Friday, April 1, 2016

Committee of Experts meet in Addis Ababa ahead of the African Finance Ministers Meeting in Ethiopia to Deliberate on Collective goals for Sustainable Development.

n
The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz, during the opening session of the Committee of Experts of the 9th Joint Annual Meetings of the African Union Specialized Technical Committee on Finance, Monetary Affairs, Economic Planning and Integration and the ECA Conference of African Ministers of Finance, Planning and Economic Development, held in Addis Ababa, Ethiopia from 31st March to 5th April 2016.
(picture courtesy of Tanzanian Embassy in Addis Ababa Ethiopia)
……………………………………………………………………………………………………..
The work on implementing Africa’s Development Agenda 2063 has been directed towards helping African countries overcome their continued vulnerabilities and promote diversification in order to accelerate the achievement of structural transformation.
The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz, said this during the opening session of the Committee of Experts of the 9th Joint Annual Meetings of the African Union Specialized Technical Committee on Finance, Monetary Affairs, Economic Planning and Integration and the ECA Conference of African Ministers of Finance, Planning and Economic Development, held in Addis Ababa, Ethiopia from 31st March to 5th April 2016. The Ministerial segment is to kick start its deliberations on the 3rd of April 2016.
The Conference under the theme: Towards an Integrated and Coherent Approach to Implementation, Monitoring and Evaluation of Agenda 2063 and the SDGs at both experts and Ministerial level, will deliberate on pertinent issues of how countries can harmonise frameworks and establish common mechanisms of implementation, monitoring and evaluation to achieve Africa’s collective goals of sustainable development and transformation.
Moreover, the Conference will among other things, address the question of how African countries can adopt and implement effectively the first Ten-Year Implementation Plan of Agenda 2063, suggest ways for the integration of the said plan at national, regional and continental levels and draw lessons from the ongoing process of domesticating the First –Ten Year implementation plan.
The Conference will also discuss the harmonization of Agenda 2063 and 2030 Agenda and provide insight as to how an integrated and harmonized approach for the execution of Agenda 2063 and the Sustainable Development Goals can be designed at national level.
“As you know the foundation for Agenda 2063 lies in the fact that, whilst African countries have achieved remarkable growth performance, our success has been limited in achieving structural transformation,” adding that much remains to be done to achieve inclusive and equitable development in Africa and that the continent’s economies were still exposed to vulnerabilities and shocks that could adversely affect growth prospects.
Ambassador Naimi Aziz, who officiated the Conference in her capacity as the outgoing Chair of the Bureau of the Committee of Experts said that, the successful implementation of the continental Agenda 2063 will depend on each member countries’ ability to strongly link their planning, mobilizing and financing mechanisms.
As she handed over the Chair to South Africa, Ambassador Naimi thanked the joint Secretariat of the African Union Commission and the Economic Commission for Africa for successful organization of the conference and for the technical support  which will be provided to the bureau during the course of the meeting.
 The conference is attended by seasoned and high-level panelists from Africa and other regions, representatives from Regional Economic Communities (RECs) UN Agencies, Civil Society Organizations (CSOs), NEPAD, AfDB and other organizations. It will be interactive so as to give Ministers the opportunities to address the issues elaborated above, discuss and share their views and experiences in the advancement of Africa’s development. 
(From: Tanzania Embassy Addis Ababa, Ethiopia, 1st April 2016)

JESHI LA POLISI LAONGEZA MUDA WA KUHAKIKI SILAHA SASA ITAKUWA NI MIEZI MITATU KWA NCHI NZIMA

 Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mchakato wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo limeongeza muda wa miezi mitatu kwa nchi nzima kuanzia leo.
 Msemaji wa Jeshi Nchini, Advera Bukumbi (kulia), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha  Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya kuzungumza na waandishi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………..

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.
Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.
Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na  kuzisajili na kufanya malipo  katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.
Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa
“Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi” alisema Mssanzya.
Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.
Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.
“Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa,” alisema.

