Pages

Friday, May 1, 2015

RAIS DR. SHEIN AONGOZA KILELE CHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI


SH1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba aliposhiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.]
SH2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana Viongozi wa Chama CCM wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba aliposhiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.] SH3Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi   wakati alipowasili katika  Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo ,[Picha na Ikulu.] SH4Maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi Kisiwani Pemba yakiingia katika uwanja wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chakechake leo wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani na kupokelewa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) [Picha na Ikulu.] SH5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipunga mkono kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi kisiwani Pemba wakati akilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.] SH6Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipunga mkono kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi kisiwani Pemba wakati wa Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.] SH7Wafanyakazi wa Wizara ya Afya Kisiwani  Pemba wakipita mbele ya Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya  wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi wakati wa Kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.] SH8Wafanyakazi wa ZSTC Pemba wakipita mbele ya  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya  wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi wakati wa Kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.]
SH9Viongozi mbali mbali na wafanyakazi wakiwa katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba wakati wa sherehe za Siku ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo mgeni rasmi akiwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein [Picha na Ikulu.] SH10Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) pamopja na Viongozi wengine wakinyanyua mikono  juu wakati wakiimba wimbo maalum wa Mshikamano (Solidarity Forever) wakati wa kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani sherehe zilizofanyika leo Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba,[Picha na Ikulu.] SH11Viongozi na Wafanyakazi Mbali mbali wakishikamana kunyanyua mikono juu wakiimba kwa pamoja na kuimba wimbo maalum wa Mshikamano (Solidarity Forever) wakati wa kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani sherehe zilizofanyika leo Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba,[Picha na Ikulu.]]

Dk Ali Mohammed Shein awataka vijana kutokubali kudanganywa na baadhi ya wanasaiasa

imagesNa Masanja Mabula -Pemba .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein amewataka vijana kutokubali kudanganywa na baadhi ya wanasaiasa kwamba wanao uwezo wa kutoa ajira na kuwasihi kutumia fursa ya uwepo wa sekta binafisi kukabiliana na tatizo hilo .
Amesema tatizo la ajira linaikabili dunia nzima na kusema kuwa mwarubaini wa kutibu tatizo hilo ni kwa vijana kujiajiri wenyewe kupitia seka ya kilimo , uvuvi , ufugaji na utalii .
Dk Shein ameyasema hayo kwenye maadhisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambapo kwa Zanzibar yamefanyika kwenye ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya Makonyo Wawi Wilaya ya Chake Chake .
Amesema kuwa dhana ya kutegemea ajira kutoka Serikalini zimepita na wakati na kwani vijana wanaomaliza masomo ni wengi kulingana na nafasi za ajira zilizopo .
“Nawaomba vijana msidanganywe na mkadanganyika hakuna mtu awezaye kuleta miujiza ya kuwaajiri vijana wote wanaomaliza masomo yao , njia pekee ni kujiajii wenyewe kupitia sekta binafsi ikiwemo kilimo , utalii , mifugo na uvuvi ” alifahamisha .
Aidha amesema kuwa hakuna upendeleo wakati wa kuajiri na kuongeza kwamba nafasi za ajira hutangazwa na tume ya utumishi na ajira hutegemea na kiwango na vigezo vyua muombaji .
Ameeleza kwamba vijana wanaomaliza masomo kila mwaka ni zaidi ya elfu tano na serikali htoa ajira 2,500 kwa mwaka nafasi ambazo haziwezi kuchukua vijana hao .
“kila mwaka ni vijana zaidi ya elfu tano wanaomaliza masomo yao , na nafasi za ajira ambazo serikali hutoa kila mwaka ni 2,500 , hivyo itakuwa ni vigumu kuweza kuwaajiri vijana wote kulingana na uchache wa nafasi ” alieleza Dk Shein .
Amezidi kueleza kwamba tangu Serikali ya awamu ya saba iingie madarakani mwaka 2,010 , jumla ya ajira 25,019 zimetolewa kwa vijana ambapo kati ya hizo 20,169 zimetokana na sekta binafsi na 4,850 pekee ndiyo zilizotolewa na Serikali.
Akizungumzia suala la malimbikizi ya mishahara na posho kwa walimu , dk Shein amesema kuwa tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi katika bajeti ijayo pamoja na kuangaliwa uwezekano wa kuongeza mshahara kwa watumishi wa serikali na binafsi .
“Tatizo la malimbikizi ya mishahara na maposho ya walimu litamalizika katika bajati ijayo napenda kuahidi kwamba malipo hayo yatalipwa na pia tutangalia uweekano wa kuongeza mshahara pindi hali ya uchumi ikiruhusu” aliongeza Dk Shein .
Mapema Waziri wa nchi Ofisi ya Rais , Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman ameeleza kwamba katika kipindi cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya saba imefannya mabadiliko ya mishahara mara tatu kwa wafanyakazi na watumishi wa serikali .
Amefahamisha mabadailiko hayo yamendana na sifa , ikiwemo elimu na muda wa utumishi mabadaliko ambayo yamewawezesha wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi kupunguza ukali wa maisha .
‘Tumefanya mabadiliko mara tatu ya mishahara tangu Serikali ya Mapinduzi ya awamu ya saba aiingie madarakani , ni jambo la kujivunia ” alifahamisha Haroun .
Katika risala ya wafanyakazi wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuondoa kodi kwa malipo ya wastaafu pamoja na kuongeza kiwango cha mshahara ili kuondoa tofauti iliyopo hivi sasa .

WAFANYAKAZI WAHIMIZWA KUJITOKEA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.

Hayo yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe kuhamasisha wafanyakazi.

Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
 Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika maandamano kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI huku wakiwa na bango lenye ujumbe wao mahususi kuwahamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha na wapige kura kuchagua kiongozi bora.
 Wafanyakazi wa Mamlaka  ya anga nao  hawakuwa nyuma na mabango yao.
 Wafanyakazi wa Ofsi ya Rais – Ikulu…
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege ya Air Tanzania…
Mabango mbalimbali yamebeba kaulimbiu juu ya kuhamasisha wafanyakazi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura km. Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa wa Zamani (Picha na Christina Njovu).

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa amewataka wananchi kuisoma na kuilewa katiba inapendekezwa

                        Mkuu wa wilaya ya Korogwe HAFSA MTASIWA
         Mkuu wa wilaya ya Korogwe HAFSA MTASIWA
……………………………………………………….

Na Fredy Mgunda,Iringa
Wanachi wa mkoa wa tanga wilaya ya korogwe wametakiwa kuisoma
na kuilewa katiba inapendekezwa ili waweze kuipigia kura.
 
Akizungumza
na blog hii mkuu wa wilaya ya korogwe HAFSA MTASIWA awataka wananchi wa wilaya
hiyo kusoma na kuijadili katiba hiyo na kutosikiliza kutoka kwa watu.
 
Aidha
MTASIWA amesisitiza kuwa Tanzania bado tunakatiba yetu na tupo kwenye mchakato
wa kupata katiba mpya hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na maneno wanayo
ambiwa na watu wengine.
 
“Katiba
inayopendekezwa imeandikwa na binadamu wa kawaida kama ilivyokuwa hapo awari
katika katiba ambayo inatumika hadi sasa lakini inapaswa kuangalia kuna mambo
gani mapya ambayo yameandikwa kwenye katiba inayopendekezwa na imebeba mambo
gani muhimu katika maendeleo ya Tanzania yetu”.alisema mtasiwa
 
Lakini
MTASIWA ameendelea kuwataka watanzania kwa ujumla kuendelea kuidhamini amani
tulivyo nayo kwa sasa na tusiwafuate wananchi wengi wenye lengo la kuvuruga
amani yetu kwa maslai yao binafsi hivyo watanzania msidaganyike kwa maneno yao.
 
MTASIWA amewaomba
wazazi wote kuwapa elimu ya kutosha watoto wao juu ya kutunza amani na kuacha
tabia ya kushabikia maneno ya uchochezi yenye lengo la kuvuga amani yetu.
 
