Monday, November 23, 2015

SIKUKUU YA UHURU KUSHEREHEKEWA KWA KUFANYA KAZI, Rais Magufuli.

magufuli1 
Kwa mujibu wa  Sheria ya Sikukuu za Kitaifa  (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike  kwa kufanya kazi.  Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu  (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu.  Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.
Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi,  fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.
Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo,   sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015

Balozi Sefue awaasa watumishi wa umma kuwajibika

OM1\
Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Bw Silasi David mmoja ya wagonjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI.
OM2
Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue akizungumza na mmoja ya wagomjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI Bw. Muhusin Hamiri.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Watumishi wa umma wametakiwa kutumia muda wa kazi kuhudumia wananchi na sio kufanya kazi zao binafsi kwa kutumia ofisi na vifaa vya serikali.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya Hospitali kwa kukagua vifaa tiba na  kuongea na watendaji wakuu wa hospitali hiyo.
Balozi Sefue ameongeza kuwa  watumishi wa umma wanapaswa  kufanya kazi kwa kutoa huduma bora na kwa upendo kwa wananchi  kwani moja ya kanuni na taratibu za mtumishi wa umma ni kumhudumia mteja pasipo upendeleo.
“kwa upande wa madaktari na watoa huduma za afya mnatakiwa kutoa huduma bora na
zenye upendo  kwa wananchi ili nao wajione wanahaki ya kupatiwa huduma hiyo”.
“kwa watumishi wote wa umma tukijitambua kuwa sisi ni watumishi wa umma tutafanya kazi kwa bidii na kwa kujituma” alifafanua Balozi Sefue.
ia muda wa kuingia na wa kutoka ofisini na pia kujipima ni nini amefanya ndani ya masaa nane katika kuhudumia wananchi.
“Hizi si nguvu za soda ni lazima kubadilika pindi tunapowahudumia wateja kwa wakati na kwa ufanisi” alisema Balozi Sefue.
Kadhalika katika kuhakikisha serikali inatoa huduma bora kwa wananchi Balozi sefue ameagiza katika kila ofisi itoayo huduma kuwe na dawati la msaada kwa wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.

KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI

SEF1
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
SEF2
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
SEF3
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
SEF4
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
SEF5
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………
Katibu  Mkuu  Kiongozi  Balozi Ombeni  Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema  amekagua mashine za MRI na CT-SCAN  na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
Pia,  amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya Tehama  na kuwa na maduka yao ya ndani.
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando  na  watendaji wa MNH  ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

MAJALIWA AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE NA KUJITAMBULISHA

JA1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea shada la maua kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Savera Kazaura (kulia) Baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA2
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kuingia  ofisini kwake , Magogoni jijini Dar es salaam, Novemba 23, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Tiruka.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA3
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA4
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA5
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka ambaye alitoa taarifa ya jumla kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Waziri Mkuu kuwasili Ofisini na kujitambulisha kwa watumishi wa Ofisi yake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA6
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada tu ya kuwasili ofisni Novemba 23, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA7
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  na  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA8
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Dkt Florence Turuka  baada ya kuwasili Ofisini Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA9
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  na  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue  jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.
Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.
Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.

TANZANIA YACHAGULIWA NA UNESCO KUWA MJUMBE WA KAMATI YA URITHI WA DUNIA


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na Waandishi wa Habari (hawako pichani) leo tarehe 23/11/2015 katika Ofisi za Wizara hiyo ambapo amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kwa kipindi cha miaka minne. Uchaguzi huo umefuatia uamuzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaohusu Urithi wa Dunia uliofanyika mjini Paris, Ufaransa tarehe 18-20 Novemba 2015. (Habari Kamili SOMA TAARIFA KWA UMMA HAPO CHINI)
 
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Tanzania kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia. Alieleza kuwa katika Kamati hiyo Tanzania itawakilishwa na Bw. Donatius Makamba ambaye ni Mkurugugenzi Idara ya Mambo ya Kale Wizara ya Maliasili na Utalii akisaidiwa na Dkt. James Wakibara, Mwikolojia Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) na Dkt. Mohammed Juma, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji kutoka Zanzibar.
 Bi. Eliwasa Maro Mkurugenzi Msaidizi Utafiti Mafunzo na Takwimu Wizara ya Maliasili na Utalii akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika Mkutano huo na Waandishi wa Habari.
 Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakinukuu baadhi ya mambo muhimu.
 (Na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii)

TANAPA receive anti-poaching aircraft from Germany

ta1
1. Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier (right) handing over a symbolic key of a light Husky aircraft for anti-poaching operations to Director General of TANAPA Allan Kijazi. Others in the picture from left are Director of Wildlife Herman Keraryo and Acting Director General of Tanzania Wildlife Authority Martin Loibooki.
ta2
 Director General of TANAPA Allan Kijazi making a brief presentation about TANAPA to Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier during the handing over event of two surveillance aircrafts from Germany to Tanzania yesterday.
ta3
 Director General of TANAPA Allan Kijazi presenting some of the souvenirs of TANAPA to Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier.
ta4
5. Germany Ambassador to Tanzania Hon. Egon Kochanke (right) and the Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation Ambassador Liberata Mulamula during the event.
ta5
Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier (second right) posed in a group picture with some of the Germany Members of Parliament who accompanied him during the handing over event of two surveillance aircrafts from Germany to Tanzania yesterday.
ta6
 Director General of TANAPA Allan Kijazi speaking with media during the event.
TA7
Some of the invitees during the handing over event. From left to right are Arusha Regional Administrative Secretary Mr. Mapunda, African Wildlife Foundation Country Director John Saleh and TANAPA’s Director of Tourism and Marketing Ibrahim Mussa.
…………………………………………………………………………………….
Germany Foreign Minister Frank-Walter Steinmeier yesterday handed over symbolic key of two Husky aircrafts to Tanzania National Parks and Tanzania Wildlife Authority respectively. The aircrafts will be used for anti-poaching operations in the protected areas.
Director General of TANAPA Allan Kijazi said that the aircrafts would take the joint approach by the Germany Government through Frankfurt Zoological Society, TANAPA and TAWA to tackle poaching in the protected areas.
The Husky A-1C is an ideal plane for monitoring and anti-poaching surveys as it operates at low heights and slow speeds-similar to that of a helicopter and has proven long-term success rate for its use in finding poacher camps and recording GPS positions for follow-up actions by teams on the grounds.
The Huskies will be used to monitor two of Tanzania’s elephant hotspots, Selous Game Reserve and Serengeti National Park.
Tanzania is home to some of the most elephant and rhino populations on the planet but of recent days it has experienced a severe threat from a massive upsurge in poaching.
Issued by Corporate Communications Department
Tanzania National Parks
23rd November, 2015
T: 027 250 1933
E: dg@tanzaniaparks.com
W: www.tanzaniaprks.com

BIMA YA AFYA NHIF YAKANUSHA KUDAIWA NA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA

Na Mwandishi wetu,Dar es salaam
 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini umekanusha kuwepo kwa madai yaliyotolewa na Hospital ya Rufaa  Mkoani Mbeya kuwa  wanaudai Mfuko jumla ya shilingi bilioni 2 na kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni, 2015.
Akizungumza jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  Ndugu Michael Mhando amesema madai yaliyotolewa na Hospital hiyo ya Rufaa Mkoa wa Mbeya  hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo  unalipa madai baada ya mtoa huduma kuwasilisha kwenye Mfuko.
Amesema madai   ya mwisho ya Hospitali hiyo kulipwa ni ya mwezi Agosti, 2015. Madai ya mwezi Septemba, 2015 yamewasilishwa kwenye Mfuko tarehe 4/11/2015 ambayo mpaka sasa yana siku 15 tu. Kwa hiyo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya tumewalipa madai yao yote na kwa mwaka huu wa 2015 kuanzia Januari hadi Agosti 2015 tumewalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3.
Madai mengi ambayo yamekuwa yakiwasilishwa kwao yamegubikwa na udanganyifu mkubwa hali inayowafanya kuchukua muda mrefu katika uhakiki wake ikiwemo kuwapigia simu wagonjwa waliopewa huduma za matibabu.
Aidha Mhando amesema mfuko huo unatoa onyo kali kwa watoa huduma ambao wamekuwa bado wakijihusisha na udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa haitawaonea haya kuwafutia usajili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Amesema Mfuko pia unazidi kutoa rai kwa watoa huduma kutumia fursa zinazotolewa na Mfuko katika kuhakikisha huduma za matibabu zinaboreshwa kwa wanachama na Watanzania kwa ujumla.
 Wakati huo Kaimu mkurugenzi huyo amesema Katika kipindi hiki, baadhi ya watoa huduma wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali za kushindwa kutoa huduma nzuri ama za kuridhisha kwa wanachama wao  na wananchi kwa ujumla kwa kisingizio cha kukosa fedha hali inayosababisha kukosa dawa, kukosa vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kushindwa kuboresha mazingira ya vituo.
Watoa huduma hao wanadai hayo ama wanatoa visingizio vya kukwama huduma katika maeneo yao kutokana na NHIF kuchelewa kulipa fedha fedha za madai ambayo wametibia wanachama wake.
Amesema taarifa  hizo zinajenga mazingira kuwa NHIF ni kikwazo katika ufanisi wa vituo hivyo jambo ambalo si la kweli na limebeba taswira ya kuleta chuki baina ya wanachama ama wananchi na chombo chao ambacho kina dhamana ya kuwatibia.
Hata hivyo Mhando amekanusha kuwa wao  ndio kikwazo ama sababisho la huduma mbovu katika vituo hivyo nah ii inatokana na ukweli kwamba zipo jitihada mbalimbali ambazo NHIF imekuwa ikizifanya kuhakikisha inasaidiana na Serikali katika kuboresha huduma za vituo hivyo ili wananchi kwa pamoja wapate huduma zinazostahili.

Sekeleti achomoza Tamasha la Krismasi, kushukuru

index 
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, Ephraim Sekeleti amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji watakaopanda jukwaa la Tamasha la Krismasi na kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Sekeleti amekubali kuwa mmoja wa waimbaji wa Kimataifa watakaopanda jukwaa la Shukrani ambalo litakuwa katika Sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Masia, Yesu Kristo.
Msama alisema tamasha hilo ni la Shukrani baada ya kuombea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, Tamasha la Maombi lilifanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Tunarudisha heshima na Shukrani kwa Mungu baada ya kuiepusha Tanzania na majaribu yaliyokuwa na mlengo wa kutaka kuvuruga amani ambayo iliasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema kuandaa tamasha hilo inaonesha namna gani Watanzania tulivyo na shukrani ambako Watanzania tukumbuke kwamba Tukipewa, Tusisahau kushukuru.
Ujumbe mzito ambao ni kumbukizi kwa Wanadamu ni kwamba binaadam tunapobarikiwa na Mungu hatuna budi kushukuru, hivyo tamasha hilo ni shukrani baada ya Mungu kusikia vilio vya Watanzania baada ya kuisaidia Tanzania katika uchaguzi Mkuu.    

MISA TAKATIFU YA KUMBUKUMBU YA NYAMITI LUSINDE BALTIMORE, MARYLAND

 Picha ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde ikiwa kanisani
siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 siku ilikofanyika misa takatifu ya
kumbukumbu na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.
Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. Nyamiti
alikua mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani alipatwa na
mauti alipokua likizo Tanzania katika hospitali ya Kariuki alipokua
amekwenda kwa matibabu baada ya kuugua ghafla alipokua huko na baadae
kuaga Dunia Novemba 17, 2015. Picha na Vijimambo/Kwanza
Production
Father Honest Munishi akiongoza misa takatifu ya kumbukumbu ya
mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 na
kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson
Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. 
Father Lehandry Kimario akisaidiana na Father Honest Munishi katika
kuongoza misa takatifu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde
iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland
nchini Marekani.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Marekani akiwa na mkewe Marystella Masilingi wakifuatilia misa
takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde
iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland
nchini Marekani.
Balozi Mhe. Wilson Masilingi akiongea machache jinsi alivyomjua
Nyamiti na kutoa shukurani zake kwa watu mbalimbali ikiwemo kamati
iliyowezesha kufanikisha misa hiyo na shukurani za pekee kwa Father
Honest Munishi na Father Lehandry Kimario.
Kulia ni Sima Kazaura akisoma soma la kwanza huku akiwa
amesindikizwa na Dorothy.
Kulia ni Farida Sarita akisoma soma la pili huku akiwa
amesindikizwa na Dorothy.
 Mshereheshaji Tuma akiongea jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu
Nyamiti.
 Kulia ni Rosemary Commodores akisoma wasifu wa marehemu.
 Kulia ni Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akitoa salamu za
Ubalozi, kushoto ni mkewe.
 Dorothy akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
 Sima Kazaura akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu
Nyamiti
 Patrick Kajale akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu
Nyamiti
Eddah Gachuma akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Dj Luke akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Joyce akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Pius Mtalemwa kiongozi wa kanisa la ibada ya Kiswahili DMV
akihitimisha kwa kutoa shukurani kwa wote.
Nelson Masilingi, mtoto wa Mhe. Balozi akifuatilia misa takatifu ya
kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada
Col. Adolph Mutta akiwa na mkewe wakifuatilia misa takatifu ya
kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
Watu mbalimbali waliohudhuria misa.
 
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIZUNGUMZA NA SPIKA MSTAAFU MAKINDA

index
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na Spika Mstaafu, Anne Makinda  kwenye ikulu ya Chamwino mjini Dodoma hivi karibuni.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
index2

TFFT YATOA TUZO KWA VITUO BORA VYA MAKAO YA WATOTO

2 
Wamiliki wa vituo vya makao ya watoto wakiwa na  tuzo zao  za makao bora ya watoto.
 ………………………………………………………………………………………….
Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
 
Shirika la The Foundation For Tomorrow lenye makao yake jijini Arusha,  limevitunuku tuzo vituo bora vya makao ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi katika mkoa wa Arusha. Tuzo hizo zenye lengo la kutambua juhudi na mchango wa makao ya watoto katika kujenga jamii bora, kulinda na kuhakikisha usalama kwa watoto zilikabidhiwa kwa washiriki na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Arusha Bi. Blandina Nkini kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
 
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, iliyofanyika katika ofisi ya shirika hilo jijini Arusha, Bi. Nkini alisema kuwa uangalizi wa watoto ni  muhimu sana katika ustawi wa taifa kwa kuwa ndio unaojenga msingi wa taifa kwa kuwapa watoto malezi bora. “Viongozi wa taifa letu hutokana na malezi na makuzi bora waliyoyapata utotoni”, alisema.
 
Naye mkurugenzi mkazi wa shirika hilo ndugu, Kennedy Oulu aliwahimiza washiriki wa tuzo hizo kuendelea kuunganisha juhudi zao katika kushughulikia changamoto ziwapatazo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
 
“Inahitaji huruma, upendo na msukumo wa kweli katika kuwasaidia watoto hawa. Licha ya kuwa tatizo la watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi ni kubwa na ni vigumu kutokomeza, muunganiko wa juhudi za kila mmoja wetu litawezesha kuweka mchango mkubwa katika kupunguza tatizo lililopo”, alisema Oulu.
 
Aidha Oulu aliongeza kuwa, haki za watoto katika nchi yetu zinakiukwa sana, si kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi tu, bali hata kwa wale wasio katika mazingira hayo. Aliongeza kuwa, tafiti zinaonesha kwamba kuna ukiukwaji mkubwa zaidi kwa watoto waishio kwenye makao ya watoto kuliko walio majumbani na sehemu zingine. Hili linatokana na dhamira na malengo tofauti ya wale wanaoanzisha na kuendesha makao hayo.
 
