Pages

Wednesday, March 2, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMLAKI RAIS MUSEVENI WA UGANDA JIJINI ARUSHA LEO


JAK
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipowasili jijini Arusha leo tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Augustine Mahiga.(PICHA NA IKULU)
MHA1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiongea na wanahabari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
MHA3 MHA5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika  mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
PICHA NA IKULU

MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI TMA, YAWAPIGA MSASA WANAHABARI KUHUSU EL-NINO NA ATHARI ZAKE.

mz
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua Warsha ya Siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
…………………………………………………………………………………
Na:George Binagi-GB Pazzo
Katika Warsha hiyo, Taasisi mbalimbali pamoja na Wanajamii, zimehimizwa kutumia taarifa za Utabiri wa Hali ya Hewa kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo.
 
Pia Wanahabari ambao ni kiunganishi Muhimu katika upashanaji wa habari, wametakiwa kutumia nafasi yao katika kutoa taarifa hizo kwa wananchi ikizingatiwa kwamba, taarifa za utabiri wa hali ya hewa zikiwafikia walengwa kwa wakati, husaidia kujikinga na maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Mafuriko na ukame.
 
Warsha hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kwa ushirikiano wa karibu na Mamlaka ya Hali ya Hewa Duniani (WMO) ikiwa ni katika mpango wake wa Kidunia katika kuboresha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa ujulikanao kama Global Framework For Climate Services (GFCS).
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, akifungua Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza. Mayalla amefungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi akizungumza katika Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Ziwa, Augustino Nduganda akitoa neno la Shukrani baada ya Ufunguzi wa Semna kwa Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini.
 
 Wengine kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Hali ya Hewa nchini, Hamza Kabelwa, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Marcella Mayalla, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt.Agness Kijazi.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza
Alphonce Tonny kutoka Metro Fm Mwanza (Kushoto) akiwa pamoja na Iman Hezron Kutoka City Fm Mwanza.
Warsha ya Wanahabari Kuhusu El-Nino na athari zake katika Mvua hapa nchini, iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza

LUKUVI ATEMBELEA ENEO LA UBOMOAJI WA JENGO LA GHOROFA 16

lukv1
Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akiangalia maendeleo ya kazi ya ubomoaji wa jengo la ghorofa  kumi na sita (16) ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.
lukv2
Mafundi wakiendelea na Ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.

Bank Of Africa Yawajengea Uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar Kutengeneza Mpango wa Kujenga na Kuboresha Biashara Zao.


Mkufunzi wa Warsha ya ilioandaliwa na Bank of Africa Erick Chrispin akitowa Mada wakati wa Warsha hiyo iliowajumuisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali Zanzibar katika Kuboresha na Kujenga Biashara katika kutengeneza Mpango wa Biashara iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
 Washirikib wa Warsha hiyo wakifuatilia kwa makini Mada zinazowesilishwa wakati wa Warshi hiyo ilioandaliwa na Bank Of Africa.
 Washiriki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakifuatilia Mada zikiwasilishwa 
  Mtoa Mada Ndg Erick Chirispin akisisitiza jambo wakati wa kutoa Mada katika Warsha hiyo. Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar katika Kujenga na Kuboresha Biashara katika kutengeneza Mpango wa Biashara.  
 Washiriki wakiwa Ukumbi wa Mkutano wakifuatilia Mada .  
Washiriki wakichanjia wakati wa warsha hiyo.
Mshiriki wa Warsha ya kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Biashara na Kujenga na Kuboresha Biashara akichangia wakati wa warsha hiyo.
Mtoa Mada Ndg. Erick Chrispin akionesha kitabu chenye mpango wa Biashara wakati wa warsha hiyo kwa Wafanyabiashara wa Zanzibar na Wadau ilioandaliwa na Bank Of Africa katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Washiriki wa Warsha ya Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara Zanzibar katika kuandaa Mpango wa Biashara wakiwa nje ya ukumbi wakibadilishana mawazo wakati wa mapunziko ya mchana.
Imeandaliwa na OthmanMapara.Blogspot.com Zanzinews.com,

