Thursday, July 7, 2022

WAJUMBE WA BODI YA KAMISHENI COSTECH WATEMBELEA MIRADI ZANZIBAR

Dkt. Farid Mzee Mpatani akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi wa utengenezaji wa nyenzo inayotokana na maganda ya miwa kwaajili ya kusafishia majitaka yanayotoka hospitalini


WAJUMBE wa bodi ya makamishina ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) tarehe 5 Julai, 2022 watembelea miradi ya Utafiti na Ubunifu visiwani Zanzibar.

Miradi hiyo ni ya utengenezaji wa nyenzo inayotokana na maganda ya miwa kwaajili ya kusafishia majitaka yanayotoka hospitalini pamoja na mradi wa kuongeza thamani ya dawa za asili na kuhifadhi mimea tiba inayotumika kutibu magonjwa yasioambukiza Zanzibar.

Miradi hiyo imefadhiliwa na COSTECH kupitia mfuko wake wa kuendeleza Sayansi Teknolojia na Ubunifu MTUSATE

Aidha COSTECH kupitia MTUSATE imewekeza kiasi cha shilingi milioni100 katika Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI) ili kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.

Pia wajumbe hao walitembelea maabara za mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar na kupata maelezo mafupi kuhusu miradi hiyo.

No comments :

Post a Comment