Friday, May 1, 2015

BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI ELIMU YA JUU (HESLB), YAANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2015/16



Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi (HELSB) George Nyatega, akizungumza na waandishi wa habari nofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Mei 1, 2015
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.
Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).
Pamoja na mambo mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.
“Waombaji wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.
Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.
Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Wafanyakazi wakishikana mikono kuonyesha mshikamano wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani almaarufu kama "May Day" kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, leo Ijumaa Mei 1, 2015. Sherehe hizo zilifanyika kitaifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambako Rais Jakaya Kikwete, alikuwa mgeni rasmi. Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, Rais amewataka wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupiga kura na akawataka wananchi kjuipigia kura ya ndio katiba pendekezwa


Mashamsham ya siku ya wafanyakazi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ni mbio za kuku hizo, ;picha ya chini pia


Maandamano ya wafanyakazi yakiingia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Doaoma

Mfano wa kikao cha bunge, wafanyakazi wa bunge wakionyesha shughuliza vikao hivyo zinavyoendeshwa

Wajasiriamali wachanganya zege

Maandamano ya wafanyakazi wa mkoa wa Dodoma yakiingia uwanja wa Jamhuri

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akihutubia wananhi uwanja wa Uhuru jijini

Brass band ya JKT Makutupora, ikiongoza maandamano kjuingia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Mpambe wa bunge akionyesha umahiri wake

Wafanyakazi

Mbio za kuku

Rais mstaafu wa Marekani, ambaye sasa anaongoza Wakfu wake (Clinton Foundation), Bill Clinton, akisalimiana na wanachama wa shamba la mfano la Ngongwa, huko mkoani Iringa, wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya kijamii inayofadhiliwa na wakfu wake, Aprili 29, 2015
Clinton alipotembelea kikundi cha Sola Sister wilayani Karatu mkoa wa Arusha

Clinton akisalimiana na matatibu katika zahanati ya Nainokanoka iliyoko wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Zahanati hiyo inafadhiliwa chini ya mpango wa rais huyo wa (Clinton Health Access Initiative-CHAI)

Clinton akitembelea shamba la mfano la Ngongwa mkoani Iringa

Clinton akisalimiana na wanachama wa shamba la mfano Ngongwa lililoko kijiji cha Lugalo mkoani Iringa. Shamba hilo linaendeshwa chini ya ufadhili wa mpango wa maendeleo wa rais huyo wa (Clinton Development Initiative-CDI)

Clinton, akisalimiana na familia ya Wazia Chawala huko kijiji cha Lugalo mloani Iringa wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na wakfu wake wa CDI). Chawala anawafunza wenzake juu ya ukulima bora unavyochangia kuinua kipato chake nahivyo kuyafanya maisha yake kuwa bora zaidi

Meneja wa operesheni kwenye shamba la mfano Ngongwa linalopokea ufadhili kutoka wakfu wa Clinton Foundation (CDI), Otto Ulyate, akimuelezea rais mstaafu Clinton namna bora ya kuvuna maji na kuzuia maji kutawanyika ovyo na kusababisha mmomonyoko wa udongo na kuharibu mazao

Clinton katika mradi wa Ngongwa 
Watoto wakisubiri huduma ya afya kwenye zahanati ya Nainokanoka iliyoko wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha

Clinton akifurahia jambo na akina mama wa kikundi cha solar sister cha wilayani Karatu mkoa wa Arusha. (Picha na Clinton Foundation)

SHEREHE za siku ya wafanyakzi Duniani zinazoadhimisha leo Mei Mosi, kwa maandamano ya furaha   na maonyesho yanayoambatana na hotubaza viongozi, wakazi wa jiji la Dar es Salaam, kwa siku ya pili mfululizo, wanakionacha moto, kufuatia ugumu wa kununua umeme kupitia njia ya wakala wa Tanesco wa kuu za umeme kwenye vituo vya kununulia umeme (LUKU Vending stations) ambapo wnaume, wanawake na watoto wameonekana kwenye misururu mirefu, kwenye vituo hivyo wakisubiri kununua umeme. Ka mujibu wa tangazo la shirika la umeme Tanzania (TANESCO), kupitia kwa wdau wake wa kuuza umeme kilelektroniki, yaani makampuni ya simu, huduma ya kununua umeme kupitia  simu za viganjani imesitishwa kutokana na hitilafu ambazo hazikutajwa bayana, na hivyo ujumbe huo umnewataka wateja wa mitandao hiyo ya simu nikiwemo mimi, kununua umeme kupoitia vituo vya kuuza umeme. Pichani wakazi wa Dar es Salaam, wakiwa kwenye foleni ya kununua umeme kwenye kituo cha Luku kilichoko kituo cha kuuza mafuta Oilcom, Kijitonyama barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Alhamisi Mei 1, 2015

Wananchi kwenye foleni ya Luku


Jaji Francis Mtungi akifunguja mkutano wa wadau wa siasa  wa uimatishaji demokrasia ya vyama vingi
Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.

Dk. Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.
Dk Bana alisema hayo jana akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama vya siasa kwa ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.
Profesa Killian alitaka kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake kuhusu ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini kinastahili kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu ambapo viashiria vipo.
Dk Bana alisema kama watu hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata sheria na kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.
Alisema watu kama wanaona wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo zinaonekana ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu hizo zenye matatizo kwa kufuata utaratibu.
Katika shauri hilo la viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning) ili iweze kukabiliana navyo mapema.
Akizungumzia kama Tanzania ni nchi ya demokrasia Dk. Bana alisema kwamba kuna maendeleo makubwa yamepatikana tangu mtindo wa vyama vingi kuingia nchini miaka 23 iliyopita.
Alisema demokrasia haijengwi kwa siku moja, ina safari ndefu yenye milima na mabonde na wakati mwingine watu wasifike.
Mkurugenzi UNDP Philippe Poinsot  akizungumza katika mdahalo
Mkurugenzi wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na kiraia katika mkutano huo.
Aidha alisisitiza kwamba demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania wanastahili kujivuna kwa hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali ambayo hata mataifa mengine ya Ulaya hayajafikia.
Alisema mwaka 1994 wakati taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na vyama 13 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza kuna vyama 22 vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa umetanuka zaidi.
Pia alisema mafanikio mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuandika inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini kadhia hizo haziondoi ukweli kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari.
Dk bana akizungumza katika mdahalo
Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
Alisema taifa hili halina sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na changamoto zake katika siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa unazidi kutanuka.
Alisema pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.
Alisema kutanuka kwa wigo wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa) kunatakiwa kwenda sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi wa utamaduni wa vyama vingi.
Alisema pia kuna haja ya kuimarishwa kwa taasisi zinazosaidia utamaduni huo kama Tume huru ya Uchaguzi, Bunge na hata mfumo wa utawala ambapo wakuu wa mikoa na wilaya wasiwe katika hali ya kikada bali wale wanaoweza kutekeleza majukumu yanayostahili katika maeneo yao.
jaji Mutungi akiwa na Mkurugenzi UNDP Poinsot
Jaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.
Aidha alisema kwamba vyama vingi vya siasa vinafanyakazi ya uanaharakati badala ya kuwa na itikadi ya kuifuata .
Alizungumzia pia haja ya vyama vya upinzani kujivunja na kuanzisha chama kimoja na kutengeneza mkakati wa kutwaa dola huku akisema muungano wa Ukawa kwa sasa una mushkeri zaidi badala ya kusaidia kujiandaa kutwaa dola.
Katika mdahalo huo ambao ulielezwa na Msajili wa vyama vya Siasa jaji Francis Mutungi, si mkusanyiko wa kufanya kampeni ya uchaguzi bali jukumu la ofisi ya msajili hasa kuelekea uchaguzi mkuu, washiriki wake pia walielezwa changamoto za siasa za vyama vingi.
Profesa Rugumamu alisema kwamba katika tafiti aliyoifanya yeye na wenzake katika nchi 15 za bara la Afrika wamekumbana na changamoto takribani saba ambazo ni kikwazo katika kupata na kukuza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
IMG_4917
Jopo la wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana, Profesa Meena, Profesa Rugumamu na mwishoni ni msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Miongoni mwa changamoto hizo ni vyama vikongwe na utamaduni wake kushindwa kuainisha kati ya mamlaka ya dola na vyama vyenyewe, kuwepo kwa vyama vya kikanda na kidini katika kipindi cha mpito katika demokrasia ya vyama vingi, wanasiasa kubadili katiba waendelee kutawala, vyama na wanachama kutojua haki na wajibu wao kutokana na kutofundishwa uraia tangu awali.
Pia alizungumza uadui unaojijenga kwa nchi ambazo zimetoka vitani na uanzishaji wa makundi ya ulinzi ya vyama ambavyo husababisha mitafaruku wakati wa uchaguzi au kwenye uchaguzi na matumizi ya fedha yasiyojulikana kwa ama kukosa sheria au sheria kuwapo na watu kutoizingatia.
Alisema dosari zote hizo zinatikisa ujenzi wa utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
Awali akimkaribisha Jaji Mutungi kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot alisema Umoja wa mataifa umefurahishwa kwa wadau wa siasa nchini Tanzania kuwa na mazungumzo yenye lengo la kustawisha amani kuelekea uchaguzi na kutengeneza mfumo wa majadiliano kama kukiwepo na kutokuelewana.
Alisema mkutano huo walioufadhili ni sehemu ya makubaliano ya Ofisi ya Msajili na UNDP kupitia mradi wake wa kuimarisha demokrasia (DEP) yenye kulenga kujenga uwezo na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maelewano ndani ya vyama na kitaifa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
IMsimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian
Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Alisema ni matumaini yake kwamba mkutano huo utatengeneza mustakabari bora wa Tanzania kuwa na uchaguzi huru na wa amani.
Alisema kutokana na ushindani, uchaguzi unaweza kuleta matata kwa hiyo ni vyema kama wadau wataliangalia hilo na kuona namna ya kutanzua matata ili taifa libaki na amani na kusonga mbele katika maeneo yote ya jamii.
Naye Jaji Mutungi aliwaasa washiriki kutambua kwamba hakuna sababu ya kukamiana na kukomoana miongoni mwa vyama vya siasa kwani wote wanajenga nyumba moja na kimsingi hawana sababu ya kugombania fito.
Alitaka wadau kucheza mchezo wa siasa kwa maridhiano ili wasibomoe misingi ya amani ya taifa na mafanikio yake.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuweka sawa dhana ya demokrasia ya vyama vingi na kutafuta majibu ya changamoto zinazokabili pasipo kuvunja amani ya nchi.
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.
Profesa Rugumamu akizungumza
Profesa Rugumamu akizungumza.
IMG_4861
Baadhi ya washiriki wakijadiliana.
Washiriki wa mkutano wakijadiliana.


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishara ya makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini Harare, Zimbabwe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini Harare, Zimbabwe jana April, 29, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC jana. Picha na OMR


Rais Jakaya Kikwete, leo Alhamisi Aprili 30, 2015, amepokea hati za utambulisho (credentials), za mabalozi wanne wapya, waliokuja nchini kuziwakilisha nchi zao, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, balozi wa kwanza kuwasilisha hati zake, alikuwa ni balozi wa Australia mwenye makazi yake nchini Kenya, John Mathew Feakes, akifuatiwa na balozi wa Algeria, Saad Belabed, na baadaye aliyewasilisha hati zake alikuwa ni balozi wa Russia, Yuri F.Popov. Balozi wa mwisho kuwasilisha hati zake, alikuwa ni balozi wa Japan, Masaharu Yoshida. Mabalozi wote walipokelewa kwenye viwanja vya Ikulu na Mnikulu, Shaaban Gurumo, na baadaye kila mmoja alipigiwa wimbo wa taifa na ule wa taifa lake. Pichani, balozi wa Japan akiwasilisha hati zake

Rais akipokea hati za balozi wa Australia, John Mathew Feakes

Rais akipiga picha na balozi wa Russia, Yuri F. Popov

Rais akipiga picha na balozi wa Algeria, Saad Belabed

Rais akatika mazungumzo na balozi Yoshida

Rais akizungumza na balozi wa Algeria, Saad

Rais akizungumza na balozi wa Australia, John Mathew Feakes

Rais, Jakaya Kikwete, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, (wapili kushoto), balozi wa Japan nchini Yoshida, katuka poicha ya pamoja na maafisa toka ubalozini na mmoja toka wizara ya mambo ya nje

Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa serikali

Balozi Yuri akisaini kitabu cha wageni Ikulu

Balozi John Mathew, akisaini kitabu cha wageni

Balozi Yoshida, akisaini kitabu cha wageni

Balozi Saad, akipokea saluti wakati wa kupigwa wimbo wa mataifa ya Algeria na Tanzania

Balozi, Yuri na Mnikulu Shaaban Gurumo, wakisimama kwa heshima wakati wa kupigwa nyimbo za mataifa ya Russia na Tanzania


1 comment :

  1. Unatafuta kampuni halisi ya mkopo wa kifedha ili kupata mkopo wa euro 10,000 hadi euro 10,000,000 (kwa mikopo ya biashara au biashara, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya nyumba, mikopo ya gari, mikopo ya uimarishaji wa madeni, mikopo ya mtaji wa mradi, mikopo ya afya nk. ))Au ananyimwa mkopo kutoka benki au taasisi ya fedha kwa sababu yoyote ile?Tuma ombi sasa na upate mkopo halisi wa kifedha. Imechakatwa na kuidhinishwa ndani ya siku 3. KAMPUNI YA PACIFIC FINANCIAL MKOPO

    Sisi ni wakopeshaji wa mkopo wa kimataifa ambao hutoa fedha halisi kwa watu binafsi na makampuni kwa riba ya chini ya 2% tukiwa na kitambulisho halali au pasipoti ya kimataifa ya nchi yako ili kuthibitishwa. Malipo ya mkopo huanza saa 1 (moja) baada ya mkopo kupokelewa. na muda wa kulipa ni miaka 3 hadi 35.

    Kwa jibu la haraka na kushughulikia ombi lako la mpaka ndani ya siku 2 za kazi
    Wasiliana nasi moja kwa moja kupitia barua hii: pacififinancialloanfirm@gmail.com

    Wasiliana nasi kwa maelezo yafuatayo:

    Jina kamili: ____________________________
    Kiasi cha pesa kinachohitajika kama mkopo: _______________
    Muda wa mkopo: ___________________________________
    Madhumuni ya mkopo: ____________________
    Siku ya kuzaliwa: ___________________________________
    Jinsia: ______________________________
    Hali ya Ndoa: ___________________________________
    Anwani ya mawasiliano: ___________________________________
    Mji / Msimbo wa Eneo: ___________________________________
    Nchi: ______________________________
    Kazi: ___________________________________
    Simu ya rununu: __________________________

    Tuma ombi lako la jibu la haraka kwa: pacififinancialloanfirm@gmail.com
    asante

    Afisa Mtendaji Mkuu :Pen Fed VICTORIA JOHNSON

    ReplyDelete