Baada ya kuchukua usimamizi wa
benki hii, Benki Kuu ya Tanzania ilisitisha shughuli za utoaji wa huduma za
kibenki za Yetu Microfinance Bank Plc kwa muda wa siku tisini ili kuipa nafasi
Benki Kuu ya Tanzania kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala
hili. Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu umma kuwa mchakato wa kutathmini
hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya Yetu Microfinanc Bank Plc
haujakamilika hivyo muda wa usimamizi umeongezwa kwa kipindi cha siku
thelathini (30) kuanzia tarehe 12 Machi 2023.
Benki Kuu ya Tanzania
inauhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika
mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.
GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA
No comments :
Post a Comment