Pages

Thursday, November 19, 2015

Wajibu wa waajiri kuwasilisha michango mifuko ya penshe







Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Ngao ya ushindi ya uchangiaji bora wa michango ya pensheni Bw.Rajab Abdalla Meneja wa rasilimali watu wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakati wa utoaji wa zawadi kwa mashirika ya Umma yaliyochangia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Zanzibar (ZSSF)  kwa wakati muafaka wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanachama na wadau, wa katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF Dkt,Suleiman Rashid.

Mfumo wa hifadhi ya jamii ambayo ni ya lazima kisheria ambayo wafanyakazi pamoja na mwajiri wanachangia pamoja na kupeleka michango kwenye chombo cha mfuko wa pensheni, ingawa inatatoa mipango mengine ya hifadhi ya jamii kwa mfumo wa hiari kama mafao ya ziada.

Waajiri wanaohusika kisheria kuandikishwa katika mfumo pensheni wa mifuko ya hifadhi jamii ni waajiri wote walio katika sekta binafsi, taasisi zisizokuwa za kiserikali, ofisi za kibalozi zinazoajiri watanzania, taasisi za kimataifa zinazofanya shughuli ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, taasisi za wizara za serikali zinazoajiri wafanyakazi kwa masharti ya muda, mashirika ya umma yanayoajiri wafanyakazi kwa mashari ya muda.

Hata watu binafsi waliojiajiri wenyewe, sehemu yoyote ya shughuli kama mwajiri mlipa michango wanatakiwa kujiandikisha kisheria na kuwa waajiri wachangiaji mara tu anapoanza shughuli zao. 

Viongozi wa chama cha wafanyakazi kazini wana wajibu wa kumkumbusha mwajiri mara kwa mara ya kuhakikisha ya kuwa anawasilisha michango sahihi ya kila mfanyakazi yaani mwanachama kwa wakati muafaka na kupata taarifa ya michango yake ya kila mwezi kutoka mfuko mhusika anayokatwa kama haki yake kisheria.

Jukumu la kuhakikisha ya kuwa michango ya wanachama inalipwa kwa wakati muafaka ni la mwajiri mwenyewe na wafanyakazi wake. Hata hivyo ili kuhakikisha waajiri na wanachama wanajiandikisha na kulipa michango kwa wakati mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuwa na wakaguzi kwa ajili ya kufanya kaguzi kwa waajiri kila mara inapobidi 

Mpaka sasa idadi kubwa ya nguvukazi ndiyo inayojitoa kwa kuondoa michango yao kabla haijaifa na kwenda kinyume na malengo ya hifadhi ya jamii ambalo ni kumwezesha mwananchi kuishi maisha yenye staha kwa kuwawezesha kupata huduma za msingi pale wanapokuwa hawana kipato kutokana na sababu mbalimbali zinatokana na uzee, kifo, ugonjwa, uzazi n.k.

Cha kushangaza ni pale waajiri wanaposhindwa kupeleka michango ya wafanyakazi wao ambao ni wanachama wa mifuko hii kwa wakati muafaka, ingawa sheria za mifuko zimepewa mamlaka makubwa kisheria kuwataka waajiri kuwakilisha michango ya wanachama wa mifuko ndani ya mwezi mmoja mara tu baada ya kukatwa kila mwezi unaofuata. 

Kwa maana ya kwamba waajiri wamepewa kuchelewesha michango muda wa mwezi mmoja. Na wakichelewesha zaidi ya mwezi huo mmoja michango hiyo inavutia adhabu ya asilimia 5 ya kila mchango uliotakiwa kupelekwa kwenye mfuko.

Mifuko inafanya hivyo kwa sababu kisheria michango mara tu ya kukusanywa inatakiwa kuwekezwa kwenye vitega uchumi vya muda mfupi au mrefu na faida inayotokana na vitega uchumi vya michango hugawiwa wanachama kulingana na idadi ya michango yake kila mwaka  na kuchangia kwa ajili ya uendeshaji wa ufuatiliaji wa mara kwa mara hiyo michango kwa waajiri.

Na waajiri wasipolipa hiyo adhabu ni nani atakayewalipia faida ya kila mwaka ambayo wanachama mara nyingi wanadai kupatiwa maelezo ya hesabu zao kila mwezi inayoonyesha idadi ya michango aliyochangiwa pamoja na faida iliyoingizwa kwa mwaka

Idadi ya waajiri ambao hawalipi michango ya wanachama wa mifuko hii ya pensheni kila siku inaongezeka pamoja na mifuko kuwa na wakaguzi ambao kisheria wamepewa nguvu kubwa kisheria kuingia mahali popote kuchunguza, kuwaelemisha, kuandikisha waajiri kuwa wachangiaji wa mifuko ya pensheni, kukusanya michango na kuwakumbusha waajiri wajibu wao

Sheria inasema waajiri wanaweza kufunguliwa kesi za madai au za jinai pale mazingira yanaporuhusu ya kuweza kuokoa michango ya wanachama. Sheria inaruhusu kukamata na kuuza mali inayohamishika au isiyohamishaka au kumfilisi mwajiri ili kupata michango ya wafanyakazi wake ambao ni wanachama wa mifuko. Sheria inasema hata hivyo mwajiri atakapopatikana na hatia anaweza kutozwa faini na kufungwa kwa miaka mitatu jela

Hivyo hata kwa upande ukusanyaji wa michango wa wanachama lazima wakae mezani pamoja kwa majadiliano kwa kueleza sababu za kutolipa michango ya wafanyakazi wake kwa kwenda hatua kwa hatua ambapo huenda wanaweza sasa kufikia mahali ambapo inabidi utumie nguvu za kisheria pale ambapo mwajiri atakuwa ameshidwa kutekeleza kama walivyokubaliana. Lakini cha kusikitisha ni kwamba hata ile asilimia 10 au 5 mwajiri aliyokata kwenye mshahara wa mfanyakazi nayo unakuta  mwajiri anashidwa kulipa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii. 

Kwa kawaida mara nyingi waajiri wanatoa sababu zinazolingana zinazowafanya wasipeleke michango ya wafanyakazi wao mfano atakwambia ya kuwa hali ya kampuni kiuzalishaji kutokana na uhaba na gharama za vipuli na mali ghafi kutoka nje, kwa kupanda kwa mfumuko wa bei na riba za mikopo, na kutokana kuwa na ushindani mkubwa sokoni. 
Itaendelea wiki ijayo

No comments:

Post a Comment