MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia maelfu ya wananchi
akiwa kwenye gari, wakati akiwasili kwenye Uwanja
wa Shule ya Msingi Matarawe,
Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015 ambapo alihutubia
mkutano wa kampeni ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni akiwa
kwenye mkoa watatu baada ya kuzindua rasmi kampeni zake jijini Dar es
Salaam. Mh. Lowassa ameendelea kuonyesha "nguvu" zake kisiasa kutokana
na maelfu ya wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano yake. (Picha zote na
Othman Michuzi)
NA K-VIS MEDIA
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt.
Wilbroad Slaa, leo Septemba 1, 2015 amelitangazia taifa kupitia mkutanon
wake na waandishi wa habari uliorushwa "live" na runinga za hapa nchini
pamoja na radio mbalimbali, kuwa anaachana na siasa za vyama vya siasa,
lakini atabaki akifanya siasa nje ya vyama vya hivyo. Katika maelezo
yake, Dkt. Slaa alikishambulia chama chake cha zamani CHADEMA, pamoja na
mgombea Urais kupitia chama hicho akiwakilisha vyama vinne vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Mh. Edward Lowassa kuwa wamepotoka na
wanapotosha wananchi. Amesema, Mh. Lowassa bado anakabiliwa na tuhuma
za rushwa hususan sakata la Ricvhmond na kwamba yeye Dkt. Slaa yuko
tayari kupelekwa mahakamani kuthibitisha hilo. Hata hivyo tayar Mh.
Lowassa, mara kadhaa mekanusha kuhusika kwa namna yoyote na sakata hilo
na kwamba, baada ya kugundua kasoro kwenye mkataba wa Richmond, alitaka
kuvunja mkataba huo lkakini mamlaka za juu zilizuia kusudio hilo. Dkt.
Slaa ambaye alikuwa kimya tangu Mh. Lowassa ajiunge na chama hicho na
hatimaye kuteuliwa kuwa mgombea wake wa kiti cha Rais, alitumia mkutano
huo kumshambulia Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Frederick
Sumaye kuwa naye pia hana maadili mema. Pichani Dkt. Slaa akizungumza na
vyombo vya habari
Dkt. Slaa akiwasili tayari kuzungumza na vyombop vya habari kwenye hoyteli ya Serena jijini Dar es Salaam
NA K-VIS MEDIA
Rais
Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete leo Jumanne Septemba 1, 2015, ameagwa kwa gwaride la
heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo ndege vita zilitoa saluti kwenye anga
la uwanja huo ikiwa ni ishara ya kumuaga rasmi baada ya kuliongoza
taifa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Rais Kikwete
anatyarajiwa kuondoka rasmi madarakani mwishoni mwa mwaka huu baada ya
kupatikana mrithi wake kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu wa 2015. Baada ya sherehe hiyo ya uwanja wa Uhuru
Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Rais Kikwete,
alwatunuku Nishani kwa watumishi wa vyombo vya
ulinzi na Usalama nchini ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao wa
kulilinda taifa na kuwa na utulivu katika kipindi chake chote cha
utawala wa miaka 10. Pichani Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja
na watumishi
waliotunukiwa nishani za madaraja mbalimbali.Viongozi wengine katika
picha
waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais Wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali
Shein(watano kushoto), Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal, na
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(picha na Freddy Maro na Ramadhan Othman)
Rais akikagua gwaride uwanja wa Uhuru
Rais akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein
MOJA kati ya majengo ya shule ya Msingi
Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu
ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na
kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye
thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano
mema na jamii inayozunguka migodi.
NA
K-VIS MEDIA
MGODI
wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi,
yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na
Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa
ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi
miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa
utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.” Alisema
“Ninayo
furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi
bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta
za Afya na Elimu.”Alifafanua
Akitoa
mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash
alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi
Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa
madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa
thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za
walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.
Miradi
mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9),
Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na
gharama ya shilingi 174,392,000.
Hali
kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia
kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706.
Akitoa
shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya
Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni
faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka
mgodi huo.
“Nataka
niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati
ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.”
Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi
hiyo kuitunza.
Kukabidhiwa
kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi
huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.
Kaimu
Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML,
Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya
Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji
kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa
na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri
hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni
Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto),
akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala
Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za
walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na
kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya
wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1,
kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea
waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini humo mkoani
Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza
katika awamu ya tano.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUVUMA
Mgombea
wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli
akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika
serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa
wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza
maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya.
Mgombea
Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya
CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa
mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani
Ruvuma.
Dk
Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya
katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi
Ilani ya chama hicho.
Mgombea
wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli
akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda
kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika Mbinga mjini.
Dk
Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya
Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni
za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto
huo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni
mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia
wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea
mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi
utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa
kazi.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini
kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji
jioni ya leo.
Maelfu
ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea
jioi ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya
leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi
hao.
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga.
Waanchi
wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika mkutano
wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha-Peramiho mkoani Ruvuma
jioni ya leo.
Wananchi wakishangilia
Umati
wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa
kampeni katika uwanja wa Tamasha ndani ya jimbo la Peramiho mkoani
Ruvuma.
Baadhi ya Wananchi wa Peramiho wakifurahia jamo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto
aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la
Peramiho, mkoani Ruvuma
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga.
Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za ccm leo jioni ndani ya uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
Wananchi
wa Songea mjini wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli
alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Maji
maji mjini humo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14
milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni).
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation
mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi
choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida,
chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi
wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali,
uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule.
Mkurugenzi wa Doris Mollel
Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, akizungumza kwenye
hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni,
kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa shilingi 14 milioni na
Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation
mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia)
wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni.
Mwakilishi wa MO Dewji mkoani
Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Doris Mollel
Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakizindua choo
bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia shilingi 14 milioni
na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
Jengo la choo bora chenye matundu
nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni kwa
ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation
kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi Kibaoni mjini
Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZAZI/WALEZI wakazi wa halmashauri
ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuchangia kwa
hali na mali uboreshaji wa mazingira ya shule, kama njia moja wapo ya
kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa
MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda Mughenyi, wakati akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa,
yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao wavulana ni 377 na wasichana ni
465.
Alisema uzoefu unaonyesha kwamba
mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia
viwepo vya kutosha , maji safi na salama yawepo na vyoo bora
vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea mazingira mazuri wanafunzi ,
kujiendeleza kielimu.
Akifafanua, alisema shule ya msingi
ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na kukosa vyoo kwa ajili ya
wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation na Doris Mollel
Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO Dewji Foundation
kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Doris Mollel (Miss
Singida 2014), alisema Foundation yake itaendelea kufadhili sekta ya
elimu mkoani Singida kama njia ya kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa
kumsapoti na kufanikisha kushinda nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali Mwalimu mkuu wa shule ya
msingi Kindai tarafa ya Mungumaji iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi
Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji Foundation na Doris Mollel
Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi wa choo na kuinusuru
kufungiwa.
“Nitumie nafasi hii pia kulipongeza
shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake wa kufadhili ujenzi wa vyoo
bora ambao ujenzi wake tayari umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa
wazazi,wasaidie kwa hali na mali kuharakisha ujenzi huu”,alisema.
No comments:
Post a Comment