Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Ngao ya
ushindi ya uchangiaji bora wa michango ya pensheni Bw.Rajab Abdalla Meneja wa
rasilimali watu wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakati wa utoaji wa zawadi
kwa mashirika ya Umma yaliyochangia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Zanzibar
(ZSSF) kwa wakati muafaka wakati wa
mkutano mkuu wa kwanza wa wanachama na wadau, wa katikati ni Mwenyekiti wa Bodi
ya ZSSF Dkt,Suleiman Rashid.
Mfumo wa hifadhi ya jamii ambayo ni
ya lazima kisheria ambayo wafanyakazi pamoja na mwajiri wanachangia pamoja na
kupeleka michango kwenye chombo cha mfuko wa pensheni, ingawa inatatoa mipango
mengine ya hifadhi ya jamii kwa mfumo wa hiari kama mafao ya ziada.
Hata watu binafsi waliojiajiri
wenyewe, sehemu yoyote ya shughuli kama mwajiri mlipa michango wanatakiwa
kujiandikisha kisheria na kuwa waajiri wachangiaji mara tu anapoanza shughuli
zao.
Viongozi wa chama cha wafanyakazi
kazini wana wajibu wa kumkumbusha mwajiri mara kwa mara ya kuhakikisha ya kuwa
anawasilisha michango sahihi ya kila mfanyakazi yaani mwanachama kwa wakati
muafaka na kupata taarifa ya michango yake ya kila mwezi kutoka mfuko mhusika anayokatwa
kama haki yake kisheria.
Jukumu la kuhakikisha ya kuwa michango
ya wanachama inalipwa kwa wakati muafaka ni la mwajiri mwenyewe na wafanyakazi
wake. Hata hivyo ili kuhakikisha waajiri na wanachama wanajiandikisha na kulipa
michango kwa wakati mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuwa na wakaguzi kwa
ajili ya kufanya kaguzi kwa waajiri kila mara inapobidi
Mpaka sasa
idadi kubwa ya nguvukazi ndiyo inayojitoa kwa kuondoa michango yao kabla haijaifa
na kwenda kinyume na malengo ya hifadhi ya jamii ambalo ni kumwezesha mwananchi kuishi maisha yenye staha kwa
kuwawezesha kupata huduma za msingi pale wanapokuwa hawana kipato kutokana na
sababu mbalimbali zinatokana na uzee, kifo, ugonjwa, uzazi n.k.
Cha kushangaza ni pale waajiri
wanaposhindwa kupeleka michango ya wafanyakazi wao ambao ni wanachama wa mifuko
hii kwa wakati muafaka, ingawa sheria za mifuko zimepewa mamlaka makubwa
kisheria kuwataka waajiri kuwakilisha michango ya wanachama wa mifuko ndani ya
mwezi mmoja mara tu baada ya kukatwa kila mwezi unaofuata.
Kwa maana ya kwamba waajiri wamepewa
kuchelewesha michango muda wa mwezi mmoja. Na wakichelewesha zaidi ya mwezi huo
mmoja michango hiyo inavutia adhabu ya asilimia 5 ya kila mchango uliotakiwa
kupelekwa kwenye mfuko.
Mifuko inafanya hivyo kwa sababu
kisheria michango mara tu ya kukusanywa inatakiwa kuwekezwa kwenye vitega
uchumi vya muda mfupi au mrefu na faida inayotokana na vitega uchumi vya
michango hugawiwa wanachama kulingana na idadi ya michango yake kila mwaka na kuchangia kwa ajili ya uendeshaji wa
ufuatiliaji wa mara kwa mara hiyo michango kwa waajiri.
Na waajiri wasipolipa hiyo adhabu ni
nani atakayewalipia faida ya kila mwaka ambayo wanachama mara nyingi wanadai
kupatiwa maelezo ya hesabu zao kila mwezi inayoonyesha idadi ya michango
aliyochangiwa pamoja na faida iliyoingizwa kwa mwaka
Idadi ya waajiri ambao hawalipi
michango ya wanachama wa mifuko hii ya pensheni kila siku inaongezeka pamoja na
mifuko kuwa na wakaguzi ambao kisheria wamepewa nguvu kubwa kisheria kuingia
mahali popote kuchunguza, kuwaelemisha, kuandikisha waajiri kuwa wachangiaji wa
mifuko ya pensheni, kukusanya michango na kuwakumbusha waajiri wajibu wao
Sheria inasema waajiri wanaweza
kufunguliwa kesi za madai au za jinai pale mazingira yanaporuhusu ya kuweza
kuokoa michango ya wanachama. Sheria inaruhusu kukamata na kuuza mali
inayohamishika au isiyohamishaka au kumfilisi mwajiri ili kupata michango ya wafanyakazi
wake ambao ni wanachama wa mifuko. Sheria inasema hata hivyo mwajiri
atakapopatikana na hatia anaweza kutozwa faini na kufungwa kwa miaka mitatu
jela
Hivyo hata kwa upande ukusanyaji wa
michango wa wanachama lazima wakae mezani pamoja kwa majadiliano kwa kueleza
sababu za kutolipa michango ya wafanyakazi wake kwa kwenda hatua kwa hatua
ambapo huenda wanaweza sasa kufikia mahali ambapo inabidi utumie nguvu za
kisheria pale ambapo mwajiri atakuwa ameshidwa kutekeleza kama walivyokubaliana.
Lakini cha kusikitisha ni kwamba hata ile asilimia 10 au 5 mwajiri aliyokata
kwenye mshahara wa mfanyakazi nayo unakuta
mwajiri anashidwa kulipa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.
Kwa kawaida mara nyingi waajiri
wanatoa sababu zinazolingana zinazowafanya wasipeleke michango ya wafanyakazi
wao mfano atakwambia ya kuwa hali ya kampuni kiuzalishaji kutokana na uhaba na
gharama za vipuli na mali ghafi kutoka nje, kwa kupanda kwa mfumuko wa bei na
riba za mikopo, na kutokana kuwa na ushindani mkubwa sokoni.
Itaendelea wiki ijayo
No comments :
Post a Comment