Waziri
Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa China Nchini
Dkt. Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini
Dar es slaam Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Sudan nchini,
Dkt.Yassir Mohamed Ali Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 1,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa Sudan
nchini,Dkt. Yassir Mohamed Ali kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Majaliwa Kassim Majliwa akizungumza na balozi wa Korea nchini Mhe.
Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Desemba 1, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago balozi wa
Korea nchini, Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu
jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
……………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kasim Majaliwa
amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu kutoka nchi za China,
Sudan Kaskazini na Korea Kusini.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na
mabalozi hao leo mchana (Jumanne, Desemba mosi, 2015), ofisini kwake,
Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu aliwashukuru mabalozi hao kwa
pongezi walizokuja kumpatia na kuahidi ushirikiano zaidi pamoja na nchi
hizo.
Kwa upande wake, balozi wa China,
Dk. Lu Youqing alisema Serikali itaendelea kuisaidia Tanzania kwenye
sekta za uendelezaji viwanda, miundombinu, maji, afya na elimu ikiwa ni
ishara kuendeleza mahusiano ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu baina ya
China na Tanzania.
Alisema Tanzania imeteuliwa kuwa
miongoni mwa nchi tatu ambazo zitasaidiwa na China kuendeleza viwanda na
kwamba makubaliano ya mpango huo yatafikiwa kwenye mkutano wa uwekezaji
baina ya China na nchi za Afrika (FOCAC – 6) unaotarajiwa kuanza
Desemba 4, mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Nchi nyingine
mbili zitakazonufaika na mpango huo ni Kenya na Ethiopia.
Naye Balozi wa Sudan Kaskazini.
Dk. Yassir Mohamed Ali alisema nchi yake inao madaktari wengi na kwamba
kumekuwa na majadiliano ya kuona ni jinsi gani wanaweza kuja kuongeza
nguvu kwenye sekta ya afya. “Tuna madaktari wasiopungua 4,000 ambao
wanahitimu kila mwaka na tungependa kushirikiana na Tanzania katika eneo
hili,” alisema.
Naye Balozi wa Korea Kusini, Bw.
Chung Il ambaye pia alitumia fursa hiyo kuja kuagana na Waziri Mkuu
Majaliwa, alisema anatumaini kuona ubalozi wa Tanzania ukifunguliwa
nchini mwao katika muda siyo mrefu.
PINDA AKABIDHI RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MAJALIWA
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkaribisha Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda ambaye Novemba 30,2015 alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kukabidhi Ofisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majliwa Kassim Majliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu,
Mizengo Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi , (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka
aliposoma taarifa kabla ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi Ofisi, kwenye
ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza kabla ya kukabidhi Ofisi kwa
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kwenye ukumbi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akipokea taarifa ya makabidhiano ya
Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuujijini Dar es salaam Novemba 30,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya
makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30,
2015. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka Kikula.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya
makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30,
215. Watatu Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka
Kikula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akifurahia katika mazungumzo na Waziri
Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Dkt. Florence Turuka baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi rasmi Ofisi
ya Waziri kwa Waziri Mkuu Majliwa , kwenye ukumbi wa Ofisiya Waziri
Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
…………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU mstaafu Mizengo Pinda
amekabidhi ofisi kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kumtaka aimarishe
ufuatiliaji wa maelekezo anayoyatoa kwenda ngazi za chini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano
yaliyofanyika jana jioni (Jumatatu, Novemba 30, 2015), kwenye ukumbi wa
mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam, Bw.
Pinda alisema katika kipindi cha uongozi wake kulikuwa na ucheleweshaji
wa kupata majibu kutoka ngazi ya chini katika maelekezo aliyokuwa
akitoa.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na
ina mambo mengi ya kufuatilia. Kama kuna changamoto nilikumbana nayo ni
ucheleweshaji wa majibu kutokana na maagizo niliyokuwa nikitoa. Itabidi
uwe makini sana katika kufuatilia hili,” alisema Waziri Mkuu mstaafu.
Alimtaka ahakikishe kila idara
inakuwa na mpango kazi na kunakuwa na ufuatiliaji wa kila kilichopangwa.