“Haki za watoto zinakiukwa kwa sababu wanajamii kwa kiasi kikubwa hawatambui kuwa watoto pia wana haki zao! Sheria za watoto (LCA 2009) zimeweka wazi haki za mtoto na matokeo ya ukiukwaji wake. Sisi tunaowalea watoto na jamii kwa ujumla hatuna budi kuzitambua, kuzifuata na kuhakikisha utekelezaji wa haki za watoto”. Alisema Oulu.
 
Vituo vya makao ya watoto vipatavyo 12 kutoka wilaya za Meru, Monduli na Karatu vilishiriki katika mchakato  wa tuzo hizo kwa mwaka huu, ambapo kituo cha SMALL STEPS FOR COMPASSION (www.smallstepsforcompassion.org)  kilichopo Usa River wilaya ya Meru ndicho kilichoibuka mshindi wa jumla kimkoa, huku kituo cha RIFT VALLEY CHILDREN FUND (www.tanzanianchildrensfund.org) kikishinda tuzo ya mshindi wa wilaya ya Karatu na MAJENGO CHILDREN’S HOME chenye makao yake katika mji wa Mto wa Mbu kikiwa mshindi wa wilaya ya Monduli.
 
Akiongea wakati wa kuhitimisha hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Bi. Nkini alilipongeza shirika la The Foundation For Tomorrow kwa kutoa tuzo hizo ambazo mchakato wake huwezesha vituo vingi kuboresha huduma zao kwa watoto. Aidha alimsihi mkurugenzi wake ndugu Oulu kuwa aangalie pia uwezekano wa kutoa elimu ya malezi bora ya watoto kwa vituo vyote vilivyopo Arusha kadri inavyowezekana kwani elimu hii ni muhimu sana kuweza kufikiwa kwa vituo vyote. Aidha aliviasa vituo hivi kujisahihisha pale kunapo mapungufu na kuboresha huduma zao kwa watoto. Naye mkurugenzi wa shirika hilo, ndugu Oulu alimhakikishia Bi. Nkini kuwa shirika hilo lipo tayari kutoa elimu hii kwa vituo vilivyopo Arusha wakati wowote litakapoalikwa iwapo ofisi ya Ustawi wa Jamii mkoa wa Arusha ikiandaa mafunzo ya namna hii.
 
Tuzo hizi zimepangwa kutolewa kila mwaka na kushirikisha mikoa mingine zaidi kwa ushirikiano wa shirika la The Foundation For Tomorrow, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii Wilaya, Vituo vya Makao ya Watoto na jamii kwa ujumla.

MKUTANO WA WANAWAKE AFRIKA WAFANYIKA ARUSHA

1
Mshauri wa sheria za ardhi kwa wanawake kutoka shirika la Oxfam,Everlyne Nairesiae akiwafundisha baadhi ya wanawake mbalimbali kutoka barani Afrika katika mkutano wa kuweka mkakati wa kupaza sauti ya kumiliki ardhi na rasilimali barani Afrika,mkutano huo ulifanyika jijini Arusha na kuandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP),(picha na mahmoud Ahmad wa manyaraleo blog)
2
Baadhi ya wanawake mbalimbali barani Afrika wakishiriki mkutano wa kuweka mkakati wa kupaza sauti ya  kumiliki ardhi  na rasilimali barani Afrika,mkutano huo ulifanyika jijini Arusha na kuandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) (picha na mahmoud ahmad)
3
Baadhi ya wanawake mbalimbali barani Afrika wakishiriki mkutano wa kuweka mkakati wa kupaza sauti ya  kumiliki ardhi  na rasilimali barani Afrika,mkutano huo ulifanyika jijini Arusha na kuandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) (picha na mahmoud ahmad)

No comments :

Post a Comment