Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki Rais wa Uganda Mhe.
Yoweri Kaguta Museveni wakati alipowasili jijini Arusha leo tayari kwa
kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Augustine Mahiga.(PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri
Kaguta Museveni wakiongea na wanahabari mara baada ya kukutana na
kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi
1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo
kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri
Kaguta Museveni wakiwa katika mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha
jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda
kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
PICHA NA IKULU
MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI TMA, YAWAPIGA MSASA WANAHABARI KUHUSU EL-NINO NA ATHARI ZAKE.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana
Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua Warsha ya Siku mbili kwa
Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini,
iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
…………………………………………………………………………………
Na:George Binagi-GB Pazzo
Katika
Warsha hiyo, Taasisi mbalimbali pamoja na Wanajamii, zimehimizwa
kutumia taarifa za Utabiri wa Hali ya Hewa kwa ajili ya Mipango ya
Maendeleo.
Pia
Wanahabari ambao ni kiunganishi Muhimu katika upashanaji wa habari,
wametakiwa kutumia nafasi yao katika kutoa taarifa hizo kwa wananchi
ikizingatiwa kwamba, taarifa za utabiri wa hali ya hewa zikiwafikia
walengwa kwa wakati, husaidia kujikinga na maafa yatokanayo na
mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Mafuriko na ukame.
Warsha
hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kwa
ushirikiano wa karibu na Mamlaka ya Hali ya Hewa Duniani (WMO) ikiwa ni
katika mpango wake wa Kidunia katika kuboresha upatikanaji wa taarifa za
hali ya hewa ujulikanao kama Global Framework For Climate Services
(GFCS).
Katibu
Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa
nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Ziwa, Augustino Nduganda akitoa neno la Shukrani baada ya Ufunguzi wa Semna kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini.
Wengine
kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Hali ya Hewa
nchini, Hamza Kabelwa, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Marcella Mayalla, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza
Alphonce Tonny kutoka Metro Fm Mwanza (Kushoto) akiwa pamoja na Iman Hezron Kutoka City Fm Mwanza.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza
LUKUVI ATEMBELEA ENEO LA UBOMOAJI WA JENGO LA GHOROFA 16
Waziri wa Ardhi, Mhe. William
Lukuvi akiangalia maendeleo ya kazi ya ubomoaji wa jengo la ghorofa
kumi na sita (16) ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ambapo kwa
sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.
Mafundi wakiendelea na Ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.
Bank Of Africa Yawajengea Uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar Kutengeneza Mpango wa Kujenga na Kuboresha Biashara Zao.
Mkufunzi
wa Warsha ya ilioandaliwa na Bank of Africa Erick Chrispin akitowa Mada
wakati wa Warsha hiyo iliowajumuisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali
Zanzibar katika Kuboresha na Kujenga Biashara katika kutengeneza Mpango
wa Biashara iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort
Mazizini Zanzibar.
Washirikib wa Warsha hiyo wakifuatilia kwa makini Mada zinazowesilishwa wakati wa Warshi hiyo ilioandaliwa na Bank Of Africa.
Mtoa
Mada Ndg Erick Chirispin akisisitiza jambo wakati wa kutoa Mada katika
Warsha hiyo. Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar katika Kujenga
na Kuboresha Biashara katika kutengeneza Mpango wa Biashara.
Washiriki wakiwa Ukumbi wa Mkutano wakifuatilia Mada .
Washiriki wakichanjia wakati wa warsha hiyo.
Mshiriki
wa Warsha ya kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Biashara na
Kujenga na Kuboresha Biashara akichangia wakati wa warsha hiyo.
Mtoa
Mada Ndg. Erick Chrispin akionesha kitabu chenye mpango wa Biashara
wakati wa warsha hiyo kwa Wafanyabiashara wa Zanzibar na Wadau
ilioandaliwa na Bank Of Africa katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach
Resort Mazizini Zanzibar.
