Sunday, February 28, 2016

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AZINDUA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU – JUNIOR NATIONAL BASKET ASSOCIATION (JR.NBA)


 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya mitoano  Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana,  katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizinduwa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA),leo jijini Dar es Salaam. 
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster, leo jijini Dar es Salaam
Sehemu ya mashabiki wa  Mpira wa kikapu   walio fika katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

Yanga yaikandamiza Cercale De Joachim ya Mauritius 2-0 uwanja wa Taifa

y1
Wachezaji wa timu ya Yanga, wakishangilia sambamba na mashabiki wao, baada ya kufunga goli la pili dhidi ya timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0. Picha zote na Othman Michuzi.
y2
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akiondoka na mpira na kumuacha Beki wa Timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.

Tafrija ya mchapalo wa uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi ya Tigo 4G Mkoani Kilimanjaro yafana

 
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara kampuni ya Tigo(B2B), Rene Bascope akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makala(wa pili kulia) akimkabidhi Emmanuel Kilaga, zawadi kutoka Tigo   wakati wa hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Mtaalam wa mtandao kutoka Tigo Samira Baamar.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.
Mtaalam wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar(wa tatu kulia), akimkabidhi zawadi mmoja kati ya washindi waliojishindia zawadi mbalimbali.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mjini Moshi juzi.

Nape awapongeza Efm kwa kipindi cha (Sports Head Quarter) kutimiza mwaka mmoja

nip1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wapili kulia) pamoja na mashabiki wa Timu za Taifa wakiwa wameshika  keki ya birthday ya kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) iliyotolewa na mashabiki hao wakati wa hafla kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwa kipindi hicho jana jijini Dar es Salaam. 
nip2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.
nip3
Mkurugenzi Mtendaji wa Efm Radio Frances Ciza akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.
nip4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata keki ya birthday ya kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake.Kulia nim Mkurugenzi Mtendaji wa EFM Radio Francis Ciza.

ZIARA YA WAZIRI MKUU MAJALIWA – MTWARA

kasl1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada ya kuzungumza nao  chuoni hapo , Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada ya kuzungumza nao  chuoni hapo , Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl3
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara Februari 27, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na wafanyakazi wa  kampuni ya TPDC baada ya kuwasili kwenye mtambo wa kuchakata  gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini kukagua shughuli za gesi Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl7
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPDC baada ya kutembelea mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl8
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA.

Ernest+Mangu+Photo
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda 
wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa  kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na   Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe. Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.  
Aidha,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar es  Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria,  kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.
 Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
 Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)
 Makao Makuu ya Polisi.

Tovuti ya Proin Promotions yavamiwa, Kurudi hewani mara baada ya tatizo kushughulikiwa


Tunasikitika kuutangazia umma wa watanzania na wadau wetu kwa ujumla kuwa tovuti yetu ya www.proinpromotions.co.tz imevamiwa na watu wanaojiita Classic Flame kwa kitaalamu kunaitwa Hacked.

Timu nzima ya Proin Promotions Ltd inapenda kuwataarifu kuwa wadau wetu kuwa tunalifanyia kazi na kuhakikisha tunaongeza ulinzi katika tovuti yetu na kuirudisha hewani. Tunatarajia baada ya kuirudisha hewani itakuwa imara zaidi na zaidi na tunaamini hii ni changamoto tu katika sekta ya teknolojia.

Tunawaahidi kuwa tovuti yetu itarudi hewani mara baada ya wataalamu wetu kulishughulikia hilo tatizo kwani ni tatizo ndogo.

HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE

Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kuwataka waandishi wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na watafiti kuweka hadharani na kuueleza umma kile kilichotokea Zanzibar, Waandishi na watafiti mabalimbalai wamejitokeza  na vielelezo  vinavyoeleza jinsi uchaguzi huo ulivyoharibika
Vielelezo hivyo ni Nakala za fomu namba MUR. 12A za matokeo zilizotoka katika vituo vya kujumuisha kura ambazo zilikuwa zimejazwa kimakosa.
Hii ni fomu kutoka Kituo cha Skuli ya Mabaoni namba 23801, Jimbo la Chonga namba 2909 fomu hii siyo halali kutokana na kukosa mhuri wa tume ya uchaguzi Zanzibar.  Msimamizi wa kituo ni Khamis mkungwa Zaid.
Fomu nyingine inatoka katika kituo cha Urusi chenye namba 26503, katika jimbo la Jang’ombe namba 1940
A. Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008
Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008, Jimbo la Mkwajuni  namba 1926, fomu hii imepoteza uhalali kwasababu imefutwafutwa na haina mhuri wala jina la msimamizi wa kituo.
B. Kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi
Hii ni fomu kutoka katika kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi namba 21618, Katika  jimbo la Chumbuni namba 1931, fomu hii imekosa uhalali kwasababu imefutwa majina ya mawakala na kupandikizwa majina mengine juu ya maandishi ya kivuli.
C. Jimbo la Chumbuni namba 1937
Hizi  mbili,  fomu kutoka kiwanja cha mpira Masumbani namba 29304 kutoka jimbo la Chumbuni namba 1937, fomu hii inakosa uhalali kwa sababu haina mhuri , maandishi ya meandikwa tena kwa kalamu juu ya maandishi ya kivuli na saini imewekwa zaidi uya mara moja.  Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu inamhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
D. Mihuri ya kughushi
Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu ina mhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
Matumizi ya Mihuri Bandia katika karatasi za kujumuishia matokeo ya wagombea nafasi ya Rasi wa Zanzibar.
E. Fomu zimejirudia zaidi ya mara moja
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC alisema utata wa matokeo ulianza pale wajumbe waliopelekwa Pemba kurudi na kuiarifu Tume dhidi ya matendo yaliyofanywa na wasimamizi wa ZEC Pemba hata hivyo wakati uchunguzi na mabishano yakiendelea Mmoja wa wagombea akaitisha wanahabari na kujitangaza ameshinda kwa matokeo ambayo kila mmoja wetu alishangaa sana,
Ni kitendo cha aibu na Fedheha kubwa wanaoshabikia hawakuona madhara yake,sijui alitoa wapi Takwimu ambazo zilitoa ushindi kwa wagombea wawili tu,tena ukijumlisha asilimia ni 100 inasikitisha sana,Shinikizo la kunitaka nimtangaze mshindi kinyume na taratibu lilinifanya niubebe msalaba kusimamisha na kufuta matokeo baada tu ya kuitisha fomu chache za uthibitisho mwandishi haya ndio tuliyakuta,Ni nusu ya uchaguzi wote kila jimbo ulichezewa
Tumejiridhisha watu wetu watendaji wa ZEC walio apa walifanya haya,kutumia mihuri ya Bandia kujaza hizi fomu kinyume na taratibu kama mnavyo ona alisisitiza Mzee Jecha kwa masikitiko akiwaonyesha waanndishi waliofika kuhoji nini kilitokea hasa.

UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI WAAHIRISHWA KWA AMRI YA MAHAKA, POLISI WAPAMBANA NA MADIWANI WA UKAWA

sam1
Polisi wakipambana na Madiwani wa UKAWA mara baada ya Uchaguzi huo kuairishwa tena leo kutoka na kesi iliyoko mahakamani iliyofunguliwa(Picha kwa hisani ya Fullhabariblog)
sam2
Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiongea na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe kupata ufumbuzi baada ya uchaguzi kuahirishwa kwa amri ya mahakama.
sam3 Polisi wakiwa wamekaa kwenye jukwaa la juu wakifuatilia matukio katika uchaguzi huo ambao umeahirishwa kwa amri ya mahakama.
……………………………………………………………………………………………………………
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuairishwa  tena mwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kwa ajioi ya kutuliza ghasia zilizotokea baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana nakesi iliyoko mahakamani ambapo Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA walipinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo
Tukio hilo la aina yake limetokea mda huu Jijini Hapa mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutanga kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi huo kusimamishwa na  mahakamani , huku jambo hilo lilowachukiza madiwani wa UKAWA wakidai kuwa hawajapata barua hiyo ya kesi hiyo.
Mara baada ya UKAWA kugomea hoja hiyo ndipo wakafikia hatua ya  ya kutaka kufanya uchaguzi wenyewe huku wakisema akidi ya madiwani kufanya uchaguzi imetimia na wakaomba waendelee kufanya uchaguzi huo, jambo ambalo ni sawa na kukidi amri halali ya mahakama ya kusimamisha uchaguzi huo kutokana na kesi iliyoko mahakamani
Wakati wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo ukawa wenyewe ,ndipo Polisi zaidi ya 15 wakaingia  ukumbini humo na kuwataka  madaiwani   hao waachane na zoezi hilo na kuondoka ukumbini,jambo  ambalo liliwachukiza madiwani hao na kuanza vurugu  ndipo Polisi wakaanza kupambana na madiwani hao wa Ukawa  ili kuwatoa nje.

MAJALIWA AWASILI MTWARA KWA ZIARA YA SIKU MOJA

MTW1
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege ea Mtwara kwa ziara ya siku moja mkoani humoFebruari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA LEO

kibo1

RAIS MPYA WA FIFA NI GIANNI INFANTINO

fi1
Gianni Infantino ndiye aliyechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka duniani Fifa
Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
fi2
Infantino akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FIFA
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa mojaWingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita .
FI3
Infantino akiwahutubia wajumbe
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa’

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

d02
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salam Februari 26, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d01 d1
 Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d2
 Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Elinaza Sendoro baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Alex Molasses baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAWAZIRI WOTE WAJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI

c38d70b6-1ea3-40f3-a8b2-95c9813523f8 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12 leo jioni limetekelezwa.eza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.

TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT UNVEILS PLEDGE FOR PARITY CAMPAIGN

5bde23ee-560b-4388-b419-d5d2700d48a2 
Tanzania Women of Achievement (TWA) has announced the launch of the Pledge for Parity Campaign in commemoration of this year’s International Women’s Day care celebration. The campaign is a clarion call for this year’s International Women’s Day (IWD) that calls on everyone to take concrete steps to accelerate the achievement of gender parity in the country. It also calls on the society to practice gender-balanced leadership, respect and value differences, develop more inclusive and flexible cultures and also root out workplace bias.

No comments :

Post a Comment