Na Julius Mtatiro
Kwa ufupi
Yusuph Makamba (baba) ni mwanasiasa nguli na mwenye
jina kubwa hapa Tanzania akishikilia nyadhifa nyingi ndani ya Serikali
na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Makamba amestaafu siasa akiwa kwenye
nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM. Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni
pamoja na ukuu wa mikoa kadhaa kwa nyakati tofauti. Mama mzazi wa
January anatokea Mkoa wa Kagera na baba yake anatokea Wilaya ya Lushoto
mkoani Tanga.
Historia yake
January Makamba ni mmoja kati ya vijana machachari
katika siasa za Tanzania akiwa na sifa kubwa ya kuendesha siasa za
kisasa na zinazowavutia vijana wengi. Makamba alizaliwa Januari 28, 1974
mkoani Singida (ana miaka 41 sasa) na ni mtoto mkubwa kati ya watoto
wanne wa Mzee Yusuph Makamba. Kwa sasa January ni Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Yusuph Makamba (baba) ni mwanasiasa nguli na
mwenye jina kubwa hapa Tanzania akishikilia nyadhifa nyingi ndani ya
Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Makamba amestaafu siasa akiwa
kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM. Nyadhifa nyingine alizowahi kushika
ni pamoja na ukuu wa mikoa kadhaa kwa nyakati tofauti. Mama mzazi wa
January anatokea Mkoa wa Kagera na baba yake anatokea Wilaya ya Lushoto
mkoani Tanga.
January alisoma katika Shule za Sekondari Handeni
na Galanos mkoani Tanga na kisha akaendelea na kidato cha tano na sita
katika Shule ya Sekondari ya Forest Hill. Alijiunga na Chuo cha Quincy
huko Massachusetts, Marekani kisha akajiunga Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Yohana kilichoko Minnesota - Marekani na kusomea masomo ya amani (peace
studies).
Baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza
aliendelea na shahada ya pili (uzamili) ya sayansi akibobea katika
Uchambuzi na Usuluhishi wa Migogoro kwenye Chuo Kikuu cha George Mason –
Marekani, mwaka 2004.
Aliporejea nchini, January alijiunga na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa Ofisa wa Daraja la Pili.
Nyota yake ilianza kung’ara kisiasa pale aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Jakaya Kikwete alipoteuliwa na CCM
kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. January alijiunga na
timu ya kampeni ya Kikwete na kusafiri na “rais mtarajiwa” nchi nzima.
Baada ya Kikwete kuingia Ikulu, alimteua January
kuwa msaidizi wake katika nafasi ya “Msaidizi Binafsi wa Rais Katika
Mambo Maalumu”. Alitumikia wadhifa huo kuanzia mwaka 2005 – 2010.
Mbio za ubunge
Aliingia rasmi kwenye siasa mwaka 2010 kwa kuomba ridhaa ya CCM kuwa mbunge wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto.
Kwenye kura za maoni za chama hicho, alimshinda
mbunge mzoefu, William Shelukindo kwa kupata kura 14,612 dhidi ya 1,700
za Shelukindo. Baada ya kushinda ndani ya chama chake, January
hakukutana na mpinzani yeyote kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na
hivyo akaingia kwenye rekodi ya wabunge waliopita bila kupingwa.
Katika Bunge la 10 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na mwaka 2011 chama chake, CCM,
kilimteua kuwa katibu wa siasa na uhusiano wa kimataifa akichukua nafasi
ya Benard Membe. Alitumikia wadhifa huo ndani ya chama chake hadi mwaka
2012 alipomuachia Dk Asha-Rose Migiro.
Katika Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, January
alichaguliwa kuwa kati ya wajumbe 10 wa kamati kuu ya chama hicho
kikongwe kutokea upande wa Tanzania Bara akipata kura 2,093.
No comments:
Post a Comment