Washiriki
wa Warsha ya Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara Zanzibar katika kuandaa
Mpango wa Biashara wakiwa nje ya ukumbi wakibadilishana mawazo wakati wa
mapunziko ya mchana.
Imeandaliwa na OthmanMapara.Blogspot.com Zanzinews.com,
ZIMBABWE KUWASILI KESHO
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake ya Zimbabwe,
inatarajiwa kuwasili kesho Alhamis mchana wakiwa na msafara wa watu 29,
wakiwemo wachezaji 20 pamoja na viongozi 9 tayari kwa ajili ya mchezo wa
siku ya Ijumaa dhidi ya wenyeji Twiga Stars uwanja wa Azam Complex
Chamazi.
Zimbabwe watafikia hoteli ya DeMag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.
Upande wa waamuzi wa mchezo huo wanatrajiwa kuwasili kesho mchana kwa shirikia la ndege la Kenya (KQ) wakitokea nchini Ethiopia, huku kamisaa wa mchezo kutoka Congo DR akiwasili jioni kwa KQ.
Maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika ambapo ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, tiketi za mchezo huo zitauzwa eneo la uwanja Chamazi siku ya Ijumaa. Viingilio vya mchezo ni shilingi elfu mbili (2,000) kwa mzunguko na shilingi elfu tatu (3,000) kwa jukwaa kuu.
TFF inawaomba wadau, wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.
Zimbabwe watafikia hoteli ya DeMag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.
Upande wa waamuzi wa mchezo huo wanatrajiwa kuwasili kesho mchana kwa shirikia la ndege la Kenya (KQ) wakitokea nchini Ethiopia, huku kamisaa wa mchezo kutoka Congo DR akiwasili jioni kwa KQ.
Maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika ambapo ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, tiketi za mchezo huo zitauzwa eneo la uwanja Chamazi siku ya Ijumaa. Viingilio vya mchezo ni shilingi elfu mbili (2,000) kwa mzunguko na shilingi elfu tatu (3,000) kwa jukwaa kuu.
TFF inawaomba wadau, wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.
MALINZI AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI INFATINO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni
Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.
Katika barua hiyo, Malinzi
amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa
niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea
kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia
kila la kheri na mafanikiko mema.
MAJALIWA AWASILI WILAYANI BUSEGA KWA ZIAR
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiteta na Mkuu wa Mkoa a Simiyu, Erasto Mbwiro baada ya kuwasili
wilayani Busega kuanza ziaraya mkoa huo, Machi 2, 2016. (picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni baada ya kuwasili
wilayani Busega akiwa aktika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 2, 2016.
Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Erasto, Mbwiro. (picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya
Busega akiwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 2, 2016.(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
viongozi wengine wakipiga makofi mara baada ya Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Halmashauri ya
Wilaya ya Busega akiwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 2,
2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwapungia wananchi wa Nyashimo wilayani Busega kabla ya kukagua ujenzi
wa wodi ya wazazi kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu,
Machi, 2, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Mzindakaya. (picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa wodi ya Wazazi katika kijiji
cha Nyashimo wilaya ya Busega akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu
Machi 2, 2016. Kushoto ni Mbunge wa Busega, Dkt, Raphael Chegeni na
Kulia nI Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAREKANI YAIKABIDHI SERIKALI YA TANZANIA MBWA MAALUMU WA KUBAINI DAWA ZA KULEVYA NA PEMBE ZA NDOVU
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akizungumza katika shughuli
ambapo Marekani iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa
kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika
Bandari ya Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kulia ni Kaimu Balozi wa
Marekani nchini, Virginia Blaser. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini,
Virginia Blaser akizungumza katika shughuli ambapo nchi yake iliikabidhi
Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na
Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo.
Kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe,wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Injinia Hamad Masauni, anayefuata ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akimuaga Kaimu Balozi wa
Marekani nchini, Virginia Blaser mara baada ya Marekani kuikabidhi
Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na
Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo.