ZIMBABWE KUWASILI KESHO

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake ya Zimbabwe, inatarajiwa kuwasili kesho Alhamis mchana wakiwa na msafara wa watu 29, wakiwemo wachezaji 20 pamoja na viongozi 9 tayari kwa ajili ya mchezo wa siku ya Ijumaa dhidi ya wenyeji Twiga Stars uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Zimbabwe watafikia hoteli ya DeMag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.
Upande wa waamuzi wa mchezo huo wanatrajiwa kuwasili kesho mchana kwa shirikia la ndege la Kenya (KQ) wakitokea nchini Ethiopia, huku kamisaa wa mchezo kutoka Congo DR akiwasili jioni kwa KQ.
Maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika ambapo ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, tiketi za mchezo huo zitauzwa eneo la uwanja Chamazi siku ya Ijumaa. Viingilio vya mchezo ni shilingi elfu mbili (2,000) kwa mzunguko na shilingi elfu tatu (3,000) kwa jukwaa kuu.
TFF inawaomba wadau, wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.

MALINZI AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI INFATINO

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.
Katika barua hiyo, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikiko mema.
infatino

MAJALIWA AWASILI WILAYANI BUSEGA KWA ZIAR

bus1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa a Simiyu, Erasto Mbwiro baada ya kuwasili wilayani Busega kuanza ziaraya mkoa huo, Machi 2, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bus2
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni baada ya kuwasili wilayani Busega akiwa aktika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 2, 2016. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Erasto, Mbwiro. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bus4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega akiwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 2, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bus5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na viongozi wengine wakipiga makofi mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega akiwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 2, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bus6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Nyashimo wilayani Busega kabla ya kukagua ujenzi wa wodi ya wazazi  kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi, 2, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Mzindakaya. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bus9
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua  ujenzi wa wodi ya Wazazi   katika kijiji cha Nyashimo  wilaya ya Busega akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 2, 2016. Kushoto ni Mbunge wa Busega, Dkt, Raphael Chegeni na Kulia nI Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAREKANI YAIKABIDHI SERIKALI YA TANZANIA MBWA MAALUMU WA KUBAINI DAWA ZA KULEVYA NA PEMBE ZA NDOVU

sau1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akizungumza katika shughuli ambapo Marekani iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau2
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser akizungumza katika shughuli ambapo nchi yake iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe,wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni, anayefuata ni  Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau3
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akimuaga Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser mara baada ya Marekani kuikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Usalama Kanda, Ubalozi wa Marekani nchini, Bruce Paluch. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau4
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akiwafafanulia jambo waandishi wa habari mara baada ya Serikali ya Marekani kuikabidhi Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (D/IGP), Abdulharam Kaniki. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau5
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akisindikizwa  na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser (kushoto) pamoja na Maafisa wengine wa ubalozi huo, mara baada ya kumaliza shughuli ya Marekani ya kuikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

UMILIKI WA ARDHI KWA WANAWAKE WAONGEZEKA – ELUKA KIBONA


Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Eluka Kibona amesema uelewa wa wanawake katika kumiliki ardhi na kufuatilia haki zao za ardhi unaongezeka siku hadi siku nchini na kuondoa ile dhana kwamba wanawake wako nyuma katika shughuli za maendeleo.
Bi Eluka ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Blogs za Mikoa kuhusu namna taasisi binafsi zinavyotetea harakati za wanawake katika kumiliki ardhi hapa nchini na kujiendeleza kiuchumi ambapo amesema kwa kulinganisha miaka 10 iliyopita na sasa, wanawake kwa sasa wamekuwa na muamko zaidi wa kupambana na changamoto za umiliki wa ardhi wanazokutana nazo.
”Sisi tunaunga mkono harakati na jitihada za kuleta usawa kati ya wanaume na wanawake mjini na vijijini na hii ni baada ya kutambua kuwa matatizo ya umiliki wa ardhi kwa wanawake wa mjini na vijijini yako sawa kutokana na
mfumo ulivyo katika jamii.”Ameeleza Bi Eluka.

