Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu
bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya
mitoano Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana
kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya
mpira wa kikapu kwa vijana, katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu
ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akizinduwa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA),leo jijini Dar
es Salaam.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, leo jijini Dar es
Salaam.
Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster, leo jijini Dar es Salaam
Sehemu
ya mashabiki wa Mpira wa kikapu walio fika katika uzinduzi wa Ligi
ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
Yanga yaikandamiza Cercale De Joachim ya Mauritius 2-0 uwanja wa Taifa
Wachezaji wa timu ya Yanga,
wakishangilia sambamba na mashabiki wao, baada ya kufunga goli la pili
dhidi ya timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo
wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa
jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga
imeshinda 2-0. Picha zote na Othman Michuzi.
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi
Tambwe akiondoka na mpira na kumuacha Beki wa Timu ya Cercale De Joachim
ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya
Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa
Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.
Tafrija ya mchapalo wa uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi ya Tigo 4G Mkoani Kilimanjaro yafana
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. |
Mkuu wa Kitengo cha Biashara kampuni ya Tigo(B2B), Rene Bascope akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. |
Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. |
Mtaalam wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar(wa tatu kulia), akimkabidhi zawadi mmoja kati ya washindi waliojishindia zawadi mbalimbali. |
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mjini Moshi juzi. |
Nape awapongeza Efm kwa kipindi cha (Sports Head Quarter) kutimiza mwaka mmoja
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wapili kulia) pamoja na
mashabiki wa Timu za Taifa wakiwa wameshika keki ya birthday ya kipindi
cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) iliyotolewa na
mashabiki hao wakati wa hafla kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwa
kipindi hicho jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya
kutimiza mwaka mmoja kwa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head
Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Efm Radio
Frances Ciza akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa
kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa
hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata keki ya birthday ya
kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa
hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho
kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake.Kulia nim Mkurugenzi
Mtendaji wa EFM Radio Francis Ciza.
ZIARA YA WAZIRI MKUU MAJALIWA – MTWARA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada
ya kuzungumza nao chuoni hapo , Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada
ya kuzungumza nao chuoni hapo , Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akitembelea bandari ya Mtwara Februari 27, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara Halima Dendego.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya TPDC baada ya kuwasili
kwenye mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini kukagua
shughuli za gesi Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na
viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPDC
baada ya kutembelea mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini
Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda
wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.
Mabadiliko hayo ni pamoja na
aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi
Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi
SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam. Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi
cha Kuzuia dawa za kulevya. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa
kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe. Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa
Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda kuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao
Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi
mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa
Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na nafasi yake
kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka
Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa
Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda kuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu
ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni pamoja na Naibu
Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar
es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam
pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe anakwenda
kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)
Makao Makuu ya Polisi.
Tovuti ya Proin Promotions yavamiwa, Kurudi hewani mara baada ya tatizo kushughulikiwa
Tunasikitika
kuutangazia umma wa watanzania na wadau wetu kwa ujumla kuwa tovuti
yetu ya www.proinpromotions.co.tz imevamiwa na watu wanaojiita Classic
Flame kwa kitaalamu kunaitwa Hacked.
Timu
nzima ya Proin Promotions Ltd inapenda kuwataarifu kuwa wadau wetu kuwa
tunalifanyia kazi na kuhakikisha tunaongeza ulinzi katika tovuti yetu
na kuirudisha hewani. Tunatarajia baada ya kuirudisha hewani itakuwa
imara zaidi na zaidi na tunaamini hii ni changamoto tu katika sekta ya
teknolojia.
Tunawaahidi kuwa tovuti yetu itarudi hewani mara baada ya wataalamu wetu kulishughulikia hilo tatizo kwani ni tatizo ndogo.
HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE
Baada ya Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kuwataka waandishi
wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na watafiti kuweka hadharani na
kuueleza umma kile kilichotokea Zanzibar, Waandishi na watafiti
mabalimbalai wamejitokeza na vielelezo vinavyoeleza jinsi uchaguzi huo
ulivyoharibika
Vielelezo hivyo ni Nakala za fomu
namba MUR. 12A za matokeo zilizotoka katika vituo vya kujumuisha kura
ambazo zilikuwa zimejazwa kimakosa.
Hii ni fomu kutoka Kituo cha
Skuli ya Mabaoni namba 23801, Jimbo la Chonga namba 2909 fomu hii siyo
halali kutokana na kukosa mhuri wa tume ya uchaguzi Zanzibar. Msimamizi
wa kituo ni Khamis mkungwa Zaid.
Fomu nyingine inatoka katika kituo cha Urusi chenye namba 26503, katika jimbo la Jang’ombe namba 1940
A. Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008
Hii ni fomu kutoka kituo cha
Gamba namba 2008, Jimbo la Mkwajuni namba 1926, fomu hii imepoteza
uhalali kwasababu imefutwafutwa na haina mhuri wala jina la msimamizi wa
kituo.
B. Kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi
Hii ni fomu kutoka katika kituo
cha Skuli ya Mwembe Makumbi namba 21618, Katika jimbo la Chumbuni namba
1931, fomu hii imekosa uhalali kwasababu imefutwa majina ya mawakala na
kupandikizwa majina mengine juu ya maandishi ya kivuli.