“Pia ninashauri uandaliwe kikao na watu wa Hazina ili wakueleze jinsi
bajeti ya Serikali inavyoandaliwa ili iwe rahisi kwako kufuatilia
vipengele kadhaa vya bajeti ya Serikali pindi maswali yanapoulizwa
bungeni,” alisema.
Pia alimkabidhi taarifa yenye
kurasa 104 ambayo inaelezea majukumu mbalimbali ya taasisi na idara
zilizo chini ya Ofisi wa Waziri Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu ina taasisi
nane, idara nane na vitengo saba. Taasisi hizo ni Msajili wa Vyama vya
Siasa, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Kuratibu na Kudhibiti
UKIMWI (TACAIDS), Tume ya Uchaguzi (NEC) na Mamlaka ya Ustawishaji Makao
Makuu (CDA). Nyingine ni Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC).
Idara zilizopo kwenye ofisi hiyo
ni Utawala na Rasimali watu, Sera na Mipango, Uratibu wa Maadhimisho ya
Kitaifa na Sekta binafsi na Uwezeshaji. Nyingine ni Bunge na Siasa,
uatibu wa shughuli za Serikali, Mpigachapa Mkuu wa Serikali na Ofisi
Binafsi ya Waziri Mkuu.
Alisema pia ameridhishwa na kasi
ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu
wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi wao na uadilifu wao,
anaamini wataweza kuivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati
ambako Serikali imejielekeza kufika.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa alimshukuru Waziri Mkuu mstaafu na kumuahidi kutekeleza
yote yaliyomo kwenye taarifa aliyomkabidhi. Pia aliahidi kusimamia kwa
karibu suala la ufuatiliaji wa maelekezo anayotoa pamoja na yale
yanayotoka ngazi za juu.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na
Katibu Mkuu, Dk. Florens Turuka, Naibu Katibu Mkuu (OWM), Bibi Regina
Kikuli, wakuu wa taasisi zote nane, wakuu wa idara na vitengo vya Ofisi
ya Waziri Mkuu pamoja na Wasaidizi wa Waziri Mkuu walioko ofisi yake
binafsiRAIS DK. SHEIN ATEMBELEA MRADI UIMARISHAJI MRADI WA MAJI SAFI MAKUNDUCHI.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
maji safi (ZAWA) Dkt.Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea
Uimarishaji wa mradi wa maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya
na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa
Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji
safi (ZAWA) Dkt.Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea
Uimarishaji wa mradi wa Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na baadhi ya wanachama cha Mapinduzi na Wananchi wa
Makunduchi wakati alipotembelea Mradi wa Uimarishaji wa Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akifuatana na Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati
Ramadhan Abdalla Shaaban (wa pili kulia) wakati alipotembelea Mradi wa Uimarishaji wa Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi
Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini
Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na
Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman,[Picha na Ikulu.]
PINDA ATOA WITO KUENZI UTAMADUNI
Waziri
Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China
Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa
China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
Mshauri
wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw.
GAO Wei akitoa ufafanuzi wa picha za matukio mbalimbali kwa Waziri Mkuu
mstaafu Mizengo Pinda (katikati) mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu
kufungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo
jijini Dar es Salaam.
Kundi
la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha
China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda
(hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi
wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo
cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya
Kichina mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo
pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo
hicho.
Waziri
Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa
China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
………………………………………………………………………………………
Na Nyakongo Manyama
MAELEZO
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa wito kwa Watanzania kutambua kuenzi na kuutunza utamaduni wetu ikiwemo lugha ya Kiswahili kwani ndiyo utambulisho mkubwa wa nchi yetu.
Mhe. Pinda ametoa wito huo leo jijini Dae es Salaam wakati akifungua kituo cha Utamaduni China nchini. Kituo hicho pekee cha utamaduni Afrika Mashariki kitatoa fursa kwa Watanzania na Wachina kubadilishana utamaduni.
Kwa kutumia kituo hichi, Watanzania wanaweza kuongeza uhusiano kwa vijana wetu hasa wenye umri mdogo kujifunza utamaduni wa China.