Mmoja wa wanawake (Kulia) akipokea hati yake ya kumiliki ardhi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster katika kijiji cha Gongoni wilayani Kilosa.
”Kuna madai ya ardhi ambayo wanawake wanakumbana nayo katika jamii kwa kudhulumiwa na wengine kwa kunyimwa haki zao za msingi hivyo tunawasaidia katika kuwawezesha kutambua namna ya kupigania haki zao.”Amesisitiza Bi Eluka.
Kuhusu siku ya wanawake duniani ambayo huazimishwa kila Machi 8 kila mwaka, Bi Eluka amesema Oxfam Tanzania imejipanga kufanya maadhimisho katika mkoa wa Mtwara ili kuunga mkono jitihada za wanawake katika kujikwamua na mifumo kandamizi hapa nchini na kujiendeleza kiuchumi.
Mmoja wa wanawake akiwa katika kilimo
Kwa mujibu wa Bi Eluka, Oxfam imewezesha wanawake wengi kuweza kupata haki zao katika mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya mikoa hiyo ni Shinyanga, Arusha, Tanga Morogoro/
Aidha kwa mujibu wa sheria ya ardhi inatamka bayana kuwa mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi. (Kifungu 3(2) cha sheria ya ardhi na sheria ya ardhi ya vijiji za 1999).
Hata hivyo ni muhimu kila mmiliki wa ardhi awe na hati/ cheti halisi cha hakimiliki kuthibithisha haki yake ya kumiliki ardhi kisheria.

UKWELI KUHUSU OLDUVAI GORGE, NGORNGORO CRATER, MBWANA SAMATTA NA ABDUL NASIB (DIAMOND PLATNUMZ).


MAELEZO YA MHE. UMMY ALLY MWALIMU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WAKATI AKIPOKEA MSAADA WA FEDHA KWA AJILI YA KUWEZESHA MATIBABU YA WAGONJWA WA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

msd1
Awali ya yote nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujali afya njema na hatimaye ametuwezesha tukusanyike mahali hapa. Vile vile, nitumie fursa hii kuwashukuru watumishi wote wa Afya kwa kazi nzuri wanayoifanya ya utoaji wa huduma za afya kwa watanzania wote. Pia, nitumie nafasi hii kuwapongeza ndugu zetu wa Jumuiya ya Kihindu ya hapa Dar es Salaam ijulikanayo kama BAPS, kwa kuguswa kwao na kutoa msaada mkubwa na upendo waliouonyesha kwa watanzania hawa wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.
Nimeafiriwa kuwa kiasi cha msaada unaotolewa utawezesha wagonjwa wapato 100 kupatiwa matibabu ya moyo. Hii ni faraja kubwa kwa wagonjwa wetu waliokuwa wakisubiri huduma hizi kwa muda mrefu.
Takwimu zinaonyesha kuwa, kuna ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo, kisukari, n.k. Wizara yangu imejipanga kuhakikisha kuwa inaweka mkazo katika kutoa elimu ya kujikinga na maradhi mbalimbali ili kuokoa maisha ya watanzania walio wengi. Ni dhahiri kuwa gharama za matibabu zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku. Hivyo, nitoe rai kwa watanzania wote, tujaribu kuzingatia Kanuni za Afya kama kufanya mazoezi, kula vyakula kwa kuzingatia mahitaji ya miili yetu, na kupima afya zetu mara kwa mara.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imekuwa ikiendesha huduma hizi za kambi, kila inapoona kuna ongezeko la wagonjwa wanaohitaji tiba za aina hii.  Kitendo hiki ni kizuri kwa kuwa kinawezesha wananchi/wagonjwa kupata huduma hii kwa haraka zaidi. Ni matarajio yangu kuwa kambi itakayoanza tarehe 7/3/2016, itanufaisha wagonjwa wengi zaidi ikiwezekana nusu ya wagonjwa hao wanaosubiri huduma hii.
Mmetaarifiwa kuwa wagonjwa waliopo sasa wanatoka karibu kila pembe ya nchi yetu, mathalani katika wagonjwa watakaofanyiwa matibabu, wagonjwa 10 wanatoka Zanzibar na waliobaki wanatoka Tanzania Bara.
Lengo la Serikali ni kuboresha huduma za Tiba za Rufaa nchini ili kupunguza idadi ya rufaa za wagonjwa nje ya nchi. Mfano: kati ya mwaka 2000 hadi 2014 jumla ya wagonjwa 7,363 walipewa rufaa kwenda kutibiwa nje ya nchi sawa na wastani wa wagonjwa 526 kwa mwaka ambapo kati yao wagonjwa 4,413 sawa na wastani wa wagonjwa 315 kwa mwaka waliweza kwenda nje ya nchi kwa matibabu. Aidha, kati ya mwaka 2012 na 2015 wagonjwa 1465 walitibwa nje ya nchi kwa gharama za Serikali. Karibu asilimia 50 ya wagonjwa waliotibiwa nje ya nchi kwa gharama za Serikali kati ya mwaka 2012 hadi Novemba, 2015 walikuwa wanaugua magonjwa ya moyo. Kutokana na ukubwa wa tatizo la magonjwa ya moyo Serikali mwaka 2008 iliamua kuanzisha huduma za upasuaji mkubwa wa moyo na hatimaye kujenga Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambayo ilianza Aprili, 2015. Tangu kuanza kwa Taasisi hii, kambi maalumu za upasuaji moyo zimekuwa zikiendeshwa na wataalamu wa hapa nchini kwa kushirikiana na wa kutoka nje ya nchi ambapo jumla ya wagonjwa 247 wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Kambi za upasuaji zimesaidia kupunguza idadi ya wagonjwa ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Aidha, hatua hii imepunguza gharama kwa Serikali kwa sababu idadi ya wagonjwa wa moyo waliopata rufaa imepungua toka 198 hadi 89 kati ya mwaka 2013 na Novemba 2015.
Matibabu nje ya nchi yana gharama kubwa ambazo zinatofautiana kulingana na ugonjwa husika. Gharama za kumtibu mgonjwa mmoja wa moyo ni Shs.16,500,000.00 mgonjwa mmoja wa figo ni Shs.57,750,000.00 na mgonjwa mmoja wa saratani ni Shs.74,250,000.00. Matumizi ya fedha kwa ajili ya matibabu nje ya nchi yamekuwa yakiongezeka kulingana na kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa. Kuongezeka idadi ya wagonjwa wa rufaa kumesababisha Serikali kuwa na limbikizo la deni lililofikia Shs.28,743,586,356/= hadi kufikia mwezi Desemba, 2015.
Kabla sijamaliza maelezo yangu, nitoe shukurani za dhati kwa Madaktari na Wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete  (JKCI). Kipekee kabisa niwashukuru Jumuiya ya Kihindu ya BAPS kwa msaada mkubwa walioutoa katika kuhakikisha wanaokoa maisha ya watanzania hao, niendelee kuwaomba pale mtakapoguswa zaidi, saidieni katika maeneo mengine pia kama ununuzi wa vifaa tiba na ikiwezekana basi msaidie ili wagonjwa waliobaki wapate tiba wote hapa nchini. Huu ni uzalendo wa hali ya juu na tunashukuru kwa kumuunga mkono Mhe. John Pombe Magufuli Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma zote za msingi kadri inavyowezekana siku zote tunasema “kutoa ni moyo usambe si utajiri”.