Wakati
huohuo MTASIWA amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujua umuhimu wa kutumia bima
na wajitokeze kuchangia katika mifuko ya bima.
 
Bima ya afya
inafaida kubwa sana katika maisha yako hivyo lazima wananchi watambue umuhimu
wa kuchangia bima kwa kuwa serikali imepanga kuwachangia wananchi kwa kiasi
kile ambacho wamekichanga kwa mfano wananchi wakichanga milioni 100 na serikali
itatoa milioni 100 kwa lengo la kuboresha sekta ya afya.alisema MTASIWA.
 

WAZABUNI WAGOMA KULISHA SHULE YA ILBORU KUTOKANA NA MADENI

Na Gladness Mushi, Arushaindex
Katika hali isiyokuwa ya kawaida shule ya vipaji maalumu ya Ilboru
iliopo Jijini Arusha inakabiliwa na tatizo la chakula cha wanafunzi
kutokana na wazabuni kujitoa kupeleka chakula shuleni hapo kwa muda
sasa.
Pia kinacho sababisha wazabuni kujitoa kwenye suala hilo ni kutokana
na kushindwa kulipwa madeni yao kwa wakati maalumu hali ambayo nayo
inawafanya washindwe kuendeleza kazi zao za kila siku hasa za
biashara.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shule hiyo Julius Shula kwenye maafali
ya 23 ya kidato cha sita wakati akiongea na wazazi, walezi wa
wanafunzi hao mapema jana.
Shula alisema kuwa shule hiyo imekuwa na changamoto kubwa sana ya
uhaba wa chakula hali ambayo wakati mwingine inasababisha walimu ambao
ni walezi wakuu wa wanafunzi hao kuwa katika wakati mgumu
ukilinganisha kuwa shule hiyo ni ya vipaji maalumu.
“madeni ambayo bado hajalipwa na serikali yamesababisha wazabuni ambao
walikuwa wanasambaza chakula hapa shuleni kuweza kusitisha huduma yao
hivyo basi kuna umuhimu hata wa wazazi nao kuweza kuangalia namna ya
kuwanusuru wanafunzi dhdii ya njaa”aliongeza mkuu huyo.
Aliwaomba  wadau wa elimu kuweza kuangalia suala hilo kwa undani na
kisha kutoa misaada ya vyakula kwani wanafunzi hao wakipata chakula
bora pia wataweza kuwa vizuri kwenye masomo yao ya kila siku.
Katika hatua nyingine alisema kuwa mbali na tatizo hilo la uhaba wa
chakula lakini pia kuna changamoto ya ukosefu wa uzio wa shule ambapo
pia wanafunzi wapo hatarini sana kuiga tabia za watu wa nje ambao mara
zote wanatumia njia ambazo wanafunzi nao wanazitumia.
“shule yetu ilijengwa Miaka mingi sana sasa mazingira ya wakati ule na
wakati huu ni tofauti sana hivyo basi kwa sasa vijana hawa wanahitaji
ulinzi sana kutokana na hata maadili yenyewe yalivyooyumba na kama
kila mtu atakuwa anakatisha hatuwezi kujua mwema ni yupi na mbaya ni
yupi hivyo basi tunaomba jamii iweze kuliangalia suala hilo”aliongeza
Mkuu huyo
Awali wahitimu hao waliwaomba wadau mbalimbali kuweza kuatatua
changamoto ambazo zimedumu na kuwafanya wanafunzi kushindwa kufuraia
mazingira ya shule na badala yake kujikuta wakiwa na hofu sana.
Wakitolea mfano wa mazingira ambayo yanawapa hofu pindi wanapokuwa
kwenye mazingira ya shule ni pamoja na miundombinu mibaya ya
umeme(Wiring System)ambayo ipo kwenye mabweni , nyumba za watumishi na
hata madarasa ambapo pia uchakavu huo umedumu kwa miaka mingi sana.
Naye mgeni rasmi Philemon Mollel”Monaban”alisema kuwa amechukua
changamoto zote hizo na atazifanyia kazi kwani elimu ni muhimu sana
kwenye maisha ya vijana wa sasa na ili vijana waweze  kufanya vema
kwenye mithiani yao hata ya mwisho kunahitajika kuwepo na mazingira
mazuri na imara.

Mratibu wa asasi ya Better Living Aid atoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi!

Watangazaji Hamisa Mussa Lubilo na Deogratius Yagomba wa VOT fm 89.0 wakimuuliza maswali mratibu wa asasi ya Better Living Aid walipomualika leo asubuhi katika kipindi cha Meza huru!
Mratibu wa asasi ya kiraia ya Better Living Aid Bw Mkala Fundikira leo akiwa amavalia fulana ya mkakati wa Imetosha unaopinga mauaji dhidi ya watu wenye ualbino ambao yeye ni mjumbe wa kamati kuu, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi mjini Tabora waiunge mkono asasi yake inayodhamiria kujenga vyoo na zahanati katika kijiji  cha Amani kilichopo Ipuli Tabora, kijiji chenye wakazi wazee na wasiojiweza na waishio na gonjwa sugu la ukoma. Alitoa wito huo akiongea katika kipindi cha meza huru cha Vot fm89.0 alisema “nawaomba wenye maduka ya vifaa vya ujenzi watuunge mkono kwa kuchangia hata mifuko mitano ya simenti, bati mbili au hata kifaa chochote cha ujenzi ambacho kitataumika katika ujenzi wa vyoo na zahanati katika kijiji hicho alimradi tunahitaji michango ya aina yeyote ile” 
Mkala Fundikira akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na watangazaji wa kipindi cha Meza huru, kipindi kinachoruka ktk kituo cha redio cha VOT fm 89.0 ya Tabora leo asubuhi.
Pamoja na kueleza kuwa asasi yao inayoundwa na marafiki toka mitandao ya jamii kama Facebook  na Viber pia alieleza kuwa tangu waanze kusadia kijiji hicho washapeleka vyakula, vyandarua na masweta kwa nyakati tofauti, pia ikiwemo kulipia upulizwaji wa dawa za kuuwa wadudu pamoja na kunguni ambao walikuwa wakisumbua wakazi wa kijiji cha Amani. 
Mkala akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wenye kupinga mauaji kwa watu wenye ualbino ya mkakati wa Imetosha.
Alipoulizwa dhamira ya asasa yao ni kusaidia Tabora tu au na mikoa mingine? Mratibu huyo alijibu “Hapana, Better Living Aid itasaidia na kwingineko pia, kwa mfano tunatafuta wahisani ili tukajenge zahanati kijijini Masweya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Masweya hakuna zahanati pamoja na kuwa pana wakazi zaidi ya 7000, nafikiri wa Tanzania tuwe wahalisia kuwa serikali yetu haitoweza kukidhi mahitaji ya wa Tanzania wote kwa wakati mmoja hivyo basi ni wakati muafaka wa sisi kama jamii kuanza kujitolea na kuwezesha asasi kama yetu kupeleka huduma za afya sehemu kama Masweya”
Fundikira pia alimshukuru Mh Munde Tambwe Abdallah kwa kutoa ahadi ya Mifuko 50 ya simenti, lori 10 za mchanga pamoja na tano za mawe na kokoto , alisema “Tena kabla sijasahau nimpongeze na kumshukuru sasa sana sana Mh Munde Tambwe kwa kutupa msaada ambao ni msingi, kwa maana ya kuwa ahadi yake ndiyo itaanzisha ujenzi wa majengo hayo ya vyoo na zahanati, hivyo basi na wengine wajitolee ili tusonge mbele” 
Hoteli ambamo chakula cha usiku cha uchangishaji fedha kwa ujenzi wa vyoo na zahanati utafanyika baadae mwezi huu jijini Dar es Salaam iliyopo maeneo ya Ocean road.
Aidha asasi hiyo ina mpango wa kuandaa chakula cha usiku jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Southern Sun baadae mwezi huu ambapo Mh Samuel Sitta(waziri wa uchukuzi) amekubali kuwa mgeni rasmi, karamu hiyo itaandaliwa ili kuchangisha fedha za kuwezesha miradi hiyo iweze kukamilika. “Bado tupo kwenye hatua za mwanzo za maandalizi lakini tunataraji karamu hiyo ya uchangishaji pesa ifanyike ama mwishoni mwa mwezi wa MEI au mwanzoni mwa mwezi Juni 2015. Pia Fundikira aliwashukuru Mh Aden Ragen(Mbunge wa Tabora mjini), Mh Munde Tambwe(Viti maalum), Sylvester Koka(Mbunge wa Kibaha) na wanachama na wote wa Better Living Aid kwa kuwezesha kifedha upulizwaji wa dawa kijiji cha Amani uliogharimu Tsh Laki 980.
Tembelea mtandao wa betterlivingaid.Blogspot.Com ujue zaidi kuhusu asasi hii na malengo yake au piga namba 0754 666620 kwa maelezo.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI UKISHIRIKIANA NA PROIN PROMOTIONS WAZINDUA RASMI MANUNUZI YA FILAMU ZA KITANZANIA ONLINE

 Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johson Lukaza akizungumza machache na kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Diodorus Kamala[l] akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali katika uzinduzi wa filamu za kitanzania ambazo sasa zitakuwa zikiuzwa online.sherehe hizo za uzinduzi ambazo zilifanyika jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Dr.Pendo akifanya mahojiano machache na Mheshimiwa Emmanuel kuhusiana na Filamu za kitanzania ambazo zitakuwa ziliuzwa mitandaoni pipote duniani.
Mwenyekiti wa Proin Promotion Tanzania ndugu Johson Lukaza [r] akiwa na viongozi wa Kitanzania nchi Ubelgiji katika sherehe za uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania onlione.
Kiongozi wa watanzania nchini Ubelgiji bwana Macha[r] akiwa na kiongozi wa watanzania jijini Antwerpen kwenye uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online popote duniani
Mwenyekiti wa Proin Promotion bwana Johnson Lukaza [l] akiwa na mmoja wa wageni waalikwa katika uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online jijini Brussel nchini Ubelgiji hapo jana.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mheshimiwa Dr.Kamala akibadilishana mawazo na wageni wake mara tu baada ya uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online duniani kote.Balozi ni mmoja wa washiriki waliofanikisha shughuli nzima ya uzinduzi huo.
Warembo kutoka mataifa mbalimbali walikuwepo kwenye uzinduzi huo hapo jana.kwa manunuzi ya filamu zote za kitanzania sasa waweza kununua popote pale duniani kwa kutembelea website hii ya www.proinpromotions.co.tz 
Pendelea vya kwenu kwa kununua vyenu,sheme Watanzania,Warundi,Wanyarwanda,Wakongo,Wazambia,Waganda,Wakenya na waafrika woote tunaomba ushirikiano wenu kwa kununua filamu zetu sasa.

RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI WAWILI WA MAHAKAMA YA RUFAA

index 
Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia Jumamosi iliyopita, Aprili 24, 2015, taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, leo, Alhamisi, Aprili 30, 2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) imesema.
Taarifa hiyo imewataja wajaji hao kuwa ni Jaji Augustine Gherabast Mwarija na Jaji Stella Ester Augustine Mugasha, ambao wote wamekuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tokea walipoteuliwa Novemba 28, 2006.
Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mwarija alikuwa Jaji Mfawadhi, Kitengo cha Biashara, Mahakama Kuu, Dar Es Salaam. Kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kati ya mwaka 2003 na 2006.
Aliajiriwa kama Hakimu Mkazi Daraja la Tatu Februari 2, mwaka 1987, baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka 1986.
Naye Jaji Mugasha, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Jaji Mfawidhi, Dar es Salaam. Alikuwa Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha na awali Kanda ya Moshi tangu 2009 hadi alipohamishiwa Mahakama Kuu, Dar Es Salaam.
Aliajiriwa kama Wakili wa Serikali mwaka 1983 baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka huo huo, 1983.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
30 April, 2015

No comments:

Post a Comment