Tuesday, September 1, 2015

JK AFANYA MAZUNGUMZO YA FALAGHA NA RAIS KABILA WA DRC, UWANJA WA NDEGE WA JNIA LEO Posted by Ngabwe Mlulu on 13:26 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo Septemba 1, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Joseph Kabila alkiposimama kwa muda wakati akiwa njiani kurejea nchini mwake. Soma Zaidi LOWASSA AENDELEA "KUTISHA" MAELFU WAFURIKA KUMSIKILIZA HUKO RUVUMA Posted by Ngabwe Mlulu on 13:11 MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia maelfu ya wananchi akiwa kwenye gari, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015 ambapo alihutubia mkutano wa kampeni ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni akiwa kwenye mkoa watatu baada ya kuzindua rasmi kampeni zake jijini Dar es Salaam. Mh. Lowassa ameendelea kuonyesha "nguvu" zake kisiasa kutokana na maelfu ya wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano yake. (Picha zote na Othman Michuzi) Soma Zaidi DKT. SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA ZA VYAMA VYA SIASA, AISHAMBULIA CHADEMA, LOWASSA NA SUMAYE Posted by Ngabwe Mlulu on 13:00 NA K-VIS MEDIA Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, leo Septemba 1, 2015 amelitangazia taifa kupitia mkutanon wake na waandishi wa habari uliorushwa "live" na runinga za hapa nchini pamoja na radio mbalimbali, kuwa anaachana na siasa za vyama vya siasa, lakini atabaki akifanya siasa nje ya vyama vya hivyo. Katika maelezo yake, Dkt. Slaa alikishambulia chama chake cha zamani CHADEMA, pamoja na mgombea Urais kupitia chama hicho akiwakilisha vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Mh. Edward Lowassa kuwa wamepotoka na wanapotosha wananchi. Amesema, Mh. Lowassa bado anakabiliwa na tuhuma za rushwa hususan sakata la Ricvhmond na kwamba yeye Dkt. Slaa yuko tayari kupelekwa mahakamani kuthibitisha hilo. Hata hivyo tayar Mh. Lowassa, mara kadhaa mekanusha kuhusika kwa namna yoyote na sakata hilo na kwamba, baada ya kugundua kasoro kwenye mkataba wa Richmond, alitaka kuvunja mkataba huo lkakini mamlaka za juu zilizuia kusudio hilo. Dkt. Slaa ambaye alikuwa kimya tangu Mh. Lowassa ajiunge na chama hicho na hatimaye kuteuliwa kuwa mgombea wake wa kiti cha Rais, alitumia mkutano huo kumshambulia Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Frederick Sumaye kuwa naye pia hana maadili mema. Pichani Dkt. Slaa akizungumza na vyombo vya habari Dkt. Slaa akiwasili tayari kuzungumza na vyombop vya habari kwenye hoyteli ya Serena jijini Dar es Salaam Soma Zaidi JK AAGWA KWA HESHIMA KUBWA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, AWATUNUKIA NISHANI IKULU Posted by Ngabwe Mlulu on 12:41 NA K-VIS MEDIA Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumanne Septemba 1, 2015, ameagwa kwa gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo ndege vita zilitoa saluti kwenye anga la uwanja huo ikiwa ni ishara ya kumuaga rasmi baada ya kuliongoza taifa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Rais Kikwete anatyarajiwa kuondoka rasmi madarakani mwishoni mwa mwaka huu baada ya kupatikana mrithi wake kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu wa 2015. Baada ya sherehe hiyo ya uwanja wa Uhuru Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Rais Kikwete, alwatunuku Nishani kwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na Usalama nchini ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao wa kulilinda taifa na kuwa na utulivu katika kipindi chake chote cha utawala wa miaka 10. Pichani Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi waliotunukiwa nishani za madaraja mbalimbali.Viongozi wengine katika picha waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais Wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein(watano kushoto), Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(picha na Freddy Maro na Ramadhan Othman) Rais akikagua gwaride uwanja wa Uhuru Rais akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein Soma Zaidi MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU, BGML, WAKABIDHI MIRADI YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA WILAYA YA MSALALA Posted by Ngabwe Mlulu on 08:07 MOJA kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi. NA K-VIS MEDIA MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi, yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.” Alisema “Ninayo furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta za Afya na Elimu.”Alifafanua Akitoa mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200. Miradi mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9), Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na gharama ya shilingi 174,392,000. Hali kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706. Akitoa shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka mgodi huo. “Nataka niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.” Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi hiyo kuitunza. Kukabidhiwa kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake. Kaimu Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML, Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1. Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015. Soma Zaidi HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOITIKISA RUVUMA, MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA Posted by Ngabwe Mlulu on 21:14 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini humo mkoani Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUVUMA Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya. Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma. Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho. Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini. Dk Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto huo. Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa kazi. Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji jioni ya leo. Maelfu ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea jioi ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi hao. Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga. Waanchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha-Peramiho mkoani Ruvuma jioni ya leo. Wananchi wakishangilia Umati wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tamasha ndani ya jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma. Baadhi ya Wananchi wa Peramiho wakifurahia jamo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga. Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za ccm leo jioni ndani ya uwanja wa Maji Maji mjini Songea. Wananchi wa Songea mjini wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Maji maji mjini humo. Soma Zaidi MO DEWJI FOUNDATION YAKABIDHI MATUNDU NANE YA CHOO BORA KWENYE SHULE YA MSINGI KIBAONI SINGIDA Posted by Ngabwe Mlulu on 21:07 DSC01579 Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni). DSC01583 Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule. DSC01592 Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni. DSC01596 Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni. DSC01600 Mwakilishi wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni. DSC01603 Jengo la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu). Na Nathaniel Limu, Singida WAZAZI/WALEZI wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule. Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa, yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao wavulana ni 377 na wasichana ni 465. Alisema uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu. Akifafanua, alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa shilingi 2,300,000. Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu. Kwa upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda nafasi ya Miss Singida mwaka jana. Awali Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi wa choo na kuinusuru kufungiwa. “Nitumie nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali kuharakisha ujenzi huu”,alisema.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo Septemba 1, 2015, amekutana na  kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Joseph Kabila alkiposimama kwa muda wakati akiwa njiani kurejea nchini mwake.


 MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia maelfu ya wananchi akiwa kwenye gari, wakati akiwasili kwenye  Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015 ambapo alihutubia mkutano wa kampeni ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni akiwa kwenye mkoa watatu baada ya kuzindua rasmi kampeni zake jijini Dar es Salaam. Mh. Lowassa ameendelea kuonyesha "nguvu" zake kisiasa kutokana na maelfu ya wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano yake. (Picha zote na Othman Michuzi)




NA K-VIS MEDIA
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, leo Septemba 1, 2015 amelitangazia taifa kupitia mkutanon wake na waandishi wa habari uliorushwa "live" na runinga za hapa nchini pamoja na radio mbalimbali, kuwa anaachana na siasa za vyama vya siasa, lakini atabaki akifanya siasa nje ya vyama vya hivyo. Katika maelezo yake, Dkt. Slaa alikishambulia chama chake cha zamani CHADEMA, pamoja na mgombea Urais kupitia chama hicho akiwakilisha vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Mh. Edward Lowassa kuwa wamepotoka na wanapotosha wananchi. Amesema, Mh. Lowassa bado anakabiliwa na tuhuma za rushwa hususan sakata la Ricvhmond na kwamba yeye Dkt. Slaa yuko tayari kupelekwa mahakamani kuthibitisha hilo. Hata hivyo tayar Mh. Lowassa, mara kadhaa mekanusha kuhusika kwa namna yoyote na sakata hilo na kwamba, baada ya kugundua kasoro kwenye mkataba wa Richmond, alitaka kuvunja mkataba huo lkakini mamlaka za juu zilizuia kusudio hilo. Dkt. Slaa ambaye alikuwa kimya tangu Mh. Lowassa ajiunge na chama hicho na hatimaye kuteuliwa kuwa mgombea wake wa kiti cha Rais, alitumia mkutano huo kumshambulia Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Frederick Sumaye kuwa naye pia hana maadili mema. Pichani Dkt. Slaa akizungumza na vyombo vya habari
Dkt. Slaa akiwasili tayari kuzungumza na vyombop vya habari kwenye hoyteli ya Serena jijini Dar es Salaam
NA K-VIS MEDIA
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumanne Septemba 1, 2015, ameagwa kwa gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo ndege vita zilitoa saluti kwenye anga la uwanja huo ikiwa ni ishara ya kumuaga rasmi baada ya kuliongoza taifa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Rais Kikwete anatyarajiwa kuondoka rasmi madarakani mwishoni mwa mwaka huu baada ya kupatikana mrithi wake kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu wa 2015. Baada ya sherehe hiyo ya uwanja wa Uhuru Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Rais Kikwete, alwatunuku Nishani kwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na Usalama nchini ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao wa kulilinda taifa na kuwa na utulivu katika kipindi chake chote cha utawala wa miaka 10. Pichani Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi waliotunukiwa nishani za madaraja mbalimbali.Viongozi wengine katika picha waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais Wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein(watano kushoto), Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(picha na Freddy Maro na Ramadhan Othman)
 Rais akikagua gwaride uwanja wa Uhuru

 Rais akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein
 MOJA kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.

NA K-VIS MEDIA
MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi, yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.” Alisema
“Ninayo furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta za Afya na Elimu.”Alifafanua
Akitoa mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.
Miradi mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9), Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na gharama ya shilingi 174,392,000.
Hali kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706.
Akitoa shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka mgodi huo.
“Nataka niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.” Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi hiyo kuitunza.
Kukabidhiwa kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.
 Kaimu Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML, Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015. 
 










 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini  humo mkoani Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUVUMA
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya. 

 Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini.
 Dk Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga  mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto huo.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa kazi.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji jioni ya leo.
 Maelfu ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea jioi ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi hao.
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga.
 Waanchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha-Peramiho mkoani Ruvuma jioni ya leo.
 Wananchi wakishangilia 
 Umati wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tamasha ndani ya jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma. 
 Baadhi ya Wananchi wa Peramiho wakifurahia jamo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga.
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za ccm leo jioni ndani ya uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

 Wananchi wa Songea mjini wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Maji maji mjini humo.
DSC01579
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni).
DSC01583
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule.
DSC01592
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
DSC01596
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni.
DSC01600
Mwakilishi wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
DSC01603
Jengo la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZAZI/WALEZI wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa, yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao wavulana ni 377 na wasichana ni 465.
Alisema uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu.
Akifafanua, alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi wa choo na kuinusuru kufungiwa.
“Nitumie nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali kuharakisha ujenzi huu”,alisema.

No comments :

Post a Comment