“Watanzania tunatakiwa kuutambua, na kuuenzi utamaduni wetu hasa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili badala ya kuona raha kuongea lugha za wageni. Tuongee na tutumie fursa hii ya kituo cha utamaduni kuendeleza utamaduni wetu ,” amesema.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, utamaduni kwa nchi yoyote ni kila kitu ambacho mtu anakua nacho katika maisha ya kila siku.
“Ndio maana taifa lolote linalopuuzia utamaduni wake linajidhalilisha bila kujua,” amesema na kuongeza kuwa, “wenzetu wanaenzi utamaduni wao. Wana ngoma zao za asili na wamekataa kuiga tamaduni za nje hata katika ala za muziki wao zinatokana na asili yao.”
“Ala zao zinatumia Bamboo (mianzi), hata hapa tunazo kule Iringa, sisi pia tunaweza kuitumia kwa mambo mazuri kama haya badala ya kunywea pombe.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel amesema wizara yake itashirikiana na taasisi, au mtu yoyote mwenye lengo la kukuza uatmaduni wetu.
“Wizara itatoa ushirikiano kwa kila mtu au taasisi yenye lengo la kukuza utamaduni wetu kwasababu suala la utamaduni ni jukumu letu sote, kuulinda kwa nguvu zetu zote,” amesema.
Hafla hiyo pia imehudhuliwa na Balozi wa China nchini Dr. Lu Youqing.
MAELEZO
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa wito kwa Watanzania kutambua kuenzi na kuutunza utamaduni wetu ikiwemo lugha ya Kiswahili kwani ndiyo utambulisho mkubwa wa nchi yetu.
Mhe. Pinda ametoa wito huo leo jijini Dae es Salaam wakati akifungua kituo cha Utamaduni China nchini. Kituo hicho pekee cha utamaduni Afrika Mashariki kitatoa fursa kwa Watanzania na Wachina kubadilishana utamaduni.
Kwa kutumia kituo hichi, Watanzania wanaweza kuongeza uhusiano kwa vijana wetu hasa wenye umri mdogo kujifunza utamaduni wa China.
“Watanzania tunatakiwa kuutambua, na kuuenzi utamaduni wetu hasa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili badala ya kuona raha kuongea lugha za wageni. Tuongee na tutumie fursa hii ya kituo cha utamaduni kuendeleza utamaduni wetu ,” amesema.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, utamaduni kwa nchi yoyote ni kila kitu ambacho mtu anakua nacho katika maisha ya kila siku.
“Ndio maana taifa lolote linalopuuzia utamaduni wake linajidhalilisha bila kujua,” amesema na kuongeza kuwa, “wenzetu wanaenzi utamaduni wao. Wana ngoma zao za asili na wamekataa kuiga tamaduni za nje hata katika ala za muziki wao zinatokana na asili yao.”
“Ala zao zinatumia Bamboo (mianzi), hata hapa tunazo kule Iringa, sisi pia tunaweza kuitumia kwa mambo mazuri kama haya badala ya kunywea pombe.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel amesema wizara yake itashirikiana na taasisi, au mtu yoyote mwenye lengo la kukuza uatmaduni wetu.
“Wizara itatoa ushirikiano kwa kila mtu au taasisi yenye lengo la kukuza utamaduni wetu kwasababu suala la utamaduni ni jukumu letu sote, kuulinda kwa nguvu zetu zote,” amesema.
Hafla hiyo pia imehudhuliwa na Balozi wa China nchini Dr. Lu Youqing.
MKUTANO MKUU WA TFF KUFANYIKA TANGA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linatarajia kufanya mkutano wake Mkuu wa
Mwaka kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo
wajumbe wa mkutano huo tayari walishatumiwa taarifa za mkutano.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF,
Kaimu Mkurugenzi wa Sheria na Wachama, Elliud Mvela amesema maandalizi
ya mkutano huo yanaendelea vizuri.
Mvella amesema ajenda za mkutano
mkuu wa kawaida ni zile zilizopo kikatiba, ila itaongezeka ajenda ya
marekebisho ya katiba ambayo ni mapendekezo yaliyotolewa na FIFA.
Agenda za mkutano mkuu ni:
1.Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa Wajumbe
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita.
5. Yatokanayo na Mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Ripoti kutoka kwa Wanachama
8. Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
9. Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013.
10. Kupitisha bajeti ya 2016
11. Marekebisho ya Katiba
12. Mengineyo
13. Kufunga Mkutano.
KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI AFANYA ZIARA TRL
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka akizungumza na waandishi wa
habari wakati alipofanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania
(TRL)ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa shirika hilo linaendana na kasi
yaRais wa awamu ya tano Mh. John Pombe Magufuli.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka akikagua maeneo mbalimbali
wakati alipofanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjakaakikagua karakana ya
Shirika la Reli Tanzania (TRL)wakati alipotembelea shirika hilo leo.
……………………………………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo
DsmKatibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka amefanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL)ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa shirika hilo linaendana na kasi yaRais wa awamu ya tano Mh. John Pombe Magufuli.
Katika ziara hiyo Bw. Mwinjaka alikagua karakana za shirika hilo ili kuona utendaji wake na kusisitiza ukarabati wa mebehewa yaliyobaki kumaliziwa ndani ya siku 30.
Hata hivyo katibu huyo amestushwa na habari ya kuanguka kwa mabehewa 50 ya mafuta yaliyokuwa yanajaribiwa huko Tanga.
“Nimestushwa na taarifa ya kuanguka kwa mabehewa 50 ya mafuta katika majaribio baada ya kujazwa maji ,yangekuwa yana mafuta ingekua hasara kubwa kwa Tanzania hivyo nataka tatizo hilo lishughulikiwe haraka iwezekanavyo kunusuru mabehewa yaliyobaki .”alisema Mwinjaka
Mbali na hayo Bw.Mwinjaka alisema kwamba reli ambazo zimehifadhiwa katika karakana hizo ziondolewe na zikamalizie ujenzi wa reli ambazo hazijaisha kuliko kukaa bila ya matumizi huku kukiwa na shida ya mataaluma hayo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw.Elias Mshana amesema kwamba wapo katika mchakato wa kumalizizia ukarabati wa mabehewa yaliyobaki pamoja na marekebisho ya reli zilizoharibika na mpaka 31 Desemba mwaka huu zitakua zimetengemaa.
“Tunatarajia mpaka tarehe 31 Decemba mwaka huu tutakua tumemaliza kukarabati mabehewa na reli zilizoharibika ili zianze kutumiwa rasmi ili kuleta maendeleo katika Nchi” Alisema Bw. Mshana.
WAFUASI WA NKWERA WAANDAMANA KUOMBEA AMANI YA TAIFA
Wafuasi
wa Kasisi Felician Nkwera chini ya kituo cha Huduma za Maombezi
wameandamana leo jijini Dar es Salaam kumwomba mwenyezi Mungu aendeldee
kuilinda amani ya nchi pamoja na kuombea amani iliyopo iendelee kudumu.
Pichani ni sehemu ya umati
walioandamana kutoke eneo la Tazara mpaka Ubungo jirani na River Side
wakifanya sala, mfululizo wakiwa wamebeba sanamu za bikira Maria,
sakramenti ya ekaristi takatifu na kufukiza ubani kama ilivyo utamaduni
wa kanisa katoliki lililomtenga kasisi huyo miaka mingi iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa uiliyotolewa
na viongozi wa kituo hicho, haya ni matembezi ya sala ya tisa katika
mfululizo wa matembezi ya sala ambayo huduma za maombezi zimekuwa
zikifanywa jijini Dar es Salaam, Mbeya na Sumbawanga tangua
ilipoanzishwa mwaka 1969.
‘Huduma za maombezi ni
utumemaalumwa sala za tiba: yaani uponyaji wa maradhi na kupunga pepo.
Hauna ubaguzi kwa misingi yoyote na ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa
Watanzania na ulimwengu mzima’ Alisema Kasisi Nkwera.
(HABARI KWA HISANI YA http://robertokanda.blogspot.com)
TAMASHA LA ASASI ZA KIRAIA AZAKi 2015 LAFANYIKA UBUNGO PLAZA
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bibi Sihaba
Nkinga akifungua Tamasha la 13 la AZAKi lililoandaliwa na shirika la the
Foundation For Civil Society na kufanyika katika ukumbi wa Hoteli ya
Blue Pearl Ubungo Dar es salaam tarehe 1/12/2015
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bibi Sihaba
Nkinga (mwenye suti ya blue) akiwa akiwa na baadhi ya wadau wa
waliohudhuria Tamasha la 13 la AZAKi lililoandaliwa na shirika la the
Foundation For Civil Society na kufanyika katika ukumbi wa Hoteli ya
Blue Pearl Ubungo Dar es salaam tarehe 1/12/2015.
………………………………………………………………………………………………….
Erasto T. Ching’oro, Msemaji – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Wadau wa Asasi za Kiraia
wamekutana ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Dar es salaam kuanzia tarehe 1-
2/12/2015 kushiriki Tamasha la maonesho ya shughuli zinazotekelezwa na
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Akizindua Tamasha hilo la siku
mbili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Bibi Sihaba Nkinga, ametoa shukrani kwa shirika la the Foundation for
Civil Society kwa kuandaa Tamasha hilo la Kumi na Tatu la mwaka 2015
lenye Kauli Mbiu: ‘Wajibu wa Asasi za Kiraia katika Utekelezaji wa
Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030’.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo yenye
dhamana ya kusimamia na kuratibu shughuli za AZAKi hapa nchini ameeleza
kufurahishwa na wadau wa AZAKi kwa kuendelea kushiriki na kuchangia
katika jitihada za kuleta maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa ushiriki na kauli mbiu ya Tamasha la mwaka 2015 ni
ushahidi tosha kuwa AZAKi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni wabia
muhimu katika maendeleo.
Akimkaribisha mgeni rasimi, Bibi
DKT. Stigmata Tenga ambaye ni Rais wa Foundation for Civil Society
alieleza kuwa malengo ya Tamasha ni Kutoa fursa kwa washiriki kujadili
na kuainisha masuala yatakayozingatiwa na jinsi ya kuimarishsa ushiriki
mpana wa wananchi na Asasi za Kiraia (AZAKi) na kuyapa kipaumbele wakati
wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Aidha, Tamasha hilo
litajenga jukwaa kwa wadau wa AZAKi kujadili namna ambavyo Foundation
for Civil Society itaboresha huduma za kujenga uwezo wa Asasi za Kiraia
nchini kwa kutoa ruzuku na huduma za kuimarisha uwezo wa asasi
kiutendaji na kiutawala.
Tamasha la Azaki linakutanisha
takribani wadau 300 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Bibi Nkinga
amaeleza kuwa fursa hii itatumiwa na wadau kujenga uelewa wa pamoja
kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu na kuweka mikakati ya kukuza
ushiriki katika utekelezaji wa malengo hayo kwa kuzingatia misingi ya
uwazi, uwajibikaji na ushirikishaji wa jamii. Amewaasa wadu kushiriki
katika mchakato wa kuandaa Malengo Mapya ya Maendeleo endelevu ya mwaka
2030 kusaidia kuwafahamisha washiriki wengine mchakato uliotumika
kuandaa Malengo hayo ili wayafahamu na kuyatekeleza kwa lengo la
kufanikisha azma ya kuondoa umasikini kwa kushirikiana na Serikali na
wadau wengine.
MISS TANZANIA USA 2015-2016 AEESHA KAMARA ASHINDA KUWA COVER GIRL KWENYE CALENDA YA MISS AFRICA USA 2015-2016
Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha
Kamara (kushoto) akiibuka mshindi na kuwa Cover Girl kwenye Kalenda ya
Miss Africa USA 2015-2016 shindano ililofanyika New York siku ya
Jumamosi Novemba 28, 2015.
Mamiss wengine walioshiriki shindano hilo wakipita mbele ya majaji.
Wadau wakipata picha na mamiss wakati mratibu wa mashindano ya miss Africa Lady Kate alipokua akitangaza shindi.
Ma Winny Casey (gauni jeusi) pamoja na Lady Kate (mwenye miwani) wakiwa na mamiss.
No comments :
Post a Comment