Kushoto ni Ofisa Usalama Kanda, Ubalozi wa Marekani nchini, Bruce
Paluch. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akiwafafanulia jambo waandishi
wa habari mara baada ya Serikali ya Marekani kuikabidhi Tanzania Mbwa wa
Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio
lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (D/IGP), Abdulharam Kaniki. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akisindikizwa na Kaimu
Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser (kushoto) pamoja na Maafisa
wengine wa ubalozi huo, mara baada ya kumaliza shughuli ya Marekani ya
kuikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya
Kulevya na Pembe za Ndovu katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es
Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
UMILIKI WA ARDHI KWA WANAWAKE WAONGEZEKA – ELUKA KIBONA
Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Eluka Kibona amesema uelewa wa wanawake katika kumiliki
ardhi na kufuatilia haki zao za ardhi unaongezeka siku hadi siku nchini
na kuondoa ile dhana kwamba wanawake wako nyuma katika shughuli za
maendeleo.
Bi
Eluka ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Blogs za Mikoa kuhusu
namna taasisi binafsi zinavyotetea harakati za wanawake katika kumiliki
ardhi hapa nchini na kujiendeleza kiuchumi ambapo amesema kwa
kulinganisha miaka 10 iliyopita na sasa, wanawake kwa sasa wamekuwa na
muamko zaidi wa kupambana na changamoto za umiliki wa ardhi wanazokutana
nazo.
”Sisi tunaunga
mkono harakati na jitihada za kuleta usawa kati ya wanaume na wanawake
mjini na vijijini na hii ni baada ya kutambua kuwa matatizo ya umiliki
wa ardhi kwa wanawake wa mjini na vijijini yako sawa kutokana na
mfumo ulivyo katika jamii.”Ameeleza Bi Eluka.
mfumo ulivyo katika jamii.”Ameeleza Bi Eluka.
Mmoja wa wanawake (Kulia) akipokea hati yake ya kumiliki ardhi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster katika kijiji cha Gongoni wilayani Kilosa.
”Kuna
madai ya ardhi ambayo wanawake wanakumbana nayo katika jamii kwa
kudhulumiwa na wengine kwa kunyimwa haki zao za msingi hivyo
tunawasaidia katika kuwawezesha kutambua namna ya kupigania haki
zao.”Amesisitiza Bi Eluka.
Kuhusu siku ya wanawake duniani ambayo huazimishwa kila Machi 8 kila mwaka,
Bi Eluka amesema Oxfam Tanzania imejipanga kufanya maadhimisho katika
mkoa wa Mtwara ili kuunga mkono jitihada za wanawake katika kujikwamua
na mifumo kandamizi hapa nchini na kujiendeleza kiuchumi.
Mmoja wa wanawake akiwa katika kilimo
Kwa mujibu wa Bi Eluka, Oxfam imewezesha wanawake wengi kuweza kupata haki zao katika mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya mikoa hiyo ni Shinyanga, Arusha, Tanga Morogoro/
Kwa mujibu wa Bi Eluka, Oxfam imewezesha wanawake wengi kuweza kupata haki zao katika mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya mikoa hiyo ni Shinyanga, Arusha, Tanga Morogoro/
Aidha kwa mujibu wa sheria ya ardhi inatamka bayana kuwa mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi. (Kifungu 3(2) cha sheria ya ardhi na sheria ya ardhi ya vijiji za 1999).
Hata hivyo
ni muhimu kila mmiliki wa ardhi awe na hati/ cheti halisi
cha hakimiliki kuthibithisha haki yake ya kumiliki ardhi kisheria.
MAELEZO YA MHE. UMMY ALLY MWALIMU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WAKATI AKIPOKEA MSAADA WA FEDHA KWA AJILI YA KUWEZESHA MATIBABU YA WAGONJWA WA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE
Awali ya yote nichukue fursa hii
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujali afya njema na hatimaye
ametuwezesha tukusanyike mahali hapa. Vile vile, nitumie fursa hii
kuwashukuru watumishi wote wa Afya kwa kazi nzuri wanayoifanya ya utoaji
wa huduma za afya kwa watanzania wote. Pia, nitumie nafasi hii
kuwapongeza ndugu zetu wa Jumuiya ya Kihindu ya hapa Dar es Salaam
ijulikanayo kama BAPS, kwa kuguswa kwao na kutoa msaada mkubwa na upendo
waliouonyesha kwa watanzania hawa wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.
Nimeafiriwa kuwa kiasi cha msaada
unaotolewa utawezesha wagonjwa wapato 100 kupatiwa matibabu ya moyo.
Hii ni faraja kubwa kwa wagonjwa wetu waliokuwa wakisubiri huduma hizi
kwa muda mrefu.
Takwimu zinaonyesha kuwa, kuna
ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo,
kisukari, n.k. Wizara yangu imejipanga kuhakikisha kuwa inaweka mkazo
katika kutoa elimu ya kujikinga na maradhi mbalimbali ili kuokoa maisha
ya watanzania walio wengi. Ni dhahiri kuwa gharama za matibabu zimekuwa
zikiongezeka siku hadi siku. Hivyo, nitoe rai kwa watanzania wote,
tujaribu kuzingatia Kanuni za Afya kama kufanya mazoezi, kula vyakula
kwa kuzingatia mahitaji ya miili yetu, na kupima afya zetu mara kwa
mara.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) imekuwa ikiendesha huduma hizi za kambi, kila inapoona kuna
ongezeko la wagonjwa wanaohitaji tiba za aina hii. Kitendo hiki ni
kizuri kwa kuwa kinawezesha wananchi/wagonjwa kupata huduma hii kwa
haraka zaidi. Ni matarajio yangu kuwa kambi itakayoanza tarehe 7/3/2016,
itanufaisha wagonjwa wengi zaidi ikiwezekana nusu ya wagonjwa hao
wanaosubiri huduma hii.
Mmetaarifiwa kuwa wagonjwa
waliopo sasa wanatoka karibu kila pembe ya nchi yetu, mathalani katika
wagonjwa watakaofanyiwa matibabu, wagonjwa 10 wanatoka Zanzibar na
waliobaki wanatoka Tanzania Bara.
Lengo la Serikali ni kuboresha
huduma za Tiba za Rufaa nchini ili kupunguza idadi ya rufaa za wagonjwa
nje ya nchi. Mfano: kati ya mwaka 2000 hadi 2014 jumla ya wagonjwa 7,363
walipewa rufaa kwenda kutibiwa nje ya nchi sawa na wastani wa wagonjwa
526 kwa mwaka ambapo kati yao wagonjwa 4,413 sawa na wastani wa wagonjwa
315 kwa mwaka waliweza kwenda nje ya nchi kwa matibabu. Aidha, kati ya
mwaka 2012 na 2015 wagonjwa 1465 walitibwa nje ya nchi kwa gharama za
Serikali. Karibu asilimia 50 ya wagonjwa waliotibiwa nje ya nchi kwa
gharama za Serikali kati ya mwaka 2012 hadi Novemba, 2015 walikuwa
wanaugua magonjwa ya moyo. Kutokana na ukubwa wa tatizo la magonjwa ya
moyo Serikali mwaka 2008 iliamua kuanzisha huduma za upasuaji mkubwa wa
moyo na hatimaye kujenga Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac
Institute (JKCI), ambayo ilianza Aprili, 2015. Tangu kuanza kwa Taasisi
hii, kambi maalumu za upasuaji moyo zimekuwa zikiendeshwa na wataalamu
wa hapa nchini kwa kushirikiana na wa kutoka nje ya nchi ambapo jumla ya
wagonjwa 247 wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Kambi za upasuaji zimesaidia
kupunguza idadi ya wagonjwa ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa
matibabu. Aidha, hatua hii imepunguza gharama kwa Serikali kwa sababu
idadi ya wagonjwa wa moyo waliopata rufaa imepungua toka 198 hadi 89
kati ya mwaka 2013 na Novemba 2015.
