Tuesday, May 29, 2012

IPP Media uwanjani na Habari Z`bar NSSF

13th March 2012
Chapa
Maoni
Timu ya soka ya IPP Media, leo inaingia uwanjani kutupa karata yake ya kwanza kwenye mashindano ya vyombo vya habari yanayodhaminiwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), watakapocheza na timu ya Habari Zanzibar.
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na uwezo mkubwa wa timu hizo, utachezwa kwenye uwanja wa Chuo Cha Ualimu Chang'ombe (DUCE) kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.
Akizungumza na NIPASHE, kocha wa IPP Media, Ally Mkongwe alisema kuwa timu yake imejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na wapo tayari kwa ushindani.
"Tumefanya maandalizi ya kutosha... tunajua Habari Zanzibar ni timu nzuri lakini hatuna shaka na ushindi kwa kuwa tumejiandaa kukabiliana nao," alisema Mkongwe.
Alisema kuwa licha ya timu yake kuandamwa na majeruhi baada ya baadhi ya nyota wake kuumia kwenye mechi za kirafiki za maandalizi ya mashindano hayo, anaamini wachezaji waliopo badio wana uwezo wa kufanya vizuri.
IPP Media leo itaingia uwanjani ikiwa na wachezaji wake nyota kama, Maulid Kitenge, Faustine Feliciane, Paul Urio na Patrick Nyembela.
Wachezaji wengine ni pamoja na Damdel Ndunguru, Stanley Shempemba, Peter Mchome, Simon Rogers na Fadhil Duma.
Jumamosi timu ya wanawake ya netiboli ya IPP Queens iliwaadhibu vikali wenzao wa Mwananchi kwa magoli 16-12 katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo na watacheza mechi yao ijayo Jumamosi dhidi ya wenyeji wa michuano, NSSF.
IPP Media katika soka imepangwa katika kundi D moja na timu za Global Publishers na Habari Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment