Pages

Tuesday, December 1, 2015

MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI WA CHINA, KOREA NA SUDAN

lu1

Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es slaam  Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu2 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Sudan nchini, Dkt.Yassir  Mohamed Ali Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu3 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa   akisalimiana na balozi wa Sudan nchini,Dkt. Yassir Mohamed Ali kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu4 
Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majliwa akizungumza na balozi wa Korea nchini Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu5 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago balozi wa Korea nchini, Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kasim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu kutoka nchi za China, Sudan Kaskazini na Korea Kusini.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo mchana (Jumanne, Desemba mosi, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu aliwashukuru mabalozi hao kwa pongezi walizokuja kumpatia na kuahidi ushirikiano zaidi pamoja na nchi hizo.
Kwa upande wake, balozi wa China, Dk. Lu Youqing alisema Serikali itaendelea kuisaidia Tanzania kwenye sekta za uendelezaji viwanda, miundombinu, maji, afya na elimu ikiwa ni ishara kuendeleza mahusiano ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu baina ya China na Tanzania.
Alisema Tanzania imeteuliwa kuwa miongoni mwa nchi tatu ambazo zitasaidiwa na China kuendeleza viwanda na kwamba makubaliano ya mpango huo yatafikiwa kwenye mkutano wa uwekezaji baina ya China na nchi za Afrika (FOCAC – 6) unaotarajiwa kuanza Desemba 4, mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Nchi nyingine mbili zitakazonufaika na mpango huo ni Kenya na Ethiopia.
Naye Balozi wa Sudan Kaskazini. Dk. Yassir Mohamed Ali alisema nchi yake inao madaktari wengi na kwamba kumekuwa na majadiliano ya kuona ni jinsi gani wanaweza kuja kuongeza nguvu kwenye sekta ya afya. “Tuna madaktari wasiopungua 4,000 ambao wanahitimu kila mwaka na tungependa kushirikiana na Tanzania katika eneo hili,” alisema.
Naye Balozi wa Korea Kusini, Bw. Chung Il ambaye pia alitumia fursa hiyo kuja kuagana na Waziri Mkuu Majaliwa, alisema anatumaini kuona ubalozi wa Tanzania ukifunguliwa nchini mwao katika muda siyo mrefu.

PINDA AKABIDHI RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MAJALIWA

pi1 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkaribisha  Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  ambaye Novemba 30,2015 alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kukabidhi Ofisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi2 
Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo  Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi , (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi3 
Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka aliposoma taarifa kabla ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi Ofisi, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi4 
Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda  akizungumza  kabla ya kukabidhi Ofisi kwa  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa,  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi5 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akipokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuujijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
pi6 
Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi7 
Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 215. Watatu Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi8 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akifurahia  katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda  na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri  kwa  Waziri  Mkuu Majliwa , kwenye ukumbi wa Ofisiya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU mstaafu Mizengo Pinda amekabidhi ofisi kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kumtaka aimarishe ufuatiliaji wa maelekezo anayoyatoa kwenda ngazi za chini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika jana jioni (Jumatatu, Novemba 30, 2015), kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam, Bw. Pinda alisema katika kipindi cha uongozi wake kulikuwa na ucheleweshaji wa kupata majibu kutoka ngazi ya chini katika maelekezo aliyokuwa akitoa.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na ina mambo mengi ya kufuatilia. Kama kuna changamoto nilikumbana nayo ni ucheleweshaji wa majibu kutokana na maagizo niliyokuwa nikitoa. Itabidi uwe makini sana katika kufuatilia hili,” alisema Waziri Mkuu mstaafu.
Alimtaka ahakikishe kila idara inakuwa na mpango kazi na kunakuwa na ufuatiliaji wa kila kilichopangwa. “Pia ninashauri uandaliwe kikao na watu wa Hazina ili wakueleze jinsi bajeti ya Serikali inavyoandaliwa ili iwe rahisi kwako kufuatilia vipengele kadhaa vya bajeti ya Serikali pindi maswali yanapoulizwa bungeni,” alisema.
Pia alimkabidhi taarifa yenye kurasa 104 ambayo inaelezea majukumu mbalimbali ya taasisi na idara zilizo chini ya Ofisi wa Waziri Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu ina taasisi nane, idara nane na vitengo saba. Taasisi hizo ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Kuratibu na Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Tume ya Uchaguzi (NEC) na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA). Nyingine ni Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Idara zilizopo kwenye ofisi hiyo ni Utawala na Rasimali watu, Sera na Mipango, Uratibu wa Maadhimisho ya Kitaifa na Sekta binafsi na Uwezeshaji. Nyingine ni Bunge na Siasa, uatibu wa shughuli za Serikali, Mpigachapa Mkuu wa Serikali na Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu.
Alisema pia ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi wao na uadilifu wao,  anaamini wataweza kuivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati ambako Serikali imejielekeza kufika.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimshukuru Waziri Mkuu mstaafu na kumuahidi kutekeleza yote yaliyomo kwenye taarifa aliyomkabidhi. Pia aliahidi kusimamia kwa karibu suala la ufuatiliaji wa maelekezo anayotoa pamoja na yale yanayotoka ngazi za juu.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Dk. Florens Turuka, Naibu Katibu Mkuu (OWM), Bibi Regina Kikuli, wakuu wa taasisi zote nane, wakuu wa idara na vitengo vya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wasaidizi wa Waziri Mkuu walioko ofisi yake binafsi

RAIS DK. SHEIN ATEMBELEA MRADI UIMARISHAJI MRADI WA MAJI SAFI MAKUNDUCHI.

sei1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji safi (ZAWA) Dkt.Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea Uimarishaji wa mradi wa maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
sei2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji safi (ZAWA) Dkt.Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea Uimarishaji wa mradi wa Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
sei3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na baadhi ya wanachama cha Mapinduzi na Wananchi wa Makunduchi wakati  alipotembelea Mradi wa Uimarishaji wa  Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja,[Picha na Ikulu.]
sei4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban (wa pili kulia) wakati alipotembelea Mradi wa Uimarishaji wa  Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman,[Picha na Ikulu.]

PINDA ATOA WITO KUENZI UTAMADUNI

miz1 
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
miz2 
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei akitoa ufafanuzi wa picha za matukio mbalimbali kwa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kufungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
miz3 
Kundi la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.
miz4 
Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya Kichina mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
miz5 
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
………………………………………………………………………………………
Na Nyakongo Manyama
MAELEZO
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa wito kwa Watanzania kutambua kuenzi na kuutunza utamaduni wetu ikiwemo lugha ya Kiswahili kwani ndiyo utambulisho mkubwa wa nchi yetu.
Mhe. Pinda ametoa wito huo leo jijini Dae es Salaam wakati akifungua kituo cha Utamaduni China nchini. Kituo hicho pekee cha utamaduni Afrika Mashariki kitatoa fursa kwa Watanzania na Wachina kubadilishana utamaduni.
Kwa kutumia kituo hichi, Watanzania wanaweza kuongeza uhusiano kwa vijana wetu hasa wenye umri mdogo kujifunza utamaduni wa China.
“Watanzania tunatakiwa kuutambua, na kuuenzi utamaduni wetu hasa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili badala ya kuona raha kuongea lugha za wageni. Tuongee na tutumie fursa hii ya kituo cha utamaduni kuendeleza utamaduni wetu ,” amesema.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, utamaduni kwa nchi yoyote ni kila kitu ambacho mtu anakua nacho katika maisha ya kila siku.
“Ndio maana taifa lolote linalopuuzia utamaduni wake linajidhalilisha bila kujua,” amesema na kuongeza kuwa, “wenzetu wanaenzi utamaduni wao. Wana ngoma zao za asili na wamekataa kuiga tamaduni za nje hata katika ala za muziki wao zinatokana na asili yao.”
“Ala zao zinatumia Bamboo (mianzi), hata hapa tunazo kule Iringa, sisi pia tunaweza kuitumia kwa mambo mazuri kama haya badala ya kunywea pombe.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel amesema wizara yake itashirikiana na taasisi, au mtu yoyote mwenye lengo la kukuza uatmaduni wetu.
“Wizara itatoa ushirikiano kwa kila mtu au taasisi yenye lengo la kukuza utamaduni wetu kwasababu suala la utamaduni ni jukumu letu sote, kuulinda kwa nguvu zetu zote,” amesema.
Hafla hiyo pia imehudhuliwa na Balozi wa China nchini Dr. Lu Youqing.
.

MKUTANO MKUU WA TFF KUFANYIKA TANGA

gs 
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linatarajia kufanya mkutano wake Mkuu wa Mwaka kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo wajumbe wa mkutano huo tayari walishatumiwa taarifa za mkutano.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF, Kaimu Mkurugenzi wa Sheria na Wachama, Elliud Mvela amesema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri.
Mvella amesema ajenda za mkutano mkuu wa kawaida ni zile zilizopo kikatiba, ila itaongezeka ajenda ya marekebisho ya katiba ambayo ni mapendekezo yaliyotolewa na FIFA.
Agenda za mkutano mkuu ni:
1.Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa Wajumbe
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita.
5. Yatokanayo na Mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Ripoti kutoka kwa Wanachama
8. Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
 9. Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013.
10. Kupitisha bajeti ya 2016
11. Marekebisho ya Katiba
12. Mengineyo
13. Kufunga Mkutano.

KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI AFANYA ZIARA TRL

mp2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya  ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL)ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa shirika hilo linaendana na kasi yaRais wa awamu ya tano Mh. John Pombe Magufuli.
mp4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka akikagua maeneo mbalimbali wakati alipofanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL).
MP5 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjakaakikagua karakana ya  Shirika la Reli Tanzania (TRL)wakati alipotembelea shirika hilo leo.
……………………………………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo
Dsm
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka amefanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL)ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa shirika hilo linaendana na kasi yaRais wa awamu ya tano Mh. John Pombe Magufuli.
Katika ziara hiyo Bw. Mwinjaka alikagua karakana za shirika hilo ili kuona utendaji wake na kusisitiza ukarabati wa mebehewa yaliyobaki kumaliziwa ndani ya siku 30.
Hata hivyo katibu huyo amestushwa na habari ya kuanguka kwa mabehewa 50 ya mafuta yaliyokuwa yanajaribiwa huko Tanga.
“Nimestushwa na taarifa ya kuanguka kwa mabehewa 50 ya mafuta katika majaribio baada ya kujazwa maji ,yangekuwa yana mafuta ingekua hasara kubwa kwa Tanzania hivyo nataka tatizo hilo lishughulikiwe haraka iwezekanavyo kunusuru mabehewa yaliyobaki .”alisema Mwinjaka
Mbali na hayo Bw.Mwinjaka alisema kwamba reli ambazo zimehifadhiwa katika karakana hizo ziondolewe na zikamalizie ujenzi wa reli ambazo hazijaisha kuliko kukaa bila ya matumizi huku kukiwa na shida ya mataaluma hayo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw.Elias Mshana amesema kwamba wapo katika mchakato wa kumalizizia ukarabati wa mabehewa yaliyobaki pamoja na marekebisho ya reli zilizoharibika na mpaka 31 Desemba mwaka huu zitakua zimetengemaa.
“Tunatarajia mpaka tarehe 31 Decemba mwaka huu tutakua tumemaliza kukarabati mabehewa na reli zilizoharibika ili zianze kutumiwa rasmi ili kuleta maendeleo katika Nchi” Alisema Bw. Mshana.

WAFUASI WA NKWERA WAANDAMANA KUOMBEA AMANI YA TAIFA

KN4 KN3 KN1 
Wafuasi wa Kasisi Felician Nkwera chini ya kituo cha Huduma za Maombezi wameandamana leo jijini Dar es Salaam kumwomba mwenyezi Mungu aendeldee kuilinda amani ya nchi pamoja na kuombea amani iliyopo iendelee kudumu.
Pichani ni sehemu ya umati walioandamana kutoke eneo la Tazara mpaka Ubungo jirani na River Side wakifanya sala, mfululizo wakiwa wamebeba sanamu za bikira Maria, sakramenti ya ekaristi takatifu na kufukiza ubani kama ilivyo utamaduni wa kanisa katoliki lililomtenga kasisi huyo miaka mingi iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa uiliyotolewa na viongozi wa kituo hicho, haya ni matembezi ya sala ya tisa katika mfululizo wa matembezi ya sala ambayo huduma za maombezi zimekuwa zikifanywa jijini Dar es Salaam, Mbeya na Sumbawanga tangua ilipoanzishwa mwaka 1969.
‘Huduma za maombezi ni utumemaalumwa sala za tiba: yaani uponyaji wa maradhi na kupunga pepo. Hauna ubaguzi kwa misingi yoyote na ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa Watanzania na ulimwengu mzima’ Alisema Kasisi Nkwera. 

