Afisa wa Mfuko wa PSPF akiwaelemisha wafanyakazi jinsi ya kujiandikisha, kupeleka michango ya hifadhi ya jamii na kufungua madai ya mafao
Christian Gaya, Mwananchi Alhamisi,
Disemba3, 2015
Hifadhi ya jamii imeundwa
kwa ajili ya kuwapatia mfanyakazi ulinzi dhidi ya majanga ya kiuchumi na ya
kijamii yanayosababishwa na kukoma au kupungua kipato kutokana na maradhi,
uzazi, kuumia kazini, ukosefu wa ajira, ulemavu, uzee, kifo na kuongezeka kwa
gharama za matibabu.
Hifadhi ya jamii ni kwa
ajili ya manufaa ya kumkinga mfanyakazi dhidi ya majanga. Na ili kuwepo na
hifadhi ya jamii ambayo ni kinga lazima ichangiwe fedha. Kwa ukweli ni kwamba hifadhi
ya jamii inachangiwa na michango kutoka kwa mwajiri na mfanyakazi pamoja.
Kwa kawaida mfanyakazi ambaye ni mwanachama wa mfuko wa
pensheni hukatwa asilimia 10 ya jumla ya mapato yake yote kwa mwezi na mwajiri
analazimika huchangia asilimia 10 ya mapato yote ya mshahara wa mfanyakazi
hivyo na kufanya kuwa jumla ya asilimia 20 na yote hupelekwa kwenye akaunti ya
mwanachama wa mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii.
Au mwajiri huweza kuchangia asilimia 15 na mwajiriwa
asilimia 5 au asilimia yote 20 inaweza kutolewa na mwajiri kwa mfanyakazi wake
kulingana na makubaliano kama sehemu ya motisha kwa mfanyakazi.
Michango anayochangia
mwajiri ni wazi ya kuwa ni gharama kwa mwajiri, ambapo matokeo yake inaweza kusababisha
kupunguza faida kwa mwajiri. Kadri faida
inavyopungua kwa mwajiri, hii inaweza kusababisha ukuaji wa kuajiri kwa wafanyakazi
kuteremka chini zaidi na hatimaye kusababisha wafanyakazi kupunguzwa au
kuachishwa kazi.
Waajiri pia wanaweza kuwa
na njia mbili zingine za kuchagua kutawanya gharama. Wanaweza kutawanya gharama
zinazoongezeka kama hizi za michango ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya
wafanyakazi wao kwa kuwaongezea ndani ya bei ya huduma au bidhaa za walaji wao.
Hivyo basi, kuongezeka bei ya
bidhaa kwenye masoko ya kimataifa mara nyingi inapunguza ushindani wa bidhaa za
nchi husika,na hata kupunguza ukuaji wa ajira wakati mwingine. Kwa upande
mwingine mwajiri anaweza kuwa na uwezo wa kupunguza mshahara wa mfanyakazi wake.
Hii itategemea na mpangilio
wa soko la ajira lilipo nchini au kwa wafanyakazi kulipizwa makato ya michango
kwa mwajiri wao moja kwa moja kwa kupewa mshahara uliopunguzwa tayari na
mwajiri au kwa njia ya kuwa na ukuaji mdogo wa ajira, au kuwa na nguvukazi
kubwa ambayo haina ajira.
Kwa kawaida wafanyakazi
hupokea mafao wakati wa kustaafu unapowadia, ingawa wao wafanyakazi hulipa kwa
ajili ya haya mafao wakati wanapofanya kazi kwa njia ya kuchangia michango yao
kila mwezi.
Kuongezeka kwa mafao ya
hifadhi ya jamii kwa upande mwingine kunasababisha kuongezeka kwa gharama za kuendesha
mfumo wa hifadhi ya jamii. Kwa hiyo hapa kuna mabadilishano kwa wafanyakazi
kati ya mfumo wa hifadhi ya jamii wenye mafao makubwa yanayovutia na wenye
gharama kubwa na mfumo wa hifadhi ya jamii wenye mafao madogo yasiyovutia na
wenye gharama ndogo.
Mchaguzi na mapangaji wa
mfumo huu mara nyingi hufanywa na serikali kwa kufuata matakwa ya wadau wa
sekta ya hiafadhi ya jamii au wananchi, kwa kupitia mdhibiti na msimamizi wa
sekta ya hifadhi ya jamii mfano kwa hapa Tanzania ni SSRA.
Wafanyakazi wakati mwingine
wanaweza kujisikia ya kuwa wangependelea kutumia fedha zao zaidi wakati wa
miaka ya kufanya au wangali bado wana nguvu za kufanya kazi na waje watumie
kidogo baada ya kustaafu kinyume na utaratibu wa sheria ya sekta ya hifadhi ya
jamii.
Wafanyakazi wa aina hiyo
unakuta wana ari ndogo sana ya kuendelea kufanya kazi kwa miaka yote ya kufanyia
kazi kwenye sekta rasmi.
Wao wangependa kufanya kazi
kwenye sekta isiyo rasmi sehemu ambayo ingewawezesha kupata nafasi nzuri zaidi
kuweza kutumia sehemu kubwa ya mapato yao leo badala ya kuwekeza au kuchangia
kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya kupata pensheni watakapokuwa
hawana nguvukazi kwenye soko la ajira kwa siku sijazo.
Muundo wa gharama na mapato
yalichaguliwa na serikali yanapokuwa ya
juu sana, yanaweza kufanya idadi kubwa ya wafanyakazi kuangukia katika kundi
hili na kufanya kuongezeka kwa kukua kwa sekta isiyo rasmi na ukwepaji wa
kutolipa mchango ya pensheni ya hifadhi ya jamii pia kuongezeka
Jambo la pili ni kwamba
muundo wa mapato na gharama wa sekta ya hifadhi ya jamii kwa hapa Tanzania
unaosimamiwa na SSRA unaweza ukawa hautoi thamani nzuri za mafao kwa
mfanyakazi.
Kwa mfano, kama wafanyakazi
mara kwa mara wanapokea pensheni ndogo zaidi kuliko thamani ya michango
waliyochangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, ni dhahiri ya kwamba
wafanyakazi hao hawawezi kuendelea kuchangia tena.
Ni kweli ya kwamba kila
mfanyakazi hawezi kupata thamani ya michango ile ile kamili aliyochangia. kwa
wale wastaafu waliobahatika kuishi kwa
miaka mingi zaidi ni wazi ya kuwa
watapokea pensheni kubwa zaidi kuliko wale watakao kufa mapema baada ya
kustaafu, hii ni kawaida ya utaratibu wa bima ya pensheni ya hifadhi ya jamii
inavyofanya kazi.
No comments :
Post a Comment