C. Jimbo la Chumbuni namba 1937
Hizi mbili, fomu kutoka kiwanja
cha mpira Masumbani namba 29304 kutoka jimbo la Chumbuni namba 1937,
fomu hii inakosa uhalali kwa sababu haina mhuri , maandishi ya meandikwa
tena kwa kalamu juu ya maandishi ya kivuli na saini imewekwa zaidi uya
mara moja. Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na
namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu inamhuri ambao siyo
wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar
ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
D. Mihuri ya kughushi
Fomu ya pili ni kutoka jimbo la
Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali
kwasababu ina mhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
Matumizi ya Mihuri Bandia katika karatasi za kujumuishia matokeo ya wagombea nafasi ya Rasi wa Zanzibar.
E. Fomu zimejirudia zaidi ya mara moja
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC
alisema utata wa matokeo ulianza pale wajumbe waliopelekwa Pemba kurudi
na kuiarifu Tume dhidi ya matendo yaliyofanywa na wasimamizi wa ZEC
Pemba hata hivyo wakati uchunguzi na mabishano yakiendelea Mmoja wa
wagombea akaitisha wanahabari na kujitangaza ameshinda kwa matokeo
ambayo kila mmoja wetu alishangaa sana,
Ni kitendo cha aibu na Fedheha
kubwa wanaoshabikia hawakuona madhara yake,sijui alitoa wapi Takwimu
ambazo zilitoa ushindi kwa wagombea wawili tu,tena ukijumlisha asilimia
ni 100 inasikitisha sana,Shinikizo la kunitaka nimtangaze mshindi
kinyume na taratibu lilinifanya niubebe msalaba kusimamisha na kufuta
matokeo baada tu ya kuitisha fomu chache za uthibitisho mwandishi haya
ndio tuliyakuta,Ni nusu ya uchaguzi wote kila jimbo ulichezewa
Tumejiridhisha watu wetu
watendaji wa ZEC walio apa walifanya haya,kutumia mihuri ya Bandia
kujaza hizi fomu kinyume na taratibu kama mnavyo ona alisisitiza Mzee
Jecha kwa masikitiko akiwaonyesha waanndishi waliofika kuhoji nini
kilitokea hasa.
UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI WAAHIRISHWA KWA AMRI YA MAHAKA, POLISI WAPAMBANA NA MADIWANI WA UKAWA
Polisi wakipambana na Madiwani wa
UKAWA mara baada ya Uchaguzi huo kuairishwa tena leo kutoka na kesi
iliyoko mahakamani iliyofunguliwa(Picha kwa hisani ya Fullhabariblog)
Mbunge wa Kibamba John Mnyika
akiongea na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe kupata ufumbuzi
baada ya uchaguzi kuahirishwa kwa amri ya mahakama.
Polisi wakiwa wamekaa kwenye jukwaa la juu wakifuatilia matukio katika uchaguzi huo ambao umeahirishwa kwa amri ya mahakama.
……………………………………………………………………………………………………………
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuairishwa tena mwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kwa ajioi ya kutuliza ghasia zilizotokea baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana nakesi iliyoko mahakamani ambapo Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA walipinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo
……………………………………………………………………………………………………………
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuairishwa tena mwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kwa ajioi ya kutuliza ghasia zilizotokea baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana nakesi iliyoko mahakamani ambapo Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA walipinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo
Tukio
hilo la aina yake limetokea mda huu Jijini Hapa mara baada ya
mkurugenzi wa Jiji kutanga kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi
huo kusimamishwa na mahakamani , huku jambo hilo lilowachukiza
madiwani wa UKAWA wakidai kuwa hawajapata barua hiyo ya kesi hiyo.
Mara baada ya UKAWA kugomea hoja hiyo ndipo wakafikia hatua ya ya
kutaka kufanya uchaguzi wenyewe huku wakisema akidi ya madiwani kufanya
uchaguzi imetimia na wakaomba waendelee kufanya uchaguzi huo, jambo
ambalo ni sawa na kukidi amri halali ya mahakama ya kusimamisha uchaguzi
huo kutokana na kesi iliyoko mahakamani
Wakati
wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo ukawa wenyewe ,ndipo Polisi zaidi ya
15 wakaingia ukumbini humo na kuwataka madaiwani hao waachane na
zoezi hilo na kuondoka ukumbini,jambo ambalo liliwachukiza madiwani hao
na kuanza vurugu ndipo Polisi wakaanza kupambana na madiwani hao wa
Ukawa ili kuwatoa nje.
RAIS MPYA WA FIFA NI GIANNI INFANTINO
Gianni Infantino ndiye aliyechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka duniani Fifa
Raia
wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama
rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.katibu huyo mkuu wa Fifa
alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya
mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein
alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa
kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza
kupigwa mjini Zurich.
Infantino akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FIFA
Raundi ya kwanza ya upigaji
kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa mojaWingi wowote wa
kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa
unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri
wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland
,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza
shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya
kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha
miaka sita .
Infantino akiwahutubia wajumbe
Baada ya kutangazwa mshindi,
Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea
kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa’
MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salam Februari 26, 2016.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa dini
wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa dini
wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Elinaza Sendoro baada ya
kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Alex Molasses baada ya
kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es
salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es
salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es
salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAWAZIRI WOTE WAJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao
hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12
leo jioni limetekelezwa.eza agizo hili atakuwa
amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.
TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT UNVEILS PLEDGE FOR PARITY CAMPAIGN
Tanzania
Women of Achievement (TWA) has announced the launch of the Pledge for
Parity Campaign in commemoration of this year’s International Women’s
Day care celebration. The campaign is a clarion call for this year’s
International Women’s Day (IWD) that calls on everyone to take concrete
steps to accelerate the achievement of gender parity in the country. It
also calls on the society to practice gender-balanced leadership,
respect and value differences, develop more inclusive and flexible
cultures and also root out workplace bias.
No comments:
Post a Comment