Matibabu nje ya nchi yana gharama
kubwa ambazo zinatofautiana kulingana na ugonjwa husika. Gharama za
kumtibu mgonjwa mmoja wa moyo ni Shs.16,500,000.00 mgonjwa mmoja wa figo
ni Shs.57,750,000.00 na mgonjwa mmoja wa saratani ni Shs.74,250,000.00.
Matumizi ya fedha kwa ajili ya matibabu nje ya nchi yamekuwa
yakiongezeka kulingana na kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa. Kuongezeka
idadi ya wagonjwa wa rufaa kumesababisha Serikali kuwa na limbikizo la
deni lililofikia Shs.28,743,586,356/= hadi kufikia mwezi Desemba, 2015.
Kabla sijamaliza maelezo yangu,
nitoe shukurani za dhati kwa Madaktari na Wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI). Kipekee kabisa niwashukuru Jumuiya ya Kihindu ya
BAPS kwa msaada mkubwa walioutoa katika kuhakikisha wanaokoa maisha ya
watanzania hao, niendelee kuwaomba pale mtakapoguswa zaidi, saidieni
katika maeneo mengine pia kama ununuzi wa vifaa tiba na ikiwezekana basi
msaidie ili wagonjwa waliobaki wapate tiba wote hapa nchini. Huu ni
uzalendo wa hali ya juu na tunashukuru kwa kumuunga mkono Mhe. John
Pombe Magufuli Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma zote za msingi kadri
inavyowezekana siku zote tunasema “kutoa ni moyo usambe si utajiri”.
TANZANIA YAIOMBA KOICA KUONGEZA MUDA WA MKATABA WA MRADI WA GEBR
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati)
akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdula Lutavi (aliyeipa
mgongo kamera) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo
pichani) kwa ajili ya kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi
endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini,
kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara
linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Mkoani Tanga. Kulia
ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika,
Firmin Matoko. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Kongamano
la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira
kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu
Kusini mwa Jangwa la Sahara (GEBR) limefanyika mkoani Tanga.
Wenyeji
wa kongamano hilo walikuwa ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
sayansi na Utamaduni (UNESCO) ofisi ya Dar es salaam.
Akifungua
kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Korea kusini kupitia
shirika lake la maendeleo na ushirikiano la kimataifa (KOICA) kuongeza
muda wa mkataba wa mradi wa GEBR ambao unafikia ukomo mwishoni mwa mwaka
huu.
Akizungumza
na washiriki mbalimbali wapatao 40 kutokana ndani na nje ya nchi
zikiwemo Ghana na Nigeria kutoka Afrika, alisema ombi hilo linatokana na
ukweli kuwa walengwa wamekuwa wakifaidika na mradi huo, kwa kuweza
kubadilisha maisha yao na kuwa bora zaidi.
Makamu
wa Rais alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na
kutoweka kwa uotoasili unaotoa fursa ya uoto wa mimea zaidi ya 10,000,
jamii 6,000 ya wadudu, jamii ipatayo 1000 ya ndege warukao.
Aidha
Samia katika hotuba yake alirejea msimamo wa serikali wa kutaka
kuhifadhi mazingira, pamoja na kuziweka rasmi chini ya uangalizi halali
jumla ya hekta milioni 33.5 za misitu asili, huku akitanabaisha kuwa
serikali pia ina mapori ya akiba yapatayo 800 pamoja na misitu mingine.
Aliwakumbusha
washikadau pamoja na nchi wafadhili kwamba Tanzania inakabiliwa na
ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wake wanaotegemea raslimali kwa matumizi
yao ya kila siku pamoja na mahitaji ya nishati.
“Tunaelewa
kwamba kuna shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zinazopelekea
uharibifu wa misitu na mazingira”, alisema Samia na kuongeza kwamba kuna
kupokonyana kwa ardhi na maji.
Katika
warsha hiyo wafaidika wakubwa katika mradi huo, ambao walitekeleza kwa
vitendo elimu iliyopatikana kutokana na mradi huo, walikabidhiwa vyeti
ya ushiriki kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa walioonyesha.