WATENDAJI WATAKIWA KUHAKIKISHA USALAMA WA RASILIMALI ZA MISITU

6Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkururugenzi wa Idara ya Misitu na nyuki kutoka Maliasili Bi. Gladness Mkamba mapema  leo katika kuadhimisha siku ya upandaji miti iliyofanyika ruvu kaskazini Mkoani Pwani.
7Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akitoa maelekezo kwa Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya  Maliasili na Utalii Injinia Angelina Madete( katikati) kuhusu upandaji miti katika sehemu mbalimbali katika hifadhi ya misitu kibaha Mkoani Pwani,mapema hii leo katika siku ya upandaji miti.
8Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkururugenzi wa Idara ya Misitu na nyuki kutoka Maliasili Bi. Gladness Mkamba mapema  leo katika kuadhimisha siku ya upandaji miti iliyofanyika ruvu kaskazini Mkoani Pwani.
PICHA NA MPIGA PICHA WETU
…………………………………………………………………….
EVELYN MKOKOI KIBAHA-PWANI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, amewataka watendaji katika ngazi za uteuzi nchini kushiriki kikamilifu katika kuhahikisha usalama wa rasilimali za misitu.
Naibu Waziri Mpina ameyasema hayo leo katika Pori la Ruvu Kaskazini ikiwa ni siku ya Kitaifa ya kupanda miti na kueleza kuwa Serikali imekuwa na lengo la kupanda miti milioni moja nukta tano (milioni 1.5) kwa mwaka mzima katika kila wilaya, na kuwataka watendaji waliopo katika ngazi za uteuzi yaani Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu wakuu, kuhakikisha lengo hili linafikiwa na kueleza kuwa  viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi hili majina yao yatapelekwa katika mamlaka za uteuzi na kuchukuliwa hatua, hii ikiwa ni njia ya kupima usalama wa rasilimali hizi.
Akiongea na wananchi katika Pori la Ruvu Kaskazini, Mh. Mpina alisema kuwa asilimia 61 ya ardhi ya nchi ipo kwenye hatari ya kuwa jangwa kutokana na  uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti ovyo, na  takwimu zinaonyesha kuwa takribani hekta laki tatu nukta sabini na mbili za misitu zinakatwa kila mwaka kwa matumizi mbali mbali. “mikoa nane nchini iko hatarini kuwa jangwa”. Alisisitiza.
Akielezea athari, zitokanazo na  uharibifu wa misitu, Mh. Mpina alisema taifa linaweza kutumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kununua chakula kuwalisha wa Tanzania kutokana na ukosekanaji wa mvua ,vyanzo vya maji kukauka, upatakinaji wa umeme kuwa wa kusuasua kutokana na uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji.
Kwa upande Mwingine Mh. Mpina alisema kuwa serikali imekata miti kwa sababu mbalimbali za msingi ikiwa ni pamoja ujenzi wa miundo mbinu kama vile barabara, reli ujenzi wa bomba la gesi, hivyo basi kuna jukumu kubwa la kupanda miti mingi zaidi ya hiyo iliyokatwa.
Akitolea Mfano wa taasisi za huduma ya misitu Nchini (TFS) iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,  Mh. Mpina aliainisha kuwa taasisi zote za serikali zisaidie taifa kubainisha ni mazao  gani ya misitu yanaweza kupandwa katika maeneo gani kulingana na mahitaji ili kuweza kunusuru upotevu wa rasimali ya misitu.

Serikali yawashukuru wadau wamichezo walioisaidia Twiga Stars

2Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa Wanawake (Twiga Stars) alipokutana nao leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake (TWFA) Bi. Amina Karuma na Makamu Mwenyekiti wa TWFA Bibi. Rose Kisiwa.
1Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakifuatilia mkutano baina yao na Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
3Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake (TWFA) Bi. Amina Karuma akifafanua jambo wakati wa mkutano baina ya Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam. Kulia niMakamu Mwenyekiti wa TWFA Bibi. Rose Kisiwa.
4Meneja wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) Bibi. Furaha Francis akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (hayupo pichani) na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam.
5Mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) Bi.Fatuma Omary akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (hayupo pichani) na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHUSM.

LUHWAVI AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA NJOMBEA NA RUVUMA LEO

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi akiwasili ukumbini na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe, Deo Sanga maarufu kwa jina la ‘Jah Peole’ kuzungumza na viongozi na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka mkoa huo na mkoa wa Rumuma leo mkoani Njombe
Baadhi ya viongozi wa CCM kutoka mkoa wa Ruvuma, wakiwa kwenye kikao hicho cha viongozi, watumishi wa CCM na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhwavi kilichofanyika leo mkoani Njombe. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Katibu wa CCM mkoa wa Njombe, Osea Mbagike akifanya utambulisho wa waalikwa kwenye kikao cha viongozi, watumishi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Njombe na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi (katikati) kilichofanyika leo mjini Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Deo Sanga.

JOKATE NA MO DEWJI FOUNDATION KUJENGA KIWANJA CHA MICHEZO SEKONDARI YA JANGWANI

Jokate
Mwanzilishi wa ujenzi huo, Jokate Mwegelo akiandika jambo wakati ujenzi wa kiwanja ukiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa kupata uwanja wa michezo ambao unajegwa kwa ushirikiano wa Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Taasisi ya Mo Dewji.
Akizungumza na Mo Blog, Jokate amesema ujenzi wa kiwanja hicho cha michezo ni sehemu ya mipango aliyokuwa nayo baada ya kuanzisha mwaka jana bonanza la Kidoti ambalo lilikuwa na malengo ya kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri kimasomo na kushiriki katika michezo ili kukuza vipaji vyao.
Jokate amesema ameamua kuanza na shule ya Jangwani kwa kutambua kuwa shule hiyo ina hosteli za wanafunzi walemavu na wamekuwa wakipata shida kupata viwanja vya michezo hivyo kupitia kiwanja hicho wataweza kushiriki michezo kwa urahisi zaidi.
“Pale Shule ya Jangwani kuna wanafunzi walio na ulemavu na kama unavyojua mlemavu anatakiwa kufanya mazoezi ili kuweka afya yake vizuri na kama wakitaka kushiriki michezo hadi waende Gymkhana lakini tunawajengea uwanja wa Basketball na Netball,” amesema Jokate wakati akifanya mahojiano na Mo Blog.
Ameongeza kuwa ili kufanikisha ujenzi huo alizungumza na Mohammed Dewji ambaye alikubali kutoa Milioni 10 kupitia Taasisi yake ya Mo Dewji na hivyo kuanza kufanyika kwa ujenzi huo ambao utawawezesha wanafunzi wa Jangwani kushiriki michezo tofauti na hapo awali.
Aidha amesema kuwa ujenzi wa viwanja vya michezo utakuwa endelevu katika shule za serikali ambazo bado hazijawa na viwanja na baada ya kukamilika kwa ujenzi katika shule ya Jangwani amepanga kufanya ujenzi wa viwanja vya michezo katika Shule ya Sekondari Kinyerezi na Shule ya Sekondari Maposeni iliyopo wilayani Peramiho, Ruvuma.
14581134867112 
Ujenzi wa kiwanja cha michezo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani ukiendelea

TAARIFA KUKATIKA KWA UMEME HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI NA ATHARI ZAKE

TAARIFA KWA UMMA

LUHWAVI: WATUMISHI WA CHAMA CHACHU YA CCM KUNG’ARA KATIKA JAMII

Na Bashir Nkoromo, Njombe
………………………………………………
Watumishi wa Chama ni sehemu muhimu inayokifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa bora na imara kwa kuwa ndiyo jiko la kubuni na kuandaa taswira ya muonekano wa Chama katika jamii.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajabu Luhwavi wakati akizungumza na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka wilaya za mkoa wa Njombe na Ruvuma, jana, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo kuzungumza na kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili watumishi wa Chama. 
Alisema, ni kutokana na kutambua umuhimu wa watumishi hao ndiyo sababu Chama Cha Mapinduzi kinafanya kila jitihada kuhakikisha kinakutana nao ili kujua mazigira walioyomo na changamoto na kero zinazowakabili ili kuweza kutafuta njia za kuzitatua kwa kadri inavyowezekana.
“Unajua mimi ndiyo nasimamia utumishi katika chama, kazi zingine zote zinazonihusu naweza kuzifanya kupitia mafaili nikiwa ofisini, lakini hili la kuhusu mazingira na hali za watumishi ambalo pia linanihusu siweze kulifanya nikiwa ofisini, ndiyo sababu nimeamua kufanya ziara hizi, ili niwasilikilize kero na changamoto zinazowakabili tukiwa pamoja”, alisema Luhwavi.

Wakuu wa Mikoa Waagizwa kutumia Mfumo wa Kieletroniki kukusanya Mapato

K2 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao cha kujadili mwelekeo wa bajeti za Mikoa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
K1 
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawalawa Mikoa kutoka Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani)  katika kikao cha kujadili mwelekeo wa bajeti za Mikoa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kilichofanyika katika ukumbiwaKarimjeejijini Dar es Salaam hivikaribuni.
K3 
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Felix Ntibenda (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
K4 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa  Mtwara Mhe.  Fatma Dendego (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
K5 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Rehema Nchimbi (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA JENGO JIPYA LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

9 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais- Muungano Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea kukagua mradi wa ujenzi wa  jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mohamed Omary.
10 
Katibu Mkuu  Ofisi ya Mkamu wa Rais Mbarak Abdulwakil akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais mbele ya Wajumbe wa Kmati ya bunge ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) walipotembelea Ofisini hapo kukagua mradi huo.
11 
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na sheria wakisikiliza kwa makini taarifa ya mradi wa ujenzi wa  jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais iliyokua ikisomwa na Katibu Mkuu (hayupo pichani)
PICHA NA MPIGA PICHA WETU

KAMATI YA NIDHAMU TFF KUKUTANA KESHO

mvella 
Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitaendelea kesho Jumamosi saa 3 asubuhi katika ofisi za TFF zilizopo Karume, na maamuzi yake yatatangazwa saa 7 mchana.
Kamati inakutana kwa ajili ya kumalizia shauri la upangaji wa matokeo Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League) kundi C inayozihusisha timu za Geita Gold, JKT Kanembwa, JKT Oljoro na Polisi Tabora.
Viongozi watakaohojiwa na Kamati ya Nidhamu ni, Yusuf Kitumbo (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabora), Fateh Remtullah (Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabaora), viongozi wa benchi la ufundi Polisi Tabora, Mrisho Selemani, Boniface Komba, Bernard Rabiamu.
Kamati pia itawahoji Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita, Salum Kurunge na mwenyekiti wa Klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita.

KUZIONA SERENGETI BOYS V THE PHARAOHS 2,000/= TU

tanefa17Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi elfu mbili tu (2,000) ndio kitakachotumika katika mchezo wa kesho Jumamosi kati ya Serengeti Boys (Tanzania) v The Pharaohs (Misri) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
TFF imeweka kiingilio cha shilingi elfu mbili tu (2000) uwanja mzima, kutoa nafasi kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuja kushuhudia mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za vijana za Tanzania v Misri.
Serengeti Boys inashuka dimbani kucheza na The Pharaohs mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima nguvu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi na kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya Shelisheli Juni – Julai mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utachezeshwa na waamuzi wa kimataifa wenye beji za FIFA ambao ni Israel Mjuni, akisaidiwa na Soud Lila, Frank Komba, mwamuzi wa akiba Jonesia Rukyaa, huku kamisaa wa mchezo akiwa Isabella Kapera.
Upande wa kikosi cha timu ya Taifa ya Misri kimewasili nchini jana mchana saa 7:30 mchana kwa shirika la ndege la Ethiopia, kikiwa na msafara wa watu 33 wakiwemo wachezaji 25 na viongozi 8.
The Pharaohs wanatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni saa 10 kamili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa, baada ya kuwa wamefanya mazoezi jana jioni katika uwanja wa Karume.
efa17Wakiongea na waandhishi wa habari, makocha wa timu zote mbili, Bakari Shime (Serengeti Boys) na Yasser Muhamadain (The Pharaous) wameshukuru kwa kupata mchezo huo wa kirafiki wa kiamataifa.
Kocha Shime ameishukuru TFF kwa kufanikisha mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa, baadaya kuwa kambini na kucheza michezo ya kirafiki na timu za ndani, wao kama benchi la ufundi watautumia kama kipimo sahihi cha mchezo wa kimataifa katika maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Shelisheli.
Naye Yasser wa The Pharaohs, ameshukuru kwa kupata nafasi ya kucheza na Tanzania mchezo wa kirafiki, kwao ni mara ya kwanza kucheza mchezo wa kirafiki nje ya ukanda wa Afrika Kaskazini, hivyo anaamini kesho kutakua na mchezo mzuri wenye ushindani.

Waziri Simbachawene afanya kikao na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka.

2 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa         (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale.
3 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jaffo.
4 
Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Lwekatare akitoa taarifa ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jaffo.
5 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (wa pili kulia) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
6 
Msajili Masaidizi wa Hazina Jones Mwalemba akitoa ufafanuzi namna  ofisi yake inavyochangia katika kukamilisha mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene  alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
7Mkurugenzi wa Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene  alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
8 
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene  alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………..
Na EleuteriMangi-MAELEZO
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa         (OR-TAMISEMI) George Simbachawene amewaagiza wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha wanampatia taarifa ifikapo Aprili 3, 2016 ni lini mradi huo utaanza kutoa huduma.
Uamuzi huo wa Waziri Simbachawene unafuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kikao na wadau hao Machi 31, 2016 kilichofanyika ofisi za DART jijini Dar es salaam ili kuhakikisha wanatoa huduma ya usafiri wa uhakika kwa Watanzania na hasa wakazi wa jiji hilo.
“Kama mambo yote yataenda vizuri mradi huu utaanza mapema angalau mabasi 50 yaanze kutoa huduma mapema iwezekanavyo” alisema Simbachawene.
Simbachawene alisema kuwa hadi sasa mabasi mawili yamesha anza kufanya majaribio katika barabara za mradi huo na kuwahimiza wadau hao waongeze idadi ya mabasi yanayofanya majaribio angalau yafike 15 ili madereva wazoee barabara kabla ya mradi kuanza kutoa huduma rasmi.
Ili kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo, Simachawene amewataka wadau hao wa mradi wa mabasi yaendayo haraka wawe na utaratibu wa kukutana kila siku kwa kuzingatia kazi walizojipangia na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi na kumpatia taarifa kila baada ya siku mbili.
Aidha, Simbachawene amewaasa wa kazi wa jiji la Dar es salaam wawe watulivu kwa kuwa kazi kubwa ya mradi huo imekamilika na mradi umekaribia kuanza kuleta matunda na hivyo waitunze miundombinu hiyo ikiwemo barabara na vifaa vitakavyokuwa vinatumika wakati wa kutoa huduma.
“Kuhujumu miundombinu ya DART ni kulihujumu taifa letu, watu wote ni lazima wawe na uzalendo kwa mali yao ili mradi uwe wa tija kwa manufaa ya nchi yetu” alisema Simbachawene.
Simbachawene amesema kuwa utunzaji wa miundombinu hiyo utafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya wananchi, wadau wa mradi wa DART na Serikali.
Katika kikao hicho na wadau wa mradi wa DART, Waziri Simbachawene aliambatana na Naibu Waziri wake Selemani Jaffo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka yatakuwa yanafanya safari zake ya kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi kupitia eneo la Kimara, Ubungo, Morocco, Magomeni, Feri na Kariaakoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj amesema kuwa kutakuwa na jumla ya mabasi 140 ambayo yanatarajiwa kutoa huduma katika mradi wa DART jijini Dar es Salaam.
Kikao cha Waziri Simbachawene kilihuwahusisha wadau wa mradi huo ambao ni DART, TANROAD, Msajili wa Hazina, Kampuni ya Simon Group, SUMARTA, Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na Jeshi la Polisi.

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA BANGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATUMISHI WA WIZARA MKOANI KIGOMA



No comments :

Post a Comment