TANZANIA YAIOMBA KOICA KUONGEZA MUDA WA MKATABA WA MRADI WA GEBR

Zulmira Rodrigues
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdula Lutavi (aliyeipa mgongo kamera) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Mkoani Tanga. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara (GEBR) limefanyika mkoani Tanga.
Wenyeji wa kongamano hilo walikuwa ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO) ofisi ya Dar es salaam.
Akifungua kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Korea kusini kupitia shirika lake la maendeleo na ushirikiano la kimataifa (KOICA) kuongeza muda wa mkataba wa mradi wa GEBR ambao unafikia ukomo mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na washiriki mbalimbali wapatao 40 kutokana ndani na nje ya nchi zikiwemo Ghana na Nigeria kutoka Afrika, alisema ombi hilo linatokana na ukweli kuwa walengwa wamekuwa wakifaidika na mradi huo, kwa kuweza kubadilisha maisha yao na kuwa bora zaidi.
Makamu wa Rais alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na kutoweka kwa uotoasili unaotoa fursa ya uoto wa mimea zaidi ya 10,000, jamii 6,000 ya wadudu, jamii ipatayo 1000 ya ndege warukao.
Aidha Samia katika hotuba yake alirejea msimamo wa serikali wa kutaka kuhifadhi mazingira, pamoja na kuziweka rasmi chini ya uangalizi halali jumla ya hekta milioni 33.5 za misitu asili, huku akitanabaisha kuwa serikali pia ina mapori ya akiba yapatayo 800 pamoja na misitu mingine.
Aliwakumbusha washikadau pamoja na nchi wafadhili kwamba Tanzania inakabiliwa na ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wake wanaotegemea raslimali kwa matumizi yao ya kila siku pamoja na mahitaji ya nishati.
“Tunaelewa kwamba kuna shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zinazopelekea uharibifu wa misitu na mazingira”, alisema Samia na kuongeza kwamba kuna kupokonyana kwa ardhi na maji.
Katika warsha hiyo wafaidika wakubwa katika mradi huo, ambao walitekeleza kwa vitendo elimu iliyopatikana kutokana na mradi huo, walikabidhiwa vyeti ya ushiriki kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa walioonyesha.
Washiriki hao wengi walitoka katika miradi midogo midogo inayotekelezwa Amani, Muheza ambayo ni pamoja na ufugaji nyuki, samaki, vipepeo na uyoga.
Zulmira Rodrigues
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) alipowasili kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort jana kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara lililoandaliwa na UNESCO. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza aliwataka wakazi wa Tanga na Tanzania kwa ujumla kutumia vyema nafasi adhimu kwenye miradi ya maendeleo inayogharimiwa na wafadhili na kuwasihi wawe makini kwani mafanikio yao huwa ni kivutio kwa wafadhili kuweza kuendelea kutoa ufadhili kwa misaada.
Mradi wa GEBR ambao uko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wake, unafadhiliwa na serikali ya Korea kupitia Shirika lake la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA).
Mradi huo wa Unesco wa binadamu na bayosfia (MAB) unatekelezwa nchini Ghana, Nigeria na Tanzania kwenye milima ya Usambara.
Katika hotuba yake Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Firmin Matoko alimpongeza Makamu wa rais kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu katika utawala tangu historia ya kuundwa kwa Tanzania.
Alisema amefurahishwa sana na wanawake kuchukua nafasi kwa kuwa Unesco wameweka kipaumbele wanawake katika maendeleo.
Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano hoteli ya Tanga Beach Resort akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko.
Akizungumzia mradi wa GEBR alisema umelenga kutekelezwa katia msingi wa wazo la UNESCO la binadamu na bayosfia.
Alisema kwamba mradi huo umelenga kutumia elimu ya asili, elimu ya sayansi na utamaduni ili kuboresha maisha ya biandamu huku wakihifadhi mazingira.
Aidha alitaka kuwapo ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo na hifadhi ya bayosfia kwa lengo la kuwezesha maendeleo endelevu.
Washiriki wa mradi huo pia walipata nafasi ya kutembelea eneo la hifadhi ya Usambara mashariki.
Naye Balozi wa Jamhuri ya Korea, Bw Geum-Young Song alisema kwamba wataendelea kushiriki katika mradi huo ambao umejikita katika kuwezesha maendeleo endelevu huku mazingira yakihifadhiwa.
Maimuna Tarishi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Alisema ni lengo la taifa lake la kuwezesha hifadhi endelevu kwa maendeleo endelevu.
Aidha alitaka kuwepo na fikra za mradi kuwa endelevu baada ya wafadhili kuondoka.
Viongozi waliohudhuria siku ya ufunguzi ni pamoja na Makamu wa Rais Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Bw. Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Mh. Geum -Young Song, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Unesco nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues, Wawakilishi wa KOICA nchini Ghana, Nigeria na Tanzania; mwakilishi wa KOICA nchini Korea, Seoul; na kamati za MAB kutoka nchi zinazotekeleza mradi huo.
DSC_5118
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
IMG_4589
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Afrika, Firmin Matoko kuhutubia kwenye kongamano hilo.
Firmin Matoko
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UNESCO, Irina Bokova wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Song Geum-Young
Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song ambao ni wafadhili wa mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui akisoma taarifa yake baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufungua Kongamano hilo la pili la Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
DSC_5078
Pichani juu na chini washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
IMG_4562
IMG_4616
IMG_4549
Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Uyoga (DMGA), Bi Judith Simon Muro, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui.
IMG_4733
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira asili Amani (Amani Forest Nature Reserve – ANR), Bi. Mwanaidi Kijazi, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui. Wanaoshuhudia tukio hilo kulia Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar (wa kwanza kushoto).
DSC_5150
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Amiri Saidi Sheghembe wa mradi wa Vipepeo Amani kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui.
Mary Kawar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan , akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar.
Samia Suluhu Hassan
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki kutoka nje ya Tanzania wanaohudhuria Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
IMG_4817
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Samia Suluhu Hassan
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UNESCO walioshiriki kwenye maandalizi ya kongamano hilo.
Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Afisa Tathimini na Logistki wa UNESCO Ofisi ya Dar es Salaam, Rahma Islem (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
Firmin Matoko, UNESCO
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko (kushoto) akisalimiana na mmoja wadau wa maendeleo Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song .
IMG_4886
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi katika picha ya kumbukumbu na Mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye pia ni Katibu Klabu ya Safe Space inayojihusisha na utunzaji wa Mazingira, Lilian Tadei wa Shule ya Sekondari Potwe, Muheza.
Zulmira Rodrigues
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.