Washiriki
hao wengi walitoka katika miradi midogo midogo inayotekelezwa Amani,
Muheza ambayo ni pamoja na ufugaji nyuki, samaki, vipepeo na uyoga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) alipowasili kwenye hoteli ya Tanga
Beach Resort jana kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi
endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini,
kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara
lililoandaliwa na UNESCO. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza aliwataka wakazi wa Tanga na
Tanzania kwa ujumla kutumia vyema nafasi adhimu kwenye miradi ya
maendeleo inayogharimiwa na wafadhili na kuwasihi wawe makini kwani
mafanikio yao huwa ni kivutio kwa wafadhili kuweza kuendelea kutoa
ufadhili kwa misaada.
Mradi
wa GEBR ambao uko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wake,
unafadhiliwa na serikali ya Korea kupitia Shirika lake la Kimataifa la
misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA).
Mradi huo wa Unesco wa binadamu na bayosfia (MAB) unatekelezwa nchini Ghana, Nigeria na Tanzania kwenye milima ya Usambara.
Katika
hotuba yake Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Firmin
Matoko alimpongeza Makamu wa rais kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika
nafasi ya juu katika utawala tangu historia ya kuundwa kwa Tanzania.
Alisema amefurahishwa sana na wanawake kuchukua nafasi kwa kuwa Unesco wameweka kipaumbele wanawake katika maendeleo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano hoteli ya Tanga Beach Resort akiwa
ameambatana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko.
Akizungumzia mradi wa GEBR alisema umelenga kutekelezwa katia msingi wa wazo la UNESCO la binadamu na bayosfia.
Alisema
kwamba mradi huo umelenga kutumia elimu ya asili, elimu ya sayansi na
utamaduni ili kuboresha maisha ya biandamu huku wakihifadhi mazingira.
Aidha
alitaka kuwapo ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo na
hifadhi ya bayosfia kwa lengo la kuwezesha maendeleo endelevu.
Washiriki wa mradi huo pia walipata nafasi ya kutembelea eneo la hifadhi ya Usambara mashariki.
Naye
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Bw Geum-Young Song alisema kwamba
wataendelea kushiriki katika mradi huo ambao umejikita katika kuwezesha
maendeleo endelevu huku mazingira yakihifadhiwa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua
Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuai katika
hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo
endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa
Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani
Tanga.
Alisema ni lengo la taifa lake la kuwezesha hifadhi endelevu kwa maendeleo endelevu.
Aidha alitaka kuwepo na fikra za mradi kuwa endelevu baada ya wafadhili kuondoka.
Viongozi
waliohudhuria siku ya ufunguzi ni pamoja na Makamu wa Rais Tanzania,
Mh. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya
Afrika, Bw. Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania,
Mh. Geum -Young Song, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Unesco nchini
Tanzania, Zulmira Rodrigues, Wawakilishi wa KOICA nchini Ghana, Nigeria
na Tanzania; mwakilishi wa KOICA nchini Korea, Seoul; na kamati za MAB
kutoka nchi zinazotekeleza mradi huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akifungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuwai
katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na
maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo
limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach
Resort Mkoani Tanga.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Afrika, Firmin Matoko kuhutubia kwenye kongamano
hilo.
Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UNESCO, Irina Bokova wakati
wa ufunguzi wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu
unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda
bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea
katika hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Balozi
wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song ambao ni wafadhili wa
mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui akisoma taarifa yake
baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufungua Kongamano hilo la pili la Kimataifa
inayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na
uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la
Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa
Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Pichani
juu na chini washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi
endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini,
kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara
linaloendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani
Tanga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Uyoga (DMGA), Bi
Judith Simon Muro, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye
kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira asili Amani (Amani
Forest Nature Reserve – ANR), Bi. Mwanaidi Kijazi, kwa kutambua
mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa
kulinda Bayoanui. Wanaoshuhudia tukio hilo kulia Mkurugenzi Mkuu
Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri
ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song (wa pili kushoto) pamoja na
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda
na Burundi, Bi. Mary Kawar (wa kwanza kushoto).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti Amiri Saidi Sheghembe wa mradi wa Vipepeo Amani kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ,
akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania,
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki kutoka nje ya Tanzania
wanaohudhuria Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu
unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda
bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea
katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la pili
la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia
ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini
mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UNESCO
walioshiriki kwenye maandalizi ya kongamano hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akiteta jambo na Afisa Tathimini na Logistki wa UNESCO Ofisi ya Dar es
Salaam, Rahma Islem (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko (kushoto)
akisalimiana na mmoja wadau wa maendeleo Balozi wa Jamhuri ya Korea
nchini, Mh. Geum-Young Song .
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi
katika picha ya kumbukumbu na Mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye pia
ni Katibu Klabu ya Safe Space inayojihusisha na utunzaji wa Mazingira,
Lilian Tadei wa Shule ya Sekondari Potwe, Muheza.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati)
akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi (kushoto) na Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
WAZAZI WALALAMIKA KUFUNGWA KWA MATAWI YA CHUO KIKUU CHA ST, JOSEPH
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
BAADHI
ya wazazi wa wanafaunziwaliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph
katika matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo
vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi
hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.
NAPE ATEMBELEA MITAMBO YA KURUSHA MATANGAZO YA TBC ARUSHA
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo
ya kutoka kwa Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.
Clement Mshana (kushoto)mara baada ya kutembelea maeneo ya TBC yaliyopo
Themi na Themi Hill mkoani Arusha na kujionea mitambo ya TBC na ile
iliyokuwa ya Radio Tanzania .
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia
mitambo iliyokuwa ya Radio Tanzania kwenye nyumba iliyokuwa ikitumika
kurusha matangazo, Themi mkoani Arusha.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akionyeshwa
moja ya eneo la TBC mkoani Arusha na Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC)Bw. Clement Mshana
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungunmza na
Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Bw. Clement Mshana mara baada ya kutembelea eneo la TBC lililopo Themi mkoani Arusha,katikati ni Mkuu wa Kanda wa Shirika la Utangazaji TBC Ndugu Christopher Mkama
Bw. Clement Mshana mara baada ya kutembelea eneo la TBC lililopo Themi mkoani Arusha,katikati ni Mkuu wa Kanda wa Shirika la Utangazaji TBC Ndugu Christopher Mkama
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia
baadhi ya mitambo ya zamani ya kurushia matangazo iliyopo Themi Hill,
Arusha.
EWURA YATANGAZA KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA NCHINI
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta nchini kuanzia kesho Machi 2, 2016.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta nchini kuanzia kesho Machi 2, 2016.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI MWANZA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , Magesa Mulongo baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo
baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016.
(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabulla baada ya kuwasili kwenye uwanja
wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwasalimu wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza
Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo. (picha
na Ofisi ys Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akitazama ngoma ya nyoka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Magessa Mulongo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wanakwa wa Makongoro Vijana wakiimba wakati Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MKUTANO WA 10 WA KUTATHMINI SEKTA YA AFYA UNAOFANYIKA KILA MWAKA WAFUNGULIWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.
Muhammed Jidawi akiwakaribisha washiriki wa Mkutano wa siku tatu wa
kutathmini sekta ya Afya Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach
Resort, Mazizini.
Kiongozi wa washirika wa
maendeleo kutoaka Mashiriki ya Umoja wa Mataifa DKT. Kirsten Havemann
akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya
Zanzibar unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Baadhi ya washirika wa maendeleo
na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano
huo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua Mkutano wa 10 wa
kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya Zanzibar kwa niaba ya Rais wa
Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizi nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar
Mahmoud Thabit Kombo akiteta jambo na kiongozi wa washirika wa maendeleo
kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Dkt. Kirsten Havemann wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar.
No comments :
Post a Comment