFAA VYA USALAMA BARABARANI KWA WAENDESHA BODABODA MBEZI

SGS01Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti maalum la usalama barabarani Bw. Thobias Msua  mmoja wa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4 na wametoa msaada huo kwa waendesha  bodaboda zaidi ya 4000, makabidhiano hayo yamefanyika Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam.
SGS1Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti maalum la usalama barabarani kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4
SGS2 SGS4Waendesha Bodaboda wakiwa wamejipanga mara baada ya kukabodhiwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani.
SGS5Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi  vikoti maalum vya usalama barabarani  kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4. Kulia ni Ofisa mwandamizi wa kampuni hiyo Bi. Sophia Kaihula.
……………………………………………………………………………………………………………

Nape Apania Kuiboresha Tasnia ya Habari

index 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu. ……………………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Sekta ya habari ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao. Ndiyo maana wanazuoni hupenda kusema kuwa habari ni muhimili wa nne wa dola. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kuchekecha huku na huko, Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akamteua mtu mahiri kuongoza sekta hii, Mhe. Nape Moses Nnauye.
Kwa uteuzi huu ninadiriki kusema hatimaye Wizara imepata mtu sahihi na mchapakazi anayeweza kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais Magufuli na ni dhahiri kabisa kuwa kumpa Mhe. Nape ni kuthibitisha usemi wa wahenga usemao upele umepata mkunaji.

DC HAPI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU, MBWENI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali.
Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mkuu wa Wilaya akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam na mainjinia wa manispaa alitembelea eneo hilo na kuona adha inayowapata wananchi.

MBUNGE WA MONDULI JULIUS KALANGA AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MORINGE

JU1 
Mbunge wa Monduli Julius Kalanga akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Moringe iliyoko wilayani huko jana wakati wa mahafali ya kidato cha sita.picha zote na Mahmoud Ahmad arusha 
JU2 
Mbunge wa Monduli Julius Kalanga akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Moringe iliyoko wilayani huko jana wakati wa mahafali ya kidato cha sita.picha zote na Mahmoud Ahmad arusha 
JU3
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika mahafali hayo yaliyofanyika jana wilayani Monduli.

Mkakati wa utozaji wa faini kwa Wamiliki wa ardhi.

index 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rehema Kilonzi (Kushoto) akielezea mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu hatua ya kazi ya mkakati wa utozaji wa faini kwa Wamiliki wa ardhi waliokiuka masharti ya uendelezaji na ulipaji kodi ya pango la ardhi leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Uliopo jijini Dar es Salaam.
Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO.

Sio kila homa ni malaria, nenda ukapime

UMM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipima afya yake kujua kama ana vimelea vya ugonjwa wa malaria baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mjini Dododma Aprili 25 mwaka huu.
……………………………………………………………………………………………

MKUU WA WILAYA YA MOSHI ,NOVATUS MAKUNGA AAJIONEA ATHARI YA MAFURIKO

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi kabla ya ndege kuruka.
Mkuu wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo lililo athirika kwa mafuriko.
Maeneo mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.
Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.
Maashamba yamejaa maji ,
Maeneo mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.
Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.
Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu.
 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MAAFISA WATEULE DARAJA LA KWANZA , MKOANI MOROGORO

1Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
2 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
3 
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
4 

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akimvisha cheo cha RSM mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili.
5 
Baadhi ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza kama wanavyoonekana katika picha.
6 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
7 
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni kama wanavyoonekana katika picha.
8 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano na baadhi ya Wawakilishi wa Vyombo vya Habari, Mkoani Morogoro.
9 
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza waliosimama mstari wa nyuma.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO SAID MECKY SADICK AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WILAYA YA HAI.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na watumishi,wakuu wa idara za Halmashauri na Wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika wilaya ya Hai wakati wa kikao cha utamburisho kilichoafnyika katika ukumbi wa KKKT Bomang’ombe.
Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali katika wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya watumishi na viongozi mbalimbali wa Dini wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Hai,Said Mderu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Wenyeviti wa vitobgoji na vijiji,

PROF.MUHONGO ASAINI KIBALI CHA KUHAMISHA LESENI YA MADINI

M1 
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo,(katikati) akiwa na ujumbe utoka ubalozi wa china ukuongozwa na kansela Gou
Haodong(kulia kwa Waziri) pamoja na watendaji wa Wizara wakiwa katika kikao cha pamoja kabla ya kusainiwa kwa kibali cha
uhamisha leseni ya uchimbaji wa kati  wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia  Geo-
ngeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu EM Tanzania Limited.
M2 
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo akisaini kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati  wa madini kutoka
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa
Dhahabu ZEM Tanzania Limited, tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini .
M3 
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo( wa pili kulia), Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(wa pili kushoto) na  Maneja wa
ampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo kwa pamoja wakionesha kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa
kati  wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia  Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda
Kampunia uchimbaji wa Dhahabu ZEM Tanzania Limited,uchimbaji wa madini hayo utafanyika katika kijiji cha Nyasirori Wilayani Butiama Mkoani Mara kuanzia mwezi Desemba mwaka 2016.
M4 
Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(kushoto) akiweka saini kitabu cha wageni ofisi kwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo(kulia) mara baada ya kumaliza kutano wao.
M5 
Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kulia), Wakibadilishana mawazo na Kansela wa ubalozi wa China, Gou
Haodong(wa pili kushoto) katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini baada ya kumaliza kusaini kibali cha kuhamisha leseni
chimbaji wa madini katika kijiji cha Nyasirori wilayani Butiama utakaoanza mwezi Desemba mwaka huo, Maneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo(kulia)

YANGA YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

yangasc 
Coastal Union imepoteza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga baada ya washabiki wake kuwa chanzo cha Mwamuzi kuvunja mchezo huo uliofanyika Aprili 24, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

WANDISHI ZANZIBAR WAPEWA semina JUU YA GONJWA LA KIPINDUPINDU

1Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Muh’d Dahoma akifungua mafunzo ya siku moja kwa wandishi wa Habari kuhusu maradhi ya kipindupindu katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
2 3 
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Zanzibar Nd. Kheri Makame Kheri akitoa ufafanuzi kuhusiana na maradhi hayo na kuwataka waandishi kujikita zaidi kuelimsha jamii.
4 
Mwandishi wa habari kutoka Zenj F M Radio Mustafa akichangia mada zilizowasilishwa katika mafunzo ya siku moaja ya waandishi wa habari iliyofanyika Wizara ya Afya Zanzibar Mnazimmoja.
5 
Mtaalamu wa mabadiliko ya tabia katika afya na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Salum Aboubakar akitoa tathmini ya maradhi ya kipindupindu tokea yalipoanza mwezi Septemba mwaka jana mpaka hivi sasa.
6 
Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya siku moja juu ya maradhi ya kipindupindu wakifuatilia mafunzo hayo katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar..

WANAMUZIKI NA WADAU WA MUZIKI KUKUTANA NA MKUU WA MKOA DSM ALHAMISI HII

MAKOWanamuziki wa dansi, taarab, bongo fleva na wadau wa muziki waishio Dar es Salaam, Alhamisi hii watakutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ili kubadilisha mawazo juu mwenendo wa kazi zao.

Waajiri Wote Wanaodaiwa Malimbikizo Ya Michango Ya NSSF watakiwa Kulipa Michango Kabla Ya Tarehe 30.06.2016

1 
Bw. James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la  Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza na waandhishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Benjamin Mkapa wakati akielezea kuhusu waajiri wanaodaiwa madeni sugu ya michango ya wafanyakazi wao na kutamka kwamba wasipolipa michango hiyo mpaka ifikapo Juni 30 mwaka huu shirika hilo linawapeleka mahakamani, kulia ni mmoja wa maofisa waandamizi wa shirika hilo Bw. Salim Khalifan pamoja na maofisa wengine wa shirika hilo waliohudhuria katika mkutano huo.
2 
Baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwa katika mkutano huo.
_MG_5980 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo wakati Bw James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la  Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza nao katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………………………………
Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla ya tarehe 30.06.2016.
Waajiri ni moja kati ya wadau  wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12 (1) cha sheria ya NSSF, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili.
  1. Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa.
  1. Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika.
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya NSSF no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.
Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Kitendo cha kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao  kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya NSSF na ambayo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.

BANDARI YA DAR KUUNGANISHA SINGAPORE NA EAC

MAJ1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAJ2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia ) na ujumbe wake kabla ya mazungumzo yao , Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………….

BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU YAPITISHWA NA BUNGE MJINI DODOMA

w2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihitimisha  hoja  ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)w1Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  akijibu baadhi ya hoja za  kuhitimisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  akijibu baadhi ya hoja za  kuhitimisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
w3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipongezwa na wabungeu)baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipongezwa na wabungeu)baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
w4 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akipongezwa na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Angella mabula (kulia) na Mbunge wa Buchosa, Dkt. Charles Tizeba   baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
w7 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na  Makatibu Wakuu wa Ofisi yake baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Kutoka kushoto ni Erick Shitindi, Dkt. Hamis Mwinyimvua na Uledi Mussa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
w8 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama   baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Wengine pichani ni Makatibu Wakuu wa ofisi ya Waziri Mkuu, Erick Shitinidi ( kushoto) na Dkt. Hamis Mwinyimvua (watatu kushoto)) na Dkt (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
w9 
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia)  baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016.  Wengine ni Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto) na  na wapili kushoto ni  Uledi Mussa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyakazi na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
w11 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Watendaji wakuu wa mifuko ya Jamii baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Watendaji wakuu wa mifuko ya Jamii baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
w12Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Wafanyakazi na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
w13Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu  na Watndaji wa Ofisi na Taasisi zilizochini ya Wizara yake  baada ya  bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MJANE WA MWALIMU BABA WA TAIFA MAMA MARIA ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI LEO

mama1Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,  akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam. Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka  mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina  la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na nvijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa..
PICHA NA IKULU
mama2 mama3 
Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.
Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongoro Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.
Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere  kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.
“Mimi ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni nani?” Amesisitiza Mama Maria Nyerere.
Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 32, njia sita za magari na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

SERIKALI YAZUIA UINGIZAJI HOLELA WA MCHELE

images 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya dola viimarishe ulinzi kwenye mipaka ya nchi na hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi

CCM ZANZIBAR YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SH. MIL.5 KWA WAHANGA WA MAFURIKO NA KIPINDUPINDU ZANZIBAR

zan1Katibu wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi, Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa pili wa rais, Joseph Abdallah Meza huko kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere “C” Unguja.Katibu wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi, Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa pili wa rais, Joseph Abdallah Meza huko kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere “C” Unguja.
zan2 
Katibu wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi, Waride Bakar Jabu akikagua wahanga wa mafuriko katika kambi ya mwanakwere zanzibar. 

USAID WAZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MTWARA

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akizungumza wakati wa Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 Abdul Kitula ambaye ni mtaalam wa fedha wa mradi wa PS3 akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mradi huo wakati wa uzinduzi hii leo mjini Mtwara.
Mwakilishi wa USAID, Laura Kikuli alikuwepo na kutoa salamu zake katika uzinduzi huo a,mbao ulishirikisha watendaji wa Halamashauri zote za Mkoa wa Mtwara.
 Baadhi ya viongozi wa meza kuu wakifuatilia hotuba za ufunguzi
 Washiriki mbalimbali ambao ni watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akisema neno.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu pamoja na wakuu wa Wilaya za Mkoa huo wakifuatilia mawasilisho kutoka kwa maafisa Mradi wa PS3.
 Afisa Rasilimali watu wa  mradi wa PS3, Godfrey Nyombi akitoa mada.
**************
Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Mtwara  siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016.

No comments:

Post a Comment