TAMASHA LA ASASI ZA KIRAIA AZAKi 2015 LAFANYIKA UBUNGO PLAZA

AZ1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akifungua Tamasha la 13 la AZAKi lililoandaliwa na shirika la the Foundation For Civil Society na kufanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es salaam tarehe 1/12/2015
AZ2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (mwenye suti ya blue) akiwa akiwa na baadhi ya wadau wa waliohudhuria Tamasha la 13 la AZAKi lililoandaliwa na shirika la the Foundation For Civil Society na kufanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es salaam tarehe 1/12/2015.
………………………………………………………………………………………………….
Erasto T. Ching’oro, Msemaji – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Wadau wa Asasi za Kiraia wamekutana ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Dar es salaam kuanzia tarehe 1- 2/12/2015 kushiriki Tamasha la maonesho ya shughuli zinazotekelezwa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Akizindua Tamasha hilo la siku mbili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bibi Sihaba Nkinga, ametoa shukrani kwa shirika la the Foundation for Civil Society kwa kuandaa Tamasha hilo la Kumi na Tatu la mwaka 2015 lenye Kauli Mbiu: ‘Wajibu wa Asasi za Kiraia katika Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030’.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo yenye dhamana ya kusimamia na kuratibu shughuli za AZAKi hapa nchini ameeleza kufurahishwa na wadau wa AZAKi kwa kuendelea kushiriki na kuchangia katika jitihada za kuleta maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Ameongeza kuwa ushiriki na kauli mbiu ya Tamasha la mwaka 2015 ni ushahidi tosha kuwa AZAKi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni wabia muhimu katika maendeleo.
Akimkaribisha mgeni rasimi, Bibi DKT. Stigmata Tenga ambaye ni Rais wa Foundation for Civil Society alieleza kuwa malengo ya Tamasha ni Kutoa fursa kwa washiriki kujadili na kuainisha masuala yatakayozingatiwa na jinsi ya kuimarishsa ushiriki mpana wa wananchi na Asasi za Kiraia (AZAKi) na kuyapa kipaumbele wakati wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Aidha, Tamasha hilo litajenga jukwaa kwa wadau wa AZAKi kujadili namna ambavyo Foundation for Civil Society itaboresha huduma za kujenga uwezo wa Asasi za Kiraia nchini kwa kutoa ruzuku na huduma za kuimarisha uwezo wa asasi kiutendaji na kiutawala.
Tamasha la Azaki linakutanisha takribani wadau 300 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Bibi Nkinga amaeleza kuwa fursa hii itatumiwa na wadau kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu na kuweka mikakati ya kukuza ushiriki katika utekelezaji wa malengo hayo kwa kuzingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji na ushirikishaji wa jamii. Amewaasa wadu kushiriki katika mchakato wa kuandaa Malengo Mapya ya Maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kusaidia kuwafahamisha washiriki wengine mchakato uliotumika kuandaa Malengo hayo ili wayafahamu na kuyatekeleza kwa lengo la kufanikisha azma ya kuondoa umasikini kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine.

MISS TANZANIA USA 2015-2016 AEESHA KAMARA ASHINDA KUWA COVER GIRL KWENYE CALENDA YA MISS AFRICA USA 2015-2016

 Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara (kushoto) akiibuka mshindi na kuwa Cover Girl kwenye Kalenda ya Miss Africa USA 2015-2016 shindano ililofanyika New York siku ya Jumamosi Novemba 28, 2015.
 Mamiss wengine walioshiriki shindano hilo wakipita mbele ya majaji.
 Wadau wakipata picha na mamiss wakati mratibu wa mashindano ya miss Africa Lady Kate alipokua akitangaza shindi.
Ma Winny Casey (gauni jeusi) pamoja na Lady Kate (mwenye miwani) wakiwa na mamiss.

No comments:

Post a Comment