Kwa
mujibu wa Sheria ya Sikukuu za Kitaifa (The Public Holidays Act, Cap
35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku
yoyote kuwa sikukuu au mapumziko, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa
maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9
Desemba, 2015, yatumike kwa kufanya kazi. Kwamba maadhimisho ya Uhuru
ya mwaka huu (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya
kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu. Mheshimiwa Rais
ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi
mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi
wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.
Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi, fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.
Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi, fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.
Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru
na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi
yetu. Hivyo, sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama
kawaida kuanzia mwaka 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015
Balozi Sefue awaasa watumishi wa umma kuwajibika
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Bw Silasi David mmoja
ya wagonjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akizungumza na mmoja ya wagomjwa waliolazwa katika kitengo
cha mifupa cha MOI Bw. Muhusin Hamiri.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Watumishi wa umma wametakiwa kutumia muda wa
kazi kuhudumia wananchi na sio kufanya kazi zao binafsi kwa kutumia
ofisi na vifaa vya serikali.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya
Hospitali kwa kukagua vifaa tiba na kuongea na watendaji wakuu wa
hospitali hiyo.
Balozi Sefue ameongeza kuwa watumishi wa
umma wanapaswa kufanya kazi kwa kutoa huduma bora na kwa upendo kwa
wananchi kwani moja ya kanuni na taratibu za mtumishi wa umma ni
kumhudumia mteja pasipo upendeleo.
“kwa upande wa madaktari na watoa huduma za afya mnatakiwa kutoa huduma bora na
zenye upendo kwa wananchi ili nao wajione wanahaki ya kupatiwa huduma hiyo”.
“kwa watumishi wote wa umma tukijitambua
kuwa sisi ni watumishi wa umma tutafanya kazi kwa bidii na kwa kujituma”
alifafanua Balozi Sefue.
ia muda wa kuingia na wa kutoka ofisini na pia kujipima ni nini amefanya ndani ya masaa nane katika kuhudumia wananchi.
“Hizi si nguvu za soda ni lazima kubadilika pindi tunapowahudumia wateja kwa wakati na kwa ufanisi” alisema Balozi Sefue.
Kadhalika katika kuhakikisha serikali inatoa
huduma bora kwa wananchi Balozi sefue ameagiza katika kila ofisi itoayo
huduma kuwe na dawati la msaada kwa wananchi waweze kupata huduma kwa
haraka.
KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari
ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa
hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani
ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John
Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala
chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan
Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman
Wanin Kiloloma.
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia),
Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati
baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa
anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba
mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji
wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika
Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo amefanya
ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine
amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili
kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema
amekagua mashine za MRI na CT-SCAN na kueleza kuwa spea zimeshafika na
kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa
kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja
wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
Pia, amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri
wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za
serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali,
Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia
mifumo ya Tehama na kuwa na maduka yao ya ndani.
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya
kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando na watendaji
wa MNH ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.
MAJALIWA AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE NA KUJITAMBULISHA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akipokea shada la maua kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Savera Kazaura (kulia) Baada ya kuwasili ofisini kwake
Novemba 23, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt,
Florence Turuka. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kuingia ofisini kwake , Magogoni
jijini Dar es salaam, Novemba 23, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Dkt. Florence Tiruka.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati
alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha , Ofisini kwa Waziri
Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati
alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha , Ofisini kwa Waziri
Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt.
Florence Turuka ambaye alitoa taarifa ya jumla kuhusu Ofisi ya Waziri
Mkuu baada ya Waziri Mkuu kuwasili Ofisini na kujitambulisha kwa
watumishi wa Ofisi yake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano
wa kujitambulisha alioufanya baada tu ya kuwasili ofisni Novemba 23,
2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha
alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Dkt Florence
Turuka baada ya kuwasili Ofisini Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha
alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim
Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu
walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo
ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na
pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo
tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi,
wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano
uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo
ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye
Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Pamoja na kazi nyingine tunayo
majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala
mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa
Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,”
alisema.
Aliwataka watumishi hao wawe
tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa
ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya
utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.
Alisema ana imani kuwa watumishi
hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi
wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.
TANZANIA YACHAGULIWA NA UNESCO KUWA MJUMBE WA KAMATI YA URITHI WA DUNIA

Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawako pichani) leo tarehe 23/11/2015 katika Ofisi
za Wizara hiyo ambapo amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kwa kipindi cha
miaka minne. Uchaguzi huo umefuatia uamuzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa nchi
Wanachama wa Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) unaohusu Urithi wa Dunia uliofanyika mjini Paris,
Ufaransa tarehe 18-20 Novemba 2015. (Habari Kamili SOMA TAARIFA KWA UMMA
HAPO CHINI)

Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru kushoto
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Tanzania kuchaguliwa
kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia. Alieleza kuwa katika Kamati
hiyo Tanzania itawakilishwa na Bw. Donatius Makamba ambaye ni
Mkurugugenzi Idara ya Mambo ya Kale Wizara ya Maliasili na Utalii
akisaidiwa na Dkt. James Wakibara, Mwikolojia Mkuu wa Shirika la Hifadhi
ya Taifa (TANAPA) na Dkt. Mohammed Juma, Mkurugenzi wa Mipango Miji na
Vijiji kutoka Zanzibar.

Bi.
Eliwasa Maro Mkurugenzi Msaidizi Utafiti Mafunzo na Takwimu Wizara ya
Maliasili na Utalii akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika Mkutano
huo na Waandishi wa Habari.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakinukuu baadhi ya mambo muhimu.
TANAPA receive anti-poaching aircraft from Germany
1. Germany Foreign Minister Hon.
Frank –Walter Steinmeier (right) handing over a symbolic key of a light
Husky aircraft for anti-poaching operations to Director General of
TANAPA Allan Kijazi. Others in the picture from left are Director of
Wildlife Herman Keraryo and Acting Director General of Tanzania Wildlife
Authority Martin Loibooki.
Director General of TANAPA Allan
Kijazi making a brief presentation about TANAPA to Germany Foreign
Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier during the handing over event of
two surveillance aircrafts from Germany to Tanzania yesterday.
Director General of TANAPA Allan
Kijazi presenting some of the souvenirs of TANAPA to Germany Foreign
Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier.
5. Germany Ambassador to Tanzania
Hon. Egon Kochanke (right) and the Permanent Secretary Ministry of
Foreign Affairs and International Cooperation Ambassador Liberata
Mulamula during the event.
Germany Foreign Minister Hon.
Frank –Walter Steinmeier (second right) posed in a group picture with
some of the Germany Members of Parliament who accompanied him during the
handing over event of two surveillance aircrafts from Germany to
Tanzania yesterday.
Director General of TANAPA Allan Kijazi speaking with media during the event.
Some of the invitees during the
handing over event. From left to right are Arusha Regional
Administrative Secretary Mr. Mapunda, African Wildlife Foundation
Country Director John Saleh and TANAPA’s Director of Tourism and
Marketing Ibrahim Mussa.
…………………………………………………………………………………….
Germany Foreign Minister
Frank-Walter Steinmeier yesterday handed over symbolic key of two Husky
aircrafts to Tanzania National Parks and Tanzania Wildlife Authority
respectively. The aircrafts will be used for anti-poaching operations in
the protected areas.
Director General of TANAPA Allan
Kijazi said that the aircrafts would take the joint approach by the
Germany Government through Frankfurt Zoological Society, TANAPA and TAWA
to tackle poaching in the protected areas.
The Husky A-1C is an ideal plane
for monitoring and anti-poaching surveys as it operates at low heights
and slow speeds-similar to that of a helicopter and has proven long-term
success rate for its use in finding poacher camps and recording GPS
positions for follow-up actions by teams on the grounds.
The Huskies will be used to monitor two of Tanzania’s elephant hotspots, Selous Game Reserve and Serengeti National Park.
Tanzania is home to some of the
most elephant and rhino populations on the planet but of recent days it
has experienced a severe threat from a massive upsurge in poaching.
Issued by Corporate Communications Department
Tanzania National Parks
23rd November, 2015
T: 027 250 1933
E: dg@tanzaniaparks.com
W: www.tanzaniaprks.com
Issued by Corporate Communications Department
Tanzania National Parks
23rd November, 2015
T: 027 250 1933
E: dg@tanzaniaparks.com
W: www.tanzaniaprks.com
BIMA YA AFYA NHIF YAKANUSHA KUDAIWA NA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA
Na Mwandishi wetu,Dar es salaam
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya nchini umekanusha kuwepo kwa madai
yaliyotolewa na Hospital ya Rufaa Mkoani Mbeya kuwa wanaudai Mfuko
jumla ya shilingi bilioni 2 na kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni,
2015.
Akizungumza
jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Ndugu Michael Mhando amesema madai yaliyotolewa na Hospital hiyo ya
Rufaa Mkoa wa Mbeya hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo unalipa
madai baada ya mtoa huduma kuwasilisha kwenye Mfuko.
Amesema
madai ya mwisho ya Hospitali hiyo kulipwa ni ya mwezi Agosti, 2015.
Madai ya mwezi Septemba, 2015 yamewasilishwa kwenye Mfuko tarehe
4/11/2015 ambayo mpaka sasa yana siku 15 tu. Kwa hiyo Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya tumewalipa madai yao yote na kwa mwaka huu wa 2015 kuanzia
Januari hadi Agosti 2015 tumewalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3.
Madai
mengi ambayo yamekuwa yakiwasilishwa kwao yamegubikwa na udanganyifu
mkubwa hali inayowafanya kuchukua muda mrefu katika uhakiki wake ikiwemo
kuwapigia simu wagonjwa waliopewa huduma za matibabu.
Aidha
Mhando amesema mfuko huo unatoa onyo kali kwa watoa huduma ambao
wamekuwa bado wakijihusisha na udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa
haitawaonea haya kuwafutia usajili na kuwafikisha katika vyombo vya
sheria.
Amesema
Mfuko pia unazidi kutoa rai kwa watoa huduma kutumia fursa zinazotolewa
na Mfuko katika kuhakikisha huduma za matibabu zinaboreshwa kwa
wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Wakati
huo Kaimu mkurugenzi huyo amesema Katika kipindi hiki, baadhi ya watoa
huduma wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali za kushindwa kutoa huduma
nzuri ama za kuridhisha kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla kwa
kisingizio cha kukosa fedha hali inayosababisha kukosa dawa, kukosa
vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kushindwa kuboresha mazingira ya
vituo.
Watoa
huduma hao wanadai hayo ama wanatoa visingizio vya kukwama huduma
katika maeneo yao kutokana na NHIF kuchelewa kulipa fedha fedha za madai
ambayo wametibia wanachama wake.
Amesema
taarifa hizo zinajenga mazingira kuwa NHIF ni kikwazo katika ufanisi
wa vituo hivyo jambo ambalo si la kweli na limebeba taswira ya kuleta
chuki baina ya wanachama ama wananchi na chombo chao ambacho kina
dhamana ya kuwatibia.
Hata
hivyo Mhando amekanusha kuwa wao ndio kikwazo ama sababisho la huduma
mbovu katika vituo hivyo nah ii inatokana na ukweli kwamba zipo jitihada
mbalimbali ambazo NHIF imekuwa ikizifanya kuhakikisha inasaidiana na
Serikali katika kuboresha huduma za vituo hivyo ili wananchi kwa pamoja
wapate huduma zinazostahili.
Sekeleti achomoza Tamasha la Krismasi, kushukuru
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa
Injili Afrika Mashariki na Kati, Ephraim Sekeleti amethibitisha kuwa
mmoja wa waimbaji watakaopanda jukwaa la Tamasha la Krismasi na
kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Sekeleti amekubali kuwa
mmoja wa waimbaji wa Kimataifa watakaopanda jukwaa la Shukrani ambalo
litakuwa katika Sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Masia, Yesu Kristo.
Msama alisema tamasha hilo ni la
Shukrani baada ya kuombea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25,
Tamasha la Maombi lilifanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
“Tunarudisha heshima na Shukrani
kwa Mungu baada ya kuiepusha Tanzania na majaribu yaliyokuwa na mlengo
wa kutaka kuvuruga amani ambayo iliasisiwa na baba wa Taifa Mwalim
Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema kuandaa
tamasha hilo inaonesha namna gani Watanzania tulivyo na shukrani ambako
Watanzania tukumbuke kwamba Tukipewa, Tusisahau kushukuru.
Ujumbe mzito ambao ni kumbukizi
kwa Wanadamu ni kwamba binaadam tunapobarikiwa na Mungu hatuna budi
kushukuru, hivyo tamasha hilo ni shukrani baada ya Mungu kusikia vilio
vya Watanzania baada ya kuisaidia Tanzania katika uchaguzi Mkuu.
MISA TAKATIFU YA KUMBUKUMBU YA NYAMITI LUSINDE BALTIMORE, MARYLAND
Picha ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde ikiwa kanisani
siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 siku ilikofanyika misa takatifu ya
kumbukumbu na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.
Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. Nyamiti
alikua mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani alipatwa na
mauti alipokua likizo Tanzania katika hospitali ya Kariuki alipokua
amekwenda kwa matibabu baada ya kuugua ghafla alipokua huko na baadae
kuaga Dunia Novemba 17, 2015. Picha na Vijimambo/Kwanza
Production
siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 siku ilikofanyika misa takatifu ya
kumbukumbu na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.
Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. Nyamiti
alikua mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani alipatwa na
mauti alipokua likizo Tanzania katika hospitali ya Kariuki alipokua
amekwenda kwa matibabu baada ya kuugua ghafla alipokua huko na baadae
kuaga Dunia Novemba 17, 2015. Picha na Vijimambo/Kwanza
Production
Father Honest Munishi akiongoza misa takatifu ya kumbukumbu ya
mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 na
kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson
Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae.
mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 na
kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson
Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae.
Father Lehandry Kimario akisaidiana na Father Honest Munishi katika
kuongoza misa takatifu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde
iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland
nchini Marekani.
kuongoza misa takatifu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde
iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland
nchini Marekani.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Marekani akiwa na mkewe Marystella Masilingi wakifuatilia misa
takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde
iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland
nchini Marekani.
nchini Marekani akiwa na mkewe Marystella Masilingi wakifuatilia misa
takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde
iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland
nchini Marekani.
Balozi Mhe. Wilson Masilingi akiongea machache jinsi alivyomjua
Nyamiti na kutoa shukurani zake kwa watu mbalimbali ikiwemo kamati
iliyowezesha kufanikisha misa hiyo na shukurani za pekee kwa Father
Honest Munishi na Father Lehandry Kimario.
Nyamiti na kutoa shukurani zake kwa watu mbalimbali ikiwemo kamati
iliyowezesha kufanikisha misa hiyo na shukurani za pekee kwa Father
Honest Munishi na Father Lehandry Kimario.
Kulia ni Sima Kazaura akisoma soma la kwanza huku akiwa
amesindikizwa na Dorothy.
amesindikizwa na Dorothy.
Kulia ni Farida Sarita akisoma soma la pili huku akiwa
amesindikizwa na Dorothy.
amesindikizwa na Dorothy.
Mshereheshaji Tuma akiongea jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu
Nyamiti.
Nyamiti.
Kulia ni Rosemary Commodores akisoma wasifu wa marehemu.
Kulia ni Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akitoa salamu za
Ubalozi, kushoto ni mkewe.
Ubalozi, kushoto ni mkewe.
Dorothy akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
Sima Kazaura akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu
Nyamiti
Nyamiti
Patrick Kajale akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu
Nyamiti
Nyamiti
Eddah Gachuma akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Dj Luke akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Joyce akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Pius Mtalemwa kiongozi wa kanisa la ibada ya Kiswahili DMV
akihitimisha kwa kutoa shukurani kwa wote.
akihitimisha kwa kutoa shukurani kwa wote.
Nelson Masilingi, mtoto wa Mhe. Balozi akifuatilia misa takatifu ya
kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada
Col. Adolph Mutta akiwa na mkewe wakifuatilia misa takatifu ya
kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
Col. Adolph Mutta akiwa na mkewe wakifuatilia misa takatifu ya
kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
Watu mbalimbali waliohudhuria misa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
TFFT YATOA TUZO KWA VITUO BORA VYA MAKAO YA WATOTO
Wamiliki wa vituo vya makao ya watoto wakiwa na tuzo zao za makao bora ya watoto.
………………………………………………………………………………………….
Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
Shirika la The Foundation For
Tomorrow lenye makao yake jijini Arusha, limevitunuku tuzo vituo bora
vya makao ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi
katika mkoa wa Arusha. Tuzo hizo zenye lengo la kutambua juhudi na
mchango wa makao ya watoto katika kujenga jamii bora, kulinda na
kuhakikisha usalama kwa watoto zilikabidhiwa kwa washiriki na Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Arusha Bi. Blandina Nkini kwa niaba ya
mkuu wa mkoa wa Arusha.
Akizungumza katika hafla ya
utoaji wa tuzo hizo, iliyofanyika katika ofisi ya shirika hilo jijini
Arusha, Bi. Nkini alisema kuwa uangalizi wa watoto ni muhimu sana
katika ustawi wa taifa kwa kuwa ndio unaojenga msingi wa taifa kwa
kuwapa watoto malezi bora. “Viongozi wa taifa letu hutokana na malezi na
makuzi bora waliyoyapata utotoni”, alisema.
Naye mkurugenzi mkazi wa
shirika hilo ndugu, Kennedy Oulu aliwahimiza washiriki wa tuzo hizo
kuendelea kuunganisha juhudi zao katika kushughulikia changamoto
ziwapatazo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
“Inahitaji huruma, upendo na
msukumo wa kweli katika kuwasaidia watoto hawa. Licha ya kuwa tatizo la
watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi ni kubwa na ni
vigumu kutokomeza, muunganiko wa juhudi za kila mmoja wetu litawezesha
kuweka mchango mkubwa katika kupunguza tatizo lililopo”, alisema Oulu.
Aidha Oulu aliongeza kuwa, haki
za watoto katika nchi yetu zinakiukwa sana, si kwa watoto waishio
katika mazingira hatarishi tu, bali hata kwa wale wasio katika mazingira
hayo. Aliongeza kuwa, tafiti zinaonesha kwamba kuna ukiukwaji mkubwa
zaidi kwa watoto waishio kwenye makao ya watoto kuliko walio majumbani
na sehemu zingine. Hili linatokana na dhamira na malengo tofauti ya wale
wanaoanzisha na kuendesha makao hayo.
“Haki za watoto zinakiukwa kwa
sababu wanajamii kwa kiasi kikubwa hawatambui kuwa watoto pia wana haki
zao! Sheria za watoto (LCA 2009) zimeweka wazi haki za mtoto na matokeo
ya ukiukwaji wake. Sisi tunaowalea watoto na jamii kwa ujumla hatuna
budi kuzitambua, kuzifuata na kuhakikisha utekelezaji wa haki za
watoto”. Alisema Oulu.
Vituo vya makao ya watoto
vipatavyo 12 kutoka wilaya za Meru, Monduli na Karatu vilishiriki katika
mchakato wa tuzo hizo kwa mwaka huu, ambapo kituo cha SMALL STEPS FOR
COMPASSION (www.smallstepsforcompassion. org) kilichopo Usa River wilaya ya Meru ndicho kilichoibuka mshindi wa jumla kimkoa, huku kituo cha RIFT VALLEY CHILDREN FUND (www.tanzanianchildrensfund. org)
kikishinda tuzo ya mshindi wa wilaya ya Karatu na MAJENGO CHILDREN’S
HOME chenye makao yake katika mji wa Mto wa Mbu kikiwa mshindi wa wilaya
ya Monduli.
Akiongea wakati wa kuhitimisha
hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Bi. Nkini alilipongeza shirika la The
Foundation For Tomorrow kwa kutoa tuzo hizo ambazo mchakato wake
huwezesha vituo vingi kuboresha huduma zao kwa watoto. Aidha alimsihi
mkurugenzi wake ndugu Oulu kuwa aangalie pia uwezekano wa kutoa elimu ya
malezi bora ya watoto kwa vituo vyote vilivyopo Arusha kadri
inavyowezekana kwani elimu hii ni muhimu sana kuweza kufikiwa kwa vituo
vyote. Aidha aliviasa vituo hivi kujisahihisha pale kunapo mapungufu na
kuboresha huduma zao kwa watoto. Naye mkurugenzi wa shirika hilo, ndugu
Oulu alimhakikishia Bi. Nkini kuwa shirika hilo lipo tayari kutoa elimu
hii kwa vituo vilivyopo Arusha wakati wowote litakapoalikwa iwapo ofisi
ya Ustawi wa Jamii mkoa wa Arusha ikiandaa mafunzo ya namna hii.
Tuzo hizi zimepangwa kutolewa
kila mwaka na kushirikisha mikoa mingine zaidi kwa ushirikiano wa
shirika la The Foundation For Tomorrow, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii kwa kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii Wilaya, Vituo vya Makao ya
Watoto na jamii kwa ujumla.
MKUTANO WA WANAWAKE AFRIKA WAFANYIKA ARUSHA
Mshauri wa sheria za ardhi kwa
wanawake kutoka shirika la Oxfam,Everlyne Nairesiae akiwafundisha baadhi
ya wanawake mbalimbali kutoka barani Afrika katika mkutano wa kuweka
mkakati wa kupaza sauti ya kumiliki ardhi na rasilimali barani
Afrika,mkutano huo ulifanyika jijini Arusha na kuandaliwa na mtandao wa
jinsia Tanzania(TGNP),(picha na mahmoud Ahmad wa manyaraleo blog)
Baadhi ya wanawake mbalimbali barani
Afrika wakishiriki mkutano wa kuweka mkakati wa kupaza sauti ya
kumiliki ardhi na rasilimali barani Afrika,mkutano huo ulifanyika
jijini Arusha na kuandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) (picha
na mahmoud ahmad)
Baadhi ya wanawake mbalimbali barani
Afrika wakishiriki mkutano wa kuweka mkakati wa kupaza sauti ya
kumiliki ardhi na rasilimali barani Afrika,mkutano huo ulifanyika
jijini Arusha na kuandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) (picha
na mahmoud ahmad)



No comments:
Post a Comment