IPP Media uwanjani na Habari Z`bar NSSF
13th March 2012
B-pepe
Chapa
Maoni
Timu
ya soka ya IPP Media, leo inaingia uwanjani kutupa karata yake ya
kwanza kwenye mashindano ya vyombo vya habari yanayodhaminiwa na Shirika
la Hifadhi ya Jamii (NSSF), watakapocheza na timu ya Habari Zanzibar.
Mchezo
huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na uwezo mkubwa wa timu hizo,
utachezwa kwenye uwanja wa Chuo Cha Ualimu Chang'ombe (DUCE) kuanzia
majira ya saa 10:00 jioni.
Akizungumza
na NIPASHE, kocha wa IPP Media, Ally Mkongwe alisema kuwa timu yake
imejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na wapo tayari kwa ushindani.
"Tumefanya
maandalizi ya kutosha... tunajua Habari Zanzibar ni timu nzuri lakini
hatuna shaka na ushindi kwa kuwa tumejiandaa kukabiliana nao," alisema
Mkongwe.
Alisema
kuwa licha ya timu yake kuandamwa na majeruhi baada ya baadhi ya nyota
wake kuumia kwenye mechi za kirafiki za maandalizi ya mashindano hayo,
anaamini wachezaji waliopo badio wana uwezo wa kufanya vizuri.
IPP
Media leo itaingia uwanjani ikiwa na wachezaji wake nyota kama, Maulid
Kitenge, Faustine Feliciane, Paul Urio na Patrick Nyembela.
Wachezaji wengine ni pamoja na Damdel Ndunguru, Stanley Shempemba, Peter Mchome, Simon Rogers na Fadhil Duma.
Jumamosi
timu ya wanawake ya netiboli ya IPP Queens iliwaadhibu vikali wenzao wa
Mwananchi kwa magoli 16-12 katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo
na watacheza mechi yao ijayo Jumamosi dhidi ya wenyeji wa michuano,
NSSF.
IPP Media katika soka imepangwa katika kundi D moja na timu za Global Publishers na Habari Zanzibar.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment