The
Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic
Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia
H.E. Naimi Hamza Aziz, during the opening session of the Committee of
Experts of the 9th Joint Annual Meetings of the African Union
Specialized Technical Committee on Finance, Monetary Affairs, Economic
Planning and Integration and the ECA Conference of African Ministers of
Finance, Planning and Economic Development, held in Addis Ababa,
Ethiopia from 31st March to 5th April 2016.
(picture courtesy of Tanzanian Embassy in Addis Ababa Ethiopia)
……………………………………………………………………………………………………..
The
work on implementing Africa’s Development Agenda 2063 has been directed
towards helping African countries overcome their continued
vulnerabilities and promote diversification in order to accelerate the
achievement of structural transformation.
The
Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic
Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia
H.E. Naimi Hamza Aziz, said this during the opening session of the
Committee of Experts of the 9th Joint Annual Meetings of the
African Union Specialized Technical Committee on Finance, Monetary
Affairs, Economic Planning and Integration and the ECA Conference of
African Ministers of Finance, Planning and Economic Development, held in
Addis Ababa, Ethiopia from 31st March to 5th April 2016. The Ministerial segment is to kick start its deliberations on the 3rd of April 2016.
The Conference under the theme: Towards an Integrated and Coherent Approach to Implementation, Monitoring and Evaluation of Agenda 2063 and the SDGs
at both experts and Ministerial level, will deliberate on pertinent
issues of how countries can harmonise frameworks and establish common
mechanisms of implementation, monitoring and evaluation to achieve
Africa’s collective goals of sustainable development and transformation.
Moreover,
the Conference will among other things, address the question of how
African countries can adopt and implement effectively the first Ten-Year
Implementation Plan of Agenda 2063, suggest ways for the integration of
the said plan at national, regional and continental levels and draw
lessons from the ongoing process of domesticating the First –Ten Year
implementation plan.
The
Conference will also discuss the harmonization of Agenda 2063 and 2030
Agenda and provide insight as to how an integrated and harmonized
approach for the execution of Agenda 2063 and the Sustainable
Development Goals can be designed at national level.
“As
you know the foundation for Agenda 2063 lies in the fact that, whilst
African countries have achieved remarkable growth performance, our
success has been limited in achieving structural transformation,” adding
that much remains to be done to achieve inclusive and equitable
development in Africa and that the continent’s economies were still
exposed to vulnerabilities and shocks that could adversely affect growth
prospects.
Ambassador
Naimi Aziz, who officiated the Conference in her capacity as the
outgoing Chair of the Bureau of the Committee of Experts said that, the
successful implementation of the continental Agenda 2063 will depend on
each member countries’ ability to strongly link their planning,
mobilizing and financing mechanisms.
As
she handed over the Chair to South Africa, Ambassador Naimi thanked the
joint Secretariat of the African Union Commission and the Economic
Commission for Africa for successful organization of the conference and
for the technical support which will be provided to the bureau during
the course of the meeting.
The
conference is attended by seasoned and high-level panelists from Africa
and other regions, representatives from Regional Economic Communities
(RECs) UN Agencies, Civil Society Organizations (CSOs), NEPAD, AfDB and
other organizations. It will be interactive so as to give Ministers the
opportunities to address the issues elaborated above, discuss and share
their views and experiences in the advancement of Africa’s development.
(From: Tanzania Embassy Addis Ababa, Ethiopia, 1st April 2016)
JESHI LA POLISI LAONGEZA MUDA WA KUHAKIKI SILAHA SASA ITAKUWA NI MIEZI MITATU KWA NCHI NZIMA
Kamishna
wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo mchana, kuhusu mchakato wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo
limeongeza muda wa miezi mitatu kwa nchi nzima kuanzia leo.
Msemaji wa Jeshi Nchini, Advera Bukumbi (kulia), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya kuzungumza na waandishi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.
Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.
Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na kuzisajili na kufanya malipo katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.
Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa
“Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi” alisema Mssanzya.
Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.
Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.
“Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa,” alisema.
………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.
Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.
Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na kuzisajili na kufanya malipo katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.
Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa
“Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi” alisema Mssanzya.
Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.
Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.
“Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa,” alisema.
WATENDAJI WATAKIWA KUHAKIKISHA USALAMA WA RASILIMALI ZA MISITU
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkururugenzi wa Idara ya Misitu
na nyuki kutoka Maliasili Bi. Gladness Mkamba mapema leo katika
kuadhimisha siku ya upandaji miti iliyofanyika ruvu kaskazini Mkoani
Pwani.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina akitoa maelekezo kwa Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii Injinia Angelina Madete( katikati) kuhusu upandaji miti katika
sehemu mbalimbali katika hifadhi ya misitu kibaha Mkoani Pwani,mapema
hii leo katika siku ya upandaji miti.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkururugenzi wa Idara ya Misitu
na nyuki kutoka Maliasili Bi. Gladness Mkamba mapema leo katika
kuadhimisha siku ya upandaji miti iliyofanyika ruvu kaskazini Mkoani
Pwani.
PICHA NA MPIGA PICHA WETU
…………………………………………………………………….
EVELYN MKOKOI KIBAHA-PWANI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, amewataka
watendaji katika ngazi za uteuzi nchini kushiriki kikamilifu katika
kuhahikisha usalama wa rasilimali za misitu.
Naibu Waziri Mpina ameyasema hayo
leo katika Pori la Ruvu Kaskazini ikiwa ni siku ya Kitaifa ya kupanda
miti na kueleza kuwa Serikali imekuwa na lengo la kupanda miti milioni
moja nukta tano (milioni 1.5) kwa mwaka mzima katika kila wilaya, na
kuwataka watendaji waliopo katika ngazi za uteuzi yaani Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu wakuu, kuhakikisha lengo hili
linafikiwa na kueleza kuwa viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi hili
majina yao yatapelekwa katika mamlaka za uteuzi na kuchukuliwa hatua,
hii ikiwa ni njia ya kupima usalama wa rasilimali hizi.
Akiongea na wananchi katika Pori
la Ruvu Kaskazini, Mh. Mpina alisema kuwa asilimia 61 ya ardhi ya nchi
ipo kwenye hatari ya kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa mazingira
utokanao na ukataji miti ovyo, na takwimu zinaonyesha kuwa takribani
hekta laki tatu nukta sabini na mbili za misitu zinakatwa kila mwaka kwa
matumizi mbali mbali. “mikoa nane nchini iko hatarini kuwa jangwa”.
Alisisitiza.
Akielezea athari, zitokanazo na
uharibifu wa misitu, Mh. Mpina alisema taifa linaweza kutumia mabilioni
ya fedha kwa ajili ya kununua chakula kuwalisha wa Tanzania kutokana na
ukosekanaji wa mvua ,vyanzo vya maji kukauka, upatakinaji wa umeme kuwa
wa kusuasua kutokana na uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji.
Kwa upande Mwingine Mh. Mpina
alisema kuwa serikali imekata miti kwa sababu mbalimbali za msingi ikiwa
ni pamoja ujenzi wa miundo mbinu kama vile barabara, reli ujenzi wa
bomba la gesi, hivyo basi kuna jukumu kubwa la kupanda miti mingi zaidi
ya hiyo iliyokatwa.
Akitolea Mfano wa taasisi za
huduma ya misitu Nchini (TFS) iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na
Utalii, Mh. Mpina aliainisha kuwa taasisi zote za serikali zisaidie
taifa kubainisha ni mazao gani ya misitu yanaweza kupandwa katika
maeneo gani kulingana na mahitaji ili kuweza kunusuru upotevu wa
rasimali ya misitu.
Serikali yawashukuru wadau wamichezo walioisaidia Twiga Stars
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James
Wambura akizungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa Wanawake (Twiga Stars)
alipokutana nao leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake (TWFA) Bi. Amina Karuma na Makamu
Mwenyekiti wa TWFA Bibi. Rose Kisiwa.
Baadhi
ya wachezaji wa Twiga Stars wakifuatilia mkutano baina yao na Naibu
Waiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James
Wambura (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake (TWFA) Bi. Amina Karuma akifafanua
jambo wakati wa mkutano baina ya Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) na wachezaji wa
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar
es Salaam. Kulia niMakamu Mwenyekiti wa TWFA Bibi. Rose Kisiwa.
Meneja
wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) Bibi. Furaha
Francis akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Naibu Waiziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (hayupo
pichani) na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake
(Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam.
Mchezaji
wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake (Twiga Stars) Bi.Fatuma
Omary akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Naibu Waiziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (hayupo
pichani) na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Wanawake
(Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHUSM.
LUHWAVI AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA NJOMBEA NA RUVUMA LEO
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi akiwasili ukumbini na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe, Deo Sanga maarufu kwa jina la ‘Jah
Peole’ kuzungumza na viongozi na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka
mkoa huo na mkoa wa Rumuma leo mkoani Njombe
Baadhi ya viongozi wa CCM kutoka mkoa wa Ruvuma, wakiwa kwenye kikao
hicho cha viongozi, watumishi wa CCM na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu
Luhwavi kilichofanyika leo mkoani Njombe. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa
wa Ruvuma Verena Shumbusho.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Katibu wa CCM mkoa wa Njombe, Osea Mbagike akifanya utambulisho wa
waalikwa kwenye kikao cha viongozi, watumishi wa Chama Cha Mapinduzi
mkoani Njombe na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi
(katikati) kilichofanyika leo mjini Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM
mkoa huo, Deo Sanga.
JOKATE NA MO DEWJI FOUNDATION KUJENGA KIWANJA CHA MICHEZO SEKONDARI YA JANGWANI
Mwanzilishi wa ujenzi huo, Jokate Mwegelo akiandika jambo wakati ujenzi wa kiwanja ukiendelea.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa
kupata uwanja wa michezo ambao unajegwa kwa ushirikiano wa Mwanamitindo
Jokate Mwegelo na Taasisi ya Mo Dewji.
Akizungumza na Mo Blog,
Jokate amesema ujenzi wa kiwanja hicho cha michezo ni sehemu ya mipango
aliyokuwa nayo baada ya kuanzisha mwaka jana bonanza la Kidoti ambalo
lilikuwa na malengo ya kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri kimasomo na
kushiriki katika michezo ili kukuza vipaji vyao.
Jokate
amesema ameamua kuanza na shule ya Jangwani kwa kutambua kuwa shule
hiyo ina hosteli za wanafunzi walemavu na wamekuwa wakipata shida kupata
viwanja vya michezo hivyo kupitia kiwanja hicho wataweza kushiriki
michezo kwa urahisi zaidi.
“Pale
Shule ya Jangwani kuna wanafunzi walio na ulemavu na kama unavyojua
mlemavu anatakiwa kufanya mazoezi ili kuweka afya yake vizuri na kama
wakitaka kushiriki michezo hadi waende Gymkhana lakini tunawajengea
uwanja wa Basketball na Netball,” amesema Jokate wakati akifanya
mahojiano na Mo Blog.
Ameongeza
kuwa ili kufanikisha ujenzi huo alizungumza na Mohammed Dewji ambaye
alikubali kutoa Milioni 10 kupitia Taasisi yake ya Mo Dewji na hivyo
kuanza kufanyika kwa ujenzi huo ambao utawawezesha wanafunzi wa Jangwani
kushiriki michezo tofauti na hapo awali.
Aidha
amesema kuwa ujenzi wa viwanja vya michezo utakuwa endelevu katika
shule za serikali ambazo bado hazijawa na viwanja na baada ya kukamilika
kwa ujenzi katika shule ya Jangwani amepanga kufanya ujenzi wa viwanja
vya michezo katika Shule ya Sekondari Kinyerezi na Shule ya Sekondari
Maposeni iliyopo wilayani Peramiho, Ruvuma.
Ujenzi wa kiwanja cha michezo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani ukiendelea
LUHWAVI: WATUMISHI WA CHAMA CHACHU YA CCM KUNG’ARA KATIKA JAMII
Na Bashir Nkoromo, Njombe
………………………………………………
Watumishi
wa Chama ni sehemu muhimu inayokifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuendelea kuwa bora na imara kwa kuwa ndiyo jiko la kubuni na kuandaa
taswira ya muonekano wa Chama katika jamii.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajabu Luhwavi wakati
akizungumza na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka wilaya za mkoa wa
Njombe na Ruvuma, jana, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo
kuzungumza na kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili watumishi wa
Chama.
Alisema,
ni kutokana na kutambua umuhimu wa watumishi hao ndiyo sababu Chama Cha
Mapinduzi kinafanya kila jitihada kuhakikisha kinakutana nao ili kujua
mazigira walioyomo na changamoto na kero zinazowakabili ili kuweza
kutafuta njia za kuzitatua kwa kadri inavyowezekana.
“Unajua
mimi ndiyo nasimamia utumishi katika chama, kazi zingine zote
zinazonihusu naweza kuzifanya kupitia mafaili nikiwa ofisini, lakini
hili la kuhusu mazingira na hali za watumishi ambalo pia linanihusu
siweze kulifanya nikiwa ofisini, ndiyo sababu nimeamua kufanya ziara
hizi, ili niwasilikilize kero na changamoto zinazowakabili tukiwa
pamoja”, alisema Luhwavi.
Wakuu wa Mikoa Waagizwa kutumia Mfumo wa Kieletroniki kukusanya Mapato
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George
Simbachawene akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa
Mikoa katika kikao cha kujadili mwelekeo wa bajeti za Mikoa na
Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kilichofanyika katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi
ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawalawa Mikoa kutoka Tanzania Bara
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George
Simbachawene (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mwelekeo wa
bajeti za Mikoa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017
kilichofanyika katika ukumbiwaKarimjeejijini Dar es Salaam hivikaribuni.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George
Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Felix Ntibenda (kulia) hivi karibuni katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George
Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Fatma Dendego (kulia) hivi karibuni katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kushoto ni Naibu
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George
Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Rehema Nchimbi (kulia) hivi karibuni katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA JENGO JIPYA LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais- Muungano Mazingira Mh. January Makamba
akiongea na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria
walipotembelea kukagua mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya
Makamu wa Rais. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mohamed Omary.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Rais Mbarak Abdulwakil akisoma taarifa ya mradi
wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais mbele ya Wajumbe wa
Kmati ya bunge ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) walipotembelea
Ofisini hapo kukagua mradi huo.
Sehemu
ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na sheria wakisikiliza kwa makini taarifa
ya mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais iliyokua
ikisomwa na Katibu Mkuu (hayupo pichani)
PICHA NA MPIGA PICHA WETU
KAMATI YA NIDHAMU TFF KUKUTANA KESHO
Kikao
cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kitaendelea kesho Jumamosi saa 3 asubuhi katika ofisi za TFF zilizopo
Karume, na maamuzi yake yatatangazwa saa 7 mchana.
Kamati inakutana kwa ajili ya
kumalizia shauri la upangaji wa matokeo Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes
League) kundi C inayozihusisha timu za Geita Gold, JKT Kanembwa, JKT
Oljoro na Polisi Tabora.
Viongozi watakaohojiwa na Kamati
ya Nidhamu ni, Yusuf Kitumbo (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
mkoa wa Tabora), Fateh Remtullah (Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu
mkoa wa Tabaora), viongozi wa benchi la ufundi Polisi Tabora, Mrisho
Selemani, Boniface Komba, Bernard Rabiamu.
Kamati pia itawahoji Mwenyekiti wa
Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita, Salum Kurunge na mwenyekiti wa
Klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita.
KUZIONA SERENGETI BOYS V THE PHARAOHS 2,000/= TU
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi
elfu mbili tu (2,000) ndio kitakachotumika katika mchezo wa kesho
Jumamosi kati ya Serengeti Boys (Tanzania) v The Pharaohs (Misri) katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
TFF imeweka kiingilio cha shilingi
elfu mbili tu (2000) uwanja mzima, kutoa nafasi kwa wapenzi wa mpira wa
miguu nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuja kushuhudia
mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za vijana za Tanzania v
Misri.
Serengeti Boys inashuka dimbani
kucheza na The Pharaohs mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima
nguvu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi na kujiandaa na mchezo wa kuwania
kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya
miaka 17 dhidi ya Shelisheli Juni – Julai mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa
kimataifa utachezeshwa na waamuzi wa kimataifa wenye beji za FIFA ambao
ni Israel Mjuni, akisaidiwa na Soud Lila, Frank Komba, mwamuzi wa akiba
Jonesia Rukyaa, huku kamisaa wa mchezo akiwa Isabella Kapera.
Upande wa kikosi cha timu ya Taifa
ya Misri kimewasili nchini jana mchana saa 7:30 mchana kwa shirika la
ndege la Ethiopia, kikiwa na msafara wa watu 33 wakiwemo wachezaji 25 na
viongozi 8.
The Pharaohs wanatarajiwa kufanya
mazoezi leo jioni saa 10 kamili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaa, baada ya kuwa wamefanya mazoezi jana jioni katika uwanja wa
Karume.
Wakiongea
na waandhishi wa habari, makocha wa timu zote mbili, Bakari Shime
(Serengeti Boys) na Yasser Muhamadain (The Pharaous) wameshukuru kwa
kupata mchezo huo wa kirafiki wa kiamataifa.
Kocha Shime ameishukuru TFF kwa
kufanikisha mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa, baadaya kuwa kambini na
kucheza michezo ya kirafiki na timu za ndani, wao kama benchi la ufundi
watautumia kama kipimo sahihi cha mchezo wa kimataifa katika maandalizi
ya mchezo wao dhidi ya Shelisheli.
Naye Yasser wa The Pharaohs,
ameshukuru kwa kupata nafasi ya kucheza na Tanzania mchezo wa kirafiki,
kwao ni mara ya kwanza kucheza mchezo wa kirafiki nje ya ukanda wa
Afrika Kaskazini, hivyo anaamini kesho kutakua na mchezo mzuri wenye
ushindani.
Waziri Simbachawene afanya kikao na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi
wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) akiongea na wadau wa mradi wa
mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu
Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) Selemani Jaffo.
Kaimu
Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald
Lwekatare akitoa taarifa ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi
Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Waziri
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
Selemani Jaffo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene (wa pili kulia) akiongea na wadau wa
mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi
Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Msajili
Masaidizi wa Hazina Jones Mwalemba akitoa ufafanuzi namna ofisi yake
inavyochangia katika kukamilisha mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati
wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau
wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi
Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj akifafanua jambo wakati wa mkutano wa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi
wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) mkutano wa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi
wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………..
Na EleuteriMangi-MAELEZO
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene
amewaagiza wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha wanampatia taarifa
ifikapo Aprili 3, 2016 ni lini mradi huo utaanza kutoa huduma.
Uamuzi huo wa Waziri Simbachawene
unafuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kikao na wadau hao Machi
31, 2016 kilichofanyika ofisi za DART jijini Dar es salaam ili
kuhakikisha wanatoa huduma ya usafiri wa uhakika kwa Watanzania na hasa
wakazi wa jiji hilo.
“Kama mambo yote yataenda vizuri
mradi huu utaanza mapema angalau mabasi 50 yaanze kutoa huduma mapema
iwezekanavyo” alisema Simbachawene.
Simbachawene alisema kuwa hadi
sasa mabasi mawili yamesha anza kufanya majaribio katika barabara za
mradi huo na kuwahimiza wadau hao waongeze idadi ya mabasi yanayofanya
majaribio angalau yafike 15 ili madereva wazoee barabara kabla ya mradi
kuanza kutoa huduma rasmi.
Ili kuongeza kasi ya kukamilisha
mradi huo, Simachawene amewataka wadau hao wa mradi wa mabasi yaendayo
haraka wawe na utaratibu wa kukutana kila siku kwa kuzingatia kazi
walizojipangia na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi na kumpatia
taarifa kila baada ya siku mbili.
Aidha, Simbachawene amewaasa wa
kazi wa jiji la Dar es salaam wawe watulivu kwa kuwa kazi kubwa ya mradi
huo imekamilika na mradi umekaribia kuanza kuleta matunda na hivyo
waitunze miundombinu hiyo ikiwemo barabara na vifaa vitakavyokuwa
vinatumika wakati wa kutoa huduma.
“Kuhujumu miundombinu ya DART ni
kulihujumu taifa letu, watu wote ni lazima wawe na uzalendo kwa mali yao
ili mradi uwe wa tija kwa manufaa ya nchi yetu” alisema Simbachawene.
Simbachawene amesema kuwa utunzaji
wa miundombinu hiyo utafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mzuri
kati ya wananchi, wadau wa mradi wa DART na Serikali.
Katika kikao hicho na wadau wa
mradi wa DART, Waziri Simbachawene aliambatana na Naibu Waziri wake
Selemani Jaffo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo
haraka yatakuwa yanafanya safari zake ya kutoa huduma ya usafiri kwa
wananchi kupitia eneo la Kimara, Ubungo, Morocco, Magomeni, Feri na
Kariaakoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj amesema kuwa kutakuwa na jumla ya mabasi 140
ambayo yanatarajiwa kutoa huduma katika mradi wa DART jijini Dar es
Salaam.
Kikao cha Waziri Simbachawene
kilihuwahusisha wadau wa mradi huo ambao ni DART, TANROAD, Msajili wa
Hazina, Kampuni ya Simon Group, SUMARTA, Wakala ya Serikali Mtandao
(eGA) na Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment