Friday, May 1, 2015

UCHAGUZI CCM 2015: January Makamba: Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

 
 
Na Julius Mtatiro
Kwa ufupi
Yusuph Makamba (baba) ni mwanasiasa nguli na mwenye jina kubwa hapa Tanzania akishikilia nyadhifa nyingi ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Makamba amestaafu siasa akiwa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM. Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni pamoja na ukuu wa mikoa kadhaa kwa nyakati tofauti. Mama mzazi wa January anatokea Mkoa wa Kagera na baba yake anatokea Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Historia yake
January Makamba ni mmoja kati ya vijana machachari katika siasa za Tanzania akiwa na sifa kubwa ya kuendesha siasa za kisasa na zinazowavutia vijana wengi. Makamba alizaliwa Januari 28, 1974 mkoani Singida (ana miaka 41 sasa) na ni mtoto mkubwa kati ya watoto wanne wa Mzee Yusuph Makamba. Kwa sasa January ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Yusuph Makamba (baba) ni mwanasiasa nguli na mwenye jina kubwa hapa Tanzania akishikilia nyadhifa nyingi ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Makamba amestaafu siasa akiwa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM. Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni pamoja na ukuu wa mikoa kadhaa kwa nyakati tofauti. Mama mzazi wa January anatokea Mkoa wa Kagera na baba yake anatokea Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
January alisoma katika Shule za Sekondari Handeni na Galanos mkoani Tanga na kisha akaendelea na kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Forest Hill. Alijiunga na Chuo cha Quincy huko Massachusetts, Marekani kisha akajiunga Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana kilichoko Minnesota - Marekani na kusomea masomo ya amani (peace studies).
Baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza aliendelea na shahada ya pili (uzamili) ya sayansi akibobea katika Uchambuzi na Usuluhishi wa Migogoro kwenye Chuo Kikuu cha George Mason – Marekani, mwaka 2004.
Aliporejea nchini, January alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa Ofisa wa Daraja la Pili. Nyota yake ilianza kung’ara kisiasa pale aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Jakaya Kikwete alipoteuliwa na CCM kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. January alijiunga na timu ya kampeni ya Kikwete na kusafiri na “rais mtarajiwa” nchi nzima.
Baada ya Kikwete kuingia Ikulu, alimteua January kuwa msaidizi wake katika nafasi ya “Msaidizi Binafsi wa Rais Katika Mambo Maalumu”. Alitumikia wadhifa huo kuanzia mwaka 2005 – 2010.
Mbio za ubunge
Aliingia rasmi kwenye siasa mwaka 2010 kwa kuomba ridhaa ya CCM kuwa mbunge wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto.
Kwenye kura za maoni za chama hicho, alimshinda mbunge mzoefu, William Shelukindo kwa kupata kura 14,612 dhidi ya 1,700 za Shelukindo. Baada ya kushinda ndani ya chama chake, January hakukutana na mpinzani yeyote kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na hivyo akaingia kwenye rekodi ya wabunge waliopita bila kupingwa.
Katika Bunge la 10 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na mwaka 2011 chama chake, CCM, kilimteua kuwa katibu wa siasa na uhusiano wa kimataifa akichukua nafasi ya Benard Membe. Alitumikia wadhifa huo ndani ya chama chake hadi mwaka 2012 alipomuachia Dk Asha-Rose Migiro.
Katika Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, January alichaguliwa kuwa kati ya wajumbe 10 wa kamati kuu ya chama hicho kikongwe kutokea upande wa Tanzania Bara akipata kura 2,093.
1 | 2 | 3 | 4 | 5 Next Page

No comments :

Post a Comment