WAZAZI WALALAMIKA KUFUNGWA KWA MATAWI YA CHUO KIKUU CHA ST, JOSEPH

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 
BAADHI   ya wazazi wa wanafaunziwaliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph katika  matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.

NAPE ATEMBELEA MITAMBO YA KURUSHA MATANGAZO YA TBC ARUSHA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo ya kutoka kwa Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kushoto)mara baada ya kutembelea maeneo ya TBC yaliyopo Themi na Themi Hill mkoani Arusha na kujionea mitambo ya TBC na ile iliyokuwa ya Radio Tanzania .
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia mitambo iliyokuwa ya Radio Tanzania kwenye nyumba iliyokuwa ikitumika kurusha matangazo, Themi mkoani Arusha.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akionyeshwa moja ya eneo la TBC mkoani Arusha na Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)Bw. Clement Mshana
 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungunmza na Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Bw. Clement Mshana mara baada ya kutembelea eneo la TBC lililopo Themi mkoani Arusha,katikati ni Mkuu wa Kanda wa Shirika la Utangazaji TBC Ndugu Christopher Mkama
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia baadhi ya mitambo ya zamani ya kurushia matangazo iliyopo Themi Hill, Arusha.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI

guf

EWURA YATANGAZA KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA NCHINI

 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu bei kikomo za mafuta aina ya petroli kuanzia leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Umeme, Mhandisi Anastas Mbawala.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (katikati), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Umeme, Mhandisi Anastas Mbawala na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Petroli, Gerald Maganga.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta nchini kuanzia kesho Machi 2, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI MWANZA

mul1
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , Magesa Mulongo baada ya kuwasili kwenye uwanja  wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mul2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mul3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mul4
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, Angelina Mabulla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mul5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo. (picha na Ofisi ys Waziri Mkuu)
mul6
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama ngoma  ya nyoka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Magessa Mulongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mul8
Wanakwa wa Makongoro Vijana wakiimba wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 

MKUTANO WA 10 WA KUTATHMINI SEKTA YA AFYA UNAOFANYIKA KILA MWAKA WAFUNGULIWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI

zaz1
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Muhammed Jidawi akiwakaribisha washiriki wa Mkutano wa siku tatu wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mazizini.
zaz2
Kiongozi wa washirika wa maendeleo kutoaka Mashiriki ya Umoja wa Mataifa DKT. Kirsten Havemann akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
zaz3
Baadhi ya washirika wa maendeleo  na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
zaz4
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua Mkutano wa 10 wa kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Zanzibar  katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
zaz5
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiteta jambo na kiongozi wa washirika wa maendeleo kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Dkt. Kirsten Havemann wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment