Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi (HELSB) George Nyatega, akizungumza na waandishi wa habari nofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Mei 1, 2015 |
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) leo (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji
wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/2016
unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao
unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz),
waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu,
Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.
Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na
ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia
mfumo maalum (Online Loans Application and Management System) ulioanzishwa na
HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya
Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).
Pamoja na mambo mengine, mwongozo huo
unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa
ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala
(Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.
“Waombaji wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa
ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa
nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi hiyo.
Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa
wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za
elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.
Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine
kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha
maombi.
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9
ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu
mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za
elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote
iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati
Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.
Mashamsham ya siku ya wafanyakazi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ni mbio za kuku hizo, ;picha ya chini pia |
Maandamano ya wafanyakazi yakiingia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma |
Doaoma |
Mfano wa kikao cha bunge, wafanyakazi wa bunge wakionyesha shughuliza vikao hivyo zinavyoendeshwa |
Wajasiriamali wachanganya zege |
Maandamano ya wafanyakazi wa mkoa wa Dodoma yakiingia uwanja wa Jamhuri |
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akihutubia wananhi uwanja wa Uhuru jijini |
Brass band ya JKT Makutupora, ikiongoza maandamano kjuingia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma |
Mpambe wa bunge akionyesha umahiri wake |
Wafanyakazi |
Mbio za kuku |
Clinton alipotembelea kikundi cha Sola Sister wilayani Karatu mkoa wa Arusha |
Clinton akitembelea shamba la mfano la Ngongwa mkoani Iringa |
Clinton katika mradi wa Ngongwa |
Watoto wakisubiri huduma ya afya kwenye zahanati ya Nainokanoka iliyoko wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha |
Clinton akifurahia jambo na akina mama wa kikundi cha solar sister cha wilayani Karatu mkoa wa Arusha. (Picha na Clinton Foundation) |
Wananchi kwenye foleni ya Luku |
Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
Dk. Benson Bana wa Chuo
Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa
amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani
kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.
Dk Bana alisema hayo jana
akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la kuimarisha
demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama vya siasa kwa
ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.
Profesa Killian alitaka
kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake kuhusu
ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini kinastahili
kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu ambapo viashiria
vipo.
Dk Bana alisema kama watu
hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata sheria na
kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.
Alisema watu kama wanaona
wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo zinaonekana
ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu hizo zenye
matatizo kwa kufuata utaratibu.
Katika shauri hilo la
viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya
kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa
kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning)
ili iweze kukabiliana navyo mapema.
Akizungumzia kama Tanzania
ni nchi ya demokrasia Dk. Bana alisema kwamba kuna maendeleo makubwa
yamepatikana tangu mtindo wa vyama vingi kuingia nchini miaka 23
iliyopita.
Alisema demokrasia haijengwi kwa siku moja, ina safari ndefu yenye milima na mabonde na wakati mwingine watu wasifike.
Mkurugenzi
wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe
Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na
kiraia katika mkutano huo.
Aidha alisisitiza kwamba
demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania wanastahili kujivuna kwa
hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali ambayo hata mataifa mengine
ya Ulaya hayajafikia.
Alisema mwaka 1994 wakati
taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na vyama 13 kwa ajili
ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza kuna vyama 22
vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa umetanuka zaidi.
Pia alisema mafanikio
mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuandika
inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la kufungiwa kwa gazeti la
Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini kadhia hizo haziondoi ukweli
kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari.
Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
Alisema taifa hili halina
sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na changamoto zake katika
siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa unazidi kutanuka.
Alisema pamoja na
mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni
wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na aidolojia
(itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa
na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.
Alisema kutanuka kwa wigo
wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa) kunatakiwa kwenda
sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi wa utamaduni wa
vyama vingi.
Alisema pia kuna haja ya
kuimarishwa kwa taasisi zinazosaidia utamaduni huo kama Tume huru ya
Uchaguzi, Bunge na hata mfumo wa utawala ambapo wakuu wa mikoa na wilaya
wasiwe katika hali ya kikada bali wale wanaoweza kutekeleza majukumu
yanayostahili katika maeneo yao.
Jaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.
Aidha alisema kwamba vyama vingi vya siasa vinafanyakazi ya uanaharakati badala ya kuwa na itikadi ya kuifuata .
Alizungumzia pia haja ya
vyama vya upinzani kujivunja na kuanzisha chama kimoja na kutengeneza
mkakati wa kutwaa dola huku akisema muungano wa Ukawa kwa sasa una
mushkeri zaidi badala ya kusaidia kujiandaa kutwaa dola.
Katika mdahalo huo ambao
ulielezwa na Msajili wa vyama vya Siasa jaji Francis Mutungi, si
mkusanyiko wa kufanya kampeni ya uchaguzi bali jukumu la ofisi ya
msajili hasa kuelekea uchaguzi mkuu, washiriki wake pia walielezwa
changamoto za siasa za vyama vingi.
Profesa Rugumamu alisema
kwamba katika tafiti aliyoifanya yeye na wenzake katika nchi 15 za bara
la Afrika wamekumbana na changamoto takribani saba ambazo ni kikwazo
katika kupata na kukuza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
Jopo la wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana,
Profesa Meena, Profesa Rugumamu na mwishoni ni msimamizi wa mdahalo
Prof Bernadetta Killian.
Miongoni mwa changamoto
hizo ni vyama vikongwe na utamaduni wake kushindwa kuainisha kati ya
mamlaka ya dola na vyama vyenyewe, kuwepo kwa vyama vya kikanda na
kidini katika kipindi cha mpito katika demokrasia ya vyama vingi,
wanasiasa kubadili katiba waendelee kutawala, vyama na wanachama kutojua
haki na wajibu wao kutokana na kutofundishwa uraia tangu awali.
Pia alizungumza uadui
unaojijenga kwa nchi ambazo zimetoka vitani na uanzishaji wa makundi ya
ulinzi ya vyama ambavyo husababisha mitafaruku wakati wa uchaguzi au
kwenye uchaguzi na matumizi ya fedha yasiyojulikana kwa ama kukosa
sheria au sheria kuwapo na watu kutoizingatia.
Alisema dosari zote hizo zinatikisa ujenzi wa utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
Awali akimkaribisha Jaji
Mutungi kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot
alisema Umoja wa mataifa umefurahishwa kwa wadau wa siasa nchini
Tanzania kuwa na mazungumzo yenye lengo la kustawisha amani kuelekea
uchaguzi na kutengeneza mfumo wa majadiliano kama kukiwepo na
kutokuelewana.
Alisema mkutano huo
walioufadhili ni sehemu ya makubaliano ya Ofisi ya Msajili na UNDP
kupitia mradi wake wa kuimarisha demokrasia (DEP) yenye kulenga kujenga
uwezo na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maelewano ndani
ya vyama na kitaifa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Alisema ni matumaini yake kwamba mkutano huo utatengeneza mustakabari bora wa Tanzania kuwa na uchaguzi huru na wa amani.
Alisema kutokana na ushindani, uchaguzi
unaweza kuleta matata kwa hiyo ni vyema kama wadau wataliangalia hilo na
kuona namna ya kutanzua matata ili taifa libaki na amani na kusonga
mbele katika maeneo yote ya jamii.
Naye Jaji Mutungi aliwaasa washiriki
kutambua kwamba hakuna sababu ya kukamiana na kukomoana miongoni mwa
vyama vya siasa kwani wote wanajenga nyumba moja na kimsingi hawana
sababu ya kugombania fito.
Alitaka wadau kucheza mchezo wa siasa kwa maridhiano ili wasibomoe misingi ya amani ya taifa na mafanikio yake.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuweka
sawa dhana ya demokrasia ya vyama vingi na kutafuta majibu ya changamoto
zinazokabili pasipo kuvunja amani ya nchi.
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.
Profesa Rugumamu akizungumza.
Baadhi ya washiriki wakijadiliana.
Washiriki wa mkutano wakijadiliana.
Rais akipokea hati za balozi wa Australia, John Mathew Feakes |
Rais akipiga picha na balozi wa Russia, Yuri F. Popov |
Rais akipiga picha na balozi wa Algeria, Saad Belabed |
Rais akatika mazungumzo na balozi Yoshida |
Rais akizungumza na balozi wa Algeria, Saad |
Rais akizungumza na balozi wa Australia, John Mathew Feakes |
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa serikali |
Balozi Yuri akisaini kitabu cha wageni Ikulu |
Balozi John Mathew, akisaini kitabu cha wageni |
Balozi Yoshida, akisaini kitabu cha wageni |
Balozi Saad, akipokea saluti wakati wa kupigwa wimbo wa mataifa ya Algeria na Tanzania |
Balozi, Yuri na Mnikulu Shaaban Gurumo, wakisimama kwa heshima wakati wa kupigwa nyimbo za mataifa ya Russia na Tanzania |
Unatafuta kampuni halisi ya mkopo wa kifedha ili kupata mkopo wa euro 10,000 hadi euro 10,000,000 (kwa mikopo ya biashara au biashara, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya nyumba, mikopo ya gari, mikopo ya uimarishaji wa madeni, mikopo ya mtaji wa mradi, mikopo ya afya nk. ))Au ananyimwa mkopo kutoka benki au taasisi ya fedha kwa sababu yoyote ile?Tuma ombi sasa na upate mkopo halisi wa kifedha. Imechakatwa na kuidhinishwa ndani ya siku 3. KAMPUNI YA PACIFIC FINANCIAL MKOPO
ReplyDeleteSisi ni wakopeshaji wa mkopo wa kimataifa ambao hutoa fedha halisi kwa watu binafsi na makampuni kwa riba ya chini ya 2% tukiwa na kitambulisho halali au pasipoti ya kimataifa ya nchi yako ili kuthibitishwa. Malipo ya mkopo huanza saa 1 (moja) baada ya mkopo kupokelewa. na muda wa kulipa ni miaka 3 hadi 35.
Kwa jibu la haraka na kushughulikia ombi lako la mpaka ndani ya siku 2 za kazi
Wasiliana nasi moja kwa moja kupitia barua hii: pacififinancialloanfirm@gmail.com
Wasiliana nasi kwa maelezo yafuatayo:
Jina kamili: ____________________________
Kiasi cha pesa kinachohitajika kama mkopo: _______________
Muda wa mkopo: ___________________________________
Madhumuni ya mkopo: ____________________
Siku ya kuzaliwa: ___________________________________
Jinsia: ______________________________
Hali ya Ndoa: ___________________________________
Anwani ya mawasiliano: ___________________________________
Mji / Msimbo wa Eneo: ___________________________________
Nchi: ______________________________
Kazi: ___________________________________
Simu ya rununu: __________________________
Tuma ombi lako la jibu la haraka kwa: pacififinancialloanfirm@gmail.com
asante
Afisa Mtendaji Mkuu :Pen Fed VICTORIA JOHNSON